Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 546 | 547 | (Page 548) | 549 | 550 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarest Ndikilo (kulia) na Katibu wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Joyce Masunga baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza  leo August 22, 2014 ambako August 23, 2014 atakagua ujenzi wa uwanja wa ndege na baadaye anatarajiwa kuongoza  harambee  iliyoandaliwa na Mkapa Foundation. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda kesho, Jumamosi Agosti 23, 2014 anatarajiwa kukagua ujenzi wa kiwanja wa Ndege wa Mwanza unaopanuliwa miundombinu na majengo ili kuwezesha ndege kubwa za safari za mizigo zinazolingana na BOEING 747  (CODE D  to CODE E) kutua na pia kuhudumia abiria zaidi ya milioni 2 katika jengo jipya la abiria. Waziri Mkuu atakuwa mkoani hapa Mwanza kwa ziara ya kiserikali kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kushiriki kama mgeni rasmi katika shughuli za BWM Foundation..

  Uwanja wa ndege wa Mwanza unapanuliwa kwa gharama ya sh,. Bilioni 105. Kati ya fedha hizo, Serikali ya Tanzania inatoa sh. Bilioni 85 na benki ya BADEA na Shirika la OFID kwa pamoja (sh. Bilioni 20) zikiwa ni mkopo.

  Maeneo ambayo Waziri Mkuu, Mh. M.K. Pinda anatarajiwa kukagua ni jengo la kuongozea ndege (control tower), njia ya kurukia na kutua ndege inayorefushwa kwa mita 500 zaidi kutoka mita 3,300 za sasa ili kuwezesha ndege kubwa za mizigo za Boeing 747 kutua na kuruka katika uwanja huo bila matatizo.

  Eneo lingine litakalotembelewa na Waziri Mkuu ni la mtambo wa lami (asphalt plant) itakayozalisha lami inayotumika kujenga barabara inayorefushwa  ya kuruka na kutua  ndege.Mtambo huu unamilikiwa na mkandarasi wa mradi huu, kampuni ya Beijing Construction Engineering Group ya China.

   Mhandisi Mshauri wa mradi huo ni Kampuni ya United Engineering and Technical Construction (UNETEC) ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) inayofanya kazi ya usanifu na usimamizi wa mradi  kwa gharama ya dola za Marekani 3,376,031.00.

  Akiwa uwanjani hapo katika ziara itakayoanza saa 3.00 asubuhi kesho, Jumamosi, Waziri Mkuu, Pinda  anatarajiwa kupata taarifa ya maendeleo ya mradi huo wa ujenzi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wanaojenga miundombinu hiyo ya usafiri wa anga.

  Kazi ya ujenzi ilianza Julai 2012 na mkataba wa kazi na mkandarasi ulisainiwa Juni 2012. Awali muda wa kumaliza kazi ulipangwa uwe miezi 24 , yaani mwishoni mwa mwaka huu 2014 lakini kutokana na ufinyu wa bajeti ya serikali sasa kazi itamalizika Oktoba 2015.. Kazi zinazofanyika mpaka sasa ni urefushaji wa njia ya kurukia ndege na kutua, upanuzi wa maegesho ya ndege za abiria, ujenzi wa jengo la abiria na miundombinu yake(barabara ya kuingia na kutoka kwenye maegesho).

  Nyingine ni ujenzi wa jengo la mizigo, ,maegesho ya  ndege za mizigo, jengo la kuongozea ndege, kituo cha umeme, maegesho ya magari , mifumo ya maji ya mvua na mifumo wa  maji safi na taka kwa ajili ya kiwanja kizima.

  Ujenzi huu utakapokamilika utaufanya uwanja wa ndege wa Mwanza kuwa kitovu cha usafiri wa anga  kwa nchi za maziwa makuu na kuwezesha ndege za kimataifa (intercontinental flights) kutua.

  Pia  utaongeza uwezo wa jengo la abiria kuhudumia abiria na mizigo kutoka abiria  500,000 kwa mwaka hadi abiria milioni 2 kwa mwaka.

  Upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Mwanza ni utekelezaji  wa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010.

