Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 574 | 575 | (Page 576) | 577 | 578 | .... | 3353 | newer

  0 0

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ban ki  Moon akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani) siku ya jumanne ambapo alitumia fursa hiyo kuainisha masuala mbalimbali yatakayopewa kipaumbele wakati wa  Mkutano wa 69 wa  Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa  unaoanza wiki ijayo  hapa  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,  jijini New York, Marekani.  Mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola ni  moja ya  suala litakalopewa kipaumbele cha pekee wakati wa mkutano huo utakaohudhuriwa na  wa viongozi  zaidi ya 140 wakuu wa nchi na serikali,   viongozi wa  asasi za kiraia, na wakuu wa mashirika mbalimbaliya Kimataifa.

  ======  ======= =======
  UMOJA WA MATAIFA KUJADILI UGONJWA WA EBOLA-BAN KI MOON


  Na  Mwandishi Maalum, New  New York

   Viongozi  Wakuu wa Nchi na Serikali  zaidi ya 140 kutoka mataifa mbalimbali duniani  wamethibitisha  kuhudhuria na  kushiriki  majadiliano ya  jumla wakati wa Mkutano  wa  69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaoanza wiki ijayo.


  Akizungumza na  waandishi wa habari hapo siku ya  Jumanne, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban Ki Moon, amesema,  viongozi hao pamoja na  kujadili  changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia hivi sasa,  watautumia mkutano huu kujadiliana kwa kina kuhusu  mchango na ushiriki wa jumuiya ya kimataifa katika kuukabili  mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete  ni miongoni wa viongozi hao 140 na anaongoza  ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu.

   Akizungumzia zaidi kuhusu mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola na athari zake kwa uhai wa mwanadamu na kwa maendeleo ya  kiuchumi na kijamii,   Ban ki  Moon amewaeleza  waandishi hao, kuwa Jumuiya ya kimataifa haiwezi kuendelea kuufumbia macho na kwamba kadiri inavyochelewa kuutafutia ufumbuzi ndivyo  hatari yake inavyozidi kuongezeka.


  “Tutatoa kipaumbele cha peke kuhusu ugonjwa wa Ebola ambao umeleta athari kubwa kwa baadhi ya nchi za Afrika ya Magharibi na maeneo mengine. Siku mbili zijazo ( Alhamisi) Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana kwa dharura kuzungumzia mlipuko wa Ebola. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Margaret Chan na Mimi tutazungumza katika mkutano huo” akasema Ban Ki Moon.


  Akaongeza kwa kusema wiki ijayo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa litakuwa na mkutano wa kilele kuhusu mahitaji ya watu na nchi zilizokabiliwa na ugonjwa wa Ebola. Pamoja na  kujadili  na kutafuta mkakati wa pamoja wa kukabiliana na Ebola,  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  anasema  viongonzi hao wakuu wa nchi na serikali pia wanatarajiwa  kujadili na kubadilishana  mawazo kuhusu  changamoto za mabadiliko ya tabia nchi katika  mkutano utakaofanyika septemba 23.

  Mhe. Rais Jakaya  Kikwete ni kati ya  Viongozi  walioalikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  kuhudhuria na kuzungumza katika mkutano huu muhimu kuhusu  suala zima la mabadiliko ya tabia nchi na  athari zake.


  Akielezea zaidi kuhusu mkutano huo wa mabadiliko ya tabianchi, Ban Ki Moon anasema  mkutano huo utakuwa na malengo mawili, kwanza ni kukusanya utashi wa kisiasa  ili kufikia makubaliano ya pamoja hapo mwakani katika mkutano utakaofanyika huko Paris , Ufaransa. Na pili kuchukua hatua madhubuti za kupunguza  uzalishaji wa gesi chafu.


  Akiainisha zaidi  kuhusu ajenda mbalimbali zitakazojadiliwa wakati wa Mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa,  Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, amesema,   majadiliano ya Baraza Kuu ( General Debate) yatakayoanza septemba 24   yatatumika  kukusanya nguvu za pamoja za  kuushinda umaskini, na kupitisha ajenda za malengo mapya ya maendeleo endelevu .Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya  Mrisho Kikwete atalihutubia Baraza Kuu Septemba 25.

