Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 556 | 557 | (Page 558) | 559 | 560 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Bw Johnson Lukaza akitoa neno kwa wadau waliojitokeza kushuhudia fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) lililokuwa pia likirushwa live kupitia Kituo Cha Runinga cha ITV
  Mwanaafa Mwinzago (katikati) akishangilia Mara baada ya kutangazwa Mshindi wa Kitita Cha Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Kumsaka Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mlimani City na Kuhudhuriwa na Mamia ya Watanzania.
  Mwanaafa Mwinzago (katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na wazazi wake na timu ya wafanyakazi wa TMT na washiriki wenzie mara baada ya kukabidhiwa mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni 50 za Kitanzania Mara baada ya Kuwabwaga Washiriki wenzie tisa na Kuibuka Mshindi wa Kitita Cha Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Kusaka Vipaji Vya Kuigiza Nchini lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambalo limefikia Ukingoni Jana Katika Ukumbi wa Mlimani City.


  0 0

   Wananchi wa Mwanagati-Kitunda jijini Dar es Salaam  na maeneo jirani wamelilalamikia shirika la TANESCO  kwa kukatiwa umeme kwa siku tatu mfululizo,bila taarifa yoyote kutolewa kwa wakazi hao.''hatuna umeme kwa siku 3 mfululizo usiku na mchana mpaka sasa na hakuna taarifa zozote toka shirika la umeme Tanesco kuelezea hali hii inayoendelea mpaka sasa'',alilalama mmoja wa wakazi  wa eneo hilo.

  Wakielezea kwa masikitiko makubwa juu ya tatizo hilo,Wananchi hao wamesema kuwa hawakupata taarifa yoyote ile toka Tanesco, na mpaka sasa wengi wao wamepata hasara kubwa kibiashara kutokana na tatizo hilo la kukosekana kwa umeme.

  Mbali na matatizo hayo, Mji huo mpya ambao una chanzo chao cha kipekee kikubwa cha maji,kinachotegemea umeme katika uzalishaji wa maji na kufanya wananchi hao kukosa maji pia kwa siku 3 mfululizo na kufanya maisha yao kuwa magumu zaidi.

  Tunaliomba shirika la TANESCO lisikilize kilio chetu haraka iwezekanavyo,na kuhakikisha tatizo la umeme linatatuliwa kwa wakati ili kutuepusha na adha tunayoipata sisi wakazi wa Managati-Kitunda


  Juhudi za kuweza kuwapata wahusika toka shirika la umeme Tanesco ili kuelezea tatizo ili kwa wananchi wa Mwanagati - Kitunda zilishindikana mpaka tunapotoa habari hii.

  0 0

  Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG), Mhe. Anna Abdallah akifungua Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
  Katibu wa Umoja wa Wanawake Wabunge Tanzania (TWPG), Mhe. Angellah Kairuki (MB) akizungumzia masuala mbalimbali ya kijinsia katika Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Bi. Usu Mallya akitoa mada kuhusiana na suala la kijinsia katika Katiba, wakati wa Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Profesa Ruth Meena akitoa mada juu ya masuala muhimu ya Jinsia ya kuzingatiwa katika Katiba Mpya wakati wa Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Bi. Stella Gailos akitoa mada akitoa mada juu ya masuala muhimu ya Jinsia ya kuzingatiwa katika Katiba Mpya wakati wa Semina iliyoandaliwa na Umoja huo kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwaajili ya Wajumbe wa Bunge Maalum kuhusu masuala ya Jinsia na Katiba iliyofanyika leo 30 Agosti, 2014 kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.


  0 0


  0 0


  0 0

  Muonekano wa Soko jipya la Mazao la Matombo lilinozinduliwa hivi karibuni na Mh. Rais Jakata Kikwete.

   Muonekano wa Soko la zamani.

  PICHA NA JOHN NDITI.

