Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

DKT. SHEIN MGENI RASMI KATIKA SHEREHE ZA ELIMU BILA MALIPO AMAAN ZANZIBAR LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Walimu na Wanafunzi katika Sherehe za Miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi kombe Msaidizi Afisa Elimu Mkoa wa Kaskazini Unguja Maulid Nafasi Juma wakati wa Sherehe za Miaka 50 ya Elimu bila malipo zilizofanyika kitaifa katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanafunzi waliopita mbele ya jukwaa la viongozi katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar wakati wa sherehe za kilele cha miaka 50 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika leo.
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika sherehe za miaka 50 ya Elimu bila Malipo zilizofanyika katika uwanja wa Amaan Studium na mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.


MH. CHENGE AWASILISHA RASIMU YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA KWA MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba Mhe. Andrew Chenge akimkabidhi Mwenyekiti wa Bunge hilo Mhe. Samuel Sitta Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi cha Bunge hilo jana. Kamati ya Uandishi imemaliza kazi ya kuandaa Rasimu hiyo na inatarajiwa kusomwa Bungeni leo. Picha na Owen Mwandumbya.

Warsha ya uhamasishaji ,mawasiliano na utetezi wa Lishe bora katika jamii itakayochukua siku tatu imefunguliwa leo

$
0
0
Watanzania, Asasi zisizo za serikali na wadau mbalimbali hapa nchini wametakiwa kuwa mabalozi waLishe Bora katika jamii zinazo wazunguka, hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Ndugu Charles A. Pallangyo katika warsha ya siku 3 iliyofunguliwa leo tarehe 23 hadi 25 September 2014 katika Hotel ya Serena jijin Dar es salaam.

“Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara yake ya Afya na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania imeendelea kuratibu masuala la lishe bora nchini, mfano mwaka 2013 serikali kupitia wizara ya afya imeanzisha kampeni nchi nzima yenye kuhamasisha lishe bora, na katika kutekeleza Mpango Mkakati wa Lishe Tanzania (National Nutrition Implementation Plan) e, serikali imeajiri maafisa wa lishe katika Halmashauri takribani 147 na mikoa 20 huku ikiazimia kufikia halmashauri zote na Mikoa yote Tanzania Bara. Alisema Ndugu Charles A. Palangyo

Aidha Katibu Mkuu aliweza kuzungumzia changamoto wanazokumbananazo katika kuhamasisha maswala ya Lishe bora nchini na kuwataka wadau, mashirika na Asasi zisizo za kiserikali kuendelea na mkakati huo.

“Pamoja na jitihada tunazozifanya , bado kuna changamoto katika zoezi zima la kuboresha lishe kwa watanzania, kwa mfano asilimia 42 ya watoto chini ya umri wa miaka 5 wamedumaa, asilimia 16 ya watoto hao wanaukondefu , na watoto wanaozaliwa na uzito pungufu wanakaribia kuwa asilimia 21.

Ukiachalia hilo, kwa upande wa kina mama, inakadiriwa kuwa asilimia 11 huwa wanakuwa na uzito pungufu, huku 53% ya wajawazito wanakumbwa na tatizo la upungufu wa wekundu wa damu. “Hivyo ningependa kuwaomba wadau, mashirika yaliyo bega kwa bega na serikali yaendelee kujitolea katika safari hii ya kuhakikisha kila mtanzania anapata lishe bora”, Aliongeza katibu mkuu Charles A. Palangyo.

Warsha hiyo ya kuhamasisha lishe bora katika jamii za kitanzania imefunguliwa leo na katibu mkuu wa wizara ya afya na ustwahi wa jamii katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam huku ikitazamiwa kufikia tamati tarehe 25 Septemba 2014.