  Masuala mengine ambayo pia  yanatarajiwa kutawala mkutano huo wa Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa  kwa mujibu wa  Ban Ki Moon, ni pamoja na  migogoro na machafuko yanayoendelea katika nchi za Syria,  Iraq, Libya, Mali,  Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ukraine, Sudan ya Kusini ukiwamo pia  mgogoro  kati ya Palestina na Israel. 


  0 0

   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (katikati) akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy nchini, Philippe Corsaletti (kulia) baada ya kupokea hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 40 msaada uliotolewa kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inayotarajiwa kufanyika wiki ijayo, jijini Arusha. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ukumbi mdogo wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (katikati) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea hundi ya Sh. Milioni 40 kwa ajili ya maandalizi ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy nchini, Philippe Corsaletti (kulia). Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inatarajiwa kufanyika wiki ijayo, jijini Arusha. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ukumbi mdogo wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (katikati) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea hundi ya Sh. Milioni 40 kwa ajili ya maandalizi ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy nchini, Philippe Corsaletti (kulia). Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inatarajiwa kufanyika wiki ijayo, jijini Arusha. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ukumbi mdogo wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Na Dotto Kahindi.
  Nianze kwa kuwasalimu na kutoa shukran zangu kwa Blogu hii kwa kunipa nafasi ya kuwasilisha hoja yangu ambayo inalenga kuishirikisha jamii katika kupata suluhisho la ajali za barabarani ambazo zimekuwa ni janga kubwa la kitaifa.
  Mara kadhaa niliwahi kusikia takwimu za vifo vinavyotokana na magonjwa mbalimbali yakiwemo UKIMWI, Malaria, Vifo vya mama wajawazito n.k, na vifo hivi vilitia uchungu sana kwa jamii kiasi kampeni kadhaa zilianzishwa ili kupunguza vifo hivyo au kuvikomesha kabisa.

  Jamii kwa kutambua athari zilizokuwa zikisababishwa na majanga hayo kijamii,  kiuchumi na kitaifa waliunga mkono kampeni hizo kwakuwa wao pia walikuwa wahanga wakuu na walipaswa kushiriki katika kubadili tabia na mienendo ili kuelekea kwenye Tanzania iliyo salama.

  Nasikitika kutangaza kuwa Tanzania sasa kuna ugonjwa mpya unaitwa AJALI, kila siku ajali zinapoteza maisha ya wapendwa wetu. 

  Takwimu zilizotolewa na Waziri wa Uchukuzi, Dr. Harrison Mwakyembe mwisho wa wiki iliyopita zinaonyesha watu 1,126 wamepoteza maisha kwa ajali za barabarani kwa kipindi cha miezi mitatu, huku majeruhi ni 3,827 katika ajali 3,338.

  Idadi hii ya ajali na vifo siyo ya kawaida, inatisha na kusikitisha sana ni wakati huu tunatakiwa kupambanua na kupata dawa ya kukabiliana na janga hili la ajali.

  Tunaanzaje? Nani tuanze kumbana anayechangia ajali hizi? Ni maswali tunatakiwa kuyajibu kwanza kabla ya kuanza kutoa lawama, ni lazima tujue akina nani wanaohusika kwenye sekta hii ili tupate pa kuanzia kama tunataka kuziba ufa kwelikweli.

  Mwakyembe ameunda kamati maalumu ya kutafuta chanzo na dawa ya ajali hizo, nimeona ni vyema kuunga mkono jitihada hizo kwa kuanzisha kampeni ya #DerevaMakini ambayo inalenga kuishirikisha jamii katika kukabiliana na ajali hizo ambazo zimekuwa mwiba kwa taifa. 

  Kwa maoni yangu wafuatao ni wadau wa moja kwa moja wa sekta ya usafiri ambao wakitekeleza sawasawa majukumu yao ajali zitapungua; Askari wa Usalama Barabarani, Madereva, Abiria, Wamiliki wa vyombo vya usafiri, TRA, Sumatra, Bima, Vyombo vya habari, Tanroads, Miundombinu , NIT na vyuo vya namna hiyo, TBS, Wauzaji wa magari, mafuta na vipuli vya magari. 

