Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 570 | 571 | (Page 572) | 573 | 574 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wasanii wa kikundi cha wanawake wa cha Tanga cha Msanja baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Tanga kwa ziara ya siku moja ya kikazi Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo Chiku Gwao. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0

  Mkurugenzi Mkuu na Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Dunia, Dk. Sri Mulyani Indrawati (wapili kushoto) na Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe (watatu kushoto) wakimsikiliza kwa makini Meneja wa kitengo cha mafuta cha Kurasini Oil Jet (KOJ), Capt. Mwingamno wakati Dk. Sri Mulyani Indrawati alipokitembelea kitengo hicho kilichopo ndani ya bandari ya Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu na Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Dunia, Dk. Sri Mulyani Indrawati (katikati) na mwenyeji wake Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumzia jambo na Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadh Massawe wakati alipoitembelea bandari hiyo hivi karibuni.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Aloyce Matei akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu na Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Dunia, Dk. Sri Mulyani Indrawati (hayupo pichani) wakati alipoitembelea bandari hiyo hivi karibuni.
  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la DFID nchini Tanzania Bibi Ros Cooper akizungumza jambo wakati wa ziara ya Mkurugenzi Mkuu na Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Dunia, Dk. Sri Mulyani Indrawati alipoitembelea bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni.
  Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaabaan Mwinjaka, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la DFID nchini Tanzania Bibi Ros Cooper, Afisa Mtendaji Mkuu wa TradeMark East Africa (TMEA), Bw. Frank Matsaert na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Philippe Dongier wakisaini makubaliano maalumu (MoU) na TPA ya kuendeleza miradi mbalimbali maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam. Makubaliano hayo yalisainiwa mbele ya Mkurugenzi Mkuu na Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Dunia, Dk. Sri Mulyani Indrawati na Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe.
  Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe akikabidhi zawadi ya kuutangaza utalii wa Tanzania kwa Mkurugenzi Mkuu na Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Dunia, Dk. Sri Mulyani Indrawati wakati alipoitembelea Bandari ya Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu na Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Dunia, Dk. Sri Mulyani Indrawati (wapili kulia) na Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) wakimsikiliza kwa makini Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadh Massawe akifafanua jambo wakati Dk. Sri Mulyani Indrawati alipoitembelea bandari hiyo hivi karibuni.
  Mkurugenzi Mkuu na Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Dunia, Dk. Sri Mulyani Indrawati (wapili kulia) na Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mashirika ya Kimataifa, Wizara na TPA.Picha kwa hisani ya: Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)

  0 0

  Na Father Kidevu Blog
  Wanyange 30 wanao wanbia taji la Redd's Miss Tanzania 2014 leo wameingia kambini tayari kwa safari ya fainali za Miss Tanzania 2014 zitakazo fanyikia mapema mwezi Oktoba jiji Dar es Salaam.


  Warembo hao waliowasdili kwa muda tofauti kuanzaia saa 12 alfajiri ya leo na kupokelewa na waandaaji wa Miss Tanzania katika hoteli ya JB Belmont iliyopo katikati ya jiji la maraha la Dar. 


  Warembo kutoka Kanda ya Ziwa walitia fora pale warembo hao walipowasili kambini hapo wakiwa ndani ya gari ya Mshindi wa Kanda ya Ziwa ambayo alizawadiwa hivi kjaribuni katika shindano lao.
   Warembo wa Kanda ya Ziwa wakiteremka katika gari lao baada ya kuwasili na inaelezwa waliendesha kutoka jijini Mwanza.

  0 0

   Sehemu ya mbele.

   ENEO:      Nyumba ipo  PUGU-Umbali wa  mita 100  toka  Barabara Kuu ya lami. Nyumba  3 za familia zipo ndani  ya  eneo  moja  kila  moja  inajitegemea.
  UKUBWA: Kila  moja  ina vyumba  3 vya kulala, jiko, siting room kubwa na daining ya kutosha.
   UMEME:  Kila  moja  inatumia  Mita  ya Luku kwa kujitegemea.  pamoja  na  maji.
   PAKING:  Eneo kubwa kwa zaidi ya magari 5 kwa wakati mmoja.
  BEI.  Ni maelewano kuanzia  miezi  6  au zaidi kutegemea hitaji la mteja.
   kwa mawasiliano: 0686-569999
       Wako  katika makazi bora na ya kisasa. 

