Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 555 | 556 | (Page 557) | 558 | 559 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Kigoma, Josephat Komba akimuelezea Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene huduma mbalimbali zitolewazo na NSSF kwenye banda lao wakati wa maonesho ya wajasiriamali Kanda ya Kati.
   Banda la NSSF linavyooneka kwenye maonesho ya Wajasiriamali wa Kanda ya Kati yanayofanyika 
   Maofisa wa NSSF walioshiriki Kwenye Maonesho ya wajasiriamali kanda ya Kati wakiwa na Meneja wa 
  Daktari wa NSSF akimpima Shinikizo la Damu Afisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF ,Theopista Muheta wakati wa maonesho ya wajasiriamali kanda ya kati.
  Mmoja ya Washiriki wa Maonesho ya Wajasiliamali Kanda ya kati akipima uzito tayari kupewa Ushauri juu ya uwiano wa uzito wake na urefu (BMI) na Daktari wa NSSF.
   Wakazi wa Mkoa wa Kigoma wakipata maelekezo ya Mafao yatolewayo na NSSF kwa wanachama wa Hiari na wasio wa Hiari.


  0 0


   
  Meneja Usimamizi, Uendeshaji na Mazingira toka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Bi.Modesta Mushi akiwaonesha wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) ramani ya maeneo yatakayoguswa na Ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Kidunda lenye ujazo wa Mita milioni 190, wakati wa Ziara ya Bodi hiyo katika eneo la Mradi Mkoani Morogoro.
  Mkuu wa Msafara wa Timu ya Ulipaji fidia kwa Wakazi walio katika Eneo la Mradi Mhandisi John Kirecha akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) (Hawapo pichani)kuhusu kukamilika kwa taratibu za ulipaji fidia kwa wakazi waliopisha ujenzi wa mradi wa bwana la Kidunda litakaloweza kutoka huduma kwa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro, wakati wa Ziara ya Bodi hiyo katika eneo la Mradi Mkoani Morogoro.
  Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Alhaji Said El-Maamry akimueleza jambo Mkuu wa Msafara wa Timu ya Ulipaji fidia kwa Wakazi walio katika Eneo la Mradi Mhandisi John Kirecha ikiwemo kuhakikisha taratibu hizo haziathiri maendeleo ya ujenzi wa mradi huo,ikiwamo kuwataka wakazi wenye matatizo ya Mirathi kuyamaliza ndipo waweze kupatiwa fidia zao.

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Bw. Archard Mtalemwa (katikati mwenye shati jeupe)  akiwaonesha Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Ramani ya Viwanja 1000 vilivyopimwa  vya Makazi mapya eneo la Bwira juu kwa wakazi 2068 waliopisha Mradi wa  ujenzi wa Bwawa la Kidunda, wakati wa Ziara ya Bodi hiyo katika eneo la Mradi huo Mkoani Morogoro.
  Msimamizi wa  Kitengo cha Usimamizi na Upimaji Ramani wa Wilaya Mkoani Morogoro Bw. Kitomaga Francis(aliyevaa Kaunda suti)  akiwaeleza Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) mgawanyiko wa matumizi wa viwanja hivyo ikiwamo kwa ujenzi wa shule, makazi, Hospitali, Polisi, Ofisi na huduma nyingine muhimu za jamii, wakati wa Ziara ya Bodi hiyo katika eneo la Mradi huo Mkoani Morogoro.
  Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) wakiondoka eneo la Bwira Juu , eneo lililotegwa kwa ajili ya makazi mapya kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Kidunga, wakati wa Ziara ya Bodi hiyo katika eneo la Mradi huo Mkoani Morogoro. 

