Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 583 | 584 | (Page 585) | 586 | 587 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Shibula iliyoko Mkoani Mwanza wamefaidika na vitabu kupitia mradi wa Airtel shule yetu ambapo Airtel imetoa msaaada wa vitabu vya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni moja na Laki tano vitakavyowawezesha wanafunzi hao kupata elimu bora.

  Kwa zaidi ya miaka 10 sasa mpango huu wa Airtel shule yetu umekuwa ukisaidia shule za sekondari kwa kuwapatia nyenzo muhimu kma vile vitabu, vifaa za kufundishia , madawati, kuboresha majengo ya shule lengo likiwa ni kuboresha ubora katika kutoa elimu nchini.

  Akiongea wakati wa hafla ya kikuabithi vitabu Meneja Mauzo wa Airtel kanda ya Ziwa Bwana Raphael Daudi alisema “ Airtel imewekeza kiasi cha kutosha katika kusaidia malengo mkakatika katika sekta ya elimu kwa kushirikiana na serikali katika kutoa elimu bora. Kwa kupitia mradi wa Airtel Shule yetu tumeweza kuzifikia shule zaidi ya 1000 zilizoko katika maeneo mbalimbali nchini kwa kuwapatia vifaa vya kujisomea na kupunguza changamoto za uhaba wa vitabu huku tukifanikiwa kupunguza uwiano wa kitabu kwa mtoto kutoka watoto 6 kwa kitabu kimoja hadi watoto 2 kwa kitabu kimoja.

  Leo tunatoa vitabu vya masomo ya sayansi ikiwemo Hisabati Fizikia, Kemia na Baiologia kwa shule ya Shibula sekondari tukiamini utachangia katika kuongeza kiasi cha ufaulu na kuchochea wanafunzi wengi kujiunga na masomo ya sayansi. Tutaendelea na jitihada hizi katika kuboresha sekta ya elimu na kuhakikisha tunazifikia shule nyingi zaidi nchini aliongeza Daudi.

  Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ilemema Mkoani Mwanza Juma Kasandiko ameishukuru Airtel kwa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari zilizoko mwanza na kuwaasa wanafunzi kutumia muda wao kujisomea na kuacha tabia ya utoro shuleni na kwa kufanya hivyo kutasaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi shuleni hapo na Mwanza kwa ujumla.

  Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Shibula Bwana James Elias Chitanda alisema” Napenda kuwashukuru Airtel kwa kutoletea msaada huu wa vitabu shule ni hapa, vitabu ni nyenzo muhimu katika kuongeza maarifa na ujuzi hivyo vitabu hivi vitasaidia kuhamasisha wanafunzi wengi kujisomea na kuongeza upeo, vitawasadia walimu kuandaa masomo yao na kuwahamasisha wanafunzi wengi kujiunga na masomo ya sayansi na kuongeza idadi ya wanasayansi kwa ujumla.

  Tunatoa wito kwa makampuni mengine kujiunga na kuchangia katika sekta ya elimu kwani ina mahitaji na changamoto nyingi.
  Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Juma Kasandiko (kulia) akimkabithi vitabu mkuu wa shule ya shule ya Sekondari Shibula James Chisanda vilivyotolewa na Airtel chini ya mpango wake wa Airtel Shule yetu.
  Waalimu wa shule ya Sekondari Shibula wakifurahia vitabu mara baada ya kampuni ya simu za mkononi ya Airte kukabithi vitabu hivyo chini ya mpango wake wa Airtel shule yetu ambapo shule hiyo imepokea vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi millioni moja na Laki tano
  Wanafunzi wa shule ya Sekondari Shibula wakifurahia vitabu vya sayansi walivyokabidhiwa na Kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel, chini ya mpango wa Airtel shule yetu Airtel ilikabithi vitabuvya sayansi vyenye thamani ya shilingi millioni moja na nusu kwa shule hiyo

