Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 596 | 597 | (Page 598) | 599 | 600 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Na Sultani Kipingo
  Yaani ni kama kwamba kubadilika kimchezo kwa  kipa wa Man U David de Gea kutoka kuwa mchekea hadi mmoja wa makipa bora wa ligi kuu ya Uingereza kumekamilika. De Gea, hapana shaka, leo amedhihirisha kuwa mmoja wa walinda mlango hodari, tofauti na na msimu uliopita alipookuwa chini ya kocha David Moyes. Leo Mhispania huyu ameokoa penati na kupangua mipira kibao kumyima Mzee Arsene Wenge na Arsenal yake pointi 2 na kumuokoa kocha mpya Louis van Gaal kutoka katika kuti kavu

  Ngoma ilikuwa nzito toka kipyenga cha kwanza.  Ulikuja pale  Cesc Fabregas alipotoa pande tamu kwa Diego Costa ambae alipiga bao moja tamu sana. Kofi la uso kwa mashabiki walioanza kumbeza. Hata hivyo jambo ambalo lingempa hofu Wenger na timu zote zingine ni kwamba leo Chelsea wametandaza kabumbu lisilo la kawaida, na kuhakikisha kuwa hio sio timu ya mtu mmoja. Naam, Costa alifunga tena, lakini hakuwa akihitajika sana. Maana ngoma aliyopiga Eden Hazard si ya kawaida kiasi hata Costa asingefunga, bado tu Chelsea wangepata mabao kwa njia zingine.


  0 0

  Ratiba inaporuhusu kupata kamuda ka kupumua Ankal hupiga makubazi na kula quality time na familia yake. Hapo ni ufukweni akicheza na bintiye Sellah katika kusherehekea sikukuu ya Iddi.
  Wewe je? Unakumbuka kuwa na familia wakati wa mapumziko? 
  Ni muhimu, usisahau hilo....

  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameutaka uongozi wa mkoa wa Kagera ukae na kuzungumza ili kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa katika Manispaa ya Bukoba kwa manufaa ya wananchi.
   
  Ametoa wito huo jana usiku (Jumamosi, Oktoba 5, 2014) wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa Serikali wa mkoa huo mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo iliyowasilishwa kwake na Mkuu wa Mkoa huo, Kanali (Mst) Fabian Massawe.

  Waziri Mkuu aliwasili Bukoba jana jioni akitokea Dodoma ili kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete kwenye maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Kagera

  Waziri Mkuu Pinda alisema: “Ninatumaini viongozi mtakaa na kuzungumza na kukubaliana kuondoa kesi mahakamani ili kazi za kusaidia wananchi zifanyike…. Wewe kiongozi si kitu chochote, wenye kustahili kupewa uzito ni wananchi,” alisema.

  Alisema anaumizwa na viongozi wa mkoa huo kukosa uchungu kwa kuwanyima wakazi wa manispaa hiyo uwezo wa kupata maendeleo kwa ajili ya mtu mmoja.

  “Kuna hela zimetolewa na Benki ya Dunia kiasi cha sh. bilioni 18/- lakini zitapotea hivi hivi kwa sababu ya maslahi binafsi ya watu wachache. Pesa za maendeleo zinatakiwa zifanyiwe maamuzi katika vikao, lakini watu hawawezi kukutana sababu ya mtu mmoja.”

  “Kuna fedha za maendeleo zinazotolewa na Serikali na ili zitumike ni lazima zipitishwe kwenye vikao lakini bila kujali maslahi mapana ya watu mtu anaenda mahakamani na kuzuia kila kitu kisifanyike hadi matakwa yake yatimizwe.”

  Mapemaakiwasilisha taarifa ya mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Kanali (Mst) Fabian Massawe alimweleza Waziri Mkuu kwamba tatizo la kisiasa katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba bado linaendelea.

