Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 590 | 591 | (Page 592) | 593 | 594 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Mwenyekiti wa bodi ya benki ya Twiga Bancorp Prof.Amon Mbelle(wapili toka kulia) akipongezana na Mkuu wa Mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya Pwani, Herieth Koka,mara baada ya kuzinduliwa kwa huduma ya ”M-PESA SUPER AGENCY” Itakayowawezesha wateja wa benki hiyo kupata huduma za kifedha kiurahisi kupitia simu za mkononi.Kushoto ni Kaimu Ofisa mkuu wa Benki hiyo Willace Msemo na Meneja uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (kulia).
  Mkuu wa Mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya Pwani, Herieth Koka(kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na huduma ya ”M-PESA SUPER AGENCY” Itakayowawezesha wateja wa benki ya Twiga Bancorp kupata huduma za kifedha kiurahisi kupitia simu za mkononi.katikati ni Mwenyekiti wa bodi wa benki hiyo Prof.Amon Mbelle na kushoto ni Meneja uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu.

  0 0

   Jenerali Ulimwengu ambaye ndiye mwezeshaji  akiendelea kutoa Mwongozo katika mkutano wa siku mbili juu ya mabadiliko ya Tabianchi, uhakika wa Chakula na haki za Ardhi mkutano ulioandaliwa na Oxfam pamoja na Forum CC


  Robert Muthami Program Support Officer kutoka Pan African Climate Justice Alliance (PACJA) akitoa ufafanuzi juu ya baadhi ya mambo yanayohusu mabadiliko ya Tabianchi.

   Meza  ya Majaji wakiwa wanasikiliza kwa makini malalamiko ya walalamikaji kutoka Loliondo juu ya kuchukuliwa ardhi pamoja na Malalamiko kutoka Wilaya ya Kishapu.


  0 0

  Na Veronica Simba – Dar es Salaam

  Maafisa Wakuu 35 kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Afrika Kusini (South African National Defence College – NDC), wametembelea Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini Septemba 30, 2014 kwa lengo la kujifunza kuhusu Sera ya Tanzania kuhusu vyanzo vya nishati nchini hususan mafuta, gesi, makaa ya mawe na uvumbuzi wa madini mengine na changamoto zake.

  Maafisa hao waliongozwa na Mkuu wa Chuo Brigedia Jenerali G.M. Yekelo pamoja na Maafisa kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao ndiyo wenyeji wa wageni hao hapa nchini.

  Wakiwa Wizarani, Maafisa hao walipokelewa na Viongozi na Maafisa Waandamizi wa Idara za Nishati na Madini na kupewa maelezo mafupi kuhusu vyanzo vya nishati nchini pamoja na rasilimali za madini.

  Ujumbe huo upo nchini kuanzia Septemba 27 kwa ziara ya mafunzo na wanatarajia kurejea Afrika Kusini Oktoba 2, 2014.
  Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Afrika Kusini (South African National Defense College – NDC), Brigedia Jenerali G.M. Yekelo akiuliza swali kuhusu rasilimali ya gesi asili kwa Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mhandisi Nobert Kahyoza (wa kwanza kushoto).
  Mmoja wa Maafisa kutoka Chuo cha NDC akitoa salamu za shukrani kwa Wizara ya Nishati na Madini kwa niaba ya wenzake.
  Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mhandisi Nobert Kahyoza (kushoto), akipeana mkono na mmoja wa Maafisa kutoka NDC, baada ya kukabidhiwa zawadi kwa niaba ya Wizara ya Nishati na Madini.
  Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mhandisi Nobert Kahyoza akitoa maelezo kuhusu Kitabu chenye kueleza rasilimali za madini yaliyopo Tanzania kabla ya kukikabidhi kama zawadi kwa Ujumbe wa Maafisa wa NDC.
  Kamishna Msaidizi wa Gesi, Mhandisi Nobert Kahyoza akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Ujumbe wa Maafisa kutoka NDC waliofika kutembelea Wizarani.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante OleGabriel akiongea na wahitimu wa programu ya kujitolea wa Vyuo Vikuu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa VSO International Tanzania Bw. Jean Van Wetter.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habar i Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante OleGabriel katikati akimpa Cheti Dada Ndidi Tumpe wakati wa kuhitimisha Programu ya kujitolea kwa Vijana Wahitimu wa Vyuo Vikuu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuila ni Mkurugenzi Mkazi wa VSO International Tanzania Bw. Jean Van Wetter.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habar i Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante OleGabriel aleyekaa katikati katikapicha ya Pamoja na wahitimu wa Programu ya kujitolea kwa Vijana Wahitimu wa Vyuo Vikuu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuila ni Mkurugenzi Mkazi wa VSO International Tanzania Bw. Jean Van Wetter.

