Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 545 | 546 | (Page 547) | 548 | 549 | .... | 3285 | newer

  0 0

  East African Legislative Assembly, Arusha, August 21, 2014: The East African Legislative Assembly (EALA) resumes business next week holding its Plenary in Karimjee Hall, Dar es Salaam. The Plenary which takes place from Wednesday, August 27th 2014, through to Thursday, September 4, 2014, is the 1st Meeting of the 3rd Session of the 3rd Assembly.
    
  President Jakaya Mrisho Kikwete is expected to address a Special Sitting on Wednesday, August 27, 2014.  

  The Assembly to be presided over by the Speaker, Rt. Hon Dr. Margaret Nantongo Zziwa, shall during the two-week period discuss matters of legislative business. The Sitting expects to debate on the following Bills and reports:


  • The EAC Integration (Education) Bill, 2014 (2nd & 3rd Reading)
  • receive and consider reports from various Committees of the Assembly.  The Reports include that of the Committee on Regional Affairs and Conflict Resolutions and the African Leadership Centre on East African Societies and Regional Security; Report of the Committee on Agriculture, Tourism and Natural Resources on Regional Parliamentarians’ Workshop on Forests and Climate Change and Report of the Committee on Communication, Trade and Investment on the EAC Aviation Sector.  Other reports include that of the Committee on General Purpose on the capacity building workshop on the legislative process of bills, Report of the Committee on Legal Rules and Privileges and the report of the Committee on Accounts on EAC Audit Process.
  • consider Motions and Questions brought before the House.

  EALA shall also prior to the Plenary hold a Retreat of the Commission and one for the Whole House.  The said Retreats shall be held on August 22-23, 2014 and August 24-26, 2014 respectively. The Assembly shall also seize the moment to visit various stakeholders and to sensitise citizens.  

  EALA is expected to visit the IPP Media on August 22, 2014.  The visit to the IPP Media is expected to set the basis for collaboration and enhance partnership between both organizations.   It further hopes to create sustained networking between media and legislators thus popularizing the integration agenda.

  Other institutions to be visited include the Tanzania Ports Authority on August 29th, 2014. and the Taasisi ya Sanaa na Utamaduni – TASUBA (Institute of Arts and Culture) in Bagamoyo on August 30th, 2014. The visits are expected to enhance the collaboration between EALA and the stakeholders in question.

  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa Kamati Namba 11 ya Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Hamad Yussuf Massauni akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo kwenye ukumbi wa mikutano wa St. Gasper kuhusu mambo yaliyojiri katika Kamati yake.Kulia ni Katibu wa Kamati hiyo Bakari Kishoma.
  Baadhi wa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wa Kamati Namba 11 wakiwa wanaendelea na kikao cha Kamati hiyo mjini Dodoma leo kwenye ukumbi wa mikutano wa St. Gasper.
  Mwenyekiti wa Kamati Namba Moja ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Ummy Ali Mwalimu(katikati) akizungumza na akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo kwenye ukumbi wa mikutano wa St. Gasper kuhusu mambo yaliyojiri katika Kamati yake.Kulia ni Makamu wake ,Profesa Makame Mbarawa na kushoto ni mjumbe wa Bunge hilo, Ali Kessy.
  Baadhi wa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wa Kamati Namba Moja wakiwa wanaendelea na kikao cha Kamati hiyo mjini Dodoma leo kwenye ukumbi wa mikutano wa St. Gasper.

  0 0


  0 0

   NANI kati wa washiriki 17 ataibuka kuwa mshindi wa shindano la Redd's Miss Temeke 2014, linalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa TCC Club Chang'ombe Dar es Salaam.

  Jumla ya warembo 17 kutoka vitongoji vya Mbagala, Kurasini na Chang;ombe watapanda jukwaani kuwania taji hilo, huku washindi wa tatu watapata nafasi ya kushiriki shindano la Miss Tanzania mwaka 2014.

  Akizungumza Dar es Salaa jana Mkurugenzi BMP Promotions, Benny Kisaka, alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yamekamilika kama yalivyopangwa.

  Kisaka alisema kuwa taji linaloshikiliwa na mrembo kutoka kanda ya kati, lakini mwaka huu Temeke imejizatiti kutoa si tu Miss Tanzania, mbali warembo watatu wa kwanza wa Taifa kutokana na viwango vya warembo wa mwaka huu.

