Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 561 | 562 | (Page 563) | 564 | 565 | .... | 3285 | newer

  0 0


  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassary (anaeonekana kunyanyua kitu) akishirikiana na baadhi ya Wananchi wa vijiji vya Ushili na Sura Arumeru Mashariki kuchimba sehemu inayotakiwa kupita barabara ya Sawmill- Ushili mpaka Sura.
  Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassary akiendelea na kazi hiyo kwa kushirikiana na Wananchi wake.
  Kazi ikiendelea.

  Mapumziko kwa chakula cha mchana mara baada ya kuchapa kazi ya kutengeneza barabara.

  0 0

   Mzungu Kichaa will be performing at the opening of the South African music trade fair MOSHITO in Johannesburg Tonight (4th of September at 21.30). This marks the artists first first performance in South Africa.

  Mzungu Kichaa is originally from Denmark but grew up in Zambia and Tanzania where he currently has his base. Mzungu Kichaa will stay on for the duration of the Moshito Music Conference to represent DOADOA, an East African Performing Arts convention that provides a platform for professional networking and joint learning of music stakeholders within East Africa. – www.doadoa.org

  “I am very happy to finally be making this move, as I have had an ambition to visit South Africa for a long time now. I grew up in Zambia and recently performed at a festival in Zimbabwe so it was a “natural-next-step” for me to come to South Afirca”.

  “I will also be representing the East African Performing Arts Market DOADOA at Moshito. I am very proud to be on their steering committee as a representative from the music industry in Tanzania, and to be part of supporting and promoting East African music beyond its borders.

  I am hoping that this visit will open new opportunities for our music in Tanzania but also for other East African countries including Kenya, Uganda, Rwanda and Burundi.” Mzungu Kichaa was born in Denmark in 1980 and moved to Africa with his family in 1986. His name, which means the Crazy White Man in Swahili, was given to him by Juma Nature, one of the greatest rappers from Tanzania.


  0 0


  0 0


  0 0  0 0

  3Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akipokea mashine za kufyatulia matofali kutoka kwa Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Wilaya ya Temeke Bw. Wencenslaus Tillya ambazo zilikabidhiwa kwa vikundi vya vijana wilayani humo.
  4Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akikabidhi mashine kwa mwenyekiti wa kikundi cha Sokoine Youth Development William Gabriel.
  8Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akikabidhi mashine ya kufyatulia matofali mwenyekiti wa kikundi cha Chapakazi Youth Youth Nathanaeli Daniel Kidaila baada ya kuzipokea kutoka kwa Shirika la Nyumba la Taifa NHC. 


  0 0

  Katika maendeleo ya jamii yoyote, moja ya kitu muhimu ni kukuwa kwa maarifa ya wanajamii. Maarifa yatakayowapa uwezo wa kutumia ujuzi kwenye kutenda. Haijalishi upo kwenye fani gani, bali siku ya mwisho ni lazima uweze kutenda na siyo kuishia vitabuni.

   Kwa miaka mingi, nimekuwa nikifuatilia tatizo la ajira, umasikini nk hapa nchini, ingawa kuna mambo mengi sana ndani yake, lakini mzizi wa yote ni maarifa. Kizazi chetu SIYO kizazi cha watu wenye maarifa. Hii inawezekana ni kutokana na uvivu wa kujifunza au kutokuwa na nyenzo za kujifunza. Na kwakuwa na kizazi cha watu wasio na maarifa, kinapelekea kurudisha nyuma mambo mengi sana.

   Leo hii, kazi nyingi zinafanywa nje ya nchi, hata Toothpick tunaagiza kutoka nje, leo hii ukienda Supermarket zaidi ya asilimia tisini ya vitu, vinatoka nje. Sasa, swali la kujiuliza je hapa nyumbani hatuna watu wenye uwezo wa kutenda? Jibu, ni tunao, ila ni wachache na kasumba yetu inatuumiza pia wengi hawajiamini.

    Kitu ambacho nimejifunza na kukipenda nilipokuwa China (kwa miaka tisa) ni jinsi gani Wachina wamefanikiwa kujenga kikazi chenye maarifa. Na wana njia nyingi sanasana za kujifunza na siyo lazima uende chuoni. 

  Na wameweza kuitumia lugha yao kuwawezesha watu wake, Jiulize, leo hii hapa nyumbani kuna sehemu ngapi za kujifunza bila kulipia gharama ya ziada? Jiulize, leo hii kama utapata tatizo la kiufundi, kuna mtandao gani unaweza kutuma tatizo lako na ukapata msaada wa haraka? Ni michache sana sana kama siyo hakuna.