  0 0

  Wanyange 30 wanao wanbia taji la Redd's Miss Tanzania 2014 leo wameingia kambini tayari kwa safari ya fainali za Miss Tanzania 2014 zitakazo fanyikia mapema mwezi Oktoba jiji Dar es Salaam.
  Warembo hao waliowasdili kwa muda tofauti kuanzaia saa 12 alfajiri ya leo na kupokelewa na waandaaji wa Miss Tanzania katika hoteli ya JB Belmont iliyopo katikati ya jiji la maraha la Dar. 
  Warembo kutoka Kanda ya Ziwa walitia fora pale warembo hao walipowasili kambini hapo wakiwa ndani ya gari ya Mshindi wa Kanda ya Ziwa ambayo alizawadiwa hivi kjaribuni katika shindano lao.
   Warembo wakiwasili kambini
   Warembo wa Kanda ya Ziwa wakiteremka katika gari lao baada ya kuwasili na inaelezwa waliendesha kutoka jijini Mwanza. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Mimi Clement Bocco, napenda kuwakaribisha marafiki zangu, madiwani wenzangu wa manispaa ya kinondoni, wanakwaya wenzangu wa kkkt Kijitonyama, wanasiasa wenzangu, ndugu, jamaa na majirani zangu wote mje kufurahi pamoja na familia yangu kwenye sherehe ya mahafali (graduation) yangu ya Masters kwenye chuo cha IFM mwezi ujao tarehe 10.10.2014, baada ya ratiba ya chuoni itafuatiwa na tafrija itakayofanyika Sinza..hakuna kiingilio, KARIBUNI WOOOTE

  0 0

  Bwana Mfaume Kilangi wa Tuangoma Marela-Kigamboni Jijini Dar es Salaam anasikitika kutanga kifo cha baba yake mzazi MZEE IDRISA KILANGI  (pichani) kilichotokea alfajiri ya kuamkia leo jijini Dar es Salaam. Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa mtoto wa Marehemu, Mfaume Kilangi Marela Tuangoma jirani na Nyumba za NSSF.

  Mwili wa marehemu unataraji kusafirishwa kesho asubuhi saa 3:00 kwenda Iringa mjini kwa Mazishi.


  Habari ziwafiukie Ndugu Jamaa na Marafiki wote wa Familia ya Mzee Kilangi, popte pale alipo. 

  Enzi za Uhai wake Marehemu alikuwa Mkurunzi Mkuu wa Agrofocus, Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC) pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wasindikaji Korosho Tanzania (CPAT), na pia Rais wa Mpito wa African Cashew Alliance (ACA). 

  0 0

  Basi la Ruksa aina ya Scania lenye namba za usajili  T 273 ACX llililokuwa likitokea mkoani Kigoma kwenda wilayani Kahama mkoani Shinyang'a likiwa limepata ajali katika kijiji cha Kanyonza wilayani Kakonko,mkoani Kigoma ambapo watu Wawili walipoteza maisha papo hapo na wengine 65 kujeruhiwa katika Ajali hiyo ya Septemba 08,2014,majira ya saa Sita mchana
  Pichani juu na chini ni Jeshi la polisi wilaya ya Kakonko lilifika eneo hilo na kuwachukuwa waliojeruhiwa  na kuwapeleka katika hospitali ya wilaya  kwa ajili ya matibabu.
  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  0 0

   Makamu wa Rais Dkt Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Viongozi wa Taasisi ya Shirikisho ya kamati za Hijja alipowasili Viwanja vya Karimjee Dar es salaam leo
   Baadhi ya Mahujjaji wanaotarajiwa kwenda kutekeleza ibada ya Hijja huko Makka, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal alipokua akiwahutubia katika viwanja vya Karimjee Dar es salaam leo
   Baadhi ya Mahujjaji wanaotarajiwa kwenda kutekeleza ibada ya Hijja huko Makka, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal alipokua akiwahutubia katika viwanja vya Karimjee Dar es salaam leo 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwahutubia baadhi ya Mahujjaji wanaotarajiwa  kwenda kutekeleza Ibara ya Hijja huko Makka, katika viwanja vya Karimjee Dar es salaam leo  0 0


