Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

MARIA SHILA NDIYE REDD'S MISS KINONDONI 2014

$
0
0
Redd's Miss Kinondoni 2014, Maria Shila akipunga mkono baada ya kutawazwa kuwa malkia wa Kanda ya Kinondoni katika shindano lililoshirikisha wanyange 16 waliokuwa wakiwania tiketi ya  kushiriki shindano la Miss Tanzania 2014. Shindano hilo lilifanyika Dar es Salaam usiku wa kuamia leo. 

Shila ameungana na warembo wengine Camila Cindy John aliyeshika nafasi ya pili na Queenlatifa Hashim aliyeshika nafasi ya tatu ambao kwa pamoja wamepata tiketi ya kuiwakilisha Kanda ya Kinondoni katika mashindano ya taifa ya Miss Tanzania 2014 yanayotaraji kufanyika mapema mwezi Oktoba.
  Redd's Miss Kinondoni 2014, Maria Shila (katikati) akipunga mkono baada ya kutangazwa kuwa ndie mshindi wa taji hilo na kuwaongoza warembo wengine 15 waliokuwa wakiwania taji hilo. Wengine mshindi wa pili Camila Cindy John (kulia) na mshindi wa tatu Queenlatifa Hasim. Shindano hilo lilifanyika Dar es Salaam usiku wa kuamia leo. PICHA ZAIDI: FATHER KIDEVU BLOG

MAZABE POWDER WATAMBA KUINGIA NUSU FAINALI YA DANCE 100%CHINI YA VODACOM TANZANIA

$
0
0
Kikundi cha Mazabe Powder cha kwandevu Tegeta jijini Dar es Salaam,kinachoshiriki shindano la Dance 100% wakielekee mazoezini kujindaa na robofainali itakayofanyika Agosti 23 mwezi huu. Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Washiriki wa shindano la dance 100% wa kundi la Mazabe Powder la kwandevu Tegeta jijini Dar es Salaam,wakiwa mazoezini kujiandaa kwa mchuano wa robo fainali itakayofanyika Agosti 23 mwezi huu. Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Baadhi ya washiriki wa shindano la Dance 100% wa kundi la Mazabe Powder la Tegeta kwandevu jijini Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja Uhusiani wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (watatu kutoka kushoto) na Mratibu wa shindano hilo kutoka EATV Happy Shame walipowatembelea kambini kuwapa moyo vijana hao na kujionea jinsi wanavyofanya mazoezi yao kujiandaa na robo fainali ya mashindano hayo yatakayofanyika Agosti 23 mwezi huu.

SOKA NDANI YA SUPERSPORT

MH. PINDA AFUNGA KONGAMANO LA JIOLOJIA AFRIKA

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda, akihutubia wakati akifunga Kongamano la 25 la Wajiolojia Barani Afrika lililofanyika tarehe 14-16 Jijini Dar es Salaam. Wakati akifunga Kongamano hilo, Waziri Pinda amewataka watafiti barani Afrika kufanya tafiti ambazo zina mahusiano ya moja kwa moja na jamii ili tafiti hizo zitumike katika kuwazesha wananchi kufaidika na rasilimali zilizopo barani Afrika.
Baadhi ya Wajilojia kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wanaohudhuria Kongamano la 25 la Wajiolojia Afrika wakifuatilia hotuba ya kufungamano hiyo iliyosomwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani).
Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajiolojia waliohudhuria kongamano hilo kutoka nchi mbalimbali Barani Afrika. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Sadik Meck Sadik na Rais wa Wajolojia Afrika Profesa Aberra Mogassie.

Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam
Wajiolojia barani Afrika wametakiwa kufanya tafiti zenye uhusiano wa moja kwa moja na jamii na kuzionesha tafiti hizo ili ziweze kutumiwa  kama ufumbuzi wa  matatizo mbalimbali yanayolikabili bara la hilo, jambo ambalo litaiwezesha  Afrika  kunufaika  na rasilimali zilizopo na hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi , maendeleo ya watu na mapato ya mataifa yao.

