Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 538 | 539 | (Page 540) | 541 | 542 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0

   Idara ya Uhamiaji nchini  imewakamata raia wanane  wa kigeni  (pichani chini) wakati wakiingia nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu  Nyerere wakiwa na pasipoti bandia za kusafiria za Mataifa tofauti ya Ulaya. 

  Wageni hao walikuwa wakijaribu kuingia nchini leo tarehe 15.08.2014 majira ya saa nane na nusu usiku kwa ndege ya shirika la ndege la Uturuki yenye Namba TK 603,  wakitokea Uturuki na kujitambulisha kuwa ni raia wa Sweden na Belgium. 

     Maofisa Uhamiaji katika kituo hicho baada ya kuwatilia mashaka na kuwafanyia ukaguzi wa kina, waligundua kuwa wageni hao ni Raia wa Iraq wakijaribu kuingia nchini Tanzania na pasipoti za bandia.       
  Kukamatwa kwa wageni hao ni jitihada za Idara ya Uhamiaji kupambana na Uhamiaji haramu nchini ambapo suala la zima la udhibiti wa mipaka linapewa kipaumbele. 

  Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tatu Burhan, anasema, kwa kutumia ujuzi na weledi walionao Maofisa Uhamiaji wanaendelea kufanyakazi usiku na machana kuhakikisha Sheria na Taratibu za Uhamiaji zinafuatwa.

   "Idara ya Uhamiaji, iko macho hatulali ili kuhakikisha ulinzi na usalama wa nchi ikiwa ndio jukumu letu namba moja unaimarika. kwahivyo, kila mtu awe raia wa kigeni na Watanzania wanapaswa kufuata Sheria na Taratibu zilizopo za kuingia na kutoka nchini"

     Hadi sasa, Wageni hao wamezuiliwa kuingia nchini na wanaendelea kushikiliwa na Maofisa wa Idara ya Uhamiaji kituoni hapo huku wakisubiri kurudishwa walikotoka.  

  Hili ni wimbi lilioibuika hivi karibuni kwa baadhi ya raia wa nchi za Iraq, Iran, Syria kujaribu kuingia nchini isivyo halali huku ikisemekana lengo lao kubwa ni kuingia Tanzania na baadae kutoka kuelekea mataifa ya Ulaya.

   Majina ya Wageni hao na Pasipoti bandia walizokuwa wakitumia pamoja na Majina halisi na Pasipoti zao za Iraq zilizogunduliwa baada ya upekuzi kwenye mabano ni kama ifuatavyo;
    
  1. ADEL SHAALAN MOHAN - SWEDISH, PPT. NO. EI282207 ( ADEL SHAALAN MOHAN Pasipoti Nam. G1489664)

  2. SAMER HELMI KAMIT    -  SWEDISH, PPT. NO. 87187804 ( LAZIM MOSA HITEET, PPT. Namba, A 13466001)

  3. MOHAMMED JAFAR AL MOSAWI - SWEDISH, PPT.NO. 87168871 (ALI HUSSEIN OLEIWI, PPT. NO. G 1111623)

  4. DAVID GABRIEL POBLETE    - SWEDISH PPT.NO. 86867751 (AYAD SAMI MAKTTOOF, PPT NO. A 4910203)

  5. SADDAM ALKHAMERI AREF   - SWEDISH, PPT NO. 81640513 (SAIF ALDAN FALIH HASAN, PPT. NO. G 1489664)

  6. ALI MOHAMMED ABDULLAH - IRAQ, PPT. NO. A 5931725

  7. OSAMAH ZAID GHAEB AL-OBAIDI    - IRAQ, PPT. NO. A 6175951

  8. ALI HUSSEIN OLEIWI      - IRAQ, PPT. NO. G 1111623 

      

  0 0
 • 08/15/14--14:08: Redd's Miss Temeke
 •  Warembo wanaotarajia kushiriki mashindano ya Redd's Miss Temeke, wakipozi wakati wa mazoezi  katika Klabu ya TCC, Chang'ombe, Dar es Salaam. Mashindano yatafanyika kwenye klabu hiyo, Agosti 22,mwaka huu. PICHA NA MDAU KHAMIS MUSSA

  0 0

  Mkuu wa Bregedi ya Nyuki ambae ni Makamo Mwenyekiti wa michezo ya Majeshi Bregedia Jenerali Sharif Sheikh Othman akizungumza na waandishi wa habari kuhusu michezo ya nane ya Majeshi ya Jumuia ya Afrika Mashariki. Mkuta huo umefanyika huko Bregedi ya Nyuki Migombani Zanzibar.
  Waandishi wa Habari kutoka vyombo tofauti wakimsikiliza Bregedia Jenerali Sharif Sheikh Othman (hayupo pichani) katika Mkutano wake na wandishi leo. 
  Mkurugenzi wa ufundi wa mashindano hayo upande (JWTZ) Luteni Kanali Joseph Bakari akitoa ufafanuzi wa Michezo hiyo. 


