Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live

HAPPY BIRTHDAY TO BEST DAUGHTER THE WHOLE WIDE WORLD!

$
0
0
Having a daughter means...
Seeing a thousand rainbows every day,
A thousand occasions of sweet hurray,
A thousand sweet dreams every night,
And a thousand reasons to laugh and smile!

As parents we hope that you touch the life of thousands of other people with the same happiness, care and love that you have touched ours. 
We feel so proud and happy to see that our little girl has grown into such a fine, young and beautiful woman. Much love and blessings coming your way.

Happy Birthday to the best 
daughter in the whole wide world!

NHIF kuendelea kuboresha huduma za afya nchini.

$
0
0



Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Raphael Mwamoto akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)kuhusu mpango wa kuendelea kuboresha huduma za Afya nchini, wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na Uwekezaji kutoka Mfuko huo Bw. Deusdedit Rutazaa.

Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na Uwekezaji kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Deusdedit Rutazaa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wa kuanza kutoa mikopo ya dawa kwa vituo ambavyo vimesajiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti kutoka Mfuko huo Bw. Raphael Mwamoto.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwasikiliza wawasilishaji kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Mkongo wa Taifa wasaidia kushuka kwa gharama za mawasiliano nchini

$
0
0

Msemaji wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Bi. Prisca Ulomi akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya mkongo wa Taifa ikiwamo kusaidia kushuka kwa gharama za Mawasiliano nchini. Kushoto ni Mkurugenzi huduma za mtandao wa TTCL Mhandisi Joram Lujara.
Mratibu wa Ufundi kutoka Ofisi ya Mkongo wa Taifa Mhandishi Anifa Chingumbe akiwaonesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) maeneo ambayo mkongo wa Taifa umepita, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. 

(Picha na Hassan Silayo)
 
Frank Mvungi
Serikali imesema Mkongo wa Taifa umesaidia kushuka kwa gharama za  mawasiliano kwa watumiaji wa mwisho nchini kutoka sh.147 kwa dakika mwaka 2009 hadi shilingi 62 kwa dakika mwaka 2013.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Wizara ya Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mawsiliano Sayansi na Teknolojia Bi Prisca Ulomi wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akifafanua Bi Prisca amesema kuwa mkongo wa taifa umesaidia pia kushuka kwa gharama za intaneti kutoka shilingi 36,000 hadi shilingi 9000/Gb kufikia mwaka 2013.
“Mkongo wa Taifa umesesaidia kuharakisha usambazaji wa huduma za mawasiliano katika maeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara”alisisitiza bi Ulomi.
Katika hatua nyingine, Bi Ulomi alisema faida nyingine ya Mkongo ni kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma za mawasiliano na uwezo wa kusafirisha masafa.
Akieleza kuhusu gharama Bi Prisca amesema gharama za maunganisho ya mawasiliano ya simu za mkononi kutoka  kampuni moja kwenda nyingine  (interconnection fees) ambapo sasa gharama imepungua kutoka sh. 115 hadi shilingi 34.92 kwa dakika.
Mkongo wa Taifa umesaidia kuongeza ushirikiano wa kikanda  kati ya nchi za Afrika Mashariki na kati ambapo nchi za Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi, Uganda, na Kenya ambapo hali hiyo imeongeza fursa za kibiashara na kukuza uchumi wa nchi.

Kufikia mwaka 2013 makampuni yafuatayo yalikuwa yameunganishwa na mkongo wa Taifa ni TTCL, TIGO, Zantel,  Airtel, Vodacom, Simbanet na infinity.

SHIRIKA LA NYUMBA TANZANIA (NHC) LAKARABATI SHULE YA HASSANGA JIJINI MBEYA

$
0
0
 Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas  Kandoro akikata utepe kuzindua ukarabati wa Madarasa manne na Jengo moja la Utawala katika Shule ya Msingi Hasanga uliofanyika leo Uyole Mbeya.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas  Kandoro, viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa Tanzania (NHC), Viongozi wengine wa Serikali na Walimu wa Shule ya Msingi ya Hasanga wakifurahia Baada ya Kuzindua Rasmi ukarabati wa ujenzi huo.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akizungumza na wananchi, wanafunzi na Walimu wa Shule ya Msingi ya Hasanga katika Sherehe ya kukabidhi Majengo ya Shule hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa NHC Nehemia Mchechu akizungumza jambo wakati wa Sherehe hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigallah King akimkaribisha Mkuu wa Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

RITA NA NBS WAENDESHA MAFUNZO YATAKAYOWEZESHA KUFANYA TATHMINI YA KINA YA MATUKIO MUHIMU YA MWANADAMU.

