Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 540 | 541 | (Page 542) | 543 | 544 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizewngo Pinda (wa tatu kulia) akikagua ujenzi wa daraja la kigamboni jijini Dar es salaam August 16, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizewngo Pinda akisalimiana na baadhi ya wataalam wa ujenzi wa nyumba hizo unaofanywa na Shirika la NSSF katika eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam August 16, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua ujenzi wa nyumba unaofanywa na Shirika la NSSF katika eno la Kigamboni jijini Dar es salaam August 16, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Bibi Doreene Mkandara na Mwanae Adastus Aporinary ambao ni miongoni mwa wateja waliouziwa nyumba na Shirika la Nyumba la Taifa la NHC zilizoko eneo la Kibada Kigamboni jijini Dar es salaam ambako Waziri Mkuu aliembelea August 16, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Meck Sadik na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema (kushoto) kukagua nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa NHC zilijengwa na kuuzwa eneo la Kibada Kigamboni jijini Dar es salaam August 16, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua ujenzi wa nyumba katika mradi wa DEGE ECO VILLAAGE unaomilikiwa na Shirika la NSSF eneo la Kigambaoni August 16, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Paulina Nyoni (Mama wa mtoto Fatuma Msuya) akiwa amembeba mwanaye ambaye anahitaji msaada wa matimabu .

  ----------------------
  Paulina nyoni mkazi wa kijiji cha Hanga wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma anaomba msaada kwa yeyote atakaye guswa na tatizo la mwanaye  aitwaye Fatuma Msuya ili aweze kupata matibabu katika hospitali ya KCMC moshi.

  Paulina ni mama mwenye watoto wa tano anayejishugulisha na kilimo , Mume wake aitwaye  Jafari Msuya amemtelekeza baada ya kujifungua mtoto mwenye tatizo hili na kukimbia kusikojulikana hivyo kumfanya mama wa mtoto huyu kutokuwa na msaada wowote ule,

  Fatuma Msuya (1) amezaliwa tarehe 24/2/2013 katika Hosptali ya mkoa wa Ruvuma akiwa na tatizo la kutokuwa na sehemu ya kutolea haja kubwa na hivyo kulazimika kufanyiwa upasuaji tumboni ambapo kwa sasa anatolea haja kubwa,awali kabla ya kupasuliwa alikuwa akitolea haja kubwa sehemu ya aja ndogo.

  Upasuaji wa awali alifanyiwa katika Hospitali ya Mission Peramiho iliyopo wilaya ya songea tarehe 19 04/ 2013
  Na kwa sasa mtoto huyu anakabiliwa na tatizo jingine la kutokwa na vidonda sehemu anayojisaidia  hali inayomsababishia maumivu wakati wote na anapojisaidia haja kubwa hutokwa na damu.

  Gharama za matibabu zinazohitajika  ni shilingi milioni tatu, Yeyote atakayeguswa anaweza kutoa msaada kwa Mpesa no 0767 710 113 .
  “Kutoa ni moyo”

  0 0  Na Mwandishi Wetu

  BODI ya Wadhamini ya Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB), imemteua  Jaji wa Mahakama ya Rufaa nchini, Dk.Stephen Bwana Kuwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la chuo hicho.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), Mikocheni Dar Es Salaam, Dk.William Kudoja alisema  Bodi ya Wadhamini ya chuo hicho ambayo Inaongozwa na Professa Paramaganda Kabudi Ndiyo ilimteua Jaji Bwana kushika wadhifa huo mpya baada ya kuona Ana sifa za vigezo Vya kushika wadhifa huo.

  Dk.Kudoja ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa UB anayeshughulikia Taaluma, alisema jaji Bwana ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa  ya Jinai (ICC) ya nchini Cambodia.

  Jaji Bwana aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali Kama Jaji wa Mahakama Kuu  Seychelles 1994-1999, Jaji wa Mahakama Rufaa ya Seychelles 2004-2009 , Kaimu wa Rais wa Mahakama hiyo ya Rufaa ya Seychelles kuanzia  Mwaka 2006-2008.

