Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 560 | 561 | (Page 562) | 563 | 564 | .... | 3283 | newer

  0 0  Shiriko lisilo la Kiserikali la Farm Africa kwa kushirikiana na wakulima wa uyoga wa wilaya za Mbulu na Babati wiki iliyopita waliandaa siku maalum ya kula uyoga kwa wakazi wa wilaya hizo.

  Tukio hilo lilifanyika katika katika kitongoji cha Magugu wilayani Babati ambapo wakazi walipata nafasi ya kuonja aina mbalimbali za mapishi ya uyoga.Wakulima 15 wa uyoga walio katika mradi wa Misitu wa Farm Africa walishiriki shughuli hiyo kwa kupika na kugawa  bure uyoga uliopikwa kwa wakazi wa eneo hilo.

  Kilimo cha uyoga ni njia mbadala iliyopo kwenye mradi wa misitu ambapo wakulima badala ya kukata miti kwa ajili ya kuitumia kwa kuwapatia kipato, wanapanda uyoga ambao wanauuza na kuwaingizia kipato.
  Siku ya kuonja uyoga ilikuwa na madhumuni ya kuwahamasisha wakazi wa Babati kuhusu faida za kilimo cha uyoga, mapishi yake na jinsi kilimo hicho kinavyoweza kuwaingizia kipato cha ziada.
   Ni wakati wa kula uyoga!
   Wadau wakipatiwa mafunzo ya kilimo cha uyoga na wakulima walio kwenye mradi wa misitu wa Farm Africa
   Wakulima wakionyesha jinsi uyoga unavyooteshwa
   Wananchi wakiburudika na rosti ya uyoga
  Wananchi wakipakuliwa rosti ya uyoga.

  0 0

  Tunduru District Commissioner Mr. Chande Bakari Nalicho officially launching a partnership to implement Participatory Forest Management - PFM among Tunduru District Council, World Wide Fund for Nature (WWF) Tanzania, Mpingo Conservation Development Initiative (MCDI)and Mtandao wa Jamii wa Usimamizi Misitu Tanzania (MJUMITA) in Tunduru on the 3rd September 2014.
  Members from the Tunduru District Council participating in the launching event to implement Participatory Forest Management - PFM among Tunduru District Council, World Wide Fund for Nature (WWF) Tanzania, Mpingo Conservation Development Initiative (MCDI)and Mtandao wa Jamii wa Usimamizi Misitu Tanzania (MJUMITA) in Tunduru on the 3rd September 2014.
  World Wide Fund for Nature (WWF) Tanzania, Forest Program Coordinator , Mr. Isaac Malugu making a presentation during the launch of Participatory Forest Management - PFM among Tunduru District Council, World Wide Fund for Nature (WWF) Tanzania, Mpingo Conservation Development Initiative (MCDI)and Mtandao wa Jamii wa Usimamizi Misitu Tanzania (MJUMITA) in Tunduru on the 3rd September 2014.
  Tunduru District Commissioner Mr. Chande Bakari Nalicho, other District leaders and Partnership officials in a group photo during the launch of Participatory Forest Management - PFM among Tunduru District Council, World Wide Fund for Nature (WWF) Tanzania, Mpingo Conservation Development Initiative (MCDI)and Mtandao wa Jamii wa Usimamizi Misitu Tanzania (MJUMITA) in Tunduru on the 3rd September 2014.

  0 0

  MKURUGENZI mtendaji wa Azania benki,Charles Singili amewataka wananchi kuwa na mazoea ya kujiwekea akiba kwa manufaa ya baadae.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa akauni mpya ya benki hiyo iitwayo Dhamira, Singili amesema kuwa utaratibu wa kujiwekea akiba utapunguza tatizo la umasikini kwa wananchi.

  Aliongezea kuwa, endapo wananchi wakipatiwa elimu kuhisu faida za kutunza fedha zao,itasaidia kupunguza hali ya umasikini uliopo sasa.

  "Kwa kutambua matatizo yanayoikabili nchi yetu, Azania bank imeamua kufungua akaunti ambayo itamwezesha mwananchi kutunza fedha bila makato ya aina yeyote" alisema Singili.

  Singili aliongezea kuwa, akaunti ya Dhamira, itamsaidia mwananchi yeyote kutunza fedha kuanzia Sh. 50,000 na atapatiwa riba ya asilimia 8 kila mwenzi.