Waratibu wa warsha hiyo ni shirikisho la SUN Movement Secretariat ambalo ni jumuhisho la nchi hamsini na nne (54) waliodhamiria kuboresha masuala ya lishe ndani ya jamii zao, ikishrikiana na Serikali ya Tanzania, PANITA pamoja na World Vision. Warsha hii inawashiriki kutoka nchi tisa Africa ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Nigeria, Zambia, Zimbabwe, Mozambique, Malawi na Tanzania
Mgeni Rasmi,Ndg. Charles A.Pallangyo akiwahutubia wageni waliofika katika warsha hiyo serena hotel.
Mkurugenzi Mtendaji PANITA, Ndg. Tumain Mikindo akitoa nasaha zake kwa washiriki.
Mheshimiwa Mbunge Lediana Mafuru Mungo'ng'o akielezea nafasi yake katika masuala ya lishe bora.
Ndg. Brenda kaijuka , mshauri kutoka SUN akiwaelezea washiriki namna ya kuhamasisha lishe bora.

Watumishi wa afya waonywa

$
0
0
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid akizungumza wakati za uzinduzi wa Mpango wa Maboresho kwa Wafanyakazi wa Sekta ya Afya (HRHSP 2014/2019), uliofanyika Dar es Salaam jana.


Baadhi ya wadau wa afya wakifuatilia uzinduzi wa wa Mpango wa Maboresho kwa Wafanyakazi wa Sekta ya Afya (HRHSP 2014/2019), uliofanyika Dar es Salaam jana. Picha na Joseph Zablon.

Wafanyakazi katika sekta ya afya wanadaiwa kutumia muda wa asilimia 20 na isiyozidi 30 kwa mwa mwezi jambo ambalo ni kinyume chja mikataba yao ya ajira inayowataka kuwepo kazini hadi saa nane hivyo kukwamisha Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid alisema hayo wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Maboresho ya Wafanyakazi wa Sekta ya Afya 2014/2019 ambao upo chini ya wahisani wa Global Fund, kupitia shirika la Misaada la Japani (Jica).

Alibainisha kuwa wafanyakazi katika sekta ya afya wanatumia asilimia 20 na isiyozidi 30 kwa mwezi katika kufanyakazi ambazo hazihusiani na ajira zao jambo ambalo linasikitisha na kukwaza jitihada za serikali katika sekta hiyo.

Dk Rashid alisema chini ya utaratibu wa BRN, serikali imefanikiwa kuvuka lengo la kusomesha na kuwandaa watalaam katika kada tofauti za afya na awali ilikuwa wawe wamefikia 10,000 hadi kufika 2017 kutoka idadi ya mwaka 2013 ya wahitimu 3,000 lakini lengo hilo hadi sasa limeishavukwa.

“Hadi hivi sasa tumeishahitimisha wanafunzi 10,700 hivyo kupitia mpango huu ambao tumeuzindua leo tayari tumevuka malengo hivyo tutapanga mapya kuelekea 2017” alisema na kuongeza kuwa mpango wa BRN hautaangalia wingi wa idadi na mgawanyiko pekee wa raslimali watu.

Alisema hivi sasa mpango uliopo ni kuhakikisha wale ambao wamepangiwa vituo vya kazi wanafika na ku muda ambao wanatakiwa wawepo na sio tofauti na hivyo.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi wa program hiyo, Mkurugenzi wa Mafunzo na Maendeleo ya Raslimaliwatu katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Otilia Flavian Gowelle alisema pia kuna ambao wanakacha kwenda vituo vya kazi walivyopangiwa.

Alisema asilimia 60 ya waliopangiwa sehemu za kufanyiakazi hawaendi katika kwa visingizo mbalimbali na kubadilisha dakika za mwisho na mipango inafanywa ili wahitimu hao wa ngazi ya kati katika sekta ya afya wawe na mikataba na serikali ya kufanyakazi miaka mitatu kabla ya kwenda kwingineko.

