Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 547 | 548 | (Page 549) | 550 | 551 | .... | 3270 | newer

  0 0


  EdExpo Tanzania, 2015 will be part of the Africa Student Fairs Series to be held in five countries from 2nd to 16th March, 2015.  The series kicks off with the Addis Student Fair in Addis Ababa, Ethiopia (2nd & 3rd March), followed by EdExpo Kenya in Nairobi (6th & 7th March), EdExpo Tanzania in Dar es Salaam (9th & 10th March), Uganda International Education Fair in Kampala (13th & 14th March) and finishes in Rwanda with the Rwanda International Fair in Kigali (16th March). 
   
  EdExpo Tanzania 2015, is set to take place at Serena Hotel in Dar es Salaam, and is organized by Catalyst International (Tanzania) Ltd., in partnership with WR Education Consultants (Uganda) Ltd.
   
  Dates and venues for the student fairs are:
  - Addis Student Fair - 2nd and 3rd March, 2015 (Radisson Blu Hotel, Addis Ababa)
  - EdExpo Kenya  - 6th and 7th March, 2015 (Hilton Hotel, Nairobi)
  - EdExpo Tanzania - 9th & 10th March, 2015 (Serena Hotel, Dar es Salaam)
  - Uganda International Education Fair - 13th and 14th March, 2015 (Hotel Africana, Kampala) 
  - Rwanda International Education Fair - 16th March, 2015 (Hotel des Mille Colline, Kigali)
   
  EdExpo Tanzania 2015, and indeed the Africa Student Fairs Series, will undoubtedly meet a real need in the higher education market place, providing an ideal platform for students to get all the information they need on study abroad options available from around the world.
   
  Admission to the fairs is free.
   
  For more information visit www.edexpo.catalystexpo.com.

  0 0

  PG4A2748
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na  Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa kwenye Ikulu ya Mwanza  ambako atakuwa  mgeni rasmi katiaka harambee ya Mkapa Foundation inayotarajiwa kufanyika  jijini Mwanza.

  PG4A2753
  Waziri Mkuu Mizengo  Pinda akizungumza na  Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa kwenye Ikulu ya Mwanza  ambako  atakuwa   mgeni rasmi katiaka harambee ya Mkapa Foundation inayotarajiwa kufanyika  jijini Mwanza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Wanahabari mahiri wa mji wa Morogoro ambao wanaongozana na Rais Kikwete katika ziara yake ya mkoa huo wakiwa kazini wakati wa kutembelea kituo cha afya cha Mwaya, Morogoro vijijini.

  0 0

  Kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam akionesha noti bandia zilizokamatwa

  Jeshi la Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata kundi la watu saba wanaotengeneza noti bandia za dola ya Kimarekani huko maeneo ya Sinza katika Hotel iitwayo Mombasa Kinondoni, jijini Dar es Salaam. 


  Watuhumiwa hao walikamatwa mnamo tarehe 04/8/2014 wakiwa na noti bandia zipatazo 10,640 za dola mia (100) ambazo ni sawa na dola 1,064,000 ambazo ni zaidi ya shilingi za Kitanzania bilioni moja katika nyumba namba 07 walimokuwa wamepanga.
  Polisi walipata taarifa kutoka kwa wananchi na kuweka mtego ambapo askari walifika katika eneo hilo na kuwatia mbaroni watuhumiwa wakiwa na noti hizo bandia zilizokuwa zimefungwa mabunda themanini na kasiki ndogo ambayo imefungwa kwa namba za siri. Aidha watuhumiwa walikiri kujihusisha na utengenezaji wa noti bandia. 
  Watuhumiwa hao ni:-
  1.AHMAD S/O MOHAMED Miaka 50, mfanyabiashara, mkazi wa Mombasa Kenya
  2.RICHARD S/O MAGOTI Miaka 61, mfanyabiashara, mkazi wa Musoma mkoani Mara.
  3.SIMONI S/O LUKIKO Miaka 58, mkazi wa Magomeni Kagera
  4.HUMPHREY S/O LEONARD Miaka 34, mlinzi, mkazi wa Mburahati
  5.FRANK S/O CHARLES Miaka 31 mfanyabiashara, mkazi wa Sinza
  6.ABDALLAH S/O YUSUPH, Miaka 34, mfanyabiashara, Mkazi wa Sinza
  7.BAKARI S/O BAKARI, Miaka 31, mfanyabiashara, mkazi wa Mbezi, Kimara.
  Watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

  0 0

  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inawatangazia wanafunzi wote wa Tanzania wanaosoma katika vyuo vya Lugansk, Ukraine na maeneo mengine Chini ya Ufadhili wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambao hivi sasa wako likizo hapa nchini kuwa kutakuwepo na mkutano kujadili, pamoja na mambo mengine, hali ya usalama na hatua za kuchukua kabla ya kurudi Lugansk kuendelea na masomo, mwezi Septembea, 2014. 

