Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110150 articles
Browse latest View live

KIKAO KAZI CHA WATENDAJI WA SHIRIKA LA MAGEREZA NA GEPF CHAENDELEA LEO MKOANI MOROGORO

$
0
0


 Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Naibu Kamishna wa Magereza, James Selestine(wa kwanza kushoto) akiteta jambo na Watendaji Waandamizi wa Shirika la Magereza na GEPF kabla ya kutembelea katika eneo la Kihonda, Morogoro ambapo mradi wa Majengo ya vitega uchumi kwa ubia kati ya Shirika la Magereza na GEPF utakapojengwa(wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi wa Uwekezaji, Bw. Festo Fute(wa pili kulia) ni Mtendaji Mkuu wa Shirika la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga.
 Watendaji Wakuu wa Shirika la Magereza, GEPF na Wataalam Washauri wakiendelea na Kikao kazi katika eneo la Kihonda, Mkoani Morogoro ambapo mradi wa Majengo ya vitega uchumi utakapojengwa kama inavyoonekana katika picha.
Mkuu wa Gereza Kihonda, Mkoani Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Ben Mwansasu akiwaonesha eneo la Uwekezaji Watendaji Wandamizi wa GEPF na Wataalam washauri walipotembelea eneo hilo leo Agosti 1, 2014 Mkoani Morogoro. Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Magereza limeingia Makubaliano ya ubia na Mfuko wa Jamii wa GEPF katika miradi ya ujenzi wa Majengo ya vitega uchumi katika eneo la Karanga, Kilimanjaro na Kihonda Mkoani Morogoro.
 Msanifu wa Majengo toka Kampuni CONS AFRIKA ya Jijini Dar es Salaam, Bw. Henry Mwoleka(wa kwanza kushoto) akisisitiza jambo muhimu wakati Watendaji wa Shirika la Magereza, GEPF na Wataalam washauri walipotembelea eneo la Uwekezaji la Kihonda, Mkoani Morogoro ambapo mradi wa Majengo ya vitega uchumi utafanyika. Timu hiyo ya Wataalam imeendelea na Kikao chake leo Agosti 1, 2014 Mkoani Morogoro(wa pili kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Naibu Kamishna wa Magereza, James Selestine(wa pili kushoto) ni Mtendaji Mkuu wa Shirika la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga wakisikiliza maelezo ya Msanifu Majengo wa Kampuni ya CONS AFRIKA ya Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Magereza Mkoani Morogoro, Naibu Kamishna wa Magereza, James Selestine akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Waandamizi wa Shirika la Magereza, GEPF na Wataalam washauri mara tu baada ya kikao kazi cha kupitia na kuangalia maeneo ya Uwekezaji katika miradi ya vitega uchumi utakaofanyika. Kikao hicho kimeendelea leo Agosti 1, 2014 Mkoani Morogoro(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
========  ====== =========
Na; Lucas Mboje

Kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Shirika la Magereza, Mfuko wa Jamii wa GEPF na Wataalam Washauri kimeendelea leo Agosti 1, 2014 Mkoani Morogoro. Lengo la Kikao hicho ni kupitia na kuangalia maeneo ambayo Uwekezaji katika mradi wa Majengo ya vitega uchumi utafanyika.

Kikao hicho ni sehemu ya maandalizi ya mwanzo ya kuanza shughuli rasmi za ujenzi wa Majengo ya vitega uchumi kwa ubia kati ya Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Uzalishaji mali(Prisons Corporation Sole) na Mfuko wa Jamii wa GEPF.

Mpango huu wa ujenzi wa Majengo ya vitega uchumi unatarajiwa kuanza mapema mwishoni mwa Mwaka 2014 mara baada ya kukamilika kwa michoro na mahitaji mengine muhimu ambapo unatarajiwa kutekelezwa katika maeneo ya Jeshi la Magereza ya Kihonda Mkoani Morogoro na Karanga - Moshi Kilimanjaro.

Tayari, Jeshi la Magereza nchini kupitia Shirika lake la Uzalishaji Mali limetiliana Mkataba wa Uwekezaji wa Mfuko wa Jamii wa GEPF ambapo Majengo ya vitega uchumi yatajengwa katika maeneo ya Kihonda Mkoani Morogoro na Karanga - Moshi Mkoani Kilimanjaro. Utiwaji sahini ya Mkataba huo ulifanyika Mei 29, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano ulioko Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.

