Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

Simba Chawene awataka Watanzania kuacha kuingia barabarani kufanya maandamano ya kupinga mchakato wa Katiba

0
0
Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.

MJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. George Simba Chawene amesikitishwa na kauli zilizotolewa na baadhi ya Wajumbe walioko nje ya bunge hilo kuhusiana na uhalali wa bunge hilo linaloendelea Kisheria.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akichangia mada katika mjadala ndani ya bunge hilo huku akisisitiza kuwa huo ni upotoshwaji mkubwa na watu hao wanapaswa kuangaliwa kuhusu uzalendo wao.

Mhe. Chawene ameeleza kuwa inasikitisha zaidi hasa pale shutuma zinapoelekezwa kwa Mwenyekiti wa bunge hilo, Mhe. Samuel Sitta, kuwa bunge hilo sasa linaonekana ni mali ya Mwenyekiti wa bunge hilo wakati si kweli.

“Gazeti linachukua kurasa tatu hadi nne kuzungumzia habari Sitta king’ang’anizi, hivi hili bunge lipo kama liliitishwa na Sitta ama na Rais wa nchi?, hili bunge liko kisheria”, alisema Mhe. Chawene.

Aliongeza kuwa kwa niaba ya Watanzania wanafanya kazi ya bunge hilo kwa mujibu wa sheria huku akisisitiza kuwa wajumbe waliotoka nje ya bunge hilo wamevunja sheria na kwamba hawawezi kutafuta uhalali nje ya sheria.

“Wanamlazimisha Rais avunje bunge hili, Rais wa kufuata utawala bora anavunja kwa mamlaka yapi? Mamlaka ya Rais yako kwa mujibu wa sheria”, alisema Mhe. Chawene.

Aidha, ameeleza kuwa Sheria inayoendesha mchakato wa Katiba ni Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo imetungwa kutoka katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye hatua tatu zikiwemo hatua ya kukusanya maoni ambayo Tume ya Warioba ilifanya kazi hiyo na kumaliza, hatua ya Pili ni bunge hilo kujadili kwa niaba ya wananchi wa Tanzania kwa uwakilishi uliopo ndani ya bunge hilo na hatua ya tatu ni wananchi kwenda kutunga Katiba.

“Sisi hapa tunatoa Katiba inayopendekezwa, inayofuata ni Watanzania kwenda kutunga Katiba kwa kutunga kwa kupiga kura ya kusema ndiyo au hapana yale tuliyoyajadili na kuletwa na Tume”, alisisitiza Mhe. Chawene.

Aidha, amewataka watanzania kuwaona watu hao kuwa ni watu wabaya na wasio na nia nzuri na nchi na kuepuka kuingia barabarani kufanya maandamano ya kuipinga Katiba hiyo.

Balozi Idd mgeni rasmi kwenye Tamasha la Kuliombea Taifa na Kuhamasisha amani linalofanyika mjini Bagamoyo

0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Viongozi wa Kidini wanapaswa kuwa macho katika kuzikataa choko choko zozote na ushawishi unaotolewa na wanasiasa kwa kuzingatia maslahi yao badala ya manufaa ya Taifa zima.

Alisema kazi kubwa inayotakiwa kufanywa na Viongozi hao wa Kidini ni kuwaombea watu wakiwemo Viongozi wa Nchi ili Baraka ziongezeke ndani ya Taifa pamojana umma jambo ambalo litasaidia kupunguza misuguano.

Balozi Seif alisema hayo wakati akilifungua Tamasha la Kuliombea Taifa na Kuhamasisha  amani linalofanyika katika Ukumbi wa Masai Laugwa uliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani  Pwani.

Alisema mifarakano au choko choko zinapotokea kwa upande wowote ule Viongozi wa Kidini lazima wawe tayari kupatanisha na sio kutumia dhamana yao kuwa wararuaji huku wakielewa kwamba kazi wanayofanya ni wito kutoka kwa Muumba wao.

Balozi Seif alieleza kwamba amani na utulivu wanaojivunia Watanzania walio wengi kwa miaka mingi sasa ni miongoni mwa neema zinazopaswa kutumiwa vizuri na wananchi wa rika zote.

Mapema Askofu Sedrick Ndonde wa Kanisa la Restoration { Restoration Bible Church } alisema Taifa hivi sasa limekuwa na cheche hatarishi inayoonekana kuchochea  choko choko za Kidini, kisiasa pamoja na vitendo vya kigaidi.

Alisema hali hiyo yenye kwenda sambamba na ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya inasababisha mfumko wa uhalifu unaowafanya wananchi waendelee kuishi katika maisha ya mashaka na hofu.

Alifahamisha kwamba baadhi ya watu wamekosa uzalendo  kwa kutaka kunufaisha matundo yao. Hivyo ni vyema kwa  Jamii isikubali amani iliyopo nchini  ikachezewa na kuyayuka kama barafu.