  0 0


  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akionyesha mashine ya kisasa aina ya LG iliyokamatwa kutoka kwa watuhumiwa wa kurudufu kazi za wasanii (CD FEKI) katika maeneo ya Kariakoo na Kimarta Bonyokwa jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akionesha mashine ya kisasa aina ya LG waliyokamatwa nayo watuhumiwa wa kurudufu CD feki za kazi za wasanii katika maeneo ya Kariakoo na Kimara Bonyokwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP, Denis Moyo. (Picha na Francis Dande)  

  Msama akionyesha wino na vifaa vingine vinavyotumika katika kutengeneza CD feki za kazi za wasanii.
  Msama akionesha mashine ya kuprint Cover za CD.
  CD feki zilizokamatwa katika maeneo ya Kariakoo.
  Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   SIMBA SC imewafunga mabingwa wa Zanzibar, KMKM mabao 5-0 katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  KMKM inayofundishwa na Ally Bushiri ‘Bush’ ambayo Jumatano wiki hii ilifungwa 2-0 na Yanga SC, leo iligeuzwa asusa na Wekundu wa Msimbazi.

  Simba SC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza mabao 4-0, yaliyotiwa kimiani na Amisi Tambwe mawili, Amri Kiemba na Shaaban Kisiga ‘Malone’ moja kila mmoja.

  Amri Kiemba ndiye aliyefungua karamu ya mabao ya Simba SC hii leo, dakika ya tatu ya mchezo baada ya kupewa pasi nzuri na kiungo Mrundi, Pierre Kwizera na kuwatoka wachezaji wawili wa KMKM kabla ya kufumua shuti kali lililogonga mwamba wa ndani wa lango.
  Amisi Tambwe akafuatia dakika ya 14 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Salim Amour kufuatia yeye mwenyewe kupiga mkwaju wa penalti, baada ya kiungo, Haroun Chanongo kuangushwa kwenye boksi.
  Tambwe tena akafunga bao la tatu dakika ya 23 akimalizia krosi maridadi ya Ramadhani Singano ‘Messi’ kabla ya Kisiga kufunga la nne dakika ya 37, kufuatia kazi nzuri ya Kiemba.
  Kipindi  ha pili, kocha Mzambia, Patrick Phiri alibadilisha kikosi kizima akimuacha Nahodha Jopseph Owino pekee na dakika ya 60 Elias Maguri akahitimisha karamu ya mabao kwa bao safi la tano.
  Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi aliyetangaza juzi kurejea Simba SC kutoka kwa mahasimu, Yanga SC usiku huu alikuwepo, lakini alibaki benchi muda wote wa mchezo.
  Beki wa Simba SC, Issa Rashid 'Baba Ubaya' akimtoka mchezaji wa KMKM

  Wazito; Kutoka kulia Musley Ruwey, Hans Poppe na Salim Abdallah 'Try Again'


  Okwi katikati akiwa na Mosoti kulia na Butoyi kushoto

  Amisi Tambwe na Ramadhano Singano 'Messi' kulia wakishangilia usiku huu uwanja wa Amaan

  0 0


   Bw. Rished BADE, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akiongea na wanahabari. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kamishna wa Polisi, Afande Isaya Mngulu, na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Bw. Richard Kayombo

  0 0

   Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai akisalimiana  na  Dkt. Jabiri Bakari, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa e-Government pamoja na ujumbe wake wakitokea New Delhi ambako walikuwa na mkutano na Wakala wenzao wa Serikali ya India.Katika mazungumzo yao, wamezungumzia jinsi ya kupata ufadhili kwa ajili ya kujenga uwezo wa Wakala wa Serikali kwa njia ya Mtandao(e- Government)
   Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai akiongea  na  Dkt. Jabiri Bakari, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa e-Government pamoja na ujumbe wake 
   Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai akipata picha ya kumbukumbu  na  Dkt. Jabiri Bakari, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa e-Government pamoja na ujumbe wake 