Kupitia ubia huo Shirika la Magereza litapata pato ambalo litaimarisha zaidi upanuaji wa shughuli za miradi ya Shirika hilo sambamba na kuipunguzia gharama Serikali.

Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake tayari limefikia makubaliano na Wawekezaji mbalimbali wa ndani na nje ya nchi ambao wamevutiwa na shughuli za kiuwekezaji kwa lengo la kuingia ubia hivyo kukuza mitaji na kubadilishana ujuzi katika miradi mbalimbali ikiwemo ya Madini na Kilimo katika maeneo ya Jeshi la Magereza.

Wakati huo huo, Jeshi la Magereza Tanzania Bara lipo katika maandalizi ya mwisho ya kuzindua TOVUTI yake ambapo kupitia Tovuti hiyo itarahisisha Mawasiliano pia Wananchi na Wadau mbalimbali watapata taarifa muhimu kuhusiana na Jeshi hilo. Tovuti hiyo itapatikana kupitia akaunti ya Anuani ya www.magereza.go.tz.

Vijana washauriwa kujiajiri katika sekta ya Sanaa

$
0
0
 Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kulia) akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.

 Mmoja wa wabunge wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Susan Nakawuki (mwenye blauzi ya pinki) akinunua bidhaa kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.

 : Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akiweka saini katika daftari la wageni katika moja ya kikundi cha wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.

 Baadhi ya Wabunge wa Afrika Mashariki akiwemo Mhe. Shyrose Bhanji anayewakilisha  Tanzania katika bunge hilo wakiangali kazi za sanaa ya uchingaji kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.

 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Shyrose Bhanji wa Tanzania akimkabidhi zawadi ya sinia lililotokana na kazi za uchongaji Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Margareth Zziwa mara baada ya kupenda bidhaa hiyo na kuamua kumnunulia spika huyo jana wilayani Bagamoyo wakati wa ziara ya Wabunge wa Afrika Mashariki katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa).

Katikati ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki ambaye pia ni mtoto wa Baba wa Taifa Mhe. Makongoro Nyerere (katikati) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afika Mashariki wa  Serikali ya Tanzania Bibi. Joyce Mapunjo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel walipokuta katika viwanja vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) wakati wa ziara ya wabunge wa Afrika Mashariki katika Taasisi hiyo. Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Habari.Vijana, Utamaduni na Michezo.

Tume ya Utumishi wa Umma yaendelea kuimarisha uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za masuala ya ajira

$
0
0

Naibu Katibu wa Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Neema Tawale akieleza kwa waandishi wa Habari (Hawapo pichani) kuhusu tathmini ya Tume juu ya uzingatiaji wa sheria,kanuni na taratibu za masuala ya ajira katika utumishi wa uuma, wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Kaimu Katibu Msaidizi wa Tume hiyo Bw. John Mbisso.

Kaimu Katibu Msaidizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Umma Bw. John Mbisso  akiongea na waandishi wa (Hawapo pichani) kuhusu jitihada wanazozifanya katika kuwaongezea uelewa wadau juu ya haki na wajibu wao katika masuala ya ajira katika utumishi wa umma, wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Naibu Katibu wa Tume hiyo Bi. Neema Tawale.

Baadhi ya waandishi wa habari waliwasikiliza wawasilishaji toka Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Umma wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Hassan Silayo)
Na Fatma Salum
Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma imeendelea kuimarisha Kiwango cha uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za masuala ya ajira katika Utumishi wa Umma.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu wa Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma  Bi Neema Tawale katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Bi Tawale alisema kuwa tathmini kuhusu uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za  masuala ya ajira iliyofanywa na Tume hiyo mwaka 2010/2011 katika Wizara, Idara zinazojitegemea, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sekretarieti za Mikoa imebainisha kuwa kiwango cha uzingatiaji kimeongezeka hadi kufikia asilimia 64 kwenye vipengele  vya Uajiri, Upimaji wa Utendaji Kazi wa Wazi (OPRAS), Likizo ya Mwaka na Likizo ya Ugonjwa.
Akifafanua zaidi Bi Tawale aliongeza kuwa ukilinganisha na utafiti wa kwanza uliofanyika mwaka 2005/2006 ambapo kiwango kilikuwa ni asilimia 50 ongezeko hilo limetokana na elimu inayotolewa na Tume kwa wadau kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na.8 ya mwaka 2002 na Marekebisho yake Na.18 ya mwaka 2007.
“Tume ya Utumishi wa Umma inajitahidi kuweka mikakati ili kuhakikisha inakabiliana na changamoto za masuala ya ajira katika kuongeza uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu kwa kuendelea kutoa elimu kupitia miongozo, vipindi kwenye vyombo vya habari na maonyesho mbalimbali ya kitaifa”. Alisema Bi Tawale.
Aidha Bi Tawale alisema kuwa Mwongozo uliotolewa na Tume hiyo kuhusu masuala ya ajira katika Utumishi wa Umma unawawezesha Waajiri na Mamlaka za Ajira kufuata taratibu wanaposhughulikia masuala ya ajira kwenye mamlaka zao.
Aliongeza kuwa katika kuhakikisha sheria, kanuni na taratibu za ajira zinatekelezwa ipasavyo Tume huagiza Waajiri au Mamlaka za Ajira kuchukuliwa hatua ikiwemo kuwaita mbele ya Tume kujieleza ikithibitika wamekiuka sheria au wameshindwa kutekeleza majukumu yao.
Naye Kaimu Katibu Msaidizi wa Tume hiyo Bw. John Mbisso alitoa msisitizo kwa waajiri kushughulikia masuala ya ajira ya watumishi wao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu ili kuepuka migogoro na kupunguza malalamiko kuhusu masuala ya ajira kwenye utumishi wa umma.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta awaahidi walemavu kutendewa haki katika Katiba Mpya