“Najua watafiti wanaweza kusema serikali zetu hazitumii tafiti zetu, lakini mkifanya tafiti zenye uhusiano wa moja kwa moja na jamii, mkazitoa kwa jamii tutazitumia msizifungie makabatini,” amesisitiza Pinda.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda  leo jijini Dar  es Salaam wakati akifunga kongamano la 25 la Wajiolojia barani Afrika  na kueleza kuwa, ili Afrika  iweze kuendelea na kufaidika na rasilimali zake, inahitaji kuzalisha wataalamu wengi  katika taaluma ya sayansi ikiwemo wajiolojia.

KANISA LA YESU CHRISTO LA WATAKATIFU WA SIKU ZA MWISHO WAFANYA UKARABATI JENGO LA YATIMA GROUP TRUST FUND MBAGALA CHAMANZI

$
0
0
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Yesu Cristo la watakatifu wa siku za mwisho wakipaka rangi bweni la kituo cha watoto yatima cha yatima group trust fund kilichopo mbagala chamanzi ambapo waumini hawo walitumia siku hiyo kufanya usafi wa mazingira mbalimbali ikiwemo kukata kuni pamoja na kucheza na watoto wanaoishi katika kituo hicho kama njia moja ya kuwafariji
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Yesu Cristo la watakatifu wa siku za mwisho wakipaka rangi bweni la kituo cha watoto yatima cha yatima group trust fund kilichopo mbagala chamanzi ambapo waumini hawo walitumia siku hiyo kufanya usafi wa mazingira mbalimbali ikiwemo kukata kuni pamoja na kucheza na watoto wanaoishi katika kituo hicho kama njia moja ya kuwafariji
Muhumini wa Kanisa la Yesu Cristo la watakatifu wa siku za mwisho Charles Nyamuhanga akikati kuni kwa mashine kwa ajili ya
watoto yatima wa group trust fund kilichopo mbagala chamanzi ambapo waumini hawo walitumia siku hiyo kufanya usafi wa mazingira mbalimbali ikiwemo kukata kuni pamoja na kucheza na watoto wanaoishi katika kituo hicho kama njia moja ya kuwafariji
Baadhi ya waumini wakinamama wa Kanisa la Yesu Cristo la watakatifu wa siku za mwisho wakimenya viazi kwa ajili ya kupika na watoto wa kituo cha Yatima group trust fund cha mbagala chamanzi Dar es salaam.

Ambassador Jaap meets Former Prime Minister Lowassa

$
0
0
Former Prime Minister and Monduli's MP,Hon. Edward Lowassa ( L ) in discussion with Netherlands Ambassador to Tanzania, Jaap Frederiks. The ambassador visited the former PM who is also the Monduli MP in his office in Dar es Salaam yesterday to discuss issues related to land disputes in Monduli . Photo: Staff Photographer.

Rais Kikwete ahudhuria Mkutano wa 34 wa SADC Victoria Falls

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea maua kutoka kwa watoto leo muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mji wa Victoria Falls nchini Zimbabwe ambapo atashiriki katika mkutano wa 34 wa siku mbili wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa 34 wa wakuu wa nchi za SADC unaofanyika katika mji wa Victoria Falls nchini Zimbabwe.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Hifikepunye Pohamba wa Namibia na Rais Jackob Zuma wa Afrika ya kusini wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa mkutano wa 34 wa wakuu wa nchi za SADC unaofanyika katika hoteli ya Elephant Hills, mjini Victoria Falls nchini Zimbabwe leo(picha na Freddy Maro).

Shindano la Tanzania Movie talents (TMT)