  Mbali na kushika nyadhifa hizo Jaji Dk.Bwana  pia aliwai Kuwa Mshauri wa Benki ya Dunia kuhusu  Uboreshaji  wa Shughuli za Mahakama Afrika Kati ya Mwaka 2003-2008, Msajili wa Mahakama ya rufaa nchini Mwaka 1989-1994 na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania  Mwaka 1989  na Hakimu na Hakimu Mkazi Mwaka 1974.

  Dk.Kudoja alisema Mwenyekiti huyo wa Baraza la UB, Jaji Bwana atawaongoza wajumbe  wajumbe 19 wa Baraza Hilo kutekeleza majukumu hayo ambao nao wanapitishwa na Bodi ya Wadhamini wa chuo hicho na watatekeleza majukumu waliyopewa.

  Mbali na Jaji Bwana  Alisema wajumbe wa Baraza Hilo ni Profesa Esther Mwaikambo kutoka Taasisi ya Vyuo Vikuu Binafsi(IES), Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya juu nchini, Dk.Sylvia Temu, Mkurugenzi Mtendaji Mstaafu wa Kituo Cha Uwekezaji nchini(TIC), Emmanuel Ole Naiko, Vicent Jonas, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi, George Simbeye, Wakili Mwandamizi wa Serikali Malata Gabriel , Mhadhiri wa Sheria wa chuo hicho, Baraka Mkami, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Halima Kihemba, Makamu Mkuu wa chuo hicho ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge la Katiba, Profesa Costa Mahalu, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mercy Sila, Dk.William Kudoja.

  Aidha Alisema wajumbe wengine ni Naibu Makamu Mkuu wa UB anayeshughulikia Fedha, Dk. Elifuraha Mtalo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu  Cha Kilimo Sokoine  anayeshughulikia Taaluma Profesa Peter Gillah, Mwenyekiti wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Johnson Lukaza, Mathias Massawe, Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia Katika Wizara ya  ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Evelyn Mbede, Balozi na Wakili mwandamizi nchini Mwainaidi Sinare Maajar, Wakili wa kujitegemea Vulfrieda Mahalu na Mkuu wa Shule ya Elimu ya UB, Profesa Elias Bayona.

  0 0

  Mkuu wa wilaya Ya Kilwa ,Abdallah Ulega (kushoto) akipokea sehemu ya mchango uliotolewa na Kampuni ya uchimbaji gesi ya PANAFRICAN ENERGY kutoka kwa Meneja wa huduma za jamii wa kampuni hiyo,Andrew Kashangaki .

  Na Abdulaziz Kilwa Masoko

  Wananchi wilayani Kilwa mkoani Lindi wameendelea kunufaika na wawekezaji,baada ya kampuni ya uchimbaji gesi ya PANAFRICAN ENERGY kuikabidhi halmashauri hiyo zahanati ya kijiji cha Nangurukuru ambayo ujenzi wake umegharimu Tshs 262 Milioni .

  Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo ambayo yalifuatiwa na utiaji sahihi mkataba wa ujenzi wa nyumba mbili za watumishi wa zahanati hiyo ambazo ujenzi wake hadi kukamilika utagharimu shilingi 458 milioni Meneja wa huduma za jamii wa kampuni hiyo,Andrew Kashangaki alisema katika ujenzi wa zahanati hiyo kampuni ya PANAFRICA N imechangia jumla ya shilingi 216,000,000.

  Ambapo pia kutokana na tatizo la wafanyakazi pia kampuni imeamua kufadhili ujenzi wa nyumba mbili za watumishi wa zahanati hiyo ambazo mkataba wenye thamani ya shilingi 458,000,000 ulisainiwa baina ya mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bw David Roberts na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa katika hafla hiyo fupi ya kukabidhi zahanati.

  Aidha Kashangaki alibainisha kuwa sera ya kampuni hiyo licha ya kufanya kazi ya uzalishaji wa Gesi ya songosongo pia hutoa misaada kwa jamiii ikiwemo kufadhili programu ya ufundishaji lugha ya kiingereza kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule za sekondari za halmashauri hiyo,ambapo jumla ya shule za sekondari 20 kati ya 28 zimenufaika na programu hiyo.