  Alisema kuwa mbali ya shindano hilo kubwa, kulifanyika shindano dogo la awali lililoandaliwa na Michuzi Media la Miss Photogenic ambalo mshindi wake atazawadiwa kitita cha Sh. milioni 1 taslimu, shindano ambalo lililsimamiwa na jopo la wapiga picha wa kampuni hiyo ambao watamtangaza na kumpa zawadi mshindi siku ya shindano.

  Kisaka aliwataja Warembo wanaotarajiwa Subira Ally, Hellen Yughin, Catherine Alex, Dalina David, Winfrida Guntram, Salama Salehe, Grace John, Lilian Lothy, Amina Salim, Rebecca Mdamu, Sitti Mtemvu, Hellen Sule, Neema Mollel, Lucy Lewis, Esther Mnahi, Pauline Nkini na Patricia Ponsian ambao walikuwa chini ya ukufunzi wa Super Bokilo, Shadya Mohamed na Sweet Remmy.

  Alisema mkali wa bongofleva, Khalid Mohamed TID almaarufu kama Top in Dar, sanjari na Wanne Star, Makirikiri wa Tanzania, Young Suma, Super Bokilo na wasanii mbalimbali wanatarajia kupamba shoo hiyo ambayo Dj John Peter Pantelakis atalisindikiza.

  Wadhamini wa shindano hilo ni TBL Kupitia Redds wamedhamini shindano hilo sanjari na kinywaji cha Zanzi, Michuzi Media Group, Radio EFM 93.7 Cash & Carry Distributors, Kitwe General Traders, Rio Gym & Spa, CXC Africa, 88. 5 Clouds FM, City Sports Lounge, Gazeti la Jambo Leo, Kiwango Security na 100.5 Times FM.

  BMP Promotions imeshakamilisha shindano hili la 19 tangu kuanzishwa Miss Temeke chini ya undaaji wake kwa asilimia kubwa, hivyo washabiki wa Kanda ya Temeke na vitongoji vyake watarajie mabadiliko makubwa katika aina ya shindano la urembo litakavyokuwa Ijumaa.

  1996- Asela Magaka
  1997- Miriam Odemba
  1998- Khamisa Ahmed (Miss Temeke anayeendea kujiita hivyo huko Marekani)
  1999- Ediltruda Kalikawe
  2000- Irene Kiwia
  2001- Happyness Sosthnes Magesse
  super model Millen( Miss Tanzania)
  2002- Regina Mosha
  2003- Hawa Ismail ( Sylvia Bahame first runner up and Miss Tanzania same year)
  2004- Cecylia Assey ( mrs Agrey Marealle), first runner up Miss Tanzania
  2005- Seba Aggrey
  2006- Jokate Mwegelo (Miss Tanzania fisrt runner up), Irene Uwoya 1st runner Temeke & 3rd runner up Miss Tanzania
  2007- Queen David ( Miss Tanzania second runner up)
  2008- Angela Lubala (top five Miss Tanzania)
  2009- Sia Ndaskoy (top five Miss Tanzania)
  2010- Genevieve Mpangala ( Miss Tanzania)
  2011- Husna Twalib
  2012- Edda Sylvester
  2013- Svetlana Nyameyo ( Latifa Mohamedsecond runner Temeke and first runner up Miss Tanzania)

  0 0

  RATIBA YA KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MWENYEKITI MSTAAFU WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI   MHE. JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA YA RUFANI LEWIS MAKAME KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE TAREHE 22 AGOSTI, 2014.


  MUDA

  TUKIO

  MHUSIKA

  3.00- 3.30 ASUBUHI

  WANANCHI NA WATUMISHI KUWASILI

  KAMATI YA MAZISHI

  3.30 – 4.00 ASUBUHI

  VIONGOZI WASTAAFU, MAWAZIRI, MAJAJI WASTAAFU , VIONGOZI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI, SERIKALI, TAASISI NA VYAMA VYA SIASA KUWASILI