$
0
0
Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakifuatilia Filamu fupi iliyochezwa na baadhi ya washiriki wa Shindano la Tanzania Movie talents (TMT) wakati ilipokua ikionyeshwa kwenye runinga kubwa katika Ukumbi wa Makumbusho. Kutoka Kulia ni Single Mtambalike au Rich Rich katikati ni Vyonne Cherry au Monalisa na Kushoto ni Jaji Mkuu wa Shindano hilo Roy Sarungi.
 Mahosti wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Joti na Lulu wakiwajibika katika Jukwaa la Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa wakati shindano hilo lilipokuwa likiendelea alhamisi iliyopita.
 Mmoja kati ya Washindi kutoka Kanda ya Pwani, Mkoa wa Dar Es Salaam katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Shiraz Ngassa (wa Kwanza Kushoto) akiongea na Msanii Joti mara baada ya Kuaga rasmi shindano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa siku ya alhamisi.
 Fredy Kiluswa ambae pia alikuwa mmoja kati ya Washindi watano kutoka Kanda ya Pwani katika Hatua ya kuwatafuta washindi wa Kanda akitoa maneno ya Shukrani mara baada ya kuaga shindano hilo kutokana na uchache wa kura alizopata.
 Baadhi ya washiriki wa kundi la Kwanza wakiwa mbele ya Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) mara baada ya Filamu yao fupi kuonyeshwa.
Mwinshehe Mohamed ambae alikua mmoja kati ya Washindi wa Tatu kutoka Kanda ya Kati mkoa wa Dodoma akitoa pongezi na Maneno ya Shukrani kwa Timu nzima ya TMT mara baada ya kuaga shindano alhamisi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
 Baadhi ya washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) waliofanikiwa kuingia hatua ya Fainali ambapo mshindi wa Shindano hilo linalotarajiwa kufikia Tamati Mnamo mwisho wa Mwezi wa Nane kwa Mshindi Kukabidhiwa Kitita Cha Shilingi Milioni hamsini za Kitanzani.Picha Zote na Josephat Lukaza - Proin Promotions ltd

Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam.

Hatimaye Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limefikia hatua ya Mwisho kabisa mara baada ya washiriki kumi bora kupatikana katika Show ya Mchujo iliyofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa siku ya Alhamisi.
Show hiyo ya Mwisho katika katika Hatua ya mchujo ilifanyika siku ya Alhamisi na kupelekea Washiriki watatu kutoka Kanda Mbili za Tanzania yaani Kanda ya Kati na Kanda ya Pwani kuondolewa katika Kinyanganyiro hiko na Kupelekea Shindano hilo kubaki na washiriki 10 tu ambao wameingia hatua ya fainali ambapo mshindi mmoja ataondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania katika Fainali Kubwa inayotarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Mlimani City siku ya Tarehe 30 Mwezi huu wa Nane.
Washiriki waliondolewa katika Kinyanganyiro Hiko ni Mwinshehe Mohamed ambae alikuwa mmoja kati ya Washindi watatu kutoka Kanda ya Kati ambapo anafanya Idadi ya washiriki wawili kutoka Kanda ya Kati kuondolewa na Kuifanya Kanda ya Kati kuwakilishwa na Mshindi Mmoja katika Fainali hiyo. Wengine waliotoka ni Shiraz Ngassa na Fredy Kiluswa ambao wote ni Washindi kutoka kanda ya Pwani Mkoa wa Dar Es Salaam. Kanda ya Pwani walichukuliwa washindi watano huku Shiraz na Fredy wakitimiza idadi ya Washiriki wanne kuondolewa katika kinyanganyiro hiko kwa Kanda ya Pwani, Tishi Abdallah ndie Mshindi mmoja kati ya washindi watano kutoka kanda ya Pwani ambae anaiwakilisha Kanda ya Pwani katika Fainali kubwa ya Shindao la Kwanza na la Kipekee kufanyika Afrika Mashariki na Kati la Tanzania Movie Talents (TMT).

Mpaka Sasa Ni Kanda Moja tu ambayo washindi wake wote watatu ndio wanaiwakilisha Kanda hiyo katika Fainali kubwa itakayofanyika Mwishoni Mwa Mwezi wa Nane katika Ukumbi wa Mlimani city ambapo mshindi mmoja ataondoka na Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania huku washindi wote kumi waliofanikiwa kuingia Katika hatua ya Fainali watakuwa chini ya Kampuni ya Proin Promotions limited ambapo watacheza filamu ya pamoja na Hatimaye kuanza kunufaika na Mauzo ya Filamu hiyo inayotarajiwa kutoka Hivi Karibu.