MAMA SALMA KIKWETE AHUTUBIA MKUTANO WA ELIMU NA AFYA KWA VIJANA DUNIANI ULIOANDALIWA NA TAASISI YA MAMA SARAH BROWN

$
0
0
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Sarah Brown, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza na Mwenyekiti Mtendaji wa Global Business Coalition for Education muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa ‘Getting Serious About Results: The Grand Convergence of Education and Health” ulioandaliwa na Taasisi ya Mama Sarah Brown kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa. Mkutano huo umefanyika huko New York tarehe 23.9.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Bwana Gordon Brown kabla ya kuanza mkutano uliozungumzia mambo ya elimu na afya kwa vijana duniani tarehe 23.9.2014.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Dkt. Sarah Maongezi, Mkurugenzi wa Idara ya Afya katika Taasisi ya WAMA muda mfupi kabla kuanza mkutano huo.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa :’Getting serious about Results: The Grand Convergence of Education and Health’ ambao ulizungumzia mambo ya elimu na afya kwa vijana hapa duniani. Mkutano huo ilifanyika huko New York tarehe 23.9.2014.

wakazi wa Meru wapatiwa elimu ya lishe

$
0
0

Mtaalamu wa Lishe Tom Mwaipenye kutoka taasisi ya Foot Print, akiwaeleza akina mama waishio maeneo yanayozunguka hospitali ya Halmashauri ya Meru mkoani Arusha, umuhimu wa Virutubishi kwa afya bora ya mwili na akili za mtoto, ikiwa ni sehemu ya kampeni za kuelimisha umma juu ya faida za kutumia Virutubishi ili kuboresha afya. Kampeni hizi zinaendeshwa na serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Taasisi ya Chakula na Lishe, na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania

Akina mama waishio maeneo yanayozunguka hospitali ya Halmashauri ya Meru mkoani Arusha, wakipatiwa elimu ya lishe katika kampeni za matumiziya vyakula vyenye virutubishi zinazoendeshwa na serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Taasisi ya Chakula na Lishe, na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania.
Wakazi wa Halmashauri ya Meru mkoani Arusha, wakisikiliza elimu ya lishe kutoka kwa wataalamu katika kampeni za matumizi ya vyakula vyenye virutubishi zinazoendeshwa na serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Taasisi ya Chakula na Lishe, na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania.

REDIO 5 WAANDAA HAFLA YA LISHE BORA MONDULI

$
0
0
SAM_0154
Mkuu wa Wilaya ya Monduli,mkoani Arusha,Jowika Kasunga akifungua hafla ya lishe bora iliyoandaliwa na kituo cha redio 5 cha jijini Arusha kwa kushirikiana na wadau wa KABI, AVRDC,Hort Tengeru,Inades formulation pamoja na airish Aid yenya kauli mbiu ya LISHE BORA KWA AFYA yaliyofanyika katika hospitali ya wilaya ya Monduli 
SAM_0147
Meneja masoko wa Redio 5Bi.Sarah Keiya akizungumza katika hafla ya lishe bora iliyoandaliwa na kituo cha redio 5 cha jijini Arusha kwa kushirikiana na wadau wa KABI, AVRDC,Hort Tengeru,Inades formulation pamoja na Airish Aid yenye kauli mbiu ya LISHE BORA KWA AFYA yaliyofanyika katika hospitali ya wilaya ya Monduli .

SAM_0110
SAM_0138
Sehemu ya wageni waliohudhuria hafla hiyo
SAM_0261 - Copy
Meneja mbunifu wa redio 5 Vicky Mwokoyo kulia,katikati  meneja biashara Angela Maina wakiwa wanamkabidhi vifaa vya upimaji magonjwa kwa mganga mkuu wa hospitali ya wilaya Monduli Zavery Benela   iliyotolewa na kampuni ya  Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha .

Ndovu Special Malt yakabidhi vifaa vitakavyosaidia kukabiliana na Ujangili katika Hifadhi za Wanyama nchini

$
0
0
 Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt,Pamela Kikuli akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya muendelezo wa harakati zake za kusaidia kuimarisha ulinzi wa Wanyama aina ya Tembo ili wasiuwawe hapa nchini,ikiwa ni Bia iliyobeba jina la Mnyama huyo,ambapo wametoa vifaa mbali mbali vya kusaidia ulinzi huo,ikiwa ni pamoja na Darubini kubwa (Binoculars) na trimble GPS ambazo zitasaidia katika harakati za kupambana na ujangili katika mbuga za wanyama nchini.Kulia ni Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete.
 Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete akizungumza na waandishi wa habari kwenye Mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa TBL jijini Dar es Salaam,ikiwa ni pamoja na upokeaji wa vifaa kutoka kwa bia ya Ndovu Special Malt.Kulia ni Meneja wa Bia ya Ndovu,Pamela Kikuli
Mkuu wa Idara ya Ulinzi katika hifadhi ya Serengeti,Agricola Lihiru akielezea namna ya matumizi ya vifaa hivyo na faida yake katika kupambana na ujangili kwenye hifadhi za wanyama nchini.
Meneja wa bia ya Ndovu Special Malt,Pamela Kikuli akikabidhi baadhi ya vifaa hivyo kwa Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete na Mkuu wa Idara ya Ulinzi katika hifadhi ya Serengeti,Agricola Lihiru.Picha zote na Othman Michuzi.

