Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

MAKANDARASI WAZALENDO JV MBUTU WAKAMILISHA UJENZI WA DARAJA LA MBUTU IGUNGA‏ NA KUKABIDHI RASMI

0
0
Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli amekuwa akiahidi kusimamia kikamilifu ujenzi wa daraja la Mbutu,taarifa za uhakika ni kuwa daraja hilo limekamilika na kukabidhiwa rasmi leo tarehe 11 Septemba 2014.

Itakumbukwa Daraja la Mbutu limejengwa na Wakandarasi Wazarendo walioungana kwa gharama ya shilingi bilioni 12. Na huu ni mradi mkubwa wa kwanza nchini kujengwa na Makandarasi wazarendo ambapo umekamilika kwa wakati kama matakwa ya mkataba yalivyohitaji.

Huu ni muendelezo wa juhudi za wizara ya ujenzi kutaka kuwawezesha na kuwaendereza wakandarsi wazarendo.
Taswira  za makabidhiano kati ya Mkandarasi na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS)


Shamsiye Seconday School form 1 entrance examination for 2015 intake

UNAJUA ASILI YA JINA IRINGA?

0
0
Jina Iringa lilitokana na neno la Kihehe "Lilinga" ambalo tafsiri yake kwa Kiingereza ni Observation Post. Wahehe walianzisha lilinga sehemu hii ilipo Iringa ya sasa, ilikuweza kuwaona maadui kwa urahisi na kuweza kutoa taarifa za kulinda Ikulu iliyokuweko Kalenga. 
Wajerumani walijenga Boma juu ya kilima hicho hicho baada ya ushindi uliopatikana baada ya kupigana na Wahehe kwa mara ya pili. 
Katika pambano la kwanza Wajerumani chini ya Von Zelewiski waliuwawa wote akabakizwa mmoja akatoe taarifa kuwa Uheheni kuna wanaume. Vita hiyo ilipigwa eneo la Lugalo mpaka Lundamatwe Kaburi la Zelewiski liko pale Lugalo. 
Kuboma ni jina walilotumia Wahehe kupaita pale ambapo Wajerumani walijenga Boma lao. Kwa habari hii na zingine kibao ungana na mkongwe John Kitime katika libeneke lake jipya....

ngoma azipendazo ankal - Kindly sponsored by Isumba lounge

0
0
Bob Marley - "Coming In From The Cold"

WAZIRI CHIKAWE ATUA KIGOMA, AKUTANA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu, Issa Machibya (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe katika ofisi za Mkoa huo zilizopo mjini Kigoma wakati Waziri Chikawe na maafisa wake walipofanya ziara ya kikazi katika mkoa huo. Waziri Chikawe alikutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ya usalama katika wilaya zote za mkoa huo. Waziri Chikawe katika ziara yake hiyo, pia anatarajiwa kutembelea Kambi za Wakimbizi zilizopo mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu, Issa Machibya akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama katika Ukumbi wa Ofisi yake. Kushoto kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe ambaye pia alishiriki katika kikao hicho kilichokuwa kinajadili masuala mbalimbali ya usalama mkoani Kigoma. Waziri Chikawe na maafisa wake waliwasili mkoani hum leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Waziri Chikawe licha ya kukutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo pia anatarajiwa kutembelea Kambi za Wakimbizi zilizopo mkoani humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika kikao kilichoitishwa kwa ajili yake, na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu, Issa Machibya. Katika kikao hicho kilichofayika katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi za Mkoa wa Kigoma, Waziri na Kamati hiyo walijadiliana masuala mbalimbali ya Ulinzi na Usalama. Waziri Chikawe na maafisa wake waliwasili mkoani humo leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Waziri Chikawe licha ya kukutana na Kamati hiyo ya mkoa, pia anatarajiwa kutembelea Kambi za Wakimbizi zilizopo mkoani humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kigoma. Watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu, Issa Machibya. Waziri Chikawe pamoja na kamati hiyo walifanya kikao kilichofayika katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi za Mkoa wa Kigoma, wakijadiliana masuala mbalimbali ya Ulinzi na Usalama ndani ya mkoa huo. Waziri Chikawe na maafisa wake waliwasili mkoani humo leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Waziri Chikawe licha ya kukutana na Kamati hiyo, pia anatarajiwa kutembelea Kambi za Wakimbizi zilizopo mkoani humo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

