Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 533 | 534 | (Page 535) | 536 | 537 | .... | 3348 | newer

  0 0


  0 0

   Gari hili lina siku 4 tu toka lifike kutoka Uingereza. Lipo Sinza karibu na Sheli ya Big Bonn Petrol Station jijini Dar es salaam. Lina hali nzuri na tayari kuanza kazi wakati wowote. Madalali hawatakiwi....
  Kama unalihitaji kwa maelewano 
  piga simu namba 


  0 0

  Na Bin Zubeiry
  Mazungumzo yamekwishanyika na makubaliano yamefikiwa baina ya Patrick Phiri kutoka Zambia (pichani)  na Simba SC na sasa atakuja kufanya kazi tena Msimbazi, akisaidiwa na Nahodha wake enzi zake akifundisha timu hiyo, Suleiman Abdallah Matola ‘Osama’.


  Phiri ni kocha anayekubalika zaidi mbele ya mashabiki wa Simba SC miongoni mwa makocha waliowahi kufundisha klabu hiyo- rekodi yake ya kukumbukwa zaidi ikiwa ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2009/2010 bila kufungwa hata mechi moja.
  Lakini pia, namna alivyoweza kuiongoza Simba SC kuwatambia watani wa jadi, Yanga SC ni jambo lingine linalomfanya awe kocha mwenye heshima ya kipekee Msimbazi.  Katika awamu zote tatu alizofundisha Simba SC awali, Phiri hajawahi kufukuzwa- kwani amekuwa akiondoka mwenyewe kwa sababu mbalimbali.
  Kwa sasa, mume huyo wa Cecilia Mutale waliyezaa naye watoto wawili, Melesianiah na Patrick Junior, anarejea Simba SC akitokea Green Buffaloes ya Ligi Kuu ya Zambia.  Phiri ni kocha mwenye mafanikio tangu anacheza soka katika klabu za Rokana United (sasa Nkana F.C.) na Red Arrows zote za nyumbani kwao, Zambia kama mshambuliaji.
  Alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zambia kilichocheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 1978 na 1982, kabla ya kuiwezesha Chipolopolo kufuzu kwa AFCON ya mwaka 2008 nchini Ghana. 
  Akiwa kocha, Phiri pia aliiongoza timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Zambia kucheza Fainali za kwanza kabisa za Kombe la Dunia nchini Nigeria mwaka 1997 kabla ya kushinda tuzo ya kocha bora wa mwaka nchini mwake mwaka 1999.
  Simba SC imevunja  mkataba na Mcroatia, Zdravko Logarusic ikiwa ni siku moja tu baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na ZESCO ya Zambia katika mchezo wa kirafiki juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Loga ambaye aliongezewa Mkataba wa mwaka mmoja mwezi uliopita- inadaiwa amefukuzwa kwa sababu za kutotii miiko na maadili ya klabu


  Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva alisema jana kwamba uamuzi huo umekuja baada ya kumvumilia kwa kiasi cha kutosha.
  Loga ameondoka Simba SC baada ya kuiongoza katika mechi 21 tangu Desemba mwaka jana, kati ya hizo akishinda nane, sare tano na kufungwa nane.
  Loga aliyerithi mikoba ya Mzalendo, Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’, aliikuta Simba SC bado ipo kwenye mbio za ubingwa msimu uliopita, lakini mwishowe ikamaliza nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City, Yanga SC na Azam FC mabingwa.

  0 0

    Makamu wa Rais Dkt  Mohamed Gharib Bilal (kulia) akimzawadia tuzo Meneja wa Tigo Kanda ya Kusini Bw. Daniel Mainoya pale kampuni hiyo ya simu ilipoibuka mshindi wa nafasi ya kwanza kwa kundi la taasisi za mawasiliano katika maonesho ya Nanenane yaliyomalizika hivi karibuni mkoani Lindi.
  Bw. Daniel  Mainoya na mfanyakazi mwenzake Joe wakionyesha cheti cha ushiriki pamoja na kombe la mshindi wa nafasi ya kwanza kwa kundi la taasisi za mawasiliano katika maonesho ya Nanenane kitaifa yaliyomalizika hivi karibuni mkoani Lindi.
   Furaha iliyoje kutoka kwa wafanyakazi wa Tigo.