MICHUANO YA Dr Mwaka Sports Extra Ndondo Cup KUANZA KUTIMUA VUMBI IJUMAA

$
0
0
Viongozi na wawakilishi wa timu shiriki za Dr Mwaka Sports Extra Ndondo Cup wakizionesha jezi watakazozitumia katika michano hiy, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi keshokutwa Ijumaa kwenye Uwanja wa Makurumla, Magomeni jijini Dar es Salaam.
 Dr Mwaka (kulia), Dauda wakimkabidhi mwakilishi wa timu shiriki za Dr Mwaka Sports Extra Ndondo Cup jezi.
Mdhamini Mkuu wa michuano ya  Dr Mwaka Sports Extra Ndondo Cup ,Dr Mwaka akifafanua jambo mbele ya wanahabari kuhusiana na michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi keshokutwa Ijumaa kwenye Uwanja wa Makurumla, Magomeni jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Waratibu wa Mwaka Sports Extar Ndondo Cup  Alex Luambano kutoka Clouds FM (aliyesimama) akiwatambulisha baadhi ya waratibu,wasiamizi na Wadhamini  wa Dr Mwaka Sports Extar Ndondo Cup inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi keshokutwa Ijumaa kwenye Uwanja wa Makurumla, Magomeni jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa timu shiriki wa Dr Mwaka Sports Extra Ndondo Cup wakiwa na waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo uliofanyika kwenye kiota cha maraha cha Escape One,Mikocheni jijini Dar. 
Mratibu wa Dr Mwaka Sports Extra Ndondo Cup kutoka Clouds FM, Shafih Dauda akielezea ushiriki wa michuano hiyo kwenye Ufukwe wa Escape One, Mikocheni jijini Dar es Salaam, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi keshokutwa Ijumaa kwenye Uwanja wa Makurumla, Magomeni jijini Dar es Salaam. 

VIWANJA VINAUZWA

$
0
0
VIWANJA HIVI VIPO KIGAMBONI,KATA YA PEMBA MNAZI,MTAA WA MUHIMBILI (TANDAI CENTER),VIPO UMBALI WA MITA 600 - 700 KUTOKA BARABARA KUU NI VIWANJA VILIVYOPIMWA.

KWA MAELEZO ZAIDI JUU YA VIWANJA HIVYO,WASILIANA NA NDG. JAMES MPAYO KWA NAMBA HIZO HAPO CHINI.
0784 207877 NA 0754 780878
PIA UNAWEZA KUMTUMIA EMAIL: 
JMPAYO@OVI.COM

PECHE BOY KUMKABILI JUMA FUNDI

$
0
0
Bondia anayechipukia kwa kasi issa omar nampepeche au  “Peche boy” kama wengi wanavyomwita, ataoneshana umwamba na bondia mkongwe mwenye rekodi nzuri ya kuwapiga kina nasibu ramadhan,majia na kupoteza kwa tabu kwa miyeyusho pia ana  historia ya kuwa bondia wa kwanza  Tanzania kuwasumbua wafilipino na kucheza mapambano mengi ya ubingwa,nae  Issa Omar “peche boy” bondia wa mwananyamala anayejifua katika gym ya bigright boxing, ni kijana mwenye kipaji cha mchezo tangu mdogo na  mwenye rekodi ya kushinda mapambano yote 18  huku moja likikosa mshindi.