$
0
0
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Eliya Ntandu akifungua mafunzo ya siku sita ya maofisa watakaoshiriki katika Tathmini ya kina ya Matukio Muhimu ya Mwanadamu. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa NBS, Bi Aldegunda Komba, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk. Albina Chuwa, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bi Emmy Hudson na Kamishna wa Sensa, Hajjat Amina Mrisho Said.

 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bi. Emmy Hudson akitoa maelezo kuhusu ushiriki wa RITA katika tathmini.

 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dk. Albina Chuwa akitoa maelezo kuhusu ushiriki wa NBS katika tathmini.

Picha ya Mgeni Rasmi na washirki wa Mafunzo.


Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wanaendesha mafunzo ya siku sita kwa maofisa watakaoshirki kufanya tathmini ya kina ya Usajili na Takwimu za matukio muhimu ya mwanadamu ambayo ni Vizazi, Vifo, Ndoa na talaka. Mafunzo hayo yamefunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Eliya Ntandu Jana Jumanne tarehe 2 Septemba 2014 na yanafanyika katika ukumbi wa 88 Motel, Mkoani Morogoro.

Mafunzo hayo yanawashirikisha maofisa kutoka taasisi mbali mbali zinazohusika na masuala ya usajili wa wananchi ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya kuwapa uwezo wa kufanya tathmini ya kina ya mifumo na sheria zilizopo zinazohusika na usajili wa matukio muhimu ya mwanadamu ambayo ni Vizazi, vifo, Ndoa na Talaka .

 Tathmini inategemewa kufanyika tarehe 15 -30 Septemba 2014 katika mikoa na wilaya mbalimbali nchini na maofisa waliopewa mafunzo wataweza kukusanya taarifa katika vituo vya tiba, vituo vya polisi, ofisi za wasajili wa wilaya, ofisi za kata, nyumba za ibada na katika makazi ya wananchi.

 Matokeo ya Tathmini yanategemewa kutoa mwelekeo katika mchakato wa kuweka vipaumbele na mipango ya utekelezaji wa mfumo thabiti wa usajili wa raia na utoaji wa takwimu za matukio muhimu, mfumo utakaokuwa kiungo muhimu katika utekelezaji wa utawala bora na pia chanzo cha msingi cha takwimu za matukio kama vizazi, ndoa, talaka na vifo na sababu zake.

RITA NA NBS wanafanya tathimini hii ikiwa ni utekelezaji wa moja ya maazimio ya  Mkutano Mawaziri wanaohusika na masuala ya usajili wa raia wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Mwaka 2012 katika Jiji la Duban, Afrika ya Kusini. Kwa mujibu wa azimio hilo kila nchi mwanachama inatakiwa kufanya tathmini hii na kuwasilisha matokeo yake katika kikao kama hicho kinachotegemewa kufanyika  mwanzoni mwa mwaka ujao.

BALOZI KAMALA ATEMBELEA KAMPUNI INAYOTENGENGEZA NYUMBA ZA MBAO ZA GHARAMA NAFUU

$
0
0
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (aliyevaa miwani) akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki wa kampuni ya Ubelgiji inayotengeza nyumba za mbao za gharama nafuu. Wa pili kulia ni Afisa mfawidhi wa Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji Bwana Nyamtara Mukome. Ziara hii imefanyika leo mjini Charleroi  Ubelgiji.

Benki ya BOA kuwawezesha wasambazaji wa bidhaa za Vodacom

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza (kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akizindua ushirikiano wa kampuni yake na Benki ya Afrika (BOA) Tanzania unaowawezesha mawakala wa M-pesa na wasambazaji wa huduma za Vodacom kupata miko nafuu na bila dhamana kuinuua biashara zao. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya BOA, Ammish Owusu – Amoah.Hafal hiyo imefanyika Makao Mkauu ya Vodacom, Dar es salaam.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Afrika (BOA) Tanzania Ammish Owusu – Amoah (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza wakipongezana mara baada ya kutangaza rasmi ushirikiano unaowawezesha mawakala wa M-pesa na wasambazaji wa huduma za Vodacoyam kupata mikopo nafuu na bila dhamana kutoka BOA kwa lengo la kuinuua biashara zao. Mikopo hiyo ni kati ya Sh 10 Milioni na 75 Milioni.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Afrika (BOA), Ammish Owusu – Amoah(kushoto)akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na kuingia ubia na Vodacom Tanzania ambao utawawezesha mawakala wa kuuza na kusambaza bidhaa za kampuni hiyo kupata mikopo ya masharti nafuu na bila amana ili kuwawezesha kutoa huduma bora kwa wateja wao,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Rene Meza.

