Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 569 | 570 | (Page 571) | 572 | 573 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Mwigizaji nyota wa filamu nchini Steven Jacob a.k.a JB "akitema yai" wakati akitoa mada yake kwenye  wa uzinduzi wa Ripoti ya Benki ya Dunia Kuhusu ajiora Zenye Tija Tanzania leo Septemba 12, 2014 katika hoteli ya Hyatt regency kilimanjaro
   Rais Kikwete akimpongeza mwigizaji nyota wa filamu nchini Steven Jacob a.k.a JB kwa kutoa mada yake vyema wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Benki ya Dunia Kuhusu ajiora Zenye Tija Tanzania leo Septemba 12, 2014 katika hoteli ya Hyatt regency kilimanjaro
   Mwigizaji nyota wa filamu nchini Steven Jacob a.k.a JB akisalimiana na Bi Sri Mulyani Indrawati baada ya kutoa mada yake katika  uzinduzi wa Ripoti ya Benki ya Dunia Kuhusu ajiora Zenye Tija Tanzania leo Septemba 12, 2014 katika hoteli ya Hyatt regency kilimanjaro
   Rais Kikwete akiendelea kumpongeza mwigizaji nyota wa filamu nchini Steven Jacob a.k.a JB kwa kutoa mada yake vyema wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Benki ya Dunia Kuhusu ajiora Zenye Tija Tanzania leo Septemba 12, 2014 katika hoteli ya Hyatt regency kilimanjaro.

  0 0

   Mpiganaji Danford Mpumilwa, Afisa Habari wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia mauaji ya Kimbari ya Rwanda (UN-ICTR) yenye makazi yake mjini Arusha.akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wa Uganda mjini Kampala kuhusu kazi za mahakama hiyo inayoadhimisha miaka 20 mwezi Novemba mwaka huu. Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mambo ya Nje wa Mahakama hiyo Bocar Sy. ICTR inategemea kumaliza kazi zake hapo mwakani baada ya kuwakamata na kuwahukumu watuhumiwa 83 kati ya 92 waliokuwa wakitafutwa kwa kuhusika na mauaji hayo. Watu 9 bado wanatafutwa. 


  0 0

   Ankal akiwa na wapiganaji Max (kushoto) na Mike wa Jamii Forum kwenye uzinduzi wa ripoti ya Benki ya Dunia Kuhusu Ajira Zenye Tija Tanzania leo katika hoteli ya Hyatt regency kilimanjaro
  Wapiganaji wa Jamii Forum Max na Mike wakiwa hewani live kwenye uzinduzi wa ripoti ya Benki ya Dunia Kuhusu Ajira Zenye Tija Tanzania leo katika hoteli ya Hyatt regency kilimanjaro

  0 0

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dk.Seif Rashid (kushoto) akimsikiliza Ofisa Mkuu wa taasisi ya Udhibiti na Kinga ya Magonjwa ya CDC, Angela Makota (kulia) kwenye makabidhiano ya hundi ya Sh. Milioni 149 iliyotolewa na Vodacom Foundation kwa ajili ya kuunga mkono kampeni ya kuboresha huduma ya afya na Uzazi na Mtoto inayojulikana kama Wazazi Nipendeni.Makabidhiano yalifanyika katika ofisi ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam jana.Katikati ni Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Georgia Mutagaghywa.
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Waziri wa Afya (kushoto) akipokea mfano wa hundi wa fedha Sh.Milioni 149 iliyotolewa na Vodacom Foundation kwa ajili ya kuunga mkono kampeni ya kuboresha huduma ya afya na Uzazi na Mtoto inayojulikana kama Wazazi Nipendeni. Anayekabidhi ni Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusuiano wa Vodacom Tanzania, Georgia Mutagaghwa.Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Ofisa Mkuu wa taasisi ya Udhibiti na Kinga ya Magonjwa ya CDC, Angela Makota.
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid (katika) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, kituo cha Udhibiti na Kinga cha CDC na wizara hiyo mara baada ya makabidhiano mfano wa hundi ya fedha Sh.Milioni 149 iliyotolewa na Vodacom Foundation kwa ajili ya kuunga mkono kampeni ya kuboresha huduma ya afya na Uzazi na Mtoto inayojulikana kama Wazazi Nipendeni. Hafla ya makabidhiano yalifanyika katika ofisi za wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam jana.

