Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

Benki ya Exim yaingia ubia kuongeza ufanisi katika udhibiti wa majanga

$
0
0
 Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano kutangaza kuingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London ikishirikiana na  StraitsBridge Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM). Wakishuhudia wa kwanza kulia ni Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Maurice Kilavuka na Bw. Laurent Chauvet (wa kwanza kushoto).
 Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala (watatu kulia) akibadilishana hati na Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Maurice Kilavuka (wapili kulia) wakati benki hiyo ilipoingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London ikishirikiana na  StraitsBridge Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM). Wakishuhudia wa kwanza kulia ni Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu wa Ndani, Bw. Goerge Binde na Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Laurent Chauvet (wa kwanza kushoto).
 Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala (kushoto) akibadilishana hati na Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Maurice Kilavuka (kulia) wakati benki hiyo ilipoingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London ikishirikiana na  StraitsBridge Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM)
Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti Majanga wa Benki ya Exim, Bw. David Lusala (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano kutangaza kuingia ubia na kampuni ya Hymans Robertson ya London ikishirikiana na  StraitsBridge Advisors (SBA) ya Singapore katika utoaji wa huduma kwenye masuala ya UdhibitI Majanga ijulikanayo kama Enterprise-Wide Risk Management (ERM). Wakishuhudia wa kwanza kulia ni Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu wa Ndani, Bw. Goerge Binde, Mwakilishi toka Hymans Robertson Bw. Maurice Kilavuka (wapili kulia), Mkuu wa Kitengo cha Hazina wa Benki ya Exim, Bw. George Shumbusho (wakwanza kushoto) na Mwakilishi toka Hymans Robertson  Bw. Laurent Chauvet (wa kwanza kushoto).

WAMA KWA KUSHIRIKIANA NA UNICEF WAANDAA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WALIMU WA SEKONDARI WAMA-NAKAYAMA

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Uragibishi na Mawasiliano kutoka Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Ndugu Philomena Marijani akiwakaribisha walimu na wageni waalikwa wakati wa sherehe ya ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama iliyoko katika Kijiji cha Nyamisati huko Wilayani Rufiji yaliyofanyika shuleni hapo tarehe 15.9,2014.
Baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufungunzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu haokatika masuala ya jinsia na stadi za maisha. Hotuba hiyo ilikuwa ikitolewa na Mkurugenzi wa Elimu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Dkt. Mikidadi Alawi (hayupo pichani) tarehe 15.9.2014.
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu katika Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Dkt. Mikidadi Alawi akifungua rasmi mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama. Waliokaa kushoto kwake ni Ndugu Obeth Mwakatobe, Makamu Mkuu wa Shule akifuatiwa ni Mwezeshaji wa mafunzo hayo Ndugu Anitha Masaki kutoka Shirika la FAWE na Kulia kwa Mgeni rasmi ni Ndugu Philomena Marijani kutoka WAMA. Mafunzo hayo ya siku tano yalifunguliwa rasmi tarehe 15.9.2014 na yameandaliwa na Taasisi ya WAMA wakishirikiana na UNICEF.
Mwezeshaji wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama Ndugu Anitha Masaki kutoka Shirika la FAWE (Forum For African Women Educationalists-Tanzania Chapter) akitoa moja ya mada zake mara tu baada ya ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo shuleli hapo tarehe 15.9.2014.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama mara baada ya ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo tarehe 15.9.2014. PICHA NA JOHN LUKUWI.

Court hears a case against the Government of Uganda on a hydro power unit construction dispute

$
0
0
The East African Court of Justice First Instance Division, today heard a matter seeking the determination of the Court on a case challenging the Memorandum of Understanding (MoU) that was signed between the Republics of Uganda and China to construct Kaluma Hydro Power Unit 600MW in Uganda. 