  'Wana kilwa tulianza kusaidia elimu ya kiingereza kwa kuzifikia shule 20 ila kwa umuhimu wa elimu kuanzia mwakani tutazifikia shule zote 28 za sekondari ikiwemo kusaidia upatikanaji wa Umeme Jua kwa shule ambazo hazina umeme 'Alimalizia Kashangaki.

  Mkuu wa wilaya Ya Kilwa ,Abdallah Ulega licha ya kuishukuru kampuni hiyo aliwataka wananchi kupuuza kauli zinazosemwa ikiwemo baadhi ya Vyombo vya habari kupotosha na kudai Manufaa ya Gesi yapo katika kijiji cha Songosongo pekee Na kubainisha baadhi ya maeneo yanayonufaika ikiwemo hapo Nangurukuru,Njinjo ,Somanga na kilwa masoko

  'Wananchi wa Kilwa nadhani ni mashahidi kampuni hii imesaidia wilaya yote si Kama Gazeti moja lilivyoandika hivi karibuni Huu ni upotoshaji mkubwa kwani elimu inasaidiwa wilaya yote,Afya Hivyo hivyo,Maji wananufaika mpaka Njinjo na hata mrahaba unaolipwa na kampuni hiyo zaidi ya Nusu inachangia katika sekta ya elimu Tuwe makini kuyajua haya yenye ukweli si maneno tu ya vijiweni...Alimalizia Ulega.

  Awali akifungua hafla hiyo Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Nangukuru,Hamis Ligweje alisema kabla ya PANAFRICAN kufadhili ujenzi huo,wananchi wa kijiji hicho kwa kushirikiana na wahisani wengine ikiwamo shirika la Action Aid walichangia walichangia jumla ya shilingi Milion 46 ujenzi ambao ulikuwa wa kusuasua mpaka wahisani hao walipojitokeza kusaidia kuikamilisha.

  'Hakika tulishindwa kabisa na Tulifikia hatua ya Kumuomba Rais Kikwete Kusaidia alipokuja katika ziara yake ambapo aliwaagiza Viongozi wa Wilaya kuangalia uwezekano ndipo Mkurugenzi aliehama Bw Mapunda Alifanikisha kuwaomba hawa wahisani na leo wametukamilishia na tunafarijika zaidi walipoamua kutujengea na Nyumba 2 kwa 4 za watumishi itasaidia sana si kwa Nangurukuru tu hata wasafiri watakaopata dharula katika barabara kuu.

  Licha ya kukabidhi Zahanati hiyo Mkurugenzi mkuu wa Pan African Energy,David Roberts Alikabidhi Vitanda Viwili vya kujifungulia akina mama ikiwa ni hatua ya awali ya kuokoa Akina mama katika suala la Uzazi.

  0 0

  Naibu waziri maji Amos Makalla leo ameongoza waumini wa kanisa kkkt dayosisi ya mashariki , viongozi wa majimbo na sharika zake katika harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa shule ya Elbeneza itakayokuwa kwa ajili ya shule ya msingi na sekondari. 

  Katika harambee hiyo fedha sh 124m zilipatikana kati ya hizo fedha taslimu sh 57m zilipatikana na 67m ikiwa ni ahadi. lengo la harambee ni kupata sh 120m kukamilisha majengo muhimu kuwezesha shule hiyo kufunguliwa januari mwakani. 