  Mkuu huyo wa mkoa alisema hivi sasa kuna zuio la mahakama (court injuction) la kutofanyika kwa vikao katika halmashauri lilitolewa Agosti 25, 2014 hadi hapo kesi namba 2/2014 iliyopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba itakapohitimishwa.


  Alisema kesi nyingine mbili bado zinaendelea mahakamani baada ya kesi ya kutaka madiwani sita wavuliwe udiwani kutolewa hukumu mnamo Juni 25, 2014.

  “Kuna kesi ya rufaa namba 11/2014 katika Mahakama Kuu ya Tanzania – Bukoba ya Mhe. Yusufu G. Ngaiza na wenzake watano dhidi ya Chifu Adronicius Kalumuna na Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, wakipinga uamuzi wa kuondolewa udiwani. Rufaa hiyo ilipokelewa Julai 18, 2014 na imepangwa kusikilizwa tarehe 13 Oktoba, 2014,” alisema.

  Kesi ya pili ni kesi namba 02/2014 iliyopo Mahakama ya hakimu Mkazi Bukoba ya Mhe. Anatory Amani ya kutaka Mkurugenzi wa Manispaa amtambue kuwa yeye ni Meya wa Manispaa hiyo na kumpatia haki na stahiki zake. Kesi hii ilifunguliwa Agosti 12, 2014 na imepangwa kuanza kusikilizwa Oktoba 6, mwaka huu.”

  Alimweleza Waziri Mkuu kwamba kulikuwa na kesi nyingine namba 01/2014 katika Mahakama Kuu ya Mhe. Anatory Amani dhidi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na mwanahseria Mkuu wa Serikali ambayo ilifunguliwa Machi 7, mwaka huu ambapo mlalamikaji alitaka mambo kadhaa kuhusiana na taarifa ya ukaguzi maalum iliyotolewa Januari 17, 2014 yatenguliwe na mahakama.

  “Aliiomba mahakama itengue taarifa hiyo kuwa batili na isitambulike kisheria lakini mahakama imeiondoa kesi hiyo tarehe 25 Septemba, 2014 kwa kuwa ilipelekwa mahakamani hapo chini ya kifungu kisicho sahihi,” alisema.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  DAR ES SALAAM.

  JUMAPILI, OKTOBA 5, 2014

  0 0  0 0  0 0

  Sekretarieti ya CPA Kanda ya Afrika inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, (CPA) Dkt. William Ferdinand Shija (pichani) kilichotokea katika Hospitali ya Charring Cross, London Uingereza tarehe 4 Oktoba, 2014.


  Taarifa ya kifo chake imekuja wakati ambapo Mkutano wa 60 wa CPA unafanyika Yaoundé, Cameroon.


  Dkt. William Shija amefanya kazi kwa takriban miaka 8 kama Katibu Mkuu wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola. Amefanya kazi kubwa kwa CPA na ameacha rekodi kubwa ya utendaji wa kazi akiwa pia ndio Katibu Mkuu wa kwanza kutoka Afrika katika Chama hicho.


  Katika uhai wake, Dkt. William Shija amefanya kazi ikiwa ni pamoja na kushikilia nyadhifa zifuatazo katika Serikali ya Tanzania:-


  §  Waziri wa Viwanda na Biashara;

  §  Waziri wa Nishati na Madini;

  §  Waziri wa Habari na Utangazaji

  §  Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu; na

  §  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.


  Aidha, Dkt. William Shija amekuwa Mbunge kwa takriban miaka 15. Akiwa Mbunge, Dkt. William Shija alikuwa Mwenyekiti na Mjumbe katika Kamati zifuatazo:-

  §  Mambo ya Nje; na

  §  Habari; Utamaduni na Utalii.


  Vile vile, amewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika ambapo aliongoza Timu ya Uangalizi wa Uchaguzi kutoka Bunge hilo kwa Uchaguzi Mkuu wa Malawi mwaka 2004.