  0 0
 • 08/11/14--23:49: mambo ya kipanya


 • 0 0

  CHAMA CHA MAPINDUZI TAWI LA UINGEREZA LINAPENDA KUWATANGAZIA WANACHAMA NA WAPENZI WOTE WA CCM KUTOKA PANDE ZOTE ZA UINGEREZA KWAMBA KUTAKUWA NA MKUTANO MKUU WA TAWI TAREHE 30.08.2014 UTAKAOFANYIKA KATIKA JIJI LA READING KATIKA ANUANI IFUATAYO;
  THE PAVILION (FORMERLY RILEYS CLUB)
  143 – 145 OXFORD ROAD READING
  RG1 7UP

  KATIKA MKUTANO HUO PIA KUTAFANYIKA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA TAWI LA CCM UINGEREZA ILI KUJAZA NAFASI INAYOACHWA WAZI NA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA TAWI HILI TOKA KUANZISHWA KWAKE NDUGU AINA OWINO ANAYENG’ATUKA NAFASI HIYO.

  WAGOMBEA WA NAFASI YA MWENYEKITI WA TAWI WALIOPITISHWA NA HALMASHAURI KUU YA TAWI ILIYOKUTANA TAREHE 02.08.2014 NI;
  PETER GABAGAMBI
  KANGOMA KAPINGA 
  SAID SURURU
  WANACHAMA WOTE NA WAPENZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI UINGEREZA MNAHIMIZWA KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA MKUTANO HUO ILI KUTUMIA NAFASI YAKO PEKEE KUMCHAGUA KIONGOZI ATAKAYELETA MABADILIKO KATIKA TAWI.

  Imetolewa na Idara ya Itikadi Siasa na Uenezi 
  Chama Cha Mapinduzi Tawi La Uingereza.

  0 0  “Kwa wanaDMV: Inaelekea kumebakia suitafahamu au tafsiri fulani kuhusu matokeo ya uchaguzi wa DMV 2014 kufuatia takwimu za kura tulizotoa na kuwasilisha kwa bodi ya DMV. 
  Tamko hili linaweka wazi mshindi katika kila nafasi iliyogombaniwa. Hivyo kwa mujibu wa matokeo ya kura na wa katiba, wafuatao ndiyo viongozi wapya wa jumuia yetu kwa miaka miwili ijayo:
  RAIS- Iddy Sandaly
  MAKAMU WA RAIS - Harriet Shangarai
  KATIBU- Saidi Mwamende

  MAKAMU WA KATIBU-  Bernadetta Kaiza
  MWEKA HAZINA- Jasmine Rubama

  Tamko hili pia limefikisha Kamati ya Uchaguzi wa 2014 kwenye tamati yake.
  Mungu ibariki DMV, na adumishe mshikamano imara wa Watanzania.”

  Safari Ohumay
  Mwenyekiti

  0 0

  Mwanamitondo afanyae kazi zake za mitindo nchini Marekani Flaviana Matata, yuko nchini kwa ajili ya kufanya kazi za kijamii kupitia taasisi yake ya Flaviana Matata Foundation. katika mradi wa Back to school project /FMFstationarykit ambao unafadhiliwa na mfuko wa penseni PSPF,
  Baada ya mwezi January Flaviana kugawa vifaa shule za msingi za jijini awamu hii ameenda Mtwara na kufanikiwa kugawa shule za Msingi Mtua na Chemchem ziliyopo Nachingwea pamoja nashule za msingi Litingi na Mnengulo ziliyopo Lindi.
  bado wanaendelea kugawa vifaa hivyo kwa shule za msingi mikoa mingine "hadi sasa tumeshagawa vifaa kwa watoto 700 na bado kuna kits 800 vitasambazwa Tunduma ,Tunduru na Monduli"
  Flaviana alitoa shukran kwa PSPF kwa kudhamini huu mradi na akasisitiza makampuni na mashirika kujaribu kuwezesha elimu kama hali halisi inavyoonekana kwenye picha hadi leo kuna wanafunzi wanasoma chini na mti, na walio madarasani,madarasa ni mabovu na hayana madawati.
  2G2A8088 Flaviana Matata ameongozana na Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin pamoja na wafanyakazi wa PSPF katika zoezi la kukabidhi vifaa hivyo. Martin2G2A81742G2A81962G2A82342G2A8279IMG-20140811-WA0044IMG-20140811-WA0029

  0 0

  Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), wakizindua kwa pamoja huduma mpya ya India Desk  inayowaunganisha wawekezaji na wafanyabiashara nchini India kufanya huduma za kibenki bila ya kuwa na akaunti nchini. Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay, mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi, Ally Laay (kushoto), Celina Mkonyi (kulia). Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay, mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi, Ally Laay (kushoto), Celina Mkonyi (kulia).
  Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay wakiwa na furaha baada ya kuzindua huduma hiyo. 
   Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (katikati) akiwa na maofisa wa Benki hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya India Desk.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  Na Eleuteri Mangi- MAELEZO

   Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 30 wa mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki (BOG) utakaofanyikia jijini Dar es salaam tarehe 22 mwezi huu. 
   Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (pichani)   na Rais wa Benki ya PTA kwa vyombo vya habari, mkutano huo utakuwa wa siku moja. 
   Taarifa hiyo imeeleza kuwa lengo la mkutano huo ni kujadili masuala mbalimbali ya kibenki ikiwemo mpango mkakati wa benki hizo na masuala ya fedha na uchumi kwa nchi washirika. 
   Wajumbe wa mkutano huo ni Mawaziri wa Fedha na uchumi wa nchi washirika ambao ndio chombo cha juu cha ngazi ya maamuzi ya benki katika nchi zao. 
   Aidha, taarifa hiyo imeongeza kuwa mkutano huo utatanguliwa na semina ya wafanyabiashara itakayofanyika Agosti 21 siku moja kabla ya mkutano mkuu wa Magavana hao. 
   Benki ya PTA ilianzishwa mwaka 1985 ikiwa na jumla ya washirika 22 ikiwemo nchi 18 ambazo ni Burundi, Comoros, Djibouti na Congo. 
   Nchi nyinine ni Misri, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Malawi, Mauritius, Rwanda, Seychelles, Somalia, Sudan, Uganda, Zambia, Zimbabwe na mwenyeji Tanzania. 
   Aidha, PTA inashirikiana na nchi nyingine nje ya bara la Afrika ambazo ni Belarus na China. Washirika wengine Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Kampuni ya Bima ya Mauritia iitwayo Eagle na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Mauritius.

  0 0

  Mtuhumiwa Abdul Ghan Peer Bux.

   Imeelezwa kwamba Wapakistani wawili, Abdul Ghan Peer Bux na Shahbaz Malk (pichani) waliokamatwa  wakiwa  na  Watanzania  wanaotuhumiwa kwa kukutwa  na  madawa ya kulevya wametoroka nchini. 

  Watuhumiwa hao walikamatwa Februari 21, 2011wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya  shilingi  bilioni 6.2,  Mbezi Beach  maeneo ya  Jogoo  jijini Dar sa Salaam.Habari za uchunguzi ndani ya Mahakama Kuu zinasema kuwa, Jaji Grace Mwakipesile anayesikiliza kesi  hiyo  inayotarajiwa kuendelea kusikilizwa kesho Jumatano, ametoa amri ya kukamatwa  kwa  watuhumiwa  hao. 
  Kesi hiyo ambayo ilisikilizwa mahakamani hapo Julai 4, mwaka huu ilidaiwa kuwa Wapakistani hao walikamatwa  na  kikosi  kazi  cha  kuzuia na kupambana na madawa  ya kulevya kisha kudhaminiwa lakini wametoweka bila kuhudhuria mahakamani hata siku moja.

  Mtuhumiwa Shahbaz Malk. 

  Imeelezwa kuwa, baada ya watuhumiwa hao kudhaminiwa na wadhimini wawili, Julai 4, mwaka mahakama iliambiwa kuwa wadhamini hao wamefariki dunia. Hata hivyo, jaji anayesikiliza kesi hiyo aliwaagiza ndugu waliotoa taarifa hiyo kupeleka cheti halisi cha kifo kesho na watuhumiwa wahudhurie mahakamani  hapo.
  Madawa ya kulevya yaliyokamatwa na watuhumiwa
   hao yenye thamani ya  shilingi  bilioni 6.2.

  Watanzania waliokamatwa na Wapakistani hao waliachiwa huru baada ya kulipa dhamana ya shilingi 10,000,000 ambapo wadhamini wao ni Raza Hussein Kanji ambaye alipewa stakabadhi namba 3406367 na Nazar Mohamed Nurd alikatiwa yenye namba 3406355.
  Kamanda wa Kupambana na Kudhibiti 
  Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa.