  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa bodi wa Resolution Insurance, Richard Kasesela (katikati) akikata utepe wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la Karikoo la kampuni hiyo uliofanyika Dar es Salaam leo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Oscar Asir na Mkurugenzi wa Utoaji Bima ya Afya wa Kampuni hiyo, Leonard Chacha.
  Mkurugenzi wa Kampuni Resolution Insurance, Oscar Asir (kushoto) akiwaelekeza mandhali ya ofisi ya tawi jipya la ofisi hiyo iliyopo Lumumba Kariakoo,Mwenyekiti wa bodi wa kampuni hiyo, Richard Kasesela (kulia) na Mkurugenzi wa Utoaji Bima ya Afya wa Kampuni hiyo, Leonard Chacha. 
  Mwenyekiti wa bodi wa Resolution Insurance, Richard Kasesela(katikati), Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Oscar Asir na Mkurugenzi wa Utoaji Bima ya Afya wa Kampuni hiyo, Leonard Chacha wakikata keki kuashilia uzinduzi wa tawi jipya la kampuni hiyo lilipo mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Resolution Insuarance wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Mhe. Andrew Chenge (kushoto) akiwasili bungeni kwa ajili ya kuwasilisha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, leo 24 Septemba, 2014. Kulia ni mjumbe wa Bunge hilo, Dkt. Tulia Ackson.
  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiongoza bunge hilo leo 24 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Bunge Maalu la Katiba, Mhe. Andrew Chenge akiwasilisha Rasimu iliyopendekezwa ndani ya bunge hilo leo 24 Septemba, 2014 mjini Dodoma.

  0 0

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akifungua mafunzo ya siku 27 kwa wakufunzi na wadadisi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar watakaoendesha Utafiti wa Tathmini ya utoaji wa Huduma za Afya nchini 2014/15 leo mkoani Kilimanjaro.
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza na washiriki wa mafunzo ya Utafiti wa Tathmini ya utoaji wa Huduma za Afya nchini leo mkoani Kilimanjaro.
  Mkufunzi wa mafunzo ya wasimamizi na wadadisi wa Utafiti wa Tathmini ya Utoaji wa Huduma za Afya nchini Bi. Saumu Said akiendelea kutoa mafunzo kwa washiriki wa utafiti huo mkoani Kilimanjaro leo.


  0 0


  0 0


  0 0


   There has recently been a noticeable increase in the number of people importing used vehicles directly from Japan. This rise in popularity has given way to some very common mistakes people make when importing them for the first time, and this article highlights the key points and terms you should be aware of in order to import vehicles successfully from Japan.


  1.    The complete cost of import.
  Many first-time car importers lack the basic knowledge of the complete cost along with the peripheral costs associated while importing vehicles from Japan, and this is one of the areas where they commonly fall flat.
  Let’s start by examining the costs you should bear in mind when importing used vehicles.

  The first step you’ll most likely take when importing vehicles is you’ll go to car-exporters’ website. You’ll first of all check the condition of the vehicles, and the cost payable to the exporter.

  Cost of the vehicle (FOB):
  You will find most companies listing the prices of the vehicles in FOB – this refers to the cost of the vehicle. FOB which is short for Free on Board, represents the complete cost until the vehicle is loaded onto a ship in Japan.

  Freight:
  The freight charge is for the cost of delivery from Japan to your nearest/selected port (such as Dar es Salaam). It is very commonly calculated by the dimension of the vehicle, m3 = height x width x length, therefore freight for compact cars would be cheap, and trucks and buses more expensive depending on their sizes.
  The freight charges can differ widely from one company to another, so please take that into account when comparing prices.


  Insurance (Warranty)
  This is another element that differs widely between many companies, because the terms and conditions of what Insurance covers depend on which company you purchase from. Some companies’ insurance is limited to only covering the loss of the vehicle in the event that the ship carrying the vehicle sinks, while other companies offer their own, specifically devised Warranty which additionally covers various break-downs and theft.
  Please make sure you check the details of what insurance covers before your purchase.

  The total amount payable to the Japanese car exporter is referred to as the CIF price, and we get this price if you combine the cost of the car (FOB) + Freight + Insurance. For example, even if the FOB price of the vehicle is just $100, you might find the CIF price to amount to $2,000 after you combine freight charge and insurance.

  We will now take a look at the costs you need to consider after the ship carrying your vehicle has left Japan.

  Duty/Tax:
  Many first-time car importers purchase vehicles from Japan without the full knowledge of how much tax they must pay in order to register vehicles in their countries.
  How much you will have to pay will of course depend on many elements, such as the type of vehicles, engine sizes, and the countries you’re registering the vehicles in, but tax very commonly costs anywhere between 45%~80 of the CIF price. It is therefore highly advisable that you check with shipping agents or national tax offices to get the most detailed information.