 Issa Nampepeche  baada ya kuwapiga kitandula,moro best na juma seleman, inaonekana amekwishaa komaa na sasa anakabiliana na mtihani mwingine mgumu wa juma fundi katika pambano la round nane litakalopigwa siku ya jumamosi tarehe 27/ 9/ 2014 katika ukumbi wa friends kona uliopo manzese huku yakifuatiwa na mapambano mengine ya kina Mohamed Rashid Matumla atayeminyana na Nasibu Ramadhan, Sadiki Momba na Adam Ngange pia kutakuwepo na mchezo mwingine wa kina dada nao ni kati ya lulu kayage atakayezipiga na mtoto wa bondia mkongwe Fatuma Omar yazidu.

Akizungumza na vyanzo vya habari kiongozi wa ngumi na msemaji wa pambano  Ibrahim Kamwe alisema  “ni kuwa maandalizi ya pambano zima yamekamilika na mabondia wote wapo katika hari nzuri ya mchezo huku dogo issa nampepeche akijiamini zaidi kumshinda juma fundi, na Nasibu Ramadhan akijigamba kulipa kisasi kwa muddy matumla kwa kipigo cha mbwa mwizi,. 

Ibrahim kamwe aliongeza kwa kusema kuwa yale malalamiko ya watu kuwa friends corner hotel viti huwa vichache yamefanyiwa kazi na katika pambano hili viti vitakuwa vingi na askari watakuwepo wengi kulinda watu na mali zao na kiingilio kimewekwa kizuri ili watu wenye heshima zao waweze kuja na kufurahia mashindano haya yenye kushirikisha mabingwa vijana wenye vipaji na  uwezo wa hali ya juu katika masumbwi

UN Secretary-General appoints special Envoy on Ebola

$
0
0
David Nabarro
United Nations Secretary-General Ban Ki-moon today announced the appointment of David Nabarro  of the United Kingdom as his Special Envoy for Ebola and Anthony Banbury as his Special Representative and Head of the United Nations Mission for Ebola Emergency Response (UNMEER). 

These appointments follow the unanimous adoption of General Assembly resolution 69/1 on 19 September, and the adoption of Security Council resolution 2177 on the Ebola outbreak. They are made following close consultations with Dr. Margaret Chan, Director-General of the World Health Organization. 

In his vital role as Special Envoy for Ebola, Dr. Nabarro will provide strategic and policy direction for a greatly enhanced international response and will galvanize essential support for affected communities and countries.

Under Mr. Banbury’s leadership, UNMEER, the new Mission, will provide the operational framework and unity of purpose to ensure the rapid, effective and coherent action necessary to stop the Ebola outbreak, to treat the infected, to ensure essential services, to preserve stability and to prevent the spread to countries currently unaffected.

Dr. Nabarro and Mr. Banbury will work closely in support of the governments in the region, and other partners, in pursuit of these critical objectives.  

Dr. Nabarro has more than 30 years’ experience of public health, nutrition and development work at country, regional and global levels, and has held positions in non-governmental organizations, universities, national Governments and the United Nations system. He serves as Special Representative of the Secretary-General for Food Security and Nutrition and Coordinator of the SUN Movement. Dr. Nabarro’s other recent positions include Senior Coordinator for Avian and Pandemic Influenza from 2005 to 2014 and coordinator of the UN’s High Level Task Force on Global Food Security from 2009 to 2014.  Last month he was appointed as Senior UN Coordinator for Ebola.  

Mr. Banbury brings more than 25 years of experience in political, peacekeeping, and emergency management roles across several different regions and organizations. He has served as Assistant Secretary-General for Field Support since June 2009. He also served as Acting Deputy Special Representative in MINUSTAH after the 2010 earthquake, and was the Asia Regional Director for the World Food Progamme in Bangkok from 2003 to 2009, where he managed humanitarian relief and development operations in 14 countries. He also was an integral part of the relief operations for the 2004 tsunami and the 2008 Cyclone Nargis.

HEPI BESDEI YA KUZALIWA MWANALIBENEKE FAUSTINE RUTA

$
0
0

Leo tarehe 24 mwezi wa tisa ni siku ya kuzaliwa kwa mpiganaji mwanalibeneke na mdau Faustine Ruta wa bukobasports.com.