  Hivyo basi, katika kuhakikisha wanajamii wa Kitanzania wanapata maarifa, wale walio vyuoni wanajifunza kwa ufanisi (hawatoki wakiwa wamekariri tu), na wale walio mitaani wanajinoa na kuhakikisha wanakuwa wapya kila siku.

   Tunakuletea Dudumizi Forums , uwanja wa kujinoa maarifa ya IT. Ni uwanja utakaoweza kusoma, kuuliza na kijiendeleza zaidi.  Ni uwanja huru kwa wanajamii wote wenye moyo na hamu ya kujifunza na kusaidiana kwenye IT ili kufikia malengo. Jumuika sasa.

   Tembelea Dudumizi Forums  forum.dudumizi.com

   Huu ni mwanzo tu, katika kuhakikisha tunajenga jamii yenye maarifa, mambo mengi yatawajia toka Dudumizi kadri siku zinavyozidi kusonga . Hivyo, kuwa pamoja nasi.

  0 0

  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akiongeza Bunge hilo leo 5 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Fatma Hamid Saleh akiwasilisha taarifa ya kamati yake kwenye Bunge hilo leo 5 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
  Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba nao wakiwasilisha taarifa za kamati zao kwenye Bunge hilo leo 5 Septemba, 2014 mjini Dodoma.


  0 0

  Kamanda wa Polisi  Kanda Maalum ya Dar es salaam,Kamishna Suleiman Kova (wa nne kutoka kushoto) amewataka askari wote  wa Kanda hiyo  kufanya kazi kwa weledi, kuzingatia haki za binadamu, na kufuata maadili ya  kazi katika utendaji wao wa kila siku.

  Kamishna Kova ameyasema hayo mwanzoni mwa wiki hii wakati akiongea na Maafisa na Wakaguzi wa Polisi katika kikao cha utendaji kilichofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, Kinondoni, jijini Dar es Salaam na kusisitiza  umuhimu wa kutoa huduma bora kwa wateja kulingana na matarajio ya wananchi.

  Aidha  Kamishna Kova amesisitiza usiri katika Taarifa zinazoletwa au zinazotolewa na wananchi na kwamba kwa kufanya hivyo  kutalifanya Jeshi la Polisi kuaminika kwa wananchi. Akizungumzia suala la rushwa, Kamishina Kova amewaasa askari kutojihusiasha  na kupokea rushwa kwani ni adui wa haki na kinyume na maadili ya kazi za Polisi.

  Amehimiza ushirikishwaji wa wananchi katika kila hatua hasa katika mashauri mbalimbali ya kesi zao na kutenda kazi kwa uwazi hasa wakati wananchi wanapotakiwa kupata taarifa za mashauri yao au wanapoomba ushauri katika kero zinazowasibu.

  Kila Afisa, Mkaguzi na askari lazima afanye kazi kwa bidii na ukakamavu ili mchango wa Jeshi la Polisi uonekane wazi kwa jamii ya watanzania na wageni wanaoingia na kutoka nchini pia wale wanaoishi nchini.


  0 0

  Bunge La Afrika Mashariki Lilifikia Tamati Katika Vikao Vyake Vya Dar Es Salaam Kwa Kuahirishwa Kabla Ya Muda Wake Kutokana Na Akidi Kutotimia kufuatia Wabunge wa Burundi na Rwanda kutoka nje na Wengine Kutokuwepo.
   Sheria Inataka Ili Kikao Kiendelee Lazima Bungeni Kuwe Na Nusu Ya Wabunge Wa Kuchaguliwa Na Angalau Wabunge Watatu Kutoka Kila Nchi Mwananchama. 
  Kikao Kiliahirishwa Baada Ya Rwanda Kuwa Na Mbunge Mmoja Na Burundi Wawili. Hii Ilikua Mara Ya Pili Baada Bunge Hilo Kuahirishwa Kwa sababu Kama Hizo Wiki Iliyopita. 
  Akizungumza Baada Ya Kuahirishwa Kwa Bunge Hilo Naibu Waziri Wa Afrika Mashariki Dkt Abdulla Juma Saadalla Alisema Serikali Imesikitishwa Na Vitendo Hivyo Vya Wabunge Kwakua Wanatumia Kodi Kubwa Ya Wananchi Wa Afrika Mashariki. 
  Bunge Hilo Lilianza Agosti 25 Na Lilitarajiwa Kuahirishwa Jioni Lakini Liliahirishwa Mchana.
  Spika wa Bunge la Afrika Mashariki akiahirisha kikao cha Bunge hilo baada ya Akidi kutotimia kufuatia Wabunge wa Rwanda na Burundi kutoka nje na wengine kutokuwepo kabisa katika siku ya mwisho wa bunge hilo Ukumbi wa Karimjee Dar-es-Salaam Septemba 4, 2014.
  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt Richard Sezibera akijibu hoja zilizoulizwa na Wabunge wakati wa kikao cha Bunge hilo Karimjee Dar-es-Salaam Septemba 4, 2014 kabla hakijaahirishwa kufuatia Wabunge wa Rwanda na Burundi kutotimiza akidi.
  Naibu waziri wa Wizara ya Afrika Mashariki Mh. Abdulla Juma Saadalla akijibu hoja wakati kikao cha Bunge la Afrika Mashariki Ukumbi wa Karimjee Dar-es-Salaam Septemba 4, 2014 kabla hakijaahirishwa.
  Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakifuatilia mjadala uliokuwa ukiendelea Bungeni katika Ukumbi wa Karimjee Dar-es-Salaam Septemba 4, 2014 kabla Bunge hilo kuahirishwa kutokana na Akidi kutotimua kufuatia Wabunge wa Rwanda na Burundi kutoka nje na wengine kutokuwepo kabisa.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Afrika Mashariki akiongea na Waandishi wa Habari baada ya kikao cha Bunge la Afrika Mashariki Ukumbi wa Karimjee Dar-es-Salaam, Septemba 4, 2014.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua mkutano wa wadau wa mifugo kwenye ukumbi wa hoteli ya Malaika jijini Mwanza Septemba 5, 2014.