Vipindi vya Shindano hili la Tanzania Movie Talents (TMT) vitaendelea kurushwa katika Kituo cha Runinga cha ITV siku ya Jumamosi Saa 4 Usiku huku marudio yake yakiwa siku ya Jumapili Saa 10 Jioni na Siku ya Jumatano saa 5 usiku.
Ili Kuendelea kumuwezesha Mshiriki wako kuibuka mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kwa Mwaka 2014 unachotakiwa ni kuendelea kumpigia kura kwa wingi kadri uwezavyo kwa Kuandika Ujumbe Mfupi wa Maneno (SMS) Neno TMT acha nafasi ikifuatiwa na namba ya Mshiriki halafu tuma kwenda 15678. Mfano TMT 00 halafu tuma kwenda 15678 au unaweza kupiga kura pia kupitia Ukurasa wetu wa Facebook kwa kufungua kiunganishi hiki https://www.facebook.com/tztmt/app_316963748468949


Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) yazindua rasmi zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu mkoani Mtwara

$
0
0
Ndugu Joseph Makani, Mkurugenzi Mifumo ya Komputa akisoma hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA, wakati wa uzinduzi wa kuanza kwa zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu mkoani Mtwara.
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imezindua rasmi zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu kwa wananchi na wakazi wa mkoa wa Mtwara, zoezi ambalo litadumu kwa siku 14 kuanzia Jumatatu tarehe 18/08/2014.
 Akizungumza katika sherehe fupi ya uzinduzi wa zoezi hilo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho; ndugu Joseph Makani amesema kuanza kwa zoezi hilo Mtwara ni utekelezaji wa mpango wa Usajili wa wananchi na wakazi waishio kihalali nchini wenye lengo la kuwapatia vitambulisho vya Taifa Raia, Wageni na Wakimbizi baada ya zoezi kama hilo kukamilika wa wananchi wa Tanzania Zanzibar, mikoa ya Dar-es-salaam, Pwani na sasa Mtwara.
Amesema ufanisi wa zoezi hilo unategemea sana ushirikiano toka kwa viongozi katika serikali, vyama vya siasa na viongozi wa Dini ambao walikuwepo kushuhudia tukio hili. 
Naye mgeni rasmi kaimu Katibu Tawala Mkoa ndugu Jehasen Bukwali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, ameahidi kutoa ushirikiano na kusimamia kwa dhati zoezi hilo kufanyika katika mkoa wa Mtwara, huku akiwataka viongozi katika ngazi zote kushiriki kikamilifu katika kufanikisha zoezi la Usajili ambalo linamatokea makubwa katika ustawi na maendeleo ya Taifa.
Amewaasa wananchi na wanasiasa kutohusisha zoezi hilo la Siasa, kwani vitambulisho vya taifa havihusiani na itikadi za chama chochote, na haki ya kila Mtanzania kusajiliwa na kupata haki yake msingi kikatiba.

Ufunguzi huo uliwakilishwa na viongozi katika ngazi za juu Mkoa, na Wilaya zikiwemo kamati za Ulinzi na Usalama. (picha na Rose Mdami (NIDA) 

MABORESHO YA USIMAMIZI FEDHA ZA UMMA YANAVYOBORESHA MAISHA

$
0
0
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha, Ingiahed Mduma  (wa pili kushoto) na  Kassim Kobelo Mkuu wa Hazina ndogo Mkoa wa Lindi ( wa pili kulia) wakiwa wameshika cheti cha ushindi wa pili wa maonyesho ya Kitaifa  ya Nanenane  yaliyofanyika Ngongo, Mkoani Lindi hivi karibuni. Kwa habari kamili BOFYA HAPA

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Msikilize Juma Bhalo (RiP) katika "Ila ni wewe fulani"

mjue James Hadley Chase, mwandishi wa riwaya za kusisimua aliyefanya wengi wapende kusoma vitabu

$
0
0
Na Sultani Kipingo


Wengi tumesoma  vitabu vya James Hadley Chase (pichani),  mwandishi wa riwaya za kusisimua  maarufu sana wa Uingereza, hasa wakati tukipambana na kujua lugha ya Kiingereza wakati wa shule kidato cha kwanza hadi cha nne, na hata high school.
Nadhani kwa hili hata Profesa Mbele ataniunga mkono ninaposema kuwa utamaduni wa kupenda kusoma huanzia kwenye kuwepo kwa vitabu vya kusisimua kama vya Chase. Na wengi tuliua ndege wawili kwa jiwe moja – yaani kupenda kusoma na pia kujifunza Kiingereza bila shuruti. Au unasemaje Profesa Mbele?
Enzi hizo hamasa ya kusoma vitabu vya riwaya vya Kiingereza ilikuwa kubwa mno kiasi hata kulikuwa na mashindano ya nani kasoma “Chase” nyingi kuliko wenzie. Binafsi nimesoma “Chase” kama 30 hivi, na steringi wangu niliyempenda  sana ni Mark Girland, nikianza na kitabu cha “This is for Real” na baadaye “Have this one on me”, “You have yourself a deal”na “The Whiff of money”. Vic Malloy pia nilipenda visa vyake.