  KAMATI YA MAZISHI

  4.00 -4.15 ASUBUHI

  WAH. MAJAJI WA MAHAKAMA KUU KUWASILI

  KAMATI YA MAZISHI

  4.15 – 4.20 ASUBUHI

  MHE. JAJI KIONGOZI


  KAMATI YA MAZISHI

  4.20 – 4.25 ASUBUHI

  MAHAKAMA YA RUFANI KUWASILI

  KAMATI YA MAZISHI

  4.25 – 4.30 ASUBUHI

  JAJI MKUU KUWASILI

  KAMATI YA MAZISHI

  4.30 – 4.40 ASUBUHI

  SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO KUWASILI

  KAMATI YA MAZISHI

  4.40  - 4.45 ASUBUHI

  MHE. WAZIRI MKUU KUWASILI

  KAMATI YA MAZISHI

  4.45  - 4.50   ASUBUHI

  MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUWASILI

  IKULU/ KAMATI YA MAZISHI

  4.50 – 5.00 ASUBUHI

  MHE. RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUWASILI

  KAMATI YA MAZISHI

  5.00 – 5.05  ASUBUHI

  MWILI WA MAREHEMU KUWASILI

  KAMATI YA MAZISHI  5.05 – 5.10 ASUBUHI

  SALA


  5.10 – 5.20

  WASIFU WA MAREHEMU

  MWANAFAMILIA

  5.20 – 5.30 ASUBUHI

  NENO KUTOKA KWA CHAMA CHA MAJAJI WASTAAFU

  MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAJAJI WASTAAFU, MHE. JAJI MIHAYO

  5.30 -5.40

  NENO KUTOKA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

  MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI MHE. JAJI LUBUVA

  5.40 -5.50 ASUBUHI

  NENO KUTOKA KWA MHE. JAJI MKUU

  MHE. JAJI MOHAMED CHANDE OTHMAN

  5.50 – 6.00 ASUBUHI

  NENO KUTOKA KWA MHE. RAIS

  MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE

  6.0 -6.10 MCHANA

  NENO LA SHUKURANI

  MSEMAJI WA FAMILIA

  6.10 MCHANA  6.50 MCHANA

  KUAGA

  KAMATI YA MAZISHI

  6.50 -7.00 MCHANA

  KUWASILI KANISANI – ST. ALBAN - UPANGA

  KAMATI YA MAZISHI

  7.00 MCHANA  - 9.00 ALASIRI

  MISA YA KUMUOMBEA MAREHEMU


  9.00 ALASIRI

  KUONDOKA KUELEKEA MUHEZA - TANGA

  KAMATI YA MAZISHI


  0 0

   Mtangazaji wa michezo wa E FM 93.7 Maulid Kitenge akiwa na Gwiji wa zamani wa Real Madrid Luis Figo alipowasili usiku huu jijini Dar es salaam na wachezaji wenzie nyota wa zamani wa timu hiyo ya Hispania ambayo Jumamosi itakipiga na wachezaji nyota wa Tanzania kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uwanja wa Taifa


  0 0

  Mratibu wa Ziara ya Wachezaji wa Zamani wa Timu ya Real Madrid,Ssebo (wa tatu kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mechi ya kirafiki kati ya Tanzania Eleven na Timu ya Wachezaji wa Zamani wa Real Madrid kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kesho.Mpaka sasa ni wachezaji watatu tu ndio waliowasili nchini huku wengine kadhaa wakitegemewa kuwasili mchana wa leo.Wachezahi hao ambao wapo nchini hivi sasa ni Luis Figo (wa tatu kulia),Christian Karembeu (kulia) na Beki Fernando Sanz Duran (wa pili kushoto).wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya TSN,Farough Baghoza na Kocha wa Timu ya Tanzania Eleven,Jamhuri Kihwelo "Julio"
  Kocha wa Timu ya Tanzania Eleven,Jamhuri Kihwelo "Julio" (katikati) akizungumzia namna Timu yake ilivyojiandaa kuwakabili Wakali hao wa soka Duniani wakati wa Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye Hoteli ya SouthernSun jijini Dar es Salaam.Kulia ni Luis Figo na kushoto ni Fernando Sanz Duran ambao ni wachezaji wa zamani wa timu ya Real Madrid ya nchini Hispania.
  Mchezaji Kiongozi wa Timu ya Wachezaji wa Zamani wa Real Madrid,Luis Figo akizungumza na Waandishi wa habari juu ya ujio wao hapa nchini.Figo amewaahidi wa Tanzania kuwa yeye na Wenzake watatoa burudani kabambe katika Uwanja wa Taifa jijini Dar hapo kesho.
  Mchezaji Fernando Sanz Duran (kati) nae akitoa maneno yake kuhusu mchezo huo.
  Mwanasoka Christian Karembeu akizungumza.

