Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

KAA MKAO WA KULA,BIG BROTHER INAKUJA.....


JK ataja hatua saba za kupunguza msongamano wa magari Dar

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametaja hatua saba ambazo Serikali yake imeanza kuzichukua ama inakusudia kuzichukua ili kukabiliana na msongamano wa magari katika Jiji la Dar Es Salaam.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa msongamano wa magari ni ishara ya ubora wa maisha ya wananchi na ustawi wa Watanzania kwa sababu miaka 20 ama hata 10 iliyopita, Jiji la Dar Es Salaam halikuwa na msongamano. 
“Sasa kila mtu ana gari, naambiwa nyumba nyingine zina magari matatu – la baba, la mama na la watoto.” alisema.

Hata hivyo, Rais Kikwete ameonya kuwa, kama ilivyo katika miji yote mikubwa duniani, ni jambo lisilowezekana kumaliza tatizo la msongamano wa magari katikati ya Jiji la Dar Es Sslaam (Central Business District), hasa kwa kutilia maanani kuwa hakuna shaka kuwa watu wataendelea kununua magari na huwezi kuvunja nyumba zote katikati ya Jiji ili kupanua barabara.

Rais Kikwete ambaye alikuwa anazungumza leo, Jumatano, Oktoba Mosi, 2014, wakati akizindua rasmi Barabara kisasa ya Mwenge -Tegeta kwenye Barabara ya New Bagamoyo Road, amezitaja hatua hizo za kukabiliana na msongamano wa magari katika Mji wa Dar Es Salaam kuwa ni pamoja na ujenzi wa njia ya Mabasi Yaendayo Kasi (DART), ambao awamu yake ya kwanza inakaribia kukamilika pamoja na uanzishwaji wa huduma za kisasa za usafiri wa treni katika maeneo mbali mbali ya jiji hilo.

“DART inalenga kuwashawishi wananchi kupunguza matumizi ya magari binafsi na kutumia zaidi usafiri wa umma. Na hili litawezekana ikiwa mabasi yenyewe yatakuwa mazuri na huduma ikawa bora,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

“Usafiri wa treni ambao nausema mimi ni usafiri wa treni za kisasa zenye mabehewa ya kubeba abiria mijini siyo ule wa sasa ambako mabehewa ya kwenda Kigoma na Mwanza ndiyo yanatumika kubeba abiria kati ya Dar Es Salaam na Tabata.”

Hatua ya tatu ambayo Rais Kikwete ameitaja ni kujengwa kwa barabara za juu kwa juu (flyovers) katika maeneo ya TAZARA na Ubungo, yenye msongamano wa watu wengi, na ujenzi wa barabara 12 za kuzunguka Jiji (Ring Roads) na nyingine za kuunganisha maeneo ya jiji hilo kama vile upanuzi wa Barabara ya Uhuru kuwa njia mbili kila upande badala ya njia moja ya sasa.

Aidha, Rais Kikwete amezitaja hatua nyingine kuwa ni ujenzi wa Daraja jipya la Salender ambalo litapitia baharini, usafiri wa kivuko kipya kutoka Bagamoyo hadi Dar Es Salaam na ujenzi wa miji midogo ya kisasa inayojitegemea katika maeneo ya Kigamboni, Mabwepande na Luguruni.

Rais Kikwete amesema kuwa baadhi ya hatua hizo zinazochukuliwa ama zinalengwa kuchukuliwa na Serikali zimekuwa zinakabiliwa na siasa nyingi za kupinga miradi hiyo kutoka kwa baadhi ya viongozi na wanasiasa nchini ambao amewaita “watu wenye upeo mfupi”.

“Kiongozi anayehubiri upinzani wa maendeleo kwa sababu za siasa ni kiongozi mbovu. Huyu ni mtu mwenye uongozi mbovu, na ana upeo mfupi, usiiona mbali, kwa sababu kiongozi mzuri hawezi kuhubiri siasa za kupinga maendeleo ya wananchi wake.”


Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu – Dar es Salaam.