  0 0

  Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 
  Taasisi binafsi zimeshauriwa kutoa Likizo kwa Wafanyakazi wao pale wanapojifungua ili wapate muda wa kutosha wa kuwanyonyesha Watoto wao. Kufanya hivyo kutasaidia makuzi mema kwa Watoto hao sambamba na kuwaepushia magonjwa ambayo sio ya ulazima katika maisha yao. 
  Ushauri huo umetolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Khamis Jabir Makame kwa Niaba ya Waziri wa Afya katika hafla ya kilele cha Wiki ya Unyonyeshaji bora kwa watoto iliyofanyika kitaifa Nungwi Kaskazini Unguja. 
  Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hutoa siku 82 kwa wafanyakazi wake pale wanapojifungua ili kuwanyonyesha vyema watoto wao jambo ambalo linapaswa kuigwa na Taasisi binafsi. 
  Jabir amefahamisha kuwa ili kuboresha uhai na maendeleo bora ya Mtoto,Wazazi wanalazimika kufuata mipangilio bora ya unyonyeshaji ikiwa ni pamoja na kuwanyonyesha watoto wao mfululizo kwa muda wa miezi sita. 
  “Utaratibu wa kitaalamu ni Mtoto kunyonyeshwa Miezi sita mfululizo bila kupewa kitu chengine” Alisema Kaimu huyo wa Mkoa. 
  Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Jamala Adam Taibu amesema hali ya unyonyeshaji kwa Zanzibar hairidhishi ambapo watoto hunyonyeshwa kwa wastani wa Wiki mbili jambo ambalo ni hatari. 
  Amefahamisha kuwa Watoto wanaonyonyeshwa na Mama zao kwa wastani wa miezi sita bila kupewa chakula kingingne hupata kinga nzuri ya mwili na makuzi mema katika maisha yao.
  Dkt Jamala ameongezea kuwa Wazazi wanaofuata utaratibu nzuri wa unyonyeshaji huwasaidia pia kuepukana na magonjwa mbali mbali katika miili yao ikiwa ni pamoja na Ugonjwa wa Saratani ya Titi. 
  Awali Mkuu wa Shirika la Kuhudumia watoto duniani UNICEF Ofisi ya Zanzibar Bibi Francesca Morandini amefahamisha kuwa Mtoto anapocheleweshwa kunyonyeshwa au kupewa vitu vingine kabla ya kutimia miezi 6 Akili na Mwili wake hudumaa jambo ambalo litasababisha Taifa kukosa nguvu kazi bora mbeleni. 
  Ameshauri Wazazi wa Kiume kushirikiana vyema na Wake zao ili kuhakikisha Mtoto anapata haki yake ya Msingi ambayo imesisitizwa pia katika Vitabu vya Dini. 
  Kila ifikapo Septemba 13, Zanzibar hungana na nchi nyingine Duniani kuadhimisha Siku ya unyonyeshaji Bora Dunia ambapo malengo yake makuu ni kukumbushana Mikakati bora ya unyonyeshaji ili kuboresha Uhai na maendeleo ya Watoto duniani.
   Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini ‘A’ Khamis Jabir Makame akisalimiana na kina mama wanyonyeshaji waliofika katika madhimisho ya siku ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika huko kijiji cha Nungwi Kaskazini Unguja.
  Kaimu katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Jamala Adam Taib akitoa hutuba yake katika madhimisho ya siku ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika katika Kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  Baadhi ya waalikwa walioshiriki katika madhimisho ya siku ya Unyonyeshaji Duniani  wakitizama ngoma ya Mchikicho (haipo Pichani) iliyotumbuiza katika madhimisho hayo.
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini ‘A’ Khamis Jabir Makame akiwahutubia wananchi katika madhimisho ya siku ya Unyonyeshaji Duniani iliyoadhimishwa leo septemba 13 katika Kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja (kusho) Mwakilishi wa Shirika la kuhudumia watoto Dunia UNICEF Bi. Francesca Morandini. 
  Mgeni Rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini ‘A’ Khamis Jabir Makame wakati kati waliokaa akiwa katika Picha ya pamoja na Waalikwa waliofika katika madhimisho ya siku ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika huko kijiji cha Nungwi Kaskazini Unguja. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapunduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na  Mkurugenzi Mtendaji pia Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Dunia Bibi Sri Mulyani Indrawati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe aliofuatana nao leo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapunduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji pia Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Dunia Bibi Sri Mulyani Indrawati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe aliofuatana nao leo. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu, Zanzibar.

  0 0

   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na   Ali Juma Mkangala ,mmoja washiriki wa Mkutano wa Kutatua mgogoro wa kiwanda cha chai cha Liponda kilichopo Bumbuli Tanga. Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Ofisi  ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Septemba  13, 2014.
  Mbunge wa Mlalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Hassan Ngwilizi (kushoto) na Mbunge wa  Bumbuli , Januari Makamba (kulia) wakiteta na Waziri wa Kilimo , Chakula na Ushiriki Mhandisi Christopher  Chiza katika mkutano wa kutatua mgogoro wa kiwanda cha chai cha Liponde kilichopo Bumbuli Tanga kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga, Septemba 13, 2014. Kikao hicho kiliongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