Pamoja na kumsoma sana James Hadley Chase, wengi wetu hatukujisumbua kumjua yeye ni nani, zaidi ya kuburudika na riwaya zake za kusisimua, ambazo nina uhakika zilihamasisha hata waandishi wetu kina Elvis Musiba , Ben Mtobwa,  Hammie Rajabu, Eddie Ganzel ambao sasa wote ni marehemu – ila vitabu vyao bado vingali hai.
Tukirudi kwa James Hadley Chase mstuko wa kwanza utaokupata ni kwamba yeye jina lake halisi halikuwa hilo ambalo alilitumia kiuandishi tu. Jina lake lilikuwa René Lodge Brabazon Raymond. Alitumia pia majina mengine ya kiuandishi kama vile  James L. Docherty, Raymond Marshall, R. Raymond na   Ambrose Grant.
Pamoja na hayo Chase aliibuka kuwa mwandishi mashuhuri wa riwaya, akiwa ameandika jumla ya vitabu 90, na kujulikana kama mfalme wa riwaya za kusisimua barani Ulaya na duniani kote, ambapo riwaya ya vitabu vyake 50 zilichezewa filamu.

René Lodge Brabazon Raymond (James Hadley Chase) alizaliwa Desemba 24,  1906  huko London, Uingereza., akiwa mtoto wa mwanajeshi wa jeshi la kikoloni la India Kanali  Francis Raymond. Huyu baba akiwa daktari wa mifugo, alipania mwanae asomee sayansi pia, na kumpeleka shule ya  King's School, Rochester, huko Kent.
Hata hivyo Chase aliondoka nyumbani akiwa na umri wa miaka 18. Mwaka 1932 alimuoa Sylvia Ray, nao wakajaaliwa mtoto wa kiume. Mwaka 1956 wakahamia Ufaransa, ambapo mwaka 1969 wakaenda kuishi Uswisi, wakiishi  maisha ya kipweke maeneo ya Corseaux-sur-Vevey, katika ziwa Geneva. Chase alifariki huko Februari 6, 1985
Wakati wa vita kuu ya pili ya dunia, Chase alijiunga na jeshi la anga na kupanda vyeo hadi kufikia Kiongozi wa Skwadi (Squardon leader). Huko pia alikuwa akihariri jarida la Jeshi la Anga la Uingereza, na kuandika riwaya kadhaa kutoka humo baada ya vita katika kitabu kilichoitwa Slipstream: A Royal Air Force Anthology.
Baada ya  Chase  kuondoka nyumbani akiwa na umri wa miaka 18, akawa anafanya kazi za kuuza vitabu, hasa vya watoto, katika duka moja la vitabu. Kabla ya kuanza kuandika riwaya, aliwahi kuwa mpiga picha wa kulipwa, na hobby zake kubwa zilikuwa muziki wa classic na opera,

Matatizo ya kiuchumi huko Marekani kati ya miaka 1929 na 1939, iliyopelekea kuwepo na Usongo mkuu (Great Depression) kuliibua makundi mengi ya kijambazi. Hayo na kuchanganya na biashara ya vitabu ya Chase, akagundua kuna fursa ya kuwa mwandishi wa riwaya za kijambazi. 
Na baada ya kusoma kitabu cha James M. Cain cha “The Postman Always Rings Twice cha mwaka 1934, na baada ya kusoma hadithi ya kundi la kijambazi liloongozwa na mwanamke aitwaye Ma Barker na watoto wake, akaandika kitabu chake cha kwanza cha riwaya za kusisimua kilichoitwa “No Orchids for Miss Blandish. Kitabu kilipanda chati sana na kuweza kuwa bora kwa mwongo mzima. Kuanzia hapo kitabu kimoja baada ya kingine kikafuata hadi kufikia 60.

