The Applicant, Mr. Henry Kyarimpa represented by his Lawyer Mr. Mohamed Mbabazi asked the Court to find that the MoU signed by Uganda and China was an infringement of the provisions of the Treaty for the Establishment of the East African Community on fundamental principles of good governance, democracy and rule of law, Articles 6, 7 and 8 of the Treaty. He also asked the Court to interpret Article 38 (2) of the same.

Mr. Mbabazi submitted that there were court orders issued on 18 and 22 April 2013 by the Uganda High Court Nakawa and after those orders on 23 of the same month the contract committee went ahead and cancel all bids which according to the Applicant is a violation of the Treaty provisions.

Among those court orders were for the Government of Uganda (the Respondent) to preserve the status queue (maintain the existing situation), ordering the award of the contract to the best evaluated bidder for the engineering, procurement and construction contract for 600MW Karuma Hydro Power and the status queue be maintained. Mr. Mbabazi said that none compliance by the Government of Uganda with the Court’s order is an infringement of the Treaty because the awarding of the contract was done outside the procurement process. 

Mr. Bafirawala Elisha, Senior State Attorney and Mr. Richard Adrole State Attorney also Counsels for the Respondent urged that at the time when the High Court of Nakawa issued the order, there was no best evaluated bidder, there was no statute restraining the government from proceeding with the new procurement process and the Inspector General of Government (IGG) had issued a cancellation report to the Ministry of Energy and Minerals to stop the procurement process because it was allegedly riddled with bribery and corruption. He also urged that the government of Uganda not being satisfied with the High Court order mentioned above, it is in the process to of appealing. 

 Mr Adrole added that in a bi-lateral arrangement between the government of Uganda and China signed July 2013 does not touch the Karuma dam construction but other areas of development. He concluded that, Uganda therefore nullified the previous procurement process after investigations by the IGG and found out the process was not accurate and not recommended by the Ministry of Energy and Minerals of Uganda as well which led to the cancellation of the previous procurement process and now the government in the implementation of the new one. 

He also said that Section 75 of the Public Procurement and Disposal of Public Assets Act (2003), gives powers to the procurement committee to reject any or all bids at any time prior to the award of the contract.

The Court will deliver the Judgment on notice.

The hearing came before Hon. Mr. Justice Jean Bosco Butasi, Principal Judge, Hon. Isaac Lenaola, Deputy Principal Judge, Hon. Dr. Justice Faustin Ntezilyayo, Hon. Lady Justice Monica Mugenyi and Hon. Mr. Justice Fakihi A. Jundu 

Mdau Innocent Mungy ndani ya kipindi cha mawazo huru

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA TATU WA AFRIKA KUHUSU MASUALA YA USIMAMIZI WA KODI

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi mkutano mkuu wa tatu wa Afrika kuhusu masuala ya usimamizi wakodi uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo Septemba 16, 2014.
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua rasmi mkutano mkuu wa tatu wa Afrika kuhusu masuala ya usimamizi wakodi uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo Septemba 16, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (wa pili kulia) wakiwa meza kuu na baadhi ya viongozi wa TRA wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa tatu wa Afrika kuhusu masuala ya usimamizi wakodi uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo Septemba 16, 2014.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, waliohudhuria mkutano huo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo Septemba 16, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa TRA, baada ya kufungua mkutano mkuu wa wa tatu wa Afrika kuhusu masuala ya usimamizi wakodi uliofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree, jijini Dar es Salaam, leo Septemba 16, 2014. Picha na OMR