  0 0

    Waheshimiwa Wabunge walioitwa kusikiliza ajenda ya mtoto na kuhakikisha inaingia katika mchakato wa katiba.

  kamati kuu la Baraza la watoto limekutana mjini Dodoma chini ya Uongozi wa mwenyekiti wake Ummy Jamaal kutoa tamko la watoto kwa waheshimiwa wabunge na waandishi wa habari wakitoa msisitizo wa ajenda ya mtoto kuwa sehemu ya mchaakato wa katiba.

  Jambo kubwa walilosisitiza ni kuwaomba Ukawa warudi bungeni ili kumalizia mchakato wa kutengeneza katiba.
  Mheshimiwa Sophia Simba, waziri wa maendeleo ya jamii, Jinsia na watoto akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati kuu ya baraza la watoto waliokaa pamoja Dodoma na kutoa Tamko lao mbele ya waandishi wa habari na baadhi ya waheshimiwa wabunge.

  0 0
 • 08/22/14--04:01: Article 22


 • 0 0

  Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Bwana Sunil Colasa akiongea na waandishi wa habari leo hii (hawapo pichani) akiwatangazia kuanza kutumika rasmi kwa huduma mpya ya kutuma na kupokea pesa kutoka kwenye mitandao mingine moja kwa moja kwenye akaunti  zao za Airtel money, (interoperability) huduma hii ni ya kwanza Duniani ambapo inaaminika kuwa itasaidia sana wateja wa Airtel Money na Wakala kuokoa muda wa kupata na kutoa huduma kwa haraka Zaidi. 
  ===========  ==========
  • Wateja Airtel Money sasa wanaweza kutuma na kupokea pesa kwenye akaunti zao za Airtel Money toka Tigo Pesa
  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua huduma itakayowawezesha wateja wake wa huduma ya Airtel Money kutuma na kupokea pesa kutoka kwenye mitandao mingine moja kwa moja kwenye akaunti  zao za Airtel money ,  huduma hii ni ya kwanza Afrika na duniani kwa ujumla na hivyo inaweka historia nchini kuzinduliwa ya kwanza kupitia njia ya  mtandao wa simu.

  Huduma hii ya kwanza Duniani na Afrika inayohusisha makampuni ya simu Airtel na Tigo ulitangazwa kuwa itaanza kutumika mwishoni mwa mwezi wa Julai na sasa iko tayari ambapo wateja wa Airtel Money  wataweza kutumia  huduma hii kabambe na yenye utofauti kwa inaaminika kuwa ni  rahisi zaidi, salama na ina unafuu katika kutuma pesa kwa kutoka mteja mmoja kwenda mwingine na kuingia moja kwa moja katika (e-wallet) akaunti yake ya simu/mtandao anaotumia na kuweza kuitoa popote alipo.

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Mkurugenzi wa Airtel Bwana Sunil Colaso alisema” Tunayofuraha kushirikiana na makampuni mengine ya simu katika kuhakikisha tunaendelea kutoa huduma za kisasa, zenye ubunifu na kwa gharama nafuu. Ushirikiano huu utawawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa kutoka kwenye mitandao mingine .  sasa wateja wetu watapokea pesa kutoka kwenye mitandao mingine na kuingia moja kwa moja kwenye (e-wallet) akaunti  zao za Airtel money hivyo kuondoa usumbufu ulikuwepo awali  ambapo mteja anapotumiwa pesa kutoka mtandao mwingine alitakiwa kuzitoa ndani ya siku 7.

  Kwa uzinduzi huu  leo tunafanya huduma hii ya kifedha kwa njia ya mtandao kukidhi mahitaji ya wateja. Vile vile mawakala wetu pia wamerahisishiwa utoaji huduma  ambapo sasa hakutakuwa na haja ya wakala kupata udhibitisho wa ujumbe kutoka kwa simu ya mteja kabla ya kufanya malipo.  Tunaamini huduma hii itaongeza usalama wa mawakala na wateja nchini, Pia itamuongezea wakala muda wa kuhudumia wateja wengi Zaidi kwa uhakika, haya ni mapinduzi ya huduma za kifedha ambayo tunaamini ni maendelea makubwa ya maboresho ya huduma hii aliongeza kwa kusema Colaso.