  TAA  inasimamia viwanja 58 yya ndege vya serikali, inajenga vipya na kuendeleza vilivyopo ambapo hivi sasa inaendelea  na ujenzi wa jengo la tatu la abiria kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyrere (JNIA), Dar Es Salaam, lenye uwezo wa kuhudumia abiria milioni 6 kwa mwaka. Jengo hilo la kisasa linajengwa na mkandarasi, BAM International ya Uholanzi na linatarajiwa kukamilika Oktoba 2015.

  Aidha, TAA imekamilisha miradi kadhaa ukiwemo wa kiwanja cha ndege cha Mpanda, Mafia na cha Songwe, Mbeya.


      IMETOLEWA NA GODFREY JOHN LUTEGO    

     AFISA UHUSIANO - OFISI YA SHERIA NA UHUSIANO TAA


      (TEL. O713-507777)


  0 0

  Bi Scholastika Mhagama akiwa katika mlango wa nyumba yake.
   ---------------------
  Na Oswald Ngonyani wa demashonews - Peramiho.
  Wahenga walisema ‘Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni;’ Jamii inazidi kujawa na chuki na ukatili ndani yake, imekuwa kawaida siku hizi kusikia fulani kamuua fulani kwa kisa kisichokuwa na maana.

  Maalbino wanakatwa viungo vyao kwa visingizio vya kupata utajiri kwa watu wasiokuwa na huruma, watoto wadogo wananyimwa haki zao na kuwekwa ndani ya maboksi na wengine kuishi maisha yao katika uvungu za kitanda yote haya ni mambo ya kutisha yanayotendeka katika jamii zetu.
  Hali imekuwa tete amani na upendo vinazidi kuyeyuka kama barafu, watu hawana utu tena, wamejivika ngozi za kondoo wakati mioyo yao ni ya Simba, hakuna tena roho ya huruma kwa wanadamu wa dunia ya leo.
  Choo cha bibi Scholastika Mhagama

  Wakati haya yote yanaendelea kutendeka katika jamii zetu ni kama vile tunazidi kuugeuza ulimwengu tunaoishi kuwa ‘Uwanja wa dhambi’ ulimwengu wa kutojaliana  tena, wanadamu wamebadilika na kuwa kama wanyama na tena hata zaidi ya mnyama.
  Katika hali isiyo ya kawaida Bibi mmoja ambaye ni mlemavu wa miguu na mzee sana anayeishi peke yake katika kibanda ambacho kwake ni kama gereza ambalo hataweza kutoka tena maisha yake yote, amejikuta akifanya kitu kisicho cha kawaida kwa binadamu wa kawaida.
  Jeneza la bibi likitolewa ndani kwake na wanachama wa Kombination Camp

  Namzungumzia Bibi Scholastica Mhagama mwenye umri unaokadiriwa kufikia (76), ambaye ni mlemavu wa miguu anayejongea kwa kutambaa ambaye anaishi peke yake katika kibanda chake katika kijiji cha Lundusi mtaa wa Linga huko Peramiho Songea mkoani Ruvuma. Ni jambo la kusikitisha sana kwa bi kizee kama huyu kuishi peke yake akiwa hana msaada wa kueleweka kutoka kwa jamii inayomzunguka.

  Bibi huyu anayeishi kwa uchungu na majonzi amekata tamaa kabisa ya maisha hali iliyomfanya aamue kuchonga jeneza lake mwenyewe akijiandaa kufa siku yoyote.Bibi huyu anaishi na jeneza hilo chumbani kwake.
  “Maisha yangu ni magumu sana, naishi kama mnyama, sipendwi na ndugu zangu wala na jamii inayonizunguka. Wamenichoka sina raha natamani hata Mungu anichukue sasa hivi ili nikapumzike, nasali kwa sala zote natubu na kujuta kila siku lakini wala Mungu hanichukui, sijui kwanini” Anasema Bi Scholastica Mhagama kwa uchungu.
    Jeneza la Bi Scholastika Mhagama

  Akielezea historia ya maisha yake Bi Scholastika anasema alizaliwa akiwa na miguu yote lakini alipata bahati mbaya ya kugongwa na nyoka alipokuwa darasa la pili hali iliyomfanya kukatwa mguu ili kuepusha madhara mengine kama vile kifo. Hivyo maisha yake yalibadilika na tangu hapo akawa mlemavu.

   Hali hiyo ya ulemavu lakini pia uzee alionao vimemfanya ashindwe kujihudumia kwa lolote zaidi ya kupika tu. Hata hivyo anakosa mahitaji muhimu kama vile maji na chakula hali inayomfanya alale na njaa kwa baadhi ya siku.