  Mkutano huo utafanyika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, siku ya Jumatano, tarehe 3 Septemba, 2014 saa nane mchana. Aidha, wanafunzi wengine wanaosoma Lugansk kwa udhamini binafsi wanaombwa kuhudhuria ili kushiriki katika mkutano huo. 

  Imetolewa na: 

  Katibu Mkuu 
  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi 
  7 Mtaa wa Magogoni, 
  Post Code 11479, 
  S.L.P. 9121, 
  DAR ES SALAAM.

  0 0

  Say no to abortion ni kampeni iliyojidhatiti katika kuelimisha vijana wadogo kuhusiana na hasara za utoaji mimba, mahusiano ya mapenzi mashuleni katika umri mdogo na elimu ya uzazi.

  'Utoaji mimba usio katika hali salama, mazingira mazuri na vitendea kazi viivyodhibitishwa hufanyika kila siku katika jamii zetu ingawa serekali na sheria ya nchi yetu hairuhusiwi. 

  Tunapoteza nguvu kazi, vijana wa taifa letu' alisema Mkurugenzi wa kampeni hiyo, ndugu Veronica Lugenzi ambayo imezinduliwa rasmi 22 august 2014 shuleni Aureke secondary na kaimu mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni Dr. Guninita Kamba, Mbezi, jijini Dar es salaam.
  Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni, Dr. Guninita Kamba (kushoto), Bi. Veronica Lugenzi na mwalimu mkuu wa Aureke secondary school wakiwa kwenye uzinduzi huo.
  Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni, Dr. Guninita Kamba akiwahutubia wanafunzi.​
  Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni Dr. Guninita Kamba akizindua rasmi kampeni ya Say no to abortion shuleni Aureke secondary school, jijini Dar es salaam.

  0 0

  Kumekuwepo na habari ambazo zimeendelea kushamiri kila uchao katika mitandao ya kijamii na pia habari hizo kuripotiwa na magazeti kadhaa, ambapo kwa mara ya kwanza gazeti la mtanzania la Jumanne ya tarehe 19th Aug 2014, kisha gazeti la Jambo leo la Alhamis ya tarehe 21st Aug 2014 na baadae gazeti la An nuur la Ijumaa ya tarehe 22ndAug 2014, kwa mfululizo, kwa mfanano wa dhamira na maandishi magazeti hayo yote yameandika habari ya upotoshaji, uchonganishi na kukuza chuki ya kidini hapa nchini. 
  Habari katika magazeti hayo zimebeba hoja kuu UDINI wa PROF MUHONGO ambae ni Waziri wa Nishati na Madini wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo vyombo hivyo vya habari vimeripoti “unbalanced story” kuwa miongoni mwa wanafunzi 10 waliopewa scholarship na Serikali ya China hivi karibuni wote ni wakristo, na kwamba jambo hilo limefanywa kimkakati hili kuwatenga, kuwabagua na kuwakandamiza waislamu wa Nchi HII.
  Ukweli halisi ni kuwa jumla ya Scholarship za Msc Oil/Gas ambazo zimetolewa katika chuo cha Petroleum nchini china ni 15 ambapo katika hizo 10 zinalipiwa na Serikali ya China na 5 zinalipiwa na Serikali ya Tanzania chini ya Wizara ya Nishati na Madini. Katika nafasi hizo 15 kwa ujumla wake, waislamu ni watano (5) na wakristo ni (10) na kigezo kikubwa kilichotumika kupata wanafunzi ni ufaulu wao katika masomo yao ya shahada ya kwanza. Miongoni wa wanafunzi watano waislamu ni A. Athuman, Swalehe L, Salum S, Hijira Yassin na Salum J.