  Na Miza Othman Makame Maelezo- Zanzibar .
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Michezo ya nane ya Majeshi ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki itafanyika Zanzibar kuanzia tarehe 18 mwezi huu. 

  Akitoa Taarifa ya Mkuu wa Majeshi ya Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Makao Mkuu ya Brigedi Migombani kwa waandishi wa Habari, Mkuu wa Brigedi hiyo Brigedia Jenerali Sharif Sheikh Othman amesema lengo la michezo hiyo ni kujenga mashirikiano kati ya Majeshi na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Amesema katika Michezo hiyo kutakuwa hakuna mshindi wala aliyeshindwa na wote watakuwa washindi, lengo ni kujenga uweledi na nidhamu ndani ya majeshi yetu.

  “Hii ni fursa ya wanajeshi wetu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kukutana pamoja kama tunavyofanya katika mazoezi ya pamoja ya kijeshi”, alisema Brigedia Jenerali Sharif Sheikh Othman. 

  Amezitaja Nchi za Jumuiya hiyo zitakazoshiriki Michezo hiyo kuwa ni wenyeji Tanzania, Burundi, Rwanda, Kenya na Uganda. Amesema Michezo itakayochezwa na wanajeshi hao ni Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete, Mpira wa Mikono, Mpira wa Kikapu na Mbio za nyika na ameelezea viwanja vitakavyofanyika kwa ajili ya michezo hiyo Polisi ziwani ,Vyuo vya Mfunzo Kilimani, JKU Saateni, Pamoja na Viwanja vya Zimamoto na Uokozi.

  Brigedia Jenerali Sharif Sheikh ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa Michezo hiyo, amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuona vipaji vitakavyoonyeshwa na wanajeshi kutoka Nchi hizo .

  Akitoa ufafanuzi wa Michezo hiyo Leftinenti Kanali Joseph Bakari amesema pamoja na micheo hiyo kutakuwa na Burudani ya Ngoma za Utamaduni kutoka Vikosi vya Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Amesema jumla ya wanamichezo 505 wakiwemo Viongozi kutoka Nchi hizo watashiriki michezo hiyo itakayodumu kwa muda ya wiki mbili. 

  0 0

  Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Hon. Bernard K. Membe (C) with Hon. Abdallah Kigoda (R), Minister for Industry and Trade and Ambassador Rajabu Gamaha (L), Acting Permanent Secretary in the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation during the SADC Ministerial Conference held in Victoria Falls, Zimbabwe. Hon. Membe leads the Tanzanian delegation to the SADC Ministerial conference.
  Hon. Membe in a briefing meeting.


  SADC MINISTERIAL CONFERENCE GETS UNDERWAY

  The Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Hon. Bernard K. Membe, arrived in Victoria Falls, Zimbabwe, early today to lead the Tanzanian delegation to the SADC Ministerial conference.
  Ministers from the 15 SADC member countries are meeting in the Zimbabwean resort town to prepare the agenda for the 34th SADC Summit on August 17 and 18, which is expected to be attended by H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania.
  The Ministerial delegation includes Hon. Abdallah Kigoda, Minister for Industry and Trade.
  The SADC Heads of State and government are scheduled to deliberate on a range of issues on regional cooperation, including review of the region's Industrial Strategic Development Programme.
  They will also discuss establishment of a Regional Development Fund, which is proposed to have a seed capital of 1.2billion US dollars.
  The Ministerial conference was preceded by a meeting of Senior Officials.
  Ambassador Rajabu Gamaha, Acting Permanent Secretary in the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation led the Tanzania delegation to the meeting.
  SADC member countries are Tanzania, Botswana, Angola, Namibia, Mozambique, Malawi, Lesotho, Swaziland, Mauritius, Madagascar,Democratic Republic of Congo,South Africa, Zimbabwe and Zambia.

