Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 571 | 572 | (Page 573) | 574 | 575 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Washiriki wa shindano la dance 100% wa kundi la”Wakali sisi” Buguruni jijini Dar es Salaam,wakionesha umahiri wao wa kudansi wakati wa mchuano wa nusu fainali ya shindano hilo lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania lililofanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay,Makundi 5 kati ya 10 yameingia fainali itakayofanyika mwezi ujao.
  Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu,akikausha maji ya mvua iliyokuwa ikinyesha kwa wingi wakati shindano la nusu fainali ya Dance 100% na kusababisha shindano hilo kusimama mara kwa mara,Makundi 5 kati ya 10 yaliingia fainali itakayofanyika mwezi ujayo.Shindano hilo lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania lilifanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay.
  Washiriki wa shindano la dance 100% wa kundi la ”The Winners Crew” la jijini Dar es Salaam,wakionesha umahiri wao wa kudansi wakati wa mchuano wa nusu fainali ya shindano hilo lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania lililofanyika kwenye viwanja vya Don Bosco Oysterbay,Makundi 5 kati ya 10 yameingia fainali itakayofanyika mwezi ujao.


  0 0

  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Margareth Sitta akifungua semina ya Wanawake iliyohusu kuwawezesha wanawake katika masuala ya uongozi, utatuzi wa migogoro pamoja na harakati za uchaguzi iliyofanyika leo 13 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Pindi Chana akiwahutubia baadhi ya wanawake na wanaume waliohudhuria semina maalum iliyohusu kuwawezesha wanawake katika masuala ya uongozi, utatuzi wa migogoro pamoja na harakati za uchaguzi iliyofanyika leo 13 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  Mwakilishi wa Shirika la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) akichangia mada wakati wa semina ya wanawake iliyofanyika leo 13 Septemba, 2014 ambayo ikihusu iliyohusu kuwawezesha wanawake katika masuala ya uongozi, utatuzi wa migogoro pamoja na harakati za uchaguzi iliyofanyika leo 13 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  Baadhi ya wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia uwasilishwaji wa mada toka kwa viongozi wakati wa semina hiyo.


  0 0

   Warembo wanaoshiriki shindano la Redd's Miss Tanzania 2014 leo wameingia siku ya pili ya kambi yao jijini Dar es Salaam na baada ya semina asubuhi na mapumziko ya mchana jioni hii wamefanya mazoezi katika chumba maalum cha mazoezi 'Gym', ungana na mpigapicha wa Father Kidevu Blog katika picha mbalimbali za warembo hao katika kambi yao.   0 0
 • 09/14/14--09:34: YANGA YAIFUNGA AZAM FC 3-0
 • Mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngasa, kushoto akimtoka  beki wa Azam FC, Erasto Nyoni katika mchezo wa Ngao ya Hisani uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanya imeshinda 3-0.
   
  Kikosi kamili cha Yanga kilichoifunga Azam FC 3-0 katika mchezo wa Ngao ya Hisani leo.
  Kikosi cha Azam FC.

  0 0

  05 GOT_6307 (HH the Aga Khan and PM Harper unveil a plaque at the opening of the Aga Khan Museum as Prince Amyn Aga Khan and Minister Glover look on - AKDN Gary Otte)
  HH the Aga Khan and PM Harper unveil a plaque at the opening of the Aga Khan Museum as Prince Amyn Aga Khan and Minister Glover look on - AKDN / Gary Otte).
  11 DSC_0460 (PM Harper and HH the Aga Khan waving to crowds outside the Ismaili Centre, Toronto - AKDN Zahur Ramji)
  PM Harper of Canada and HH the Aga Khan waving to crowds outside the Ismaili Centre, Toronto - AKDN / Zahur Ramji).