  Kwa hali aliyo nayo ni wazi kuwa Bi Scholastika anahitaji baiskeli ya miguu mitatu (wheel chair) ambaye itamwezesha  kutembea  kwa kuwa hivi sasa anatambaa na kupata maumivu makali kutokana na nyama iliyobakia kwenye nyonga baada ya kukatwa mguu.

  Bi Scholastika anazidi kueleza kuwa kuna watu waliwahi kufika kumuandikisha jina lake na kumuingiza katika orodha ya watu wanaostahili kupata msaada lakini anasikia misaada inafika kwa jina lake lakini yeye mwenyewe hajawahi kuipata.

  Vipi kuhusu Sera ya Wazee?
  Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 inaweka bayana kuwa suala la uzee na kuzeeka limekuwa lenye umuhimu mkubwa ambapo karne ya ishirini imeshuhudia ongezeko kubwa la idadi ya wazee.

  Kwa kurejelea takwimu zilizopo ni kwamba, ifikapo mwaka 2050 idadi ya wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60 nchini hapa itaongezeka na kufikia wazee milioni 8.3 (Sawa na asilimia 10 ya watanzania wote)

  Kama hiyo haitoshi, Taarifa ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 1999 inaeleza kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wazee duniani na kwamba ongezeko hilo linaonekana zaidi katika nchi zinazoendelea (Tanzania ikiwepo) ambapo viwango vya ongezeko hilo havilingani na uwezo wa rasilimali zilizopo za kuwahudumia.

  Rasilimali hizo zinajikita zaidi katika Nyanja za msingi katika makuzi ya binadamu yoyote zikiwemo Nyanja za afya, lishe na huduma nyingine za msingi zisizoweza kuepukwa na binadamu yeyote.

  0 0


  0 0

  Mbunge Filikunjombe akishiriki kuchimba mfereji  wa maji kijiji cha Madindo
  Wananchi  wa madindo wakishirikiana na mbunge wao Filikunjombe kukamilisha mradi wa maji

  Diwani  wa kata ya Mlangali kushoto na katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe  wakijumuika na wanawake wa  kijiji cha madindo kucheza kwa furaha baada ya mradi huo kukamilika ,kulia ni mbunge Filikunjombe akishuhudia
  Diwani wa kata ya  Mlangali Faraja Mlelwa akisaidia  kukunja nguo kwa ajili ya kumwongeza mbunge Filikunjombe kata kichwani huku mbunge huyo akiwa na  wanawake wakiwa na ndoo za maji kichwani.
  Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akifafanua juu ya malipo ya mishahara ya watumishi yaliyofanyika mwezi Julai mwaka huu leo jijini Dar es salaam ambapo ameonya mamlaka husika ziwe na taarifa sahihi za idadi ya watumishi ili kuondoa makosa ya kulipa mishahara hewa, endapo kutatokea makosa ya ulipaji wa mishahara hewa watachukuliwa hatua za kisheria na kufikishwa mahakamani. (Picha zote na Eleuteri Mangi – MAELEZO)


  0 0

  Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akisaini Kitabu cha Maombolezo ya Waziri Mkuu wa zamani wa Ireland Mhe. Albert Reynolds. Kitabu hicho kimefunguliwa leo katika Ubalozi wa Ireland Ubelgiji.

  0 0


  0 0  0 0

   Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wakuu wa Taasisi ya kifedha ya UTT Microfinance, baada ya kukata utepe kuzindua taasisi hiyo, Dar es Salaam jana.
  Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mwigulu Nchemba (wa pili kushoto), akikata utepe kuzindua rasmi Taasisi ya huduma za Kifedha ya UTT Microfinance, Dar es Salaam jana. Wa pili Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi Balozi Fadhili Mbaga na Mtendaji Mkuu wa UTT, Bw. James Washima (kushoto).
  Naibu Waziri wa Fedha Bw. Mwigulu Nchemba (katikati), akimsikiliza kwa makini Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kifedha ya UTT Microfinance, Bw. James Washima wakati akimuonyesha vipeperushi, Dar es Salaam jana.  Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Balozi Fadhil Mbaga.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kifedha ya UTT Balozi Fadhil Mbaga (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Bw. James Washima wakimwangalia Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mwigulu Nchemba.  0 0

  Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB), Profesa Costa Mahalu akizungumza wakati wa kufunga  Mafunzo hayo ya siku 14 yaliyoshirikisha maofisa wa juu wa fani ya biashara wa Serikali za nchi nane ambayo yaliratibiwanna Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB) ambayo yalifadhiliwa na Chuo Kikuu Cha  Nordric Africa Institute.
  Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Bw. Shirwan Naseh, raia wa Netherlands  mwenye asili ya Iraq aliyezuiliwa kuingia nchini na kupigwa pigwa PI na Idara ya Uhamiaji
  0 0

  Uiyonavyo sivyo ilivyo hadi UISIKIAPO, Cheif wa swahilivilla Ebou Shatry akutana na mtaalamu wa vichekesho, Hussein China ndani ya Jjiji la Dar,  kwa Video Clip fupi, ya WhatsApp  WADAU wetu kaeni mkao wa kula...
  Cheif wa blog ya swahilivilla Abou Shatry kutoka Washington DC nchini Marekani akipata picha ya pamoja na Mtaalamu wa Vichekesho, Hussein China, baada ya miaka 15 kutoona kijiwezi Jijini Dar, katika mpango mzima wa kipindi cha Msakatonge na Azamtv bingwa wa vichekesho kuandaa mualiko rasmi.

  0 0


   BENDI ya Masai Safari ya jijini Dar es salaam inatarajia kuzindua albam yake ya kwanza kabisa watakayozindua siku ya  Agosti  30, mwaka huu  katika ukumbi wa Lunch Time,  Tip Top Manzese jijini Dar.
  Akizungumzia uzinduzi wa albam hiyo rais wa bendi hiyo Fransic Mwaisela amesema kwamba siku hiyo watasindikizwa na bendi mbalimbali wakiongozwa na bendi ya Extra bongo inayo ongozwa na Ali Choki.
  Alizitaja nyimbo zilizomo katika albam hiyo ni sita itakayozinduliwa siku hiyo ikiwa nyimbo ambayo iliyobeba albam ni akuna kama baba ya pili ni njia panda,mikono ni kazi,ndoa ni mpango wa mungu,usiwasikilize wambeya,kilio changu nyimbo hizo ndio zitakazokuwa katika albam hiyo itakayo zinduliwa mwishoni mwa mwezi huu.
  aliongeza kwa kutaja wasanii wengine watakaokuwepo siku hiyo ni Omari Tego,Maua Tego pamoja na wasanii mbalimbali wa bondo flefa watakaosindikiza uzinduzi huo.
  Bendi hiyo kwa sasa ipo kwenye mazoezi ya nguvu kwa ajili ya kutoa burudani kabambe siku ya uzinduzi wa albam ya bendi hiyo

  0 0

  During the verification exercise of the 2014/2015 loan application forms, the Board has come across loan applications which are incomplete or are missing some vital information for further loans processing. For that reason, the Board would like to inform concerned Loan applicants that such incomplete applications will not be processed until the missing information is provided.  
  Therefore, loan applicants and/or guarantors who have not signed their documents are required to come physically at HESLB offices on Plot No. 8, Block No. 46 Sam Nujoma Road, Mwenge- Dar es Salaam for correction of their loan applications.
  Applicants who have not attached (to their application forms) birth certificates, guarantor’s particulars such as photocopy of Passport or voter’s registration card or passport size photograph should send the missing documents to the Board with a covering letter indicating their full names and form four index numbers through the following address:


  The Executive Director,
  Higher Education Students’ Loans Board,
  P. O. Box 76068
  ,
  DAR ES SALAAM.


  Please note that, the deadline for correction of the shortcomings is 10thSeptember 2014.  All attachments must be certified by a Commissioner of Oaths. *The list of loan applicants who are required to correct their loan applications can be viewed through HESLB Website: www.heslb.go.tz 

  NB:       The Board cautions loan applicants to be careful with some unscrupulous individuals who might take advantage of this opportunity to make financial demands.