Tamasha hilo lilipamba kwa njimbo mbali mbali zilizotayarishwa na kwaya za madhehebu mbali mbali wakiongozwa na waimbaji maarufu wa nyimbo za injili akiwemo Noel Pascol,Stela Joel pamoja na Dr.Magret Sdoris Kongera.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiingia ndani ya Ukumbi wa Masai Laugwa Wilaya ya Bagamoyo kuzindua Tamasha la Kuliombea Taifa Amani lililoandaliwa na Kanisa la Restoration { Restoration Bible Church } .Kulia ya Balozi Seif ni Makamu Askofu Mkuu wa Restoration Bible Church Tanzania Askofu Sedrick Ndonde na kushoto yake ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Nd. Ahmed Kipozi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akilizindua rasmi Tamasha la kuliombea Taifa Amani hapo katika Ukumbi wa Masai Laugwa Wilayani Bagamoyo. Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Nd. Ahmed Kipozi na Kushoto yake ni Makamu Askofu Mkuu wa Restoration Bible Churh Tanzania Askofu Sedrick Ndonde. 
Muimbaji wa Nyimbo za Injili Kutoka Mkoani Morogoro Dr. Magereth Isdori Kongera kati kati akiwa na wana kwaya wenzake kwenye Tamasha la Kuliombea Taifa Amani hapo Ukumbi wa Masai Laugwa Wilayani Bagamoyo.
Baadhi ya waumini wa madhehebu mbali mbali ya Dini ya Kikristo waliohudhuria uzinduzi wa Tamasha la Kuliombea Taifa Amani lililofanyika Masai Laugwa Bagamoyo. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Topland Kinondoni mabingwa Safari Pool 2014

0
0
KLABU ya Topland ya Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni yenye makazi Magomeni jijini Dar es Slaaam imefanikiwa kutetea ubingwa wa ke wa fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mkoani Kilimanjaro kwa kuifunga timu ya Anatory ya Mkoani Morogoro 13-3.

Timu ya Topland kwa kutwaa ubingwa huo ilizawadiwa Kikombe,Medali za dhahabu na pesa taslimu Shilingi 5,000 000/= wakati mshindi wa pili Anatory ya Morogoro walizawadiwa pesa taslimu Shilingi 2,500 000/= pamoja na medali za fedha.

Mshindi wa tatu katika fainali hizo ni timu ya Mashujaa kutoka Mkoa wa kimichezo wa Ilala jijini Dar es Salaam ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 1,250,000/= pamoja na medali za shaba wakati washindi wanne ni timu ya Mboya ya Mkoani Kilimanjaro ambao ndio walikuwa wenyeji wa Mashindano hayo kwa mwaka 2014 ambao walizawadiwa pesa taslimu Shilingi 750,000/=.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja Wanaume, Mussa Mkwega kutoka klabu ya Anatory ya Mkoani Morogoro alitwaa ubingwa kwa kumfunga Innocent Sammy kutoka Mkoa wa kimichezo wa Temeke 5-4 na hivyo Mkwega kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 500,000/=,medali ya dhahabu pamoja na ngao wakati Innocent Sammy kwa kuchukua nafasi ya pili alizawadiwa fedha taslimu shilingi 250,000/= pamoja na medali ya fedha.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja wakina Dada, Neema Hamis kutoka Mmkoa wa Tanga alitwaa ubingwa kwa kumfunga Sada Tulla kutoka Shinyanga na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 350,000/= pamoja na medali ya Dhahabu wakati Sada Tullah yeye kwa kukamata nafasi ya pili alizawadiwa pesa taslimu Shilingi 200,000/=.

Akikabidhi zawadi hizo Naibu Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia aliipongeza Kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake ya afari Lager kwa kudhamini mashindano ya Pool Taifa na alliwaomba waendelee kufadhili kwani mpaka sasa ni mchezo pekee ulioiletea sifa Nchi kupia fainali za Afrika ambapo Mtanzania Patrick Nyangusi anashikilia Ubingwa wa Afrika.

Nkamia aliwataka pia Chama cha Pool Taifa(TAPA) kutumia vyema fursa ya TBL kwa manufaa ya kuendeleza mchezo huo nchini na Kimataifa na kwa jinsi hiyo aliwapa siku 60 wawe wameshafanya uchaguzi na kupata viongozi wa kuchaguliwa kikatiba na wa muda tangu chama hicho kianzishwa kama ilivyo sasa.

Mwisho Waziri Nkamia aliwatakia safari njema wanamichezo wote kurejea majumbani salama na kuwaomba walichokipata kwa Safari Lager kama zawadi wakakitumie vyema kwa maezndeleo yao.
Nahodha wa timu Topland ya Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni, Patrick Nyangusi akishangilia na kikombe mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wachezaji wa klabu ya Topland wa mkoa wa kimichezo wa Kinondoni wakishangilia na kikombe pamoja na pesa taslimu Shilingi 5,000 000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mkoani Kilimanjaro.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MBUNGE WA SHIRIKISHO LA UJERUMANI

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Mhe. Charles M. Huber (wa pili kushoto) ambaye ni Mbunge na Mjumbe wa Kamati ya Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo na Mambo ya Nje ya Bunge la Shirikisho la Ujerumani wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo leo Septemba 15, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Charles M. Huber (kulia kwa Makamu wa Rais), Stefan Reith Mwakilishi wa Konrad Adenauer Stiftung (KAS) kushoto, Naibu Balozi wa Ujeruman nchini John Reyels (wa pili kulia) na Richard Shaba baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu Dar es Salaam Septemba 15, 2014. Picha na OMR

WAFANYAKAZI WA BENKI YA NBC WAJIMWAGIA MAJI BARIDI KUCHANGISHA FEDHA KUPAMBANA NA UGONJWA WA FISTULA

0
0
Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Flora Lupembe (kulia) akimwagiwa maji baridi na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Rukia Mtingwa katika hafla ya kumwagiana maji baridi iitwayo ‘Ice Bucket Challenge’ yenye makusudi ya kuchangisha fedha kwa ajili kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mhazini Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Ivan Tarimo (kushoto) akimwagiwa maji baridi na mmoja wa mfanyakazi mwenzake katika hafla ya kumwagiana maji baridi iitwayo ‘Ice Bucket Challenge’ yenye makusudi ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Mussa Jallow (katikati) naye akimwagiwa maji baridi ili kutimiza azma ya benki hiyo katika kutafuta fedha ili kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa fistula nchini.

Bilioni 3 kutumika mwaka wa masomo 2014 – 2015 kutoka mfuko wa pensheni wa LAPF kwa wanachama wake.