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wa nne kushoto) akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya WENTWORTH inayochimba gesi katika eneo la Mnazi Bay Mkoani Mtwara , Robert MacBean (wa tatu kushoto) mara baada ya kusaini Makubaliano ya Mkataba wa Kuuziana Gesi kati yake na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Wengine katika picha ni baadhi wa Watendaji Wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC na wawakilishi wa kampuni za WENTWORTH na MAUREL & PROM.
  Wajumbe waliohudhuria kikao cha Kusaini Mkataba wa Kuuziana Gesi kati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na Kampuni zinazochimba gesi katika eneo la Mnazi Bay Mkoani Mtwara za WENTWORTH Resources Limited na MAUREL & PROM wakisaini MKataba huo. Anayeshuhudia mbele ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo pamoja na wawakilishi wengine kutoka kampuni hizo, TPDC, Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
  Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) James Andilile (wa kwanza kulia) wakipitia Mkataba kwa pamoja na mmoja wa wawakilishi wa Kampuni hizo wakati wa kusaini Mkataba huo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya MAUREL & PROM, Michael Hochard na wa kwanza ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya WENTWORTH Robert MacBean.

  0 0

  Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa (Bawacha), wakifungua shampeni kusherehekea ushindi wa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema Taifa, Halima Mdee (kushoto) baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo. (Picha na Francis Dande)
   Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bara), Hawa Mwaifunga akilia kwa furaha baada ya kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika juzi.
   Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Baraza la Wanawake wa Chadema wakiwa katika mkutano huo.
   Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema Taifa, Halima Mdee (kulia) akipongezwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa Baraza la Wanawake wa Chadema. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bara), Hawa Mwaifunga.
   Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema Taifa, Halima Mdee (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wake (Bara), Hawa Mwaifunga (kushoto) na  Makamu Mwenyekiti (Zanzibar), Hamida Abdallah.
  Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema, Halima Mdee akizungumza baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Baraza hilo.

  0 0

  Kiungo mshambuliaji wa Simba, Amri Kiemba (katikati),  akiwatoka  mabeki wa timu ya URA ya Uganda  katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. URA imeshinda 1-0. (Picha na Francis Dande)

  0 0

  Rais wa Soko la Almasi la Antiwerpen Mhe. Stephane Fischler (katikati) akizungumza na Mabalozi wa Afrika wanaokaa Ubelgiji wa nchi zinazozalisha almasi. Soko la Almasi la Antiwerpen kila mwaka linauza almasi yenye thamani ya Euro bilioni 52. Rais huyo pamoja na mambo mengine amewaeleza Mabalozi mpango wa soko hilo kuanzisha utaratibu wa kutoa takwimu za uzalishaji na mwenendo wa bei ya almasi katika soko la dunia. Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala ameshiriki katika kikao hicho kilichofanyika Antiwerpen Ubelgiji.

  0 0  0 0

  Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania JUKATA Deusi Kibamba akizungumza na wanahabari leo jijini dar es salaam juu ya mchakato huo wa katiba mpya. 
  Jukwaa la katiba Tanzania (JUKATA) leo wamemtaja mwenyekiti wa  bunge maalum la katiba mh SAMWELI SITTA  pamoja na mwanasheria mkuu wa serikali mh JAJI  FREDRICK WEREMA kuwa ndio maadui wapya wawili wakubwa wa mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya.
  Akizungumza na wanahabari jiji ni Dar es salaam mwenyekiti wa JUKATA ndugu DEUCE KIBAMBA amesema kuwa watu hao wawili watanzania waelewe kuwa ndio chanzo cha kukwama kwa mchakato huo kwa kile ambacho amekiita ni kuweka maslahi yao mbele kuliko maslahi ya watanzania kwa ujumla.