  Kupitia forum hii naomba kupata ushiriki wako mdau ili tutajadili kwa pamoja, toa maoni yako, ushauri na mapendekezo ukizingatia wadau waliotajwa hapo juu, maoni yako tutayatumia kwenye mada ifuatayo ambayo itakwenda kuchambua majukumu ya mdau mmoja mmoja.

  Hii ni Kampeni ya Usalama barabarani yenye lengo la kupunguza ajali za barabarani ikilenga hasa mabasi ya abiria na imewezeshwa na Michuzi Blog, Tabianchi Blog na Transevents Marketing Limited.

  Makala haya yatakuwa yakikujia kila wiki, kwa taarifa zaidi tembelea ukurasa wetu wa facebook

  0 0   Aunty akitia saini kitabu cha wageni alipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani siku ya Jumanne Sept 16, 2014.
   Aunty Ezekiel akipata picha ndani ya mjengo wa Ubalozi wa Tanzania Washington, DC
   Aunty akipata picha nje ya mjengo wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
   Aunty na Cassim Mganga wakipata menu ndani ya jiji la Washington, DC
   Shabiki akipata picha na wasanii Aunty na Cassim Mganga
    Shabiki akipata picha na wasanii Aunty na Cassim Mganga

  0 0
 • 09/17/14--04:04: SHUKRANI
 • FAMILIA YA MAREHEMU APPOLINARY MUSABILA KUSAYA INAPENDA KUTOA SHUKRANI ZAKE ZA DHATI KWA NDUGU,JAMAA,MARAFIKI NA MAJIRANI KWA JINSI MLIVYOSHIRIKIANA BEGA KWA BEGA NA FAMILIA HIYO TANGU KIFO CHA MAMA YAO MPENZI YUSTINA YAKOBO KUSAYA KILICHOTOKEA JIJINI DAR ES SALAAM TAREHE 21/08/2014 HADI ALIPOPUMZISHWA TAREHE 25/08/2014 KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE KIJIJINI KAGUNGULI UKEREWE.NI WAZI KUWA KATIKA KUFANIKISHA MSIBA HUO MZITO MLITUMIA RASLIMALI ZENU KUBWA AMBAZO HAZIWEZI KUREJESHWA HATA KIDOGO.

  FAMILIA KWA PAMOJA HAINA CHA KUWALIPA KWA MOYO WENU WA UPENDO MLIOUONESHA ZAIDI YA KUSEMA NENO AHSANTE.FAMILIA HIYO INAWAOMBEA KWA MWENYEZI MUNGU MZIDI KUBARIKIWA NA KUPEWA NA ZIADA. BWANA ALITOA,BWANA AMETWAA,JINA LA BWANA LIHIDIMIWE..AMEN

  0 0
 • 09/17/14--04:05: DICOTA CONVENTION 2014


 • 0 0

   Askari Polisi wakiwa eneo la tukio ikiwa ni kuimarisha ulinzi
  (Picha Zote na demasho.com)
  -------------

  ASKARI watatu  wa jeshi la Polisi wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa  wa Ruvuma  (Homso) iliyopo mjini songea Mkoani humo  wakiwa wanapatiwa matibabu ya majeraha ambayo waliyapata baada ya kushambuliwa kwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni Bomu la kurushwa kwa mkono.

  Tukio hilo limetokea  September 16, 2014 majira ya saa moja na nusu jioni katika kata ya Msufini karibu na daraja la Matarawe, wilayani Songea Mkoani Ruvuma  ambapo watu watatu wasiofahamika walitupa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono ambalo limetengenezwa kienyeji na kuwajeruhi askari  hao watatu waliokuwa doria.

  Askari hao waliojeruhiwa ni  WP. 10399 PC Felista aliyejeruhiwa mguu wa kulia  kwenye unyayo na pajani  ,G. 7351 PC Ramadhani aliye jeruhiwa mguu wa kulia karibu na goti na tumboni upande wa kulia na  G. 5515 pc John aliyepata majeraha katika mguu wa kulia chini ya goti na jeraha dogo tumboni.

  Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr. Daniel Malekela ameeleza kutoa vipande vya bati na misumari katika majeraha ya askari hao na mpaka sasa wanaendelea na matibabu.