"Namushukuru Mungu kwa Zawadi ya Uhai, afya njema na kunijalia Mpaka sasa hapa nilipo.Napenda kuwashuku sana wadau wangu wote tunaoshirikiana kila siku katika ujenzi wa Taifa katika kuhabarisha. 

Pia natoa shukrani kubwa kwa wadau, Wanalibeneke wenzangu ndugu na marafiki wanao endelea kuniunga mkono." 
Asanteni sana !

SIKILIZA RHUMBA JIPYA LA ISHA MASHAUZI A.K.A JIKE LA SIMBA

$
0
0
NYOTA wa miondoko ya taarab, Isha Mashauzi amekuja kivingine ambapo ameachia rhumba kali la miondoko ya muziki wa dansi. Ngoma hiyo inakwenda kwa jina la “Nimlaumu Nani”. Ni wimbo wa dakika tano uliorekodiwa katika studio ya Soft Records chini ya producer Pitchou Meshaa. Sauti zote utakazozisikia katika wimbo huu, zimewekwa na Isha Mashauzi mwenyenye – ameimba peke yake mwanzo mwisho.

DK. TIZEBA ATOA MISAADA KWA WAHANGA WA MOTO JIMBONI KWAKE

$
0
0
SAM_0783
Naibu Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles Tizeba akipanda boti kuelekea kisiwa cha Nyamango kulikotokea ajali ya moto kwa ajili ya kukabidhi misaada.

Na Daniel Makaka, Sengerema
NAIBU Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Buchosa Dk Charles Tizeba ametoa msaada kwa wahanga wa ajali ya moto na nyumba zilizoezuliwa na mvua ya upepo katika kisiwa cha Nyamango kijiji cha Lushamba kata ya Bulyaheke jimbo la Buchosa wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.

Misaada aliyoitoa kwa wahanga hao ni Blanketi mia tatu na Magunia manne ya Unga wa Mahindi na moja la Maharagwe vyote vyenye thamani ya shilingi million tatu na laki tano ambavyo vimetolewa kwa kaya hamsini na moja ambazo zilikumbwa na janga hilo Septemba 19 na 20 mwaka huu.

Akikabidhi misaada hiyo Dk Tizeba aliwataka viongozi kuhakikisha misaada hiyo inawafikia walengwa na siyo vinginevyo lakini pia aliwaasa wahanga hao hao kutumia misaada kwa lengo la kuwasaidia wakati kamati ya maafa wilaya ya Sengerema ikiwa bado inaendelea kufanya tathimini il iione namna ya kuwasaidia.
SAM_0723
Naibu Waziri wa Uchukuzi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles Tizeba akiwa ndani ya boti kuelekea kukabidhi misaada katika kisiwa cha Nyamango jimboni kwake.


Workshop Artmobile at The Institute of Arts and Culture Bagamoyo

KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHATOA TAARIFA KUHUSU AWAMU YA PILI YA KAMPENI YA KUSAMBAZA UELEWA WA RASIMU YA PILI-KAMPENI GOGOTA

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dk.Helen Kijo-Bisimba (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akitoa taarifa kuhusu awamu ya pili ya kampeni ya kusambaza uelewa wa rasimu ya pili (Kampeni Gogota). Kulia ni Mratibu wa Dawati la Katiba wa kituo hicho, Anna Henga na Mwanasheria wa Kituo hicho, Harold Sungusia.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

Picha/Habari na Dotto Mwaibale

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu kimedai kuwa Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea linaendeshwa kimabavu kwa kutumia fedha za wananchi bure wakati wakijua fika hakuna katiba itakayopatikana.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadam (LHRC) Dk. Helen Kijo-Bisimba, wakati akitoa taarifa kuhusu awamu ya pili ya kampeni ya kusambaza uelewa wa rasimu ya pili (Kampeni gogota) kwa wananchi.

"Cha kusikitisha ni kwamba tumepoteza mabilioni ya fedha ambazo zingeweza kusaidia kwenye sekta mbali mbali zikiwemo za afya na elimu kwa kuwalipa wajumbe wa bunge la katiba," alisema.

