Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live

NEC yafafanua kuhusu daftari la kudumu la wapiga kura

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajiwa kuanza hivi karibuni linamhusu kila raia mwenye sifa ya kupiga kura.

Ufafanuzi huu unakuja wakati pakiwa na mawazo tofauti ya nani hasa anatakiwa kushiriki katika zoezi hilo huku baadhi ya watu wakidhani kuwa jambo hili linawahusu wale ambao hawakupata kujiandikisha kupiga kura au waliopoteza kadi au waliofikia umri wa kupiga kura.



Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva (pichani) amesema jana jijini Dar es Salaam kuwa katika kufanya maboresho hayo na kupata daftari linaloaminika zaidi, Tume inatarajia kutumia mfumo mpya wa “Biometric Voters Registration System” au mfumo ambao utatumia utambuzi wa watu kwa alama za binadamu.

Kwa kutumia mfumo huu, muhusika atachukuliwa alama za vidole vyote vya mikono 10, picha na sahihi yake.

Hii ni tofauti na mfumo uliokuwa unatumika wa “Optical Mark Recognition” (OMR) ambapo muhusika alikuwa anajaza fomu na kuchukuliwa alama ya kidole kimoja tu ambao Jaji Lubuva anasema ulikuwa na uwezekano wa watu kujiandikisha hata mara mbili bila kutambulika.

 “Watu wote wenye sifa watatakiwa kujiandikisha upya katika mfumo huu mpya na kupatiwa kadi mpya,” alisema.

Akitoa ufafanuzi zaidi alisema uboreshaji wa daftari hilo unatokana na matakwa ya kisheria na malalamiko ya wadau mbalimbali.

Alisema tangu kufanyika kwa uchuguzi mkuu mwaka 2010 pamekuwa na malalamiko toka kwa wadau mbalimbali kama vyama vya siasa, mashirika yasiyo ya kiserikali na wapiga kura wenyewe kuhusu haja ya kuboresha daftari hilo na kuondoa watu ambao hawastahili kuwamo kama waliofariki na kuongeza wengine wenye sifa.

“Malalamiko haya yanafanya imani ya watu juu ya daftari la wapiga kura iwe ndogo,” alisema.

Alifafanua kuwa sheria inaitaka NEC kuboresha daftari la wapiga kura mara mbili kati ya uchaguzi uliopita na uchaguzi unaokuja.

“Ni kutokana na matakwa ya kikatiba na sheria na malalamiko haya, NEC imelazimika kufanya zoezi hili kabla ya kura ya maoni na uchaguzi mkuu ujao 2015,” alisema.

Akizungumzia matayarisho ya zoezi hilo, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Bw. Julius Mallaba alisema yanaridhisha na kuendelea vizuri.

Alisema maboresho ya daftari hilo kwa awamu hii ni mahsusi kwa ajili ya kura ya maoni kuhusu katiba mpya mapema mwaka 2015, uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 pamoja na chaguzi ndogo zitakazofuata baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

“Sehemu kubwa ya maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura yamekamilika,” alisema.

Akielezea zaidi Bw. Mallaba alisema tayari NEC imeanzisha na kuhakiki vituo vipya na kuviweka katika ngazi ya vitongoji, vijiji na mitaa.

Vituo hivyo vimeongezeka kutoka vituo vya awali 24,919 na kufikia vituo 40,015 nchi nzima.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa tayari ununuzi wa vifaa vya uandikishaji ikiwemo Biometric Voter Registration Kits umeshafanyika.

“Maandalizi ya melekezo kwa maafisa waandikishaji, waandishi wasaidizi pamoja na vyama vya siasa yameshafanyika,” alisema na kuongeza kuwa kanuni za uboreshaji zimeshaandaliwa.

Alisema kuwa maandalizi ya kituo cha kuhifadhia taarifa na mkakati wa utoaji wa elimu ya mpiga kura na machapisho mbalimbali tayari yameshakamilika.

Aliongeza kuwa katika maandalizi hayo, Tume imeshakutana na wadau mbalimbali kama wahariri, viongozi wa dini na vyama vya siasa ili kujadiliana na kupata maoni yao kuhusiana na zoezi hilo.