   (Picha na Hassan Silayo)

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakwanza kushoto  akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mbunge wa Mpwapwa Mheshimiwa Gregory Teu pamoja na Mbunge wa Kibakwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa George Simbachawene, akiweka jiwe la msingi kama ishara ya kuzindua rasmi ujenzi wa Daraja la Mto Gulwe lenye urefu wa mita 170 litakalo unganisha kati ya Wilaya ya Mpwapwa na Kibakwe.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglicana Tanzania Jacob Chimeleja, Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi, Mbunge wa Mpwapwa Mheshimiwa Gregory Teu, Mbunge wa Kibakwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa George Simbachawene pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe,  akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi ujenzi wa Daraja la Mto Gulwe lenye urefu wa mita 170.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wakiwa katika picha ya  pamoja na Mkandarasi,viongozi wa dini na kitaifa mara baada ya Rais kuzindua rasmi ujenzi wa daraja la Gulwe.
   Daraja la Gulwe linalotumika sasa kama linavyoonekana hali iliyopelekea Serikali ya awamu ya nne kupitia Wizara ya Ujenzi kuanza kujenga daraja kubwa na la kisasa la Gulwe litakalokuwa na mita 170 mara baada ya kukamilika kwake.

  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema tatizo la mabadilko ya tabianchi ni kubwa sana na kama hazitachukuliwa hatua stahiki Dunia itaisha.

  Ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Agosti 29, 2014) wakati akifungua mkutano wa pamoja wa Mawaziri wa Mambo ya Nje na Mazingira ambao ni wajumbe wa Kamati ya Wakuu wa Nchi Barani AfrikainayosimamiaMabadiliko ya Tabianchi (Committee of African Heads of States and Governments on Climate Change-CAHOSCC) wanaokutana kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

  Alisema tatizola mabadiliko ya tabianchi linachangiwa kwa kiasi kikubwa na hewa chafu ambayo inazalishwa viwandani kutokana na matumizi makubwaya nishati.

  "Kuna vyanzo vya nishati ambavyo si rafiki na kimojawapo ni makaa ya mawe. Ili uweze kupata nishati yakeni lazima uyaunguze nakwa kufanya hivyo unatoa hewa ukaa nyingi sana. Viko viwanda vinatumia mafuta mazito, vinginedizeli kwa wingi sana. Yote haya yanachangia hewa chafuambayo inafanya utando unaozuia hewa ya joto kurudi kwenye mfumo wa sayari na kutumika tena,"alisema.

  Akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari,  Waziri Mkuu alisema kiwango kikubwa cha hewa chafu inayozalishwa viwandani kutokanana matumizi ya nishati kinatoka nchi zilizoendelea wakati Bara la Afrika linazalisha asilimia tatu tu ya hewa hiyo.

  "Sisi Afrika tunapaswa tusifiwekwa kupunguza kasi ya ongezeko la jotoduniani.Nchi tajiri zinapaswa kutupongeza kwa sababu bado tuna misitu ambayo inasaidia kunyonya hiyo hewa chafu,"aliongeza.

  Waziri Mkuu alisema mkutano huo ni muhimu kwa sababu unaandaa kauli kwa ajili ya Wakuu wa Nchi watakayokwenda kuiwasilisha kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Kujadili masuala ya Tabianchi utakaofanyika New York, Marekani mwezi ujao.

  "Ninatumaini Mawaziri wote watatoka na kauli moja itayowawezesha Wakuu wa Nchi zetu waende na kauli moja. Natumaini watafanikiwa,"alisisitiza Waziri Mkuu.

  Akizungumza na washiriki wa mkutano huo kutoka nchi za Algeria,  Jamhuri ya Congo,  Misri, Kenya, Uganda,  Sudan,  Msumbiji, Ethiopia,  Ghana, Mauritania na wenyeji Tanzania,  Waziri Mkuu alisema suala la mabadiliko ya tabianchi yanaziathiri nchi zote duniani bila kujali kipato, umri, mahali nchi ilipo, matabakawala kazi za wananchi.

  "Nchi za Afrika ambazo kazi za uchumi wa wananchi wake zinategemea zaidi hali ya hewa, ndizo zinaathirika maradufu zikichangiwa zaidi na kukosekana kwa mbinu za kujihami pamoja na misingi dhaifu ya kiuchumi,"alisema.