Alisema wakati wa kampeni hiyo ambayo imefanyika kwenye mikoa 20 nchini kituo hicho kimebaini kuwa wapo asilimia kubwa ya wananchi wanakerwa na mwenendo wa mchakato wa bunge hilo kwa kuchakachua maoni yao yaliyokusanywa na Tume ya mabadiliko ya katiba.

Alisema wakati wa kampeni hiyo ya gogota kituo hicho kimefanikiwa kufika kwenye wilaya zote, na kata tatu kwa kila mkoa ambapo kilifanikiwa kurudisha ajenda ya katiba na uelewa wa rasimu ya pili ya katiba kwa wananchi.

Alisema hiyo ni moja ya mafanikio waliyoyapata kuyajua kwa wananchi kwenye kampeni hiyo ambayo ililenga kuhamasisha wananchi kushiriki katika mchakato hususani kufuatilia bunge la katiba na upigaji wa kura ya maoni muda utakapo fika.

Pamoja na mafanikio hayo pia kitu hicho kimekutana na changamoto mbali mbali ikiwemo ya uelewa mdogo kuhusu katiba hususani walio pembezoni mwa miji.

Alitaja mikoa hiyo ni Arusha, Tanga, Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu, Mbeya, Rukwa, Kilimanjaro, Manyara, Katavi, Iringa, Mara, Njombe, Ruvuma, Pemba Kaskazini, Kusini, Pemba mjini Magharibi, Unguja Kusini na Kasazini.

Alitaja changamoto nyingine ni kutokujua kusoma na kuandika kwa baadhi ya wananchi, umangi meza kwa badhi ya viongozi wa mikoa, hofu ya kutopata katiba na mfumo dume kwenye jamii.

Africa Magic Swahili Rebrands!!!

$
0
0
On Wednesday September 24 at 9:00am, in what is destined to be a key moment for M- Net in the market, its existing Africa Magic Swahili that airs on DStv channel 158 and GOtv channel 3 will be rebranded with a new name, and going forward the channel will be known as Maisha Magic Swahili.

This latest development brings the channel in line with the new Maisha Magic identity that the television operator recently launched, a brand which has already been enthusiastically embraced throughout East Africa. Following the launch of the general entertainment focussed Maisha Magic (DStv channel 161) earlier this month, Maisha Magic Swahili is the latest step from M-Net to entrench a more relevant channel brand for the region.

Commenting on the name change, M-Net Director for East Africa Michael Ndetei is positive about the future of Swahili programming, as content in one of the world’s oldest languages remains in high demand. “Africa Magic Swahili was launched in 2011 to showcase Swahili culture and to meet a wide audience demand for such a platform. Now, three years later, while the name may be changing, the objective to celebrate Swahili content still remains central to Maisha Magic Swahili. We are however very excited to be rebranding the channel, as the new name serves to again remind our audiences that our commitment to East Africa is tangible, ongoing and evolving.”

Highlights coming up on Maisha Magic Swahili over the next few weeks include a festival of big name Tanzanian movies made in the past two years. Viewers can tune in on 5th October for Nguvu ya Imani starring Simon Mwapangata and Khadija Mohammed as well as Waves of sorrow on 12th Then on 2nd Omari when the channel screens Trapped.

Other content from Tanzania included on the channel are the series Siri ya Mtungi and High Heels. In addition, audiences can still tune in for the popular favourite Mashariki Mix, hosted in Swahili by the gorgeous, talented Sarah Hassan. Other must-watch programs on the channel include Sumu la Penzi, Ajabu, Kijakazi and Taxi Driver. Plus fans can look out for exciting movie titles from the Africa Magic Original Films initiative, which has also been rebranded in East Africa and is now called the Maisha Magic Original Films initiative.

Meanwhile, you can contribute to the fun conversation about Maisha Magic Swahili by simply following @MaishaMagicSwa on Twitter or by liking the Maisha Magic Swahili page on Facebook. You can also get more information on programming by logging on to www.maishamagic.tv. Maisha Magic Swahili is available 24/7 across all DStv and GOtv bouquets October starring Khadija Mohammed, Rose Ndauka and Vincent Kigosi.