0
0
“PIGA KITABU NA LAPF”
WANACHAMA WA LAPF KUNUFAIKA NA FAO LA ELIMU

Bilioni 3 kutumika mwaka wa masomo 2014 – 2015 kutoka mfuko wa pensheni wa LAPF kwa wanachama wake.

15 Septemba 2014, Dodoma: Wanachama wa mfuko wa penseni wa LAPF kunufaika na fao jipya lilozinduliwa hivi karibuni nchini kwa Baraka zake Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI Mh. Hawa Ghasia. 

Fao hilo lijulikanalo kama ‘Piga Kitabu na LAPF’ limelenga kuwakopesha wanachama wa LAPF mikopo ya elimu ya juu kwani ni ombi la muda mrefu kutoka kwa wanachama wa mfuko huo. Hivyo kwa kuthamini na kuona umuhimu wa elimu Mfuko wa Penseni wa LAPF umjibu kiu yao ya muda mrefu ili kumpunguzia mzigo mwajiri.

Akiongea kutoka Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bwana Eliud Sangaalieleza kuwa  mfuko wa Pensheni wa LAPF una huduma nyingi na ambazo zimelengwa kwa ajili ya jamii na hususani zinazochangia sana kwenye maendeleo. 

“Huduma hii mpya ya Fao la Elimu imetengewa shilingi Bilioni Tatu (3) kwa mwaka huu wa fedha ikiwa ni kianzio cha mfuko huu, tunaahidi mwaka unaofuata fao hili litatengewa bajeti kubwa zaidi kutokana na umuhimu wake katika nchi yetu, wanachama wengi wameshanufaika mpaka sasa na wengine wengi zaidi wanazidi kutuma maombi ya kupata mkopo wa elimu ya juu. Fao hili litawanufaisha wanachama maelfu na maelfu, wanachama wengi watume maombi kunufaika na huduma hii”

“Mwanachama anatakiwa kujaza fomu ya mkopo wa elimu LAPF/LON.2, ambayo hupatikana katika ofisi zote za LAPF pamoja na ofisi za waajiri wachangiaji na pia kwenye tovuti ya LAPF www.lapf.or.tz. Baada ya kukamilisha fomu na kuambatisha vielelezo vinavyotakiwa atawasilisha fomu hiyo kwenye ofisi za LAPF au atatuma kwa njia ya posta. Fao hili la Mkopo wa Elimu kwa mwanachama utalipwa moja kwa moja chuoni kila mwaka wa masomo kwa taratibu za chuo husika na urejeshaji wake utakuwa kwa muda wa miaka mitano tangu ulipoanza kutolewa” Aliongeza Bwana Sanga.




‘Piga Kitabu na LAPF’ ni fao la elimu litakalotolewa kwa  mwanachama yoyote wa lapf ambaye amekidhi vigezo kama kupata kibali cha kusoma toka kwa mwajiri wake, barua (admission letter) ya kukubalika kujiunga na chuo cha hapa nchini kilichosajiliwa na nacte au tcu na awa na michango inayozidi kiasi cha mkopo unachoombwa kwa asilimia 25.

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI CHUO CHA UFUNDI STADI MASIGITUNDA

0
0
CHUO CHA UFUNDI STADI CHA MASIGITUNDA KILICHOPO PERAMIHOKATIKA KIJIJI CHA MSHIKAMANO KINATANGAZA NAFASI ZIFUATAZO ZA

1. MKUU WA CHUO NAFASI MOJA (1):

AWE NA SIFA ZIFUATAZO;

1. AMEMALIZA KIDATO CHA NNE
2. AWE NA DEGREE YA UALIMU NA UONGOZI
3. AWE NA UFAHAMU WA UTUMIAJI COMPUTER
4. AWE NA UZOEFU WA UTAWALA
5. AWE NA UZOEFU WA KAZI MIAKA MIWILI (2)

2. MWALIMU WA UASHI NAFASI MOJA (1):

AWE NA SIFA ZIFUATAZO;

1. AMEMALIZA KIDATO CHA NNE
2. AWE NA CHETI CHA UFUNDI UASHI GRADE I AU CBET LEVEL III
3. AWE NA CHETI CHA UALIMU (MVTTC)
4. AWE NA UJUZI WA COMPUTER
5. AWE NA UZOEFU WA KAZI MIAKA MIWILI (2)

3. MWALIMU WA USHONAJI NAFASI MOJA (1):

AWE NA SIFA ZIFUATAZO;

1. AWE AMEMALIZA KIDATO CHA NNE
2. AWE NA CHETI CHA UFUNDI USHONAJI GRADE I AU CBET LEVEL III
3. AWE NA CHETI CHA UALIMU (MVTTC)
4. AWE NA UJUZI WA COMPUTER
5. AWE NA UZOEFU WA KAZI MIAKA MIWILI (2)

4. MWALIMU UFUNDI WA MAGARI NAFASI MOJA (1):

AWE NA SIFA ZIFUATAZO;

1. AWE AMEMALIZA KIDATO CHA NNE 
2. AWE NA CHETI CHA UFUNDI MAGARI (MV MECHANICS) GRADE I AU CBET LEVEL III
3. AWE NA CHETI CHA UALIMU (MVTTC)
4. AWE NA UJUZI WA COMPUTER
5. AWE NA UZOEFU WA KAZI MIAKA MIWILI (2)

5. MWALIMU WA KAWAIDA (ALIYE NA DIPLOMA):

AWE NA SIFA ZIFUATAZO;

1. AWE AMEMALIZA KIDATO CHA NNE
2. AWE NA CHETI CHA DIPLOMA YA UALIMU
3. AWE NA UFAHAMU WA COMPUTER
4. AWE NA UZOEFU WA KAZI MIAKA MIWILI (2) KATIKA KUFUNDISHA TECHNICAL DRAWING NA ENGINEERING SCIENCE