“Tunashukuru sana kwa michango ya mawazo yao…tunayapokea na kuyafanyia kazi,” alisema na kuongeza kuwa katika kuboresha zaidi, Tume inatarajia kukutana na makundi mengine kama vijana, kina mama na walemavu.


NEC imepewa jukumu la kisheria kuandikisha wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura na kuliboresha daftari hilo kwa ajili ya uchaguzi wa Rais na wabunge ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


BURIANI ROBIN WILLIAMS

$
0
0

Mcheza sinema na mchekeshaji maarufu duniani aliyepata kushinda tuzo ya Oscar Robin Williams amefariki dunia katika kifo kinachoshukiwa ni cha kujiua mwwenyewe. Alikuwa na umri wa miaka 63.

 

Kwa mujibu wa polisi wa Marin huko Calofornia, Marehemu Williams alikutwa hana fahamu huku akiwa hapumui majira ya saa sita za mchana Jumatatu nyumbani kwake Tiburon, kufuatia simu ya dharura iliyopigwa polisi hapo. Alitangazwa amefariki dunia saa sita na dakika mbili baada ya wahudumu wa huduma za dharura kufika. Alionekana hai kwa mara ya mwisho Jumapili.
 Uchunguzi wa kifo chake unaendelea, lakini ofisi ya Sheriff  inashuku ni kifo cha kujiua mwenyewe kwa dawa ya asphyxia. Msemaji wa familia Mara Buxbaum amesema kwamba Williams alikuwa na tatizo lam usongo wa mawazo (depression) hivi karibuni. Ametoa ujumbe wa familia kwamba wangependa wasibugudhiwe katika wakati huu mgumu wa msiba
 Mke wa marehemu Susan Shneider amekaririwa akisema kwamba: “Asubuhi hii nimempoteza mume, rafiki yangu mkubwa wakati dunia imempoteza msanii wake kipenzi. Nimevunjika moyo kabisa. Kwa niaba ya familia ya Robin, tunaomba kusiwe na bugudha wakati huu mgumu. Tunatumai shabaha ya wote haitolenga katika kifo cha Robin bali katika muda wake wa furaha na vicheko alivyotoa kwa mamilioni ya watu”
  

Airtel yazindua huduma mpya ya mitindo kwa njia ya simu kwa kushirikiana na Mbunifu Mahiri Afrika Mustafa hassanali.

$
0
0
 Mbunifu nguli wa mitindo Afrika, Mustafa Hassanali akizungumza na wageni waalikwa kuhusiana na huduma mpya ya kuwa karibu naye kwa mashabiki wa mitindo kupata taarifa zake kupitia simu zao za  mkononi za Airtel  kwa kupiga *148*82# na moja kwa moja utakuwa umeunganishwa na huduma hiyo na kutozwa shilingi 90 za kitanzania kwa siku.
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, imeshirikiana na mbunifu wa mitindo Afrika ,Mustafa Hasanali katika kusheherekea miaka 15 ya mafanikio yake makubwa katika sekta ya mitindo.
 Mustafa Hassanali amefanya maonyesho katika miji 27 katika nchi 18, na kugusa maisha ya watu mbali mbali  kwa njia tofauti. Na anaendelea kuwa maarufu katika sekta ya mitindo nchini na Afrika kwa ujumla.
Ushirikiano huo kati ya Airtel na Guru wa mitindo  Tanzania na nje ya Tanzania, utawezesha wateja wa Airtel na washabiki wa mitindo kuwa karibu  zaidi na ulimwengu wa mitindo kwa kupata habari mbali mbali na za kisasa kupitia simu zao za mikononi.
Akiongea kuhusu muungano huo Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Tanzania Adriana Lyamba, alisema “mitindo ni moja kati ya vipengele muhimu katika maisha yetu, zikiwemo nguo, vifaa na vyombo mbalimbali. 
Kila mtu anataka kupendeza na kujihusisha na mitindo ya kisasa. Ila , hivi sasa upatikanaji wa habari na huduma za mitindo ni mgumu sana. Hivyo Airtel tumekuwa wa kwanza katika kuwapatia wananchi huduma hii kupitia simu zao za mkononi itakayowasaidia kupata habari mbali mbali za mitindo kwa ujumla . Huduma hii inajulikana kwa jina la “Airtel Fasheni”. 
Tunaamini kuwa , huduma hii itawasaidia wateja wetu wote ambao wangependa kupata habari mbali mbali na kuwafikia wabunifu wa mitindo ili kupata ushauri na pia kununua bidhaa zao.”
Mustafa Hassanali, mbunifu mitindo mahiri Afrika alisema , “ Airtel fasheni ni huduma ya kipekee ambayo wateja wa Airtel wanaweza kuipata mahali popote na wakatii wowote kwa kupiga *148*82#. Huduma hii ni Tsh.90 kwa siku.”