 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Afrika (BOA)-Tanzania na wa Vodacom Tanzania wakifuatilia  mkutano wa waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa ushirikiano kati ya BOA benki na  Vodacom Tanzania  ambao utawawezesha mawakala wa M-pesa na wauzaji wakubwa wa bidhaa za Vodacom kupata mikopo ya kati ya Sh 10 Milioni na 75 Milioni kwa masharti nafuu na bila amana ili kuwawezesha kutoa huduma bora kwa wateja.

Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Hassan Saleh(kulia) na Mkuu wa Mauzo  wa M pesa Franklin Bagala wakifuatilia  mkutano wa waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa ushirikiano kati ya BOA benki na  Vodacom Tanzania  ambao utawawezesha mawakala wa M-pesa na wauzaji wakubwa wa bidhaa za Vodacom kupata mikopo ya kati ya Sh 10 Milioni na 75 Milioni kwa masharti nafuu na bila amana ili kuwawezesha kutoa huduma bora kwa wateja.

JESHI LA POLISI LATOA ONYO KALI KWA WANAOTUMIAJI VIBAYA MITANDAO

$
0
0
MSEMAJI wa Jeshi la Polisi, Advera Senso akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Septemba 3,2014 kuhusu kupiga marufuku watu wanaotumia mitandao kinyume na taratibu.HABARI/PICHA NA PHILEMON SOLOMON

======== ======  ======
JESHI la Polisi nchini limetoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao vibaya ikiwemo kutuma ujumbe wa matusi, uchochezi, picha za utupu sanjari na kukashifu viongozi wa Serikali, dini na watu mashuhuri.

Akizungumza Dar es Salaam, Septemba 3,2014  Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema kuwa tayari baadhi ya watu wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo na wengine wanaendelea kuhojiwa.

"Kumejitokeza tabia kwa baadhi ya watu kutumia mitandao ya kijamii na simu za kiganjani kinyume na malengo yaliyokusudiwa kwa kusambaza taarifa za uchochezi, kashfa,kuchafua viongozi wa Serikali.

"Wengine wamekuwa wanasambaza picha utupu ambazo hazina maadili, hali ambayo ni kosa la jina, ingawaje mwingine anaweza hasijue kuwa kufanya hivyo ni kosa lakini sheria haitamuacha, alisema.

Senso aliendelea kubainisha kuwa kuvunja kutofahamu sheria kwa kutoifahamu si sehemu ya kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria, atakabainika kutenda kosa hilo bila kujali anaifahamu sheria au la, atachukuliwa adhabu kali.

Alisema oparesheni ya kuwabaini wanaosambaza ujumbe zinaendelea nchi nzima kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa lengo la kuwakamata waharifu wa aina hiyo.

Aliongeza kuwa hatua hiyo pia inawatia hatiani wale wote wanaotumia mitandao kufanya utapeli na kujipatia kipato kwa watu mbalimbali nchini sanjari na blogs zinazosambaza picha chafu ambazo ni kinyume na maadili.

"Wapo baadhi ya watu wanatumia mitandao ya simu kutapeli watu na kujipatia kipato, hivyo nao ni sehemu ya waharifu wanaotafutwa na jeshi la polisi na yeyote atayekamatwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yake," alisema.

Hivyo alisisitiza kuwa Jeshi hilo linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uharifu huo, na kuwataka wale wanaotumiwa wa aina hiyo kutousambaza kwa wengine bali waufute.


Pia aliziomba kampuni za simu za mkononi pindi wanapoona ujumbe wa aina hiyo wasiruhusu uende kwa mwingine ili nao wawe sehemu ya kupambana na uovu huo.