RAIS WA ZANZIBAR AENDELEA NA ZIARA YAKE COMORO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mawaziri mbali mbali wakati alipowasili katika Ikulu ya Comoro kwa mazungumzo na Rais wa Nchi hiyo Dr. Ikililou Dhoinine jana akiwa katika ziara ya kiserikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine Ikulu Mjini Comoro jana,Dk.Shein yupo Comoro kwa ziara ya kiserikali akiwa na ujumbe aliofuatana nao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine baada ya mazungumzo Ikulu Mjini Comoro jana,akiwa katika ziara ya kiserikali na ujumbe aliofuatana nao.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwa na Mke wa Rais wa Jamuri ya Muungano wa Comoro Mama Dhoinine wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine katika viwanja vya Ikulu ya Comoro jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteta na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine Ikulu Mjini Comoro jana, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ujumbe Serikali ya Mapinduzi ukiwa katika ziara Nchini Comoro.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Rais wa Jamuri ya Muungano wa Comoro Dr.Ikililou Dhoinine wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa ujumbe Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika ziara ya kiserikali nchini Comoro. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Ujumbe wa CPA watembelea Bunge la Singapore

$
0
0
Kiongozi wa Msafara wa Ujumbe wa CPA Kanda ya Afrika Mhe Zitto Kabwe akiwasilisha ujumbe maalum wa CPA kwa Bunge la Singapore ambayo ilipokelewa na Dr Lam Pin Min ambae pia ni Naibu Waziri wa Afya wa Singapore na Mwakilishi wa CPA Kanda ya Asia Kusini(kulia).
Ujumbe wa CPA katika mazungumzo na Uongozi wa CPA Bunge la Singapore.
Picha ya pamoja. Picha kwa hisani ya Ofisi ya Bunge.

Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Wizara ya Mambo ya Nje akutana na Balozi wa China nchini

$
0
0
Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (kulia) akutana na Balozi wa China nchini Mhe. Lu Youqing,  kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano kati ya Tanzania na China yatakayofanyika nchini China mwezi Oktoba 2014.  
Maafisa kutoka Hazina na Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo hayo kwa makini. 
Maafisa walioambatana na Balozi wa China wakinukuu mazungumzo kati ya Balozi Mbelwa na Balozi Lu Youqing (hawapo pichani).
Kikao kikiendelea.
Picha na Reginald Philip

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Utumishi azindua kampeni ya upimaji afya kwa Watumishi

$
0
0
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi (kulia) akichukua kipimo kuzindua kampeni ya upimaji Afya kwa Watumishi wa Umma hasa Virusi Vya Ugonjwa wa UKIMWI (VVU), zoezi hilo limefanyika Ofisini kwake mapema leo.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAb Mkwizu (wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na watumishi wengine wakati wa zoezi la kupima afya kwa Watumishi wa Umma hasa VVU mapema leo, Ofisi ya Rais-Utumishi.
ehemu ya Maofisa na Viongozi waliohudhuria zoezi la upimaji afya kwa Watumishi wa Umma lililofanyika leo Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dar es salaam.

BLOG YA VIJIMAMBO YAKABIDHI MCHANGO WAKE WA KUSAIDIA KUPAMBANA NA UJANGILI KWA MHE. LAZARO NYALANDU

$
0
0
Baraka Daudi, Mwenyekiti wa Tamasha la Utalii na kukemea ujangili lililoadhimisha miaka 4 ya Blog ya Vijimambo akimkabidhi pesa tasilimu $1,000 kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu kwa ajili ya kupambana na ujangili makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani siku ya Jumatatu Sept 15, 2014
Mhe. Lazaro Nyalandu, Balozi Leberata Mulamula Afisa Ubalozi Suleiman Saleh (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Vijimambo Baraka Daudi na Mayor Mlima baada ya makabidhiano ya pesa ya kupambana na Ujangili

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AAGIZA MAMLAKA ZA HALI YA HEWA KUSINI MWA AFRIKA KUSHIRIKIANA KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZA HUDUMA ZA HALI YA HEWA KATIKA KANDA YA SADC

$
0
0
Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa niaba ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa mwenyeji wa mkutano wa kila mwaka wa umoja wa taasis za hali ya hewa katika nchi za Kusini mwa Afrika (MASA).