  Kitaaluma, Dkt. Shija amesoma na kuhitimu Shahada za Uzamili na Uzamivu katika Chuo Kikuu cha Howard Nchini Marekani. Alisoma na kuhitimu Shahada ya kwanza na Stashahada ya Uandishi katika Chuo Kikuu cha New Delhi. Amefanya kazi kama Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii, Nyegezi na pia amewahi kufundisha katika Chuo cha Utumishi wa Umma na Chuo cha Uhazili Tabora.


  Dkt. Shija ameacha Mke Bibi Getruda Peter Shija na watoto watano; Leo, Anna, George, Ferdinand na Monica.


  Sekretarieti ya CPA kwa kushirikiana na Familia ya marehemu, Bunge la Tanzania, Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza na Mwajiri wake CPA Makao Makuu na CPA Makao Makuu inaratibu mazishi yake ambapo mwili wa marehemu utawasili nchini tarehe 11 Oktoba, 2014 na kuagwa rasmi katika Viwanja vya Karimjee siku ya Jumapili tarehe 12 Oktoba, 2014 kabla ya kusafirishwa kuelekea Sengerema kwa mazishi.


  Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi;


  AMINA

                                           
  Dkt. Thomas Didimu Kashililah
  KATIBU WA CPA KANDA YA AFRIKA


  0 0

  Niliwasiliana na G Fullah mara ya mwisho tarehe 14 September. Nilikua ninampa taarfia kwamba yumo kwenye singo yangu mpya aki-chana, na kwamba mixing na mastering inafanywa Marekani, na akafurahi sana. Nikamwambia nitamuita wiki ifuatayo tuje kuongea zaidi kuhusu project yetu. Ile wiki ilyofuatia sikumwita. Nilibanwa sana kikazi. Nikaja kumtumia SMS tarehe 27 Septemba lakini hakujibu. Nikajaribu tena tarehe 1 Octoba, hakujibu. Nikapiga simu mara kibao, hapatikani.

  Jana jioni nilikua na video producer wangu Meja tukijadili mikakati ya kutengeneza video, nikamwambia Fullah kapotea. Sijui yuko wapi. Nilikua na hofu sana.

  Cha ajabu, asubuhi ya leo napata habari ya kwamba mwenzetu amefariki leo asubuhi, na kwamba alikua anaumwa sana. Nimetoka kuongea na shemeji yako hivi punde, na kaniambia wanaterajia kumzika kesho. Kwao wanapoishi familia yake na palipo msiba ni Mbezi Beach.

  Ni pigo kubwa sana. Kama mwalimu wake na msanii
  wangu kwenye lebo yangu Joett Music, nimehuzunishwa sana na kifo cha G Fullah. Singo yangu mpya ambayo nimemshirikisha yeye pamoja na vijana wa Level One (ambao pia ni wasanii wangu), tunaiachia rasmi Octoba 13, na nimeamua kwamba nita dedicate the video to him. Tunaterajia ku-shoot baada ya wiki kadhaa, na mapaka hapo tutakapokamilisha zoezi hilo, nina muomba mungu atupe nguvu katika wakati huu mgumu. Fullah alikua ni mtu mzuri, mkarimu na mwenye subra na upendo kwa jamii iliomzunguka. Nawapa pole wanafamilia, ndugu na marafiki zake wote. Mola ailaze roho yake pema peponi.

  JOETT

  0 0


  0 0
 • 10/05/14--14:58: ZIARA YA JK WILAYANI NYASA

 • 0 0

  The Lord Mayor of Coventry in West midlands in the United Kingdom  Count Hazel Noonan and her consort visited the Tanzania community living in the city of Coventry. The Mayor also visited  projects run by the Community.