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA AMANI NA USALAMA WA BARAZA LA AMANI NA USALAMA LA UMOJA WA AFRIKA JIJNI NAIROBI

$
0
0

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenzatta jijini Nairobi leo kujiunga na viongozi wengine wanaounda Baraza la Amani na Usalama la nchi za umoja wa Afrika (AU) kwenye mkutano wa kuzungumzia masuala ya tioshio la ugaidi linalolikabili bara hilo na dunia kwa ujumla.
Inspekta Jenerali wa Polisi Ernest Mangu na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakielekea kwenye ukumbi wa mikutano katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenzatta jijini Nairobi katika mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la nchi za umoja wa Afrika (AU) kuzungumzia masuala ya tioshio la ugaidi linalolikabili bara hilo na dunia kwa ujumla.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Yoweri Kaguta Museveni wakiteta jambo katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenzatta jijini Nairobi katika mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la nchi za umoja wa Afrika (AU) kwenye mkutano wa kuzungumzia masuala ya tishio la ugaidi linalolikabili bara hilo na dunia kwa ujumla.
Nyimbo za AU na Kenya zikipigwa kabla ya mkutano wa kuzungumzia masuala ya tishio la ugaidi linalolikabili bara hilo na dunia kwa ujumla katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenzatta jijini Nairobi. PICHA NA IKULU.

Microsoft Windows Phone 8.1yatambulishwa Tanzania kupitia Lumia 930, Lumia 630 and Lumia 530

$
0
0
 Meneja uzalishaji wa kampuni ya Nokia Afrika Mashariki, Kingori Gitahi akiwaonesha waandishi wa habari moja kati ya simu tatu zilizozinduliwa.

Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Nokia Afrika Mashariki, Bi.Lilian Nganda akizungumza na waandishi wa habari Septemba 3,2014 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya Nokia aina ya Lumia 530, 630 na 930.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia tukio la uzinduzi wa simu hizo.
 Kati ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakishuhudia uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo.
Miongoni mwa wafanyakazi wa kampuni hiyo wakishuhudia uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo.HABARI / PICHA NA PHILEMON SOLOMONI

WAFANYABIASHARA na watumiaji wengine wa simu za kiganjani wamepata matumaini mapya baada ya simu nyingine tatu aina ya Nokia Lumia 530, 630 na 930 kuzinduliwa.

Kwa mujibu wa Meneja uzalishaji wa kampuni ya Nokia Afrika Mashariki, Kingori Gitahi akizungumza Dar es Salaam, Septemba 3, 2014  wakati wa kuzindua simu hizo alisema zinauwezo mkubwa kwa matumizi ya mtandao.

"Naamini kwa wafanyuabiashara na watumiaji wa kawaida watakuwa wamepata fursa nzuri ya kutumia na kupkea email kwa urahisi sanjari na kuchukua picha za video na zilizomo katika mitandao kwa wepesi,"alisema.

Pia aliongeza katika kuhakikisha wanatoa huduma nzuri za uhakika wameshirikiana na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Vodacom na Airtel ambao hutoa vifurushi mitandao kwa wateja watakaonunua simu hizo.


Gitahi aliongeza kuwa simu hizo zinauwezo wa kupiga picha kwa haraka zaidi na kurekodi matukio mbaliombali kwa ustadi mkubwa na anaamini watu wengi watakuwa watumiaji wazuri ili kujiweka katika kiwango cha kimataifa.

MMOJA NA WENZAKE WAWILI MBARONI KWA KUKUTWA NA PEMBE ZA NDOVU MKOANI DODOMA

$
0
0
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kw ajina la DOUGLAS S/O MNYEKE, Miaka 46, Mkaguru Mukulima na Mkazi wa kijiji cha Silwa Kata ya Pandambili, Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma akiwa na pembe za ndovu vipande vitatu vyenye uzito wa jumla ya kilo 12 na gramu 30 vyenye thamani ya Tshs. 11, 162, 250/= vikiwa nyumbani kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema tukio hili limetokea tarehe 30/08/2014 majira ya 15:02hrs katika kijiji cha Silwa Kata ya Pandambili, Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.

Kamanda MISIME amesema baada ya mtuhumiwa huyo kuhojiwa alikiri kuwa na mzigo ndani  ya nyumba yake  wenye vipande vinne vya pembe za ndovu vikiwa kwenye mfuko wa salfeti maarufu kama kiroba cheupe na kueleza kuwa aliletewa na watu wawili ambao ni NORBERT S/O KAHWIL, Miaka 32, Mbena, Mkulima wa Ngomai Wilaya ya Kongwa na BONIFACE S/O MASINGISA, Miaka 30, Mkaguru, Mkazi wa Silwa Kata ya Pandambili Wilaya ya Kongwa.