  Aliongezea kuwa, akaunti hiyo inatafunguliwa na mtu ambae ametimiza miaka 18 na kuendelea na itamsaidia kuweka riba kadri awezavyo.

  "Dhamira akaunti itamsaidia mwananchi kutimiza malengo au ndoto zao, pia kipindi cha chini kuweka akiba ni miezi 12," alisema.
  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Azania,Charles Singili akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa akauni mpya ya benki hiyo iitwayo Dhamira (Dhamira Account) uliofanyika leo kwenye Makao Makuu ya Benki hiyo,Ubungo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria kwenye uzinduzi huo wakimsikilizwa kwa makini Mkurugeni Mkuu wa Benki ya Azania,Charles Singili.
  Mkurugeni Mkuu wa Benki ya Azania,Charles Singili akimuelekeza namna ya kujaza fomu,Bi. Naomi Mapunda ambaye alikuwa mteja wa kwanza kufungua akauni hiyo ya Dhamira.
  Baadhi ya Maofisa wa Benki ya Azania.

  0 0
 • 09/04/14--08:04: Gari liko sokoni
 • Gari aina ya Toyota Rav4,liko sokoni kwa gharama nafuu kabisa au waweza sema ni karibu na bure.Gari iko kwenye hali nzuri sana. Gia ni automatic, mafuta inayotumia ni petrol, imetembea 128,000 km. 

  kwa atakayeihitaji,asasiliwane na ndugu kwenye Mawasiliano haya 
  0683 206230
  Linavyoonekana kwa nyuma na ubavu wa kushoto.
  ndani.
  Mbele.

  0 0


  0 0

  Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) amekutana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Covvin ya Ubelgiji Bwana Raymond Douniaux (kulia). Balozi Kamala amemuomba Mhe Meya huyo kutangaza Utalii wa Tanzania na amemkabidhi vifaa ya kutangaza utalii wa Tanzania.

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Pudenciana Kisaka akizungumza
   
  Na Denis Mlowe,Iringa

  JUMLA ya sh. bilioni 1.3 zimetumika katika ujenzi wa maabara za sayansi, hosteli za wasichana na chumba cha darasa katika shule za sekondari za Ismani, Nyang’ro na Kalenga zilizoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa mkoani Iringa.
   
  Akizungumza na wahabari hivi karibuni ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Iringa,Pudenciana Kisaka  alisema kuwa halmashauri kupitia idara ya elimu Sekondari imekamilisha maabara tatu za masomo ya sayansi , chumba cha darasa na hostel katika shule hizo zilizokuwa zina upungufu wa majengo hayo.
   
  Alisema kuwa maabara moja imejengwa katika shule ya sekondari Ismani na ujenzi wake kukamilika  kwa asilimia 100 na inatumika kwa masomo ya Bailojia na imegharimu zaidi ya shilingi milioni 89.
   
  Kisaka alisema shule ya sekondari Kalenga imejengewa maabara mbili ambazo zimekamilika kujengwa na zinatumika kwa masomo ya Fizikia na Kemia na kugharimu shilingi milioni 29.
   
  Aidha alisema halmashauri hiyo imejenga hostel ya wasichana wa shule ya sekondari Kalenga ambao umegharimu sh. Milioni 258 mpaka kukamilika na ujenzi wa chumba kimoja cha darasa shule ya sekondari Nyang’oro  uliogharimu sh. Milioni 13.