  Akiongea kuhusu huduma hiyo mmoja wa wakala ambae alijaribu wa Airtel Money Pasco Woiso alisema “Tunafurahia huduma iliyoanzishwa na Airtel kwa kushirikiana  na mitandao mingine,  leo nimeitumia huduma hii kwa mara ya kwanza lakini nimefurahishwa na ufanisi wake na jinsi wateja wanavyoipokea vizuri nikiwapasha habari kuhusu huduma hiii.  Kwa sisi wakala awali tulikuwa na tatizo la kupata ujumbe wa malipo, kitambulisho cha malipo na pesa kurudi baada ya muda wa siku saba,  lakini kwa sasa ushirikiano huu umeifanya huduma hii ya pesa kwa mtandao kuwa bora zaidi na kupunguza muda niliokuwa nautumia kumuhudumia mteja moja na hivyo


  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, , Yamungu Kayandabila akionyesha mbegu za mahindi zilizohifadhiwa kwenye ghala aina ya Silo, wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la wadau wa kusimamia upotevu wa nafaka baada ya kuvunwa. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, , Yamungu Kayandabila akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la wadau wa kusimamia upotevu wa nafaka baada ya kuvunwa.
   Baadhi ya washiriki wa uzinduzi wa jukwaa hilo.
   Mmoja wa wadau wa kilimo akichangia mada katika uzinduzi wa jukwaa la kusimamia upotevu wa nafaka baada ya kuvunwa.
   Ghala la kuhifadhia chakula aina ya Silo.


  SERIKALI kupitia Wizara ya kilimo, Chakula na Ushirika imekili uwepo wa tatizo la upotevu wa mazao hasa jamii ya Mikunde na Nafaka ambalo ni tatizo kubwa, linalowakumba wakulima na wafanyabiashara kwa ujumla.

  Akizungumza katika uzinduzi wa jukwaa la wadau watakaoangalia mazao mara baada ya kuvunwa jana, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Yamungu Kayandabila alisema, hata wizara yake inalitambua suala hilo, na imeanza harakati za kupambana na janga hilo, hasa kwa kuwaamasisha wakulima na wauzaji kutunza mazao hayo katika maghara.

  “Tatizo la upotevu wa mazao ni tatizo kubwa, na hilo linachangiwa na uhifadhi duni ambapo zaidi ya asilimia 30 utokea katika upotevu wa mazao hayo,”alisema Kayandabila.

  Kayandabila ambaye alikuwa mgeni rasm katika uzinduzi wa jukwaa hilo ulioandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Ansaf, aliipongeza taasisi hiyo kwa jitihada ambazo wanazionyesha katika kukomesha tatizo hilo, huku pia akiyataka mashirika, taasisi mbalimbali kuiga mfano wa Ansaf.

  “Tunawashukuru sana Ansaf kwa kufanya uzinduzi huu, na naimani taasisi na mashirika mengine yatafuata nyayo zao katika kutokomeza suala hili la upotevu ili wakulima na wafanya biashara waweze kuzihifadhi vizuri,”alisema Kuyandabila na kusema kuwa Serikali pekee haiwezi bila ya sapoti ya watu kama wao.

  Naye Katibu Mtendaji wa Ansaf, Audax Rukonge alisema, wamegundua changamoto mbalimbali juu ya mazao hayo, ambazo uwakumba wakulima na wafanya biashara kwa ujumla na hiyo ndiyo sababu iliyowafanya kuzindua jukwaa hilo.

  Naye mmoja wa wajumbe walioudhulia uzinduzi huo, Lusekelo Mwandemange ambaye ni mkulima wa zao la Mpunga kutoka Kyera, alisema, amefarijika kupata nafasi hiyo, huku akiwataka Ansaf kuhakikisha wanatoa elimu zaidi kwa wakulima walioko Mikoa mbalimbali.