  Alisema taarifa za hivi karibuni kutoka Intergovernmental Panel on ClimateChange zinaonyesha kwamba kiwango cha utoaji wa hewa chafu kila mwaka kimeongezeka kwa asilimia 2.2huku hewa chafu kutoka viwandani ikiongoza kwa kuchangia asilimia 80 ya hewa hiyo kwenye nchi zilizoendelea.

  Mapema, Kamishna wa Umoja wa Afrika anayesimamia Kilimo na Uchumi wa Vijijini, Bibi Rhoda Tumusiime alisema bara la Afrika linapaswa lijipange vizuri na kutoa matamko mazito kwenye mikutano ya kimataifa ili kukemea matumizi matumkzi makubwa ya nishati yanayochangia uharibifu wa mazingira.

  "Afrika lazima iendelee kutetea nafasi yake kwenye mikutano hii mikubwa. Lazima itoa kauli nzito kwani kuharibiwa kwa mazingira kunaathiri pia sektanyingine za utalii, maji, nishati na kadhalika,"alisema.

  0 0
 • 08/29/14--22:54: GADO LEO


 • 0 0

   

  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  ULAJI wa nyama nyekundu imeelezwa uchangia kwa kiasi kikubwa kupatwa na ugonjwa wa saratani ya matiti ambao umekuwa ni tishio duniani.

  Hayo yalibainishwa na Daktari  bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti Profesa Anthony Pais kutoka Bangarole India katika semina ya siku moja kwa madaktari wa Tanzania na wadau wa sekta ya afya iliyofanyika Dar es Salaam juzi.

  “Ulaji wa nyama nyekundu na vyakula vyenye mafuta unachangia kwa kiasi kikubwa kupata ugonjwa huo ambao umekuwa tishio duniani” alisema Pais.

  Profesa Pais alisema mfumo wa maisha wa kula vyakula bila mpangilio na kukosa kufanya mazoezi pia ni moja ya sababu inayoweza kumsabishia mtu kupata ugonjwa huo.

  “Ni muhimu kujenga tabia ya kufanya mazoezi walau kwa dakika 20 kila siku itasaidia kupunguza changamoto ya ugonjwa huo.
  Akizungumzia ugonjwa wa saratani ya matiti alisema hauwapati wanawake pekee bali na wanaume lakini kutokana na kukuwa kwa teknojia mpya wamekuwa wakiutibu bila ya kuliondoa titi lenye matatizo.

  Alisema hivi sasa dunia imekuwa ikitumia gharama kubwa kwa matibabu ya  ugonjwa wa saratani huku vikifunguliwa vituo vingi vya kutibu ugonjwa huo.

  Mkurugenzi Mtendaji  wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) , Dk.Malina  Njelekela alisema ni muhimu sasa kwa madaktari wa kitanzania kujifunza teknolojia hiyo ya upasuaji wa saratani ya matiti bila ya kuliondoa titi husika.

  Mshauri  wa Kimataifa wa Kujitegemea James Rugemalira ambaye amemleta Profesa huyo hapa nchini amesema baada ya kuona changamoto ya ugonjwa huo aliona ni vema kumleta mtalaamu huyo ili kuona namna ya kusaidia.

  Alisema profesa huyo pamoja na kutoa mafunzo hayo mafupi pia atapata fursa ya kutembelea mikoa kadhaa ya kanda ya kati ili kutoa uzoefu wake kuhusu ugonjwa huo.

  Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd ilidhamini semina hiyo iliyofanyika Hoteli nya Protea Courtyard kupitia vinywaji vyake vya Windhoek Draught na Windhoek Lager.
  Daktari bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti kutoka nchini India, Profesa Anthony Pais, akitoa mafunzo kuhusu ugonjwa huo kwa madaktari wa kitanzania na wadau mbaliombakli wa sekta ya afya. Semina hiyo ilifanyika Dar es Salaam jana, Hoteli ya Protea Courtyard Seaview.
  Profesa Anthony Pais (kushoto), akielezea jambo kuhusu ugonjwa huo.
  Mkurugenzi Mtendaji  wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) , Dk.Malina  Njelekela(kulia), akizungumza na wadau mbalimbali katika semina hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Benadicta Rugemalira, akizungumza katika semina hiyo. Kampuni hiyo ilidhamini semina hiyo.
  Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer wines and Spirits Limited, Benadicta Rugemalira.
  Profesa Pais (katikati), akiwa na wenyeji wake. Kutoka kulia ni Dk.Paul Mareale, James Rugemalira, Dk.Malina Njelekela na Benedicta Rugemalira.