  The Right Honourable Stephen Harper, Prime Minister of Canada, and His Highness the Aga Khan formally opened the Ismaili Centre Toronto and Aga Khan Museum today. These projects, which are initiatives of the Aga Khan, the 49th hereditary Imam of the Shia Ismaili Muslims and founder and Chairman of the Aga Khan Development Network, are intended to foster knowledge and understanding both within Muslim societies and between these societies and other cultures.

  Speaking at the opening ceremony of the Ismaili Centre, His Highness the Aga  Khan saluted the many leaders, volunteers and staff who have made possible the completion of these new institutions, including the Prime Minister, and many members of government at the federal, provincial and municipal levels. These spaces “will be filled with sounds of enrichment, dialogue and warm human rapport, as Ismailis and non-Ismailis share their lives in a healthy gregarious spirit," he remarked.

  Prime Minister Harper commented that the site will be “a source of inspiration, spiritual renewal and cultural awareness,” not only for Torontonians, but for all visitors. The Prime Minister paid a special tribute to the Aga Khan’s vision of Islam, which “stresses its social traditions of peace, tolerance and pluralism."

“The decision to establish this significant initiative in Canada reflects the deep and longstanding partnership between the Imamat and Canada,” said the Prime Minister. 
  FOR MORE NEWS CLICK HERE

  0 0  0 0

  Yafuatayo ni majina yaliyotangazwa na bench la ufundi la timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa FC) ambayo itafanya ziara mkoani Iringa kuanzia Oktoba 3. Majina hayo yamepitishwa na kikao cha uongozi wa timu na kuamua kuyaweka hadharani kwa sababu mbalimbali.

  MAJINA YA WACHEZAJI
  1.       Mwarami Seif
  2.       Mbozi Katala
  3.       Edward Mbaga
  4.       Elius Kambili
  5.       Wilbert Molandi
  6.       Eddo Kumwembe
  7.       Faustine Felician
  8.       Julius Kihampa
  9.       Zahoro Mlanzi
  10.   Fred “Chuji” Mbembela
  11.   Deogratius “Super Deo” Maganga
  12.   Athumani  Jabiri
  13.   Sweetbert Lukonge
  14.   Martin Peter
  15.   Muhidin Sufiani
  16.   Gulle Mandago
  17.   Saleh Ally
  18.   Mohamed Akida
  19.   Peter Mchome
  20.   Deus Saleh
  21.   Ally
  22.   Hussein Omary
  WAKUU WA BECNCHI LA UFUNDI:
  23.   Ally Mkongwe
  24.   Saidi Seif
                 UONGOZI:
  25.   Majuto Omary-Mwenyekiti-Mkuu wa Msafara
  26.   Salum Jaba-Makamu

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha mjumbe malumu wa Rais Salvar Kiir Mayardit wa Sudani Kusini,Jenerali James Kok Ruea alieleta Ujumbe maalum toka kwa Rais huyo wa Sudan Kusini Jumamosi September 14, Ikulu jijini Dar es salaam. Mjumbe huyo aliongozana pia na Mkuu wa Kituo cha Martti Ahtisari (Martti Ahtisari Centre) kwa nchi za Afrika chini ya Jangwa la Sahara, Bw. Itonde Kakoma.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekisoma ujumbe maalumu toka kwa Rais Salvar Kiir Mayardit wa Sudani Kusini ulioletwa na mjumbe malumu Jenerali James Kok Ruea Jumamosi September 14, Ikulu jijini Dar es salaam. Mjumbe huyo aliongozana pia na Mkuu wa Kituo cha Martti Ahtisari (Martti Ahtisari Centre) kwa nchi za Afrika chini ya Jangwa la Sahara, Bw. Itonde Kakoma.


  0 0

   Msondo Ngoma Music Band (formerly known as NUTA Jazz Band, renamed Juwata Jazz Band, and then OTTU Jazz Band) is an influential and long-lived Tanzanian muziki wa dansi (Bongo Dansi). Having been established in 1964, it is the oldest active dansi band in Tanzania as well in Africa.