  0 0

  Wahudumu wa Bunge wakibeba masanduku ya kura ili kuyapeleka kwenye chaumba cha kuhesabia kura baada ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kumaliza kazi ya kupiga kura Septemba 30, 2014.
  Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka wakiteta bungeni Mjini Dodoma Septemba 30, 2014. Kushoto ni Spika wa Bunge, Anne Makinda.
   Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Kingunge Ngombale Mwiru (kulia) wakizungumza na Mama Loyce Samike, Mama mzazi wa Mjumbe wa Bunge hilo, Dkt. Angelina Samike (wapili kushoto) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 30, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  CRDB Microfinance Insurance Brokers ambao ni wakala wa bima za aina zote ikiwemo bima ya afya, moto, nyumbani na maisha wakishirikiana na kampuni zaidi ya kumi za bima nchini Tanzania,wamefanikiwa kuwapatia huduma ya bima ya maisha,mazishi na ulemavu wa kudumu Kundi la Wasanii wa Vichekesho la Orijino Komedy Company wao na familia zao kupitia African life Assurance (Tanzania) Ltd na bima ya afya wao na familia zao kupitia Kampuni ya AAR Insurance Tanzania.

  CRDB Microfinance wanayo furaha kubwa kwa kuwapatia wasani hao huduma hiyo,kwani siku zote imekuwa ikifahamika kuwa msanii ni kioo cha jamii.Wasanii hao waliofanikiwa kujiunga na huduma hizo ni pamoja na Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’, Mjuni Silvery ‘Mpoki’, Lucas Mhuvile ‘Joti’, Alex Chalamila ‘McRegan’ na Kiongozi wa kundi hilo,Sekioni David na wengine ni Herry pamoja na Jonas.

  Huduma hii inawahamasisha wasanii wengine,wanahabari,wanamitindo na watanzania wote wa hali zote kutembelea ilipo CRDB Bank tawi lolote nchini Tanzania,ili waweze kupata huduma nzuri ya na haraka ya bima "ndani ya mikono salama" .
  Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Arthur Mosha (kushoto) akimkabidhi Kadi ya huduma ya bima ya maisha,mazishi na ulemavu wa kudumu Kiongoni Mkuu wa Orijino Komedy Company,Sekioni David (kulia) wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo kwenye ofisi za CRDB Mikocheni jijini Dar.
  Msanii Lucas Mhuvile ‘Joti’ akipokea kadi yake kutoka kwa Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Arthur Mosha.
   Msanii Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’ (kulia) akipokea kadi yake kutoka kwa Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Arthur Mosha.(wa pili kulia) ni Meneja Mkuu wa African Life Assurance,Nura Masoud na Kushoto ni Meneja Mkuu wa AAR Insurance,Majala Manyama.
  Meneja Uhusiano wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Nargis Mohamed (kulia) akiwa na Msanii wa Kundi la Wasanii wa Vichekesho la Orijino Komedy Company,Mjuni Silvery ‘Mpoki’ katika hafla hiyo.
  Picha ya pamoja.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Bw. Jack Mugendi Zoka (pichani) kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada.

  Bw. Zoka anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Alex Masinda, ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Zoka alikuwa Ofisa Mwandamizi Ofisi ya Rais Ikulu.