mwanamuziki nyota wa nyimbo za injili wa congo Natalie Makoma atembelea BBC London

$
0
0
Mzee wa Macharanga Charles Hilary akiwa na Natalie Makoma, mwanamuziki wa nyimbo za Injili kutoka Congo alipotembelea  studio za BBC jijini London. Mwanamuziki huyu ni maarufu kwa nyimbo kibao zikiwemo 'Butu na Moyi', 'Moto Oyo, na 'Nzambe na Bomoyi' ulio katika mahadhi ya reggae. Hebu msikilize hapo chini

Hoja ya haja: DIASPORA NA URAI PACHA (dual citizenship)

$
0
0


Na Ndugu Kagutta N.Maulidi





Tunapoendelea kufuatilia majadiliano  ya wajumbe maaluum wa bunge la katiba si vibaya tukaweka msisitizo au kuwakumbusha wajumbe wetu kuhusu mada iliyopo katika rasimu ya katiba sura ya tano inayozungumzia  urai pacha.

Nchi yetu bado haitambui uraia wa nchi mbili, kwa maana kuwa ukichukua uraia wa nchi nyingine unapoteza haki ya Urai wako  wa Tanzania.
 
Tunashukuru kuwa swala hili limeingizwa katika rasimu ya pili ya katiba,ili liweze kujadiliwa .Sisi Watanzania tunaoishi nje ya nchi   ni matumaini yetu kuwa wajumbe wa bunge maalumu wataliangalia swala hili kwa mapana zaidi na kulikubali kwa faida ya watanzania na nchi yetu kwa jumla.

Wengi wa watanzania wanaoishi nje(Diaspora) wamelazimika  kuomba uraia wa nchi wanazoishi ili kupata haki zao baada ya kuishi na kufanya kazi kati katika nchi hizo kwa muda mrefu. 