  The band began in 1964 and was originally named "NUTA Jazz Band", after its sponsor, the National Union of Tanganyika (NUTA), which was the main Tanzanian trade union. In the early years of dansi, the NUTA Jazz Band was very influential both artistically and in terms of financial organization; namely, it was one of the first dansi bands to constitute itself into a "cooperative" of salaried musicians (a model that would become widespread in the 1970s).
  In the 1960s, NUTA Jazz Band was led by trumpeter-singer  late Joseph Lusungu  and saxophonist Mnenge Ramadhani, who defined the brass-centered sound of the band.
  NUTA Jazz Band held its position as one of the major Tanzanian dansi bands throughout the latter half of the 1960s and most of the 1970s. In 1977 it experienced a major change in personnel, with many of its most talented musicians (including Muhiddin Maalim Gurumo and Hassani Rehani Bitchuka) leaving the band to form a new ensemble, Mlimani Park Orchestra. In 1977, the band changed its name to "Juwata Jazz", after the Swahili name of its sponsor (NUTA), Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania. About at the same time, guitarist Saidi Mabera became the new leader of the band. He wrote several of Juwata's hit songs of the 1980s. After Mabera, both Maalim and Bitchuka (who rejoined the band in 1991) became leaders.Late Muhidini Gurumo is credited with on the major hits of Juwata in the 1990s, Usia kwa watoto.
  The band changed its name again in 1991 from Juwata Jazz to OTTU Jazz, when the trade union that sponsored it was renamed Organization of Tanzanian Trade Unions. The band is still active as "Msondo Ngoma", performing regularly at different venues in Dar-es-salaam, including their weekly show every Friday at the Leaders Club, for example,and is the oldest active dansi band in Tanzania as well as in Africa. This is reflected by its motto baba ya muziki, "father of music".
  "Msondo Ngoma Music Band" also known as "Baba ya Muziki" means "father of Music" .
  You may book or Contact band manager Mr. Kibiriti 
  Telephone +255 (0)655921223


  0 0

  Msanii mwingine anaekuja vyema kwenye anga ya muziki wa Bongofleva aitwaye Kadja ambaye anatamba na wimbo wake wa Maumivu niache akiimba pamoja na Linah.
  Mkali wa Bongo Hip Hop Farid Kubanda a.k.a Fid Q akikamua vilivyo juu ya jukwaa na la Fiesta.
  Msanii wa Bongofleva,Kadja akiimba wimbo wake wa Maumivu niache mbele ya maelfu ya wakazi wa Tabora (hawapo pichani) waliofika kwenye tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo.
   Ilikuwa buruuudani ya kusambaza upendo wa kweli kwa wakazi wa Tabora ndani ya tamasha la Fiesta
  Palikuwa hapatoshi usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mjini Tabora,ambapo tamasha la Fiesta lilirindima.
  Wasanii chipukizi kutoka Tabora nao walionesha umahiri wao jukwaani
  Sehemu ya umati mkubwa wa watu waliofika kulishuhudia tamasha la Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mjini Tabora.PICHA NA MICHUZI JR-TABORA

  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh,Stephen Masele akizungumza kwenye uzinduzi huo uliovuta hisia za wanakijiji wengi.Naibu Waziri wa Nishati na Madini akizungumza na Wananchi Mkurugenzi Mtendaji wa Geita Gold Mine,Michael Van Anen Mwakilishi Mwandamizi kutoka Benki ya Dunia ambaye pia ni mtaalamu wa madini kutoka idara ya nishati endelevu nchini Marekani,Bwa.Mamadou Barry akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi mkubwa wa uchimbaji madini kwa wachimbaji wadogo wadogo katika kijiji cha Lwamgasa mkoani Geita,hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele.Mradi huo Umefadhiliwa na Benki ya Dunia na Serikali kwa kushirikiana na Wawekezaji wakubwa wakiwemo Geita Gold Mine na African Barrick Gold Mkuu wa Wilaya ya Geita ,Mh.Omary Mangochie akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi huo.
  VIDEO CLIP NA MICHUZI JR-LWAMGASA-GEITA

  0 0

  Mdau Hendrich Nambira au Kenny kama alivyojulikana kwenye mchezo wa kuigiwa wa Mambo hayo katika runinga ITV wakati huo, Alifunga pingu za maisha na mke wake Florence kutoka Visiwani Zanzibar. Harusi ilifanyika katika kanisa la Anglican UMCA, Upanga jijini Dar es Salaam  tarehe 23/08/2014. 