  Mh KIBAMBA anasema mwenyekiti wabunge hilo mh SAMWELI SITTA  huku akijua kabisa kuwa  bunge maalum la katiba linapaswa kutoongozwa na mtu mwenye maslahi ya moja kwa moja katika serikali  aliamua kugombea katika nafasi hiyo ya uenyekiti na kukubali kuchaguliwa kwake huku akiwa ni kinara wa kushambulia vyombo vya habari,pamoja na upotoshaji mkubwa wa mchakato huo.
  “Mfano mheshimiwa Sitta alitoa tamko lake kuwa hadhi ya bunge maalum la katiba ipo juu kidogo ya tume ya mabadiliko ya katiba ni upotoshaji wa makusudi wakati iko wazi kuwa vyombo hivyo viwili viko sawa kabisa, labda anataka kuonyesha kuwa yuko juu ya jaji Warioba”alisema mh Kibamba.

  Aidha amesema kuwa mwenyekiti huyo mh Sitta ameamua kuendelea na bunge maalum la katiba huku akijua wazi kuwa upatikanaji wa katiba mpya haupo huku akiwa ni kinara wa kuwaaminisha watanzania kuwa katiba mpya itapatikana hata kama hakuna ushiriki wa UKAWA,wala waziri wa katiba na sheria wa Zanzibar,na mwanasheria mkuu wa Zanzibar,ambao nao wamejitoa katika mchakato huo.

  Akimzungumzia mwanasheria mkuu wa Tanzania jaji FREDRICK WEREMA amesema kuwa jaji huyo amekuwa bingwa wa kutoa tafsiri tata ambapo aliwahi kushauri kuwa tafsiri ya siku 70 ya bunge hilo ni pamoja na siku za mapumziko na sikukuu ndipo wabunge walianza kufanya kazi hadi siku za jumamosi na baadae alitoa tafsiri tofauti tena ambayo imewafanya wabunge kutofanya kazi siku za mapumziko.

  “mh WEREMA amekuwa mshauri mbaya wa viongozi wa bunge hilo akiwaminisha mambo ambayo siyo, ambapo amewashauri kuwa mchakato wa katiba unaweza kukamilika bila hata ya wajumbe waliotoka nje,ndugu werema amekuwa akishauri pia muundo wa serikali tatu ulio katika rasimu unaweza kubadilika kirahisi tu jambo ambalo linapingwa na wanasheria wengi”amesema mwenyekiti wa JUKATA.
  Akizungumzia maamuzi ambayo jukata wamechukua kuhusu
  viongozi  KIBAMBA amesema kuwa viongozi hao kutokana na makosa yao wameamua kuwatangaza rasim kuwa maadui wapya wa katiba mpya ambapo wamesema kuwa wanapendekeza kuwa wasifikiriwe kupewa nafasi yoyote ya uongozi ndani ya nchi hii kwa miaka kumi  ili wapate nafasi ya kujifikiri na kujitathmini.

  Aidha katika hatua nyingine JUKATA wamemtaka mwenyekiti wa bunge maalum la katiba kusitisha mara moja bunge hilo ambapo wametao wiki mbili na kama halitasitishwa wao kama JUKATA kwa wingi wao wataelekea mjini Dodoma wakiwa na makufuki kwa ajili  ya kulifunga wenyewe.

  0 0

   Baadhi ya waandishi wa habari wanaosafiri kwenda Malawi wakiwa wanamsikiliza Katibu tawala msaidizi wakati wa kuagana.
   Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mbeya, Leonard Magacha akizungumza na waandishi wa Habari wanaotarajia kusafiri.
   Mwenyekiti wa safari ya Malawi, Ulimboka Mwakilili, akitoa ufafanuzi wakati wa kuagana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
   Mwandishi Christopher Nyenyembe, mmoja wa Waandishi wanaosafiri akifafanua jambo.
   Katibu tawala Msaidizi akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya.

  Kaimu Mkurugenzi wa Jiji Akiongea na Waandishi wa Habari wanaokwenda Safarini Malawi


   Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dk. Samwel Lazaro, akiwasikiliza waandishi wa habari walipoenda kumuaga ofisini kwake.

   baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa ofisini kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya wakimsikiliza kwa makini walipoenda kumuaga tayari kwa safari ya Malawi.
   Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dk. Samwel Lazaro akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wanaotarajia kusafiri baada ya kuagana.