   Issued by:
  Executive Director            


  HIGHER EDUCATION STUDENTS’ LOANS BOARD


  0 0

   Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Kebwe Steven Kebwe (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Afya na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Afya na Ustawi Dkt. Elias Chinamo moja ya kifaa (kamera) itakayotumika kupima dalili za ugonjwa wa Ebola kwa wasafiri wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege ili kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa salama kwa kuuzuia ugonjwa huo kuingia nchini.
   Mkurugenzi wa Ugavi wa Bohari ya Dawa Tanzania (MSD),Heri Mchunga (kushoto)  akimpima Mkurugenzi wa Afya na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Afya na Ustawi Dkt. Elias Chinamo (kulia) kuonyesha namna moja ya kifaa cha kupimia joto la mwili wa Binadamu kinavyofanya kazi kwa kubaini dalili za Ugonjwa wa Ebola eneo la uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
   Moja ya kifaa (kamera) nne zilizoagizwa na Serikali kupimia dalili za ugonjwa wa Ebola maeneo ya viwanja vya ndege. Kifaa  hicho kina uwezo wa kutunza picha na kumbukumbu za msafiri, muda , joto la msafiri, tarehe aliyoingia nchini pia uwezo wa kupata takwimu kutoka kwenye hali ya majimaji au jasho la Binadamu pindi kinapoelekezwa kwake.
   Naibu Waziri wa Afya Dkt. Kebwe Steven Kebwe akiongea na waandishi wa habari eneo la uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa kupokea na kukabidhi vifaa vya kupima dalili za ugonjwa wa Ebola. Wengine ni Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Dharula na Maafa (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifani.
  Naibu Waziri wa Afya Dkt. Kebwe Steven Kebwe akiangalia kwa karibu taarifa zilizorekodiwa na moja ya kifaa (kamera) nne zilizoagizwa na Serikali kupimia dalili za ugonjwa wa Ebola maeneo ya viwanja vya ndege. Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

  0 0


  0 0


  Tanzania’s towering Goal Shooter (GS) Mwanaidi Hassan prepares to slot home one of her many attacks as they mauled Burundi 113-10.
  ----------------------------
   Hosts and defending champions Tanzania made a flying start in the eighth edition of the EAC military netball competition with smashing 113-10 win over Burundi at the JKU ground in Zanzibar yesterday.

  Tanzania’s towering Goal Shooter (GS) Mwanaidi Hassan was a thorn in Burundi’s defence .Burundi’s Goalkeeper Mutoni Bertiel was completely overshadowed by Mwanaidi’s swift and accurate goals.
  In another netball match, Uganda walloped Rwanda 30-12.

  In soccer, a second half early goal by Brian Birgen gave Kenya 1-0 victory over hard-fighting Uganda. Both teams displayed brilliant soccer skills and all made several near misses until in the 53rd minute when striker Birgen sealed Uganda’s fate.

  In the opening match on Wednesday, Tanzania whipped Burundi 3-1. In Hanball, Uganda and Kenya fought a 26-26 draw in a close and exciting tussle. Uganda had taken an early lead of 17-8 against Kenya. However, the never-say-die Kenyans came back like injured buffaloes in the second half and leveled the score and even went ahead by 26-25 in the dying minutes. The Ugandans did not give and managed an injury time equalizer.

  Kenya’s goal star was Nicholas Ireri with eight shots whereas for Uganda were Mohamed Suleiman and Alworanga Chester with six goals each to their credit.In Basketball, Tanzania defeated Rwanda 67-56 in another thrilling match and Burundi defeated Kenya 45-41.

  The two-week EAC military games will climax on 31 October. This year’s theme is:” Is one people, one destiny through EAC Military Games and Cultural Event 2014”.


  0 0

   Mwanamuziki Mkongwe hapa nchini,almaarufu kama Mzee Njenje akizungumza machache mbele ya wasanii mbalimbali wa bongofleva waliofika nyumbani kwake Sahare,nje kidogo ya jiji la Tanga,kumjulia hali kutokana na maradhi yake yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda sasa.