  Alisema kufutia hali hiyo Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linaendelea na uchunguzi  wa kina ili kuwakamata wahusika wa tukio hilo kwa hatua zaidi za kisheria.
   Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe. Saidi Mwambungu kasema  amesikitishwa sana na kitendo hicho cha wahalifu kujeruhi askari tena kwa makusudi na amesema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata.
   Eneo la tukio  likiwa limezungushiwa alama na Jeshi la Polisi.
   Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwangu akizungumza jambo na waandishi wa habari katika hoptal ya mkoa wa Ruvuma baada ya kuwatembelea majeruhi hao
   Kamati ya ulinzi na Usalama wakiwa Hospital ya mkoa wa Ruvuma.
   Aliye lala kitandani ni WP ambaye amejeruhiwa akiwa amelazwa katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma
   Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr Daniel Malekela akizungumza na wandishi wa habari hopitalini hapo.
  Askari Ramadhani Ally akiwa anaelezea jinsi mkasa huo ulivowakuta wakiwa kazini


  0 0

  Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (UN-ICTR) leo imetoa msaada wa Kompyuta 22, Monitor 154 na Printers 66 kwa mashule, vyuo, vituo vya afya, mashirika yasiyo ya serikali na taasisi zakidini na kijamii pamoja na idara za serikali katika jitihada zake za kusaidia jumuiya ya Kitanzania ambayo imeweza kuilea mahakama hiyo nchini kwa miaka karibu 20 sasa. 

  Ofisi ya ya Mkuu wa Mkoa yenyewe iliongezewa gari moja la deraya na ulinzi. Makabidhiano hayo yalifanya mjini Arusha na viongozi wa UN-ICTR kwa wawakilishi wa wafadhiliwa hao katika sherehe fupi zilizofanyika kwenye uwanja wa rumande ya mahakama hiyo Kisongo.

  Huu ni mwendelezo wa mahakama hiyo kuisaidia jamii hasa ya Arusha katika kipindi hiki ambapo imo mbioni kumaliza shunguli zake za kuwahukumu wale wote walioongoza mauaji hayo nchini Rwanda mwaka 1994. Taasisi na mashirika hayo yalikabidhiwa kila moja Computer moja, printer saba na monitor tatu. 
   Waliokabidhiwa ni; ABC Vocational Training Centre; Ambassador of Hope Netowrk of People with HIV/AIDS; Arusha Charity Pre and Primary School; Caucus of Children's Rights; Costigan Primary School Karatu; Gilbert Sarungi; Institute of Accountancy Arusha; Karatu School Association; Lurelle Vocational Handcraft Training Centre; M & M Kiwera Dispensary; Okutu Primary School Simanjiro; Renea Secondary School; Samaritan Village Tanzania; Toto Aid (NGO); Faraja Young Women; Maroroni Secondary School; Dolly Primary School; Arusha RC's Office; Shuku Foundation; Arusha Mosque; Support + Empowering Women and Sidai Design; na Chalao Secondary School Kilimanjaro.
  baadhi ya vifaa hivyo vilivyokabidhiwa.

  0 0

   Sehemu ya Watoto yatima wanaolelewa na Kituo cha Tanzania Mitindo Houshe chini yake Mwanamitindo nguli hapa nchini,Khadija Mwanamboka wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wasimamizi wao wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 7 ya kituo hicho iliyofanyika mwishoni mwa wiki,Msasani jijini Dar es Salaam.
   Sehemu ya watoto hao wakifurahia kwa pamoja michezo mbali mbali iliyokuwepo.
   Taswira ya mtoto akiwa kachora uso wake.
  Mlezi wa Tanzania Mitindo House,Mwanamitindo,Khadija Mwanamboka akikata keki pamoja na Watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho.