  0 0

  Na Josephat Lukaza

  Msanii wa Muziki wa Dansi anayejulikana kama Christian Bella anayetamba na kibao chake cha Nani Kama Mama ni Mmoja wa Wasanii watakaotoa Burudani ya Kufa mtu katika Ukumbi wa Mlimani City Siku ya Jumamosi Tarehe 30 katika Fainali kubwa ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT).

  Bella Amehaidi kutoa Burudani ya uhakika ambapo wapenzi wa muziki wake watafurahi na kufurahishwa na show atakayoitoa siku hiyo katika Fainali ya Kumkabidhi Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.

  Katika Fainali hiyo inayotarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Siku ya Jumamosi tarehe 30 huku viingilio vya Kuja kutazama fainali ya Kwanza kubwa vikiwa ni V.I.P Shilingi 50,000 na Kawaida 30,000 huku fainali hiyo ikirushwa live kupitia Kituo cha Runinga cha ITV na milango itakuwa wazi kuanzia Saa 7.30 Usiku.

  Tanzania Movie Talents (TMT) ni shindano la Kwanza kufanyika Afrika Mashariki na Kati ambalo limeanzishwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd likiwa na lengo la Kuibua na Kusaka Vipaji vya kuigiza kwa watanzania ambao wana vipaji lakini walikosa fursa ya kuonekana. 

  TMT ilianza Rasmi tarehe 1 April 2014 katika Mkoa wa Mwanza, Kanda ya Ziwa ambapo baadae shindano likaendelea katika Kanda nyingine Tano huku katika Kila Kanda Washindi walikuwa ni watatu huku kanda ya Pwani washindi walikuwa Ni 5 ambapo jumla ya Washindi 20 walipatikana na kuletwa Dar Es Salaam katika kambi na Hatimaye Mchujo kuanza na Kubakiwa na Washiriki 10 ambao leo hii wameingia Fainali ya kuzisaka zile Milioni 50 za Kitanzania.

  Katika Fainali hiyo Kubwa kutakuwa na Burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.Sikiliza Moja ya Nyimbo atakazoimba Live Stejini Siku Hiyo ya Fainali.

  0 0

  Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue akitoa nasaha zake kwa wanafunzi (watanzania) waliopata udhamini kamili wa masomo nchini Uholanzi wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jaap Frederiks akitoa hotuba yake kwa wanafunzi (watanzania) waliopata udhamini kamili wa masomo nchini Uholanzi wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wanafunzi waliopata udhamini kamili wa masomo nchini Uholanzi wakisikiliza kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
  Makamu Mkuu wa Misheni ya Uholanzi, Bi. Hinke Nanta (kushoto) akijadiliana jambo na Katibu Mkuu Kiongozi (katikati) wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
  Wanafunzi wakitanzania waliopata udhamini kamili wa masomo katika vyuo mbalimbali nchini Uholanzi wakifurahi kwa pamoja wakiwa na wageni wegine waalikwa pamoja na mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Benedict Liwenga-MAELEZO).

  0 0

  Wakala wa Usajili,Ufilisi na Udhamini (RITA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) itafanya tathmini ya mfumo wa usajili wa matukio muhimu ya maisha na ukusanyaji wa takwimu nchini.

  Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA,Bw. Phillip Saliboko  alisema Tathimini hiyo itafanyika kikanda kwa siku 15 kuanzia tarehe Septemba 15 - 30, 2014 na kujumuisha wadau wakubwa wa mambo ya usajili kutoka kwenye baadhi ya Wizara,Taasisi ,Idara Vyuo vikuu na Wakala wa Serikali huku ikijikita zaidi katika kuangalia matukio makuu manne ambayo ni vizazi, vifo na sababu zake,ndoa na talaka.

  Matokeo ya tathimini hiyo itatumika kuisaidia Serikali kutekeleza mikakati yake ya kurekodi na kutunza taarifa hizo muhimu badala ya kutegemea Sensa peke yake ambayo hata hivyo huchukua muda mrefu kufanyika huku matukio hayo yakitokea kila siku na kuhitaji kufanyiwa kazi.