  0 0

  The tobacco buying season which began in Tanzania during May 2014, resulted in Alliance One Tobacco Tanzania Limited (AOTTL) purchasing 28 million kgs of Flue Cured Tobacco by third week of August 2014. 
  The Flue cured tobacco (FCV) was valued at 61.7million USD (Tshs 101.805 Billion) at an average price of 2.20 USD per kilo. Dark Fire cured tobacco (DFC) purchases stood at 0. 225 million Kgs valued at 0.278 million USD (Tshs 458.7 million) at an average price of 1.23 USD per kg. 
   AOTTL buys tobacco from 182 contracted Primary Societies with over 35,000 farmer members. 
   “The targets set at the beginning of the season stand at 35 million Kgs of Flue Cured Tobacco and 0.5 million kgs of Dark Fired Tobacco,” said AOTTL MD Mark Mason, from Morogoro on Friday. 
  “At present the bought tobacco is at 80% of the target for FCV. I am happy to report that analyzing the current buying trends it is likely that the targets will be met by the end of the buying season in October 2014 and quality has been as expected,” concluded Mason. 
  Purchased tobacco is transported to Alliance One factory in Morogoro for processing and selling to domestic and export customers. Purchases amounting to 15.177 million kgs of tobacco have already been received at the factory. 
  The processing stage for the tobacco began in June 2014, and is scheduled to go up to December 2014. AOTTL’s 50 Million USD factory employs 300 permanent staff and provides jobs for over 2000 seasonal employees at the peak of the season. 
   Tanzania Tobacco Board (TTB), the regulatory authority of the Tobacco industry in Tanzania, estimates total production in the country this season to be 104 million kgs of Flue cured tobacco valued at 219 million USD (Tshs 362 Billion) at an estimated average price of USD 2.11 per kg and 1.074 million kgs of Dark Fired Tobacco valued at 1.6 million USD (Tshs 2.640 Billion) at an average price of 1.48 USD per kg. 
  Tobacco is the leading foreign exchange earner among Tanzania’s traditional export crops earning the Country more than 300 million USD annually. 
  Alliance One Tobacco Tanzania Ltd (AOTTL) with its headquarters in Morogoro municipality at Kingolwira township is a subsidiary company of Alliance One International (AOI) of the USA, with its headquarters in North Carolina.
   It is one of the three tobacco buying companies in Tanzania buying more than 35 million kgs of tobacco from 182 Primary Cooperative Societies with more than 39,800 farmers in Tabora, Urambo, Kahama, Manyoni, Iringa, Kasulu, Songea and Mara.
  AOTTL Managing Director Mr.  Mark Mason
  Part of the 28 million kgs of Flue Cured Tobacco in Mororogo

  0 0

  Mshindi wa Miss Lake Zone 2014 Rachael Clavery (katikati) akila pozi katika picha ya ukumbusho na mshindi wa pili Mary Emanuel( kulia) na Mshindi wa tatu Nikole Sarakikya ( kushoto). Rachael amejinyakulia zawadi nono ya Gari la millioni 10 katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza usiku huu. Shindano hilo lilikuwa na Walimbwende 18 wote wakichuana vikali na kila mmoja akitaka ashinde kabla ya Rachael Clavery kuwafunika wenzake na kuibuka na ushindi. 
  Gari aliloshinda Miss Lake Zone 2014 Rachael Clavery usiku huu.  0 0

   Waziri wa Maliasili na Utalii Razaro Nyarandu (katikati mbele) akiwa na wahadhiri na wahitimu katika mahafali ya 3 ya Chuo cha Mafunzo ya Nyuki yaliyofanyika mjini Tabora chuoni hapo.
  Na Allan Ntana, Tabora
  SERIKALI imeahidi kupandisha hadhi ya Chuo cha Mafunzo ya Nyuki kilichoko mkoani Tabora ili kuwavutia wanafunzi wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi kujiunga na chuo hicho. Hayo yalibainishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Razaro Nyarandu aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 3 ya Chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo.