Vodacom yapiga jeki wiki ya usalama barabarani

$
0
0
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo imetoa msaada wa shilingi milioni 40 kwa serikali ya Jamhuri ya Tanzania kwa kupitia Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani katika kufanikisha wiki ya usalama barabarani mwaka huu itakayozinduliwa rasmi siku chache zijazo mkoani Arusha. 
 Hafla ya kukabidhi hundi ya fedha hizo imefanyika leo katika wizara ya Mambo ya Ndani ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi,Mheshimiwa Mathias Chikawe,alikuwa mgeni rasmi pia alikuwepo Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu na Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamanda Mohamed Mpinga. 
 Akiongea wakati wa halfa hiyo mgeni rasmi, Waziri wa mambo ya ndani, Mheshimiwa Chikawe,alisema” Nachukua fursa hii kuwashukuru wadhamini wa kampeni ya usalama barabarani kwa mwaka huu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa kutoa mchango wao na kushirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani kufikia malengo kwa kuhakikisha usalama wa raia na kupunguza ajali za barabarani . 
Alisema ajali za barabarani zinaongezeka kwa kasi na kusababisha upotezaji wa nguvu kazi huku zikiacha maafa makubwa kwa taifa, ni jukumu la kila Mtanzania kuwa sehemu ya kusimamia na kuzingatia sheria za barabarani na kuyataka makampuni mengine kuunga mkono jitihada hizi za kupunguza ajali nchini. 
 Akiongea  Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano,Georgia Mutagahywa alisema Vodacom Tanzania inajivunia kuwa sehemu ya juhudi za kuokoa maisha ya watanzania na mali zao na inayo dhamira ya kuhakikisha inashirikiana na wadau wote wenye wito wa kusaidia usalama barabarani”
 “Vodacom Tanzania tumeingia katika kampeni ya kupunguza ajali na madhumuni yetu makubwa ni kusaidia kufanikisha juhudi zinazofanywa na jeshi la polisi kusimamia na kupunguza matokeo ya ajali za barabarani, kila mwaka kunakuwa na matukio ya ajali za barabarani ambazo zingeweza kuepukika kama wahusika wangekuwa na elimu ya kutosha.Kama kampuni ya mawasiliano tutakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii athari za kuendesha gari wakati huo huo unaongea na simu ya mkononi”.Alisema Mutagahywa. Aliongeza kuwa Vodacom imekuwa mstari wa mbele kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii katika sekta ya elimu,afya,kupambana na umaskini na hivi sasa imejikita rasmi katika kampeni za kupunguza ajali nchini na siku zote itakuwa mstari wa mbele kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha inahamashisha na kutoa elimu itakayofanikisha kupunguza tatizo la ajali za barabarani
 Waziri wa Mambo ya ndani Mathias Chikawe,akipokea hundi yenye thamani ya shilingi Milion 40/=toka kwa Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Georgia Mutagahywa(kushoto) msaada huo umetolewa kwaajili ya maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani Mkuu wa jeshi la polisi nchini Ernest Mangu na kulia ni Mkuu wa usalama barabarani Mohamed Mpinga.
 Waziri wa Mambo ya ndani nchi Mathias Chikawe na Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Georgia Mutagahywa(kushoto)wakiwaonyesha waandishi wa habari(hawapo pichani)hundi yenye thamani ya shilingi Milion 40/=iliyotolewa msaada na Vodacom Tanzania kwaajili ya kufanikisha maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani yatakayofanyika hivi karibuni mkoani Arusha.
 Waziri wa Mambo ya ndani Mathias Chikawe,akisisitiza jambo kuhusiana na wiki ya usalama barabarani itakayofanyika hivi karibuni mkoani Arusha wakati wa alipokuwa akipokea msaada wa  hundi yenye thamani ya shilingi Milion 40/=toka kwa Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Georgia Mutagahywa(kushoto)kwaajili ya maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani,kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mbarak Abdulwakili.
.Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa(kushoto)   sakiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi msaada wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 40/= kwaajili ya maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani itakayofanyika hivi karibuni jijini Arusha.Katikati ni Waziri wa Mambo ya ndani Mathias Chikawe na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mbarak Abdulwakili.

KAMPUNI YA SEED CO KUZAWADIA WANAFUNZI MADAWATI 100 YENYE THAMANI YA MIL 15 KATIKA SHINDANO LA MASHAMBA DARASA MIKOA YA KANDA YA ZIWA.