  Kisaka akizungumzia kuhusu mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha tano alisema idara ya elimu imepangiwa jumla ya wanafunzi 2389 wa kidato cha tano katika shule sita hivyo idadi imeongezeka kutoka 1433 mpaka 2389 sawa na asilimi 156 ukilinganisha na idadi ya wanafunzi waliopokelewa kwa mwaka 2013/2014 walikuwa 1433 sawa na asilimia 93.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya Mayamaya –Mela - Bonga Km 188.15. Wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi wa Serikali ya Japan kushoto, katikati ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa upande wa Tanzania Dkt. Tonia Kandiero, Mama Salama Kikwete pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. inayojengwa kwa kiwango cha Lami. Wengine walioshika utepe ni Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania Dkt. Tonia Kandiero, Mama Salama Kikwete, Mbunge wa Viti maalum kutoka Chama cha Wananchi CUF, Mbunge wa Simanjiro Cristopher Ole Sendeka, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi na viongozi wengine wa Kitaifa.
  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli watano kutoka kulia akicheza ngoma na kikundi cha ngoma za asili cha Bicha kabla ya uzinduzi rasmi wa barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. inayojengwa kwa kiwango cha lami.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, Mama Salama Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania Dkt. Tonia Kandiero.
  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akizungumza na Mzee maarufu wa Wilaya ya Kondoa Balozi mstaafu Mustapha Nyang’anyi kabla ya uzinduzi wa Barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge.
  Katapila likisafisha sehemu ya Barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15 inayojengwa kwa kiwango cha lami.
  Taswira: ‘Mkeka mpya’ Barabara ya Bicha- Kondoa mjini inavyoonekana mara baada ya kukamilika kwake.
  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania Dkt. Tonia Kandiero muda mfupi kabla ya uzinduzi wa Barabara ya Mayamaya –Mela-Bonga Km 188.15. Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.

  0 0  0 0

  By Special Correspondent

  Tanzanian engineers have been lauded as the engine of success in the effective implementation of the government led projects including the Big Results Now (BRN) Programme.

  The call was issued on Thursday by the Deputy Chief Executive Officer of the President’s Delivery Bureau (PDB), Mr. Peniel Lyimo when giving a keynote address on the Engineers Annual Conference in Dar es Salaam. The meeting theme was on the Role of Engineers in the implementation of the BRN.

  “We can have doctors to heal our wounds; lawyers to ensure protection of our transactions or religious leaders to pacify our minds and souls; but the engineers’ physical beautification and safety of our real world is equally important,” said Mr. Lyimo.

  He emphasized that the BRN Programme which has already attained significant achievements within a year of its establishment cannot maximize more in the future if the private sector and different professionals like engineers will not play their greater part.

  “All the projects under the BRN Programme require professional inputs of engineers from the design to execution stage, therefore, the role of engineers is crucial,” he added.

  But Mr. Lyimo raised the issue of ethics in project implementation emphasizing that the BRN is a smart undertaking where all the people involved have to ensure they work ethically and with a business unusual mind-set.

  “If you fully exercise your profession, knowledge and ethics you can make a significant impact on the delivery of the BRN Programme by reducing the cost of projects and the execution periods.

  “We know that project costs can be high where there are flaws in design, supervision of works and absence of enforcement of professional ethics. All these variables are within the control of the Engineers Registration Board which is expected to play its proper role.”

  The BRN Programme was incepted in July, 2013 and is overseen by PDB which is an independent department established under the office of the President of the United Republic of Tanzania.

  The BRN has started with six initial sectors of energy, water, education, transport, agriculture and resource mobilization. The BRN approach involves priority setting, target setting and close monitoring and problem solving for timely project execution.

  0 0

  By Mr. G.Tengeneza (TANZANIA TOURIST BOARD)

  The Swahili International. Tourism Expo (S!TE) preparatory committee has held its first meeting at the Tanzania Tourist Board headquarters in which the roles of sub-committees and stakeholders were established and discussed.

  The meeting was attended by delegates from different institutions considered to stakeholders that have significant roles to play in making the event a success.

  The committee members attended the meeting were from. Regional Commissioner Office, Tanzania Revenue Authority, Immigration department, Police, Tourism Confederation of Tanzania (TCT), Hotel Keepers Association of Tanzania , Kinondoni Municipal, Dar es Salaam City Council and the host the Tanzania Tourist Board.

  The expo which is coordinated by the Tanzania Tourist Board in collaboration with Pure Grit project and Exhibition Management Company from South Africa is scheduled to take place at Mlimani City in Dar es Salaam from 1st to 4th October this year and is expected to draw a good number of exhibitors from all over the world.