  0 0
 • 08/15/14--14:21: Tehe tehe tehe...haya tena!


 • 0 0

   Standard Chartered Bank’s Chief Executive Officer for the Eastern Africa region and Kenya, Lamin Manjang, (centre), speaks to the Hon. Vice President, Dr. Bilal, when the Bank’s Officials visited him at his office earlier this week. Left is the Bank’s Chief Executive Officer for Tanzania, Liz Lloyd.


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Charles Msonde kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (NECTA).


  Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam jioni ya jana, Alhamisi, Agosti 14, 2014, na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa uteuzi huo ulianza juzi, Jumatano, Agosti 13, 2014.


  Kabla ya uteuzi wake, Dkt. Msonde alikuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo hilo la mitihani.


  Dkt. Msonde anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Joyce Ndalichako, ambaye amerudi kuendelea na kazi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya kumaliza likizo yake ya kujinoa (Sabbatical Leave).


  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu.

  Dar es Salaam.


                                                                                15 Agosti, 2014


  0 0

  United States Ambassador Mark Childress met with eighteen secondary school students and four coordinators of The Kennedy-Lugar Youth Exchange and Study (YES) program in Tanzania.  
  The students (15-17 years of age) from Zanzibar and the mainland have been selected to live and study in the United States for up to a full academic year under the YES program.
  Among these students 11 are from Zanzibar and 7 from three regions in Mainland Tanzania, including Kilimanjaro, Tanga and Coastal regions.  During the program, students will live with host families, attend high school, engage in activities to learn about American society, acquire leadership skills and help educate Americans about their country and culture.
  The Kennedy Lugar Youth Exchange and Study (YES) Program was created in 2003 by the U.S. Department of State’s Bureau of Education and Cultural Affairs as a way to build bridges between citizens of the U.S. and countries around the world. 
  The YES program was launched in Tanzania in 2006 and to date 127 Tanzanian students have participated in this program. (Photo courtesy of the U.S. embassy).