  Mtandao wa wanahabari ambao wanatumika kusambaza taarifa za upotoshaji huu pamoja na wanaowatuma wanaodhani kuwa kueneza propaganda yenye sura na taswira ya UDINI ni kumchafua Mhe Prof Muhongo na Wizara yake wamekosa ufikiri sahihi, bali kufanya hivyo kunatishia amani na mshikamano uliokuwepo baina ya watanzania. Hivyo wanaoendeleza propaganda hizo chafu ni maadui wa amani ya Taifa.

  Ni ukweli ulio bayana kuwa kutokana na misimamo ya Mhe Waziri ya kusimamia haki na kupambana na ufisadi, ulaghai na ubadhirifu wa aina mbalimbali ambao ulikuwa ukifanyika katika mashirika mbalimbali yaliyo chini ya wizara yake, umeundwa mtandao hatari wa kumkabili na kuhakikisha kuwa “wanamshughilikia”. Mtandao ambao unaundwa na baadhi ya matajiri wakubwa, wanasiasa, wanasheria na wanahabari.

  Ni vyema watanzania wakafahamu kuwa Wizara ya Nishati na Madini chini ya Profesa Muhongo imepata mafanikio makubwa ambapo katika utekelezaji wa dira ya maendeleo ya mwaka 2025, inakadiriwa kuwa Tanzania itakuwa na uchumi wa kati unaokuwa kwa asilimia 10% na kwamba matumizi ya nishati ya Umeme kwa watanzania yatakuwa zaidi ya asilimia 75%. 
  Mafuta na gesi inategemewa kuwa ndio uti wa mgongo wa Tanzania, na misingi hiyo inawekwa sasa na Mheshimiwa Muhongo, tayari mashirika ya Wizara hiyo yameanza kuonyesha matumaini kwa kupata mafanikio makubwa na kumaliza migogoro, kesi na ubadhirifu uliokuwa ukiendelea. Uzalishaji katika migodi na madini umeendelea kuwa chanzo muhimu cha mapato kwa Serikali, kampuni Tanzu ya STAMICO (Shirika la Umma) ya STAMIGOLD imeendelea kuonyesha mafanikio makubwa mpaka sasa.

  Watanzania tunapaswa kumuunga mkono Prof Muhongo katika juhudi zake za kuwaletea maendeleo watanzania. Na kwa pamoja tuiunge mkono kauli kuwa “..Tutavuka tukiwa na ushindi wa maskini na wanyonge wa nchi hii. Tutaendelea kujenga uchumi imara utakaotoa ajira na matumaini mapya kwa watanzania..”

  Mungu Ibariki Tanzania.

  0 0

   Wabunge wa EALA wakiwasili The Guardian Ltd
  Wabunge wa EALA wakipokea maelezo kutoka kwa mfanyakazi wa EATV na Radio walipotembelea vyombo vya Habari vya IPP jana
   Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Dkt Margaret Zziwa akizungumza baada ya kupokea maelezo kutoka kwa mfanyakazi wa EATV na Radio wakati wa Ziara ya wabunge hao IPP Media. Wa nne kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Joyce Mapunjo.

  Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuwataarifu wananchi kuwa Bunge la Afrika Mashariki litafanyika kuanzia Agosti 27 hadi Septemba 4 katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kulihutubia Bunge hilo siku ya ufunguzi Agosti 27.

  Vikao vya Bunge hilo vitakua vikifanyika kuanzia saa 8.30 mchana siku za Jumanne, Jumatano na Alhamis.

  Pamoja na Mambo mengine Bunge hilo litajadili Muswada wa Elimu ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa 2014 na pamoja na mambo mengine litapokea na kujadili ripoti mbalimbali.

  Wizara inawakaribisha wananchi kufuatilia kwa karibu vikao vya Bunge la Afrika Mashariki ili waweze kujua mambo mbalimbali yanayohusu mtangamano wa Afrika Mashariki.