  Clearing Fee:
  This is the customs fee you need to pay clearing agents at ports or borders.
  The payable fee is variable according the size of the vehicles, so please also check with clearing agents for the most detailed information.

  Inland Transportation Fee:
  The cost of bringing the vehicle home from the port. If you plan to go to the port and drive the vehicle back home yourself, you will need to calculate travel expenses, accommodation, food, fuel among others. You need to consult freight forwarders for their fees if you plan on using their services.

  Registration Fee:
  The cost of registering, and having a number plate issued for your vehicle.

  We have as above explored the complete cost typically associated with importing vehicles from Japan. Please make sure to remember that there are additional costs you need to consider after your payment to the Japanese car exporters, as outlined in the article above.

  2.  Reasons behind low prices?
   You may have heard stories of how people found their newly imported vehicles to have been in bad, sub-standard conditions. This seems to quite frequently happen when the price of the vehicle was purchased at an extremely low price.

  It is worth going through at this stage in the article, how vehicles are sourced and priced.

  Most used-car exporting companies source their vehicles from car auctions. Local Japanese car-dealers source their vehicles from the same auctions too.
  Many vehicles are listed, and many car dealers try to outbid each other for the vehicles.
  The final bidding prices on those units of the same model and year tend to be roughly in line with one another, but there are many conditions that can influence the prices, such as the condition of the exterior, the engine and the mileage. If a vehicle is found to have malfunctioning engine and very high mileage (e.g. more than 200,000km), the final bidding prices tend to be much lower.
  A trusted car exporter might still choose to purchase these kinds of vehicles, but they will thoroughly refurbish these themselves in their garage before putting them out for sale, although this will obviously mark up the prices due to the cost of refurbishment.  They might alternatively choose to list the vehicles as they are, but with the information about the conditions on full show to their customers for the most transparent purchase.  

  What we need to be very wary of are those companies that attract their customers with very low prices, while hiding the information about the bad condition of the vehicles. If the purchase is being done under the full knowledge of the problem points of the vehicles, it shouldn’t leave any sour tastes in anyone’s mouths, but there are some companies that purposefully don’t show these points to their customers, or rewind the mileage before selling the units.
  The prevailing point is that most companies source their vehicles from auctions, so there will be reasons if one company is selling vehicles at well below the market prices.   It is therefore very advisable to approach with caution to any offers that seem to be too good to be true.
   
  3. Receiving the vehicle safely at the port.
  There have also been some unfortunate incidents of some people damaging the vehicles after their arrival at the port, through not handling them properly.
  It is worth noting at this point that, it is standard practice to leave only the minimum level of engine oil and gasoline in the vehicles before loading them into vessels. They do this to limit the risks of explosion during transit.

  Consequently, it is advisable to check the level of engine oil when you receive the vehicles at the port, as too little engine oil can lead to over-heating, extensive engine damage and a huge repair bill. It is also wise to leave the engine running on idle for 10 to 30 minutes before setting off for the first time, because the vehicles would have been immobile for around four weeks during transit, and they need time to warm up to avoid unnecessary break-downs.

  Please don’t be too alarmed or concerned if the engine doesn’t start on ignition at first. It could very well be that it is just flat (not dead) after such a long time in transit, and all it will likely need is a simple recharge.
   
  You could save yourself many unnecessary troubles on your vehicles simply by passing on your requests to your clearing agents or freight forwards, outlining the three main points as discussed above.

  If you’re thinking of importing a vehicle from Japan in the near future, you might like to consider purchasing from the used Japanese vehicle website CardealPage, which is rapidly gaining recognition and popularity.
  CardealPage has many remarkable features that make it stand out from other sites.

  1.    You can purchase vehicles offered by many famous car exporters.
  On CardealPage, you will find thousands of vehicles listed by several big-name car exporters, so you really shouldn’t have any troubles finding the right car for yourself.   You can see every vehicle listed in its all-inclusive CIF price, so price comparison becomes easy and extremely convenient.


  2. You can purchase vehicles directly from local car dealers in Japan.
  CardealPage also offers you opportunities to purchase directly from local car dealers in Japan, with CardealPage acting as agents.
  Drivers in Japan sell their vehicles to local car dealers, these vehicles are then listed on auctions, and they are then sold to the winning bids by various car exporters.   However, some local car dealers choose to list them on CardealPage instead of putting them out on auction, so you could be driving a vehicle that was being driven in Japan only until yesterday. 