$
0
0

MWENYEKITI wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel  Sitta amewahakikishia Watu wenye Ulemavu nchini kuwa wanatendewa haki katika Katiba Mpya itakayopatikana.


Mhe. Sitta ameyasema hayo leo Septemba Mosi, 2014 katika mkutano wake na baadhi ya viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) ambalo lilikuja katika Bunge Maalum kwa lengo la kuwasilisha hoja zenye msisitizo kuhusu haki za watu wenye ulemavu katika mchakato Katiba Mpya.


Mhe. Sitta amesema kuwa kazi wanayoifanya ya kuyapokea makundi mbalimbali Bungeni hapo haina lengo la kuja na hoja mpya  na kuziwasilisha katika Bunge hilo, bali ni mawasiliano ya kawaida yanayohusu safari kutoka Rasimu Mpya ya Katiba mpaka kufikia katika Katiba Mpya inayopendekezwa ipatikane.


“Jambo lolote lililoandikwa na binadamu halikosi kasoro, katika Rasimu hii ya Katiba tumegundua inayomapungufu kadha wa kadha, kuna baadhi ya maoni ambayo hayakuzingatiwa ndiyo maana tunayafanyia kazi ili yawemo katika Katiba Mpya itakayopatikana,”.alisema Mhe. Sitta.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Inclusive Development Promoters and Consultants kutoka  Dar es Salaam, Bw. Kaganzi Rutachwamagyo ambaye pia ni mwanachama wa Shirikisho hilo,amesema kuwa Kikosi cha Ushauri kuhusu masuala ya watu wenye Ulemavu kimeweka kipaumbele cha msisitizo wao ambao unajielekeza katika hoja za kuongeza masuala ya mambo ya Muungano ambapo wamependekeza kuwa kwenye orodha ya Mambo ya Muungano kuongezewe suala moja zaidi la Nane kwa mujibu wa Rasimu ya Pili ya Katiba ambalo ni uratibu wa masuala ya haki, usawa na fursa na uwajibikaji kwa watu wenye ulemavu kama jambo la Muungano.


Bw. Rutachwamagyo  ameongeza kuwa hoja nyingine ya msisitizo inahusiana na suala la uanzishwaji wa chombo cha uratibu wa haki, usawa wa fursa na uwajibikaji wa haki za watu wenye ulemavu ambayo hii ni kwa mujibu wa Ibara ya 33 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu na Mkataba mwenza wa nyongeza iliyoridhiwa kwa pamoja na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amesema kuwa wanataka chombo hiko kijulikane kama Tume ya Kitaifa Juu ya Haki, Usawa wa Fursa na Uwajibikaji kwa Watu wenye Ulemavu.


Aidha, Bw. Rutachwamagyo  amegusia pia juu ya hoja nyingine inayohusu suala la Uwakilishi wa watu wenye ulemavu kwenye Bunge la Tanzania, Baraza la Wawakilishi, Mabaraza ya Madiwani utamkwe na Katiba na ukokotolewe kwa misingi ya asilimia badala ya kuweka idadi mahsusi. “Mathalani, tunapendekeza kifungu 113 kisomeke kuwa asilimia 5% ya Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watakuwa ni watu wenye ulemavu wakiwakilisha kundi hili na watapatikana kwa kuchaguliwa na wahusika wenyewe,” alisema .