   Februari 21, 2011 polisi chini ya kamanda wao, Godfrey Nzowa waliwakamata Wapakistani hao wakiwa na Watanzania wawili, William Chonde na Kambi Zuberi ambao wapo nje kwa dhamana wakituhumiwa kukutwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi bilioni 6.2.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Novatus Makunga ameeleza kuwa serikali wilayani humo imejipanga kuondoa kero zote zinazoawakabili wananchi wanapoenda kutibiwa katika hospitali ya serikali ya wilaya hiyo zikiwemo lugha chafu za watumishi wa hospitali hiyo 
  Mhe.  Makunga ametoa kauli hiyo katika mikutano yake ya hadhara na wananchi wa mitaa ya Kingereka na Kibaoni katika kata ya Hai Mjini. 
   Awali wananchi wa mitaa hiyo walieleza kuwa kero kubwa wanayokumbana nazo katika hospitali hiyo ni pamoja na lugha chafu katika eneo la mapokezi,ukosefu wa dawa pamoja na madaktari kutokaa katika vyumba vyao vya kuwahudumia wagonjwa. 
   Mkuu huyo wa wilaya ameeleza kuwa hatua za awali zimeshaanza kuchukuliwa ikiwemo kuanzisha mpango unaojulikana kama sauti ya jamii ambapo kupitia mpango huo wananchi wanaokumbana na kero katika hospitali hiyo wamekuwa wakitoa taarifa. 
   "Taarifa hizo zimekuwa zikijadiliwa na kamati ya uongozi ya hospitali hiyo kila mwezi na kuchukuwa hatua na baadaye mrejesho kutolewa kwa wananchi,hivyo zote kwa pamoja tupambane na uvunjaji wa maadili katika hospitali yetu" alisema Makunga 
   Aidha amewataka wananchi hao kutoa taarifa mara moja pale wanapokumbana na kero yoyote kwa mganga mkuu wa wilaya ama mganga mfawidhi ama muuguzi mkuu na hata yeye kama mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ambapo wote hao walitoa nambari zao za simu za mkononi. “Tumeanza kuchukuwa hatua na itakuwa vyema pale unapokumbana na kero kutuletea taarifa hapo hapo bila ya kuchelewa,sasa wakati umefika wa kuambiana ukweli,kama mtu anaona kuhudumia umma kunampotezea wakati basi akaanzishe zahanati yake ambapo huko atakuwa huru kutumia lugha chafu,”aliongeza Makunga 
   Ameeleza maboresho makubwa yaliyofanywa na serikali katika hospitali hiyo hayatakuwa na maana endapo kero hizo zitaendelea kudumu na kusababisha wananchi kupata huduma kwa mateso makubwa. Makunga amezitaja huduma zilizoboresha kuwa ni pamoja na upasuaji mkubwa kwa kuwa na chumba cha kisasa,ukamilishaji wa wote ya upasuaji pamoja na kukamilishwa kwa huduma za X-Ray ambayo itafunguliwa rasmi na mwenge wa uhuru mnamo tarehe 22 ya mwezi huu
   Kwa upande wake mganga mfawidhi wa wilaya ya Hai,Dk Fanuel Mollel alikiri kwamba huko nyuma kulikuwa na tatizo kubwa la madaktari wa hospitali hiyo kutumia muda mrefu kwenda kunywa chai kwa kutoka pamoja kwa makundi na hivyo kusababisha wagonjwa kusota kwa muda mrefu.
   Amesema hatua za kudhibiti tabia hiyo zimeshachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuanzisha kantini eneo la hospitali hiyo. 
   Kuhusiana na upungufu wa dawa ameeleza hali hiyo inatokana na taratibu za serikali ambapo kwa sasa zinataka dawa ziagizwe kutoka katika bohari kuu ya madawa(MSD) ambapo mara nyingine ukumbwa na upungufu wa dawa

  Wananchi wa mitaa ya Kingereka na Kibaoni katika kata ya Hai Mjini wakiwa katika mkutano huo
  Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe.  Novatus Makunga akikabidhi kadi kwenye  mkutano wake wa  hadhara na wananchi wa mitaa ya Kingereka na Kibaoni katika kata ya Hai Mjini. 
  Mganga mfawidhi wa wilaya ya Hai,Dk Fanuel Mollel akiongea na wananchi
  Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe.  Novatus Makunga akiongea mkutano wake wa  hadhara na wananchi wa mitaa ya Kingereka na Kibaoni katika kata ya Hai Mjini. 

  0 0

   Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Bw. Omari Issa akifafanua jambo wakati wa mkutano wa awali wa maandalizi ya kujadili vipaumbele vya sekta ya afya vitakavyoingizwa katika BRN. Mkutano huo wa siku nne umeanza jijini Dar es Salaam leo Jumanne. Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid.