  So why not go to CardealPage to choose your vehicle? It is packed with exciting features that aren’t found on any other sites, and your dream car can be just a few clicks away!  0 0

   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa kikao cha Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika kichozungumzia masuala ya saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti na saratani ya tezi la kiume huko New York tarehe 24.9.2014. 
   Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Penehupifo Pohamba, Mke wa Rais wa Namibia muda mfupi kabla ya kuhudhuria mkutano Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu masuala ya saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti na saratani ta tezi la kiume (prostate cancer) huko New York tarehe 24.9.2014. Mkutano huo umefadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Taasisi ya Princess Nikky Global Initiative ya nchini Nigeria. 
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Debby Rechler (wa kwanza kulia) akifuatiwa na Yvonne Feinstein ambao ni wafanyakazi wa Tanzania Children Fund wakati wa mkutano wa Wake wa Marais uliofanyika huko New York nchini Marekani tarehe 24.9.2014. Aliyesimama kushoto kwa Mama Salma ni Jill Bishop, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya TET Foundation ya Marekani.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  1.   UTANGULIZI

  Binadamu hakuumbwa katika ombwe, ameumbwa akiwa katika dimbwi la majukumu, kwake binafsi, familia, jamii na dunia kwa ujumla. Wachache sana wanaoweza kupitia ngazi zote za uwajibikaji huu. Katika hao wachache, hatutasita kumtaja Jakaya Khalifan Mrisho Kikwete. Ili kujijenga vema katika misingi ya uongozi, Jakaya Kikwete alijijenga vema katika taasisi hizi za msingi na alipikwa vema.

  Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni aina ya kiongozi pekee ambaye alihudumu nafasi mbalimbali ndani ya chama na serikali. Safari yake ya uongozi ilianzia ndani ya chama cha TANU. Alikuwa kiongozi wa Vijana wakati wa TANU na baadaye CCM hadi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi.  Wakati wote katika nafasi zake kwenye chama na serikali, Mh. Kikwete alihimiza maendeleo katika Jimbo lake na watanzania kwa ujumla.

  Kimsingi amekuwa chachu ya maendeleo katika kipindi cha urais wake kuanzia mwaka 2005 hadi 2014 ambapo ameshatekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambapo mingi imeshakamilika na mingine inategemewa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2015.


  0 0

  Madereva hapa nchini wametakiwa kufuata sheria ya matumizi bora ya barabara ili kuepusha madhara yanayosababisha kupoteza maisha ya watu,ulemavu wa kudumu na upotevu wa mali.

  Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani inayofanyika kitaifa mkoani Arusha,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya uagizaji wa magari nchini ya Be Forward Tanzania,Daniel Mtaalam amesema njia hiyo ndio suluhu za ajali zinazotokea mara kwa mara.

  Amesema wao kama wadau wa barabara wamekua miongoni wa wadhamini wakuu wa Wiki ya usalama barabarani katika kuhakikisha sheria za zinazingatiwa ili kuepusha hasara zinazojitokeza pindi ajali zinapotokea.Wadhamini wengine ni kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom na kampuni ya mafuta ya Puma.

  “Iwapo madereva watazingatia matumizi sahihi ya sheria za barabarani ,naamini ajali zitapungua kwa asilimia kubwa jambo ambalo litakuza uchumi wa Mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.”alisema Daniel

  Kampuni ya Be Forward Tanzania ni waagizaji wakubwa wa magari kutoka nchini Japan wakitoa huduma katika nchi mbalimbali kusini mwa jangwa la Sahara huku wakiwa wametoa ajira kwa watu zaidi ya 250 wanaofanya kazi katika idara mbalimbali.

  Amebainisha kuwa mchango wa kiuchumi unaotokana na kampuni hiyo hapa nchini ni mkubwa kwani kila mwezi wastani wa magari elfu kumi huagizwa kupitia bandari ya Dar es Salaam hatua inayoongeza mapato ya nchi kwa ujumla.