  0 0


  0 0
 • 08/30/14--03:20: ufugaji wa kisasa


 • 0 0

  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mh. Samuel Sitta (kulia), akisisitiza jambo kwa wawakilishi wa mashirikisho ya sanaa mjini Dodoma hivi karibuni. Mashirikisho hayo yamekuwa yakipambana kufa na kupona kuhakikisha katiba mpya inatambue wasanii kama kundi maalum na pia ilinde mali zisizoshikika yaani miliki bunifu (intellectual property). Maoni ya mashirikisho hayo yalishatolewa katika hatua za awali za utoaji maoni na pia kupitia mabaraza lakini kwa bahati mbaya, hayakujumuishwa katika rasimu. Waliokaa kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania, Bw. John Kitime, Rais wa Shirikisho la Filamu, Bw. Simon Mwakifwamba na Makamu mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bi. Samia Suluhu Hassan.
  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mh. Samuel Sitta akikabidhiwa nyaraka yenye hoja ya uzengezi (lobbying) kutoka kwa kiongozi wa msafara wa mashirikisho ya sanaa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Bw. Simon Mwakifamba, mjini Dodoma hivi karibuni.
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati namba tano ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Assumpter Mshama, akishibishwa hoja za kina kwa nini wasanii wanataka katiba mpya itambue wasanii kuwa kundi maalum na pia ilinde mali isiyoshikika au kwa lugha nyepesi miliki bunifu (intellectual property) toka kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania, Bw. John Kitime, mjini Dodoma hivi karibuni.
  Baadhi ya wasanii waliotembelea Bunge Maalum la Katiba hivi karibuni wakifuatilia hoja zao.
  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mh. Samuel Sitta katika picha ya pamoja na wawakilishi wa mashirikisho ya sanaa nchini. Kulia kwake ni makamu wake Bi. Samia Suluhu Hassan.
  Mjumbe wa Kamati namba moja ambaye pia ni Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda (aliyetupia koti), akiteta jambo na baadhi ya wawakilishi wa mashirikisho ya sanaa za nchini waliokwenda Bungeni kufanya uzengezi (lobbying) hivi karibuni. Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Ummy Ally Mwalimu.
  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mh. Samuel Sitta (kulia) na nguli wa muziki nchini, Bw. Abdul Salvador, wanaonekana wamekumbuka enzi zileee. Walikutana katika viwanja vya Bunge maalum la Katiba mjini Dodoma hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania Bi. Stara Thomas na Mwakilishi wa Shirikisho la sanaa za ufundi na mchora vibonzo ITV, Bw. Nathan Mpangala.

  0 0
 • 08/30/14--05:45: KUMBUKUMBU

 • 1944 -  URSULA SABINUS KWEKA - 2014

  MAMA YETU, LEO UMETIMIZA MWEZI MMOJA TOKEA ULIPOITWA NA MUUMBA WETU HUKO JUU MBINGUNI. HATUNA SHAKA UKO NAYE KARIBU, NA IPO SIKU TUTAONANA TENA HUKO PARADISO.  UKWELI UA ZURI LIMERUDI KWENYE BUSTANI YA EDEN. 