AGIZO RASMI KWA VYAMA VYA SIASA KUTOKA KWA WATANZANIA

TOVUTI MPYA YA HABARI ZA KIELIMU TANZANIA YAANZISHWA

TANZANITE YAZIDI KUNG'ARA KWENYE MAONYESHO YA VITO NCHINI BANGKOK

0
0
Makamu wa Rais wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito – Thailand, ambao ndiyo waandaaji wa Maonesho ya Vito ya Bangkok, Tony Brooks akizungumza na baadhi ya Watanzania wanaoshiriki katika Maonesho hayo nchini Thailand alipotembelea Banda la Tanzania.
Mkuu wa Banda la Tanzania katika Maonesho ya Vito ya Bangkok ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo akimweleza mdau wa madini ya vito aliyetembelea banda hilo kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania. Mbele yao ni vinyago vilivyochongwa kutokana na miamba.
Mfanyabiashara wa madini ya vito kutoka Tanzania, Peter Pereira akimhudumia Mteja aliyefika katika Banda la Tanzania kwenye Maonesho ya Vito ya Bangkok. Maonesho hayo ya siku tano yalianza Septemba 9 mwaka huu.
Mfanyabiashara wa madini ya vito kutoka Tanzania, Latifah Abdallah akitoa maelezo kuhusu madini hayo kwa wadau waliotembelea Banda la Tanzania katika Maonesho ya Vito ya Bangkok.
Mchimbaji mdogo wa madini ya vito, Kassim Idi Pazi akihudumia wateja waliotembelea Banda la Tanzania katika Maonesho ya Vito ya Bangkok.
Baadhi ya Washiriki kutoka Tanzania katika Maonesho ya Vito ya Bangkok wakipozi kwa picha muda mfupi kabla ya kuanza kwa siku ya tatu ya maonesho hayo. Kutoka Kushoto ni Asimwe Kafrika, Iddi Pazzi, Gregory Kibusi, Nelson Magawa, Teddy Goliama na Matiko Sanawa.

IGP MANGU AFUNGUA JENGO LA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO MKOA WA KILIMANJARO

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali wa Polisi ,Ernest Mangu akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la dawati la Jinsia katka kituo kikuu cha Polisi mjini Moshi.
Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Koka Moita akizungumza kabla ya kumkaribisha ,IGP ,Mangu kuzindua dawati la jinsia.
Mkuu wa Dawati la Jinsia mkoa wa Kilimanjaro,Grace Lyimo akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo hilo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WATANZANIA WATAKIWA KUTODANGANYWA KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA

0
0
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vyama vya Siasa vinavyounda TCD, Mhe. John Cheyo.

Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.

MJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCD Mhe. John Cheyo amewataka Watanzania kutodanganywa kuhusiana na mchakato mzima wa kusaka Katiba Mpya.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mhe. Cheyo wakati alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha asubuhi cha Jambo kinachorushwa na Televisheni ya Shirika la Habari Tanzania (TBC).

Mhe. Cheyo amesema kuwa ni vema viongozi kuacha kusema uongo na kuwa waungwana katika mchakato wa kutafuta Katiba Mpya kwani si vema kuitakia Tanzania mabaya bali ni kutaka mchakato huo wa Katiba uendelee kwa amani.

Ameongeza kuwa Taifa la Tanzania linahitaji kuwa Taifa lenye nguvu kwani amani haiwezu kuwekewa thamani kwa vurugu, hivyo ametaka amani iliyopo nchini ilindwe na kuepuka kudanganywa na baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema na nchi.

Mhe. Cheyo ameshangazwa kwa kitendo cha viongozi wa UKAWA kutoweka ajenda ya kurudi ndani ya Bunge hilo wala kuzungumzia kuhusu suala hilo la kurudi ndani, bali wamekuwa wakitaka wajumbe wengine walioko ndani watoke kwa kusema kuwa bunge hilo sio halali.

“Nawashangaa UKAWA kwa kutoweka ajenda ya kurudi ndani ya Bunge hili Maalum la Katiba na badala yake wao wanaweka ajenda ya kutoka ndani ya bunge hili tena kwa nguvu”, alisema Mhe. Cheyo.

Aidha, Mhe. Cheyo amewataka vijana nchini wawe na mshikamano na kuepuka kudanganywa na viongozi kwa kuambiwa mambo yenye uwongo huku akisisitiza kuwa Rais aliyeko sasa hivi ana nia njema ya kuipatia nchi Katiba iliyo bora na yenye kumfaa kila Mtanzania.