  0 0

  Na Ali Issa Maelezo-Zanzibar. 
  Waziri wa Habari,Utamaduni , Utalii na Michezo Saidi Ali Mbaruok amepiga marufuku shughuli zote za upigaji wa disko katika eneo la Kiwengwa mpaka pale Serikali ya wilaya itapotoa maelekezo maalumu ya upigaji wa disko hilo kwa utaratibu unaofaa. 
   Agizo hilo amelitoa huko Kiwengwa Mkoa wa kaskazini “A”wilaya ya kaskazini B Unguja katika Ofisi ya umoja wa maendeleo wa kijiji cha kiwengwa wakati alipokuwa akifanya mazungumzo na wamiliki wa mabaa mikahawa,na kumbi na starehe juu ya kukithiri wa upigaji wa magoma kucha. 
   Amesema amelazimika kuzifunga shughuli zote za upigaji wa madisko usiku kutokana na kutokua na utaratibu mzuri wa upigaji ngoma hizo usiku hali ambayo inapelekea wageni wa kitalii na wenyeji kuchukia hali hiyo kwa kukosa usingizi na kusumbuliwa wagonjwa wenye shindikizo la damu. 
   Amsema hali hiyo haiwezekani kuona inaendelea katika hali kama hiyo kwani inapoteza muelekeo na mstakabali mwema wanchi na raia kwaujumla.
  “Nimepokea messsege ya kwamba watalii wamefika kusema wanaondoka na kutafutiwa sehemu nyengine wakapunzike kutokana na zogo kuwa jingi la madisko,hili hiliwezekani liendelee”lisema Waziri. Aidha alisema haiwezekani kuona utamaduni wa burudani unavurugwa kituambacho ni kosa kufanya hivyo na kwenda kinyume na taratibuzao selka zao.
   “Kuazia leo napiga marufuku mpaka sheha wa shehia hii aridhie hata kama kuna kibali ,kwani sheha yeye ndio anae jua hali za raia wake kuna wagonja,na wenyemaradhi ya kuhitaji kupumzika hatutaki kuona masuala yasio na utaratibu.”aliongeza Waziri.
   “Mimi kazi yangu ni kuutangaza utalii na sio utalii uharibiwe ,tufahamu kua ulalii Zanzibar ndio uchumi unao tegemewa kwa sasa kwa hivyo tulinde,”aliongeza Waziri Said. 
   Hata hivyo waziri huyo alichukia vitendo vya uwasharati vilivyo tapakaa katika kijiji hicho na kujenga mabaa karibu na nyumba za ibada kitu ambacho aliagiza kwa mkuu wa wilaya kuyafanyia kazi. 
   Nao wazazi wa kiwengwa Othumani mnyanja na mtumwa Rashidi walisema kiwengwa hivisasa imepoteza muelekeo kwani watoto wao wanaishia katika madisko na kukosa masoma kitiambacho ni hatari kwao. Aidha walisema kua watoto wao wakiwa na umri mdogo na kujishughulisha na masuala ya kimapezi jambo linalo wafanya nialama ya kupotea na kuacha mila za kislamu. 
   Wakitaja maeneo ya nayopigwa miziki na watoto wao kwenda ni pamoja na maeneo yanayo pigwa madisko hayo ni pamoja na ,kigorofani, vishani wazalendo pub, Kamili View,Obama Baa na kigorofani eneo la mafarasi.
   Nae miliki wa ukumbi wa Disko wa PERUU B, Peruce Osward Buhoma akiulizwa swali na waziri kwanini anafanya mazogo usiku alikiri kwa kusema hufanya hivyo kwaajili ya kuvuta wateja na kufanya ushindani kila mmoja kwa ajili ya kusikika zaidi kuliko mweziwe. 
   Bibi huyo na wezake walisema wanaweza kujirekebisha lakini pawe na utaratibu wa kupiga madisko kwa zamu na utaratubu mzuri utakao wekwa na uongozi.
   Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk (wakatikati) katika ziara ya kutembele mabaa na mahoteli ya kitalii, kutokana na wananchi kulalamikia vitendo vya upigwaji wa ngoma na vitendo viovu, (kulia) Mkuu wa Wilaya Kaskani (B) Unguja Khamis Jabir Makame na kushoto ni Sheha wa Kiwengwa Bw. Maulid Masudi Ame huko Kiwengwa.
   Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk na Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B, Khamis Jabir Makame wakipata maelezo kutoka kwa mmiliki wa Baa ya Vision Pub Francis Vicoguga juu ya undeshaji wa kazi zake katika Baa hiyo.
   Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk,akizungumza na wananchi na wamiliki wa mahoteli na baa katika kijiji cha Kiwengwa mara baada ya ziara yake ya kutembelea hoteli hizo.
  Mratibu wa Wanawake na Watoto Bi Mtumwa Rashid Khalifa ,mkaazi wa Kiwengwa akizungumzia kero wanazozipata kutokana upigwaji wa madisko katika mabaa kijijini hapo.(Picha na Jamila Abdalla – Maelezo Zanzibar)

  0 0


  15
  Viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Uchumi Supermarkets Tanzania Limited (USL) wakikata keki kuashiria kuanza kwa ushirikiano endelevu baina ya NHC na USL
  16
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu akitiliana saini hati ya makubaliano na Afisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan Ciano.
  17
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu akitiliana saini hati ya makubaliano na Afisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan Ciano.
  18
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu akitiliana saini hati ya makubaliano na Afisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan Ciano.
  19
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu akitiliana saini hati ya makubaliano na Afisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan Ciano.
  21
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu wakibadilishana hati ya makubaliano na Afisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan Ciano. Kwa picha zaidi na habari kamili