Mkutano huo unafanyika mkoani Arusha. Akifungua mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Jowika W. Kasunga alizitaka taasis za hali ya hewa kusini mwa Afrika ikiwemo TMA kushirikiana katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya hali ya hewa. ‘Wote tunakubaliana kwamba umoja ni nguvu, hivyo taasis za hali ya hewa zinapaswa kudumisha umoja na ushirikiano ili kukabiliana na changamoto zinazozikabili huduma za hali ya hewa kusini mwa Afrika’ alisema Mhe. Kasunga.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa ya Malawi na Mwenyekiti wa umoja huo alisema, lengo kuu la mkutano huu ni kujaribu kutatua changamoto za taasis za hali ya hewa kusini mwa Afrika.

Kwa niaba ya TMA, Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi aliwakaribisha wageni wote Arusha na kuwatakia majadiliano yenye mafanikio. Dkt Kijazi alisema ni matarajio yake kwamba mkutano huo utatoa mapendekezo yatakayoweza kuboresha huduma za hali ya hewa katika nchi za kusini mwa bara la Afrika.

MASA ni umoja wa taasis zinazotoa huduma za hali ya hewa kusini mwa Afrika (SADC) wenye lengo la kuboresha huduma za hali ya hewa kwa nchi za ukanda wa kusini mwa Afrika. MASA ni umoja ulioanzishwa kisheria wenye katiba, mpango kazi na Bodi. Wajume wa Bodi ni wakuu wa taasis za hali ya hewa katika nchi za SADC ambapo nchi tano (5) ni wajumbe wa Bodi. Nchi hizo ni Malawi,Zimbabwe,Zambia, Afrika Kusini na Tanzania
IMETOLEWA NA MONICA MUTONI - MAMLAKA YA HALI YA HEWA
TANZANIA.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa nane wa umoja wa taasis za hali ya hewa kusini mwa Afrika, Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Jowika Kasunga (wan ne kutoka kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa TMA ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya MASA na mwenyeji wa mkutano huo Dkt. Agnes Kijazi katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo.

VODACOM YAZINDUA HUDUMA MAALUM KWA WAFANYABIASHARA WA JUMLA NA REJAREJA

$
0
0
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa (katikati) akiongea na waandishi wa habari wakati akizindua huduma ya LIPA KWA M PESA inayowawezesha wasambazaji wa huduma kupokea malipo ya mauzo kwa njia ya M-pesa kutoka kwa wauzaji wajumla. Kampuni ya Chai Bora na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia wasamabzaji wake kampuni ya Mahawi zimkuwa miongoni mwa wasambazaji wa awali kutumia huduma hiyo. Wengine pichani ni Mwakilishi wa Mahawi Enterprises Joseph Mahawi na kulia ni Meneja wa maendeleo ya Biashara wa Chai Bora Martin Ng’ethe.
aadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na Chai Bora wakifuatilia mkutano wa waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa huduma mpya ya LIPA KWA M PESA inayowawezesha wasambazaji wa huduma kupokea malipo ya mauzo kwa njia ya M-pesa kutoka kwa wauzaji wajumla. Kampuni ya Chai Bora na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia wasamabzaji wake kampuni ya Mahawi zimkuwa miongoni mwa wasambazaji wa awali kutumia huduma hiyo.

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF WATIMIZA MIAKA 15 TOKEA KUANZISHWA KWAKE

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa pensheni wa PSPF, Bw Adam Mayingu akizungumzia mafanikio ya mfuko wa PSPF katika kipindi cha Miaka 15 tokea kuanzishwa kwake katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo katika Ukumbi wa JB Belmonte Jijini Dar.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari- Maelezo, Bw Assah Mwambene akizungumza jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari na Viongozi wa Mfuko wa Hifadhi wa Pensheni wa PSPF mapema leo katika Ukumbi wa JB Belmonte, Jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mh Adam Mayingu (kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo, Mh Assah Mwambene leo katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo wakati Mkurugenzi mkuu wa PSPF alipokuwa akizungumzia mafanikio ya PSPF ndani ya miaka 15 tokea kuanzishwa Kwake.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF na wanahabari waliohudhuria mkutano kati ya Waandishi wa habari na Mfuko wa Pensheni wa PSPF uliolenga kuelezea mafanikio ya mfuko huo ndani ya Miaka 15 tokea kuanzishwa kwake.
Mmoja wa Waandishi wa Habari akiuliza swali wakati wa Mkutano kati ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF na waandishi wa habari uliofanyika leo Katika ukumbi wa JB Belmonte, Jijini Dar Es salaam, Mkutano huo ulilenga kueleza mafanikio yaliyopatikana kwa Kipindi cha Miaka 15 tokea kuanzishwa kwa mfuko huo wa PSPF.Picha na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