Aliongeza kuongeza kwa kuzitaja hoja nyingine ikiwemo suala la matumizi ya lugha sanifu kwa muktadha wa watu wenye ulemavu na amesema kuwa kuna hali ya matumizi ya misamiati na islahi ambazo zinakinzana na dhana za walemavu kimataifa hivyo ni vema kukawa na tafsiri sahihi ya majina kwa watu hao ili kuepuka kukinzana huko, aidha amegusia pia suala la Hifadhi ya jamii huku akifafanua kuwa wadau wenye ulemavu nchini wanadai kuwepo kwa ibara maalum ndani ya Katiba inayoelekeza masharti ya upatikanaji wa hifadhi ya jamii kwa watu wenye Ulemavu ikiwa ni pamoja na kulipwa gharama ama kupewa unafuu ya kupunguza makali ya walemavu kwa mujibu wa ibara ya 28 ya Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu ya 2006.


Akiongea kwa niaba ya watu wenye ulemavu, Mhe. Amon Mpanjo ambaye ni mjumbe wa Bunge hilo amemuomba Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba kuunga mkono sio kupokea maoni mapya, bali kuyaboresha yale yaliyokwisha wasilishwa hapo awali. “Tukuombe Mwenyekiti ulisisitizie Bunge letu Maalum la Katiba liweze kuzingatia haki za watu wenye Ulemavu ili nao wapate kuwa na maisha bora,” alisema Mpanjo.

Naye Makamu Mwenyekiti wa SHIVYAWATA, Bi. Amina Mollel amesisitiza juu ya hitaji la wanawake la hamsini kwa hamsini na kati ya hizo, asilimia 5% wawe ni wabunge walemavu na ameitaka Tanzania kuwa mfano wa kuigwa kwa kutoa nafasi nyingi za uongozi  kada mbalimbali kwa walemavu. “Hii iwe chachu katika kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanapewa nafasi kwa uwezo walionao na sio kubaguliwa,” alisema Amina.

Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.
01/09/2014.

NAIBU WAZIRI MAJI ALIVALIA NJUGA TATIZO LA MAJI CHAKWALE

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla amesema Serikali itatatua tatizo la muda mrefu la maji katika kijiji cha Chakwale, Wilaya ya Gairo, mkoani Morogoro wakati alipotembelea mradi wa maji kijijini Mhe. Makalla alisema tatizo la maji Chakwale tutalifanyia kazi na kuhakikisha tunalitatua, mimi na Mbunge, Shabiby tutashirikiana tulete maji katika kijiji hiki ambacho kimekua na malalamiko ya muda

 “Kumekuwa na ugumu na uzembe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kuleta fedha za kutekeleza miradi ya maji hapa Gairo na hili limekuwa tatizo kubwa linalochangia mradi huu kutokukamilika Naibu Waziri aliagiza ndani ya wiki mbili awe amepatikana mtaalamu wa kutafuta na kuchimba maji kijijini hapo, kwa kushirikiana na Afisa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu, Praxeda Kalugendo kufanikisha zoezi hilo.

 Pia, ameahidi Wizara yake itatoa Sh. mil 300 ili mkandarasi aanze kutekeleza mradi huo Aidha, Mbunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby, alisema wamechoshwa na kero hiyo ambayo ni muda mrefu sasa tangu mradi huo umeanza kujengwa karibu miaka tisa iliyopita, na Serikali haina budi kuhakikisha tatizo hilo linafikia kikomo ili wananchi wa Chakwale wapate majisafi na salama.

Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ina miradi miwili ya Kibedya na Chakwale na mradi wa Chakwale Mhe. Makalla alitembelea kijiji cha Chakwale kujionea utekelezaji wa mradi huo, akitekeleza agizo la Rais, Jakaya Kikwete ambaye alipokua ziarani mkoani Morogoro na kumtaka akaangalie sababu ya hapo mwishoni mwa wiki. mrefu.

mpaka leo”, aliongeza Mhe. Makalla. ifikapo katikati ya mwezi Septemba. ulianza kutekelezwa mwaka 2005 ukiwa chini ya Wilaya ya Kilosa. kusuasua kwa mradi huo.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla na Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby wakizungumza kwa nyakati tofauti na katikati ni Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Kilosa, Hosea Mwingizi.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akizungumza na wananchi wa Chakwale, akifuatiwa na Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby na Mkurugenzi Msaidizi wa Maji Vijijini, Catherine Bamwenzaki.
Tanki la maji la mradi wa Chakwale

Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai akutana na Mtendaji Mkuu wa Dubai Chamber of Commerce and Industry

$
0
0
Mhe. Omar Mjenga, amekutana na Mhe. Hamad Buamim, Rais na Mtendaji Mkuu wa Dubai Chamber of Commerce and Industry na kufanya naye mazungumzo.