  Makalla alimpongeza askofu mameo, wachungaji na waumini kwa michango yao kufanikisha ujenzi Aidha alilipongeza kanisa kwa uumuzi wa kujenga shule imeonyesha namba kanisa lilivyo tayari kushirikiana na serikali na amewahaidi kuzitafutia changamoto mbalimbali walizompatia kuziwasilisha serikalini.
  Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akitoa neno kwa ajili ya harambee ya kanisa la kkkt Bungo -Morogoro.
  Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akishiriki ibada ya harambee kanisa la kkkt Bungo-morogoro.
  Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akipata mkono wa baraka kutoka kwa baba askofu wa dayosisi ya mashariki baada ya harambee kanisa la Bungo- morogoro.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mwanafunzi wa kidato cha nne Neema Steven Mtwanga(16) anayesoma katika shule ya sekondari Naboti Makambako,Njombe baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika utunzi wa insha katika shindano lililoandaliwa na Jumuiya ya uchumi ya maendeleo kusini mwa Afrika(SADC).Rais Kikwete alimpongeza mwanafunzi huyo wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa wakuu wa nchi za SADC unaofanyika katika mji wa kitalii wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe ambapo mwanafunzi huyo aliandika insha inayohusu mabadiliko ya tabia nchi.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wakuu na wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika SADC muda mfupi baada ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa jumuiya hiyo uliofanyika katika hoteli ya Elephant Hills mjini Victoria Falls Zimbabwe leo.Katikati ji mwenyeji wa Mkutano huo Rais Robert Mugabe na mkewe Grace Mugabe(picha na Freddy Maro)

  0 0


  0 0

  Mafundi wa TANESCO mkoa wa Kilimanjaro wakitizama namna ya kuokoa mafuta yaliyokuwa yakimwagika toka kwenye mtambo wa kupozea umeme.
  Mafundi wa Tanesco wakiandaa pipa kwa ajili ya kuwekea mafuta yaliyokuwa yakimwagika toka kwenye Transforma.
  Mafundi wa Tanesco mkoa wa Kilimanjaro wakijaribu kuelekeza mafuta yaliyokuwa yakimwagika kuingia katika pipa.
  Mafuta yakiwekwa katika Pipa.
  Mafundi wa Tanesco mkoa wa Kilimanjaro wakijaribu kurudishia mafuta katika mitambo ya kupozea umeme. 
  Mitambo ya kituo kidogo cha kupozea Umeme cha Bomambuzi mkoani Kilimanjaro kilipata hitilafu

  kwenye waya mkubwa wa kupitishia umeme  kutoka kwenye transfoma,hitilafu iliyosababisha moto uliounguza waya huo na baadaye baadhi ya nyanya kuangukia kwenye bodi ya transfoma kisha mfuta yakaanza kuvuja.  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0


  0 0


  Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Rais Robert Gabriel Mugabe wa Zimbabwe akimkabidhi Bi. Sheila Hashim Mbita, binti yake Brigedia Jenerali Mstaafu Hashim Mbita Tuzo ya Juu ya Taifa la Zimbabwe ya Nishani ya Royal Order Of Mwanamutapa kwa kutambua mchango wake katika ukombozi wa Taifa la Zimbabwe na nchi nyingine kusini mwa Afrika. Rais Mugabe alikabidhi tuzo hiyo wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa wakuu wa SADC unaofanyika katika mji wa kitalii wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe. Picha na Fred Maro
  ---------------------------
  Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imeishukuru na kuipongeza tena Tanzania kwa mchango wake mkubwa na wa hali na mali uliofanikisha jitihada za mapambano ya ukombozi yaliyoleta uhuru kwa nchi za Kusini mwa Afrika.

  Aidha, SADC imemshukuru na kumpongeza aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya Afrika, Brigedia Hashim Mbita wa Tanzania, kwa mchango wake na uongozi wake wa mapambano ya ukombozi, iwe katika nyanja ya kuviwezesha vyama vya ukombozi kwa hali na mali, raslimali na ushauri.

  Pongezi hizo kwa Tanzania zilitolewa usiku wa jana, Jumamosi, Agosti 16, 2014, na Kikao cha Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC – SADC Troika- kilichofanyika kwenye Hoteli ya Elephant Hills Resort, Victoria Falls, Zimbabwe, chini ya Uenyekiti wa Rais Hifikepunye Phohaba wa Namibia.

  Mkutano huo wa SADC Troika ulihudhuriwa na wanachama wa Asasi hiyo – nchi za Namibia, Lesotho na Tanzania. Nchi za Afrika Kusini, Madagascar na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilishiriki kama waalikwa maalum wa kikao hicho.