  Alisema kutokana na umuhimu wa Chuo hicho atahakikisha kinaboreshwa zaidi ili kiwe kitovu cha ubora katika taaluma ya sayansi ya misitu na nyuki na hifadhi zake na kwa kuanzia ameahidi kuwasiliana na wataalamu wa wizara hiyo ili wahuishe mitaala yake ili kukiongezea hadhi.
  ‘Tunataka chuo hiki kiwe kimbilio la wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini na hata nje ya nchi, tutakiboresha zaidi ili kiwe kitovu cha ubora katika sayansi ya misitu na nyuki’, alisema Waziri Nyarandu.
  Aliongeza kuwa Wizara yake itajitahidi kuzishughulikia changamoto zote zinazokikabili ikiwemo suala la upungufu wa watumishi ili kuhakikisha chuo hicho na sekta zingine zilizoko ndani ya Wizara hiyo zinakuwa na watumishi wa kutosha sambamba na kutoa fursa za ajira kwa askari wa wanyama pori na wataalamu wengineo.
  Lengo ni kuhakikisha ulinzi wa kutosha unakuwepo katika maeneo yote ya hifadhi za misitu sambamba na kuwezesha shughuli zingine zote ziendelee vizuri katika maeneo hayo ikiwemo ufugaji nyuki.
  Awali akisoma risala ya Chuo mbele ya Waziri, Mkuu wa Chuo hicho Semu L. Daud alisema tangu Mafunzo ya Chuo hicho yarudishwe rasmi mkoani Tabora chuo hicho kimeanza kupata mafanikio makubwa ikiwemo kuongeza udahili wa wanafunzi  kutoka 34 kwa mwaka 2010/2011 hadi 115 kwa mwaka 2014/15, huku akibainisha kuwa wanafunzi 58 wa kike na kiume kwa mwaka 2013/14 wamehitimu mafunzo hayo katika ngazi ya Astashahada na Stashahada ya Ufugaji Nyuki .

  Alitaja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na Chuo kupata utambulisho maalumu toka Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) wa Ithibati ya muda (Partial Accreditation), ili kuthibitisha umuhimu wa taaluma inayofundishwa na Chuo hicho wamepewa fursa ya kushiriki katika Maonyesho ya Biashara na Kilimo (Sabasaba na NaneNane) kuanzia mwaka 2009 mpaka sasa ili kuelimisha wananchi.
  Aidha Mkuu wa Chuo alitaja changamoto mbalimbali zinazokikabili chuo hicho kuwa pamoja na upungufu wa watumishi wasio wakufunzi hususani Afisa Utumishi, Wakutubi, Wapishi, Madereva, Afisa Ugavi, walinzi na mwangalizi wa masijala.
  Changamoto nyingine ni tatizo la uhaba wa vifaa vya kisasa vya kufundishia ikiwemo vitabu na chombo cha usafiri hasa kwa shughuli za utawala na shughuli za mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi.
  Aidha alibainisha kuwa hadhi ya Chuo hicho itaongezeka pale tu mikakati yote ya kukipanua na kukiboresha itakapotekelezwa ipasavyo hivyo akaiomba serikali kupitia Waziri mwenye dhamana kuangalia uwezekano wa kuongeza fungu la bajeti ya Chuo hicho ili jitihada za kuboresha miundombinu hiyo zianze mra moja.

  0 0

   Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kulia) akikabidhi kitabu cha mpango mkakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe Ahmed Chipozi jana wilayani Bagamoyo wakati wa ziara ya Wabunge wa Afrika Mashariki katika taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa). Anayeshuhudia katikati ni Waziriwa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB).

   Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kushoto)  na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB).wakiwa na baadhi ya Wabunge wa Afrika Mashariki wakipata maelezo kuhusu muelekeo na malengo ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa)  kutoka Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Bw. Michael Kadinde jana wakati wa ziara ya wabunge hao.
   Kikundi cha Sanaa kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa)wakifanaya sanaa za maonyesho kwa mchezo aina ya Akrobati mbele ya wageni ambao ni wabunge wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Margareth Zziwa (Hawapo picha) walipotembelea taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.
   Kikundi cha Sanaa kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa)wakichezo ngoma yenye asili ya kabila la Kisukuma ijulikanayo kama Gobogobo mbele ya wageni ambao ni wabunge wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Margareth Zziwa (Hawapo picha) walipotembelea taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Mhe John Cheyo (kushoto) akiongea na Makamu Mwenyekiti wa TCD Mhe Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. ABdulrahman Kinana na Mhe Isack Cheyo walipowasili Ikulu ndogo mjini Dodoma kukutana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo. Nyuma yao ni Mwenyekiti wa TLP Mhe Augustine Lyatonga Mrema na Mwenyekiti wa UPDP Mhe Fahmi Dovutwa leo.TCD inaundwa na vyama vyenye uwakilishi bungeni, ambavyo ni CCM, CUF, CHADEMA, TLP, NCCR-Mageuzi na UDP.
  Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI Mhe Joseph Mbatia, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt Wilbroad Slaa wakiwasili Ikulu Ndogo mjini Dodoma leo