Katika mazungumzo, wamejadiliana uwezekano wa kuwa na ziara ya kibiashara kwenda Tanzania, kwa makampuni na viwanda vilivyopo Dubai, ili kukutana na wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda Tanzania, ili kujionea na kuibua fursa za uwekezaji. Wamekubaliana ziara hiyo ifanyike mwanzoni mwa mwaka kesho na hivyo basi kuanza maandalizi mapema.

Mwezi Novemba, kutakuwa na ziara ya kibiashara ya makampuni kutoka Falme ya Ajman.

Aidha, wamezungumzia kuhusu mkutano wa Africa Global Business Forum utakaofanyika tarehe 1-2 Oktoba 2014 hapa Dubai. Mtukufu Sheikh Mohammed bin Rashid al Maktoum amemwalika Rais Kikwete kuhudhuria pamoja na marais wengine wa Mali, Ghana, Uganda, Mozambique, Ethiopia, Senegal, Burkina Faso, Sudan na Ivory Coast.

Mkutano huu hufanyika kila mwaka ambao huzungumzia njia muafaka ya ushirikiano kati ya Serikali ya Dubai na UAE kwa ujumla na nchi za Afrika.

TAHA YAADHIMISHA SIKU YA WAKULIMA SHAMBANI KILIMANJARO

$
0
0
Asasi ya sekta binafsi ya wakulima wa mboga mboga,Matunda, maua, viungo na mbegu zake imeadhimisha siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa kijiji cha Mferejini-Machame katika  wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.
 
Maadhimisho hayo yamekuwa yakifanyika kila baada ya Mwezi mmoja mpaka miwili ili kutoa fursa kwa wananchi kujifunza mbinu bora za kilimo cha mazao ya ‘horticulture’ ikiwa ni sambamba na kujifunza mbinu fasaha za kilimo biashara.
picha 1
Afisa ufundi wa kilimo cha mboga kutoka TAHA Bw. Abdon akiwaelekeza wakulima kuhusu mbinu bora za uoteshaji wa miche ya mboga kwenye trei maalumu katika mahadhimisho ya siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa kijiji cha Mferejini-Machame katika  wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.
Wakulima wakimsikiliza Mtaalamu wa masuala ya mbolea na viuatilifu kutoka kampuni ya Triachem Bi. Baby Nkossa wakati akizungumzia suala zima la matumizi fasaha ya mbolea na viuatilifu kwenye mazao
Wakulima wakimsikiliza mtaalamu wa masuala ya mbolea na viatilifu kutoka kampuni ya Triachem Bi.Baby Nkassa  wakati akizungumzia suala zima la matumizi fasaha ya mbolea na viatilifu kwenye mazao
picha3
Katibu tawala wa Wilaya ya Hai Bi. Zuhura Chikira ambaye alikuwa mgeni rasmi, akisiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu wa kilimo cha mboga kutoka TAHA Bw. Giliard Daniel katika mahadhimisho ya siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa kijiji cha Mferejini-Machame katika  wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.
picha 6
Shamba mfano lililotumika kuwafundishia wakulima siku hiyo.

Elihuruma Ngowi joins Serengeti Breweries Ltd

$
0
0
Mr. Elihuruma Ngowi has joined Serengeti Breweries Ltd. as Brand Manager with a profound experience in Customer Care, Marketing and Sales after having spent over eight (8) years at Vodacom Tanzania Ltd.

At Vodacom, he worked in various departments from Customer Care to Marketing and finally with Sales & Distribution Department where he held key positions, most notably as Product Marketing Manager, Devices & Alternative Channels Manager and Franchise Operations Manager respectively. He is also the Vice President and co-founder of CIBN Tanzania Ltd.

Mr. Ngowi holds a Bachelor of Business Administration (Marketing) degree from the University of the Western Cape, Cape Town, South Africa. He also expects to graduate his master’s degree in International Business (Investment in Emerging markets) from the University of Dar es Salaam Business School later this year.