   Mkurugenzi wa SIKIKA, Bw. Irinei Kiria akiwasilisha mada kuhusu sekta ya afya wakati wa mkutano wa awali wa maandalizi ya kujadili vipaumbele vya sekta ya afya vitakavyoingizwa katika Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Mkutano huo wa siku nne umeanza jijini Dar es Salaam leo Jumanne. katika ukumbi wa Kunduchi Beach Hotel and Resort. 

   Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada wakati wa mkutano wa awali wa maandalizi ya kujadili vipaumbele vya sekta ya afya vitakavyoingizwa katika Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Mkutano huo wa siku nne umeanza jijini Dar es Salaam leo Jumanne katika ukumbi wa Kunduchi Beach Hotel and Resort.

   Washiriki wakifuatilia mada wakati wa mkutano wa awali wa maandalizi ya kujadili vipaumbele vya sekta ya afya vitakavyoingizwa katika Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
   Hatua nane za kisayansi zinazotumiwa na Mpango wa BRN katika kuhakikisha wananchi wanapata mafanikio ya haraka katika miradi iliyochaguliwa zilipowakilishwa na Mkurugenzi wa Mipango wa PDB, Bw. Gerase Kamugisha (hayupo pichani) wakati wa  maandalizi ya kujadili vipaumbele vya sekta ya afya vitakavyoingizwa katika Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Mkutano huo wa siku nne umeanza jijini Dar es Salaam leo Jumanne katika ukumbi wa Kunduchi Beach Hotel and Resort.

  0 0

  His Excellency the former president of the United Republic of Tanzania, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, rings the bell officiating the first trading day of Swala Oil & Gas Tanzania Plc on the Dar es Salaam Stock Exchange (DSE). With him Swala CEO, Mr. David Mestres Ridge (L) and Swala Chairman, Mr. Ernest Massawe (R)
  Swala Oil & Gas (Tanzania) Plc (“Swala” or “the Company”) (http://www.swala-energy.co.tz) today listed on the Dar es Salaam Stock Exchange (“DSE”) becoming the first public owned Oil and Gas Company in East Africa. 
   The company is the 20th to list on the DSE and the 2nd to list under the Enterprise Growth Market (“EGM”), an equity market specifically intended for Small and Medium Enterprises (SMEs) and start-ups.
  The company listed on the EGM with 99 million shares after a very successful Initial Public Offer (“IPO”) which raised 6,650,000,000 Billion TZS. This IPO was oversubscribed by nearly 4 million shares and has raised nearly 2 billion TZS more than the maximum subscription of 4.8 billion TZS.

  The momentous event took place at the DSE offices and was graced by His Excellency the former President of the United Republic of Tanzania, Ali Hassan Mwinyi who rang the bell at 10:30 am EAT to officiate the event, the traditional symbol signifying the opening of Swala’s first trading day.

  Former president Mwinyi asserted that Swala’s oversubscription shows a great investment appetite amongst Tanzanians in investing in their country’s economy and a growing confidence in the national Stock Exchange.

  Mr. Moremi Marwa, CEO of the DSE remarked, “In October of 2013, the DSE introduced the EGM segment at the Exchange whose main objective is to enable Small and Medium Sized business access to the capital market. Swala is the second company to list on EGM within a year of its launching. Listing on DSE comes with transparency, good corporate practices and proper disclosures. Swala has made the right decision to join the family of companies aiming at being open and transparent to their shareholders, the public and the world at large”.

  Chairman of Swala, Mr. Ernest Massawe further added, “Today’s listing on the EGM marks a new chapter for our company and another step forward in realizing our ambition to achieve a successful venture based on private and public partnership. We wish to extend our thanks to all those who have made this possible: the regulators, our advisors and, most importantly, our new investors. The company is now ready to commence its 2014 seismic programme and we look forward to fruitful results. I am confident that Swala, as a public company, will be able to capitalize on its achievements to date and continue to deliver for all its stakeholders”.

  0 0

   Meneja masoko wa bia ya Castle lite Vimal Vaghmaria  kushoto mwenye miwani,Meneja wa Castle lite  Geofray makau   katikati na Meneja msaidizi wa Castle lite Tanzania Victoria kimaro wakionyesha chupa ya bia hiyo kwenye uzinduzi wa kampeni ya shindano la kuwapata washindi wa Castle lite VIP Yacht Party ambapo washindi watafanya tamasha kubwa ndani ya Boti katika bahari ya Hindi.
    Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo katika Hotel ya Slip way washindi wa Castle lite VIP Yacht Party watafanya tamasha kubwa ndani ya Boti katika bahari ya Hindi.
   Meneja masoko wa bia ya Castle lite Vimal Vaghmaria kushoto mwenye miwani,Meneja wa Castle lite  Geofray makau   katikati na Meneja msaidizi wa Castle lite Tanzania Victoria kimaro wakionyesha chupa ya bia hiyo kwenye uzinduzi wa kampeni ya shindano la kuwapata washindi wa Castle lite VIP Yacht Party ambapo washindi watafanya tamasha kubwa ndani ya Boti katika bahari ya Hindi.