  Kwa upande wake, Afisa Ubora wa kampuni hiyo,Lazaro Elias alisema kutokana na kuwa ni wadau wa usalama barabarani wataendelea kuiunga mkono serikali katika kutoa elimu ya matumizi sahihi ya barabara ili kuokoa maisha ya watu.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo(kulia)akimkabidhi Ngao Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya uagizaji wa magari ya Be Forward Tanzania Co.LTD,Daniel Mtaalam ya kuwa Mdhamini Mkuu wa Wiki ya Usalama barabarani.

  0 0


  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula katikati akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Jengo jipya la Ofisi ya CCM wilaya ya Chato. Wengine katika picha ni Mbunge wa Chato Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Geita Said Magalula, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Msukuma.
  Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula kulia mara baada ya kumpokea katika kata ya Buseresere Mkoani Geita. Kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita ndugu Joseph Msukuma
  Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula juu ya gari akihutubia mamia ya wakazi wa Buseresere mara baada ya kuwasili katika eneo hilo.


  0 0
 • 09/25/14--03:12: Article 19


 • 0 0

  KUNDi la muziki wa Injili la Glorious Celebration la jijini Dar es Salaam limethibitisha kushiriki katika uzinduzi wa albamu ya Uko Hapa ya msanii John Lissu.

  Uzinduzi wa albamu hiyo unatarajiwa kufanyika Oktoba 5 mwaka huu, kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, ambapo waimbaji mbalimbali watakuwepo.

  Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions inayodhamini uzinduzi huo, Alex Msama ilisema maandalizi muhimu kuhusiana na uzinduzi huo yamekamilika.

  Msama alisema katika taarifa hiyo kuwa anashukuru wasanii hao kukubali kutumbuiza, ambapo pia atakuwepo msanii mahiri nchini Rose Muhando pamoja na kwaya mbalimbali.

  Glorious wanatamba na albamu mbalimbali ikiwemo ya Niguse yenye nyimbo za Unaweza Yesu, Ee Roho, Juu ya Mataifa, Mawazo, Ameni Haleluya, Nafsi Yangu, Nakupenda Yesu, Usilie na Niguse.

  Msama alisema mbali na Glorious, kuna waimbaji wengine galacha wa nyimbo za injili wamethibitisha kushiriki.

  Albamu ya Lissu ambaye ana sifa ya kupiga muziki wa live ina nyimbo 18 zilizogawanywa katika maeneo mawili, ambazo ni Wakusifiwa, Wastahili Sifa, Mataifa ya Kujua, Inuka, Uko Hapa, Nijaze, Nitaongozwa, Wastahili Bwana, Roho Mtakatifu, Mtakatifu na Umeinuliwa.

  Nyingine ni Yu Hai Jehova, Atikisa, Nijaze, Upendo, Mataifa Yakujue, Umejawa na Ukuu, Fungua Macho, Haleluya na Mungu Ibariki.

  0 0

  Kamati ya Lugha na utamaduni, Jumuiya ya Watanzania Washington DC, Maryland na Virginia (DMV) inapenda kuwaalika wana DMV na wadau wote wa Lugha ya Kiswahili kwenye mkutano na viongozi wa Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) utakaofanyika siku ya Ijumaa Septemba 26, 2014 kuanzia saa nane mchana. Hii ni Fursa ya kukutana wa Wahadhiri wa lugha ya Kiswahili kutoka Vyuo mbali mbali hapa Marekani kwa lengo moja la kuendeleza lugha yetu ya Kiswahili. Anuani ya Ukumbi wa Mkutano vitafuata baadaye.
  Songa mbele na Kiswahili.
  Tunaomba wale mtakaoweza kuhudhuria kujiandikisha na kama unaswali pia wasiliana kupitia Mwanakamati na Kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania hapa DMV wafuatao hapo chini:
  Mwanakamati Mkuu: Bi. Asha Nyang’anyi (301) 793-2833 
   Makamu Katibu ATC-DMV : Mhe. Bernadeta Kaiza 240-704-5899
                                              

  0 0

  Kutoka kushoto ni Gwiji wa muziki wa dansi nchini Mzee Kassim Mapili akiwa amekaa kwenye kitanda cha hospitali ya Taifa Muhimbili  kushoto ni Rais wa Shirikisho la Muziki wa Dansi Tanzania Addo November alipokwenda kumjulia hali  leo asubuhi hospitalini hapo.