He is a strong believer on strong performance. He believes that one has to over deliver and outshines their performance. He also believes that people have to network with the right people, have a positive pride on your performance and be able to sell your results, successes and achievements and celebrate. Always treat people with high integrity and honesty and learn to hold courageous discussions. Spiritual powers should not be forgotten. Remember to say your prayers at all times.

JAJI MKUU WA TANZANIA AFUNGUA RASMI MAFUNZO ELEKEZI YA MAJAJI WAPYA

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe. Mohamed Chande Othman akitoa hotuba ya ufunguzi ya Semina elekezi ya Wahe. Majaji Wateule walioishwa hivi karibuni, lengo la Mafunzo likiwemo ni kuwapa Mwongozo juu ya utendaji kazi wa Mhimili wa Mahakama.
Kundi la Majaji Wateule wakifuatilia hotuba ya Mhe. Jaji Mkuu alipokuwa akifungua rasmi Mafunzo hayo.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (aliyeketi katikati) na Viongozi wengine wa Mahakama na Chuo. Cha Uongozi wa Mahakama wakiwa katika picha ya pamoja Mara baada ya ufunguzi wa Mafunzo hayo yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama kilichopo Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga.

Wanamazingira wahamasishwa kuwalinda binadamu, viumbe hai

$
0
0
Kamishna Msaidizi wa Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Leonard Ishengoma akisoma hotuba ya ufunguzi (kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara, Eliakim Maswi) wa semina ya mafunzo kwa Maafisa Mazingira wa Wilaya kutoka Kanda ya Ziwa, juu ya mpango kazi wa mazingira wa sekta za nishati na madini, Septemba 1, 2014.
Afisa Misitu Mkuu kutoka Kitengo cha Mazingira – Wizara ya Nishati na Madini, Theodory Silinge akisisitiza jambo wakati wa semina ya mafunzo kwa Maafisa Mazingira wa Wilaya kutoka Kanda ya Ziwa, inayofanyika jijini Mwanza.
Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Gideon Kasege akizungumza na Maafisa Mazingira wa Wilaya kutoka Kanda ya Ziwa, Septemba 1, 2014 jijini Mwanza, wakati wa semina ya mafunzo kwa wanamazingira hao.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

VIDEO YA MKUBWA NA WANAWE YAZINDULIWA MAISHA CLUB CHINI YA VODACOM TANZANIA

$
0
0
Mwanamuziki wa muziki wa bongo fleva Dogo Janja akiwapagawisha mashabiki waliofurika katika ukumbi wa maisha club oysterbay jijini Dar es Salaam, wakati wa onyesho la Yamoto Bendi jana usiku wakati wa uzinduzi wa video yao ya “Mkubwa na Wanae” onyesho hilo lilidhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Waimbaji wanaounda kundi la “Yamoto Band”Aslay, Becka, Bella na Maromboso wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa video yao ya mkubwa na wanawe,uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa New Maisha Club jana usiku udhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mwimbaji mahiri wa kundi la”Yamoto band” Aslay akikonga nyoyo za wapenzi wake waliofurika katika ukumbi wa New Maisha Club oysterbay jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa video yao ya mkubwa na wanawe ,uliofanyika jana usiku na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Baadhi ya mashabiki wa kundi la Yamoto bendi lenye masikani yake TMK wakiwa kwenye pozi ya picha wakati wa uzinduzi wa video yao ya mkubwa na wanawe ,uliofanyika jana katika ukumbi wa New Maisha Club na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

Umuhimu wa vipimo na takwimu ili kuboresha biashara

$
0
0
Katika dunia hii ya utandawazi, ushindani ni kitu kisichoepukika. Haijarishi wewe unafanya biashara ya kuuza peni au una blogu yako au hata unauza dhahabu. Utandawazi umeweza kuwafanya wanunuzi wawe na sauti na machaguo mengi toka kila pande, pande hizi zinaweza kuwa hata nje ya mipaka ya nchi. Pia, wanunuzi wamepewa uwanja mkubwa wa kuijadili na kupata taarifa za biashara yako kwa urahisi zaidi, mitandao jamii ni moja ya kitendea kazi kwenye hili.

Ingawa ushindani ni mkubwa sanasana, lakini leo hii, kama utatembelea kwenye biashara kadhaa nchini Tanzania, utakubaliana na mimi kuwa, wengi tunafanya biashara kwa mazoea (business as usual)na ubunifu umekuwa mdogo sana kwa makampuni mengi sana. Iwe ya serikali au hata ya watu binafsi, iwe madogo yaliyoanza jana au hata yale yenye umri wa miongo.