  0 0  0 0

  Ofisa wa Benki ya NBC, Pendo Clement (katikati) akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Future World kuhusu masuala ya ujasiriamali na elimu ya kifedha ikiwa ni sehemu ya mpango wa wafanyakazi wa NBC wa kujitolea uitwao ‘Unlocking Youth Potential’ wa kuwafundisha vijana masuala ya ujasiriamali na mbinu za kifedha. Hafla hiyio iliandaliwa na Plan International pamoja na chuo hicho, Gongo la Mboto, Dar es Salaam jana.
  Ofisa wa Benki ya NBC, Jonathan Bitababaje (kulia) akifundisha baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Future World kuhusu masuala ya ujasiriamali na elimu ya kifedha ikiwa ni sehemu ya mpango wa wafanyakazi wa NBC wa kujitolea uitwao ‘Unlocking Youth Potential’ wa kuwafundisha vijana masuala ya ujasiriamali na mbinu za kifedha. Hafla hiyio iliandaliwa na Plan International pamoja na chuo hicho, Gongo la Mboto, Dar es Salaam.
  Mfanyakazi wa Benki ya NBC, Mtenya Cheya (kulia) akitoa maelekezo kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Future World kuhusu masuala ya ujasiriamali na elimu ya kifedha ikiwa ni sehemu ya mpango wa wafanyakazi wa NBC wa kujitolea uitwao ‘Unlocking Youth Potential’ wa kuwafundisha vijana masuala ya ujasiriamali na mbinu za kifedha. Hafla hiyio iliandaliwa na Plan International pamoja na chuo hicho,ilifanyika Gongo la Mboto, Dar es Salaam.
  Wanafunzi wa Chuo cha Future World wakiuliza maswali wakati Ofisa wa Benki ya NBC, Victor Tesha (kulia) alipokuwa akiwafundisha masuala ya ujasiriamali na elimu ya kifedha ikiwa ni sehemu ya mpango wa wafanyakazi wa NBC wa kujitolea uitwao ‘Unlocking Youth Potential’ wa kuwafundisha vijana masuala ya ujasiriamali na mbinu za kifedha. Hafla hiyio iliandaliwa na Plan International pamoja na chuo hicho, Gongo la Mboto, Dar es Salaam.
  Vijana wanaosoma katika chuo cha Future World, viongozi wa Plan International na Wafanyakazi wa Benki ya NBC wakipiga picha ya ukumbusho baada ya mafunzo.

  0 0

  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Jowika Kasunga (katikati) akikata utepe kuashilia uzinduzi wa nyumba za kisasa za kupangisha za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha AICC jijini Arusha hivi karibuni.
  Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakihakikisha wanapata taarifa na matukio muhimu katika uzinduzi katika uzinduzi wa nyumba mpya (Apartments) za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Jowika Kasunga akiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya Wakarugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) pamoja na wafanyakazi wa Kituo hicho.
  Mbunge wa Viti Maalumu kutoka Arusha, Mheshimiwa Catherine Magige (kushoto) naye alijumuika na wadau mbalimbali katika uzinduzi wa nyumba mpya (Apartments) za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).

  0 0

  Na John Gagarini, Kibaha

  WATU wawili wamefariki dunia na wengine watano wamejeruhiwa baada ya magari mawili likiwemo basi dogo la abiria waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso.

  Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoani Pwani Athuman mwambalaswa alisema kuwa tukio hilo lilihusisha gari aina ya Coaster likitokea kwenye msiba Musoma kwenda Jijini Dar es Salaam na kugongana na lori la mafuta.

  Kamanda Mwambalaswa alisema kuwa ajali hiyo ilitokea Septemba 17 mwaka huu majira ya saa 12:15 alfajiri maeneo ya Ubena Senge katika barabara ya Morogoro.

  Alisema kuwa basi hilo dogo la abiria lenye namba za usajili namba T 663 BKP lilikuwa likiendeshwa na Ally Abdul (34) lilikuwa na abiria wapatao 20 liligongana na lori hilo la mafuta aina ya Leyland  Daf lenye namba za usajili T 858 CLK na tela namba T 421 CKY mali ya kampuni ya Ramader ya Jijini Dar es Salaam lilikuwa likiendeshwa na dereva aitwaye Rashid.

  Aliwataja waliokufa kwenye ajali hiyo kuwa ni Neema Mile (39) na Jane Mtani (38) ambao miili yao pamoja na majeruhi wako kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani Tumbi kwa ajili ya matibab u na kusubiri ndugu wa marehemu.

  Aidha alisema kuwa chanzo cha ajaili hiyo dereva wa basi hilo la abiria kuhama upande wake kutokana na uchovu na usingizi unaotokana na kuendesha gari usiku kucha bila kupumzika na inamshikilia kuhusiana na tukio hilo.