  Mzee Njenje amewaasa wasanii hao ambao amekiri wazi kuwa wanafanya vizuri katika anga ya muziki wao,kupata muda mwingi wa kupumzika ikiwemo na suala la kutoendekeza masualaua ya anasa kama vile ulevi,ngono na mengineyo ambayo huchangia kuporomoka kwa wasanii wengi,amesema kuwa Muziki wa sasa una ushindani mkubwa hivyo kila msanii anapaswa kujituma kwa namna anayoona inafaa ili kutimiza malengo yake sambamba na kuitangaza nchi kwa ujumla.
   Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya,Rachael na Linah wakiwa wamepozi katika picha ya ukumbusho na Mzee Njenje.
   Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya,Alli Kiba akizungumza jambo na Mzee Njenje. 
  Mzee Njenje akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya watakaotumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Fiesta 2014 linalofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga,Wasanii hao walikwenda kumsabahi mkongwe huyo wa Muziki hapa nchini,Nyumbani kwake Sahare,nje kidogo ya jiji la Tanga ambako ndiko anaendelea kupata matibabu yake ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda sasa,Mzee Njenje amesema kuwa kwa sasa anamshukuru Mungu anaendelea vizuri na afya yake inazidi kuimarika kadiri ya siku zinavyozidi kwenda.  
   Baadhi ya Wasanii mbalimbali ambao Watatumbuiza kwenye tamasha la Fiesta jioni ya leo ndani ya uwanja wa Mkwakwani ,wakiwasili nyumbani kwa Mzee Njenje,Sahare,nje kidogo ya jiji la Tanga kumjulia hali.Picha zote na Michuzi Jr-FIESTA TANGA

  0 0

   CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akijiandaa kumtawaza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo katika sherehe za aina yake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Kinole, kata ya Makuyuni, Morogoro vijijini Agosti 22, 2014.  Rais Kikwete pia alipewa jina la CHIDUKILA, lenye kumaanisha "muibukaji", kwa maana ya kwamba Rais Kikwete ana uhuru wa kuibuka kijijini Kinole bila taarifa wala kusubiri kualikwa.
   CHIFU wa Waluguru Kingalu Mwanabanzi wa 14, akimvipa pama lililosukwa kwa ukindu  Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kumtawaza kuwa Chifu Msaidizi wa kabila hilo.
   Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akifurahia wakati wa sherehe hizo.
   Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akiongea na wananchi wakati wa sherehe hizo
   Chifu Msaidizi wa Waluguru Chidukila akihutubia  wakati wa sherehe hizo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na John Gagarini, Kibaha

  JESHI la Polisi mkoani Pwani linawashikilia raia 48 wa nchi ya Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini bila ya kibali.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha Kaimu kamanda wa Polisi mkoani humo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Athuman Mwambalaswa alisema kuwa watuhumiwa hao walitelekezwa vichakani.

  Kamanda Mwambalaswa alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 21 mwaka huu majira ya saa 7 usiku katika Kijiji cha Visakazi Ubena Zomozi tarafa ya Chalinze wilayani Bagamoyo.

  Alisema kuwa Wethiopia hao waligunduliwa na askari Magereza wa Gereza la Ubena aitwaye Sospeter ambaye aliwakuta porini alipokuwa akifanya shughuli zake na kutoa taarifa polisi.

  "Kati yao 11 wanaumwa na wamepelekwa kituo cha afya cha Chalinze kwa ajili ya matibabu baada ya kuonekana wakitapika baada ya kupewa chakula na walionekana wakiwa na hali mbaya ya kiafya huku wale wengine wakiwa wamehifadhiwa kwenye kituo cha polisi cha kiwilaya," alisema Kamanda Mwambalaswa.

  Aidha alisema kuwa raia hao wa Ethiopia wanakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 20 na 40 na wanatarajiwa kukabidhiwa idara ya Uhamiaji kwa ajili ya taratibu zingine ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma zinazowakabili.

  Wakati huo huo mtu mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja mwenye umri unaokadiriwa kuwa kati ya (25) na (28) amekufa kwa kujinyonga kwa kutumia kamaba ya katani.

  Alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 22 mwaka huu majira ya saa 2 usiku Kijiji cha Kibiki kata ya Bwiringu Tarafa ya Chalinze.

  "Mfanyakazi wa shambani wa mwenyekiti wa Kijiji hicho alimpa taarifa bosi wake aitwaye Ally Hussein (47) kuwa kuna mtu kajinyonga kwenye banda lake ambaye naye alitoa taarifa polisi kuhusiana na tukio hilo," alisema kamanada Mwambalaswa.

  Aliongeza kuwa marehemu aliacha ujumbe amabo uliandikwa kwenye karatasi kuwa anawaachia dunia ili waishi miaka 120, hakuna mtu aliyekamatwa na polisi wanaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.

older | 1 | .... | 546 | 547 | (Page 548) | 549 | 550 | .... | 3272 | newer