  Imetolewa na:


  KATIBU MKUU


  0 0

  Na Mahmoud Ahmad,Arusha. 
   Vijiji 120 vilivyopo mkoa wa Arusha vinatarajia kufikiwa na huduma ya umeme kupitia mpango wa kusambaza umeme vijijini unaofadhiliwa na (REA) na kutekelezwa na shirika la umeme la taifa (TANESCO). 
   Benedict Nkini akizungumza katika mkutano na Wananchi wa Vijiji vya Meserani juu na chini amesema kuwa kwa sasa wako katika hatua ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya mradi huo ili waweze kujiandaa kuunganishwa na huduma hiyo na pia amewataka waepuke vishoka ambao hutumia uelewa mdogo wa wananchi kujinufaisha. 
   Afisa Masoko wa Tanesco,Adelina Lyakurwa amesema kuwa amewaomba wananchi kutumia fursa hiyo kuunganishiwa umeme huo wa bei nafuu ambao Mtanzania wa hali ya chini anaweza kuumudu ,ambapo Mwanakijiji atatakiwa kuwa na kiasi cha shilingi 32900 ili aweze kuunganishiwa umeme.
   “Tunawaunganishia umeme watu wote wenye nyumba za mawe,matofali,mbao kwa hiyo tunawaomba wananchi watoe ushirikiano ili kufanikisha mradi huu,kwa upande wa nyumba za nyasi na makuti kunahitajika ushauri wa kitaalamu kwasababu za kiutaalamu ili kuepuka moto ambao unaweza kutokea kutokana na hitilifu ndogo” Alisema Afisa Masoko huyo.
   Kaimu Mkurugenzi wa TANESCO wilaya ya Monduli ,Ramadhani Mkayala amewataka wananchi watafute wakandarasi wazuri waliodhinishwa na shirika ili kuepuka vihatarishi vya moto Kwa upande wao wananchi wa Wilaya ya Monduli Sophia Mligo wa kijiji cha Miserani na Gasper Lengta wamesema kuwa wameupokea mpango huo vizuri na kuwaomba TANESCO wazidi kufanya ushirikishaji zaidi na wananchi ili uweze kufanikiwa bila vikwazo. “Kuna wakati tulihisi kuwa serikali imetusahau watu wa vijijini lakini sasa tunafarijika kuona hawa REA na TANESCO wanakuja kutuunganishia umeme na tayari wameanza kuchimba mashimo kwenye kijiji chetu shughuli iliyobaki ni kufukia nguzo ,uhakiki ulishafanyika hapo awali” Alisema Parirong’o Sipitieki ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Ingoikumeni
   Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja ,TANESCO  Arusha,Benedict Nkini (kulia) akifafanua jambo juu ya kifaa cha kujiunganishia umeme bila kusambaza waya kinachofahamika kitaalamu kama Ready Board ,kulia ni Afisa Masoko  wa Tanesco,Adelina Lyakurwa akiwa ameshika kifaa hicho ,pia  walizungumza na wananchi wa Vijiji vya Meserani juu na chini  kuhusu  mpango wa kuwaunganisha wananchi waishio vijijini  na huduma ya umeme kwa unaotekelezwa kwa awamu ya pili katika wilaya za Arumeru,Karatu,Monduli na Longido uliofadhiliwa na REA , lengo ni kuhakikisha wananchi waishio vijijini wanafikiwa na huduma hiyo muhimu.zilizopo mkoani Arusha
  Afisa Masoko  wa Tanesco,Adelina Lyakurwa akiwa ameshika kifaa cha kujiunganishia umeme bila kusambaza waya katika nyumba  kinachofahamika kitaalamu kama Ready Board ,wakati akizungumza na wananchi  wa Vijiji vya Meserani juu na chini  kuhusu  mpango wa kuwaunganisha wananchi waishio vijijini  na huduma ya umeme kwa unaotekelezwa kwa awamu ya pili katika wilaya za Arumeru,Karatu,Monduli na Longido unaofadhiliwa na REA  lengo ni kuhakikisha wananchi waishio vijijini wanafikiwa na huduma hiyo muhimu.zilizopo mkoani Arusha.Picha na Mahmoud Ahmad wa Globu ya Jamii,Arusha

  0 0

  H.E Michael D. Higgins, President of Ireland

  H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania, has sent a condolence message to H.E. Michael D. Higgins, President of the Republic of Ireland, following the demise of the former Irish Prime Minister H.E. Albert Reynolds (pictured) on 21st August 2014.
   The message reads as follows:-
  “H.E. Michael D. Higgins
    President of the Republic of Ireland
    Dublin
    IRELAND