  The SITE will definitely be a unique platform for Tanzania tourism stakeholders to market a country as a tourism destination as well as promoting their products and services international.
  The Acting Managing Director of Tanzania Tourist Board (TTB), Devota Mdachi opening the 1st National S!TE Committee Meeting which held at TTB Headquarter.
  The TTB's Tourism and Service Manager, Mr. Phillip Chitaunga as a Coordinator of SITE Tanzania elaborating some issues to the members during the of S!TE committee meeting. — at TTB's board room.
  Among the other tourism stakeholder, Lathifa k. Sykes, the CEO of the Hotel Keepers Association (HAT) contributing some ideas during the meeting.
  The Chairperson, Devota Mdach and the Cordinator of S!TE, Phillip Chitaunga listening to Rosemary Mukulas from Kinondoni Municipal.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava akiwasilisha hotuba yake katika Kongamano la 12 la Uwekezaji katika sekta ya Madini linalofanyika kila mwaka katika mji wa Perth nchini Australia. Mwaka huu linafanyika tarehe 3-5, 2014 mjini hapo.
  Baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wanaoshiriki kwenye Kongamano la 12 la Uwekezaji katika sekta ya Madini linalofanyika kila mwaka katika mji wa Perth nchini Australia. Mwaka huu linafanyika tarehe 3-5, 2014 mjini hapo na linakwenda sambamba na maonesho ya makampuni na taasisi mbalimbali zilizowekeza katika sekta ya madini Barani Afrika. 
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini Eng. Ngosi Mwihava (wa saba kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara na Taasisi zilizochini ya Wizara hiyo zinazoshiriki katika Kongamano la 12 la Uwekezaji katika sekta ya Madini linalofanyika kila mwaka katika mji wa Perth nchini Australia. Mwaka huu linafanyika tarehe 3-5, 2014 mjini hapo na linakwenda sambamba na maonesho ya makampuni na taasisi mbalimbali zilizowekeza katika sekta ya madini Barani Afrika. PICHA NA KOLETA NJELEKELA, PERTH AUSTRALIA

  0 0

  Na Mwene Said wa Blog ya Jamii

  NAIBU Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, leo amewasilisha pingamizi la awali dhidi ya kesi ya kuhoji mamlaka ya  Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma iliyofunguliwa na  Mwandishi wa Habari Said Kubenea dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kwamba maombi hayo ni batili kisheria na hayawezi kuthibitishwa mahakamani, hivyo yatupiliwe mbali.

  Masaju amewasilisha pingamizi hilo akitoa sababu nne, akiitaka mahakama kutupilia mbali maombi yaliyopo mbele ya jopo la majaji watatu, wakiongozwa na Mwenyekiti Jaji Augustino Mwarija, Dr. Fauz Twaib na Aloyisius Mujuluzi katika Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.

  Katika pingamizi hilo lililoambatana na hati ya kiapo, AG kupitia naibu wake, amedai kuwa maombi hayo ya mlalamikaji yana dosari ambayo haiwezi kurekebishika kwa kuwa zinahitaji kifungu maalum cha sheria kinachoipa nguvu mahakama ya kuridhia maombi hayo.

  Sababu nyingine, AG anadai kuwa maombi hayo yaliyopo mahakamani hayawezi kuthibitishwa na kwamba hayana mashiko ya kisheria.

  Pia, Masaju amedai kuwa maombi yaliyopo mahakamani ni batili kisheria hivyo mahakama iyatupilie mbali.

  Jaji Mwarija alisema kesi hiyo itasikilizwa kesho mahakamani hapo.

  Katika kesi ya msingi, kesi  hiyo namba 28 ya mwaka 2014, Kubenea anaiomba mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya Mamlaka ya Bunge la Katiba chini ya  vifungu vya 25 (1) na 25 (2) vya Sheria ya Marekebisho ya Katiba namba Namba 83 ya mwaka  2011 imepangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Augustino Mwarija, Dr. Fauz Twaib na Aloyisius Mujuluzi.

  Pamoja na mambo mengine katika kesi hiyo ya kuomba tafsiri ya mamlaka ya Bunge  hilo, pia Kubenea amewasilisha maombi mahakamani hapo akiiomba mahakama itoe zuio la muda la kusimamisha Bunge hilo ili kusubiri uamuzi wa maombi ya tafsiri hiyo.

  Maombi hayo ya kusimamisha Bunge hilo kwa muda yaliyopewa usajili wa namba 29 ya mwaka 2014, pamoja na maombi ya msingi ya tafsiri ya mamlaka ya Bunge yote yalifunguliwa mahakamani hapo leo chini ya Hati ya Dharura.

  Katika kesi hiyo ya msingi anaiomba Mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya masharti ya vifungu hivyo vya sheria hiyo na pia itamke kama Bunge hilo lina mamlaka ya kubadilisha maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwa kiwango gani.