  Mama Bishanga na mumewe hawakuweza kuwahi siku ya harusi hiyo iliyopendeza sana na kuhudhuriwa na ndugu wengine wakiwemo wadogo wa mama Bishanga Mack Innocent Hatia na Constancia Innocent Hatia, baba mkubwa mzee John Kamota na shangazi Rehema Kamota, bibi wa Kenny mwalimu Agnes Innocent Hatia na ndugu zetu wengine, pia marafiki na wawakilishi wa wasanii toka Bongo movie. Sherehe ya kukata na shoka ilifanyika Lion Hotel.
  Bwana harusi Kenny na mkewe Florence wakiwa pwani Oster Bay mara baada kumeremeta kwao.
  Maharusi wakikata keki ya harusi yao
  Kaka wa bwana harusi Kilian Kamota na mama yao mdogo Fridah Mchauru wakipiga cheers ya shampein .
  Dada wa bwana harusi Sizelina ambae ni mtoto wa kwanza wa mama Bishanga akilisakata rumba kwa raha na furaha tele ya harusi ya mdogo wake.

  0 0

  Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Ally Kessy(kulia) na Mohammed Raza (kushoto) wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa kikao cha arobaini cha Bunge hilo.
  Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wakielekea kuhudhuria kikao cha arobaini cha Bunge hilo. picha na MAELEZO_DODOMA

  0 0

  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuanzia mwezi ujao, Oktoba 2014, itaanza zoezi la kuvihakiki Vyama vya Kijamii hapa nchini.


  Pamoja na mambo mengine, zoezi hili linalenga kuvifuta kutoka katika daftari la Msajili vya Vyama vya Kijamii vyama ambavyo vitabainika kuwa havina sifa tena ya  kuendelea kuwa katika daftari hilo.


  Vigezo ambavyo vinaweza kusababisha chama kufutwa kutoka katika Daftari la Msajili wa Vyama vya Kijamii ni pamoja na kutolipa ada za mwaka kwa wakati na kutowasilisha kwa Msajili taarifa za kila mwaka za utendaji kazi na mapato na matumizi ya fedha za chama husika.  Kigezo kingine ni kwa chama kufanya shughuli tofauti na zile zilizoandikishwa katika katiba ya chama husika.

  Ili kuvishirikisha vyama husika, Wizara wakati wa kuanza zoezi hili itachapisha katika baadhi ya magazeti majina ya vyama vyote vya kijamii vilivyopo katika kumbukumbu za daftari la Msajili wa Vyama vya Kijamii.

  Baada ya kutangaza majina hayo, kila chama cha kijamii kitatakiwa kuhakikisha kuwa kimetekeleza matakwa ya kisheria yaliyobainishwa wakati wa usajili wa chama husika.

  Baada ya  kipindi cha miezi mitatu tangu kutangazwa kwa tangazo hilo, Wizara itaanza kuchukua hatua za kisheria, ikiwa ni pamoja na kukifuta katika daftari la Msajili chama cha kijamii ambacho kitakuwa hakijatekeleza matakwa hayo. 

  Aidha, pamoja na mambo mengine, taarifa zitakazopatikana kutokana na zoezi hili la uhakiki pia zitawezesha kuanzishwa kwa database ya vyama vya kijamii ambayo itasaidia kuboresha mawasiliano kati ya Msajili wa Vyama na vyama hivyo.