  Your Excellency,

  I have received with great sorrow the sad news about the untimely passing away of the former Irish Prime Minister, the late H.E. Albert Reynolds.
  I take this opportunity to extend my heartfelt condolences to you and through you to the family of the deceased, the Government and the people of Ireland during the whole mourning period.
  The world will remember the late former Prime Minister Reynolds for his tireless efforts on peace keeping processes. It is my prayer that you remain strong during this difficult moment.
  We pray to the Almighty God to rest his soul in eternal peace.
  Please accept, Your Excellency, the assurances of my highest consideration”.
  Issued by: The Ministry of Foreign Affairs 
  and International Cooperation, 
  Dar es Salaam

  0 0

  Mark Schroeder, Vice President of Africa Analysis at Stratfor in Texas, USA in his  recent conversation with the President of Tanzania, Dr. Jakaya Kikwete, following his participation at the recent U.S.-Africa Summit that took place in Washington, D.C. President Kikwete describes his vision for Tanzania for the years to come.


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete jana amezindua mradi mkubwa wa maji wa Mambogo, mkoani Morogoro, katika ziara yake aliyoainza juzi mkoani humo. 
  “Napenda kumshukuru Rais Obama na Serikali ya Marekani kwa ushirikiano mzuri na nchi ya Tanzania, hasa katika kuleta maendeleo na pia Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC na MCA-T) ambao wamekua wadau wazuri wa maendeleo nchini katika sekta mbalimbali na sio maji pekee”, alisema Rais Kikwete. 
  “Ni kazi kwetu sisi kuutunza mradi huu mkubwa wa maendeleo na kuutumia vizuri ili kuhakikisha malengo yake yanafikiwa na MORUWASA haina budi kuzingatia hilo. Huku ikishirikiana na viongozi wa mkoa kuhakikisha maji yanakua si tatizo tena”, alisema Rais Kikwete. 
  Aidha, Mhe. Kikwete aliwaasa viongozi kuwa makini na utunzaji wa vyanzo vya maji kwani ndio muhimu na bila vyanzo hivyo, upatikanaji wa maji utakuwa mgumu kutokana na upungufu wa rasilimali hiyo. 
  Aliendelea kusisitiza viongozi kutokua waoga katika kuchukua hatua na kusimamia rasimali hizo kwa nguvu zote bila uzembe. 
  Aidha, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Mbogo Futakamba alisema utekelezaji wa mradi huu ni hatua kubwa ya kuboresha upatikanaji na ubora wa maji kwa wananchi wa Manispaa ya Morogoro, na kwamba  utaleta manufaa kwa wakazi wa Manispaa wanaotumia huduma za majisafi kutoka vya maji vya Bwawa la Mindu na Mambogo. 
  Pia, Inj. Futakamba aliongeza Wizara yake imetenga fedha kiasi cha Sh. Mil 400 kwa ajili ya kupanua mtandao wa maji ili wananchi waweze kuunganishwa kwa wakati katika mwaka wa fedha 2014/15. 
  Mradi wa Mambogo ni moja ya miradi mikubwa nchini, unasimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro (MORUWASA), unategemewa kuongeza uzalishaji wa maji kutoka meta za ujazo 23,000 kwa siku hadi meta za ujazo 33,000 kwa siku katika kuhakikisha tatizo la maji mkoani humo linapatiwa ufumbuzi, huku wananchi wengi wakitegemewa kuunganishwa kwa haraka kwenye mtandao wa maji katika Manispaa hiyo. 
  Mradi huo umedhaminiwa na Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC na MCA-T) ), ukiwa ni moja ya malengo ya kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo huduma za jamii, ikiwemo seakta ya maji. 
  Mhe. Kikwete yuko mkoani Morogoro kwa ziara ya siku nane akikagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakati wa sherehe za uzinduzi wa mradi huo mkubwa wa maji wa Mambogo mkoani Morogoro ambao  umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
  Sehemu ya jengo la mradi huo

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakifunua pazia kuzindua mradi huo
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakifurahgia baada ya kuzindua mradi huo
  Rais Kikwete akibofya kitufe kupiga king'ora kuzindua rasmi mradi huo
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher na viongozi wengine wakielekea kukagua  mradi huo.