  Kwa mujibu wa hati ya madai, Kubenea anadai kuwa msingi wa kesi hiyo unatokana na uamuzi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Desemba Mosi, 2011, lililopitisha  Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Anasema sheria hiyo ilikuwa na lengo la kuratibu mchakato wa kutungwa kwa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  0 0

  Makabidhiano ya bati yaliyofanyika nje zinapojengwa ofisi za chama cha mpira  Mkoa wa Njombe ( Njolefa) kutoka kushoto ni  Mkurugenzi wa shirika la Tanwat Rajeev Singh, Edymund  Munubi afisa tawala wa Tanwat, Katibu wa Chama cha Mpira Mkoa wa Njombe  Steven Njowoka na wa Mwisho ni Afisa Utamaduni na michezo Mkoa wa Njombe Steven Sanga. Picha na James Festo.
   
   ======== ==========  ========
  Na James Festo, Njombe.

  CHAMA  chama cha mpira  Mkoa wa Njombe kimepokea mchango  wa bati, saruji na mbao wenye thamani ya zaidi ya  shilingi milioni  moja kutoka kwa wadau wa michezo zitakazazosaidia kuendelea kujenga ofisi zao ngazi za mkoa.

  Akiongea katika makabidhiano katibu wa chama hicho  Steven Njowoka alisema kuwa wamepokea   michango kutoka kwa wadau  ambapo hapo juzi walifanikiwa kupokea bati 53, Mifuko ya saruji  kumi na mbao  77 vyote vyenye thamani ya shilingi milioni  1,295,000/= na kufanya jumla ya michango kutoka kwa wadau wa michezo kufikia shilingi  milioni  1,891,000/=.

  Njowoka aliendelea kuwaomba wadau mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Njombe kuendelea kuchangia mchango utakaokifanya chama hicho mkoa wa Njombe kukamiliisha ujenzi wa ofisi zenye vyumba saba vilivyofikia hatua ya kupauliwa  kwani hivi sasa wanafanya kazi katika jengo ambalo wamepangishwa.

  "sisi kama chama cha mpira bado tunahitaji kusaidiwa ...lengo letu ni kuwa hosteri yenye uwezo wa kulaza wachezaji na unapotaka  kuchangia usiangalie sura ya Njowoka angalia Njorefa inafa inahitaji nini kutoka kwako"alisema Katibu wa Njorefa.

  Katibu huyo aliwataja wadau wakubwa  waliotoa michango hiyo kuwa ni pamoja na Mkurugenzi wa shirika la Tanwat  Rajeev Singh ambaye  alitoa Bati zenye thamani ya shilingi laki nane, Diwani wa kata ya Uwemba Bw. Edward  Mwalongo ambaye alichangia mbao zenye thamani ya shilingi 355000/= na Mkurugenzi wa kampuni ya Jr fire familigaion  Bw Raymond Ngondola alitoa mifuko  kumi ya saruji yenye thamani ya shilingi 140,000/=.


  Naye Afisa Utamaduni na michezo Mkoa wa Njombe Steven Sanga alitumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wa timu mbalimbali kuhakikisha wanaweka mipango madhubuti itakayoifanya michezo kusonga mbele  ikiwa pamoja na  kufuata taratibu na kubainisha kuwa viwanja vingi vya michezo Mkoani hapa  vinamilikiwa na taasisi za elimu hali ambayo inawalazimu kuanza kufanya marekebisho ili kuvitumia katika michezo.
   
  Nao baadhi ya wadau hao, Rajeev Singh na Raymond Ngongola aliwasihi  wazazi kuachana na itikadi ya kudhani michezo ni uhuni badala yake kuanza kufikiria kuwa michezo huchangamsha akili ya mwanafunzi na kuahidi kuendelea kukichangia chama hicho.

  0 0

   Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani) juu ya mafanikio ya uzalishaji wa chakula nchini kwenye viwanja vya Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa (NFRA) jijini Dar es Salaam leo.

   Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani) kwenye viwanja vya Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa (NFRA) jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Mkuregenzi wa Mipango na Uendeshaji wa NFRA, Anna Ngoo. 

   Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani) kwenye viwanja vya Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa (NFRA) jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa (NFRA) Charles Walwa na kushoto ni Mkuregenzi wa Mipango na Uendeshaji wa NFRA, Anna Ngoo. 
   Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa (NFRA) na waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza. 
   Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza, akiangalia magunia ya vyakula yaliyohifadhi wa kwenye ghala la Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa (NFRA) baada ya kuzungumza na waadhishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

  Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza, akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa waandishi wa habari kabla ya kuondoka kwenye viwanja vya Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa (NFRA).Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa (NFRA) Charles Walwa. Picha na Hussein Makame-MAELEZO. 