  IMETOLEWA NA
  KATIBU MKUU
  WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
  Dar es Salaam,
  Septemba 30, 2014

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadik baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea Marekani alikohudhuria Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na IGP Ernest Mangu, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadik baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea Marekani alikohudhuria Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Samuel Ndomba mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea Marekani alikohudhuria Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 30, 2014 akitokea Marekani alikohudhuria Mkutano wa 69 wa Umoja wa Mataifa. PICHA NA IKULU

  0 0

  Mkurugenzi kutoka wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa anaeshughulikia dawati la diaspora,Bi Rosemary Chambe Jairo akifungua rasmi mkutano wa Watanznia waishio nchini Botswana wakati walipokutana na Ujumbe kutoka Mfuko wa GEPF ulikuwa ukiitambulisha mpango wa GEPF DIASPORA SCHEME (GDS) nchini humo,hivi karibuni.
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Botswana,Bw Kisasi akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.
  Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka Mfuko wa GEPF,Bw Anselim Peter akiwasilisha mada kuhusu mpango wa GEPF Diaspora Scheme (GDS) na faida zake wanachama.
  Meneja Masoko wa Mfuko wa GEPF,Bw. Aloyce Ntukamazina akisisitiza juu ya umuhimu wa watanzania waishio Botswana kuanza kujiwekea akiba kupitia mpango huo wa GEPF Diaspora Scheme (GDS).
  Baadhi ya Watanzania waishio Botswana wakifuatilia kwa makini mada zilizowasilishwa na mfuko wa GEPF.
  Bw Jimmy Joseph Mwambije Mtanzania aishie Botswana akijaza fomu na kujiunga rasmi na mpango huo wa GEPF Diaspora Scheme (GDS).

  0 0


  0 0

  Assalaamu alaykum wa Rahmatul Laahi wa Barakaatuh

   Jumuia ya An Noor ya Mji wa Leicester, Uingereza, ina furaha kuwatangazia na kuwaalika Waislamu wote kutoka katika mji wa Leicester na vitongoji vyake katika Sherehe za Eid ul Adh-ha kwa Utaratibu huu hapa chini:
  SIKU:   Jumamosi tarehe 4 Oktoba 2014

  PAHALA:         Masjid An Noor Leicester, 170a Belgrave Gate, Leicester LE1 3XL

  WAKATI:         Takbeer msikitini zitaanza Saa Tatu Kamili Asubuhi (9.00am)

                      Na Sala ya Eid itasaliwa Saa Tatu na Nusu asubuhi (9.30am).

  STAFTAHI:

  Inshaa Allah baada tu ya Sala ya Eid, Khutba na kupongezana, tutajumuika kwa pamoja kupata Kifungua kinywa yaani Staftahi kama kawaida yetu ya kila mara.
  Tafadhali Tufike kwa Wakati ili shughuli ziende kwa utaratibu uliowekwa.

  Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na Omar Hussein 07565512058

  au madrasatulnoor.01@gmail.com  KULLU AM WA ANTUM BIKHAYR


  0 0

  Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
   Nchi za Zambia, Tanzania na Kenya zimesaini Mkataba wa Makubaliano kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi hizo kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme (ZTK) na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo na nchi nyingine barani Afrika. 
  Akiongea katika hafla hiyo Waziri wa Nishati na Madini, Tanzania Profesa Sospeter Muhongo ameeleza kuwa, mradi huo wa pamoja unalenga kuondoa tatizo la upungufu wa nishati ya umeme baina ya nchi hizo na nchi nyingine barani Afrika jambo ambalo litachangia katika kukuza uchumi wa mataifa hayo. 
  Waziri wa Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji wa Zambia , Christopher Yaruma ameeleza kuwa, utekelezaji wa mradi huo sio tu utaziwezesha nchi hizo kufanya biashara bali pia utafungua fursa za uwekezaji na kusaidia katika kuondoa umaskini miongoni mwa nchi wanachama kutokana kuzitumia fursa mbalimbali zinazotokana na nishati ya umeme. 
  Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Petroli Kenya, Davis Chirchir amewataka washirika wa maendeleo kusaidia katika kuwezesha utekelezaji wa mradi huo wa kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme baina ya nchi hizo kutokana na manufaa yake kwa bara la Afrika na kuongeza kuwa, kutokana na uwepo wa rasilimali asilia za kutosha katika nchi hizo hakuna sababu ya kuwepo tatizo la nishati katika nchi hizo na barani Afrika.
   Naye Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Soko la pamoja la nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika anayeshughulikia miradi (COMESA), Dkt. Kipyego Cheluget amezipongeza nchi hizo kwa kuuendeleza utekelezaji wa mradi huo ambao umechukua kipindi kirefu na kuueleza kuwa, ni miongoni mwa miradi 16 ya kipaumbele na kimaendeleo kwa Afrika. 
  Aidha, kwa upande wao Washirika wa maendeleo waliohudhuria hafla hiyo, wameonesha kufurahishwa kwao na dhamira ya nchi hizo na kuahidi kushirikana na nchi hizo kuhakikisha mradi huo unatekelezwa. Miongoni mwa washirika wa maendeleo waliohudhuria ni pamoja na uwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Benki ya Dunia, Ubalozi wa Norway, Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), African Development Bank(AfDB) na Ubalozi wa Ufaransa.
   Mawaziri wanaoshughulikia Nishati kutoka nchi za Zambia, Tanzania na Kenya wakisaini Mkataba wa Makubaliano kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi hizo kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo. Mkataba huo umesainiwa jijini Dar es Salaam leo na Waziri wa Nishati na Madini Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), Waziri wa Wizara ya   Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji  wa Zambia , Christopher Yaruma (kushoto)  na  Waziri wa Nishati na Petroli Kenya , Davis Chirchir (kulia) . Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Migodi , Nishati na Maendeleo ya Maji Zambia, Charity Mwansa, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini , Tanzania , Eliakim Maswi na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Petroli Kenya,  Mhandisi Joseph Njoroge.
   1.      Mawaziri wanaoshughulikia Nishati kutoka nchi za Zambia, Tanzania na Kenya , Waziri wa Wizara ya   Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji  wa Zambia , Christopher Yaruma (kushoto) Waziri wa Nishati na Madini , Profesa Sospeter Muhongo Tanzania (katikati) na Waziri wa Nishati na Petroli Kenya, Davis Chirchir (kulia) wakibadilishana Mkataba wa Makubaliano kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi hizo kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo mara baada ya kusaini.

   1.     Mawaziri wa wanaoshughulikia Nishati kutoka nchi za Zambia, Tanzania na Kenya , Waziri wa Wizara ya   Migodi, Nishati na Maendeleo ya Maji  wa Zambia , Christopher Yaruma (kushoto) Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo  Tanzania (katikati) na Waziri wa Nishati na Petroli Kenya, Davis Chirchir (kulia) wakionesha Mkataba wa Makubaliano mara baada ya kusaini.

  1.     Sehemu wa wadau waliohudhuria hafla ya kusaini Mkataba  wa Makubaliano kuonesha dhamira ya Serikali ya nchi za Zambia, Tanzania na Kenya kujenga miundombinu ya pamoja ya kusafirisha umeme na kufanya biashara ya kuuziana umeme wa ziada baina ya nchi hizo. Mbali na Wataalamu kutoka katika nchi hizo, hafla hiyo imehudhuriwa uwakilishi wa COMESA,  Mashirika ya Umeme kutoka nchi hizo na  baadhi ya washirika wa Maendeleo wakiwemo Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, Ubalozi wa Norway, Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), African Development Bank (AfDB), Ubalozi wa Ufaransa.


  0 0

  Karibu katika mahojiano kati ya Mubelwa Bandio wa Kwanza Production na Dr Patrick Nhighula, mgombea wa nafasi ya uRais wa DICOTA 2014. Mbali na kuielezea DICOTA yenyewe, pia ameeleza nia yake kugombea nafasi hiyo Karibu umsikilize

  0 0


  0 0

  Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

   MTU mmoja anayedaiwa kuwa ni Jambazi ameuawa na wananchi baada ya kumpora mwananchi mmoja kiasi cha Sh. 2, 100,000= wa kijiji cha Igoji One Kata ya Mima katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.