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe akisalimiana na Salum Said Mchora ambaye amepoteza mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 23 Said S. Mchora  mkazi wa Masasi,Majengo.Watu 8 wamepoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa kwenye ajali ya gari iliyotokea Mtama tarehe 8/8/2014

  Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe akititoa  mkono wa pole kwa Ndugu Said Mchora ambaye amepoteza mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 23 Said S. Mchora  mkazi wa Masasi,Majengo kwenye ajali ya gari iliyotokea Mtama karibu na stendi ya mabasi ya Masasi,Katikati ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye ambaye alitoa salaam za rambi rambi kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi.
  Watu 8 wamepoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa kwenye ajali ya gari iliyotokea Mtama tarehe 8/8/2014

  Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe akiongozana na  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye kwenda kutoa salaam za rambirambi kwa familia zilizopoteza jina wao kwenye agari ya gari iliyotokea Mtama,kulia ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Washauri wa Madini,Richard Kasesela .Watu 8 wamepoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa kwenye ajali ya gari iliyotokea Mtama tarehe 8/8/2014

  Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye wakimsikiliza Mzee Halfani Libaba ambaye ameondokewa na mtoto wake wa kiume Rajab Halfani kwenye ajali mbaya ya gari lililoacha njia wakati dereva akijaribu kumkwepa mbuzi na kusababisha vifo vya watu 8.

   Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe  na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye pamoja na viongozi wengine wa CCM Mkoa na Wilaya ya Lindi wakionyeshwa eneo ambalo ajali ilitokea.
   Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye wakimpa pole mpiga picha maarufu Mohamed Selemani ambaye amelazwa kwenye hospitali ya Nyangao mkoani Lindi.
   Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Mhesimiwa Bernard Membe akimjulia hali na kumpa pole Ndugu Shaaban Issa mmoja wa majeruhi watatu wa ajali ya a gari iliyotokea Mtama na kusababisha vifo vya watu 8.

  0 0

  Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), wakizindua kwa pamoja huduma mpya ya India Desk  inayowaunganisha wawekezaji na wafanyabiashara nchini India kufanya huduma za kibenki bila ya kuwa na akaunti nchini. Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay, mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi, Ally Laay (kushoto), Celina Mkonyi (kulia). Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay, mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi, Ally Laay (kushoto), Celina Mkonyi (kulia).
  Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay wakiwa na furaha baada ya kuzindua huduma hiyo.
  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma India Desk inayotolewa na Benki ya CRDB.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
 • 08/12/14--02:17: umbea wa nathan mpangala


 • 0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akimshukuru Ofisa wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (kushoto) baada ya kupokea hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 40 msaada uliotolewa kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, jijini Arusha. Wapili kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, na kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. 
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kupokea hundi ya Sh. Milioni  kwa ajili ya maandalizi ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, kutoka kwa Ofisa wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (watatu kulia). . Picha zote na Felix Mwagara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani  inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, jijini Arusha. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Wapili kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, na kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.

  Picha zote na Felix Mwagara wa 
  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  0 0

  Mkuu wa Habari wa BBC Idhaa ya Ulimwengu, Bi. Nikki Clarke akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha kurushia Matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC jijini Dar es Salaam, katika Jengo lao lililopo Mikocheni jana jioni. Kushoto ni Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC,  Bw. Ali Saleh.
  Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Bw. Ali Saleh (wa tatu kulia) akiwapatia maelekezo Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Dkt. Salim Ahmed Salim na Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba ya namna Idhaa hiyo inavyoandaa vipindi yake na inavyopeleka hewani wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Kituo cha kurushia Matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC,jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC jijini Dar es Salaam, Bw. Hassan Mhelela (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo pamoja na kuitambulisha timu yake.
  Taswira za Studio za BBC jijini Dar es salaam.
  Chumba cha Habari cha BBC jijini Dar es salaam.
  Picha na zote na Othman Michuzi.


older | 1 | .... | 533 | 534 | (Page 535) | 536 | 537 | .... | 3348 | newer