  0 0

  Na Beatrice Lyimo- MAELEZO

  Rais mstaafu wa Awamu ya pili wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Ali Hassan Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa 22 wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) utakaofanyika Septemba 18 2014.

  Msajili wa Bodi ya AQRB Bwana Jehad Abdalah Jehad amesema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

  Bwana Jehad alisema kuwa lengo kuu la mkutano huo ni kuendeleza wataaluma wa fani ya wakadiriaji majenzi na kuzijua changamoto zilizopo katika sekta hiyo.

  “Jukumu kuu la bodi hii ni kusajili wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi pamoja na kuratibu mienendo yao ya kitaalamu. Mkutano huu utasaida sana kuitangaza taalum hii,” alisema Jehad.

  Aidha, bodi imeandaa mashindano ya insha kwa wanafunzi wa kidato cha pili nchini yalionza tangu 2008 ili wazifahamu taaluma hizi na kuamua kusomea taaluma hiyo ya sayansi kwa kuwa wanafunzi ni wadau muhimu wanaohitaji kuelewa fani hii.

  Mwaka 2013 wanafunzi walishindanishwa kuandika insha yenye mada inayohusu “Uongozi wa shule yako una mpango wa kujenga majengo mawili ya madarasa na maabara bora kushinda yaliyopo kwa sasa, toa ushauri juu ya utaratibu unaotakiwa kutumika katika mchakato wa kupata majengo hayo ikiwa ni pamoja na wataalamu wanaotakiwa ukiainisha majukumu ya kila mmoja.”

  Bwana Jehad alisema kuwa tangu walipoanzisha mashindano ya insha, wamebaini kuwa dhana iliyojengeka miongoni mwa jamii kuwa wasichana hawawezi somo la sayansi ni potofu.

  Tangu mwaka 2008 mashindano hayo yalipoanzishwa,imeonekana wazi kuwa kati ya wanafunzi 109 waliopata tuzo, kati ya hao 66 ni wasichana na wavulana ni 43.

  Kwa mujibu wa Msajilii wa bodi ya usajili wa ubunifu majengo, bodi imeanzisha mafunzo kwa wanafunzi kwa kuwapatia mazoezi yanayohusu taaluma hiyo ili kuhamasisha wanafunzi kupenda somo la sayansi hususani taaluma hizi kuziba pengo la upungufu wa wataalamu nchini.

  Zaidi ya washiriki 400 kutoka katika sekta mbalimbali za wahandisi nchini watashiriki mkutano huo.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu bw. Ambwene Mwakyusa (Kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa 22 wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) utakaofanyika Septemba 18 2014 ambapo Rais wa awamu ya pili wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajia kuwa mgeni rasmi kushoto ni Msajili wa Bodi ya AQRB Bwana Jehad Abdalah Jehad .
  Msajili wa Bodi ya AQRB Bwana Jehad Abdalah Jehad(kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya kuhusu mkutano wa 22 wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) utakaofanyika Septemba 18 2014, ambapo Rais wa awamu ya pili wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajia kuwa mgeni rasmi kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu bw. Ambwene Mwakyusa.

  0 0

  Maryam Himid/Saada Saleh-ZJMMC

  Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo,Zanzibar,Mh. Saidi Ali Mbarouk amezitaka Taasisi zinazosimamia kupokea Watalii Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Amani Abeid Karume kujenga mashirikiano ili kuondosha usumbufu kwa wageni wanaoingia na kuotoka nchini. Ameyasema hayo alipofanya ziara Uwanjani hapo kwa lengo la kuangalia hali halisi ya Wageni wanaoingia na kutoka nchini.

  Waziri Mbarouk amesema suala la Mashirikiano kwa wageni ni jambo muhimu linaloweza kuijengea sifa kubwa Zanzibar kwa wageni ambao wanakuja ambao wataweza kusimulia watakaoporudi ziara zao.

  Ametoa wito kwa Taasisi husika kuhakikisha Wageni wanaoingia Zanzibar wanapata huduma stahiki na ili kuepukana na usumbufu wa aina yoyote wanapofika katika Uwanja huo wa Ndege.