  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP ameeleza kuwa tukio hilo la kumvamia mwananchi huyo huko nyumbani kwake Kijiji cha Igoji one aliyejulikana kwa jina la YARED S/O MAPATANO MSALILA limetokea mnamo tarehe 28/09/2014 majira ya saa 22:00hrs usiku na kisha kupora kiasi hicho cha fedha na kumjeruhi sehemu za kichwani na mguuni.

  Kamanda MISIME amesema baada ya kufanya tukio hilo wakiwa wanne, wananchi waliwafuatilia toka katika kijiji cha Igoji one Wilayani Mpwapwa wakishirikiana na wanakijiji wa Iwendo na Fufu na kufanikiwa kumkamata jambazi mmoja baada ya kumjeruhi mwananchi mmoja aliyefahamika kwa jina la VICENT S/O MAKALI kwenye kidole cha shahada cha mkono wa kushoto kwa risasi wakati wanamnyang’anya jambazi huyo bastola aliyokuwa nayo.

  Kamanda MISIME aliendelea kueleza kuwa wananchi hao walifanikiwa kumnyang’anya bastola hiyo yenye namba DAA 317086 aina ya Bereta ambayo imegundulika kuibiwa huko Tuangoma Kongowe Temeke Dar es Salaam tarehe 19/04/2014 baada ya SHADRACK MUGALULA nyumbani kwake na kumpora silaha hiyo.

  Adha Kamanda MISIME ameseama baada ya wananchi kuona kuwa mwananchi mwenzao amejeruhiwa ilibidi wajihami na kumshambulia jambazi huyo kitendo kilichomfanya kupoteza maisha. Jambazi huyo ametambuliwa kwa jina la LAMECK S/O CHARLES @ LUMOLWA, Mgogo, Mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa Kijiji cha Mbabala Wilaya ya Dodoma.


  Pia Kamanda MISIME amesema kuwa majambazi wengine watatu wanaendelea kusakwa ili waweze kufikishwa mahakamani.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Kiongozi wa Kampuni ya ZANCHICK inayojishuhulisha na biashara ya Kuuza Kuku (Perdue)kutoka Marekani Dk.David Elua akiwa na ujumbe wa kampuni hiyo ulipofika Ikulu Mjini Unguja jana kwa mazungumzo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya ZANCHICK inayojishuhulisha na biashara ya Kuuza Kuku (Perdue) kutoka Marekani unaoongozwa na Dk.David Elua katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja jana .[Picha na ramadhan Othman Ikulu.]

  0 0

   Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman (mwenye Kaunda suti ya kijivu) akisindikizwa kutoka nje ya viwanja vya Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma na Askari Polisi mara baada ya kushutumiwa na baadhi ya Wajumbe wa Zanzibar. 

  0 0

  Wataalamu wa sekta ya mawsiliano wakiwa katika majadiliano katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ unaofanyika jijini Dar es Salaam.  Wataalamu wa sekta ya mawsiliano wakiwa katika majadiliano katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ unaofanyika jijini Dar es Salaam. Wataalamu wa sekta ya mawsiliano wakiwa katika majadiliano katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ unaofanyika jijini Dar es Salaam.  Wataalamu wa sekta ya mawsiliano wakiwa katika majadiliano katika mkutano wa masuala ya TEHAMA ‘Connect-to-Connect Summit’ unaofanyika jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Prof. John Nkoma (kushoto) akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura wakiwa katika mkutano huo. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Prof. John Nkoma (kushoto) akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura wakiwa katika mkutano huo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Now you can not only control your venue,profits or promote your brand but can also "give back" to your customers etc. Make them win anything as they attend your event etc. See the details below and feel free to call and order RN SCRATCH AND WIN

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Lusekelo Mwaseba (pichani) kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

  Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam, leo, Jumatano, Oktoba Mosi, 2014, na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, imesema kuwa uteuzi huo unaanza leo.

  Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mwaseba alikuwa Kamishna wa Uchunguzi katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).


  Imetolewa na;

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu – Dar es Salaam.


  1 Oktoba, 2014.


older | 1 | .... | 590 | 591 | (Page 592) | 593 | 594 | .... | 3286 | newer