6. MWALIMU WA UDEREVA NAFASI MOJA (1):

AWE NA SIFA ZIFUATAZO;

1. AMEMALIZA KIDATO CHA NNE
2. AWE NA LESENI DARAJA C
3. AWE AMEPITIA NIT (CHUO CHA USAFIRISHAJI)
4. AWE NA UZOEFU WA KAZI MIAKA MIWILI (2)

7. MLINZI

AWE NA SIFA ZIFUATAZO

1. AMEMALIZA DARASA LA SABA NA KUENDELEA
2. AWE AMEPITIA MGAMBO
3. AWE NA UZOEFU WA KAZI MIAKA MIWILI (2)


KAMA UNA SIFA TAJWA HAPO JUU TUMA BARUA YA MAOMBI YA KAZI IKIWA IMEAMBATANISHWA

NA VIVULI VYA VYETI NA CV  KABLA YA TAREHE 26/10/2014 SAA 11 JIONI KWA:

MENEJA RASILIMALI WATU
MASIGITUNDA VTC
P.O.BOX 164
PERAMIHO

AU KWA E-MAIL: masigitunda.info@gmail.com

Simu 0754- 281 768

KAMATI YA SHERIA YAPITISHA USAJILI WA WACHEZAJI

0
0
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imepitisha usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza huku wenye kasoro ndogondogo klabu zao zikitakiwa kuziondoa ili waweze kupatia leseni za kucheza ligi msimu huu wa 2014/2015.

Kasoro hizo ni kufikia makubaliano na klabu ambazo wachezaji husika wametoka, kuwafanyia uhamisho (transfer) na kulipa ada za uhamisho. Kamati vilevile ilibaini wachezaji wengi hawakufanyiwa uhamisho kama kanuni za ligi hizo zinavyoelekeza.

Hivyo, klabu ambazo hazitakuwa zimeondoa kasoro hizo kwa wachezaji wao leseni zao zitazuiliwa mpaka watakapokuwa wamekamilisha kila kitu. Ni wachezaji wenye leseni tu ndiyo watakaoruhusiwa kucheza mechi za ligi.

Klabu za African Lyon, African Sports, Ashanti United, Coastal Union, Kiluvya United, Majimaji, Mji Mkuu, Polisi Dodoma, Polisi Morogoro, Red Coast na Stand United ziliwawekea pingamizi wachezaji mbalimbali kwa kutofanyiwa uhamisho.

Kuhusu Ike Bright Obina wa Nigeria aliyewekewa pingamizi na African Lyon dhidi ya Coastal Union, Kamati imezitaka klabu hizo kufikia makubaliano, na zikishindwa mchezaji huyo atabaki African Lyon.

Kamati vilevile ilijadili malalamiko ya Kocha wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic dhidi ya klabu hiyo, na kuzipa pande hizo mbili siku 14 kufikia muafaka juu ya malalamiko hayo, na zikishindwa ndipo zirejee tena mbele ya Kamati.

Logarusic aliyewakilishwa na mwanasheria wake Dickson Sanga anailalamikia klabu hiyo kwa kuvunja mkataba kinyume cha taratibu, hivyo kutaka Simba imlipe dola 6,000 kwa kuvunja mkataba, na pia kulipa dola 50,000 ikiwa ni fidia maalumu ya madhara yaliyotokana na uvunjwaji huo.

NEWS ALERT: MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI MAOMBI YA PINGAMIZI LA KUSIMAMISHA BUNGE LA KATIBA

0
0
Na Mwene Said wa Blogu ya Jamii

MAHAKAMA Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam leo imetupilia mbali maombi ya pingamizi la awali la kusimamisha  Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma, iliyofunguliwa na  Mwandishi wa Habari Said Kubenea, kwa kuwa wametumia kifungu cha sheria kisicho sahihi.

Kadhalika, mahakama hiyo imetupilia mbali pingamizi hilo la awali, kwa kuwa mlalamikaji ametumia kifungu cha sheria namba 2 kidogo cha (2) (JALA) ambacho hakina mamlaka ya kufungua maombi hayo mahakamani.

Uamuzi huo ulitolewa chini ya jopo lililoketi la majaji watatu, wakiongozwa na Mwenyekiti Mh.Jaji Augustino Mwarija, Dr. Fauz Twaib na Aloyisius Mujuluzi.

Jopo hilo lilisema mahakama imetupilia mbali pingamizi hilo la awali kwa sababu halina mashiko ya kisheria.

Upande wa mlalamikiwa uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Gabriel Malata na mlalamikaji Peter Kibatala.

Awali,  Mwanasehria Mkuu (AG) kupitia Naibu Mwanasheria Mkuu, George Masaju kuiomba mahakama hiyo kutupilia mbali pingamizi hilo kwa kuwa maombi yake ni batili kisheria na hayawezi kuthibitishwa mahakamani, hivyo yatupiliwe mbali.

Katika pingamizi hilo lililoambatana na hati ya kiapo, AG kupitia naibu wake, amedai kuwa maombi hayo ya mlalamikaji yana dosari ambayo haiwezi kurekebishika kwa kuwa zinahitaji kifungu maalum cha sheria kinachoipa nguvu mahakama ya kuridhia maombi hayo.

Mapema mahakamani hapo, Kubenea aliwasilisha maombi ya pingamizi la awali ya kusimamisha Bunge hilo kwa muda yaliyopewa usajili wa namba 29 ya mwaka 2014, pamoja na maombi ya msingi ya tafsiri ya mamlaka ya Bunge yote yalifunguliwa mahakamani hapo jana chini ya Hati ya Dharura.