$
0
0
Kampuni ya Seed Co Tz Ltd imezindua rasmi shindano la mashamba darasa kwa shule za Msingi Tanzania ambapo shule itakayokuwa imelima shamba zuri kwa kuzingatia misingi yote ya kilimo bora cha kisasa itajishindia zawadi kubwa ya madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 15 za Kitanzania. 
Tunaposema kulima kwa kuzingatia misingi ya kilimo bora cha kisasa ni pamoja na matumizi ya mbegu bora, mbolea za kupandia na kukuzia na uhifadhi bora wa mazao baada ya kuvuna. Shindano hili ni mahsusi kwa shule za msingi zilizopo katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, ambayo ni Kagera, Kigoma, Tabora, Geita, Shinyanga, Simiyu, Mwanza na Mara. 
 Hii ni baada ya kugundua kuwa ukiachia mbali juhudi za serikali katika kukifanya kilimo kuwa uti wa mgongo wa uchumi wa nchi yetu, changamoto kubwa bado imebaki kuwa katika elimu ya somo hili. 
Na ndio maana kampuni ya Seed Co ikaona kuwa kama tunataka kufikia malengo haya basi juhudi kubwa inatakiwa iwe katika kufundisha Watanzania kilimo kwa njia ya vitendo kwa kuanza kufundisha wanafunzi wa shule za msingi na kuwapa motisha ya kujishindia zawadi kemkem kutoka Seed Co. 
 Ukiachia mbali zawadi kuu ya madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 15 za Kitanzania, zawadi nyingine zitakuwa ni sare za michezo, vibao vya kuandikia, madaftari na kalamu za kuandikia. Bila kusahau kuwa mwalimu wa somo la kilimo ambaye ataifanya shule yake ishinde atazawadiwa pia simu ya kisasa ya mkononi. 
 Ili kushiriki, wanafunzi au walimu wanatakiwa kutembelea maduka ya mawakala waliothibitishwa wanaouza mbegu za Seed Co au kununua gazeti la Nipashe toleo la kesho tarehe 13 Agosti 2014 ambapo watajipatia nakala yenye tangazo au fomu ya kujiunga na shindano hili. Kumbuka mwisho wa kujisajili kwa shindano hili ni tarehe 30 mwezi Agosti 2014. 
 Katika uandaaji na usimamizi wa mashamba darasa haya, kampuni ya Seed Co itatoa pembejeo zote zinazohitajika, ikiwa ni mbegu za mahindi, mbolea ya kupandia na kukuzia na pia madawa ya kupulizia iwapo mazao yataonyesha dalili za kushambuliwa na wadudu waharibifu. Kumbuka ya kwamba kampeni hii ya Mashindano ya Mashamba Darasa imelenga kufundisha Kilimo kwa njia ya vitendo kwa wanafunzi wa Shule za Msingi, huku ikitoa nafasi kwa wanafunzi kujishindia zawadi mbali mbali kutoka Seed Co. Zawadi kuu ni kushinda Madawati 100 yenye thamani ya shilingi Milioni 15 za Kitanzania.
Hii ni motisha kubwa kwa wanafunzi kupenda shughuli za kilimo tangu wakiwa shuleni. Kuhusu Seed Co Seed Co Limited ni kampuni inayoongoza barani Afrika kwa kukuza, kuzalisha, kubangua na kusambaza mbegu bora katika masoko ya nchi 15 barani Afrika. 
Bidhaa nyingi za mbegu zinazozalishwa na kampuni hii ni pamoja na mahindi, Pamba, Ngano, Soya, Mtama na mazao mengine ya nafaka ndogondogo.
 Katika soko la Tanzania Seed Co imejikita zaidi katika uzalishaji wa mbegu chotara za mahindi na mtama. Kampuni hii kwa sasa ina viwanda vya kubangua mbegu Jijini Arusha na Mbeya. Jijini Mwanza kuna ghala kubwa la kuhifadhia mbegu ikiwa ni mkakati wa kumfikishia mkulima bidhaa hizi karibu naye.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Mbegu ya Seed Co ya jijini Arusha,Frank Wenga(kulia)akisisitiza jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari leo,kushoto ni Meneja Mauzo,Daniel Mwambugi.
Meneja Mauzo wa  Kampuni ya Mbegu ya Seed Co ya jijini Arusha,Daniel Mwambugi(kushoto) na Meneja Masoko,Frank Wenga wakionesha Fomu maalumu itakayotumiwa na wanafunzi wa Kanda ya Ziwa kushiriki shindano hilo.

mkutano wa wadau wa maendeleo kutoka maeneo kame wafanyika leo mjini Singida

$
0
0
 Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bw. Liana Hassan akifungua mkutano wa kikanda wa wadau wa maendeleo kutoka maeneo kame kanda ya Singida.