1 Oktoba, 2014.

KUHUSU UTARATIBU MPYA WA USHURU WA FORODHA KATIKA JUMUIYA YA ULAYA KUANZIA TAREHE 1 OKTOBA, 2014

Introducing Belle 9 ft Joh Makini - Vitamini Music

HOMEBOYZ ENTERTAINMENT @ RHAPSODYS ON SATURDAy

msaada tutani: Mdau APOTELEWA VITAMBULISHO

$
0
0
Uncle Michuzi habari za majukumu.
Naitwa MATHIAS NGUTU. Leo tarehe 1/10/2014   nimepoteza wallet yangu maeneo ya kituo cha daladala cha Makumbusho Dar es salaam wakati wa asubuhi. Ilikiwa na ATM Card yangu ya Benki ya NMB, Kitambulisho cha Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Morogoro na Kitambulisho cha Bima ya Afya.                            
Tafadhali naomba  kuwa aliyeokota namuomba awasiliane nami kupitia namba 0789929777 au ngutumathias@yahoo.com
Nimetoa ripoti kituo cha Polisi Mabatini.

MDAU MATHIAS

Timu ya Wizara ya Habari yawatunishia misuli Hazina.

$
0
0
 Na Eleuteri Mangi-MAELEZO 
Mji wa Morogoro na viunga vyake imepambwa kwa shamra shamra za mashindano ya Shirikisho la Michezo ya watumishi Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea katika viwanja mbalimbali mjini hapo. 
Kwa kipindi cha wiki mbili, watumishi wamekuwa wakionesha vipaji vyao katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, kuvuta kamba, riadha, mbio za baiskeli, mpira wa pete na michezo ya ndani. 
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambayo ndio Wizara yenye dhamana ya michezo imedhihirisha ukakakamavu wake katika mashindano hayo leo mjini Morogoro. Ikiwa na timu mahiri, wizara hiyi imeibuka kidedea katika mchezo wa kuvuta kamba kwa timu ya wanawake na ya wanaume dhidi ya wapinzani wao Hazina kwa kuwavuta kwa mizunguko yote miwili kwa timu zote mbili. 
Kazi ya kuvuta kamba haikuwa ngumu kwa timu za Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwani hikuwachukua muda mrefu kuwavuta wapinzani wao hata kabla ya filimbi ya mwisho ya mchezo huo. Ikumbukwe kuwa michezo ya SHIMIWI imekuwa ni sehemu ya wafanyakazi ambao ni watumishi wa umma kupata fursa ya kujenga afya zao kwa kuwa michezi ni afya kwa maendeleo ya mtumishi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. 
Zaidi ya hayo, michezo ya SHIMIWI imekuwa desturi ya kujenga udugu, amani upendo na mshikamano kati ya wachezaji na viongozi wa michezo husika katika jamii. Aidha, katika mpira wa pete, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imetoka suluhu kwa kutoa sare na timu ya Ulinzi kwa kufungana kwa magoli 18 kabla ya mechi za mwisho za hatua ya makundi ambayo inatarajiwa kumalizika siku ya Alhamisi Oktoba 2 mwaka huu. 
Mashindano hayo yanayoendelea mjini Morogoro yanafanyika katika viwanja vya Jamhuri, Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Mazimbu na chuo cha Ujenzi ili kutoa mwanya wa michezo mingi kufanyika kwa mara moja.  
 Picha ya pamoja ya timu ya kuvuta kamba wanawake kabla ya mechi ya kuvuta kamba na timu ya Hazina  ambapo walishinda kwa kuwavuta kwa 2-0
 Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu wa timu ya Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na timu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii leo mjini Morogoro.

 Wachezaji wa mpira wa pete timu ya Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo wakiwa katika pozi kabla ya kuanza mechi yao na timu ya Jeshi la Ulinzi
 Timu ya kuvuta kamba ya wanaume ya Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo iliyowatoa jasho timu ya Hazina kwa kuwavuta kwa 2-0 wakati wa mashindano ya SHIMIWI mjini Morogoro.