  Akizungumza kwenye mkutano huo kwa niaba ya nwenzake, Rais Pohamba alisema: “Tunawashukuru wananchi wa Tanzania kwa mchango wao wa kiuchumi, kijeshi na kimkakati katika kuunga mkono kwa hali na mali jitihada za mapambano ya ukombozi wa nchi zetu.”

  Aliongeza Rais Pohamba: “Sote tunaijua Tanzania, sote tunawajua Watanzania.  Kwa pamoja walitoa jasho na damu na sisi wenyewe katika kutafuta ukombozi wa nchi zetu. Tutaendelea kukumbuka na kuenzi mchango wao mkubwa na usiosahaulika kwa ustawi wa nchi zetu.”

  Kuhusu Mzee Mbita, ambaye Ripoti yake ya shughuli za ukombozi ilitarajiwa kuwasilishwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa SADC, Rais Pohamba alisema: “Brigedia Mbita alifanya kazi mchana na usiku kufanikisha shughuli za ukombozi wa Kusini mwa Afrika. Tunamshukuru sana kwa uongozi wake na mchango wake mkubwa katika kuleta uhuru wa nchi zetu.”

  Aliongeza: “Brigedia Mbita ni raia wa Tanzania na alikuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi Kusini mwa Afrika iliyokuwa na makao makuu yake mjini Dar es Salaam. Alichapa kazi kweli kweli na chini ya uongozi wake, vyama vya ukombozi vilipata misaada ya hali na mali, misaada ya kiroho na ushauri wa kijeshi kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa mtu wa shughuli za jeshi.” Mzee Mbita aliongoza Kamati ya Ukombozi tokea mwaka 1974 hadi ilipomaliza shughuli zake.

  Akizungumza kwa ufupi sana katika kikao hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alimpongeza sana Brigedia Mbita akisema kuwa alifanya kazi nzuri na kubwa na “tunampogeza kwa kazi nzuri sana ya kuandaa Ripoti hiyo.”

  Ripoti hiyo inayojulikana kama Mradi wa Hashim Mbita iliongozwa na Meneja wa Mradi, Profesa Arnold Temu wa Tanzania na imechapishwa na Kampuni ya Mkuki na Nyota, pia ya Tanzania, ambayo Mtendaji Mkuu wake, Mzee Walter Bgoya ameandamana na mwakilishi wa Mzee Mbita kwenye mkutano huo.

  Imetolewa na;

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu – Dar es Salaam.


  17 Agosti,2014


  0 0

   
   Wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania na baadhi ya wateja wakionyesha fataki kusheherekea Maadhimisho ya miaka 17 ya benki ambayo usheherekewa kila Agosti 15. Hafla hiyo ilifanyika katika  Tawi la kwanza kufunguliwa la benki hiyo la Samora tawi, lililofunguliwa mwaka 1997.
   Mkuu wa Idara ya Operesheni wa Benki ya Exim Tanzania, Eugene Masawe (wa kwanza kulia) naMeneja Mwandamizi wa Tawi la Samora, Nancy Huggin (wa kwanza kushoto) pamoja na wateja wa benki hiyo wakikata keki kusherehekea Maadhimisho ya miaka 17 ya benki ambayo usheherekewa kila Agosti 15. Hafla hiyo ilifanyika katika  Tawi la kwanza kufunguliwa la benki hiyo la Samora tawi, lililofunguliwa mwaka 1997. (Picha na mpiga picha wetu).
  Meneja Masoko Msaidizi wa Benki ya Exim Tanzania (wa kwanza kulia) Anita Goshashy akizungumza wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 17 ya benki ambayo usheherekewa kila Agosti 15. Hafla hiyo ilifanyika katika  Tawi la kwanza kufunguliwa la benki hiyo la Samora tawi, lililofunguliwa mwaka 1997.