TENZI TATU ZA KALE

$
0
0
                                                       Na Profesa Mbele

Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale. Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katika duka la vitabu la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 
Kitabu hiki ni mkusanyo wa tenzi tatu za kale maarufu: Fumo Liyongo, uliotungwa na Muhamadi Kijumwa; Al Inkishafi, uliotungwa na Sayyid Abdalla bin Ali; naMwanakupona, uliotungwa na Mwana Kupona binti Mshamu. Kitabu kimehaririwa na M.M. Mulokozi, profesa mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kilichapishwa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili mwaka 1999.

Hizi ni kati ya tenzi maarufu kabisa katika ki-Swahili. Kwa msingi wa sanaa na maudhui, tenzi hizi zina hadhi kamili ya kuwemo katika orodha ambayo kwa ki-Ingereza huitwa "classics."

Fumo Liyongo ni hadithi inayomhusu shujaa Fumo Liongo, ambaye mimi, kutokana na utafiti wangu wa miaka mingi, napendelea kumwita Liongo Fumo. Huyu ni shujaa wa kale, labda miaka elfu moja iliyopita, na ndiye anayesifika kuliko wote tangu zamani katika jamii ya wa-Swahili.

Alikuwa pandikizi la mtu, mwenye vipaji kadhaa: kuwashinda maadui, shabaha katika kutumia upinde na mshale, ufundi wa kutunga nyimbo na mashairi. Juu ya yote, alikuwa muungwana sana, mfano wa kuigwa. Lakini alifanyiwa visa na ndugu yake ambaye alikuwa mfalme, hadi hatimaye akauawa na kijana mdogo, ambaye alikuwa mpwa wake. 



mona lisa: mchoro maarufu kuliko yote duniani

$
0
0
Mona Lisa (pia huitwa La Giocconda ambayo kwa Kitaliano ina maana ya furaha au mwanamke mwenye furaha tele) ni mchoro wa mwanzoni mwa karne ya kumi na sita uliochorwa na mchoraji mashuhuri duniaLeonardo da Vinci. Inaaminika kuwa ni mmoja kati ya michoro mashuhuri duniani. Mchoro huu unapatikana katika jumba la maonyesha (makumbusho) la mjini Paris maarufu kama Louvre. Nat King Cole aliutungia wimbo mchoro huu ambao sifa zake si za kawaida

MKURUGENZI REDIO 5 AVITAKA VYOMBO VYA HABARI KUANDIKA NA KUANDAA VIPINDI VYA KILIMO

$
0
0
IMG_0085
Mkurugenzi wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  Bw Robert Francis  akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo baada ya kufanya hafla fupi iliyofanyika mjengoni kwao ,ya kuwapongeza kwa kushika nafasi ya kwanza katika sekta ya mawasiliano na habari kwa ukanda wa kaskazini maonyesho ya nane nane, Pamoja na  David Rwenyagira aliyepata Tuzo za Tanapa hivi karibuni
IMG_0073
Mkurugenzi wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  Bw Robert Francis  akiwa anampongeza Mfanyakazi wa kituo hicho David Rwenyagira kwa kupata Tuzo na kushika nafasi ya kwanza upande wa Redio katika eneo la kutangaza utalii wa ndani na mshindi wa pili pekee kundi la kutangaza masuala ya Uhifadhi upande wa Redio zilizotolewa na   Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) hivi karibuni.


MKUU WA MKOA WA DODOMA AFUNGUA MKUTANO WA KITAIFA WA KANISA MORAVIAN TANZANIA, ATAKA KANISA KULIOMBEA TAIFA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akizungumza na viongozi wa kanisa Moravian Tanzania wakati akifungua Mkutano wa Kitaifa wa kanisa hilo uliofanyika mwishoni mwa wiki hii mjini Dodoma.
Baadhi ya viongozi wa kanisa la Moravian Tanzania wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi (hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa kitaifa wa kanisa hilo hapa nchini uliofanyika mwishoni mwa wiki hii mjini Dodoma.