  Jitihada za kuanzisha mfumo huo barani Afrika zilianza mwaka 2008 wakati Mh. Dkt Asha-Rose Migiro (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria alipokuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia wakati huo akiwa kama Mwenyekiti wa Kikao cha tathimini ya malengo ya maendeleo ya milenia kwa kundi la Afrika.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA,Bw. Phillip Saliboko akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi kwenye Ukumbi wa Mikutani wa RITA,kuhusu Tathimini ya kuwezesha kupatikana kwa mfumo thabiti wa usajili wa matukio muhimu ya maisha na ukusanyaji wa takwimu.Kushoto Meneja wa Usajili wa Vizazi na Vifo,Bi.  Angela Anatory na kulia ni Meneja Masoko wa RITA,Bw. Josephat Kimaro.

  Meneja wa Usajili wa Vizazi na Vifo,Bi.  Angela Anatory akizungumza na Waandishi wa habari katika Mkutano huo uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi za RITA,Upanga jijini Dar.Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA,Bw. Phillip Saliboko.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimian na Mawaziri Wakuu, Wastaafu, Frederick Sumaye na Jaji Joseph Warioba (wapili kulia) kabla ya kuzungumza kwa niaba ya serikali na kutoa heshima za mwisho kwa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, marehemu Jaji Lewis Makame kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014. Kulia nI jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na jaji Mkuu Mohamed Chande Othman (kulia) na Mawaziri Wakuu Wastaafu, Joseph Warioba (wapili kulia) na Frederick Sumaye kabla ya kutoa salamu za Serikali na heshima za mwisho kwa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, marehemu Jaji Lewis Makame kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole Jaji Leila Makame Mgonya mmoja wa wana familia, wa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Marehemu Jaji Lewis Makame baada ya kuzungumza kwa niaba ya serikali na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu huyo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Marehemu Jaji Lewis Makame baada ya kuzungumza kwa niaba ya serikali kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Jeneza lenye mwili wa Marehemu aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame likiwa mbele ya viongozi wa Serikali, ndugu, jamaa na marafiki kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda akisaini kitabu cha maombolezo wakati wa kuuaga mwili wa Marehemu aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

  Viongozi mbalimbali wa Serikali wakilisikiza wasifu wa marehemu aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Ndugu, jamaa na marafiki wakiwa na nyuso za uzuni wakati wa kuuaga mwili wa Marehemu aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Mmoja wa wafiwa akilia kwa uchungu wakati akiuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri wa Maendeleo Jamii Jinsia na Watoto Mh Sophia Simba akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mwanamke na uchumi iliyo andaliwa na NGO ya Angels Moment Co. ltd kwa ajili ya kumkomboa mwanamke wa Kitanzania uzinduzi huo umefanyika katika Hotel ya Dodoma.
  Mkurugenzi wa Angels Moment co. ltd Naima Malima akisoma risala ya kuelezea madhumuni ya uzinduzi wa kampeni ya mwanamke na uchumi sherehe hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wabunge na pamoja na baadhi ya Mawaziri
  Burudani kidogo mara baada ya kufanyika kwa uzinduzi.
  Waziri wa Maendeleo Jamii Jinsia na Watoto Mh Sophia Simba akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi mzima kwa Angels Moment co. ltd mara baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya mwanamke na uchumi,iliyofanyija jana mjini Dodoma.


  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa Morogoro.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA Bw. Ronald Phiri zawadi ya picha ya jengo la makao makuu ya TAZARA akiwa ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa Morogoro.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na viongozi wengine ndani ya behewa maalum la VIP la treni la TAZARA wakati wa safari ya Rais Kikwete kuelekea Kisaki katika ziara yake ya mkoa wa Morogoro.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika kituo cha Kisaki baada ya kusafiri kwa treni katika ziara yake ya Mkoa wa Morogoro.


  0 0

  Washindi watatu wa kwanza wa Miss Temeke wanaopanda jukwaani TCC Club Chang'ombe leo Ijumaa August 22,watazawadiwa trip ya 3 nights kwa naana 4 days kufanya shopping ya Miss Tanzania jijini Johanesburg Afrika kusini wakilipiwa kila kitu.


  0 0

  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewashauri albino wanaoishi Jijini Dar es Salaam kuwa karibu sana na Jeshi hilo ili kurahisisha mawasiliano kati yao na Wakuu wa vituo vya Polisi vilivyo karibu na makazi yao au wanapofanyia usalama wao jijini Dar es Salaam.