Timu ya kuvuta kamba ya wanawake ya Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo ikionesha umahiri wao wakati wa mashindano ya SHIMIWI mjini Morogoro ambapo walishinda timu ya Hazina kwa kuwavuta kwa 2-0

NDUGU ABDULRAHMAN KINANA SHAMBANI KIJIJI CHA KWEMNYEFU

$
0
0

ankal agongana na wadau wa globu ya jamii dubai

$
0
0
Ankal akiwa na wadau wa Globu ya Jamii aliogongana nao Dubai. Anawashukuru kwa kuwa wadau wa Globu hii kwa muda mrefu na kwamba wao na wengine wote kila pembe ya dunia ni watu muhimu sana sana kwake...

supermodel flaviana matata atembelea ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York

$
0
0
Ankal akila konozzzz na supermodel wa Tanzania anaefanya kazi zake jijini New York, Marekani, walipokutana jijini humo hivi karibuni. Ankal anamsifia Flaviana kwa kuwa mmoja wa watu maarufu wachache wanaoendesha maisha yao bila maskendo wala kashfa. Hongera sana Flaviana. Kaza buti na endeleza kupeperusha bendera yetu vyema ughaibuni.
Picha ya chini Flaviana akiwa na maafisa wa ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini New York.

Ankal benet na balozi manongi

$
0
0
Ankal akila selfie na Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa. Balozi Manongi ni Jembe ambalo halichoki kuendeleza libeneke. Pia ni mmoja wa washauri wakuu wa Globu ya Jamii ughaibuni.

Boxi ughaibuni

ngoma azipendazo ankal - Special request from Aboubakar Liongo

$
0
0
Msondo Ngoma Music Band  - "Kalunde"

BREAKING NEWZZZZZ: MKUU WA USALAMA WA RAIS WA MAREKANI AACHIA NGAZI LEO

$
0
0


Na Sultani Kipingo
Habari zilizotufikia sasa hivi zinasema kuwa Bi Julia Pierson (pichani) , Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Rais wa Marekani maarufu kama Secret Service, amejiuzuru nafasi hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani wan chi hiyo  Bw. Jeh Johnson ametangaza leo. Katika taarifa yake Bw. Johnson kasema atamteua Bw. Joseph Clancy kukaimu wadhifa huo nyeti.

Afisa habari wa Ikulu ya Marekani Bw.  Josh Earnest amesema katika mkutano na wanahabari leo kuwa Rais Barack Obama alimwita Bi Pierson na kumshukuru kwa utumishi wake katika Idara hiyo na nchi ya Marekani, na kwamba Rais huyo aliweka bayana kwamba iko haja ya kuwa na uongozi mpya katika Idara hiyo.

Akiongea baada ya uamuzi huo wa kuachia ngazi, Bi. Pierson alisema ulikuwa ni uamuzi mchungu. “Nadhani (uamuzi huo) kwa maslahi ya Secret Service na umma wa Wamarekani.  Congress (Bunge) limepoteza imani name kuongoza Idara hii. Vyombo vya habari navyo vimeweka bayana kuwa hili ndilo wanalotarajia. Ni uchungu kuacha kazi katika Idara hii ambayo inaandamwa na kashfa mbalimbali za uwajibikaji mbovu wa usalama”.

Bi Pierson alikuwa amekalia kuti kavu na kuwekwa katika hali ngumu kufuatia matukio kadhaa ya kuhatarisha usalama  (wa Rais), ikiwa ni pamoja na mtu mmoja kuruka uzio wa White House na kuingia ndani akiwa na kisu mkononi mnamo Septemba 19 mwaka huu. Inaripotiwa kuwa aliingia humo ndani baada ya kumzidi nguvu afisa usalama aliyekuwa lindo, kabla ya kuzidiwa nguvu na afisa mwingine aliyekuwa amemaliza zamu.

Baada ya tukio hilo, matukio mengine ya kuhatarisha usalama wa Rais yakaibuka. Moja likiwa ni kuruhusiwa kwa mtu mmoja aliyewahi kufungwa jela kuingia katika lifti moja na Rais Obama alipokuwa akizuru Taasisi ya kuzuia magonjwa mwezi uliopita. Pia kuna tukio la mtu kupiga risasi Ikulu hiyo ya Marekani ambayo pia ni makazi rasmi ya Rais wa Marekani.

Jumanne iliyopita Bi Pierson aliwekwa kitimoto na kamati ya Bunge kuhusu matukio hayo. Alisema tukio la karibuni lilikuwa halikubaliki na akakiri udhaifu wa idara katika majukumu yake. “Nakubali kubeba lawama zote”, alisema. “Haitotokea tena.