  Rais Kikwete akizungumza  na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania alipokutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
   Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania baada ya kukutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
   Rais Kikwete akiagana na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania baada ya kukutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
   Rais Kikwete akiagana nna wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania baada ya kukutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Travelport Tanzania,Eliasaph Mathew akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfumo (System) mpya wa uuzaji wa tiketi za ndege uitwao Precise Sky utakaotumiwa na Mawakala wa Uuzaji wa tiketi za ndege nchini (Travel Agents)  uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Tower, jijini Dar es salaam.
  Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Mfumo (System) mpya wa uuzaji wa tiketi za ndege uitwao Precise Sky,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA),Charles Chacha akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua ramsi mfumo huo katika ukumbi wa Golden Jubilee Tower, jijini Dar es salaam.
  Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Mfumo (System) mpya wa uuzaji wa tiketi za ndege uitwao Precise Sky,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA),Charles Chacha akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa mfumo huo mpya utakaotumiwa na Mawakala wa Uuzaji wa tiketi za ndege nchini (Travel Agents)  uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Tower, jijini Dar es salaam.
  Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Mfumo (System) mpya wa uuzaji wa tiketi za ndege uitwao Precise Sky,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA),Charles Chacha (wa pili kushoto) akifurahi pamoja na Mwenyekiti wa TASOTA,Moustafa Khataw (kushoto),Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Travelport Tanzania,Eliasaph Mathew (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Zamani wa Galileo Tanzania,Mwalim Ally wakati wa kupongezana baada ya kuzindua mfumo huo mpya.
  Meneja wa Mfumo (System) mpya wa uuzaji wa tiketi za ndege kutoka Kampuni ya Travelpotr,Gloria Urassa akiwasilisha mada ya namna kutumia huduma hiyo itakayotumiwa na Mawakala wa Uuzaji wa tiketi za ndege nchini (Travel Agents) wakati wa hafla uzinduzi wake uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Golden Jubilee Tower, jijini Dar es salaam.
  Meneja wa Ufundi kwa Kampuni ya Travelport Tanzania,Julius Haule akitoa maelezo ya namna mfumo huo wa Pricese Sky unavyoweza kuwarahisishia Mawakala wa kuuza tiketi za ndege kuuza tiketi hizo za mashirika yote ya ndege ya ndani ya nchi ambazo hapo awali zilikuwa hazitumii mfumo huo.
  Mwenyekiti wa TASOTA,Moustafa Khataw akizungumza machache ikiwa ni pamoja na kutoa shukrani kwa niaba ya mawakala wa tiketi za ndege nchini kwa kufanikishiwa mfumo huo.


  0 0

  Meneja Usimamizi, Undeshaji na Mazingira toka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaama (DAWASA), Bi.Modesta Mushi akiwaneosha Wajumbe wa Bodi ya Wakurungenzi wa mamlaka hiyo ramani ya Ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Kidunda lenye ujazo wa Mita milioni 190, Agosti 29, 2014 wakati wa ziara ya Bodi hiyo katika eneo la Mradi Mkoani Morogoro.
  Mkuu wa Timu ya Ulipaji fidia kwa Wakazi walio katika Eneo la Mradi, Mhandisi. John Kirecha akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurungenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), kuhusiana kukamilika kwa taratibu za ulipaji fidia kwa wakazi waliopisha ujenzi wa mradi wa bwawa la Kidunda litakaloweza kutoa huduma kwa mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro, wakati wa Ziara ya hiyo.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Bw. Archard Mtalemwa akisisitiza jambo.
  Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Alhaji Said El-Maamry (kulia), akimuuliza swali Mhandisi. John Kirecha kuhusiana fidia kwa Wakazi walio katika Eneo la Mradi huo, likiwemo kuhakikisha taratibu hizo haziathiri maendeleo ya ujenzi wa huo.
  Mkuu wa Timu ya Ulipaji fidia kwa Wakazi walio katika Eneo la Mradi, Mhandisi. John Kirecha akitoa maelezo kuhusiana na taratibu za ulipaji fidia kwa wananchi hao.