  Shabba Ranks feat. Maxi Priest - "House Call"

  0 0


   Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu Joseph Simbakalia akikagua timu ya Simba wakati wa mchezo wa kirafiki na timu ya Ndanda FC uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
  Kikosi kamili cha timu ya Simba kilichopambana na Ndanda FC.
  Kikosi cha Ndanda FC kikiwa klatika picha ya pamoja kabla ya pambano lao na Simba.
  Wachezazaji wa Simba na Ndanda wakichuana katika uwanja wa Nangwanda Sijaona.
  Mashabiki wa soka wakifuatilia pambano la Simba na Danda FC.
  Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto) akiwasalimia wacheza ngoma ya asili ya nchini Kongo iliyokuwa ikichezwa na wakimbizi wenye asili hiyo wakati alipokuwa anaingia katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, Kasulu mkoani Kigoma kwa ajili ya kuzungumza nao. Waziri Chikawe alifanya mkutano na baadhi ya wakimbizi hao na kuwataka kulinda amani pamoja na kupinga ndoa za utotoni ambazo zinaendelea kushika kasi katika kambi hiyo kubwa inayowahifadhi zaidi ya wakimbizi 60,000.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu wakati alipofanya ziara ya kikazi katika kambi hiyo inayowahifadhi zaidi ya wakimbizi 60,000. Katika hotuba yake Waziri Chikawe aliwataka wakimbizi hao kupinga ndoa za utoto ambazo zinaendelezwa na baadhi ya familia za wakimbizi hao ambapo inawasababishia watoto hao wa kike kupata matatizo mbalimbali wakati wanapojifungua.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu, Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Waziri Chikawe ambaye yupo katika ziara ya kikazi katika kambi hiyo, aliwataka wakimbizi hao wadumishe amani pamoja na kupinga ndoa za utotoni ambazo zimeshika kasi katika kambi hiyo kubwa ambayo ina wahifadhi zaidi ya wakimbizi 60,000. Kushoto kwa Waziri ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akiwasalimia watoto wa wakimbizi wakati Waziri huyo alipokuwa anatembelea baadhi ya familia za wakimbizi hao kwa lengo la kuwasalimia pamoja na kuangalia jinsi maisha yao wanavyoyaendesha kambini hapo. Waziri Chikawe alifanya mkutano na wakimbizi hao na kuwataka kulinda amani na pia kupinga ndoa za utotoni ambazo zinaendelea kushika kasi katika kambi hiyo kubwa inayowahifadhi zaidi ya wakimbizi 60,000. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

   Mwanahabari Vedasto Msungu wa ITV (kushoto) na David Rwenyagira (Radio 5) walikuwa miongoni mwa wanahabari waliofika nje ya Jengo la Mahakama Kuu ya Pretoria ambapo ilikuwa siku muhimu ya utoaji hukumu kwa mwanariadha Oscar Pistorius aliyeshitakiwa kwa makosa ya kumuua mpenzi wake kwa silaha. Unayoyaona hapo nyuma ni magari maalum ya urushaji tukio hilo moja kwa moja katika vyombo mbalimbali vya habari duniani(OB Van) na mahema meupe ni Kambi iliyopigwa na wanahabari hao kwa ajili ya kufuatilia tukio hilo muhimu.
  Wanahabari Vedasto Msungu na David Rwenyagira walipata nafasi ya kumhoji raia huyu wa Afrika Kusini juu ya maoni yake kwa hukumu iliyotarajiwa kutolewa.
   Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 waliweza kufika hadi katika Hifadhi ya Taifa ya Pilanesberg ili kujionea wanyama mbalimbali. Kutoka Kushoto ni Mtanzania Peter Masika anayeishi Johannesburg, Vedasto Msungu (ITV), Pascal Shelutete(Meneja Mawasiliano TANAPA) na Gerald Kitabu wa The Guardian.


  0 0


  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kimanzichana leo wakati alipoanza Ziara yake ya mikoa ya Pwani ,Tanga na Iringa Ikiwa ni kuimarisha Chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2010 huku akihimiza wananchi kushiriki katika shughuli za kujiletea maendeleo katika maeneo yao, Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi na leo amefanya shughuli mbalimbali katika ziara hiyo.2 
  Mbunge wa jimbo la Mkuruanga na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Adama Malima akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mkuranga wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo leo.3 
  Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh. Mercy Silla akwahutubia wananchi wa kata ya Kimanzichana kwenye mkutano wa hadhara leo.5 

older | 1 | .... | 570 | 571 | (Page 572) | 573 | 574 | .... | 3348 | newer