Wajumbe wa Bunge la Katiba waaswa kurejea Bungeni

$
0
0
Na Rose Masaka-MAELEZO
Viongozi wa vyama vya siasa waliopo nje ya Bunge Maalumu la Katiba wameaswa kurejea bungeni ili kufanya maridhiano ndani ya bunge hilo.
Kauli hiyo imetolewa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alipokuwa akiongea na waandishi wa habari  Jijini Dar es salaam.
Jaji Werema amesema kuwa wajumbe walio nje ya Bunge Maalum hawana budi kurejea bungeni na kuacha kumshinikiza Rais kulivunja bunge hilo kwani hana mamlaka ya kulivunja kulingana na sheria inayoliongoza bunge hilo.
“Sheria inasema kuwa baada ya bunge hilo linaweza kuvujwa baada ya katiba kupatikana, kinyume na hapo bunge husitishwa kufikia maridhiano na kufikia mwafaka kwa kufuata misingi ya demokrasia.” alisema Jaji Werema.
Pia Jaji Werema alisema kuwa wajumbe walio nje ya bunge hilo hawana budi kurudi ili kuendelea kujadili vipengele vingine vya rasimu ili kuweza kupata katiba iliyo bora kwa nchi na watu wake.
Aidha, Jaji Werema aliviasa vyombo habari kutumia nafasi yao ya kuwa mhimili muhimu katika uongozaji wa nchi kutokuwa na upendeleo katika utoaji wa taarifa na kuacha kuongozwa na mawazo ya wachache ili kuweza kusaidia nchi kupata Katiba Mpya kwa manufaa na maendeleo ya nchi.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema akitoa ufafanuzi wa masuala Kisheria kwa waandishi wa habari kuhusu mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya wakati wa mkutano uliofanyika  jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema akiwaonesha waandishi wa habari Rasimu ya katiba wakati akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kisheria katika mchakato wa Katiba wakati wa mkutano uliofanyika  jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema wakati wa mkutano uliofanyika  jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Silayo

WASANII WA BONGO MOVIE WAWAOMBEA DUA WASANII WENZAO WALIOFARIKI DUNIA

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi,Abdallah Bulembo (katikati) akiwasili katika viwanja vya karimjee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuungana na wasanii kwenye dua maalum ya kuwaombea wasanii waliotangulia mbele ya haki.Kulia ni Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity,Steven Mengele maarufu kama Steve Nyerere.
Msanii wa vichekesho ambaye pia ni muinjilisti kwa sasa Emanuel Mgaya Maarufu kama Masanja Mkandamizaji akiongoza dua kwa upande wa wakristo huku Msanii Jacob Stephen JB akiwa ameishikilia Biblia.Kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Alhaj Mussa Salum ambaye aliongoza dua kwa upande wa waislam,katika shuguli hiyo ya kuwaombea Wasanii waliotangulia mbele ya haki,iliyofanyika jana kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya wadau wa Filamu nchini wakiwa kwenye shughuli hiyo ya kuwaombea Dua Wasanii wote waliotangulia mbele ya haki (waliofariki) iliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam jana.
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Alhaj Mussa Salum akijadiliana jambo na baadhi ya wadau walioshiriki kwenye dua hiyo.
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity,Steven Mengele maarufu kama Steve Nyerere akipeana mkono na watu mbali mbali baada ya kumalizika kwa dua ya kuwaombea wasanii waliotangulia mbele ya haki,iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee,Jijini Dar es salaam.

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar mgeni rasmi kwenye hafla ya kuwaaga wanafunzi wa Zanzibar wanaosoma chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro

$
0
0
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi alisema kwamba utitiri wa vyuo vikuu bila ya ubora wa elimu inayotolewa ni jambo linalopelekea vyuo hivyo kutoa vijana wasiouzika kiajira katika taasisi mbali mbali za umma na hata zile za binafsi.