  At the evening hosted by madrasatul Aqsaa , a community supplementary school,she commended the good work done by this community and pledged the support of the Government.
  The head of the school Ustadh Ally Khamisi told the audience the journey of the Madrasa where it is today. He said it has been a focal point of the community especially in social, cultural and spiritual matters. He went on to say that the school needs to expand and move to new premises that will accommodate the huge student population.
  "We are now in the process of buying a new place which will act as our community center , Prayer house and , supplementary school". 
  This event was organised by Newdeal Africa which was represented by its chairperson Ms Enzy Larusai
  The Lord Mayor of Coventry in West midlands in the United Kingdom  Count Hazel Noonan talks to the Tanzanian community in Coventry
  The Lord Mayor of Coventry in West midlands in the United Kingdom  Count Hazel Noonan and her consort with madras studends
  The Lord Mayor of Coventry in West midlands in the United Kingdom  Count Hazel Noonan  and her consort with Tanzanian community leaders

  0 0

   Mwanadada Laveda kutoka Tanzania akilakiwa kwa shangwe alipoingia ndani ya jumba la Big Brother Africa Hotshots usiku wa leo baada ya kushinda kwa kura nyingi sana shindano la vipaji ambapo kila mshiriki alipewa nafasi ya dakika tatu kuonesha kipaji chake. Laveda aliingia na Saxophone na kufurahisha kadamnasi kwa umahiri wake na hatimaye akapewa cheo cha kiongozi wa nyumba wa kwanza katika onesho hili kwa mwaka huu.
  Laveda akipuliza saxophone kwa umahiri mkubwa uliompa kura kibao usiku huu. Yaani hapa hata King Maluu atapiga saluti...

  0 0

  Jumuiya ya wa-Islam wanaozungumza ki-Swahili ktk mji wa Coventry uliopo nchini Uingereza (United Kingdom), wameadhimisha swala ya Eidil hajj kwa mafaniko makubwa. 
  Pamoja na mambo mengine waliandaa sherehe za Eid ambazo ziliendelea kwa muda wa siku mbili mfulilizo Jumamosi 4/10/2014 na  Jumapili 5/10/2014 ambapo vyakula vya kiasili vitaandaliwa. 
  Sherehe hizo pamoja na mambo mengine  zina malengo ya kuzikusanya pamoja familia kwa ajili ya kujenga jamii yenye nguvu na yenye kuhimizana maadili mema. 
  Malengo hasa ya jumuiya ni kuhakikisha kua jamii inakua pamoja kwani kwa kufanya hivyo inaamini kwamba itapatikana fursa ya kuwafundisha watoto na watu wazima malezi bora ikiwa ni pamoja na kuifahamu vizuri dini yao, utamaduni wao na kuhimizana mambo mema ambayo ulimwengu mzima unahangaika kuhakikisha kwamba, dunia inakua ni mahali pa amani na utulivu. 
  Kwa ajili ya kuifahamu zaidi COMSWA na malengo yake tembelea http://www.comswa.com/


  0 0

  Bondia Jacob Maganga na Said Mundi wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde mpaka mwisho wa mpambano matokeo ni droo
  Bondia Thomas Mashali akioneshana umwamba na Allibaba Ramadhani wakati wa mpambano wao uliofanyika katika uwanja wa mkwakwani Tanga siku ya sikukuu ya Iddi Mashali alishinda kwa T.K.O ya raundi ya tatu 
  Bondia Thomas Mashali akioneshana umwamba na Allibaba Ramadhani wakati wa mpambano wao uliofanyika katika uwanja wa mkwakwani Tanga siku ya sikukuu ya Iddi Mashali alishinda kwa T.K.O ya raundi ya tatu 
  Bondia Alibaba Ranmadhani akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Thomasi mashali wakati wa mpambano wao uliofanyika siku ya sikukuu ya Idi katika uwanja wa mkwakwani Tanga Mashali alishinda kwa T.K.O ya raundi ya tatu.