“Vijana achene kuvunjika miguu yenu bure, achene kukimbia kimbia barabarani huku mkilishwa maneno yenye uongo kuhusiana na mchakato huu wa Katiba, vunjikeni miguu kwa kufanya kazi kwa bidiii na sio kusikiliza uwongo”, alisema Mhe. Cheyo.

Akizungumzia kuhusu TCD, Mhe. Cheyo amefafanua kuwa TCD ni Jukwaa la majadiliano kwa ajili ya maridhiano na mapatano pale panapokuwa na tofauti kati ya vyama vya siasa.

“TCD ni Jukwaa kwa ajili ya kufanya majadiliano na si vinginevyo, hii ni meza ya maridhiano na nawaambia kuwa huko mnapokwenda ni kuchepuka, rudini ndani kwenye njia kuu”, alisisitiza Mhe. Cheyo.

Naye mjumbe wa Kamati namba Sita ya Bunge Malaam la Katiba Mhe. Steven Wasira amewaasa Watanzania kwa kusema kuwa, watu wanaosema kuwa Bunge limenyofoa baadhi ya mambo muhimu yanayohusu wananchi ni waongo na wenye nia ya kupotosha Umma wa Tanzania.

“Kuna watu wanasema kuwa Bunge Maalum la Katiba limenyofoa baadhi ya mambo muhimu yanayohusu wananchi huo ni uwongo, ni mambo gani hayo yaliyonyofolewa? kwasababu kuna mambo mengi yameongezwa na kuboreshwa katika mapendekezo kwa ajili ya makundi mbalimbali ndani ya hiyo Rasimu”, alisema Mhe. Wasira.

Mhe. Wasira ameongeza kuwa katika Bunge hilo kuna Ibara ya Rasimu ya Katiba na sio ibara za CCM, amewataka Watanzania nchini wafanya uchunguzi na kusikiliza kwa kuchambua ili kupata ukweli wa hayo.

“Sisi tuko tayari kuvaana na viopngozi wowote kwani tunataka Watanzania wote waamini shughuli zifanywazo ndani ya bunge hili na waepuke kudanganywa”, alisema Mhe. Wasira.

MESSAGE ON THE UNITED NATIONS DAY OF SOUTH-SOUTH COOPERATION

0
0
This year’s United Nations Day for South-South Cooperation comes as the international community is transitioning to a post-2015 development agenda centred on shared prosperity and environmental sustainability.

Despite remarkable advances in achieving the Millennium Development Goals, progress across the South has been uneven. Extreme poverty, rampant inequality, malnutrition and vulnerability to climate and weather-related shocks persist.

According to the UN Multidimensional Poverty Index, 2.2 billion people still live in abject  poverty. About 1.4 billion people, the majority in the South, still have no reliable electricity, 900 million lack access to clean water and 2.6 billion do not have adequate sanitation.

In the face of this stark reality, South-South and triangular cooperation offer a path to balancing growth and equity in the context of a new Global Partnership for Sustainable Development.

I encourage countries of the South and all development partners to come together to share, disseminate and scale up successful development solutions and technologies.  This November’s Global South-South Development Expo in Washington, D.C. will provide one such important platform.

On this United Nations Day for South-South Cooperation, let us reaffirm our commitment to pioneering South-South approaches that will ensure shared prosperity, sustainable development and a life of dignity for all. 

WASHINDI TUZO ZA HABARI TANAPA WATEMBELEA MAENEO YA KIHISTORIA AFRIKA KUSINI

0
0
Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 kutoka kushoto David Rwenyagira (Radio Five), Vedasto Msungu (ITV), Mtanzania Peter Masika wa Johannesburg na Gerald Kitabu (The Guardian) wakiwa nje ya nyumba ya Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MH. KOMBANI KUFUNGUA MICHEZO YA SHIMIWI YA MWAKA 2014

MABONDIA WA TANZANIA ,SAIDI YAZIDU NA ALIBABA RAMADHAN KUKIPIGA JIONI YA LEO NA MU-ALJERIA NA M-MALAWI KATIKA UKUMBI WA YMCA -MOSHI

0
0
Bondia toka Aljeria,Djamel Dahou akionesha mikanda anayoshikilia,muda mchache kabla ya kupima uzito .
Bondia Said Yazidu wa Tanzania (aliyenyanyua mikono) na kulia kwake ni bondia Alibaba Ramadhan wakiajiandaa na zoezi la upimaji uzito.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Sitta awapa somo Viongozi wanaojiita UKAWA

0
0
Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.