  Kwa upande wake Daktari wa kituo cha Afya uwanjani hapo Juma muhammed Juma amesema Wanaendelea kulisimamia vyema suala la kuwakagua kwa Vifaa maalumu Wageni wanaoingia kutoka Nchi zilizoathirika na Ugonjwa wa Ebola.

  Amezitaja Nchi hizo kuwa ni pamoja na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Liberia na Sera lion ambapo amesema kila abiria kutoka nchi hizo lazima Apimwe ili kuweka kinga ya Ugonjwa wa Ebola nchini.

  Hata hivyo Mkurugenzi wa uwanja wa ndege Juma Saleh Juma ameelezea baadhi ya changamoto zinazowakabili uwanjani hapo kuwa ni pamoja na upungufu wa maeneo ya kukaribisha wageni,maegesho ya Magari na Uhaba wa Wafanyakazi wanaozungumza Lunga ya Kitaliano kutokana na Wataliano hao kutumia lugha yao tu.

  Katika ziara hiyo Waziri Mbarouk alitembelea maeneo mbali mbali Uwanjani hapo ikiwemo Mapokezi, Maegesho ya Ndege na Magari na sehemu ya Mapumziko ya Abiria.
  Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar, Saidi Ali Mbarouk Mwenye Koti Jeupe akipewa Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa uwanja wa ndege Juma Saleh.Katika ziara hiyo Waziri Mbarouk alitembelea maeneo tofauti ya Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume. Baadhi ya Wageni kutoka nchi tofauti wakipata huduma kutoka Uhamiaji mara baada ya kuwasili Uwanja wa Abeid Aman Karume. Picha na Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar.


  0 0

  Ni matumaini yangu kuwa nyote muwazima na sie hatujambo huku Bondeni Sauzi.
  Maudhui ya barua hii ni kukufahamisheni kuwa kuna Mtanzania kwa jina Shukuru Goyagoya kafariki tarehe 16th mwezi huu katika Hospitali ya Baragwana Jo'burg.
  Alikua Kalazwa ICU takriban mwezi mmoja.

  Hapa Sauzi alikuwa akiitwa kwa jina la umaarufu Jastice Mliambe Manesi kazaliwa mwaka 1970.

  Maelezo niliyoweza kupata, Mama yake mzazi anaitwa  Bi Ziada Musa Kitima anaishi Mabibo CCM . Naomba msaada wenu wa kutangaza katika chombo chako habari hii ili jamaa zake marehemu taarifa hii iweze kuwafikia popote pale walipo. Na taarifa hii nimeweza kuifikisha katika Ubalozi wa Tanzania mjini Pretoria

  Mpaka sasa maiti bado ipo Hospitalini tunasubiri uamuzi wa pamoja ikiwa marehemu azikwe hapa Jo'burg au maiti yake isafirishwe hadi nyumbani kwao. Nashukuru kwa msaada
  Wenu. Kila la kheri

  Omar Mutasa
  BBC
  Joburg

  0 0

  Mfalme wa nyimbo za asili nchini Tanzania Costa Siboka, Baada ya kufanya kufuru na kuvunja Rekodi katika Miji ya Mwanza, Geita,Visiwa vya Ghana na Ukerewe Sasa anatarajia kumalizia ziara yake katika Miji ya Bunda,Bariadi,Shirati,Tarime , Butiama na Dutwa.Shoo hizo zitafanyika tarehe 22 Septemba 2014 mpaka tarehe 30 septemba 2014.Mfalme Siboka akiwa na kundi lake ametamba na kusema yeye in jeshi la Mtu mmoja...Hakunaga shiiida, Vuta raha Barimi tumpokee Mfalme.Siboka yupo katika utambulisho WA nyimbo yake mpya Engele yange aliouimba kwa lugha za makabila manne.Kisukuma,Kihaya,Kikerewe,Kijita na Kikurya.