  0 0

   Msanii mkongwe wa muziki wa dansi Mabrouk Omar a.k.a Babu  Njenje (kushoto), akiongea na wasanii wa muziki wa kizazi kipya walipomtembelea nyumbani kwake mjini Tanga , msanii huyo kwa sasa anasumbuliwa na matatizo ya kiafya. Wasanii hao wapo katika msafara wa tamasha ya Serengeti fiesta ambapo kwa mjini hapo linafanyika katika Uwanja wa Mkwakwani.
   Mkurugenzi wa  Uzalishaji  na Vipindi wa Clouds Media, Ruge Mutahaba (kushoto) na Meneja wa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney wakiteta na  Masanii mkongwe wa muziki wa dansi, Babu Njenje alipotembelewa na timu ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya ili kumpa mkono wa pole.
   Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi, Babu Njenje (wa tatu kulia) waliokaa, akipozi kwa picha na baadhi ya wasanii Serengeti fiesta pamoja na baadhi ya watu wengine wenye mapenzi mema walimpomtembelea nyumbani kwake mjini Tanga.
  Msanii wa Muziki wa kizazi kipya , Jux akimsalimia msanii mkongwe wa dansi, Babu Njenje wakati wasanii hao walipomtembelea nyumbani kwake mjini Kanga , kabla ya onyesho la Serengeti fiesta kufanyika mjini humo leo jioni.
  Kwa uhondo zaidi wa Serengeti Fiesta nenda: 

  0 0  0 0

  Na Mahmoud Zubeiry

  MSHAMBULIAJI Reuben de La Red amefunga mabao matatu peke yake, wakati magwiji wa Real Madrid wakiiangusha Tanzania Eleven 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

  De la Red alimfunga bao moja kipa Mwameja Mohamed kipindi cha kwanza na kipindi cha pili akamtungua mara mbili Manyika Peter, wakati bao pekee la Stars lilipatikana baada ya  Real kulijifunga wenyewe kupitia kwa Roberto Rojas.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alimkabidhi mpira uliotumika De La Red baada ya kuutia saini yake juu yake, kabla ya kuwakabidhi Kombe Real Madird kwa ushindi wao huo.

  Katika mchezo huo, ambao wachezaji waliingia na kutoka, Real Madird walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 10, kupitia kwa De La Red ambaye alimalizia pande tamu la Luis Figo.

  Mpira uliozaa bao hilo, ulianzia kwa kiungo Christian Karembeu, aliyezuia shambulizi la Tanzania na kuanzisha shambuizi zuri lililozaa matunda, akiuvuka msitu wa wachezaji wa wenyeji kwa umahiri mkubwa.

  Tanzania Eleven ilisawazisha dakika ya 45 baada ya kona ya Mecky Mexime kuzua kizaa langoni mwa Real na Roberto Rojas akajifunga katika harakati za kuokoa baada ya Kali Ongala kuuparaza kwa kichwa. 

  Kipindi cha pili, De la Red alifunga bao la  pili kwa penalti dakika ya 81 baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Habib Kondo kwenye eneo la hatari.

  Awali ya hapo, Figo alimtoka vizuri beki Mecky Mexime na kuingia hadi kwenye eneo la hatari akiwa kwenye nafasi ya kufunga akampasia De La Red ambaye alipiga nje.

  De la Red alikamilisha hat trick yake dakika ya 88 baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Tanzania Eeleven. 

  Wachezaji wa timu zote mbili wanatarajiwa kula chakula cha usiku na Mheshimiwa Rais Ikulu baadaye leo. 

  Luis Figo akimtoka Athumani China
  Beki wa Tanzania, Nsajigwa Shadrack kushoto akimtoka Fernando Sanz wa Real Madird
  Reuben De La Red kushoto amefunga mabao matatu peke yake Real ikishinda 3-1 Uwanja wa Taifa