  0 0

  Bw. Ally Nchahaga - mratibu wa AutoFest. kushoto Erick Babu - Director wa DriveShaft magazine , kulia Bi. Mamou Ismail - Muakilishi wa Vision Investments wakati wa mkutano na wanahabari
   Likirudi kwa mwaka wake wa saba, tamasha la magari Tanzania (autofest) litakua likionyesha magari mapya, matoleo mapya ya pikipiki, burudani za muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali wa nchini na burudani nyingine za kusisimua kwa ajili ya familia nzima kuanzia Septemba 19-21, 2014. Tamasha la mwaka huu ambalo linaandaliwa na Vision Investment, litafanyika katika viwanja vya Biafra, Kinondoni. Anayetarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi ni Mhe. Dk Abdallah O. Kigoda, Waziri wa viwanda na Biashara. 
  ‘’Tukio hili linahusisha moja ya maonyesho muhimu sana na yenye mvuto katika ulimwengu wa vyombo vya moto”. Alisema Ally Nchahaga, Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Investments. “Lengo letu ni kuendelea kuleta aina mbalimbali ya bidhaa ya vyombo vya moto na huduma kwenye ‘Autofest’ ili wadau wapate kufurahia na kuridhishwa navyo.” alisema. 
  Tukio hili la mwisho wa wiki linategemea kuvutia zaidi ya watu nusu milioni, na kulifanya kuwa tamasha kubwa na maarufu la magari Tanzania. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008, Autofest sasa imekua ni Tamasha muhimu katika ulimwengu wa vyombo vya moto, likiwa ni onyesho pekee linalowaleta wapenzi wa magari pamoja. Ni onyesho kubwa linaloonesha magari ya abiria, magari ya biashara, pikipiki, bodi za magari, sehemu za magari, mashine na zana zinazohusiana na magari. 
  Burudani kwenye tukio zitahusisha, ‘Bumper to Bumper Auto Style Zone’ ambayo ni nafasi kwa wapenzi wa magari kuonyesha walivyoyapamba magari yao, ‘Kids Car Zone,’ ambayo itawaburudisha watoto wa umri kati ya miaka mitano na 14 kwa program za magari na elimu muhimu ya magari na usalama barabarani, na kuweza kuburudika na mbinu mbalimbali za kuchezesha magari kama kubadilisha gia, kufunga breki, na kuselelesha gari. 
  “Mwaka huu tunatarajia kwamba matokeo yatakua makubwa zaidi ukilinganisha na mwaka uliopita kutokana na kuongezeka kwa matangazo na mahusiano ya umma,” alisema Nchahaga. “Autofest itapelekea kutambulika kwa wadhamini wetu na program.” alisema. 
  Tamasha la Autofest linatoa nafasi za udhamini na maonesho. Kampuni ya Vision Investment inakaribisha wadhamini na watu wanaotaka kushiriki katika maonyesho ya mwaka huu kwa kujaza fomu ya maombi iliyopo katika mtandao wa www.autofest.co.tz. Fulana za Autofest sasa zinapatikana kwa mauzo, na mapato yatayopatikana yatatumika katika kuendeleza program za Autofest  
  Kuhusu Vision Investments 
  Vision Investments ni moja ya sehemu ambapo mawazo ya mikakati mbalimbali na teknolojia mpya inapohitajika ili kuweka biashara katika mstari wa mbele. Malengo ya Vision ni kutambua, kuunda, kuendeleza, kutoa na kuuza masuluhisho yanayofaa kukidhi mahitaji ya mteja ili kuhakikisha ufanisi wa hali ya juu, uwezo na thamani. Vision pia ni wataalamu wa mtandao,graphic design, ushauri wa Masoko na usimamizi wa matukio. 

  Kwa taarifa zaidi, tembelea:www.vision.co.tz


  0 0

  KLABU 12 za timu za soka za maveterani zinazooundwa na nyota wa zamani wa kandanda nchini zinatarajiwa kuchuana katika michezo maalum ya Tamasha la Miaka 16 ya Home Gym, itakayofanyika Septemba 6 kwenye uwanja wa Mwenge, Dar es Salaam.
  Aidha zaidi ya klabu 30 za Jogging nazo zinatarajiwa kupamba tamasha hilo ambalo litahusisha pia michezo mbalimbali ikiwamo ya netiboli, kuvuta kamba, kukimbia kwenye magunia na kukimbiza kuku.
  Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo, Andrew Mangomango, klabu za maveterani zilizothibitisha kushiriki tamasha hilo ambalo litapambwa na burudani ya muziki na shoo ya watunisha misuli, wanyanyua vitu vizito, ngumi na karateka ni Mbagala Veterani, Boko, 501, Break Point, Survey, Mwenge na Msasani.
  Mangomango alizitaja nyingine kuwa ni Biafra Veterani, Meeda, Mikocheni, Mbezi, Mabenzi, Segerea na Ukonga Veterani ambazo zinaundwa na nyota wa zamani wa kandanda waliowahi kutamba na timu kama za Simba, Yanga na Taifa Stars.
  Juu ya klabu za Jogging mratibu huyo alizitaja kuwa ni pamoja na Temeke Jogging, Mwananyamala, Kingungi, Amani, Magenge, Makuka, 501, Ndiyo Sisi, Wastaarab, Makutanom, Pasada, FBI, Kongowe, Oysterbay Police, Zakheem, Kwa Nyoka, Kawe Beach, Satojio, Kawe Mkwamani na nyingine.
  Mangomango aliongeza kuwa baada ya michezo yote wanamichezo washiriki watajumuika pamoja kuwatembelea yatima wanaolelewa kituo cha Chakuhama kwa ajili ya kuwapeleka misaada mbalimbali.
  "Ni tamasha ambalo litaambatana na michezo mbalimbali kama ya kuvuta kamba, kukimbiza kuku, kukimbia kwenye magunia, na shoo za watunisha misuli, wanamieleka, mabondia na karateka kisha kwenda kutembelea yatima," alisema.
  Mangomango alisema mgeni rasmi wa shughuli zote hizo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Kikosi cha Jeshi cha 501, J.B Kapumbe.
  Hii ni mara ya pili kwa tamasha hilo kufanyika mwaja jana lilifanyika wakati Home Gym ikiadhimisha miaka 15 tangu kuasisiwa kwake ambapo shughuli zake kuu ni kufanyisha mazoezi na kutoa ushauri juu ya afya ya mwili.

