Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

NAJUA WAJUA YA CAPTAIN GARDINER G. HABASH NDANI YA MICHUZI TV LEO


Article 23

TUNDA MAN ASINDIKIZA SHOW YA VIPAJI WAREMBO MISS TANZANIA BABATI MKOANI MANYARA

$
0
0
 Warembo 15 kati ya 30 wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakisindikizwa na mkali wa Bongo Fleva kutoka Jijini Dar es Salaam, Tunda Man, wametoa burudani kali wakati wa shindano dogo la awali la kumtafuta mrembo mwenye kipaji lililofanyika Babati Mkoani Manyara. Pichani juu ni washindi wa tano waliofanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo la vipaji litakalofanyika jijini Dar es Salaam baada ya wengine 15 kufanyika Arusha mjini. 
 Msanii wa Bongo Fleva  Tunda Man akitoa burudani kwa wadau wa urembo Babati.
 Tunda Man aliburudisha vilivyo ukumbini hapo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Tanzania Yasisitiza Vipaumbele Vya Kitaifa Vipewe Umuhumu

$
0
0
Mhe. Waziri Fatma Fereji kutoka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akizungumza kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kikao Maalum cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kilichofanyika Jumatatu ambapo wakuu wa nchi na wawakilishi wa serikali kutoka nchi 193 walikutana kutathimini Mpango wa Utekelezaji walioupitisha miaka 20 iliyopita huko Cairo, Misri kuhusu uboreshaji wa maisha ya watu na masuala yahusuyo Idadi ya Watu. Mhe. Fereji ni sehemu ya Ujumbe wa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Mhe. Waziri Fatma Fereji akiwa na Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na Naibu wake, Balozi Ramadhan Mwinyi wakati wa ufunguzi wa Kikao Maalum wa ICPD ambapo Waziri Fereji aliongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo.
Kutoka kushoto ni Balozi Ramadhan Mwinyi, Waziri Fatma Fereji wakiwa na Mwakilishi kutoka Ofisi za UNFPA ambaye aliwahi pia kufanya kazi nchini Tanzania akimpongeza Waziri baada ya kutoa mchango wa Tanzania na kulia kabisa ni Dkt. Joyceline Kaganda.

President Kikwete Speaks on Climate Change

$
0
0
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete delivers his opening remarks during a meeting of the Committee of African Heads of State and Government on Climate change(CAHOSCC) held today at the office of the Permanent Observer Mission of the African Union(AU) to the United Nations in New York. On the right is the Chairperson of the African Union Commission Dr. Nkosazana Dlamini Zuma. In his remarks,President Kikwete who is also the Coordinator of CAHOSCC reiterated his call on the need for Africa to speak with one voice in advancing and championing the continent’s common position and interests on Climate Change.
Delegates who attended the session on Climate Change in New York. (photo by Freddy Maro).

NCHI ZA ME ZAWEKEZA ZAIDI KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA UHALIFU MTANDAO

$
0
0
 Ukipitia takwimu za mwaka huu na mwaka jana inaonyesha Nchi za Ulaya na Marekani zimeendelea kuathirika zaidi na uhalifu mtandao, Huku Nchi za mashariki ya kati kuonekana kunyemelewa na wahalifu mtandao. Wakati huo huo takwimu zilitabiria Nchi za Afrika  kuwa katika hali mbaya baadae kutokana na ukuaji wa kasi wa matumizi ya mitandao ambao hauendani sanjari na maandalizi madhubuti ya usalama wa mitandao.

Mengi yalizungumzwa kuhusiana na tishio jipya katika nchi za kiarabu huku kampuni inayojihusisha na ulinzi mtandao ya Kaspersky wakiandika "NCHI YA SAUDI ARABIA" imedhamiriwa zaidi na wahalifu mtandao kauli ambayo iliambatana na "UTAFITI" ukibainisha kampuni za mashariki ya kati zimeendelea kulengwa na wahalifu mtandao.

Hatua hiyo ilisababisha nchi hizo za mashariki ya kati kuwekeza zaidi na kuimarisha jitihada zake za mapambano dhidi ya uhalifu mtandao. "JEDDAH" iliyoko Saudi Arabia ilianzisha kituo kipya kilicho imarishwa maalum kwa ajili ya mapambano dhidi ya uhalifu mtandao na Hivi karibuni "JORDAN" nao wakazindua kituo chao maalum kwa ajili ya kupambana na uhalifu mtandao.