  TUNAKUKUMBUKA SANA KWA MENGI, HASA UVUMILIVU ULIOKUWA NAO,  UKARIMU WAKO KWA WATU KATIKA SHIDA MBALIMBALI NA UPENDO, HAVITASAAULIKA MILELE. UKWELI  UMEACHA PENGO KUBWA KATIKA FAMILIA YA MAREHEMU MZEE SABINUS KWEKA,  TUMEBAKI WAKIWA MNO, LAKINI FARAJA TUZIPATAZO KWA WATU MBALIMBALI, ZINATUFUTA MACHOZI NA KUTUFANYA  TUSIWE NA HUZUNI SANA .
  UNAKUMBUKWA SANA NA MIMI MWANAO JANE, NA FAMILIA YOTE YA MZEE OTTO TINGO, KWA JINSI ULIVYOTUTUNUKU NA  KUKAA NASI KWA KIPINDI KINGI CHA UGONJWA WAKO HADI MAUTI ILIPOKUKUKUTA, WANAO WENGINE  WAPENDWA FESTO, EUGENIA, ELIZABETH, CECILIA NA THADEI AMBAO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE WALIKUUGUZA SANA KWA HALI NA MALI, WIFIYO  WA PEKEE SR. DEVOTHA KWEKA CDNK,  WAKWEZO DR. IBRAHIMU MSENGI, JOHN MUSHI, VALENTINA KINAWIRO, COSTANCIA MALLYA, FABIOLA FELICIAN, NA WOTE WA KWA TERRY, WAKE WENZIO  PAULINA, LAWRENCIA, NA MONICA, WAJUKUU WOTE NA WOTE WA UKOO WA KWEKA NA CHAMI  YA NARUMU POPOTE PALE WALIPO, NDUGU,  JAMAA  NA MARAFIKI WOTE POPOTE PALE WALIPO.

  RAHA YA MILELE UMPE Eee BWANA……………

  WAKASAIDIANA KILA MTU NA MWENZAKE. KILA MTU AKAMWAMBIA NDUGU YAKE, `UWE NA MOYO MKUU`
  ISAYA 41;6

  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA Zanzibar Bi Maryam Ahmed Omar akimkabidhi fomu Salum Mwalim fomu ya kugombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho kundi la Zanzibar katika hafla fupi iliyofanyika ofisi kuu za Chadema kisiwani humo.
  Mmoja wa wachama wa CHADEMA Zanzibar Bikwao Khamis akitia saini ya fomu ya udhamini wa Salum Mwalim (aliyesimama wa kwanza kushoto) anaegombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho kundi la Zanzibar. Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyo Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisi za Chadema Zanzibar
  Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Jumbe Idrisa akitia saini ya fomu ya udhamini wa Salum Mwalim (aliyesimama wa kwanza kushoto) anaegombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chjama hicho kundi la Zanzibar. Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyo Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisi za Chadema Zanzibar
  Salum Mwalim anaewania nafasi ya ujumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA kundi la Zanzibar akitia saini kitambu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi kuu za chama hicho Zanzibar kw alengo la kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimina na wachezaji wa timu ya mpira wa Miguu ya Jeshi la Uganda katika kilele cha michuano ya majeshi ya Nchi za Afrika ya Mashariki kwenye uwanja wa Amaan Zanzibar August 29, 2014.. Katika mechi ya kufunga mashindahayo Uganda na Tanzania zilitoka sare ya 1-1. Wapili kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema majeshi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hayana budi kuendeleza umoja na mshikamano ili kukuza udugu uliopo.

  Ametoa kauli hiyo jana usiku (Ijumaa, Agosti 29, 2014) wakati akifunga mashindano ya Michezo ya Majeshi ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye Uwanja wa Amaan, mjini Zanzibar.

  Waziri Mkuu ambaye kabla ya kuhutubia umati ulioshiriki hafla hiyo, alikabidhi kombe kwa washindi wa soka, ambao ni timu ya Jeshi la Ulinzi la Kenya, alisema amefarijika kwa jinsi alivyoshuhudia mechi kati ya Tanzania na Uganda ikichezwa kwa staha bila vurugu zozote. Katika mechi hiyo, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 na kuifanya Tanzania iibuke mshindi wa pili kwenye mchezo wa soka na Uganda kushika nafasi ya tatu.