  0 0

  signing deal
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (Mb) (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Rand Merchant Bank (RMB), Bw. Bruce Macfarlane (wa pili kulia) wakitiliana saini ya mkopo huo wa bilioni 300 za kitanzania. Kushoto ni Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Vipul Kakad na kulia ni Gregory Havermahl wa RMB wakishuhudia tukio hilo la utiliaji saini wa mkopo baina ya RMB na MeTL Group.
  Toast
  Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji wa Rand Merchant Bank (RMB), Bw. Bruce Macfarlane wakinywa shampeni baada ya kufanya "Toast" kama ishara ya kutakiana kheri na mafanikio kwenye biashara zao.
  Chat
  Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (Mb) (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Rand Merchant Bank (RMB), Bw. Bruce Macfarlane (kulia). mara baada ya kutiliana saini mkopo wa Bilioni 300 za Kitanzania.
  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0


  0 0

  DSC_0279
  Banda la Mtandao wa mashirika yapatayo 30 ya kupambana na matumizi ya kupita kiasi ya pombe nchini (Tanzania Network Against Alcohol Abuse) kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).

  SERIKALI imeshauriwa kutunga sera madhubuti ya udhibiti wa pombe katika jamii ili pamoja na mambo mengine kuhakikisha vijana wanalindwa dhidi ya bidhaa hiyo kwenye soko.

  Akizungumza na Moblog Tanzania jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo kikuu wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana, Msemaji wa Mtandao wa kupambana matumizi ya pombe kupita kiasi (Tanzania Network Against Alcohol Abuse) Bw, Mathias Kimiro amesema kwamba kuna umuhimu wa serikali kutunga sera mpya ya pombe ili kuzuia madhara kwa vijana na taifa kwa ujumla.

  “Kwa kawaida matumizi ya pombe kupita kiasi ina madhara makubwa katika afya ya mtumiaji lakini vile vile ina madhara kwenye familia kupitia kaya moja moja na kusababisha mateso kwa familia hasa watoto,” amesema Bw Kimiro.Amesema kwamba umuhimu wa kuwa na sera madhubuti ya kudhibiti pombe katika jamii ni kuangalia upya ni kwa kiwango ngani matangazo ya pombe yanavyohamasisha unywaji kupita kiasi kwenye jamii.

  Bw Kimiro aliongeza kwamba mashirika yasiyo ya kiserikali yataendelea kuwakumbusha mamlaka zinazohusika umuhimu wa kuwa na sera ya kudhibiti pombe katika jamii pamoja na kuangalia madhara ya matangazo kwa wasomaji wa mabango.
  DSC_0300
  Mkurugenzi Mtendaji wa Makangarale Youth Theatre, ambao ni taasisi chini ya Tanzania Network Against Alcohol Abuse (TAAnet), Bw. Ismael Mnikite akifafanua jambo kwa Mgeni Rasmi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Bibi Venerose Mtenga wakati wa maadhimisho hayo.

  0 0

   
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini pamoja na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kwa ajili ya viongozi wa SADC wanaohudhuria mkutano wa 34 wa wakuu wa nchi za SADC unaofanyika katika mji wa Victoria Falls nchini Zimbabwe(picha na Freddy Maro)

  0 0

   Naibu Mkamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB),  anayeshughulikia Masuala ya Fedha, Dk. Elifuraha Mtalo (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoaj na washiriki  wa mkutano kuwajengea uwezo maofisa wa serikali wa kujadili mikataba inayohusu uwekezaji pamoja na biashara, walipotembelea  Ofisi za Chuo Kikuu cha Bagamoyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa kuwajengea uwezo maofisa wa serikali kuhusu uandikaji wa mikataba inayohusu Uwekezaji na Biashara wakiwa katika majadiliano wakati wa mkutano huo. Washiriki katika mkutano huo wanatoka katika nchi 15 nchi za Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na Afrika Kusini. Mkutano huo umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB), Nordic Africa Institute (NAI) kwa kushirikiana na Trans African University Partnership (TANUP/PUTA), pamoja na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweden (SiDA) na FAO.zinazoendelea. Mkutano huo unafanyika jijini Dar es Salaam.
   Washiriki wakiwa katika majadiliano.
  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  0 0

  MWIGIZAJI wa kike wa filamu Aisha Bui, amedai kuwa alijitoa maisha yake kutoka na filamu yake ya Mshale wa Kifo, kutokana na sinema hiyo kutengeneza porini katika msitu hatari wenye wanyama wakali.