  0 0
 • 10/05/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Joti ft aslay & Masanja / orijino komedi

  0 0
 • 10/05/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Tiwa Savage Ft. Don Jazzy - Eminado

  0 0
 • 10/05/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • J. Martins featuring Dj Arafat - Touchin Body

  0 0
 • 10/05/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Davido - Aye

  0 0

  Mrisho Mpoto akimkabidhi kifaa cha kupimia magari mmoja wa wakazi wa Dodoma Beatrice Chilewa (kulia), muda mfupi baada ya kujishindia moja ya swali lililoulizwa na msemaji wa GS1, Pius Mikongoti, ambalo lilikuwa likimtaka ataje nchi tatu za Kusini mwa Jangwa la Sahara zinazotoa Barcode na namba za utambulisho wa nchi hizo, wa kwanza kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya Josekazi Auto Garage ambaye ndiye mmiliki wa kifaa hicho cha kupimia magari.
  MKURUGENZI wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba,(wanne kushoto) akiongea na baaddhi ya wakazi wa Dodoma mjini (hawapo pichani) waliohudhuria Semina ya Kamata Fursa ndani ya Ukumbi wa Royal Village mapema jana,ambapo aliwaeleza wakazi hao namna ya kuwapatia mbinu mbalimbali za kujikwamua kupitia rasilimali zilizopo ndani ya mkoa huo wa Dodoma.
  Msemaji kutoka GS1, Pius Mikongoti akiwalezea wakzi wa Dodoma namna ya  kunufaika kupitia huduma zitolewazo na GS1, hasa katika mfumo wa kutumia Barcode. 
  Msanii wa kughani Mashairi Mrisho Mpoto akiwapa historia yake ya mafanikio na namna alivyoweza kutumia fursa hadi kufikia hapo alipo kwa sasa.
  Afisa Utekelezaji na mipango wa NSSF Ally Mkulemba akitoa semina kwa wakazi wa Dodoma, huku akiwapa mbinu za kutumia fursa katika kusongesha mafanikio kupitia mikopo mbalimbali itolewayo na Shirika hilo mapema jana ndani ya Ukumbi wa Royal Village.
  Sehemu ya watu waliojitokeza kwenye Semina ya Kamata Fursa iliyokuwa ikifanyika ndani ya Ukumbi wa Royal Village,mjini Dodoma hapo jana.
  PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha Brigedia Jenerali  (mstaafu) Hashimu Said Mtezo kilichotokea tarehe 04 Oct 14 kwa ugonjwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo     Dar es Salaam alipokuwa akipata matibabu.              

  Alizaliwa Machi 18, 1945 Wilaya ya Dodoma mjini katika Mkoa wa Dodoma, alisoma katika shule ya Sekondari ya Tabora kuanzia mwaka 1962 hadi alipohitimu Kidato cha Sita mwaka 1967.  Alijiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania tarehe 20 Juni, 1968.  Alitunukiwa Kamisheni Juni 05,1969.

  Katika utumishi wake Jeshini, alihudhuria na kufaulu kozi mbalimbali ndani na nje ya nchi.  Marehemu Brigedia Jenerali Mtezo amewahi kushika madaraka mbalimbali, Mwambata Jeshi nchini Zimbabwe 1987 hadi 1993, Mkurungenzi wa Mafunzo Makao Makuu ya JWTZ 1993 hadi 2002.  Hadi anafariki alikuwa amestaafu Juni 30, 2002 baada ya kulitumikia Jeshi kwa muda wa miaka 34.  Mazishi yatafanyika tarehe 07 Octoba, 2014 Mbezi Lous.

  MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU

  BRIGEDIA JENERALI HASHIMU SAIDI MTEZO (MSTAAFU)

  AMINA


  Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano

  Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

  S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.


  Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 - 309963


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) nchini.

  Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam, leo, Jumatatu, Oktoba 6, 2014, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Bwana Peter Ilomo imesema kuwa uteuzi huo umeanza Ijumaa iliyopita, Oktoba 3, mwaka huu, 2014.

  Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mganga alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka na Wakili wa Serikali Mfawidhi.


  Imetolewa na;

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu – Dar es Salaam.


  6 Oktoba, 2014.


older | 1 | .... | 596 | 597 | (Page 598) | 599 | 600 | .... | 3272 | newer