Taarifa Kwa Umma Kutoka Cham Cha ACT-TANZANIA Kuhusu Zitto Kabwe na Chama Cha ACT- Tanzania

$
0
0
ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPERANCY. 
--
Ndugu wanahabari kumekuwa na utaratibu wa habari zinazoupotosha umma wa watanzania kuhusu chama chetu cha ACT-Tanzania.
Katika gazeti la mwanahabari toleo na 117 la tarehe 29/09/2014 katika ukurasa wake wa mbele iliandikwa "MKAKATI WA KUKIPA NGUVU CHAMA CHA KIPYA CHA ZITTO KABWE WAVUJA".
Act-Tanzania tunaeleza kuwa ni chama cha watanzania wote kisichokuwa na mmilki wake na tunaunganishwa na misingi kumi ya chama pamoja na Itikadi yetu ya Demokrasia jamii.
Act-Tanzania tunatambua uwezo na mchango wa kisiasa na ujenzi wa demokrasia ya vyama vyingi nchini uliotolewa na Mheshimiwa Zitto Kabwe mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Na kwamba kwa sasa ana kesi na chama chake mahakamani na tunaamini atakapomaliza kesi hiyo mchango wake katika siasa za upinzani za Tanzania ni muhimu sana.
Act-Tanzania tunaamini kwamba Mheshimiwa Zitto Kabwe ni mwanasiasa mahiri na makini hivyo tunamkaribisha kwa moyo mkunjufu katika chama mbadala Tanzania.
Na kuhusiana kwamba kuna mkakati wa kuipa nguvu Act-Tanzania ni taarifa za kutunga kwani mikakati yetu ya kuimarisha chama na uenezi wake ni mkubwa na mipango yetu inayotekelezwa kwa umakini na weledi mkubwa.
Na Act-Tanzania tumejipanga kufanya siasa zitakazoleta mabadiliko nchini na kasi yetu inatokana na juhudi na mshikamano wa viongozi wa ngazi zote.
Aidha tunatumia eneo kubwa la mipango yetu ya kukieneza chama kwa mfano kwa sasa tumemaliza ziara ya mikoa 12 na majimbo 68 hivi karibuni iliyokuwa na mafanikio makubwa sana.
Pamoja na mambo mengine tulitoa maelekezo ya maandalizi ya uchaguzi wa vijiji,vitongoji na serikali za mitaa tarehe 14/12/2014,tukitekeleza azimio la kikao cha Halmashauri kuu kilichofanyika Singida.
Hivyo hakuna mkakati wa kuibeba ACT-Tanzania,Bali ACT-Tanzania inabebwa na umakini na weledi katika mipango yake.
Kuhusu Bwana Samson Mwigamba na Profesa Kitilia Nkumbo kujiunga na Act-Tanzania hawa ni watanzania na baada ya kufukuzwa na chama chao cha zamani Act-Tanzania tuliona mchango wao bado unahitajika katika siasa hapa nchini na kwa kuwa hakukuwa na kizuizi kwa wao kujiunga na Act-Tanzania basi tuliwapokea na kwa sasa wanatumikia Act-Tanzania kwa moyo wa kizalendo kabisa.
Kuhusiana na hoja ya kwamba kuna mamluki wa upinzani hizo ni siasa nyepesi kwani unapofukuza wanasiasa mahiri ndani ya chama chochote na wanapokosa fursa ya kufanya siasa pale walipofukuzwa hakuna dhambi ya kushiriki siasa katika chama kipya cha siasa hapa nchini.
Mwisho tunawashukuru watanzania wote wanaoendelea kutuunga mkono nchini kote.
Pia tunapenda kutoa tamko kwamba kwa mujibu wa maazimio ya kikao cha Halmashauri kuu kilichokutana mjini Singida tarehe 25-26/7/2014 tunaendelea na maandalizi ya uchaguzi wa vijiji,vitongoji na serikali za mitaa na maandalizi yetu yanaendelea vyema kabisa.
Lakini pia tunaheshimu uhuru wa kutoa habari waliotumia gazeti la mwanahabari lakini tumesikitishwa sana na wao kama chombo huru kushindwa kutuhoji sisi kama chama baada ya kuwa na habari wanayoiita "MKAKATI WA KUKIPA NGUVU CHAMA KIPYA CHA ZITTO KABWE WAVUJA".