  0 0

  Jaji Constancia Gabusa (wa sita kutoka kushoto) akizungumza na mtoto Abdalah Suleman (kulia) aliyefika kisimani kuchota maji katika kijiji cha Chanjagaa wilayani Same. Mradi wa kisima hicho unafadhiliwa na kampuni ya uchimbaji wa madini aina ya bauxite ya Willy Enterprises Ltd.
  Muuguzi wa zahanati ya Mteke iliyopo wilayani Same Bi. Winfrida Momoya (kulia) akizungumza na majaji Bw. Venance Bahati ( wa pili kutoka kushoto) na Bi Constancia Gabusa (wa tatu kutoka kushoto) mara walipotembelea zahanati hiyo inayofadhiliwa na kampuni ya uchimbaji wa madini aina ya bauxite ya Willy Enterprises Ltd.
  Mkurugenzi wa mgodi wa madini ya vito wa TanzaniteOne Bw. Farai Manyemba akielezea mchango wa kampuni hiyo katika huduma za jamii mara timu ya majaji na sekretarieti ilipofanya ziara kwenye mgodi huo.
  Timu ya majaji na sekretarieti ikiangalia bidhaa za urembo zinazotengenezwa na kikundi cha wakinamama wa kimasai cha Ebeneza mara walipotembelea kikundi hicho huko Mirerani. Kikundi hicho kinafadhiliwa na kampuni ya TanzaniteOne ikiwa ni pamoja na kutangaza bidhaa zake nchini Marekani.
  Jaji Constancia Gabusa (kushoto) akioneshwa urembo na kupewa maelezo na mama wa kimasai ambaye jina lake halikupatikana mara moja juu ya shughuli zinazofanywa na kikundi cha wakinamama wa kimasai cha Ebeneza kinachofadhiliwa na kampuni ya TanzaniteOne.
  Mkazi wa kijiji cha Kolila, King’ori Bw. Petro Losina akitoa maelezo kuhusu kisima cha maji kilichofadhiliwa na kampuni ya usagaji wa kokoto na utengenezaji wa matofali ya Arusha Aggregates Ltd. mbele ya majaji.

  0 0
 • 08/31/14--22:39: YALE YALEEEE......!!
 • Gari aina ya Landusider lenye nambari za usajili T540 APN lililokuwa likitokea Temeke kuelekea Tazara, Dar es salaam lilipinduka jana wakati dereva wa gari hilo alipokuwa akijaribu kulikwepa Lori lililokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara wakati akiwa kwenye mwendo kasi.Dereva huyo alikuwa akilikimbiza gari lingine aina ya Canter moja (namba zake za usajili hazikufahamika mara moja) lililokuwa likitokea Temeke nalo likiwa na mwendo kasi, na hata baada ya gari lake kupinduka dereva huyo alitoka upesi upesi bila kuijali afya yake na kisha kuchukua bodaboda na kuendelea kuifukuza ile Canter. Picha na Evance Ng'ingo wa Habari5blog
  Askari Polisi akijaribu kufanya mawasiliano na wenzake wakati wa ajali hiyo,huku mashuhuda wakiwa wamelizunguka gari hilo.


  0 0

  Stuttgart,Ujerumani,
  Usiku wa Jumamosi ya Tarehe  30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri
  Mwanamuziki nyota wa Bongo Flaver  Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,Ujerumani,baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show.

  Washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio waliahidiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijikuta wakisubiri hadi majira ya saa 10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake Mr.Awin Williams Akipomiemie raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.

  Hapo ndipo washabiki hao walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki  Diamond na promota wake,
  Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki
  ma-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa.

  Moja wa Djs hao alipoteza Lap top yake ,mwanadada DJ  Flor alipatwa shock mstuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo  DJ Drazee naye yupo hoi hospatal. 

  Polisi nchini Ujerumani wamesema tukio hili la aibu halijawahi kutokea,kwani msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari sana,kwani washabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.

  mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa
  wanachunguza thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.
  Hivi ndivyo ukumbi huo ulivyokuwqa baada ya tafrani hiyo.

  Magazeti ya Stuttgart; yameandika "Washabiki wana hasira nawe DIAMOND" link:


older | 1 | .... | 556 | 557 | (Page 558) | 559 | 560 | .... | 3348 | newer