  BAADHI ya  Waandishi wa habari Mkoa wa Mbeya wanaotarajia kufanya ziara ya kimafunzo nchini Malawi na Zambia wameagwa rasmi na viongozi wa Serikali.
  Waandishi hao wapatao 15 wanatarajia kuanza safari Septemba 14, Mwaka huu hivyo kabla ya kuondoka wameagana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
  Maagano hayo yamefanyika leo kwa nyakati tofauti na kupata Baraka zote kutoka kwa wawakilishi wa Ofisi hizo na kuwataka waandishi kuuwakilisha vema Mkoa wa Mbeya na Taifa kwa ujumla.
  Katibu Tawala Msaidizi, idara ya Utawala na rasilimali watu, Leonard Magacha, kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja, alisema matarajio ya Mkoa ni kupata mrejesho kutoka kwa waandishi baada ya kurudi kutoka safarini.
  Alisema hiyo ni fursa pekee ambayo waandishi wanaitumia kuvitangaza vivutio mbali mbali vilivyopo katika Mkoa wa Mbeya kwa watu wa Malawi ili waweze kutembelea pamoja na fursa zilizopo.
  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dk. Samwel Lazaro, amewataka waandishi wa habari kutumia nafasi hiyo kuitangaza timu ya Mbeya City kimataifa zaidi.
  Alisema hivi sasa Halmashauri imekuwa na mahusiano mazuri na wananchi kutokana na uwepo wa timu ya mpira wa miguu ambayo hivi sasa inajulikana nchi nzima hivyo ni fursa iliyotokea ya kuitangaza nchi za Nje ili ijulikane kimataifa zaidi.
  Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Msafara wa Waandishi wa Habari kwenda nchini Malawi, Ulimboka Mwakilili, ametoa shukrani kwa wadau mbali mbali waliowezesha safari hiyo kwa hali na mali.
  Alisema mbali na kila mwandishi kuchangia gharama za kwenda na kurudi lakini kuna wadau walioweza kuchangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya safari hiyo.
  Aliwataja baadhi ya wadau kuwa ni Mkurugenzi wa Hifadhi ya wanyama pori(Ifisi Zoo), Leirner, WYCS, Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Ofisi ya Katibu tawala Mkoa wa Mbeya, Faraja nursing na Maridadi Shop.
  Aliongeza kuwa wadau wengine wanakaribishwa kuchangia safari hiyo kutokana na umuhimu wake katika kutangaza fursa ambazo zinapatikana katika Mkoa wa Mbeya kwa wafanyabiashara na wananchi wa Nchi ya Malawi.
  Naye Mratibu wa Safari hiyo, Venance Matinya, alisema maandalizi ya safari yamekamilika kwa asilimia kubwa hivyo kinachosubiriwa ni tarehe ya kuondoka.
  Alisema waandishi wa habari wameshaajiandaa kwa mahitaji yote ya safari za nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kukata Hati za kudumu za kusafiria pamoja na cheti cha chanjo ya ugonjwa wa manjano kwa mujibu wa sheria.

  0 0

  Kiungo mshambuliaji wa Simba, Amri Kiemba (katikati),  akiwatoka  mabeki wa timu ya URA ya Uganda  katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. URA imeshinda Simba SC 1-0. Picha na Francis Dande

  0 0

  MODEL 2004
  ENGINE 2.5 DIESEL (MANUAL DRIVING)
  MILEAGE 89000 MILES
  ASKING PRICE: 35M/- Tshs
  THE VEHICLE WAS JUST IMPORTED FROM UK AND CUSTOM DUTY HAS BEEN PAID
  For more information contact;
  Thanks

  0 0

  Alpha Blondy - "Brigadier Sabari"

  0 0

  Pichani kati msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Rachael akiwa na madansa wake wakilishambulia jukwaa kwa namna ya kipekee usiku huu kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga.
  Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Ney Wa Mitego (pichani kulia) na Stamina wakilishambulia jukwaa kwa wimbo wao wa Huko Kwenu vipi,huku makele ya shangwe yakiwa yametawala kila kona ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga usiku huu.
  Sehemu ya mashabiki wa Fiesta wakishangilia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Fiesta 2014 ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini Shinyanga.
  Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,atambulikae kwa jina la kisanii Ommy Dimpo akiimba mbele ya mashabiki wimbo wake wa ani kama mama usiku huu katika tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage
  Wanajiita Wakata Mkaa kutoka kundi la Wanaume TMK,Chege na Temba kwa pamoja wakilishambulia jukwa la fiesta mbele ya umati wa watu (hawapo pichani) ndani ya tamasha la Fiesta lililofanyika usiku huu ndani ya uwanja mdodog wa Kambarage mjini Shinyanga.
  Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Khadija anaetamba na wimbo wake wa maumivu akiwa sambamba na mwanadada Rachael anaetamba na wimbo wake wa Ole temba,kwa pamoja wakilishambulia jukwaa la Fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
  Sehemu ya umati wa watu wakishangweka na na Fiesta usiku huu.
  Mmoja wa wakali wa kukamua mangona kutoka Clouds FM,Dj Zero akikamua  ngoma jukwaani mbele ya umati wa wakazi wa Shinyanga kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage
  Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Shinyanga wakiwa ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage,wakishuhudia tamasha la Fiesta 2014 likifanyika usiku huu.PICHA NA MICHUZIJR-SHINYANGA