  0 0

   Mama Salma Kikwete akimsindikiza Mjane wa Marehemu Jaji Lewis Makame, Mama Mary Makame kuweka udongo kwenye kaburi.
   Mama Salma Kikwete akiwa na  Mjane wa Marehemu  Jaji Lewis Makame, Mama Mary Makame,  wakati wa  mazishi huko Tongwe katika wilaya ya Muheza mkoani Tanga
   Mama Salma Kikwete akitoa salamu ya pole kwa wafiwa mara baada ya shughuli ya utiaji udongo kaburini kukamilika.
   Mjane wa Marehemu Jaji Lewis Makame, Mama Mary akiweka shada la maua kwenye kaburi la mume wake Marehemu Jaji Lewis Makame 
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea shada la maua kutoka kwa msaidizi wake tayari kuliweka kwenye kaburi la marehemu Jaji Lewis Makame aliyezikwa kijijini kwake huko Tongwe.
  Mama Salma Kikwete akiweka shada la maua kwenye kaburi la hayati Jaji Lewis Makame wakati wa mazishi yaliyofanyika katika kijiji cha Tongwe katika wilaya ya Muheza, mkoani Tanga tarehe 23.8.2014. 

  0 0

  Meneja Mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd ya jijini Arusha ,Edmund Rutaraka (kushoto)akikabidhi msaada wa jezi kwa Makamu mwenyekiti wa timu ya soka ya Machava fc,Abuu Masudi.
  Baadhi ya wachezaji wa kikosi cha timu ya Machava fc ya mkoani Kilimanjaro wakionesha uzi mpya waliopewa na kampuni ya Megatrade Investment ya jijini Arusha kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Panone fc uliondaliwa mahususi kwa ajili ya Magwiji wa soka wa klabu ya Real Madrid utakaopigwa katika uwanja wa Ushirika.
  Kwa habari kamili BOFYA HAPA

  0 0

  Mkandarasi mkuu anaeshughulikia mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, Strabag International ametangaza kufungwa kwa muda kipande cha barabara ya Mandela hadi makutano ya Ubungo Mataa kuanzia leo.

  Akiongea jana na waandishi wa habari, Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Bw. Yahya Mkumba alisema kipande cha barabara ya Mandela kuanzia makutano ya barabara ya morogoro upande wa kushoto uelekeo wa Tabata kuanzia ubungo mataa hadi darajani patafungwa.

  Kipande hicho kitafungwa kuanzia tarehe 25/08/2014 mpaka tarehe 30/08/2014 ili kupisha ujenzi wa kipande cha barabara hiyo na hivyo kuwalazimu watumiaji wa barabara hiyo kutumia barabara ya upande mmoja.

  Akifafanua zaidi ofisa uhusiano huyo alisema magari yatakayokuwa yanatokea Mwenge, Kimara na Shekilango yatalazimika kutumia barabara ya upande wa kulia ambayo pia itakuwa ikitumika na magari yanayo toka Tabata kuelekea Ubungo.

  “Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaotokea,” alisema Bw. Mkumba.

  Mradi wa Mabasi yaendayo haraka unatarajiwa kuondoa adha ya foleni katika jiji hilo na kuleta ufanisi wa usafiri.

  Awamu ya kwanza ya mradi huo inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu.

  0 0

  Wananchi wa  kijiji  cha Luvuyo kata ya Madope  wakimpokea  mbunge wao Deo Filikunjombe kwa maandamano
  Wanachama  wa  chama  cha mapinduzi (CCM)   pamoja na  wananchi wa  kijiji cha Luvuyo kata ya Madope  wakishirikiana jana na mbunge  wao Deo Filikunjombe  (kushoto) kuchimba mifereji ya  maji katika barabara ya Luvuyo - Njombe  yenye urefu wa Kilomita 6 ambayo inajengwa kwa  ufadhili wa mbunge huyo kwa kiasi cha zaidi ya Tsh milioni 50
  Wananchi wa  Luvuyo wakimsikiliza  mbunge  wao Deo Filikunjombea
  Mbunge wa  jimbo la Ludewa akiwahutubia  wananchi wa Luvuyo mara  baada ya  kuzindua  ujenzi wa barabara ya Luvuyo - Njombe
  Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe akisafirishwa katika  katika mkokoteni waw  kukokotwa na  ng'ombe  baada ya  wananchi  wa  kijiji  cha Luvuyo kata ya Madope  ambao awali  walitishia  kuhama  wilaya ya  Ludewa  kuhamia Njombe kusikilizwa  kilio  chao  cha ubovu wa  miundo mbinu kwa  kuanza kujengewa barabara na  mbunge   huyo

  0 0
 • 08/24/14--04:01: Article 14


older | 1 | .... | 547 | 548 | (Page 549) | 550 | 551 | .... | 3270 | newer