Vile vile nchi nyingine za Mashariki ya kati (ME) zimeendelea kuwekeza na kufungua vituo maalum kwa ajili ya mapambano dhidi ya uhalifu mtandao katika ukanda huo ambapo imeenda sambamba na uboeshwaji wa sharia mitandao.

NINI TUNAJIFUNZA KAMA TAIFA?


Tayari imezoeleka nchi za ulaya na Marekani zimekua vinara kwenye kuwekeza katika mapambano dhidi ya uhalifu mtandao kutokana na athari kubwa ambayo tayari imesha ziona.Na hivi sasa inaonekana Nchi za Mashariki ya kati nazo zikiwekeza katika upande huo. 



Nchi za Afrika pia zimeendelea kujipanga na kkuwekeza kwenye sekta hii ambayo inaonekana kuwa tishiokubwa mapema baadae. Jitihada zilizopo zinapaswa kuendana sambamba na kuweka vizuri sharia mtandao huku itafutwa njia rafiki itakayofungua mipaka kwenye mapambano dhidi ya uhalifu huu mtandao ambao hauna Mipaka.


Maboresho ya mara kwa mara yanahitajika kwenye vituo maalum vya mapambano dhidi ya uhalifu mtandao pamoja na kuwa na mapitio ya sheria mtandao mara kwa mara kutokana na mabadiliko na ukuaji wa teknolojia inayochangia kasi ya uhalifu mtandao kuongezeka. Haya na mengine nimepata kuya ainisha  kwa kina kwenye andiko linaloweza kusomeka "HAPA"

KINANA AITEKA CHALINZE PWANI

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi baiskeli kwa Makatibu Kata.
 Katibu Mkuu wa CCm Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali ya ujenzi wa ofisi za CCM kata ya Kiwangwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wakazi wa kata ya Miono
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kata ya Miono ambapo aliwaambia wawe makini katika kuchagua viongozi wa kijiji ili kuepusha migongano na migogoro ya ardhi zinazodaiwa kuuzwa kwa wawekezaji
 Wakazi wa Jimbo la Chalinze wakisikiliza kwa makini
 Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia wakazi hao na kuwasisitiza juu ya masula muhimu ikiwa kuchagua viongozi bora,kuwapeleka watoto shule ,kujiandikisha huduma za afya ya jamii na matumizi bora ya ardhi.

NAIBU WAZIRI SILIMA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI JIJINI ARUSHA LEO

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Kulia kwa Mwenyekiti ni Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga. Mkutano huo ambao unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika hoteli ya Golden Rose jijini Arusha leo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Kushoto ni Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga. Kulia ni Mwenyekiti wa Mafunzo na Uenezi wa Baraza hilo, Henry Bantu. Mkutano huo ambao unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika hoteli ya Golden Rose jijini Arusha leo.
Katibu wa Baraza la Usalama Barabarani ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga akizungumza na Wajumbe wa Baraza hilo kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani nchini, Pereira Ame Silima. Kulia ni Mwenyekiti wa Mafunzo na Uenezi wa Baraza hilo, Henry Bantu. Mkutano huo unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika hoteli ya Malaika Beach Resort jijini Mwanza leo.
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote chini wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Baraza hilo, Pereira Ame Silima (hayupo pichani) katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Mkutano huo unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika hoteli ya Golden Rose jijini Arusha leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MPANGO WA AWAMU YA PILI WA UTEKELEZAJI WA MAENDELEO YA SEKTA YA MAJI WAZINDULIWA TANZANIA

$
0
0
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Philippe Dongier wakikata utepe kuzindua rasmi Mpango wa Awamu ya Pili ya Utekelezaji wa Maendeleo ya Sekta ya Maji.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Mbogo Futakamba, akisoma hotuba katika uzinduzi rasmi wa Mpango wa Awamu ya Pili ya Utekelezaji wa Maendeleo ya Sekta ya Maji, akiwa na Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Philippe Dongier.
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, akisoma hotuba katika uzinduzi wa Mpango wa Awamu ya Pili ya Utekelezaji wa Maendeleo ya Sekta ya Maji.