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jacqueline Liana (kushoto) baada ya kufungua mkutano wa wadau wa sekta ya mifugo kwenye ukumbi wa hoteli ya Malaika jijini Mwanza, Septemba 5, 2014. Kulia ni mfugaji na Mkulima kutoka Kiteto. Papian Emmanuel.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Kaimu Mkuu wa Mwanza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Paschal Mabiti kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya kufungua mkutano wa wadau wa mifugo kwenye ukumbi wa hoteli ya Malaika jijini Mwanza, Septemba 5, 2014. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameitaka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kufanya upya sensa ya mifugo kwani ya mwisho ilifanyika miaka 30 iliyopita.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Septemba 5, 2014) wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa wadau wa mifugo hapa nchini ulioanza leo kwenye hoteli ya Malaika jijini Mwanza.

  Waziri Mkuu amesema ni vigumu kwa wafugaji kutaja idadi halisi ya mifugo waliyonayo lakini kama Wizara hawana budi kuweka mbinu za kisasa za kufanya sensa hiyo hata kama itawachukua miaka miwili.

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

  Want to make a real difference in the lives of women in Tanzania? Join us on 13th Sept, 2014 at KINUvation in Dar es salaam for the first fistula brainstorming hack.
  Not a programmer or developer- so what? We want anyone who is willing to share their skills to build a solution for women suffering from fistula.
  It's simple to get involved!
  1. Create your own sign using the ‪#‎tokomezafistula‬ tag (like me!)
  2. Take a photo holding your sign
  3. Post the photos on all your social networks with the hastag #tokomezafistula with these instructions and nominate your friends to do the same!
  4. Be at Kinu on the 13th September at 9am for the first brainstorming hackathon session http://goo.gl/a8oS3W
  5. Please check in, and help us keep track of the skill sets being represented, if you are down to participate: http://goo.gl/TlbKgr
  Where shall you be on Sept 13th?

  0 0

   Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara likiwa limeharibika vibaya baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika eneo la SabaSaba,Mjini Musoma mchana huu.

  Watu zaidi ya 35 wamepoteza maisha papo hapo na wengine zaidi ya 86 kujeruhiwa vibaya. Kwa mujibu wa Ripota wetu aliopo eneo la tukio hivi sasa,inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo Basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo,kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi,liliisukuma ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni.

  Hali iliyoipelekea basi hilo kuamini kuwa itawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo.Ndani ya gari hiyo ndogo kulikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa.Picha na Ahmad Michuzi,Musoma.
  Basi la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS.
  Umati wa Watu ukiwa umekusanyika kwenye eneo hilo ilikotokea ajali hiyo mbaya na kusababisha watu 35 kupoteza maisha hapo hapo,wakishuhudia tukio hilo la ajali.


  Buldoza likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK lililoshukumwa na basi hilo mpaka kuingia mtoni.Gari hii ilikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa.

  Sehemu ya waokoaji waliofika kwenye tukio hilo.
  Wanausalama wakijadiliana jambo kwenye eneo hilo la tukio.