Aidha Kamamnda MISIME amesema watuhumiwa wote watatu walikamatwa na wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa uchunguzi zaidi na pembe hizo zimehifadhiwa kama kielelezo pia watafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu kukamilika.

Wajumbe Kundi la 201 watoa tamko dhidi ya wanaolichafua Bunge Maalum la Katiba na Wajumbe wa kundi hilo.

$
0
0
 Askofu Amos Muhagachi akitoa tamko juu ya tuhuma mbalimbali dhidi ya kundi la 201 la wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo 03 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa Spika, Mjini Dodoma.

 Mwenyekiti wa kundi la 201 ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt. Francis Michael akikanusha kuhusu madai ya wajumbe wa kundi hilo kupewa rushwa kuhusu mchakato wa Katiba Mpya.

 Sheikh Hamid Jongo akiviasa vyombo vya habari kutoa ushirikiano ili kuhakikisha kuwa mchakato wa kupata Katiba Mpya unafanikiwa kwakuwa hata wao (vyombo vya habari) unawahusu pia.
Askofu Donald Mtetemela akichangia mada wakati wa mkutano wa kutoa tamko kuhusiana na tuhuma mbalimbali dhidi ya kundi la 201.
Baadhi ya wajumbe wa kundi la 201 pamoja na waandishi wa habari wakifuatilia tamko hilo leo 03 Septemba, 2014 katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Spika Bungeni mjini Dodoma.(Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma).

TIMU YA MAJAJI KWA AJILI YA KUMTAFUTA MSHINDI WA TUZO YA RAIS YA HUDUMA ZA JAMII NA UWEZESHAJI YATEMBELEA MGODI WA NORTH MARA

$
0
0
 Meneja Mahusiano wa  Mgodi wa North Mara Bi Fatuma Mssumi (mbele) akielezea shughuli za mgodi wa North Mara mbele ya jopo la majaji waliotembelea mgodi huo ili kuendelea na zoezi lake la  kumtafuta  mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji.

 Afisa Mahusiano wa Mgodi wa North Mara Bw. Zakayo Kalebo (wa tatu kutoka kushoto) akielezea mchango wa mgodi wa North Mara katika ujenzi wa nyumba za  wauguzi wa zahanati ya Matongo (zinazoonekana nyuma)  mbele ya timu ya  majaji  na sekretarieti iliyotembelea mradi wa nyumba hizo. Mradi wa nyumba hizo uligharimu   Dola za Marekani 100,000.

 Afisa Uhusiano wa Kijiji cha Matongo Bw. Magesa  Wanjara akionesha jinsi ya kutumia bomba la kisima cha maji kilichofadhiliwa na  mgodi wa North Mara mbele ya  timu ya majaji, sekretarieti na wajumbe wengine.

 Afisa Mahusiano wa Mgodi wa North Mara Bw. Zakayo Kalebo ( wa tano kutoka kushoto) akielezea mchango wa mgodi wa North Mara katika uwezeshaji wa kikundi cha vijana katika mradi wa kitalu cha mboga za majani, mbele ya majaji na sekretarieti iliyotembelea kitalu hicho. (kinachoonekana kwa nyuma).

DK SHEIN ASHIRIKI UZINDUZI WA MPANGO WA MABADILIKO YA TABIA NCHI NA CHANGAMOTO ZAKE MAGHARIBI YA BAHARI YA HINDI

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Viongozi mbali mbali baada ya  uzinduzi wa  Mpango wa Magharibi ya Bahari ya Hindi ya Changamoto za Ukanda wa Pwani wa mabadiliko ya Tabianchi  katika viwanja vya Orator Hotel,Apia Samoa.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Waziri Mkuu wa Mauritius wakati wa chakula baada ya uzunduzi wa Mpango wa Magharibi ya Bahari ya Hindi ya Changamoto za Ukanda wa Pwani wa mabadiliko ya Tabianchi jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akigonganisha glasi na Viongozi mbali mbali kuonesha ishara ya uzinduzi wa  Mpango wa Magharibi ya Bahari ya Hindi ya Changamoto za Ukanda wa Pwani wa mabadiliko ya Tabianchi  wakati wa chakula katika ukumbi wa Orator Hotel,Apia Samoa.[Picha na Ramadhan Othman,Samoa.]