Katika kesi ya msingi iliyopewa usajili  namba 28 ya mwaka 2014, Kubenea anaiomba mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya Mamlaka ya Bunge la Katiba chini ya  vifungu vya 25 (1) na 25 (2) vya Sheria ya Marekebisho ya Katiba namba Namba 83 ya mwaka  2011.

Pamoja na mambo mengine katika kesi hiyo ya kuomba tafsiri ya mamlaka ya Bunge  hilo, pia Kubenea amewasilisha maombi mahakamani hapo akiiomba mahakama itoe zuio la muda la kusimamisha Bunge hilo ili kusubiri uamuzi wa maombi ya tafsiri hiyo.

DK. SHEIN AWASILI COMORO LEO

0
0
Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiaana na Balozi Comoro Nchini Tanzania alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Comoro akiwa katika Ziara Ya Kiserikali akiwa amefuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein Na Viongozi Mbali Mbali
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Comoro Mohamed Ali Soilihi wakati Wimbo wa Taifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wimbo Wa Muungano Wa Comoro Ukipigwa. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipunga mikono kwa Wananchi wa Comoro akiwa na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Comoro,Mohamed Ali Soilihi Wakati wa mapokezo alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Comoro leo akiwa katika Zzara ya Kiserikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Comoro,Mh. Mohamed Ali Soilihi wakiangalia Ngoma za Utamaduni mara walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Comoro leo akiwa katika ziara ya Kiserikali.[Picha Na Ramadhan Othman,Ikulu Zanzibar.]

KATIBU MKUU UTUMISHI ATOA SOMO KWA WATUMISHI WA MKOA WA MWANZA

0
0
Na Atley Kuni- Afisa habari Mwanza.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi George Yambeshi, amewataka watumishi wa Umma wa Sekretarieti ya mkoa wa Mwanza kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo iliyopo ili kuleta tija katika ufanisi wa kazi zao.

Ameyasema hayo wakati alipokutana na watunishi wa sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mwanza hii leo alipokuwa ziarani mkoani humo kwa shughuli za kijamii na kuamua kutumia fursa hiyo kukutana na watumishi hao.

Yambeshi amesema kama watumishi wa umma ni lazima kuzingatia miiko inayo ongoza utumishi wa umma huku akitolea mfano wa mavazi nadhifu kwa watumishi na yasiyo na utata kwa watu " kama watumishi wa ni vema kuzingatia miiko inayo tuongoza" alisema na kuongeza. kuwa suala la kuvujisha siri za serikali ni suala lisilo kubalika hivyo moja ya sifa ya mtumishi wa umma ni lazima ajue kutunza siri.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo ameonya watumishi wa kuacha kuchanganya mambo ya siasa mahali pa kazi" Ndugu zangu haikazwi kuwa mwanachama wa chama cha siasa lakini sio vema mtumishi kufanya masuala ya siasa mahali pa kazi kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na taratibu za utumishi wa umma.

Mbali na masuala la siasa na uadilifu katika kazi ,pia katibu Mkuu huyo ametumia fursa hiyo, kusilikiliza kero mbali mbali za watumishi hao ikiwapo suala la kodi kubwa, mikopo kwa watumishi pamoja na kukosekana kwa baadhi ya miundo ya kada mpya za utumishi serikialini.

Awali akimkaribusha katibu Mkuu kiongozi kuzungumza na watumishi hao wa Skretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bwana Ndaro Kulwijila, alimuelezea kuhusu hali halisi ya watumishi katika mkoa wa Mwanza huku akitoa kilio chake kwa Katibu Mkuu huyu juu ya utofauti Mkubwa wa mishahara baina ya watumishi waliopo kwenye wakala wa serikali na wale wa serikali kuu.

Hata hivyo katika majibu yake Katibu Mkuu huyo aliahidi kushughulikia changamoto zote zilizo jitokeza katika kikao hicho na kuzipatia ufumbuzi kwa kadri itakavyowezekana.

Katibu Mkuu Utumishi ndiye mkuu wa masuala ya Utumishi wa umma katika Serikali ya jamahuri ya Muungano wa Tanzania.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi George Yambesi akizungumza na watunishi wa sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Mwanza,juu ya umuhimu wa kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo iliyopo ili kuleta tija katika ufanisi wa kazi zao.
Sehemu ya watunishi wa sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza wakiwa kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu Mkoa wa Mwanza wakati wa mkutano wao na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi,George Yambesi 
Picha ya pamoja.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM KUHUSU HALI YA KUISALAMA

MKUTANO WA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI KUFANYIKA JIJINI DAR, SEPTEMBA 18

0
0
Na Dotto Mwaibale 

 BODI ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) katika kipindi cha kuanzia mwaka 1998 hadi sasa imezifungia kampuni 36 na wakandarasi 86 kufanyakazi ya ukandarasi baada ya kushindwa kufuata sheria za ujenzi. 

 Hayo yalielezwa na Msajili wa bodi hiyo Jehad Jehad wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mkutano wa usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi utakaofanyika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Septemba 18, 2014 jijini Dar es Salaam. 

 "Kazi yetu kubwa ni kusimamia sheria ya shughuli za ujenzi na kama tukibaini kuna kampuni inakwenda kinyume tunaifungia kufanyakazi" alisema Jehad. 

 Alisema lengo mkutano huo wa Septemba 18 ni kuwanoa wataalamu wa fani hiyo ili kukabiliana na mabadiliko ya kiteknologia na kitaaluma katika sekta ya ujenzi, kubadilishana mawazo na kuboresha huduma za taaluma hiyo. 

 Akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali Mwenyekiti wa bodi hiyo Dk.Ambwene Mwakyusa alisema Tanzania haina sheria inayoratibu shughuli za ujenzi kwa ujumla (Building Codes) itakayoweza kuwabana wajenzi ya maghorofa ambayo yanabomoka hapa nchini. Dk. Mwakyusa alisema sheria hiyo ingekuwepo ingewaongoza wataalamu wa majengo jinsi ya kutumia vifaa vya ujenzi kwenye jengo husika tofauti na ilivyosasa. 
Dk.Mwakyusa alisema kutokana na sheria hiyo kutokuwepo wataalamu wa majengo wanapotumia vifaa vya ujenzi ambavyo havina kiwango na wanapofikishwa kwenye vyombo vya sheria baada ya majengo wanayojenga kuanguka wanakutwa hawana hatia. 

“Tanzania haina sheria inayoratibu shughuli za ujenzi kwa ujumla kama ikiwepo sheria itamuongoza mtaalamu wa majengo afuate sheria iliyopo jinsi ya kutumia vifaa vya ujenzi mfano kama mbao au nondo zinatakiwa zitumike aina gani kwenye jengo husika ,”alisema Dk.Mwakyusa. Katika mkutano huo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Hassan Mwinyi.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Dk.Ambwene Mwakyusa, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mkutano huo. Kushoto ni Msajili Msaidizi Utawala na Fedha, Angello Ngalla na Msajili wa Bodi hiyo, Jehad A. Jehad.
 Msajili wa Bodi, Jehad A. Jehad (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Mkaguzi wa Ndani, Ezekiel Stephen na Kaimu Nsajili Msaidizi Ufundi, Mashaka Bundala.
 Kikao na waandishi wa habari kikiendelea.

Mkasi | SO9E13 With Wagosi Wa Kaya

KINANA AZINDUA MRADI WA MAJI MUYUYU NA KIKUNDI CHA UTENGENEZAJI BATIKI KIBITI RUFIJI

0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji mama mmoja  wa Kijiji cha Muyuyu, katika Jimbo la Kibiti, alipozindua mradi wa maji katika Kijiji cha Muyuyu, wakati wa ziara yake  ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya  maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM mkoani Pwani.
 Katibu wa Ityikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia katika Kijiji cha Mchukwi ambapo Kinana alikwenda kuzindua kikundi cha Akina mama cha kutengeneza batiki.
Kinana akisaidia kutengeza batiki katika kijiji cha Mchukwi

MHE JOHN MNYIKA AMRITHI ZITTO KABWE CHADEMA

0
0
DK SLAA,SALUM MWALIM PAMOJA NA JOHN MNYIKA Uchaguzi ndani ya chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA leo usiku huu umefikia tamati kwa kamati kuu ya chama hicho kupata viongozi wake wamwisho ambao ni KATIBU MKUU ,NAIBU KATIBU MKUU BARA pamoja na NAIBU KATIBU MKUU ZANZIBAR

MATOKEO
KATIBU MKUU --DK WILLBROD SLAA--
NAIBU KATIBU MKUU BARA---JOHN MNYIKA
NAIBU KATIBU MKUU ZANZIBAR--SALUM MWALIM
Viongozi awa waliteuliwa na mwenyekiti wa chama hicho kama katiba inavyosema na hatimaye baraza kuu likawapitisha wote bila kuwapinga
mh JOHN MNYIKA anateuliwa kushika nafasi ambayo ilikuwa inashikiliwa na mbunge wa jimbo la kigoma kaskazini mh ZITTO KABWE ambaye aliondolewa katika nafasi hiyo na kamati kuu ya chama kwa kile ambacho kilisemekana kuvunja katiba ya chama hicho

AFANDE SUZAN KAGANDA APOKEA ASKARI WAPYA 75 TABORA, ATOA TAARIFA YA UHALIFU MKOANI HUMO

0
0
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP - Suzan Kaganda amewapokea askari 75 wa awamu ya kwanza walioripoti mkoani Tabora wakitokea Chuo Cha Polisi Moshi baada ya kuhitimu  mafunzo ya awali ya Polisi. Kamanda aliwataka askari hao kufanya kazi kwa weledi katika utendaji kazi pamoja na Nidhamu ya hali ya juu.  
 Askari wapya wakimsikiliza Afande Suzan Kaganda alipowapokea  mkoani Tabora wakitokea Chuo Cha Polisi Moshi 
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP - Suzan Kaganda amewapokea askari 75 wa awamu ya kwanza walioripoti mkoani Tabora wakitokea Chuo Cha Polisi Moshi.
Picha na  Fakih Abdul - mwandisi wa Polisi Tabora.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 16/09/2014.

Ndugu waandishi wa habari katika mkoa wetu wa Tabora kumetokea matukio yafuatayo:-

KUPATIKANA NA MADAWA YADHANIWAYO KUWA YA KULEVYA NA PIKIPIKI ZA WIZI: Huko wilaya ya Igunga wamekamatwa watuhumiwa watatu:-

1.  WILLY s/o MASHILINGI, 22 yrs, Msukuma, mkulima na mkazi wa Kahama.

2.  SITA s/o JILUNGA, 38 yrs, msukuma, mkulima na mkazi wa Nzega.

3.  YUSUPH s/o MIHAYO, 24yrs, msukuma, mkulima wa mtaa wa Stoo.

4.  GILALA s/o BULEBA, 35yrs, msukuma, mkulima, mkazi wa Igunga mjini.


wakiwa na madawa ya kulevya wanayoyatumiwa kulewesha watu kisha kuwapora pikipiki. Walipohojiwa walikiri kuhusika na matukio mbali mbali ya wizi wa pikipiki na kuonesha pikipiki mbili zenye namba T 892 CXB, T 522 CQZ, T.914 BUW na T.812 CGUzote aina ya SANLG ambazo walizipora huko Puge wilaya ya Nzega. Juhudi za kuwatafuta wamiliki halari wa pikipiki hizo zinaendelea.

Watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

KUPATIKANA NA BHANGI GUNIA MBILI: Huko wilaya ya Nzega amekamatwa mtuhumiwa MABULA s/o EZEKIEL, 23yrs, Msukuma, mkulima na mkazi wa Ibologero akiwa na bhangi gunia mbili. Mtuhumiwa baada ya mahojiano amekiri kuwa ni muuzaji na mtumiaji wa bhangi.upelelezi kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani

AJALI YA GARI KUGONGANA NA PIKIPIKI YA MATAIRI MATATU NA KUSABABISHA VIFO: Huko kijiji cha Ndono barabara ya Urambo gari no. T607 BNV scania lorry iliyokuwa ikiendeshwa na FUMBA s/o JUMA, 45yrs, Msambaa, mkazi wa DSM iligongana na pikipiki ya kubeba mizigo (Guta) REG no. T153 CWJ SUNLG na kusababisha vifo vya watu watatu papo hapo ambao ni MAHONA S/O MUSA WANDEZI, 30yrs, Msukuma, mkazi wa Intika dereva wa pikipiki, HIBHA S/O LUCAS, 30yrs, msukuma, mkazi wa Ndono, MABULA S/O MATONGO, 35yrs, msukuma, mkazi wa Intika chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa pikipiki.

AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO:Huko maeneo ya barabara kuu Nzega – Igunga katika kijiji cha Kitangili GARI T.300 CWB Toyota Hiace ikiendeshwa na STANSLAUS S/O JOAKIM, 33yrs, Mchaga, mkazi wa Nzega ilimgonga mtembea kwa miguu JOKU D/O MBEGESHEN, 32yrs, Msukuma, M/biashara, mkazi wa Singida na kufa papo hapo. Chanzo cha ajali ni uzembe wa mtembea kwa miguu kuvuka barabara bila tahadhali. Dereva amekamatwa kwa mahojiano zaidi.

Jeshi la Polisi linazidi kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi lao ili kukomesha na kutokomeza vitendo vyote vya uhalifu na kuwafichua wahalifu, pia  watumiaji wa barabara wafuate  sheria za usalama barabarani.


SUZAN S. KAGANDA –ACP.


KAMANDA WA POLISIMKOA WA TABORA.


HOJA YA KUSITISHA BUNGE MAALUM LA KATIBA YAHITIMISHWA RASMI

0
0
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba toka Kamati namba Tano, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro akisoma taarifa wakati wa mjadala wa jioni bungeni hapo jana 15 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Na Benedict Liwenga, 
MAELEZO-Dodoma 
HOJA ya kusitisha Bunge Maalum la Katiba imehitimishwa rasmi Kisheria kwa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutamka kwamba bunge hilo linaweza kuendelea na shughuli zake. 
Taarifa hiyo imetolewa jana 15 Septemba, 2014 na Mjumbe wa Kamati namba Tano, Mhe. Dkt. Asha-Rose-Migiro wakati wa mjadala wa jioni bungeni hapo.
 
Akisoma taarifa hiyo, Dkt. Migiro amesema kuwa mjadala wa kusitisha bunge umefungwa rasmi hapo jana licha ya kuwepo kwa madai kuwa bunge hilo halina uhalali wa kisiasa. 
“Kwaajili ya kuondoa shaka yoyote ningependa kuwaambieni takwimu tulizonazo hivi sasa, bunge hili lina jumla ya Wajumbe 630, kati ya hao waliotoka ni wajumbe 130 ambao ni sawa na asilimia 21% tu ya wajumbe wote, wajumbe waliobaki ndani ya bunge ni 500 hii ni sawa na asilimia 79% ya wajumbe wote na tukizichambua takwimu hizi, ningeomba kutambua wingi wa Kundi la 201”, alisema Dkt. Migiro. 
Akikanusha juu ya kuwepo kwa dhana iliyojitokeza ya kwamba wajumbe waliobaki ndani ya bunge hilo ni wa aina moja, Dkt. Migiro alisema kuwa taarifa hizo si za kweli, kwani kati ya wajumbe 500 walioko ndani ya bunge hilo wajumbe wanaotokana na kundi la 201 ni wajumbe 189 ambapo wajumbe wanaotoka Tanzania bara jumla yao ni 348 na kati ya hao, 125 ni wajumbe wanaotoka katika kundi hilo la 201. 
“Ukitazama takwimu hizi kwa jicho lolote lile basi wajumbe wa 201 ni sehemu kubwa na ni sehemu muhimu ya wajumbe hawa waliobaki”, alisema Dkt. Migiro. 
Akizungumzia juu ya wajumbe toka upande wa Zanzibar, Dkt. Migiro alisema kuwa wajumbe waliobaki ni 152 na kati ya hao wajumbe 64 wanatokana na kundi la 201. 
“Tunasisitiza takwimu hizi kwa wajumbe wa 201 kwasababu wajumbe hawa ndiyo wajumbe ambao kwa wingi wao kitakwimu lakini pia kwa wingi wao kimakundi wanawakilisha sura zote Kitaifa, hivyo ni dhairi kwamba kwa namna yoyote ile waliobaki ndani ni wengi, ni idadi kubwa, ni idadi wakilishi na tukiangalia kwa takwimu hizi, wajumbe walioamua kususia bunge kwa pande zote mbili hizi hawafikii hata theluthi moja ya wajumbe waliobaki”, alisisitiza Dkt. Migiro. 
Kwa kuzingatia matakwa ya kisheria, Dkt. Migiro alieleza kwamba uamuzi upatikane kwa maridhiano, kwa majadiliano na kwa kushawishiana kwa hoja wajumbe waliobaki na walio wengi wanaweza wakatumia wingi wao na wana uhalali wa kisiasa na wa kisheria. 
Dkt. Migiro aliendelea kusema kuwa, wajumbe waliotoka hawakuona kuwa utaratibu huo ungekuwa na manufaa kwao licha ya kuwepo na maridhiano katika bunge hilo, pia kupitia wadau mbalimbali Vyama vya siasa vyote vimekuwa vinazungumza nje ya bunge kupitia Msajili wa Vyama vya siasa, kupitia Kituo cha Demokrasia (TCD) na kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