  0 0
 • 08/15/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Sikiliza ngoma ya kutia huzuni ya "Rote Rote Hasna Seekho" katika filamu ya "Andhaa Kanoon"

   

  Andha Kanoon (tafsiri yake “Sheria Pofu”) ni filamu ya Kihindi ya mwaka 1983 iliyoongozwa na mkongwe T. Rama Rao, na kuchezwa na Rajnikant, Hema Malini na  Reena Roy. Amitabh Bachchan na Madhavi pia walicheza nafasi ya wachezaji wageni wakicheza kama mume na mke.
  Nyota wengine kwenye filamu hii walikuwa Pran, Danny Denzongpa, Amrish Puri, Madan Puri, Prem Chopra na  Asrani.Dharmendra. Ilikuwa filamu iliyopigwa upya kufuatia ile ya mwaka 1981 ya kutoka Tamil ya  Sattam Oru Iruttarai iliyochezwa na  Vijayakanth 

  Ngoma za filamu hii  za  "Rote Rote Hasna Seekho" na "Andhaa Kanoon" si mchezo.


  0 0

   #‎DidYouKnow‬: Mpaka nusu ya mwaka 2014 zaidi ya makampuni 400 duniani yaliwekeza kwenye teknolojia ya ‪#‎Smartwatch‬ na nusu ya makampuni hayo yanatokea ‪#‎China‬ na ‪#‎Marekani‬. Kwa nusu mwaka huo zaidi ya saa za kidigitali Mil 3.4 ziliuzwa duniani kote na kutengeneza faida ya zaidi ya Dola Milioni 700. Je,Tanzania imeipokea vipi teknolojia hii.? Kwa hayo na mengine mengi sikiliza uchambuzi yakinifu wa Brown Nyanza ndani ya ‪#‎CloudsFm‬ kesho kuanzia saa moja asubuhi kwenye kipindi cha Power Break-fast on Saturday na Abel Onesmo.
  Brown Nyanza ni Mtanzania mtafutaji, anayejihusisha na mambo ya uchambuzi wa teknolojia ya vifaa vya kisasa vya kididitali  (kwa kimombo Smart gadgets Analyst) ambaye utakuwa naye kwenye kipindi hicho> USIKOSE!

  0 0

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. 
  Transforma zinazosambaza umeme katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi Mkoani Kilimanjaro zilizoko eneo la Bomambuzi zimewaka moto asubuhi hii muda mfupi baada ya kutokea shoti ambayo haijafahamika chanzo chake ni nini. 
   Moto huo umetokea majira ya saa 1:10 na kusababisha maeneo kadhaa ya mji wa Moshi kukosa umeme hadi sasa. 
   Globu ya jamii imeshuhudia kikosi cha zimamoto kutoka manispaa ya moshi kikijaribu kuzima moto huo ambao hata hivyo ulikwisha teketeza sehemu kubwa ya  kituo hicho cha kupozea umeme.
  Askari wa kikosi cha Zimamoto wakifika eneo la tukio asubuhi hii
  Wananchi wakishuhudia juhudi za kuzima moto huo
  Moto ukiendelea 
  Juhudi zikiendelea. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini


  0 0
 • 08/16/14--03:04: NANI KAMA BABA....???
 •  Baba akiwa amembeba mwanae Mgongoni huku akiendesha baiskeli yake kuelekea nyumbani kwake kama alivyonaswa na kamera mani wa Globu ya Jamii maeneo ya Manyoni,Mkoni Singida.