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi mkutano wa Mashauriano kati ya Vyombo vya Habari na Vyombo vya Ulinzi, Usalama na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, leo Septemba 17, 2014. Mkutano huo uliandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).
  Rais wa Baraza la Habari Tanzania, (MCT) Jaji Thomas Mihayo, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua rasmi mkutano huo, uliofanyika leo Septemba 17, 2014 kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania, (MCT) Kajubi Mukajanga, akizungumza kabla ya mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua rasmi mkutano huo, uliofanyika leo Septemba 17, 2014 kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mwanafunzi wa Chuo kikuu huria cha Tanzania Bw. Mussa Omari (katikati) akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu tamko la kulaani kauli za mwenyekiti wa chadema taifa za kuhamasisha uasi kwa njia ya maandamano, wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Bw. Gulatone Masiga akitoa wito kwa wananchi kuudumisha muungano wetu na kuacha kupelekwa na wanasiasa wasio na misingi ya kidemokrasia.Kulia ni Mwanafunzi wa Chuo kikuu huria cha Tanzania Bw. Mussa Omari.
  Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Theodora Malata akiwaeleza jambo waandishi wa habari leo wakati wa Mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.

  0 0

  On September 17, 2014, U.S. Ambassador Mark Childress swore in sixty-one Peace Corps Volunteers to their two years of service in Tanzania.

  The American volunteers will work as Math, Science and English secondary school teachers, and as teacher trainers in twenty-nine districts throughout Tanzania. The swearing-in ceremony took place at the Ambassador’s residence in Dar es Salaam, and was attended by Guest of Honor Shukuru Kawambwa, Minister at the Ministry of Education and Vocational Training as well as the headmasters from the schools to which the new volunteers will be assigned.

  The American volunteers will serve their students, schools and communities through direct classroom teaching and projects involving, for example, nutrition, life skills and healthy living, environment, and literacy. The volunteers’ two-year service will also support Tanzania’s efforts to increase the number of math, science and English teachers in rural areas.

  In his remarks, the Ambassador emphasized the high expectations for the volunteers as they represent the American people to their students and community, and carry on the legacy of Peace Corps service.

  He also highlighted the strong partnership with the Ministry of Education, the schools hosting Peace Corps Volunteers, and the communities where the trainees and volunteers live and work. He thanked the language facilitators, Peace Corps staff and the host families for their dedication and commitment to ensuring that these 61 volunteers were prepared to serve.

  For more than 50 years, Peace Corps has maintained apolitical and non-sectarian ideals of technical and cultural exchange.

  Peace Corps promotes world peace and friendship through its fulfillment of three fundamental goals: providing American Volunteers who contribute to the social and economic development of interested countries; promoting a better understanding of Americans among the people who Volunteers serve; strengthening Americans' understanding of the world and its peoples.

  Over 2,000 Peace Corps Volunteers have served in Tanzania since 1962. The sixty-one volunteers sworn in today will be stationed in the following districts: Karatu, Kongwa, Chamwino, Mufindi, Iringa Rural, Hai, Rombo, Lushoto, Moshi rural, Ruangwa, Nachingwea, Hanang, Babati, Kiteto, Tukuyu, Kyela, Chunya, Mbarali, Masasi, Newala, Mtwara rural, Mbinga, Shinyanga, Kishapu,Maswa, Singida Rural, Iramba, Nzega and Lushoto.
  (Seated from left to right) The U.S. Ambassador to Tanzania Mark Childress, The Minister for Education and Vocational Training, Dr. Shukuru Kawambwa and the Peace Corps Country Director, Dr. Elizabeth O’Malley in a group photo with new American Peace Corps Volunteers. The volunteers were sworn-in to begin their two years of service as Math, Science and English secondary school teachers, and as teacher trainers in twenty-nine districts throughout Tanzania in a brief ceremony held at Ambassador’s residence in Dar es Salaam on September 17, 2014.
  A group of American Peace Corps Volunteers takes an oath to begin their two years of service in Tanzania in a swearing-in ceremony that was presided over by the U.S. Ambassador to Tanzania Mark Childress and held in Dar es Salaam on September 17, 2014. The 61 American volunteers will work as Math, Science and English secondary school teachers, and as teacher trainers in twenty-nine districts throughout Tanzania. They took the oath in presence of Tanzanian Minister for Education and Vocational Training Honorable Dr. Shukuru Kawambwa. (Photo courtesy of the American Embassy)

older | 1 | .... | 574 | 575 | (Page 576) | 577 | 578 | .... | 3353 | newer