KAMPENI YA MWANAMKE NA UCHUMI SASA KUHAMIA TANGA

$
0
0
 Mkurugenzi wa Angels Moments inayoendesha Kampeni ya Mwanamke na Uchumi, Naima Malima akitoa hotuba ya ufunguzi wa kampeni hiyo iliyofanyika mkoani mwanza hivi karibuni. Kampeni hiyo yenye lengo la kuwawezesha kiuchumi wanawake wajasiriamali ambapo kampeni hiyo itafanyika mkoani Tanga Mwezi Oktoba. Picha na Angels Moments.
 Mshairi maarufu bibi sauda akitoa burudani ya mashairi yake adhimu kwa lugha ya kufurahisha na burudani kwa wanawake wajasiliamali katika kampeni ya mwanamke na uchumi jijini mwanza.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilemela ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kampeni ya Mwanamke na Uchumi iliyofanyika Mwanza, Mh. Halima Masenza akifurahia mashairi ya Bi. Sauda (hayupo pichani) katika kughani mashairi yake kwa lugha ya kiswahili.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Tanzania kufaidika na Mfuko wa Programu ya Maendeleo ya Kimataifa ya LFI

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa alipokuwa katika mkutano na Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Fedha za Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) nchini Judith Karl na wandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa (kulia) alipokuwa katika mkutano na Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Fedha za Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) nchini Judith Karl (kushoto) na wandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Fedha za Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) nchini Judith Karl (kushoto) akiongea na wajumbe kutoka TAMISEMI na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu Mpango wa Fedha wa Kidunia na Kitaifa (LFI). Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa.
Mtaalamu wa Ushauri wa UNCDF Peter Malika (katikati) akiongea na waandishi wa habari leo jijini dara es salaam kuhusu LFI na chini ambapo amesema kuwa lengo lake ni kutoa ushauri wa kitaalamu, fedha na namna ya kuchagua miradi yenye tija katika jamii ili wananchi waweze kujiletea maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa na kushoto ni Afisa Habari TAMISEMI Rebecca Kwandu. (Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA KONGAMANO LA WATAFITI WA UFUGAJI NYUKI BARANI AFRIKA

$
0
0
TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa kongamano la watafiti na wanasayansi wa sekta ya ufugaji nyuki Barani Afrika linalotarajiwa kufanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 11 hadi 16 Novemba mwaka huu.

Kongamano hilo linatajiwa kuhudhuriwa na washiriki 550 ambapo kati yao Watanzaniani 250 na wageni kutoka nje ya nchi wanatarajia kuwa 300. Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jumanne (Septemba 16, 2014), Jijini Dar esSaalaam, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu Tanzania katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Juma Mgoo alisema lengo la kongamano hilo ni kuimarisha sekta ndogo ya ufugaji nyuki kwa kushirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Aliongeza kuwa katika kongamano hilo wadau hao pia watajadili kwa pamoja namna bora zaidi ya kusaidia mchango wa sekta hiyo katika Nyanja zautafiti, teknolojia pamoja na kubadilishana uzoefu katika uboreshaji, utunzaji na usimamizi wa makundi ya nyuki kwa uzalishaji wenye wingi na ubora.