  Baadhi ya Mizigo ya abiria wa mabasi hayo wakiwepo waliopoteza maisha.
  Uokoaji ukiendelea.
  Askari Polisi wakitoa miili ya watu wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo.


  0 0


   Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,pichani wa tatu shoto Ruge Mutahaba akiwa sambamba na baadhi ya wasanii waliokuwa wakitarajiwa kutumbuiza leo usiku mjini Musoma kwenye tamasha la Fiesta,lakini hata hivyo Uongozi wa Clouds Media Group,Prime Time Promotions ambao ndio waandaaji pamoja na Wadhamini wa tamasha hilo kwa pamoja wamekubaliana kuaihirisha onyesho hilo mpaka hapo baadae itakapotangazwa tena.

  Kuaihirishwa huko kunafuatia ajali mbaya na ya aina yake iliyopelekea simanzi na majonzi makubwa wakazi wa mji wa Musoma na vitongoji vyake.Waandaji wa tamasha hilo pamoja na Wasanii pia walipeleka vifaa mbalimbali kwa ajili ya kutoa huduma ya awali kwa majeruhi mbalimbali waliopatwa na ajali hiyo,Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara.
  Mtangazaji wa Clouds FM,Adam Mchomvu sambamba na Msanii wa muziki wa kizazi kipya ajulikanae kwa jina la kisanii Shilole sambamba na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba wakikabidhi vifaa tiba mbalimbali kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma ya awali kwa majeruhi mbalimbali waliopatwa na ajali hiyo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk.Samsoni Winani.
   Mganga Mkuu wa mkoa wa Mara,Dk.Samsoni Winani akifafanua jambo kufuatia ajali mbaya ya mabasi mawili, Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika kijiji cha SabaSaba,nje kidogo ya mji wa  Musoma mchana huu.Ambapo DK Samsoni alisema kuwa ajali hiyo ni aina yake na haijawahi tokea tangu ajali ya aina hiyo ilivyotokea mnamo mwaka 1996.
   Mkuu wa Wilaya ya Busega Paul Mzindakaya akimpa pole Mganga Mkuu wa mkoa wa Mara,Dk.Samsoni Winani kufuatia ajali mbaya ya mabasi mawili, Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika katika kijiji cha eneo la SabaSaba,nje kidogo ya mji wa  Musoma mchana huu.

  0 0


  0 0

  Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia madhara ya mapigo ya silaha mbalimbali wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014.
  Sehemu ya askari wakitoka katika mapambano wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014.
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na viongozi wengine wakisimama kwa wimbo wa Taifa wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014.
  Askari wa kikosi cha mizinga akichukua taswira meza kuu wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014.
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na viongozi wengine wakipata picha ya kumbukumbu na sehemu ya wapiganaji wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014.
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapongeza askari wanawake walioshiriki katika mapambano wakati wa ufungaji wa zoezi la medani la maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Monduli, Arusha, leo Septemba 5, 2014. PICHA NA IKULU
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Badhi ya Taswira za Zoezi la Medani la Operesheni Maliza Matata ambalo limeshirikisha mamia ya wapiganaji na maofisa  ambako zimetumika silaha za moto kwa njia ya ndege za kivita, vifaru, makombora na risasi  kwenye Sherehe za Miaka 50 ya JWTZ  kwenye eneo la Langururusu, Wilaya ya Monduli, Mkoa wa Arusha   Madhara ya shambulio hilo la mazoezi 
  Kabaaaaang!

  0 0
 • 09/05/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Billy Ocean - "Caribbean Queen"

  0 0

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza wakati wa chakula cha jioni cha kampeni za kupambana na utumikishwaji wa mtoto hapa Tanzania kilichoandaliwa na International Rescue Committee kwenye Hoteli ya Serena tarehe 5.9.2014.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi kampeni ya kadi nyekundu katika kupambana na utumikishwaji wa mtoto hapa Tanzania wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na International Rescue Committee katika Hoteli ya Serena tarehe 5.9.2014.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na aliyekuwa Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Dkt Augustine Mahiga wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na International Rescue Committee kwenye hoteli ya Serena tarehe 5.9.2014 kwa ajili ya kuhamasisha mapambano dhidi ya utumikishwaji wa watoto hapa nchini.
  Mtoto Hamadi Hatibu, 13, anayesoma darasa la pili katika Shule ya Msingi ya Sahare katika Manispaa ya Tanga akitoa ushuhuda wake jinsi alivyoishi kwa kuvua samaki katika umri wake mdogo.
  Baadhi ya wageni waalikwa walioshiriki katika hafla hiyo.
older | 1 | .... | 561 | 562 | (Page 563) | 564 | 565 | .... | 3285 | newer