MWENYEKITI wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta amewaadaa baadhi ya viongozi wanaojiita UKAWA kwa taarifa yao ya kutaka kumfikisha Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa kwa kuendeleza mchakato huo wa Katiba.

Kauli hiyo imetolewa leo 12 Septemba, 2014 mjini Dodoma na Mhe. Sitta kufuatia baadhi ya viongozi hao, kudai kuwa watampeleka katika mahakama hiyo.

Mhe. Sitta ameeleza kuwa baadhi ya viongozi wa kundi hilo kuwa wanakipaji kikubwa cha uigizaji huku akifafanua kuwa wakati walipokuwa Bungeni wakati wa mchakato wa kupiga kura za siri, viongozi wa kundi hilo walizifanya kura hizo kuwa wazi na baadaye kuja na kauli kuwa Bunge Maalum la Katiba linaloendelea sasa sio halali lihairishwe.

“Juzi Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana nao mara mbili kwa muda wa saa Saba na katika kukutana huko wakafikia maafikiano, lakini siku moja baadaye wao wamekana yote waliyokubaliana hapa mjini Dodoma, kwa hiyo ni vyema wananchi wakawapima hawa watu”, alisema Mhe. Sitta.

Aidha, Mhe. Sitta aliasa kwa kusema kuwa wananchi na viongozi wanatakiwa kujua kuwa mchakato wa bunge Maalum la Katiba sio jambo la mzaha na wao hawapo hapo bungeni kwa mzaha mzaha.

“Mimi nawaambia kuwa hapo mwakani watakaposhindwa uchaguzi basi warejee katika fani zao ambazo Mwenyezi Mungu kawajalia”, alisema Mhe. Sitta.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UONGOZI WA NEC-JAPAN IKULU JIJINI DAR LEO

0
0
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo amekutana na Uongozi wa Kampuni ya NEC yenye makao yake makuu jijini Tokyo nchini Japan. Ujumbe wa NEC-Japan umeongozwa na Rais wa Kampuni hiyo inayojishughulisha na masuala ya Mawasiliano na Teknolojia, Dkt. Nobuhiro Endo.

Ujio wa Kampuni hii nchini Tanzania unatokana na mwaliko wa Tanzania kwa makampuni ya Japan kufuatia ziara ya kikazi aliyoifanya Mheshimiwa Makamu wa Rais nchini Japan, mwezi wa Mei mwaka huu. Mheshimiwa Makamu wa Rais alitembelea Makao Makuu ya Kampuni hiyo wakati za ziara hiyo.

Katika mazungumzo na uongozi wa NEC Mheshimiwa Makamu wa Rais aliwaeleza wageni wake nia ya Tanzania kuona inatanua mawasiliano na teknolojia nchini ili kuinua uchumi na akafafanua kuwa teknolojia yoyote kutoka NEC inakaribishwa hapa nchini ili kusaidia Tanzania kupiga hatua. 

Uongozi wa NEC nao ulimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa, NEC inaushirikiano wa karibu na Shirika la Simu Tanzania (TTCL) na kwamba wanatarajia kukutana na uongozi wa wizara ya Mambo ya Ndani kwa lengo la kutazama fursa za kusaidia teknolojia katika ulinzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Rais wa Shirika la NEC Corporation la Japan, Dkt. Nobuhiro Endo, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 12, 2014 akiwa ameongozana na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Uongozi wa Shirika la NEC Corporation la Japan, wakiongozwa na Rais wao Dkt. Nobuhiro Endo, wakati walipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 12, 2014 kwa ajili ya mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwakatika picha ya pamoja na Rais wa Shirika la NEC Corporation la Japan, Dkt. Nobuhiro Endo (kushoto) na Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Masaki Okada, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Septemba 12, 2014. Picha na OMR.