  NA BONGOWEEKEND BLOGSPOT.COM
  HALI ya mwanamuziki nguli Kassim Mapili aliyelazwa katika Hospitali  ya Taifa  Muhimbili katika kitengo cha moyo inaendelea vizuri imehafamika.
  Mapili ambaye awali alilazwa katika Hopitali ya  Mwananyamala  kutokana na kusumbuliwa na  maradhi ya mapafu kujaa maji  pamoja na moyo kujaa maji ambako alilazwa kwa muda wa siku nne kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Muhimbili juzi  mchana.
  Hayo yalisemwa leo na Rais wa Shirikisho la Muziki  Addo November  ambaye aliefika hospitalini hapo mapema asubuhi kumjulia hali Mapili  ambapo alikiri kuwa amelazwa katika wodi  namba moja  katika Taasisi ya Moyo baada ya kutolewa  katika wodi ya uangalizi maalumu (ICU), Muhimbili.
  Aidha November ametoa rai kwa wadau na wanamuziki  viongozi  mbalimbali  kujitokeza kwa wingi kwenda kumjulia hali gwiji huyo wa muziki ikiwa ni sehemu ya kumpa faraja kwa ujumla.
   “Mzee wetu anaumwa sana na amevimba sana  miguu hivyo  ni wajibu wa kila mmoja wetu kutoa msaada wa hali na mali” alisema November.
  Wakati Mapili akiwa amelazwa mama yake mzazi  aliyetajwa kwa jina la  Hajena Mussa  Mchikita amefariki usiku wa juzi nyumbani kwake Nachingwea  na atazikwa  leo mkoani Songea alisema November .

  Mapili  alitamba na nyimbo za ‘Rangi ya Chungwa’, ‘Mayasa’ ambao aliuimba na Marehemu TX Moshi William enzi za uhai wake  na kutamba vilivyo katika miaka ya 1980.

  0 0

  Na Fatma Salum-Maelezo

  Serikali imejipanga kutatua tatizo la makazi kwa watumishi wa umma kwa kujenga nyumba Elfu 10 za gharama nafuu kote nchini.

  Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bw.Elius Mwakalinga wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na wakala huo jijini Dar es Salaam na Pwani.

   Mwakalinga alisema kuwa  mradi huo wa nyumba elfu 10 unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 18 unahusisha nyumba za viongozi na watumishi wa kawaida wa kada zote.

  “Lengo la kujenga nyumba hizi ni kuwapatia  watumishi wa umma makazi bora jirani na maeneo yao ya kazi ili kuongeza tija katika utoaji huduma kwa wananchi. Mradi huu utawawezesha kupata nyumba za kupanga na  kununua kwa gharama nafuu”.  Alisema Mwakalinga.

  Akifafanua zaidi  Mwakalinga alisema kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zinatokana na ruzuku ya serikali pamoja na fedha za TBA ambapo kwa mkoa wa Dar es Salaam nyumba hizo zimeanza kujengwa kwenye maeneo ya Bunju, Mbezi Beach, Ada Estate na Masaki na pia eneo la Chalinze mkoani Pwani.

  Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Ushauri kutoka TBA Bw. Edwin Nnunduma alisema kuwa ujenzi wa nyumba hizo unatumia teknolojia ya kisasa inayopunguza gharama na muda wa kukamilika.

  Pia Nnunduma alisema mpaka sasa ujenzi unaendelea vizuri kwenye mikoa mbalimbali nchini ikiwemo mikoa mipya ya Katavi, Geita, Simiyu na Njombe.

  Naye Meneja wa Kikosi cha Ujenzi cha TBA Mhandisi Wilfred Dungamu alieleza kuwa kwa sasa wakala huo unatumia kikosi cha wahandisi wa ndani kilichoanzishwa mwaka 2012 na mpango huo umesaidia kupunguza gharama kubwa zilizokuwa zikitumika kuwalipa wahandisi kutoka makampuni binafsi.  

  0 0

  Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimkabidhi Mhe. Victor Negrescu Mbunge wa Bunge Ulaya vitabu vya kuitangaza Tanzania. Mhe. Negrescu ni kati ya wabunge vijana sabini wa Bunge la Ulaya na leo hii alimtembelea Balozi Kamala ofisini kwake Brussels.

older | 1 | .... | 583 | 584 | (Page 585) | 586 | 587 | .... | 3272 | newer