TAARIFA YA WAWAKILISHI WA TAASISI ZA DINI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA TOKA WAJUMBE 201 KUHUSU MWENENDO WA SHUGHULI ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA

$
0
0
 Sisi Wawakilishi wa Jumuiya na Taasisi za Dini, tuliopendekezwa na Taasisi zetu na baadaye kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kushauriana na Rais wa Zanzibar kuwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, na kula kiapo cha utekelezaji wa jukumu hili kubwa.
Tukiamini kuandaa Katiba Mpya kwa maridhiano ya Kitaifa kwa wananchi wote, tulipokea jukumu hili kama wajibu wetu Kitaifa.  Aidha tunaamini kwamba katika kupata maridhiano ya Kitaifa ni muhimu kuheshimu kila wazo na fikra inayotolewa na kuunganisha fikra hizo kwa usahihi, kwa njia ya kidemokrasia kwa kupiga kura na kukubaliana na matokeo ya wengi.
Kama ilivyoelezwa hapo awali, kabla ya kuanza shughuli za Bunge Maalum, kila mjumbe alikula kiapo cha kuwa mwaminifu na mtiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kadiri ya uwezo wake na ufahamu wake, kufanya kazi zinazomhusu, bila upendeleo na kumuomba Mwenyezi Mungu amsaidie. 
Tumeshangazwa na kusikitishwa sana kuona kwamba mchakato wa kutayarisha Katiba itakayopendekezwa na Bunge hili kwa wananchi, unachafuliwa taswira yake.  Bunge Maalum la Katiba linachafuliwa na, shughuli zake kuingiliwa na kupotoshwa na wajumbe wenzetu walio nje ya Bunge, Makundi, Taasisi na Vyombo mbali mbali vya habari, uhalali na ukweli wa shughuli za BungeMaalum la Katiba unapotoshwa.  Wananchi wanaaminishwa yasiyo na ukweli.
Upotoshwaji huu umezua mijadala mbali mbali katika jamii ya Watanzania na bado linaendelezwa kama ifuatavyo:
1.   Kwamba Bunge Maalum la Katiba halina uhalali kwa kuwa hao wajumbe wenzetu walioondoka wameliondolea uhalali wake kwa vile hwapo, wakiwepo Bungeni basi uhalalai wake utakuwepo - utapatikana;
2.   Inadaiwa kwamba Kanuni za Bunge Maalum la Katiba zinavunjwa ovyo ovyo;
3.   Inadaiwa pia, kwamba kinachojadiliwa sasa katika Bunge hili ni Waraka mwingine na si Rasimu iliyotayarishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, iliyowasilishwa rasmi Bungeni na kuanza kujadiliwa na wajumbe;
4.   Inadaiwa na watu na Taasisi mbali mbali, kwamba viongozi wa dini, wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, na wajumbe wa Kundi la 201, wanapewa rushwa. Isitoshe Vyombo vya habari vimeandika tuhuma kama hizi.
5.   Inadaiwa pia kwamba wajumbe waliomo katika Bunge hili ni wachache, ukilinganisha na hao walioko nje ya Bunge hilo;
6.   Bunge hili, kwa tuhuma hizo, lazima lisitishwe au livunjwe na Mhe. Rais.

BALOZI KAMALA AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA KAMPUNI YA DELANOUT YA UBELGIJI

$
0
0
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye miwani) akimkabidhi zawadi ya mwamvuli unaotangaza vivutio vya Utalii Tanzania Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya DELANOUT ya Ubelgiji Bwana. Jackson Delanout. Balozi Kamala yuko kwenye ziara ya kuhamasisha makampuni ya Ubelgiji kushiriki kwenye ziara ya biashara ya makampuni ya Ubelgiji  itakayofanyika Tanzania, Novemba mwaka huu.

Karibuni Ibada ya Kiswahili - Columbus, Ohio Jumapili Septemba 07, 2014

$
0
0
Waacheni watoto wadogo waje kwangu wala msiwazuie;
kwa maana Ufalme wa Mbinguni ni wao. - Mathayo 19:14.
Karibuni wote Jumapili hii ya tarehe 7 Septemba kwenye Sikukuu ya Mikaeli na Watoto. Ibada itaongozwa na watoto ambao watatuonyesha vipaji vyao mbalimbali ambavyo Mwenyenzi Mungu amewabariki navyo. Tafadhali mkaribishe na rafiki/jirani yako. Mbarikiwe!