“Kongamano litahusisha uwasilishwaji wa mada za utafiti kwa njia za mijadala, semina kwa wafugaji nyuki, majadiliano ya kitaalamu sanjari na maonyesho ya bidhaa za ufugaji nyuki” alisemaMgoo.

Aidha Mgoo alisema washiriki wote watapaswa kujilipia ada ya ushiriki ikiwemo gharama za usafiri na malazi, ambapo kwa kutambua ukubwa wa gharamahizo Serikali ililazimika kulipia baadhi ya huduma. “Gharama za mtu mmoja kwa siku ni dola za kimarekani 120 ila mshiriki wa Tanzania hulipaTsh. 150,000/- tu” alisema Mgoo.

Kwa mujibu wa Mgoo mbali na kongamano hilo, washiriki hao pia watapata fursa ya kushiriki ziara ya mafunzo, kwa kutembelea maeneo mbalimbali yanayojihusisha na ufugaji nyuki nchini ikiwemo Mkoawa Kilimanjaro, ambapo wataweza kujionea ufugaji nyuki wasiouma pamoja na ufugaji nyuki katika nyanda kame za Mikoa ya Singida na Dodoma.

Kwa wake upande Rais wa Shirikisho la UfugajiNyuki Duniani (Apimondia) Gilles Ratia amesifu maandalizi mbalimbali yanayofanywa na Serikali ya Tanzania katika kufanikisha na kuwezesha mkutano huo nchini.

Akizungumzia sekta ya ufugaji nyuki nchini, Ratia amepongeza jitihada kubwa zilizofanywa na Serikali katika kuwasaidia na kuwaendeleza wafugaji wa nyuki, na hivyo kuwataka wafugaji kujitokeza kwa wingi kushiriki kongamano hilo litakaloweza kuwajengea uwezo katika uzalishaji na hivyo kuwaongozea kipato.
“Napenda kutoa pongezi zangu kwaMhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwaj itihada zake anazozionyesha katika kusaidia na kuendeleza sekta ya ufugaji nyuki kwani ameonyesha nia ya dhati ya kusaidia sekta hii” alisema.
Kaimu Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Gladness Mkamba (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne (Septemba 16, 2014) kuhusu kongamano la sekta ya ufugaji nyuki Barani Afrika linalotarajiwa kufanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 11-16 Novemba, 2014. Kushoto ni Afisa Nyuki Mwanadamizi, Stephen Msemo, kulia ni Mtendaji Mkuu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Juma Mgoo.
Mtendaji Mkuu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Juma Mgoo (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano la sekta ya ufugaji nyuki Barani Afrika linalotarajiwa kufanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 11-16 Novemba, 2014. Kushoto Kaimu Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Gladness Mkamba. (PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)

WASHIRIKA WA MAENDELEO WARIDHISHWA MRADI WA UMEME KINYEREZI

$
0
0
Baadhi ya Washirika wa Maendeleo wakipita jirani na unapojengwa mmoja wa mitambo wa kupokea gesi katika eneo la Kinyerezi, Jijini Dar es Salaam, walipotembelea maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupokea gesi.
Pichani ni mmoja wa Mtambo wa kuzalisha umeme ambao ni miongoni mwa mitambo itakayotumiwa katika kuzalisha kiasi cha megawati 150 za umeme katika Mradi wa Kinyerezi I.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi, Saimoni akiuleza jambo ujumbe wa Washirika wa Maendeleo wakati walipotembelea kuona maendeleo wa ujenzi wa mradi huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi, akiwaongoza Washirika wa Maendelo kuangalia namna utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme na kituo cha kupokea Gesi unavyoendelea katika eneo la Kinyerezi Jijini Dar es Salaam. Pembeni ni mojawapo ya mapipa yatakayotumika kuhifadhi mafuta ambayo yatatumika wakati wa dharura.

Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
Washirika wa Maendeleo kutoka taasisi mbalimbali nchini waliotembelea Mradi wa kuzalisha Umeme  wa Kinyerezi I na kituo cha kupokea Gesi  wameeleza kufurahishwa na kuridhika na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo.

Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, Philippe Dongier, akiongea kwa niaba ya washirika hao ameeleza kuwa, wameridhishwa na hatua ambazo miradi hiyo imefikia na kupongeza jitihada za Serikali kuhakikisha kwamba inafanyia kazi changamoto ya upatikanaji umeme wa uhakika Tanzania. Pia Dongier ameitaka Serikali kushirikiana na wadau katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya umeme ili iweze kufikia lengo lake la kuhakikisha Tanzania inazalisha umeme wa kiasi cha megawati 10,000 ifikapo mwaka 2025.

Akizungumza wakati ujumbe huo ulipotembelea kituo cha kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 150 na  kituo cha kupokea gesi katika eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim  ameeleza kuwa, Wizara imeona ni jambo la msingi kwa wadau hao kutembelea miradi hiyo ili kujionea hatua mbalimbali ambayo miradi hiyo imefikia.

Aidha, Maswi ameongeza kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, imedhamiria kuleta mabadiliko ya kiuchumi kupitia sekta ya nishati hususani kupitia gesi asilia na kuongeza kuwa, hakuna kinachoshindikana hivyo, miradi hiyo inatarajiwa kukamilishwa kwa wakati kama ilivyopangwa.

Kwa mujibu wa Meneja Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mhandisi Kapuulya Musomba, ameeleza kuwa, ujenzi wa kituo cha kupokea gesi cha Dar es Salaam umekamilika kwa asilimia 60. Naye Meneja Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha kuzalisha Umeme cha Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi, 

Saimoni Jilima ameeleza kuwa, ujenzi wa kituo hicho umekamilika kwa asilimia 70.
Washirika wa Maendeleo  waliotembelea miradi hiyo ni pamoja na  Benki ya Dunia, GIZ, USAID, MCC, Korea Exim Bank, Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB),DFID, Umoja wa Ulaya,Ubalozi wa Sweden, Ubalozi wa Norway, Ubalozi wa Ujerumani na Ubalozi wa Ufaransa.

MKURUGENZI MKUU WA BENKI YA DUNIA ALIPOKAGUA MIRADI YA BARABARA DAR ES SALAAM

USAHILI MISS UNIVERSE TANZANIA 2014 MKOANI DAR ES SALAAM KUFANYIKA GOLDEN TULIP

Tafrija ya polisi ya kuagana Mirerani wilayani simanjiro mkoani Manyara

$
0
0
 Aliyekuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Mirerani, Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara, Mkakibu wa polisi Ally Mohamed Mkalipa, ambaye ni Mkuu wa polisi (OCD) Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha, akizungumza wakati wa sherehe ya kuagwa kwake Mirerani juzi.
 Mkuu wa Kituo cha Polisi Mirerani, Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara, Mkakibu Msaidi wa polisi, ASP Lwitiko Noman Kibanda, akicheza muziki na mke wake kwenye sherehe ya kukaribishwa kwake na kumuaga aliyekuwa mkuu wa kituo hicho SP Ally Mohamed Mkalipa, ambaye hivi sasa ni Mkuu wa polisi (OCD) Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, (SACP) Deusdedit Kaizigile Nsimeki, akicheza muziki na mke wake wakati wa tafrija ya kumuaga aliyekuwa Mkuu wa kituo cha Polisi Mirerani Wilayani Simanjiro, SP Ally Mohamed Mkalipa na kumkaribisha Mkuu mpya wa kituo hicho ASP Lwitiko Noman Kibanda.
 Wapishi wakiwa tayari kuwahudumia watu mbalimbali walioshiriki kwenye tafrija ya kumuaga aliyekuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Mirerani, Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara, SP Ally Mohamed Mkalipa, ambaye ni Mkuu wa polisi (OCD) Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha na kumkaribisha Mkuu mpya wa kituo hicho ASP Lwitiko Noman Kibanda.
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images