Mashindano ya Safari Pool Taifa yafunguliwa rasmi mjini Moshi,Kilimanjaro leo

0
0
Katiba Tawala wa Wilaya ya Moshi mjini,Remida Ibrahim(wa pili kulia) akicheza kuashilia uzinduzi wa fainali za mashindano ya Pool Taifa yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014” yanayofanyika katika Ukumbi wa Kuringe Mkoani Kilimanjaro.Kutoka kushoto ni Katibu wa chama cha Pool Taifa(TAPA), Amos Kafwinga,Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Makamu Mwenyekiti wa TAPA, Fred Mushi.
Baadhi ya Wachezaji wa Pool wakiwa na zawadi mbalimbali wakielekea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi kutoa kwa wagonjwa ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii kile wanachofadhiliwa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakati wa ufungunguzi wa mashindano ya Pool Kitaifa yanayofanyika Mkoani humo yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014”.
Baadhi ya wachezaji wa Pool wakitoa zawadi za vitu mbalimbali kwa wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii kile wanachofadhiliwa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakati wa ufungunguzi wa mashindano ya Pool Kitaifa yanayofanyika Mkoani humo yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014”.

Rais Kikwete aagana na Balozi wa Ufaransa,amuaga pia Jaji wa Mahakama ya Afrika

0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na balozi wa Ufaransa aliyemaliza muda wake nchini Mhe.Marcel Escure wakati balozi huyo alipokwenda kumuaga ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na balozi wa Ufaransa aliyemaliza muda wake nchini Mhe.Marcel Escure wakati balozi huyo alipokwenda kumuaga ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na balozi wa Ufaransa aliyemaliza muda wake nchini Mhe.Marcel Escure wakati balozi huyo alipokwenda kumuaga ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza ikulu jijini Dar es Salaam na Jaji Sophia Akkufo Rais wa Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika(AFHPR) aliyemaliza muda wake(picha na Freddy Maro).

Mkutano wa 24 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wamalizika leo jijini Arusha

0
0
Mgeni Rasmi katika ufungaji wa Mkutano wa 24 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mh. Jowika Kasunga akitoa hotuba yake ya kufunga Mkutano huo uliomalizima leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.Picha zote na Othman Michuzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF,Alhaj Ramadhan Khijja azungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga Mkutano wa 24 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa PPF,uliomalizika leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio akitoa hotuba fupi wakati wa kufunga Mkutano wa 24 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa PPF,uliomalizika leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
 Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Midland cha Mbabane,Swaziland,Dkt. Michael Angelo Mlauzi,akiwasilisha mada yake kwenye Mkutano wa 24 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa PPF,uliomalizika leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.

Muwakilishi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Prof. Bakari Lemberiti akiwasilisha Mada iliyohusu umuhimu wa tiba ya Kinywa na Meno katika Mkutano wa 24 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa PPF,uliomalizika leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.

NEWS ALERT: Moto wazuka tena katika Msikiti wa Mtambani leo

0
0
Msikiti  wa  Mtambani uliopo Kinondoni jijini Dar es Saam uliungua kwa mara ya pili leo.  Msikiti huo ambao uliungua  mnamo Agosti 13, 2014 katika ghorofa yake ya juu na kuteketeza  eneo kubwa ambalo hadi sasa bado halijanza kufanyiwa  ukarabati.
Leo hii moto ambao inasemekana ulianza mmajira ya saa sita na nusu mchana   katika moja ya chumba ambacho wanafunzi wa kidato cha nne  wa kike wamekuwa wakipiga kambi ya kujisomea ikiwa ni katika maandalizi ya kukabiliana na mtihani wao wa taifa  utakaofanyika  baadaye mwaka huu.
 Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kanda ya Kinondoni Camilius Wambura  amethibitisha jambo hilo na kusema kuwa hadi wanafika eneo la tukio chanzo bado hakijafahamika, na kwamba chumba ambacho moto ulianzia ni cha wasichana ambamo  magodoro manne yameungua.
“Katika janga la moto uliounguza madarasa  mwezi uliopita Jeshi la Polisi iliunda  timu ambayo ilikuwa ikichunguza chanzo cha moto huo hivyo na sasa timu hiyohiyo itaendele na uchunguzi wake kwa kuunganisha matukio haya mawili” alisema Wambura.
Wakizungumza bila ya kutaja majina yao kina mama wa msikitini hapo wao walisema  kwamba “ sisi tulikuwa msikitini tunasoma qurani wakati tukivuta muda wa sala ya Ijumaa ndipo tuikasikia sauti za moto moto na kuona upande wa wanaume wakikimbia huku na kule kwa taharuki hivyo chanzo hasa cha moto sisi hatukijui.
Waumini wa msikiti huo walifanikiwa kuuzima moto huo na kusali swala ya Ijumaa kama kawaida. 













Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images