  Hadi sasa Daftari la Msajili wa Vyama vya Kijamii linaonyesha kuwepo kwa vyama vya kijamii 9,554 kote nchini. Kati ya hivyo, vyama vya kidini ni 956 na vyama vingine 8,598.

  Jukumu la kusajili na kusimamia Vyama vya Kijamii linafanyika chini ya Sheria ya Vyama vya Kijamii SURA 337 (Societies Act Cap. 337) iliyofanyiwa mapitio mwaka 2002.

  Vyama vinavyosajiliwa chini ya Sheria hii ni pamoja na vyama vya kidini, vyama vya kitaaluma  na vyama vya maendeleo ya kijamii.


  Imetolewa na:

  Isaac J. Nantanga

  MSEMAJI


  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia moja kati ya miti 19,270 ya korosho iliyoharibika  alipokwenda kukagua shamba la hekali 1000 katika Kijiji cha Magawa wakati wa ziara yake wilayani Mkuranga ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.PICHA NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Kinana akiongoza kukagua shamba la mikorosho iliyoharibika na kuwafanya wananchi wa Kijiji cha Magawa kuwa masikini.
   Kinana akisaidia kuranda mbao baada ya kufungua Tawi la Vijana wajasriliamali la Mayuyu Mjini Utete, Wilayani Rufiji leo
   Kinana na Nape wakiangalia viti walivyozawadiwa na kikundi hicho cha vijana. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0


  0 0

  Mgeni rasmi katika mapambano mawili ya ngumi ya kimataifa ,mkuu wa wilaya ya Hai ,Novatus Makunga akiteta jambo na Mwenyekiti wa chama cha Ngumi mkoa wa Kilimanjaro Elikunda Kipoko wakati wa mapambano hayo 
  Mgeni rasmi katika mapambano mawili ya ngumi ya kimataifa ,mkuu wa wilaya ya Hai ,Novatus Makunga akizungumza wakati wa mapambano hayo kati ya Bondia Said Yazidu(Tanzania) na Djamel Dahou(Aljeria) .
  Aleck Mwenda pia akajibu mapigo ingawaje yake yalionekana makali zaidi.
  Kamanda wa Polisi wa wilaya OCD, Deodatus Kasindo akamkabidhi mkanda Alibaba.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imefungua duka lake la Dodoma kufatia ukarabati uliokuwa unafanyika wa kuliweka duka hilo kuwa la kisasa zaidi ili kuweza kuendelea kuwapatia wateja wake huduma bora zaidi.

  Uzinduzi wa duka hilo ulifanywa na mkuu wa mkoa wa dodo dkt Rehema Nchimbi ambapo amewapongeza Airtel kwa mpango kabambe wa kuboresha maduka yake nchini pamoja na duka la Dodoma.

  Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba alisema,"Leo tunazindua rasmi duka hili lenye muundo mpya lililopo katika barabara ya Mkuu hapa Dodoma ikiwa ni moja kati ya mikakati yetu ya kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zetu na kupunguza msururu wa wateja wanaoingia dukani hapa kupata huduma mbalimbali.

  Kwa kupitia duka hili wateja wetu watafurahia huduma zetu za pesa mkononi za Airtel Money ,internet na kuweza kununua muda wa maongezi pamoja bidhaa zikiwemo simu za mkononi na vifaa vya huduma za mawasiliano na huduma nyingine nyingi.

  Sasa wateja wetu wanauhakika wa kupata huduma bora kwa haraka zaidi kupitia duka hili. Tutaendelea kutoa huduma za kibunifu zenye uhakika na zenye ubora wakati wote kupitia mtandao wetu bora na mpana ulioenea zaidi nchini. Lengo letu ni kuhakikisha tuwapatia wateja wetu uzoefu tofauti katika huduma zetu na kufikia matarajio yao. aliongeza Lyamba.

  Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh, Dkt Rehema Nchimbi alisema" nawapongeza sana Airtel kwa juhudi hizi za kuboresha utoaji wa huduma za mawasiliano kwa watumiaji nchini. Sote tunatambua mawasiliano ni nyenzo muhimu katika kuunganisha jamii na kuendesha shughuli za kibiashara na kiuchumi nachukua fulsa hii kuwaomba wakazi wa Dodoma watumie vyema nafasi hii kupata huduma bora zitakazorahisisha uendeshaji wa Shughuli zao mbalimalbali za kila siku".

  "Serikali inaunga mkono juhudi zinazofanywa na Airtel na kuwaomba waendelee kuwekeza zaidi katika kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasilaino nchini. tuko tayari kushirikiana Airtel katika kuhakikisha tunaweka mazingira bora ya kuendesha biashara ili kuwawezesha wananchi wetu kufaidika na huduma hizi za mawasiliano na hatimaye kuwa maisha bora."

  Airtel imeendelea kuboresha maduka yake nchini ambapo hivi karibuni imezindua maduka yake mapya katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha Mwanza Mbeya na Mtwara. Maduka mengine ya Morogoro, Bukoba na Zanzibar yanategemewa kuzinduliwa kabla ya mwisho wa mwezi huu wa septemba.
  Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema (kati) akikatata utepe kuashiria kulizindua rasmi duka la Airtel Dodoma lililopo barabara ya Mkuu mkoani humo, anaeshuhudia wakwanza kulia ni mkurugenzi wa airtel huduma kwa wateja Bi, Adriana Lyamba na Meneja biashara wa Airtel Dodoma Bw, Stephen Akyoo wakwanza kushoto, Airtel imefanya uzinduzi wa duka hilo jana baada ya kuzindua maduka mengine katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha Mwanza Mbeya na Mtwara. Maduka mengine ya Morogoro, Bukoba na Zanzibar pia yanatarajiwa kuzindulia mwezi huu.
  Meneja mauzo wa Airtel Mkoa wa Dodoma Bw Stephen Akyoo akiwa na wafanyakazi wengine wa Airtel Dodoma akitoa maelezo mafupi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi kuhusiana na muonekano wa duka jipya la Airtel Dodoma lililopo barabara ya Mkuu muda mfupi kabla ya mkuu wa mkoa huyo kuzindua duka hilo jana.
  Kati kati ni Mkuuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema nchimbi akiwa na Mkurugenzia wa huduma kwa Mteja Airtel Bi Adriana Lyamba (shoto) na Meneja wa Duka hilo mkoani hapo Bi Elida kulia wakikata keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya uzinduzi wa duka jipya la Airtel mtaa wa Mkuu mjini Dodoma jana.
  Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi akiongea na wananchi na wanahabari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel mkoani Dodoma barabara ya mkuu Jana, Airtel ilizindua duka hilo kwa dhumuni la kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake nchini.
  Wafanyakazi wa Airtel mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya Airtel kufungua Duka jipya mkoani hapo mtaa wa Mkuu jana, picha na mpigapicha wetu.

  0 0


  0 0

  Mganga Mkuu wa Zahanati ya TPA, Dkt. Mkunde Mlay akifungua mafunzo ya namna ya kukabiliana na Ebola kwa Wafanyakazi wa Bandari ya Dar es Salaam wa vitengo vya afya, zimamoto na ulinzi. Mafunzo hayo yalitolewa hivi karibuni bandarini hapo na madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
  Dkt. Juma Mfinanga wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, akieleza jambo kwa wafanyakazi wa Bandari ya Dar es Salaam namna ya kukabiliana na Ebola.
  Mfano wa vazi maalumu la kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ebola likioneshwa kwa wafanyakazi wa Bandari ya Dar es Salaam.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Bandari ya Dar es Salaam kutoka vitengo vya afya, zimamoto na ulinzi wakifuatilia mada ya namna ya kujikinga na virusi vya Ebola na kuwahudumia wagonjwa wa Ebola.


older | 1 | .... | 571 | 572 | (Page 573) | 574 | 575 | .... | 3348 | newer