snoop dogg aacha gumzo uingereza kwa kufikia hoteli ya kawaida ya bei poa

$
0
0
Na Sultani Kipingo
Anajulikana kwa kutumbua maraha na kuishi kifahari, lakini rapa milionea Snoop Dogg ameacha gumzo huko Uingereza kwa kukaa katika hoteli ya bei ya chini ya Holiday Inn Express wakati wa onesho lake katika kitongoji cha Devon, Exeter, wikiendi ilopita 
 Msanii huyu wa Marekani, ambaye alilipwa pauni za Uingereza 22,000 (sawa na 60,236,000/- za madafu) kwa onesho hilo la masa mawwili katiika ukumbi wa klabu ndogo ya usiku ya Timepiece, alikaa kwenye hoteli hiyo kwa bei ya pauni 70 (sawa na 191,660/- za madafyu) kwa usiku mmoja.
 Meneja wa hoteli hiyo, Debbie Hamnett, alisema Snoop na bendi yake walifanya booking toka July ila hakuna aliyejua ni yeye na kundi lake  hadi walipofika na kuingia vyumbani. 
Yeye na mwenye klabu kulikofanyika onesho hilo hadi sasa hawaamini kwamba alikuwa ni yeye. Inasemekana Snoop Dogg alikuwa amepata tenda zinazolipa maradufu kufanya maonesho sehemu zingine ila akachagua hapo Exeter ambako mmiliki wa klabu ya Timepiece George Sloane alisikika akisema “Walipokubali kuja kufanya onesho nilidhani aidha anatania ama ametucahngaya sisi na klabu ingine ya usiku.  Lakini Snoop Dogg na timu yake walikuwa wameshafanya utafiti kuhusu klabu hiyo na kugundua kuwa awali lilikuwa kanisa kuukuu, na baada ya kuona picha zake, walijua ni klabu ndogo ya usiku na kuamua kufanya onesho lisilokuwa na watu wa vurugu”
Rapa Snoop Dogg akiwa katika onesho katika kumbi wa klabu ndogo ya usiku ya Timepiece, Exter Uingereza
Hoteli aliyofikia Snoop Dogg na kuacha gumzo
Snoop Dogg akipata taswira na wafanyakazi wa hoteli hiyo
Chumba alicholala Snoop Dogg kwa bei ya takriban shilingi laki mbili kwa siku. Kutokana na utajiri alionao na dau la zaidi ya shilingi milioni 60 alizolipwa kwa onesho lake, gumzo limeachwa huko Exeter

MAGUFULI AKAGUA MIZANI YA KISASA YA VIGWAZA MKOANI PWANI PAMOJA NA UJENZI WA BARABARA YA KIBAMBA-KWEMBE-MAKONDEKO (17KM) ITAKAYOPITA KATIKA CHUO KIKUU CHA MUHIMBILI, MLOGANZILA, KIBAMBA

$
0
0
 Mhandisi kutoka Wakala wa Barabara Nchini TANROADS Ndugu Kileo akimuonesha Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli jinsi Mzani mpya wa Vigwaza utakavokuwa ukipima magari wakati yakitembea tofauti na mizani mingine nchini.
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kazi ya ujenzi  inayofanyika katika Chuo Kikuu cha Muhimbili kilichopo katika eneo la Mloganzila Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Dkt. Magufuli alipita hapo mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Kiwango cha Lami kutoka Kibamba kwenda Kwembe hadi Makondeko yenye urefu wa Kilometa 17 nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na baadhi ya Wakanadarasi wakati wa ziara yake yakutembelea na kukagua ujenzi wa   barabara ya Kiwango cha Lami kutoka Kibamba kwenda Kwembe hadi Makondeko yenye urefu wa Kilometa 17 nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA



introducing Pilot Boy-Friends Corner (Mixtape.Noiz)

mambo ya gado

$
0
0

Our Security Forces Vs Al Shabaab and the 72 Virgins!

NAJUA WAJUA YA CAPTAIN GARDINER G. HABASH NDANI YA MICHUZI TV LEO

MFANYAKAZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI(MUWSA)AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI

$
0
0
Pikipiki aina ya Suzuki ikiwa imenasa mbele ya Lori baada ya kugongana uso kwa uso .
Baada ya ajali hiyo pikipiki ilibaki ikiwa imesimama baada ya kunasa chini ya Lori la mafuta.
Askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiwa katika eneo la tukio kwa ajili ya kufanya vipimo.
Na Dixon Busagaga wa Globu
 ya Jamii kanda ya Kaskazini.