  “Michezo siyo chuki bali hujenga uelewano na mshikamano. Ni fursa ya kujenga mahusiano ya baadaye kwani hakuna ajuaye, huenda tukawa na jeshi moja la Jumuiya huko mbele,” alisema.

  Alisema kutokana na ustadi ulioonyeshwa na wachezaji, wakuu wa majeshi waangalie uwezekano wa kutafuta mechi na jumuiya nyingine za Afrika Magharibi ama Afrika Kaskazini ili kujipima kwa kiwango kikubwa zaidi badala ya wao kwa wao. “Tujaribu kwenda nje ya Jumuiya yetu tukashindane nao kwa sababu nimeona uwezo mnao,” alisema.

  Katika mashindano hayo yaliyoanza Agosti 19, 2014, Kenya iliibuka mshindi katika soka, Tanzania iliibuka mshindi kwenye Netiboli, Uganda kwenye mpira wa vikapu na Kenya ikashinda tena kwenye mpira wa mikono. Katika riadha, Tanzania ilishinda upande wa wanaume na Kenya ilishinda upande wa wanawake.

  Michuano hiyo ambayo imefanyika kwa miaka minane mfululizo katika nchi wanachama, mwaka kesho, imepangwa kufanyika nchini Uganda.

  0 0


  0 0

  Washereheshaji wakifanya vitu vyao kwenye usiku wa onesho la mavazi kutoka kwa wanamitindo na wabunifu mbalimbali kutoka nchi kusini mwa Afrika wakiwemo wabunifu wawili Watanzania waliopendezesha maonesho hayo.
   
  Juu na chini ni bendera kutoka nchini za kusini mwa Afrika zikipita kwenye ufunguzi wa maonesho hayo yaliyofanyika siku ya Ijumaa Aug 29, 2014 Silver Spring, Maryland nchini Marekani.
  kwa picha zaidi bofya hapa

  0 0

  Na Sensei Rumadha Fundi 
   Kama mtaalam wa sanaa ya Yoga au Acharya (Yoga Teacher), Rumadha (Rasadeva) alihitimu na kutunukiwa Diploma ya kufuzu sanaa hiyo mwaka 1987, toka katika chuo cha "College of Neohumanist Studies", Ydrefors, Sweden, na hatimae baada ya kumaliza kozi hiyo kwenda Culcutta, India kwa mafunzo maalum ya kuthibitiwa kama mwalimu wa sanaa hiyo. 
  Pia Rumadha ni mwalimu wa sanaa ya Karate. 
  Mwaka 1991 alitunukiwa cheo cha juu cha sanaa ya Yoga duniani kiitwacho " Avadhuta" huko Calcutta, India chini ya kiongozi mkuu wa Yoga marehemu Shrii Shrii Anandamurtiji.
  Makala hii maalumu ni ya vitu vichache ambavyo mwalimu Rumadha anapenda kuviongelea kuhusu sayansi ya Yoga na uhusiano kifikra na mawazo ya ubongo wa binaadamu.
  Sensei Rumadha katika position inayoitwa "Siddhasana"
  Position hii ya kushika miguu inaitwa "Dhanurasana"

  0 0  0 0

  Vijana wabarikiwa wakiwa katika ibada ya ubarikio kabla ya shughuli ya kuwabariki