  0 0
 • 09/04/14--20:00: Ngoma azipendazo ankal
 • Carlos Santana -- "Black Magic Woman"

  0 0

  Madaraka Nyerere, Mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Julius Nyerere, pamoja na Mwanamuziki Mzalendo Vitali Maembe wameteuliwa na shirika lisilo la kiserikali Culture and Development East Africa (CDEA) kuwa mabalozi wa kushiriki kampeni ya kupanda Mlima Kilimanjaro ili kuhamasisha jamii kuchangia ujenzi wa jukwaa la sanaa na ubunifu jijini Dar es Salaam.

  Kampeni hiyo ya kupanda Mlima Kilimanjaro imeandaliwa na CDEA kupitia njia ya kupanda Mlima Kilimanjaro kuanzia Septemba 7 hadi 13 mwaka huu ili kujenga jukwaa na sanaa na ubunifu litakalowapa fursa wasanii na vijana kukutana, kufikiri na kubuni kwa pamoja ambapo mawazo ya kisayansi yatakutana na sanaa na pia sanaa kukutana na taaluma nyinginezo nyingi.

  Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Ayeta Wangusa anasema “ili kufanikisha kampeni yetu ya mwaka mmoja tuliyoipa jina la ‘FUN FOR FUNDS’, tumeona ni vyema kupanda mlima Kilimanjaro kwa kumtumia Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya CDEA, Madaraka Nyerere pamoja na Vitalis Maembe ambaye ni mwanamuziki mzalendo”.
  DSC_0045
  Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi na Balozi wa kampeni ya "Fun For Funds", Madaraka Nyerere (wa tatu kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam dhumuni lake la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za jukwaa la sanaa na ubunifu ili kukuza vipaji vya vijana kupitia mafunzo mbalimbali ya sanaa na kutoa muongozo wa jinsi ya kuanzisha wazo la ubunifu na kulikamilisha.Na kuongeza pia vijana wataunganishwa na majukwaa mengine kama hili kwa nchi za Afrika Mashariki kama vile The Nest, PAWA 254 na Creative Garage yote ya Kenya na Africa Sanaa Kollective ya Uganda.
  DSC_0067
  Balozi wa kampeni ya kuchangisha fedha, “FUN FOR FUNDS” mwanamuziki mzalendo mzee wa ‘Sumu ya Teja’ , Vitali Maembe akizungumza na waandishi wa habari ambapo amewataka wasanii wenzake kuungana kuwa kitu kimoja katika kukuza utamaduni wetu kwa kubadilishana uzoefu wa kazi zao bila choyo.
  DSC_0104
  Mjumbe wa bodi ya shirika lisilo la kiserikali la Culture and Development East Africa (CDEA), Rose Haji Mwalimu akitoa rai kwa waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo (hawapo pichani) na kuwataka kutumia kalamu zao vizuri na kuhakikisha kampeni hii inafanikiwa.

  0 0  0 0

  Bondia maarufu wa kike mwafrika barani ulaya Bintou Yawa Schmill aka "The Voice" anatarajiwa kupanda ulingoni tarehe 26 September 2014, atapambana na bondia  Mirjana Vujickatika ukumbi wa Stadthalle/ Saalbau Frankfurt-Nied, Mjini Frankfurt ujerumani.

  Bondia Bintou Yawa Schmill aka "The Voice" mzaliwa wa Togo ambaye anapigia uzito wa Welterweight -64 Kg, urefu mita 1.71  historia yake hapo mwanzo alikuwa bondia wa ngumi za ridhaa kwa muda miaka mitano,kuanzia mwaka 2007 alianza kuingia katika ngumu za kulipwa (professional boxer) amepigana (fights) 8 kashinda 7(wins) kashinda kwa
  K.O.s 7.