TPDC YAKANUSHA UVUMI WA KUAJIRI VIJANA 500 NA KUWAPATIA MASOMO YA MAFUTA NA GESI

TAARIFA KWA UMMA

WAZIRI MKUU AKIWA MKOANI RUKWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua shule ya Sekondari ya Magnificat wilayani Siha Septemba 20, 2014. Kushoto ni mkewe Tunu.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wazee wa Mpanda baada ya kuzungumza na mjini Mpanda Septemba 22, 2014. Alikuwa njiani akitoka Sumbawanga kuelekea Dodoma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua ujenzi wa shule ya Msingi ya Kakuni wilayani Mlele Septemba 22, 2014. Alikuwa njiani akitoka Sumbawanga kuelekea Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Dkt. Rajab Rutengwe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WASANII WASISITIZWA MATUMIZI SAHIHI YA MITANDAO YA KIJAMII

$
0
0
Wasanii wamesisitizwa juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwani waandaaji wa matamasha na matukio mbalimbali ya kisanaa sehemu mbalimbali duniani wamekuwa wakiitumia katika kuwapa kazi.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa lililofanyika mapema wiki hii kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam, mdau wa Sanaa Henry Mdimu alisema kuwa ni jambo la kushangaza kuona wasanii wakitumia kurasa zao kuonesha mambo binafsi kama ya mapenzi na matusi wakati zinapaswa kutumika kwa ajili ya kazi zao za Sanaa na kuwasiliana na mashabiki wao.

Alisisitiza kwamba si kila kitu kinapaswa kuwekwa kwenye kurasa za kijamii za wasanii na kwamba lazima wasanii wajifunze kutenganisha maslahi au masuala yao binafsi dhidi ya yale ya wapenzi wao na kwamba Sanaa iko kwa ajili ya walaji na si wasanii pekee.

“Wasanii hawana budi kuelewa kuwa hawatengenezi sanaa au kurasa za mitandao ya kijamii kwa ajili yao. Wanaitengeneza ili kuwasiliana na mashabiki wao kuhusu kazi wazifanyazo na kutafuta fursa za masoko na kazi nje. Lazima waelewe mapromota wa kimataifa hutumia sana kurasa hizi katika kutoa fursa” alisisitiza Mdimu.

Aliongeza kwamba, msanii yeyote anayefanya kazi ya Sanaa kama kazi yake lazima afikirie kutumia mitandao hii ya kijamii kiweledi katika kujitangaza kwani kutokufanya hivyo ni bora kufanya kazi nyingine maana hiyo ndiyo njia kuu kwa sasa ya kujitangaza na kupata fursa za maonesho mbalimbali ya kimataifa kwa gharama nafuu.

Kwa upande wake Afisa Sanaa kutoka BASATA, Augustino Makame alisema kwamba Baraza limekuwa mstari wa mbele kusisitiza matumizi sahihi ya teknolojia za kupashana habari muiongoni mwa wasanii na kwamba sasa ni muda wa wasanii kuona umuhimu wa mitandao hii ya kijamii na kuitumia ipasavyo katika kukuza Sanaa zao.
Mdau wa Sanaa Henry Mdimu (Kulia) akisisitiza umuhimu wa kuwa na mitandao ya kijamii kwa wasanii (hawapo pichani) katika Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA). Kushoto ni Afisa Sanaa wa BASATA, Augustino Makame.
Afisa Habari wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Aristides Kwizela (Kulia) akisisitiza jambo kwa Wasanii (Hawako pichani) wakati wa Jukwaa la Sanaa lililofanyika mapema wiki kwenye Ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ilala, Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Katikati ni mdau wa Sanaa Henry Mdimu na Afisa Sanaa wa Baraza hilo Augustino Makame.
Wadau wa Sanaa pamoja na Wasanii wakipata elimu kuhusu Nafasi ya Mitandao ya Kijamii katika Kukuza Sekta ya Sanaa kwenye mapema wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA.

Tamasha la 33 la Sanaa lazinduliwa kwa kishindo

$
0
0
 Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere (kushoto) akifuatilia maonyesho mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana, katikati ni Mtendaji mkuu TaSUBa Bw. Michael J. Kadinde na kulia ni Mkurugenzi Maendeleo ya Utamaduni Prof. Hermas Mwansoko.
 Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere kati akipiga ngoma kama ishara ya uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.
 Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere kulia akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TaSUBa Bw. Ghonche Materego wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana. Picha hii imechorwa sura ya Mhe. Makongoro na msanii aliyefaamika kwa jina la Sunday Richard Kamangu.
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere kushoto akimpa mkono wa pongezi msanii Sunday Richard Kamangu baada ya kupokea zawadi ya picha iliyochorwa na msanii huyo wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo kushoto, na Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Bibi. Leah Kihimbi kulia wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokua yanaendelea wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.
 Wasanii kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo wakitoa burudani  wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.