  Pamoja na kwamba haijawahi kutoa tukio lolote dhidi ya Albino jijini Dar es Salaam kutokana na uhusiano uliopo lakini kwa sasa waongeze mawasiliano na Jeshi la Polisi kutokana na taarifa za uhalifu dhidi ya Albino katika baadhi ya mikoa hapa nchini.

  Pia Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam SULEIMAN KOVA ameongea na Albino hao ofisini kwake na kuwaambia kwamba Jeshi la Polisi kwa ujumla linaendelea na jitihada kubwa sana kupambana na maadui wa Albino ambao ni wahalifu na wengi wao wameishakamatwa na kufikishwa mahakamani ambapo wengine wameishahukumiwa.

  Albino wanatakiwa kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu na Jeshi la Polisi hata kama hakuna tishio la aina yoyote wanalolijua katika maeneo yao ya makazi au wanapofanya shughuli zao za kikazi.

  Katika kufanikisha zoezi hilo la mawasiliano ya haraka na Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi Kanda Malum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na wadau kampuni ya SAPNA ELECTRONIC ametoa simu 20 kwa Albino ambao wameudhuria kikao ili iwe rahisi kwao kuwasiliana Jeshi la Polisi kwa namba 0787-668306 ambayo ipo katika chumba cha dharura katika Kikosi cha 999.

  Kamishna Kova anaendelea kuongea na wadau mbali mbali ili misaada zaidi ipatikane kwa walemavu wa ngozi ambao ni Albino ili waweze kupata simu za mikononi, mafuta maalum ya kupaka ngozi zao na msaada mwingine wowote ambao utafaa kwa Albino hao kupitia kwa namba 0715 – 009983 hii ni namba ya Kamishna mwenyewe ya oisi na namba nyingine ya Msaidizi wake katika suala la kuwasaidia Albino ni 0756-710179 ambayo ni ya SP. MOSES NECKEMIAH FUNDI.

  Aidha zipo jitihada za makusudi zinazofanyika kati ya Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam na uongozi wa Mkoa na Kitaifa kwa manufaaa ya ulinzi na Usalama wa Albino wote.

  Hatua zingine za ziada za muda mfupi na mrefu ni uwepo wa program ya mafunzo maalum kwa Albino wa Jijini Dar es Salaam ili wapate mafunzo kupitia dhana ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kwa lengo la kupata uelewa wwa kutosha ili nao pia washiriki na kujua namna ya kutoa taarifa kwa lengo la kujikinga na maadui wao ambao wamegubikwa na tama za kujipatia mali, madaraka n.k. kwa njia za ushirikina.

  0 0

  Zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa limeendelea mkoani Mtwara, ambapo wananchi wamejitokeza kwa wingi kujisajili, kama wakazi hawa wa Wilaya za Tandahimba na Newala walivyokutwa wakishiriki kikamilifu kujisajili.

  Moja ya changamoto kubwa iliyojitokeza ni wakazi wengi hususani maeneo ya vijijini kukosa mashine za photocopy, huku baadhi wakikosa nyaraka muhimu za kuwatambulisha. Changamoto nyingine ni waombaji wengi kutokuwa na taarifa sahihi za umri wao binafsi na wazazi huku baadhi wakikosa taarifa sahihi za maeneo wanakoishi.

  Hata hivyo kwa maelekezo na mafunzo yaliyotolewa na NIDA kwa maafisa wote wanaoendesha zoezi hilo changamoto nyingi zimeweza kutatuliwa kutokana na miongozo na madodoso yanayomsaidia mwombaji kutambua baadhi ya taarifa muhimu.
  Hata hivyo NIDA imewaomba wananchi katika maeneo mengine ambayo zoezi hili halijafanyika kuanza kujiandaa kwa kuwa na nyaraka muhimu zinazoweza kuwatambulisha mathalani; cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, Cheti cha Elimu ya Msingi, Sekondari au Chuo, Leseni ya Udereva, Kadi ya kupigia Kura, Pasipoti, Kadi ya Bima ya Afya, nambari ya utambulisho ya mlipa kodi (TIN) pamoja na kuwa taarifa sahihi zinazomhusu mwombaji binafsi na wazazi, majina, tarehe na miaka ya kuzaliwa. 

older | 1 | .... | 545 | 546 | (Page 547) | 548 | 549 | .... | 3285 | newer