  Bondia Bintou Yawa Schmill ni juzi tu katimiza umri wa miaka 30,mwanafunzi wa chuo kikuu cha Bremen na ndiye aliyelipamba jarida la maarufu la warembo "Penthouse",bondia huyo wa kike anayeiliwakilisha bara Afrika Ughaibuni mara nyingi amefananishwa
  na SIMBA (Bintou is the Lioness),Simba ambaye ukimuona mpishe njia ulingoni. Bintou "The Voice" Schmill sasa kapania kuweka rekodi ya kuwachapa wapinzania wake kila kona duniani !
  Mengi kuhusu bondia Bintou Schmill aka 'The Voice" usikose at
  For more information write to
   Africans support your children and make them proud NOW! http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=iEmjbWJr


  0 0

  Maswala ya udukuzi yameendelea kushika kasi katika maeneo mbali mbali ulimwenguni ambapo mataifa mbali mbali yameamua kuunganisha nguvu ya pamoja kupambana na uhalifu mtandao. Katika "UCHAMBUZI" nilio uandikia nilibainisha umuhimu wa kupata chombo kimoja chenye jukumu la kupambana na uhalifu mtandao ambacho kitatoa nguvu kubwa ili kuweza kukabiliana na hali mbaya ya uhalifu mtandao hivi sasa.

  Kundi jipya lenye makao yake barani ulaya linalounganisha pamoja nchi wanachama wa bara ulaya pamoja na Canada, Colombia, Australia na marekani limedhamiria kuunganisha mataifa mengine na kuhakiki maswala mbali mbali yahusuyo usalama mtandao yanafanyiwa kazi ipasavyo.

  Kwa wafatiliaji wa habari za maswala ya usalama mitandao watakua wamepata  kuona taarifa mbali mbali za hivi karibuni zenye kuonyesha ukuaji wa kasi wa uhalifu mtandao ambapo umetabiriwa kushika kasi zaidi kadri muda unavyo zidi kwenda ambapo uhalifu mwingi wa sasa unategemewa kuhamia katika mitandao.

  Katika andiko la naibu mkurugenzi wa chombo cha uingereza kinacho shughulikia maswala ya uhalifu mtandao pamoja na kiongozi  wa kundi jipya la muunganiko wa nchi la kukabiliana na uhalifu mtandao kama inavyo someka "HAPA" wame elezea ukuaji wa changamoto mbali mbali kwa vyombo vya usalama katika mataifa mengi na kusisitiza kuna umuhimu mkubwa wa kuunganisha nguvu za pamoja ili kuweza kufanikiwa katika vita dhidi ya uhalifu mtandao.

  J-CAT imedhamiria kuzileta pamoja nchi wanachama pamoja na mataifa mengine yatakayo onyesha utayari ili kuweza kukabiliana kwa pamoja dhidi ya uhalifu mtandao ambapo matumaini makubwa yatakua ni kukusanya taarifa za kiuhalifu kutoka katika makampuni ya serikali na binafsi ili kubaini aina za uhalifu na kujua maeneo athirika zaidi ili kuweza kuunganisha nguvu. Nchi zaidi zitaenelea kushirikishwa baada ya majaribio ya mpango huu wa kuunganisha nguvu kuweza kufikia pazuri.

  Aidha, Chombo cha upelelezi cha Marekani (FBI) kupitia taarifa inayosomeka "HAPA" imebainisha kulipa kipaumbele cha juu swala la mapambano dhidi ya uhalifu mtandao kutokana na kilicho zungumzwa na mkurugenzi wake ya kuwa nchi hiyo tayari imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupambana na wahalifu wanao onekana na kwa sasa wahalifu mtandao kua ndio changamoto yake kubwa na hivyo wameazimia kuanza mapambano na uhalifu huo.

  Kwa upande mwingine katika mkutano mkuu wa maswala ya usalama mtandao wa mwisho wa mwaka ambapo nimeteuliwa kuwa katika panel ya washauri mada zinazotegemewa kujadiliwa na wataalam kutoka maeneo yote duniani ni pamoja na kutafuta njia rafiki ya kufikiwa kwa malengo ya kuunganisha hasa bara la afrika kuweza kuwa na njia ya pamoja ya kupambana na uhalifu mtandao huku maswala ya kisheria  za kimtandao yanavyo sumbua mataifa mbali mbali nini utatuzi wake. 

  Panategemewa kupatikana taarifa kamili ya mkutano huo mapema ili watanzania ( wenye ufahamu wa maswala ya usalama mtandao) nao waweze kushiriki.

older | 1 | .... | 560 | 561 | (Page 562) | 563 | 564 | .... | 3283 | newer