Leo hii ni kitu cha kawaida sana kwenda kwenye kibanda cha pesa na muhusika akaanza kukuhudumia hata bila ya kukusalimia, kwa wenyewe wanasema, "kama hakijaharibika, basi usikirekebishe (If it ain't broke, don't fix it)", Na wengi tumekuwa tukiaminni hivyo, kama wateja wanakuja, basi hakuna haja ya kuboresha. Sisi Dudumizi tunasema, maboresho ni wimbo wetu wa kila siku, hata hii blog ni zao la maboresho na marejesho.

CHAKE NI CHAKE

$
0
0
Kinachopita ni chake, hata kama si cha kwake,
Chochote kwake ni chake, hata kama cha mwenzake,
Ukicheka usicheke, akikipenda ni chake,
Yeye chake ni cha kwake, cha kwake si cha wenzake!


Kikipendeza ni chake, chake yeye chakwake,
Ukikiona kileke, usikitamani chake,
Macho mbele yapeleke, usigeuzie kwake, 
Yeye chake ni cha kwake, cha kwake si cha wenzake!


Kiwe kitamu cha kwake, na vitamu vya wenzake
Vyote kwake ni vyake, ati yeye haki yake, 
Ugonjwa wake ni wake, tiba ati vya wenzake!


Yeye chake ni cha kwake, cha kwake si cha wenzake!

Kina umbo uzuri chake, chake yeye peke yake,
Mara akishike shike, kuringishia wenzake, 
Atakupiga mateke, ukikigusa cha kwake!
Yeye chake ni cha kwake, cha kwake si cha wenzake!


Vya wanyonge ni vyake, na vya matajiri vya kwake, 
Si haramu huko kwake, vikizuka anga zake,
Toka Pemba Chakechake, hadi Kigoma Isike, 
Yeye chake ni cha kwake, cha kwake si cha wenzake!


Kama vya wenzake vyake, halali kula vya kwake, 
Haki haiwi ya kwake, kama siyo ya wenzake,
Akivila vya wenzake, vitaliwa na vya kwake, 
Yeye chake ni cha kwake, cha kwake ni cha wenzake!


Na. M. M. Mwanakijiji 
(Sauti ya Kijiji)

JK AFUNGUA BARABARA YA DODOMA-FUFU

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiweka jiwe la msingi kuashiraia ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma- Iringa sehemu ya kutoka Dodoma - Fufu (Km70.9) huku akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa upande wa Tanzania Bi. Tonia Kandiero kushoto pamoja na Mwakilishi kutoka Serikali ya Japan na JICA, Ndugu Kuniaki Amatsu kulia huku Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akishuhudia tukio hilo.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma- Iringa sehemu ya kutoka Dodoma - Fufu (Km 70.9) iliyojengwa kwa kiwango cha Lami. Wengine walioshika utepe ni Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania Bi. Tonia Kandiero, Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe pamoja na viongozi wengine 
 Taaswira ya mkeka mpya kutoka Dodoma hadi Fufu wa Kilomita 70.9 aliouzindua Rais Kikwete

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli pamoja na viongozi wengine wa kitaifa wakimtazama Mwakilishi kutoka Serikali ya Japan na JICA Ndugu Kuniaki Amatsu na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) kwa upande wa Tanzania bi Tonia Kandiero walipokuwa wakipanda mti kama ishara ya kumbukumbu ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma- Fufu(Kilomita 70.9)

 Waziri wa zamani wa Ujenzi Mzee Job Lusinde akipanda mti kama ishara ya kumbukumbu ya ufunguzi wa rasmi wa barabara ya Iringa-Dodoma sehemu ya Dodoma-Fufu (Kilomita 70.9) huku Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli , Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge wakishuhudia tukio hilo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli  pamoja na viongozi wengine wakitaifa katika picha ya kumbukumbu mara baada ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Dodoma-Iringa sehemu ya Dodoma- Fufu Kilomita 70.9. Picha zote kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini –Wizara ya Ujenzi

KAMPUNI YA UBELGIJI YA TPF SAMBRE YAANZA KUFANYA KAZI TANZANIA

$
0
0
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa kampuni ya ushauri ya TPF Basse Sambre baada kukutana nao leo ofisini kwake Brussels. Wa kwanza kulia ni Bwana. Stefan Pousset Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo na wa kwanza kushoto ni Bwana Jerome Bestgen Meneja wa mauzo wa kampuni hiyo. Wa pili kulia ni Bwana Nyamtara Mukome afisa katika Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji. Wawakilshi hao walimweleza Balozi Kamala  kwamba wamepata shughuli za kufanya Tanzania na wanatarajia kufungua ofisi zao Tanzania. Balozi Kamala aliwashauri watafute Watanzania wa kushirikiana nao  ili kampuni yao iweze kuimarika, kuhimili ushindani katika sekta ya ushauri, kutoa ajira na kusaidia kujenga uchumi wa Tanzania.