  0 0

   Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo (kulia), akimkabidhi Mganga Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, SSP Charles Msenga mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 24.6 kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama inayotarajia kuanza hivi karibuni. Anayeshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika Dar es Salaam jana, ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani, Naibu Kamishna Mohamed Mpinga.
   Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo (kulia), akimkabidhi Mganga Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, SSP Charles Msenga (wa pili kushoto) mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 24.6 kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama inayotarajia kuanza hivi karibuni. Wanaoshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika Dar es Salaam jana, ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu  Kamishna Mohamed Mpinga (wa pili kulia) na Mjumbe wa Kamati ya Usalama Barabarani, Henry Bantu.
   Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve  Kilindo (kushoto) na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu  Kamishna Mohamed Mpinga wakionesha moja ya fulana zilizotolewa msaada na TBL kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. TBL ilikabidhi pia hundi yenye thamani ya sh. mil. 24.6 kwa ajili hiyo.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


   
  Msanii wa kizazi kipya Cassim Mganga akipiga picha na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu walipokutana kwenye jengo la Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani ulipo jijini Washington, DC. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Na Andrew Chale

  MWANAMUZIKI nyota anayefanya vizuri katika tasnia ya muziki nchini, Juma Mussa ‘Jux’ anayetamba zaidi  na vibao vya ‘Uzuri wako’ na ‘Nitasubiri’, ameachia rasmi wimbo wake mpya wa ‘Sisikii’ katika stesheni mbalimbali za redio.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam , Jux alisema wimbo huo wa ‘Sisikii’ ameutengeneza kwa Mtayarishaji  Maneke wa AM rekodi, ambao ni zawadi nyingine kwa mashabiki wake wote duniani.
  Jux aliwataka kuupokea kwa mikono miwili na wasubiri video ambayo itakuwa ya kiwango cha hali ya juu.

  “Septemba 9, nimeachia rasmi wimbo wa ‘Sisikii’ katika redio hapa nchini na wadau wangu waoupokee kwa mikono miwili kama nyimbo nyingine ninazotoa, pia wakae mkao wa kuona video ya wimbo huu muda si mrefu,”alisema Jux.

  Awali Jux amekuwa akiwonjesha mashabiki wake kwenye shoo mbalimbali zinazoendelea nchini kupitia ziara za muziki wa Serengeti Fiesta mwaka huu.

  0 0


  Benki ya CRDB, imeendelea kuimarisha ushirikiano na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika upatikanaji wa Tiketi za kieelectroniki kwa wapenzi wa soka.  

  Mfumo wa kupatikana Tiketi kwa njia ya Kielectroniki unalengo la kuongeza mapato ya TFF na hata kwa Vilabu vinavyoshiriki katika ligi inayodhaminiwa na TFF.


  Jumapili kesho, tarehe 14/9/2014, Mfumo wa kielektroniki utatumika tena kuwauzia  wapenzi wa soka tiketi kwa ajili ya kwenda kushuhudia mechi kali kati ya Yanga na AZAM, kuwania Ngao ya Hisani.Mtanange utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.