WAZIRI MKUU PINDA NA WAJUMBE MBALIMBALI WA BUNGE LA KATIBA LEO MJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimana na Meya wa Songea, Charles Mhagama,kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 4, 2014. Katikati ni Mbunge wa Songea mjini ,Dr. Emmanuel Nchimbi.
 Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ,Mohamed Raza  (kushoto) na Ally Juma Othman Ally (katikati) wakizungumza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 4, 2014. 
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Ally Juma Othman Ally kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Septemba 4, 2014
  Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pida na Anne Kilango Malecala wakiteta kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 4, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

TAARIFA YA BONANZA LA SHIMMUTA

Serikali yaanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya wanajeshi

$
0
0

 Baadhi ya nyumba zilizojengwa eneo la Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi Nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya Wanajeshi.
Picha na Hassan Silayo. 
 Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Meja Josephat Musira akiwaeleza Waandishi wa habari (Hawapo pichani)kuhusu Mradi wa ujenzi wa Nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya Wanajeshi ambapo kwa awamu ya kwanza idadi ya nyumba 6064 zinatarajiwa kujengwa na mpaka sasa nyumba 1160 zimeshakamilika kwa ajili ya matumizi, wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika moja ya eneo la maradi Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Ushauri wa Majenzi wa Wizara hiyo Mhandisi Stephen Mpapasingo.

 Mkuu wa Kitengo cha Ushauri wa Majenzi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhandisi Stephen Mpapasingo akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) sehemu ya jiko katika moja ya nyumba hizo.

Mkuu wa Kitengo cha Ushauri wa Majenzi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhandisi Stephen Mpapasingo akiwaeleza Waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya Wanajeshi, wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika moja ya eneo la maradi Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msemaji wa Wizara hiyo Meja Josephat Musira

Frank Mvungi-Maelezo
Serikali yaanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba 10,000 kwa ajili ya makazi ya wanajeshi kote nchini.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Meja Josephat Musira wakati wa  ziara ya waandishi wa habari walipotembelea eneo la Gongo la mboto jijini Dar es salaam ambapo sehemu ya mradi huo inatekelezwa.
“Lengo la ujenzi wa nyumba hizi ni kupunguza tatizo la muda mrefu la uhaba wa nyumba kwa ajili ya makazi ya Maafisa na askari wa Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania na  Jeshi la Kujenga Taifa.”alisema Meja Musira.
Akifafanua Meja  Musira amesema awamu ya kwanza ya mradi huo imeanza ambapo  nyumba 6,064 zitajengwa na kugharimu dola za marekani milioni 300, utekelezaji wake unaendelea vizuri  katika Mkoa wa Dar es salaam na Pwani  tayari jumla ya nyumba 3128 zinajengwa.
Kwa Mkoa wa Dar es salaam Meja Musira amesema nyumba 2,228 zinajengwa katika maeneo ya Lugalo, Gongola mboto, Ukonga, Navy Kigamboni, Ubungo Kibangu, Kunduchi KTC, Mbweni JKT  na Kimbiji.
Akieleza zaidi Meja Musira amesema nyumba 1,160 kwenye maeneo manne ya Lugalo na Gongolamboto umeshakamilika kwa asilimia 100 na ukaguzi na uhakiki umeshafanyika.
Kwa upande wa Mkoa wa Pwani Meja Musira alisema  jumla ya nyumba 840 zinajengwa katika maeneo ya msangani,Nyumbu,Kiluvya,Kisarawe na shule ya mafunzo ya awali Kihangaiko.
Maeneo yanayohusika na mradi huu kwa sasa ni Arusha inatarajiwa kujengwa nyumba (792) Tanga (312) Pemba (320) Morogoro (616) Dodoma (592) Kagera (144) na Kigoma (160).
Kwa upande wake Mhandisi wa Wizara hiyo Bw. Stephen Mpapasingo amesema mradi huo unatekelezwa kwa awamu na  unalenga kuondoa kabisa tataizo la makazi kwa  Maafisa na askari wa Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania na  Jeshi la Kujenga Taifa
Mkandarasi wa mradi huu ni kampuni ya Shaghai Construction (Group) General Company  kutoka China
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live




Latest Images