Imetolewa tarehe 01/10/2014
Na Mohammed Massaga
Katibu mawasiliano na Uenezi wa ACT-TANZANIA Taifa
0718388888.

Karibuni Ibada ya Kiswahili - Jumapili Octoba 05, 2014 Kuanzia Saa tisa na nusu - 3:30pm

BENKI YA CRDB YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

$
0
0

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kulia), Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay (kushoto) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (kulia) akiwa na maofisa wa Benki hiyo kabla ya kuanza kwa mkutano.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei kuzungumza na waandishi wa habari kjuhusu Wiki ya Wateja wa Benki ya CRDB.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya wiki ya Wateja wa Benki ya CRDB itakayoanza Oktoba 6-11.
 Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
-----------------------------------------------
WATANZANIA wametakiwa kutumia huduma za kibenki katika kukuza na kujiongezea uchumi wa maisha yao.

Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei katika mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu wiki ya wateja wa benki hiyo itakayoanza Oktob 6,hadi 11,mwaka huu.

Alisema wiki hiyo ni maalum kwa ajili ya kusikiliza kero mbalimbali za wateja ikiwemo kuwashukuru kwa mchango wao mkubwa.

"Azma kubwa ya maazimisho hayo ni kuwasikiliza wateja na kutimiza mahitaji yao kwa wakati ...lengo la CRDB ni kuboresha na kuinua uchumi wa kila mtanzania kupitia mikopo, kutunza na kukuza amana pamoja na kutoa ajira kwa vijana na misaada kwa jamii"alisema Dk. Kimei.
Akifafanua zaidi alisema kwa kutambua umuhimu na mchango mkubwa wa watanzania kwa CRDB, wanatumia wiki hiyo kutoa huduma bora na kusikiliza kero zao.

NSSF YACHANGIA VIFAA VYA ICU HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

$
0
0

Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Jumanne Mbepo (kulia), akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 20 Mkurugenzi  Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk. Marina Njelekela kwa ajili ya kununulia vifaa vya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. 
Kutoka kushoto ni Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Devota Ikandilo, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk John Kimario, Mkurugenzi  Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk. Marina Njelekela na Ofisa Uhusiano wa NSSF, Jumanne Mbepo wakkwa katika picha ya pamoja baada ya NSSF kukabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 20 kwa ajili ya kununulia vifaa vya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. 
-----------------------------
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umechangia kiasi cha shilingi milioni 20 kwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Msaada huo utatumika kununulia vifaa kwa ajili ya chumba cha Wagonjwa mahututi (ICU).
 Akizungumza kwenye makabidhiano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Dk. Marina Njelekela aliishukuru NSSF kwa msaada huo na kuongeza kuwa msaada huo utaenda kuokoa maisha ya watanzania wengi.
  Pia aliwashauri NSSF kushiriki kwenye clinic Maalumu ya upimaji wa Kansa ya Matiti kwa kina mama ambalo hufanyika hospitalini hapo.
Nae Mwakilishi wa NSSF, Jumanne Mbepo alisema kua mchango uliotolewa na NSSF kwa hospitali hiyo hautoshi kununua vifaa vyote na kuomba Taasisi nyingine ziichangie Hospitali hiyo ili kuweza kuokoa maisha ya Watanzania wengi zaidi.
NSSF imekuwa ikitoa huduma ya bima ya Afya kwa wanachama wake ijulikanayo kama SHIB , Hospitali ya muhimbili ni mojawapo ya watoa huduma wa bima hiyo.

JK AFUNGUA RASMI BARABARA YA MWENGE-TEGETA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
 Wananchi wakifurahia hotuba ya  Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada  wakikata utepe  kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki, Meya wa Konondoni Mhe, Mbunge wa Kawe  Mhe Halima Mdee, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Musa Iyombe na viongozi wengine
 Sehemu ya barabara  ya Mwenge-Tegeta yenye urefu wa Km 12.9, ambayo ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mbunge wa Kawe Mhe Halima Mdee  baada ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Picha zaidi BOFYA HAPA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Oktoba Mosi, 2014, amezindua rasmi Barabara ya Kisasa ya Mwenge-Tegeta ambayo ni sehemu ya Barabara ya New Bagamoyo Road, mjini Dar Es Salaam.


Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 12.9 imegharimu kiasi cha Sh. bilioni 77.85, fedha ambazo zimetolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa la JICA. Serikali ya Tanzania imechangia asilimia 7.64 katika gharama za ujenzi wa Barabara hiyo.

Rais Kikwete amefanya uzinduzi huo katika eneo la Makutano ya Kambi ya Jeshi ya Lugalo na Barabara ya Kawe katika sherehe iliyoshuhudiwa na mamia ya wananchi. Alikuwa ni Rais Kikwete ambaye aliweke jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara hiyo Aprili 4, mwaka 2011.

Barabara hiyo ni awamu ya kwanza ya ujenzi wa Barabara itokayo Makutano ya Barabara ya Kawawa, Kinondoni hadi Tegeta. Ujenzi wa awamu ya pili wa kilomita 4.3 kati ya Mwenge na Makutano ya Barabara ya Kawawa, unatarajiwa kuanza wakati wowote baada ya mipango yote ya ujenzi huo kukamilika.

Barabara hiyo ya Mwenge-Tegeta inalenga kupunguza msongamano wa magari katika eneo la kaskazini mwa Dar Es Salaam na pia ni sehemu ya bararaba kuu inayounganisha Jiji la Dar Es Salaam na Mkoa wa Pwani, kupitia Wilaya ya Bagamoyo, na kuunganisha mikoa hiyo na mikoa ya kaskazini mwa Tanzania.

Akizungumza kwenye sherehe hiyo ya uzinduzi wa Barabara hiyo iliyojengwa na Kampuni ya Konoike kutoka pia Japan, Balozi wa Japan katika Tanzania, Mheshimiwa Masaki Okada amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo ulichelewa kukamilika mwaka jana, kama ilivyopangwa, kwa sababu ya wajenzi kukabiliwa na matatizo ya mafuriko makubwa yaliyotokea mwaka 2011.

Mbali na kutaja misaada mingi katika sekta ya miundombinu na hasa barabara ambayo imefadhiliwa na Japan katika miaka mingi iliyopita, Mheshimiwa Okada amesema kuwa Japan sasa iko tayari kuanza ujenzi wa Barabara ya Gerezani-Bendera Tatu, Dar Es Salaam, utakaogharimu Sh. bilioni 18.5, msaada kutoka Japan.

Aidha, Balozi huyo amewaomba radhi Watanzania kutokana na ucheleweshaji wa kuanza kwa ujenzi wa barabara ya juu kwa juu –flyover- katika eneo la TAZARA, Dar Es Salaam, ambao utagharimu Sh. bilioni 53 ambazo zinatolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la JICA.

Amesema kuwa ujenzi huo umechelewa kwa sababu makandarasi wa Kijapan ambao walitakiwa kujenga flyover hiyo wanakabiliwa na kazi nyingi huko nyumbani za kujenga upya miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko na kimbunga cha Great East Japan Earthquake and Tsunami, kilichotokea Machi 2011 na kusababisha uharibifu mkubwa mno.

Aidha, amesema kuwa wajenzi hao pia wanalazimika kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha miundombinu ya kuiwezesha Japan kuandaa Michezo ya Olimpiki ambayo imepangwa kufanyika nchini humo mwaka 2020.

Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu – Dar es Salaam.

1 Oktoba, 2014.
 Wana CCM na Wana CHADEMA wakifurahia kwa pamoja uzinduzi wa barabara hiyo
Tanzania kwanza!!

ERIC SHIGONGO SPEAKS ON VOA'S STRAIGHT TALK AFRICA

$
0
0
According to the Tanzanian Proverb, "A wise person will always find a way"... and so did our Straight Talk Africa Studio Guest! Tanzanian icon Eric James Shigongo, Author, Motivator, and Founder & CEO of Global Publishers & General Enterprises Ltd along with host Shaka Ssali and VOA Social Media Reporter, Mariama Diallo along with TV to Africa Producers, Paul Sisco (L) and Paul Ndiho (R).
Host Shaka Ssali and his studio guest, Eric James Shigongo. Author, Motivator, and Founder & CEO of Global Publishers & General Enterprises Ltd examine contemporary literary trends and new perspectives of publishing in Africa.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images