Baadhi ya watazamaji wakifurahia mambo yalivyokua wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana. Picha zote na: Genofeva Matemu - MAELEZO

msaada tutani: Please Vote for us mdau!!

$
0
0
Hello WADAU!

Conservation Interaction has reached the finals of a competition. This is run by the Climate Co-Lab, which is part of MIT University in Boston. I would appreciate your vote on our proposal 'A Collaborative Solutions Communication Platform' which aims to solve climate change problems for coastal communities in Tanzania using our radio programmes and supportive text messages. It only takes a minute to go to http://climatecolab.org/web/guest/plans/-/plans/contestId/1300801/planId/1309001
and vote for our proposal! If we win, not only do we receive a prize of $10,000 but we also present to investors, others NGO's, civil society groups and policymakers. If at all possible, please can you also forward to other anyone else who may be interested in supporting increasing resilience and promoting adaptation to climate change in coastal Tanzania through communicating solutions. Just forward/share/tweet the link! 

Every vote does count!
Asante/Thank you,

Anne-Marie Soulsby MSc.
Director
Conservation Interaction

Registration Number: 0004484

Mobile: +255 (0) 6850 830 47
www.conservationinteraction.org
Skype: annemarie.soulsby
Twitter: Conserveaction

CAREER OPPORTUNITIES

muimbaji wa nyimbo za Injili, Jennifer Mgendi na ujio wa filamu yake mpya "Mama Mkwe"

$
0
0

FILAMU mpya ya muimbaji wa nyimbo za Injili, Jennifer Mgendi iitwayo 'Mama Mkwe' inatarajiwa kuigizwa sokoni siku ya Alhamisi baada ya kukwama kuachiwa jana Jumatatu kama ilivyokuwa imepangwa.
Aidha Muinjilisti huyo amewataka mashabiki wake wasiikose kupata darasa la kutosha.

Jennifer alisema filamu hiyo itaachiwa rasmi Septemba 25 baada ya jana kukwama kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake ikiwa ni wiki kadhaa tangu kumalizika kurekodiwa kwake na kusema kwa ujumbe uliopo ndani yake, mashabiki hawapaswi kuikosa. 

Muimbaji huyo alisema, kisa cha Mama anayeingilia ndoa ya mwanae wa kiume akitaka kupatiwa mjukuu ni mambo ambayo yamekuwa yakiwakumba wanajamii wengi na kusambaratisha ndoa zao bila kutaka.
"Ni mambo yanayotokea ndaniya jamii na kuwaachia watu machungu, sasa waigizaji wameonyesha uhalisia wa mambo namna ndoa nyingi zinavyosambaratika kwa sababu ya mambo kama hayo," alisema.

Katika filamu hiyo, Jennifer ameigiza na wasanii wengine wakali kama kina Mussa Banzi, Bahati Bukuku, Christine Matai, Bibi Esther na wengine.
"Itakuwa mtaani Alhamisi, mashabiki wasikose kuona uhondo huu. Mama Mkwe ni zaidi ya kazi zangu za nyuma kwa namna ilivyosukwa na kutendewa haki na wasanii walioigiza," alitamba Jennifer.

YALE YALEEEE.....

Miradi iliyotekelezwa kwa ajili ya kupunguza msongamano katika halmashauri ya ilala

$
0
0
Afisa Uhusiano wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bi Tabu Shaibu akiwaeleza waandishi wa Habari (Hawapo pichani) waandishi wa Habari kuhusu Miradi iliyotekelezwa kwa ajili ya kupunguza msongamano katika halmashauri hiyo, wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Bw. Frank Mvungi.
Mhandisi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Batimagwa James akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu hatua zinazochukuliwa na Manispaa hiyo katika kuhakikisha barabara zinakuwa kwenye hali nzuri katika kipindi chote cha mwaka.kulia ni Afisa Uhusiano wa Halmashauri hiyo Bi Tabu Shaibu.PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.

PRESIDENT KIKWETE IN DIFFERENT ACTIVITIES IN NEW YORK

$
0
0
 President Jakaya Mrisho Kikwete greets Senator Chris Coons of Delaware who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly. 
  President Jakaya Mrisho Kikwete invites  Senator Chris Coons of Delaware and Chairman of  Perdue Farms Mr Jim Perdue who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly 
 President Jakaya Mrisho Kikwete in talks with  Senator Chris Coons of Delaware and Chairman of  Perdue Farms Mr Jim Perdue and their delegation who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly.

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>