  Usharika wa Kikristo wa Kiswahili, ulio chini ya kanisa la kiinjili la kilutheri marekani, umebariki vijana tisa kwa mara ya kwanza kuwa washarika kamili. Tukio hili la kihistoria lilifanyika Jumapili iliyopita (8/24/2014). 
  Mara baada ya ibada ya ubarikio, vijana, familia, ndugu, jamaa na washarika wote walielekea katika ukumbi wa mji wa Shoreview kwa ajili ya mapokezi ya vijana hao na chakula cha jioni. 
  Sherehe hizo zilihudhuriwa na Mchungaji Dk. Joseph Bocko, kutoka Chicago, Illinois, ambaye ni mkuu wa idara ya huduma za injili za kiafrika kwenye makao makuu ya Kanisa la Kiinjili la Kiluteri la Marekani (ELCA); Mchungaji Deborah Stehlin, ambaye ni msaidizi wa askofu wa Sinodi ya maeneo ya Minneapolis katika mambo ya misheni ya injili; Mchungaji Phares Kakulima ambaye ni Askofu mdogo wa jimbo la Karagwe, na Douglas Mmari, ambaye ni mwanafunzi wa uchungaji; bila kumsahau Mchungaji Andrea Mwalilino ambaye ndiye mchungaji wa Usharika wa Kiswahili wa
  Minnesota katika kanisa la Holy Trinity kusini mwa jiji la Minneapolis. Katika ibada hiyo maalum, pia kulikuwa na ubatizo wa watoto watano, na vijana wawili.
  Baada ya kubarikiwa, vijana waliimba wimbo wa “Servants Prayer” kama sala yao ya shukrani ya ubarikio, wakisaidiwa na muimbaji mashuhuri wa kikristo, dada Rachel Kurtz. Kabla ya kubarikiwa, waliimba na dada Rachel wimbo wake wa Hallelujah.
  Vijana wabarikiwa wakisubiri usafiri maalum kuelekea kwenye ukumbi wa mapokezi mjini Shoreview.
  Vijana wabarikiwa wakisubiri usafiri maalum kuelekea kwenye ukumbi wa mapokezi mjini Shoreview.
  Picha ya pamoja ya wabarikiwa pamoja na jopo la wachungaji lililowabariki (aliyekosekana katika picha ni mchungaji Deb Stehlin from MN Area Synod)
  Vijana wabarikiwa wakipiga picha ya pamoja na Father Herbert Gappa, mmisionari aliyetumikia kanisa la katoliki huko Mwanza na Shinyanga kwa miaka karibu arobaini.
  Vijana wabarikiwa wakiwa nje ya ukumbi wa jumuiya wa Shoreview, mara baada ya kushuka kutoka kwenye “limousine” lililoandaliwa rasmi kwa ajili yao: Kutoka kushoto kwenda kulia ni Nana Kwame Anokye-Agyei (Wazazi Charles Anokye-Agyei na Jennifer Lobulu), Augustino Wema Sprita (Wazazi Timothy Shima na Anna Mtoi Shima), Loveness Shanalingigwa na Glory Shanalingigwa (Wazazi Oswald na Penuel Shanalingigwa), Eliwaza Patricia Dyauli (Wazazi David na Tasiana Dyauli), Jayness Kinambora Msuya na Lisa Naojwa Msuya (Wazazi Gracious na Florence Msuya), Maame Abena Anokye-Agyei (Wazazi Charles Anokye-Agyei na Jennifer Lobulu), na Ena Ndemange Mwalilino (Wazazi Andrea na Sarah Mwalilino).
  “Ma-kipa imara” wakipokelewa ukumbini kwa nderemo, vifijo na vigelegele, chini ya mwongoza sherehe, Mwalimu Gracious Msuya. Pichani pia ni Mchungaji Mwalilino wa usharika wa Kiswahili Minnesota, na Mzee Charles Semakula, mwenyekiti wa baraza la uongozi wa usharika wa Kiswahili Minnesota.
  Vijana kabla ya kukata keki ya ubarikio. Picha kwa hisani ya Emma Nagai

  0 0

  Na. Aron Msigwa –MAELEZO,Kagera.

  Mkoa wa Kagera umechukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Ebola kwa kuongeza nguvu katika udhibiti na ukaguzi wa raia wa kigeni kutoka nchi za Burundi, Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaoingia nchini Tanzania kupitia vituo vya mpakani vya mkoa huo.

  Akizungumza katika mahojiano maalum wilayani Ngara, Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe amesema kuwa kufuatia hali hiyo serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeongeza vifaa kinga na kuwawezesha kielimu wataalam wa afya walioko katika hospitali za mkoa huo na vituo vya ukaguzi mpakani.