  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela amesema kuwa katika kuwapunguzia wapenzi wa soka usumbufu wa kupata tiketi wanapotaka kwenda kuangalia mechi mbalimbali za Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, Benki ya CRDB, inawawezesha wapenzi wa soka kununua tiketi kupitia Simu zao za Mkononi yaani kwa Simu Banking, ambapo mteja/ mpenzi wa soka aliyejiunga kwenye huduma ya Simbanking atabonyeza *150*03# na kisha atakamilisha process zingine na mwisho atapata namba ya tiketi yake  atakayo weza kuiprint kwenye Mashine Maalum zilizofungwa kwenye vituo 29 hapa jijini Dar es Salaam, ikiwemo kwenye ATM za matawi ya Benki ya CRDB Azikiwe, Holland, Vijana, Kariaakoo, Mbezi Luis Agency, Tegeta, Quality Center, Mbagala na Pugu.


  Pia Mpenzi wa Soka anaweza Kuprint Tiketi yake ya Kieletroniki (e-ticket) kupitia mashine maalum zilizofungwa  kwenye Offsite ATM za Benki ya CRDB kwenye maeneo yafuatayo: Kobil SabaSaba-Barabara ya Kilwa, Hospitali ya Temeke, Camel Station Tabata Junction  na Kawe


  Aidha mashabiki wa Soka wanaweza kununua tiketi ya kielektroniki kupitia huduma ya M-Pesa iliyo unganishwa na mfumo wa ATM za Benki ya CRDB. Mpenzi wa Soka anayetaka kununua Tiketi atabonyeza *150*03*02# kwenye simu yake kisha  kuendelea na hatua zinazofuata kukamilisha muamala ambapo hatimaye atapata namba ya tiketi na kwenda Kuprint kwenye Mashine Maalum zilizotajwa hapo juu.


  Kwa upande mwingine, Maofisa  wa TFF, walisema kuwa batch elektroniki tiketi zaweza PIA kupatika katika vituo vinavyo simamiwa na TFF katika  Uwanja wa Karume, Mgahawa wa Steers-Mtaa wa Ohio, Dar live-Mbagala, Buguruni sheli, Oilcom Ubungo, Sokoni Kariakoo, Breakpoint Kijitonyama/Makumbusho stand, Banana Ukonga, Namangan a Mwenge


  Mwandishi wa habari hizi ameshudia wapenzi lukuki wa soka wakinunua/wakiprint tiketi za kieletroniki kwenye mashine iliyofungwa kwenye tawi la Benki ya CRDB Azikiwe.
  Shabiki wa soka akinunua tiketi ya Kieletronic katika mashine maalum iliyofungwa katika tawi la Benki ya CRDB la Azikiwe jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Yanga na Azam FC utakaochezwa Septemba 14 kwenye Uwnja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela  akinunua tiketi ya kieletroniki kutoka katika mashine maalum iliyofungwa katika tawi la Benki ya CRDB la Azikiwe jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kwenda kushuhudia mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Yanga na Azam utakaofanyika Jumapili Septemba 14.

  0 0

   Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani mara tu alipowasili Ubalozini hapo kukutana na Taasisi mbalimbali za Kimarekani zinazo Tangaza Utalii wa Tanzania nchini Marekani kwenye Working Lunch iliyokua na maswali na majibu iliyochukua takribani saa 2 na nusu.
   Mhe. Lazaro Nyalandu akisalimiana na mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mama Lily Munanka.
  Afisa Utalii Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Immaculata Diyamett akifungua kikao
  Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwashukuru wadau wa Utalii kwa kuja kukutana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyarandu kwenye Working Lunch iliyofanyika Ijumaa Sept 12, 2014 katika jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
  Mhe. Lazaro Nyalandu akielezea machache kuhusu Tanzania na Utalii wake kabla ya kuanza kipindi cha maswali na majibu.
  Waziri wa Maliasili na Utalii. Mhe. Lazaro Nyarandu akiwa katika meza moja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula.
  Mhe. Lazaro Nyalandu akijibu moja ya maswali aliyoulizwa na wadu wa sekta ya Utalii nchini Marekani (Tour Oporator and Airlines) ambao wengi walitaka kujua usalama wa nchi, na kero wanayopata watalii kwa kutozwa ushuru kila wapitapo kwenyea mageti ambayo wamedai kero kubwa kwa Watalii na swala la Ebola wengi wakihofia usalama wao lakini Mhe. Waziri aliyajibu maswali yote kwa ufasaha na ustadi mkubwa.
  Picha ya pamoja.

older | 1 | .... | 569 | 570 | (Page 571) | 572 | 573 | .... | 3272 | newer