Kamati kuanza kuwasilisha Sura zilizosalia za Rasimu ya Katiba Mpya

$
0
0
Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Yahya Khamis Hamad akiongea na waandishi wa Habari kuhusu uwasilishwaji wa Sura zilizosalia za Rasimu ya Katiba Mpya utakaofanywa na Kamati zote 12 za Bunge. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Itifaki wa Bunge hilo, Bw. Jossey Mwasyuka. Mkutano huo ulifanyika Septemba 1, 2014 kwenye Ukumbi wa Spika mjini Dodoma.
Baadhi ya Waaandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini taarifa ikiyotolewa na Katibu wa Bunge Maalum la Katiba wakati wa mkutano huo ulifanyika 01 Septemba, 2014 kwenye Ukumbi wa Spika mjini Dodoma.


KAMATI 12 za Bunge Maalum la Katiba kesho zitaanza kuwasilisha Sura zilizosalia za Rasimu ya Katiba Mpya ambazo ni Sura ya Pili, Tatu, Nne na ya Tano kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa tangu tarehe 5 Agosti, Mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo na Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Yahya Khamis Hamad wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habri kwenye Ukumbi wa Spika mjini Dodoma.
“Kila Kamati imeshandaa taarifa kwa ajili ya kuiwasilisha katika Bunge hapo kesho”, alisema Katibu huyo.
Aidha, Katibu huyo ameongeza kuwa baada ya sura hizo kumalizika, Sura zitakazofuata ni Sura ya Saba, Nane na 14 na nyingine ni sura mpya.
Ameongeza zaidi kuwa, utaratibu huo utaendelea mpaka sura zote zitakapomalizika siku ya tarehe 8 Septemba, 2014 saa mbili usiku.
Katibu ameongeza kuwa Bunge hilo litaanza kujadili Sura hizo za Rasimu ya Katiba Mpya kuanzia siku ya tarehe 9 Septemba, 2014.

IN LOVING MEMORY

$
0
0
IN MEMORY OF OUR LATE MOM MRS JOYCELYN MKAMSURI SAWAYA MAWALA- MAREALLE.

TODAY 2ND SEPTEMBER 2014 YOU TURNED FOUR YEARS SINCE YOU DEPARTURE. IN YOUR MEMORY LINGERS SWEETLY TENDER, FOND AND TRUE. THERE IS NOT A DAY DEAR MOTHER THAT WE DO NOT THINK OF YOU.

MOM, YOUR TREASURE STILL, WITH LOVE SINCERE BEAUTIFUL MEMORIES OF ONE SO DEAR……. OH HOW WE WISH SHE WAS HERE TODAY TO SEE ALL THE BLESSINGS WE HAVE.

TO SEE ALL THE BLESSINGS WE HAVE, THE WORD OF GOD THEO: 5:18 SAYS IN EVERTHING GIVE THANKS. FOR THIS IS THE WILL OF GOD IN CHRIST JESUS CONCERNING YOU.

DEEPLY MISSED BY YOUR CHILDREN EMILY AND LEONARD. AND YOUR IN LAW CAROLYNE.

GRAND CHILDREN VANESSA, JOYCELYN AND EVE. YOUR BROTHERS AND SISTERS FROM THE CLAN OF SAWAYA MAWALLA.

REST IN PEACE MOM

Ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Kilwa Jazz Band - "Napenda nipate lau nafasi"

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
WESTERN JAZZ BAND - "VIGELEGELE"

TUNALETA USED PROFFESIONAL CAMERA'S NA ACCESSORIES ZAKE KWA SPECIAL

$
0
0
Tunaleta  camera aina kama hizi Sony pd175,nikon na canon na nyinginezo kwa special order,pia vitu kama lens,flash,charger,batteries etc.Pia tunaleta used plotter's,used cd printer's etc,kwa mawasiliano waweza piga number hii 0767410763 ama kwa email macamaca97@outlook.com.
  
Viewing all 110150 articles
Browse latest View live




Latest Images