November Rose Ndauka is back on the spotlight alongside Salma Jabu and Salim

NBC WAKUTANA NA MAWAKILI WA MAKAMPUNI MBALIMBALI KWA LENGO LA KUFAHAMIANA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa Benki ya NBC, Pius Tibarazwa, akizungumza katika hafla waliyowaandalia wanasheria kutoka makampuni mbalimbali ili kufahamiana na wafanyakazi wa NBC na pia kuwapa maelezo ya huduma za kibenki zinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika katika kitengo hicho kilichopo ndani ya Jengo la Coco Plaza, Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa Benki ya NBC, Pius Tibarazwa (katikati), akibadilishana mawazo na baadhi ya mawakili waliohudhuria hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wanasheria hao kukutana na wafanyakazi wa NBC na pia kupata maelezo ya huduma za kibenkizinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni, Joseph Ngiloi na Proctus Ishengoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (kulia), akifurahi na baadhi ya mawakili waliohudhuria hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wanasheria hao kufahamiana na wafanyakazi wa NBC na pia kupata maelezo ya huduma za kibenki zinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni, Joseph Ngiloi, Mkurugenzi Mtendaji wa muda wa NBC, Pius Tibazarwa na wakili Proctus Ishengoma.
Meneja Mahusiano ya Wateja wa kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha Benki ya NBC, Subira Mwaya (kushoto) akiwa na Wakili wa Kampuni ya Summit Attorneys, Bilal J. Bilal wakati wa hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wanasheria hao kufahamiana na wafanyakazi wa NBC na pia kupata maelezo ya huduma za kibenki zinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (katikati), akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo katika hafla waliowaandalia wanasheria kutoka makampuni mbalimbali ili kufahamiana na wafanyakazi wa NBC na pia kuwapa maelezo ya huduma za kibenki zinazotolewa katika kitengo cha huduma binafsi za kibenki kwa wateja wakubwa cha benki hiyo.

KESI WAFUASI WA CHADEMA KUVAMIA POLISI YASOMWA LEO MAHAKAMANI

$
0
0
UPANDE wa Jamhuri katika kesi inayowakabili wafuasi watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) umedai mahakamani kwamba washtakiwa hao walikiuka amri halali ya Jeshi la Polisi baada ya kuvuka kizuizi kilichowekwa eneo la Makao Makuu ya  jeshi hilo.

Kadhalika, washtakiwa hao Ngaiza Kamugisha (28)  dereva, mkazi wa Vingunguti, Benito Mwapinga (30) Fundi nguo mkazi wa Mtoni kwa Azizi Ally na Eliasante Bugeji (51) Mhasibu wa CCBRT mkazi wa Komakoma Kinondoni, Dar es Salaam, wanadaiwa kukiuka amri halali iliyotolewa na Inspekta Zuhura ya kuwataka kutoweka eneo la ofisi hiyo.

Madai hayo yametolewa leo na Wakili wa Serikali Mkuu, Bernad Kongola wakati akiwasomea maelezo ya awali mbele ya Hakimu Mkazi Frank Moshi.

Kongola alidai kuwa Septemba 18, mwaka huu katika makao makuu ya jeshi la Polisi, washtakiwa walizuiliwa kuingia eneo hilo lakini walikiuka amri hiyo na kuingia kwa jinai.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa wa tatu, alitoa lugha chafu na matusi kwa Inspekta Zuhura iliyosababisha uvunjifu wa amani.

Washtakiwa walikana maelezo hayo.

Hakimu Moshi alisema kesi hiyo itasikilizwa Septemba 22 na 23, mwaka huu ushahidi wa upande wa Jamhuri.

Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa Septemba 18,mwaka huu, washtakiwa waliingia kinyume na sheria ndani ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwa hali ya fujo.

Alidai tarehe na siku ya tukio la kwanza washtakiwa walikataa kutii amri ya halali ya kutawanyika eneo la makao hayo iliyotolewa na  Inspeta Zuhura, ambaye alitoa amri hiyo baada ya kuruhusiwa na viongozi wake.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images