WAKAZI WA TABORA WAKIRI WAZI KUWA MASOKO NDIO CHANGAMOTO YAO KUBWA KATIKA SHUGHULI ZAO ZA UJASILIAMALI

0
0
SEMINA ya Kamata Fursa Jitathimini,Jiamini,Jiongeze inayoendeshwa sambamba na burudani za Fiesta 2014, jana imeendelea kwa kuwapatia dira ya maisha na namna ya kuwafanya wajikwamue kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi wakazi wa Mkoa wa Tabora mjini ndani ya ukumbi wa chuo cha TEKU,kilichopo katikati ya mji wa Tabora.
Semina hiyo ambayo imeongozwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba (pichani juu) ilikuwa ya aina yake, kwani baadhi ya vitu na mbinu alizowapatia wakazi wa Mkoa wa Tabora,wengi wao wameonesha kuvutiwa nayo kutokana na mafunzo,maelekezo na mbinu mbalimbali za kupambana na changamoto zinazowakabili/zitakazowakabili katika miradi yao mbalimbali wanayotarajia kuianzisha ama wamekwishaianzisha.
 Msanii muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Weusi,Niki wa Pili  akizungumza na vijana mbalimbali waliokuwa wamegawanywa katika makundi ili kusikiliza mipango na miradi waliyonayo na namna wanavyoiendeleza,lakini pia Washiriki hao walielezwa namna ya kujikwamua na changamoto wanazokumbana nazo katika kuendeleza miradi yao,ikiwamo na namna ya kujitafutia soko ,jambo ambalo Washiriki hao wamekiri wazi kuwa ndio changamoto yao kubwa katika shughuli zao za ujasiliamali.
  Meneja wa Maxcom Africa, ‘Max malipo’,  Bernard Munubi  akiwa katikati ya vijana akiwaeleza namna ya kufanikiwa katika shughuli zao kimaendeleo na pia kuwapatia mbinu za kupambana na changamoto na hatimae kuelekea kwenye kilele cha mafanikio .Bernad pia aliwaeleza washiriki hao kwa wale ambao wanafikiria kuanza miradi ya ujasiliamali,kwamba si vibaya wakaanza kujaribu kujitafutia maendeleo kupitia mashine za Max Malipo na kujionea wenyewe namna zinavyoweza kusaidia kuondokana na umaskini kwa kiasi kikubwa miongoni mwao.Mnubi alisema kuwa mpaka sasa mashine hizo zimewaletea mafanikio makubwa ya kiuchumi watu wengi.
 Mmoja wa Wajasiliamali kutoka mjini Tabora ,Dada Flora Zakaria ambaye amejiunga kwenye moja ya kikundi kinachofanya shughuli mbalimbali kupitia kikundi chao kiitwacho JACANA Natural Products,akionesha aina ya sabuni zilizotengenezwa na kikundi chao,ambapo pia kikundi hicho hujishughulisha na utengenezaji wa vipodozi vya asili kwa akina mama pamoja na mafuta ya aina mbalimbali.Flora alieleza kuwa wamekuwa wakijitahidi kutengeneza bidhaa mbalimbali lakini changamoto yao kubwa imekuwa ni namna ya kupata soko la kuziuza bidhaa zao.
 Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha VETA wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikichambuliwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba (hayupo pichani).Ambapo washiriki wa semina hiyo waliunda vikundi na kubainisha wana miradi gani ama  wanatarajia kuanza kufanya miradi gani,ili kusaidia kutatua vikwazo na kutoa miongozo kwa namna moja ama nyingine.
 Mtangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha Jahazi,Mdau Mussa Hussein akizungumza na wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza kwenye semina ya Fursa,iliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha TEKU mjini Tabora.
 Sehemu ya Washirikiwa semina ya Fursa wakiwa ndani ya ukumbi wa Chuo cha TAKE wakisubiri kuanza rasmi kwa semina hiyo.
PICHA NA MICHUZI JR-TABORA.

KAGERA SUGAR WAIFUATA MGAMBO JKT MJINI TANGA

0
0
Na Faustine Ruta, Bukoba
Kikosi cha Timu ya Wakata Miwa Kagera Sugar wameanza leo hii safari  kuelekea jijini Tanga kwa ajili ya mchezo wa ufunguzi wa Ligi kuu soka Tanzania bara katika uwanja wa CCM Mkwakwani dhidi ya wenyeji Mgambo JKT, septemba 20 mwaka huu.
Kocha msaidizi wa Kagera Sugar, Murage Kabange amesema klabu hiyo ina jumla ya wachezaji 25 na hii leo tayari wapo safari na  viongozi watano kwenda kusaka pointi tatu muhimu.
Kabange aliongeza kuwa wameamua kuanza safari mapema kwasababu kutoka Kagera kwenda Tanga ni mbali sana.Viongozi wa Kagera Sugar
Ubutu wa safu ya ushambuliaji lilikuwa tatizo la kudumu kwa Kagera Sugar lakini kwa sasa limepata marekebisho kwani wamesajili Vijana wa nguvu msimu huu.

Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images