Ajali mbaya imetokea barabara kuu ya Arusha Moshi ikihusisha Lori aina ya Sacania lenye namba za Usajili T 137 ATA na pikipiki aina ya Suzuki yenye namba SU 40262 mali ya Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA).



Mashuhuda wa ajali hiyo waliiamia Globu ya Jamii kuwa ilitokea majira ya saa 7 katika makutano ya barabara ya Arusha/Moshi na ile itokayo chuo cha polisi Moshi kuelekea ofisi za mkuu wa wilaya ya Moshi.



Katika ajali hiyo mwndesha pikipiki aliyefahamika kwa jina la George Lyamuya, mfanyakazi wa Mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi, alifariki dunia papo hapo.

PUB BUSINESS FOR SALE @ KINONDONI MANYANYA

$
0
0
PUB BUSINESS FOR SALE @ KINONDONI MANYANYA: PRICE TSHS. Mil.45
Best located at the Busy-Business-Hub ‘Kinondoni’ along Kawawa (former Morocco) road, near NBC Bank Kinondoni Branch, Puma (the former famous ‘Mwanamboka’) Filling Station and Casablanca Bar; the Lounge is uniquely designed, walls well decorated with modern ‘crazy colours’.  

Night Club lighting is well done to suite today’s market. It is fully air-conditioned, very well furnished with modern and durable local made furniture which will last many years to come. 

The indoor lounge is fully tiled; the counter is fitted with marble top, plus beautiful paintings on the walls. Three (3) 40’ (inch) flat plasma TV sets fitted on different walls of the indoor lounge. Indoor lounge also has an almost brand new Fully-Equipped-DJ-Music-System in its own DJ room, while the outdoor bar has its own music system. There is a small outdoor counter and a big kitchen fully tiled.

The business is on-going with a good customer base with good sales 7 days a week. The place is rented for Tshs. 550,000/= per month, now already paid up to 31st December, 2014. Existing contract is valid until 2017, renewable.

Contacts:
Phone: 0788 893364
Email: tinogobba2002@yahoo.com

TAMASHA LA MTWARA FESTIVAL 2014 LASOGEZWA MBELE

Mahojiano ya Kwanza Production na Jhiko Manyika a.k.a JhikoMan

$
0
0
JhikoMan akitumbuiza kwenye Tamasha la Majahazi 2013
Karibu katika mahojiano kati ya Kwanza Production na Jhiko Manyika a.k.a JhikoMan aliyejiunga nasi moja kwa moja kutoka Helsinki Finland mwishoni mwa mwezi Julai.

Amezungumza mengi kuhusu ziara yake ya Ulaya iliyoanza mwezi wa nne, maonyesho aliyofanya, kazi alizorekodi na pia watu aliowashirikisha kwenye albamu yake mpya ijayo.

Amezungumzia IMANI ya RASTA na pia MUZIKI WA TANZANIA kwa ujumla
Ameongea mengi mema
KARIBU UJIUNGE NASI

Tamasha la Magari Tanzania (Autofest) limerudi na Matoleo Mapya ya Magari

$
0
0
Likirudi kwa mwaka wake wa saba, tamasha la magari Tanzania (autofest) litakua likionyesha magari mapya, matoleo mapya ya pikipiki, burudani za muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali wa nchini na burudani nyingine za kusisimua kwa ajili ya familia nzima kuanzia Septemba 19-21, 2014. Tamasha la mwaka huu ambalo linaandaliwa na Vision Investment, litafanyika katika viwanja vya Biafra, Kinondoni. Anayetarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi ni Mhe. Dk Abdallah O. Kigoda, Waziri wa viwanda na Biashara.