  0 0
 • 08/16/14--03:06: Msiba Boston Massachusetts
 • Familia ya ndugu Martin Kibusi na Steven kibusi inasikitika kutangaza kifo cha Mama yao mpendwa Lucia Kibusi kilichotokea August 15/2014 boston MA. Msiba upo nyumbani kwake Martin 364 Main st Apt 6 Reading, MA 01867.mipango ya kusafirisha mwili kwenda Tanzania inaendelea,tunaomba ushirikiano wenu wa hali na mali

  kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na
  Martin Kibusi 16179436400
  Steven kibusi. 16173142910
  Margareth Pelelwa Shauri 7816326161
  Mapi Andrew Mwankemwa
  857 251-8881
  Vilevile unaweza kutuma mchango kwa,Martin Richard Kibusi
  Bank of America
  Account number 4648847964
  Tunashukuru sana kwa ushirikiano wenu

  0 0

  Na Demetrius Njimbwi - Jeshi la Polisi,Dodoma

  Mkuu wa Dawati la Jinsia Nchini, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Adolfina Chialo, amewataka askari wote nchini hususan wale waliopo katika dawati la jinsia kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi ili kukomesha vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

  Hayo aliyasema jana wakati akifunga semina ya mafunzo ya siku tano yaliyotolewa  kwa Maafisa na askari wa Jeshi la Polisi pamoja na wadau wa Jeshi hilo katika mkoa wa Dodoma, wilaya ya Kongwa, ambapo washiriki hao wamepatiwa mafunzo ya namna ya kushughulikia makosa ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto.

  Kamishna Chialo, alisema kuwa, ili kutokomeza makosa yatokanayo na ukatili wa kijinsia na unyanyasaji kwa watoto, ameihasa jamii kutofumbia macho uovu au aina yeyote ya ukatili na badala yake kuripoti jambo hilo mahala husika au  katika madawati ya jinsia ya Polisi katika kituo chochote cha Polisi  ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa huku akiitaka jamii kuimarisha ulinzi dhidi ya mtoto ikiwa pamoja na malezi bora.

  Hata hivyo, akisoma lisala mbele ya mgeni rasmi na kwa washiriki wa semina ya mafunzo  hayo, Albert Bilia, ambaye pia ni mshiriki katika mafunzo hayo amesema kuwa, kutokana na mafunzo waliyopatiwa  yatasaidia zaidi katika kukabiliana na makosa ya ukatili na unyanyasaji ikiwa pamoja na vitendo viovu vinavyofanyika katika jamii husika alisema.

  Alisema kuwa, mafunzo haya pia yatasaidia kuongeza weledi uelewa na ufanisi kwa askari Polisi pamoja na wadau wengine walioshiriki mafunzo haya mahakama, waalimu, Ustawi wa jamii pamoja na madaktari, ambao tayari wamezifahamu sheria na mikataba mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ikiwa pamoja na sheria ya mtoto ya mwaka 2009 ya Tanzania Bara na sheria ya mtoto ya mwaka 2011 ya visiwani Zanzibar.

  Aidha, kamanda wa Polisi mkoani hapa, David Misime, amewataka maofisa pamoja na askari Polisi na wadau waliopatiwa mafunzo haya kuitumia vyema  elimu waliyopewa katika kutanzua na kubaini viashiria vyote vinavyosababisha ukatili kwa jamii  huku akiwaasa wananchi kuachana na mila na desturi zilizopitwa na wakati ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikichangia vitendo vya ukatili na unyanyasaji katika familia alisema.

  Kamanda, Misime, aliongeza kuwa, lengo kuu la mafunzo haya ni kujenga uelewa wakati wa kumuhudumia muathiliwa wa ukatili wa kijinsia na unyanyasaji huku akisisitiza suala la utoaji wa huduma bora kwa wateja na kuhakikisha kuwa elimu hiyo inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa alisema.

  0 0


older | 1 | .... | 538 | 539 | (Page 540) | 541 | 542 | .... | 3272 | newer