Mama Asha Suleiman Iddi alisema hayo wakati wa hafla maalum ya kuagana kwa wana jumuiya ya wanafunzi wa Zanzibar wanaosoma chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro wa ZAMUMSA ambao wanatarajiwa kumaliza mafunzo yao mwezi Novemba mwaka huu iliyofanyika katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliopo Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Katika kuunga mkono jumuiya hiyo ya wanafunzi wa Zanzibar wanaosoma chuo kikuu cha Kiislamu Mkoani Morogoro Mke huyo wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha aliahidi kuipatia mchango wa Kompyuta, Printa na Mashine ya Fotokopi Jumuiya hiyo ili ipate nguvu zaidi za kiutendaji.

Hata hivyo Mama Asha aliwaasa na kuwatahadharisha wanafunzi hao wa elimu ya juu kujiepusha na ushawishi wa wanasiasa kwa kuwatumia kujiingiza katika matendo maovu ya uvunjifu wa amani ya Nchi.

Akisoma risala ya wanajumuiya hiyo ya Wanafunzi wa Zanzibar wanaosoma Chuo Kikuu cha Kiislamu Mkoani Morogoro { ZAMUMSA } Mwanajumuiya Saleh Haji alisema lengo la kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo mwaka 2006 ni kuwaunganisha pamoja wanafunzi wote ili kuwa rahisi kukabiliana na changamoto wanazopambana nazo.

Mapema Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Zanzibar wanaosoma chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro Hamad Ali alisema wanajumiya hao wameamua kujitolea kuitumikia nchi yao licha ya changamoto wanazopambana nazo.

Hamad Ali alisema wanafunzi hao wanahitaji kuitumia taaluma waliyojifunza kwa kuisaidia jamii iliyowazunguuka katika maeneo yao.
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Zanzibar wanaosoma chuo kikuu cha Kiislamu Morogoro Nd.Kassimu N’gwali akitoa neno la shukrani kwa waalikwa wa hafla yao ya kuagana kwa wanajumiya wanaomaliza masomo yao mwezi Septemba mwaka huu wa 2014. Kulia ya Ndugu N’gwali ni Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae ndie mgeni rasmi wa hafla hiyo Mama Asha Suleiman Iddi.
Baadhi ya wana jumuiya ya wanafunzi wa Zanzibar wanaosoma chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro wakifuatilia hafla ya maagano kwa wanajumiya wanaotarajiwa kumaliza mafunzo yao mwezi Septemba mwaka huu.
Mwanajumiya ya ZAMUMSA Saleh Haji alitaja baadhi ya changa moto wanazopakabiliana nazo wakati akisoma Risala ya jumiya hiyo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa ZAMUMSA Bibi Saada akimkabidhi zawadi Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi kwenye hafla ya kuagana wanajumiiya hiyo wanaomaliza masomo yao mwezi Septemba mwaka huu.
Mama Asha Suleiman Iddi akizungumza na Wana Jumuiya ya ZAMUMSA kwenye ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Mama Asha akimkabidhi Cheti Maalum Mwenyekiti mstaafu wa ZAMUMSA Nd. Rashid Mjaka kwa niaba ya viongozi wenzake baada ya kumaliza muda wao wa utumishi wa jumuiya hiyo. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Serikali kutatua mchangamoto za barabara kuwezesha miradi ya NSSF kufanikiwa

$
0
0
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisisitiza jambo baada ya kupata maelezo juu ya maendeleo ya Mradi wa Daraja la Kigamboni kabla ya kufanya ziara ya siku moja ya kutembelea Miradi iliyofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadani Dau (kushoto) akitoa maelezo juu ya miradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village modern city Housing scheme' yenye thamani ya matrilioni. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikuwa na ziara ya siku moja ya kutembelea miradi mikubwa ya miundombinu ya mfuko huo jijini Dar es Salaam.
 Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni Mhandisi Karim Mattaka (kulia) akimuonyesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia) mchoro sanifu wa daraja la Kigamboni, wakati wa ziara ya waziri mkuu kutembelea miradi mitatu mikubwa  inayofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam.
 Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni Mhandisi Karim Mattaka (kulia) akimuonyesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia) hatua za ujenzi wa daraja la Kigamboni, wakati wa ziara ya waziri mkuu kutembelea miradi mitatu mikubwa  inayofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia) akitembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni unaofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa ziara yake ya siku kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Watano Kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali na wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mara baada ya kutembelea mradi wa daraja la Kigamboni ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi. 
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images