‘’Tukio hili linahusisha moja ya maonyesho muhimu sana na yenye mvuto katika ulimwengu wa vyombo vya moto”. Alisema Ally Nchahaga, Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Investments. “Lengo letu ni kuendelea kuleta aina mbalimbali ya bidhaa ya vyombo vya moto na huduma kwenye ‘Autofest’ ili wadau wapate kufurahia na kuridhishwa navyo.” alisema.
Tukio hili la mwisho wa wiki linategemea kuvutia zaidi ya watu nusu milioni, na kulifanya kuwa tamasha kubwa na maarufu la magari Tanzania. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008, Autofest sasa imekua ni Tamasha muhimu katika ulimwengu wa vyombo vya moto, likiwa ni onyesho pekee linalowaleta wapenzi wa magari pamoja. Ni onyesho kubwa linaloonesha magari ya abiria, magari ya biashara, pikipiki, bodi za magari, sehemu za magari, mashine na zana zinazohusiana na magari.

Burudani kwenye tukio zitahusisha, ‘Bumper to Bumper Auto Style Zone’ ambayo ni nafasi kwa wapenzi wa magari kuonyesha walivyoyapamba magari yao, ‘Kids Car Zone,’ ambayo itawaburudisha watoto wa umri kati ya miaka mitano na 14 kwa program za magari na elimu muhimu ya magari na usalama barabarani, na kuweza kuburudika na mbinu mbalimbali za kuchezesha magari kama kubadilisha gia, “Mwaka huu tunatarajia kwamba matokeo yatakua makubwa zaidi ukilinganisha na mwaka uliopita kutokana na kuongezeka kwa matangazo na mahusiano ya umma,” alisema Nchahaga. “Autofest itapelekea kutambulika kwa wadhamini wetu na program.” alisema.

Tamasha la Autofest linatoa nafasi za udhamini na maonesho. Kampuni ya Vision Investment inakaribisha wadhamini na watu wanaotaka kushiriki katika maonyesho ya mwaka huu kwa kujaza fomu ya maombi iliyopo katika mtandao wa www.autofest.co.tz. Fulana za Autofest sasa zinapatikana kwa mauzo, na mapato yatayopatikana yatatumika katika kuendeleza program za Autofest.

TBL YAKAGUA UJENZI WA KISIMA CHA MAJI CHA ZAHANATI YA MAKUBURI KILICHOJENGWA KWA MSAADA WAO

$
0
0
 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kushoto), na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwongozo, James Ngoitanile (wa tatu kushoto) wakiangalia kisima kipya cha maji kikisafishwa katika Zahanati ya Makuburi Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kiwanda hicho Kimejengwa kwa msaada wa TBL kwa gharama ya sh. mil. 25.
 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kushoto), na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwongozo, James Ngoitanile (kulia) wakipata maelezo kutoka kwa Fundi Mkuu wa Kampuni ya Drima Drilling  & Civil Works, Rashid Abdallah walipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa kisima
cha maji kikisafishwa katikaZahanati ya Makuburi, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kiwanda hicho Kimejengwa kwa msaada wa TBL kwa gharama ya sh. mil. 25..
  Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kushoto), na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwongozo, James Ngoitanile (wa tatu kushoto) wakiangalia kisima kipya cha maji kikisafishwa katika Zahanati ya Makuburi Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kiwanda hicho Kimejengwa kwa msaada wa TBL kwa gharama ya sh. mil. 25.

TFF HAITAMBUI MABADILIKO YA UONGOZI COASTAL UNION

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) halitambui mabadiliko ya uongozi ndani ya Coastal Union yanayodaiwa kufanywa na mkutano wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyika hivi karibuni.

Uongozi wa Coastal Union uliochaguliwa na mkutano wa uchaguzi wa klabu hiyo ndiyo ambao tunautambua, na tutaendelea kufanya nao kazi, na sio uongozi mwingine wowote ule.

Tunapenda kuwakumbusha wanachama wetu (ikiwemo Coastal Union) kuheshimu katiba ya TFF pamoja na katiba zao, kwani hazitambui mapinduzi ya uongozi wala kamati za muda za utendaji. TFF inafanya kazi za kamati za utendaji zilizopatikana kwa njia ya uchaguzi tu.

Tayari tumepokea barua kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mnguto ikilalamikia kusimamishwa kwake.

Hivyo, tunafuatilia suala hilo kwa kina, na ikibainika kuwa kuna viongozi wamehusika katika mapinduzi hayo watafikishwa katika vyombo husika kwa hatua zaidi.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live


Latest Images