  Amesema kuwa mkoa huo kijiografia unapakana na nchi tatu zikiwemo Uganda kwa upande wa Kaskazini, Rwanda na Burundi kwa upande wa magharibi na kuongeza kuwa mkoa kupitia kamati za Afya na wataalam wa afya walioko maeneo yote ya vituo vya ukaguzi wanafanya kazi zao ipasavyo kwa kuhakikisha kuwa kila anayeingia nchini kupitia vituo hivyo anachunguzwa dalili za Ebola.

  “Mkoa wa Kagera kama tunavyojua unapakana kwa karibu sana na nchi za Burundi, Rwanda na Uganda, kuna mwingiliano mkubwa sana wa watu kutoka eneo moja kwenda jingine hapa lazima tuchukue tahadhari kubwa , ninawahakikishia wananchi kuwa tumejipanga vizuri katika kuimarisha uchunguzi kupitia kamati zetu za afya” Amesisitiza.

  Amesema kufuatia uwepo wa ugonjwa huo katika nchi ya jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, uongozi wa mkoa kupitia kamati ya Afya na ile ya Ulinzi na Usalama unaendelea kuwaelimisha wananchi kupitia vituo vya mbalimbali vya radio vya mkoa huo kuhusu dalili za ugonjwa huo , namna ya kujikinga na namna ya kutoa taarifa kwa mamlaka husika endapo watabaini mtu mwenye dalili za ugonjwa huo.

  Kwa upande wake Afisa Afya wa Kituo cha ukaguzi cha Kabanga, mpakani mwa Tanzania na Burundi Bw. Amos Mangaluke akizungumzia hali ya ukaguzi wa raia wanaoingia nchini kupitia mpaka huo amesema kuwa zoezi la uchunguzi wa dalili za awali za ugonjwa wa Ebola linafanyika kwa ufanisi mkubwa kufuatia kituo chake kuwa na vifaa kinga vinavyomsaidia wakati wa utekelezaji wa majukumu yake.

  Amesema takribani watu 500 wanaotumia mpaka huo wa Kabanga huchunguzwa afya zao kwa siku ambapo hujaza fomu maalum ya taarifa ambayo hutumiwa na wataalam wa afya kituoni hapo.
  Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe akitoa ufafanuzi namna Serikali livyojipanga kukabiliana na ugonjwa wa Ebola mkoani humo kwa kuongeza vifaa kinga na kuwawezesha kielimu wataalam wa afya wanaofanya kazi ya uchunguzi wa dalili za ugonjwa huo walioko katika vituo vya ukaguzi mpakani.
  Afisa Afya wa Kituo cha ukaguzi cha Kabanga, mpakani mwa Tanzania na Burundi Bw. Amos Mangaluke akipitia fomu zilizojazwa na raia kutoka nje ya nchi wanaotumia mpaka huo kufuatia zoezi la uchunguzi wa dalili za awali za ugonjwa wa Ebola linalofanyika kituoni hapo.
  Ofisi ya Uhamiaji ya Kabanga mpakani mwa Tanzania na Burundi.
  Kizuizi cha magari katika mpaka wa Kabanga unaotenganisha Tanzania na Burundi, Wilayani Ngara.

  0 0

  Mbunge wa Temeke, Abbas  Mtemvu akihutubia mkutano wa hadhara uliofabyika kwenye Uwanja wa shule ya Sokoine, Temeke jijini Dar es Salaam, jana, Agosti 30, 2014.
  Mtemvu akishangiliwa wakati akihutubia mkutano huo wa hadhara
  Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akimpa kadi ya Uanachama wa UWT Maridha Rajabu wakati wa mkutano huo, wanachama wapya 45 wa jumuia hiyo walipewa kadi
  Mbunge wa temeke,  Mtemvu akimtuza msanii Omari Tego baada ya kukunwa na msanii huo kwa kuimba wimbo maalum wa CCM wakati wa mkutano huo.


older | 1 | .... | 555 | 556 | (Page 557) | 558 | 559 | .... | 3348 | newer