  Msanii huyo amedai alifanya hivyo kufuatia maoni ya wapenzi wa filamu ambao kila siku wanalalamika kwa kusema kuwa filamu zetu nyingi zimekuwa za mijini tu, huku baadhi ya matukio yakirudiwa kila katika sinema hizo jambo ambalo limekuwa likiongelewa mara kwa mara.

  “Nilijitoa maisha yangu kwa kuingia msituni kutengeneza filamu ya mapigano porini, kutafuta uhalisia, lakini najua na deni kwa wapenzi wa kazi zangu, wanajua kuwa mimi ni bora hivyo lazima niwe bora kila mwaka,”anasema Asha .

  Filamu ya Mshale wa Kifo Imetengenezwa na Yuneda Entertainment na imewashirikisha wasanii nyota kama Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’, Asha Bui, Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ na wasanii wengine

  Sinema hiyo imerekodiwa Mkoani Morogoro Vijijini ikiwa ni hatua nyingine kwa watayarishaji wa filamu kwenda kucheza filamu nje ya jiji la Dar es Salaam kama ilivyozoeleka, Aisha anasema kuwa maeneo yanayotumika yanarudiwa sana hata baadhi ya watazamaji wameyashika kwani yanaonekana kila filamu.


  Aisha Bui akiwa Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ katika moja ya scene za filamu ya Mshale wa Kifo.

  Aisha akiwa yupo porini na msanii mwenzake Gabo wakiendelea kurekodi filamu ya Mshale wa Kifo katika misitu ya Morogoro.

  0 0  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani (FIFA) limeahidi kuboresha makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) yaliyoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala ili yawe katika kiwango cha kisasa ikiwa ni pamoja na kuwa na vitendea kazi na miundombinu ikiwa ni pamoja na upanuzi wa ofisi.

  Hatua hiyo itaiwezesha TFF kuwa na mazingira bora ya kufanya shughuli zake kwa ufanisi.

  Vilevile kupitia programu zake mbalimbali ikiwemo ile ya Goal, FIFA imeahidi kushirikiana na TFF katika kuendeleza mradi wa kiuchumi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

  Mwanzoni mwa mwaka huu, TFF ilihamishia makao yake makuu katikati ya jiji ili kupisha maendeleo ya kuiwezesha Karume kuwa kituo cha kisasa kwa michezo na vitega uchumi.

  Akiongea mwishoni mwa ziara ya kikazi nchini, Meneja Miradi wa FIFA anayeshughulikia Programu za Afrika, Zelkifli Ngoufonja amesema FIFA inaunga mkono wazo la kuboresha makao makuu ya Karume na itasaidia kwa awamu uboreshaji huo.

  Katika kuhakikisha usimamizi na utekelezaji barabara wa mradi huo, ujumbe huo wa FIFA ulikubaliana na Kamati ya Utendaji ya TFF kuboresha ofisi za Karume ili jengo la utawala lianze kutumika huku mradi ukitekelezwa kwa awamu.

  Pamoja na kuongelea mradi huo muhimu kimichezo na kibiashara, ujumbe huo uliokuwa nchini kwa juma moja kufuatia mwaliko wa TFF ulikuwa na nafasi ya kujadiliana na TFF kuhusu maboresho katika masuala mbalimbali yakiwemo ya Utawala, Fedha, Masoko, Ufundi, Mashindano na timu za taifa.

  Akiongea kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya TFF, Rais wa TFF Jamal Malinzi aliushukuru ujumbe huo wa FIFA kwa msaada mkubwa katika historia ya mahusiano kati ya FIFA na TFF.

  Ujio huo unafuatia maombi ya TFF kuwa sehemu ya mradi wa Performance wa FIFA. Mradi wa Performance unaoshirikisha nchi mashirikisho 163 kati ya wanachama 209 wa FIFA, unalenga kuongeza ufanisi katika uendeshaji na uongozi wa nchi wanachama wa FIFA.

  SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

older | 1 | .... | 540 | 541 | (Page 542) | 543 | 544 | .... | 3272 | newer