Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 532 | 533 | (Page 534) | 535 | 536 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Soko la Hisa Dar es Salaam (Dar es Salaam Stock Exchange), kwa udhamini wa benki ya NMB, Selcom na FSDT, linapenda kuwajulisha wanafunzi wa elimu ya juu nchini walioshiriki katika shindano la elimu ya uwekezaji kwa mwaka 2014 (DSE Scholar Investment Challenge 2014) kuwa maandalizi yote ya kuhitimisha shindano hili kwa sasa yamekamilika.


  Mchakato wa kutambua nafasi ya kila mshiriki wa shindano umemalizika. Majina ya wanafunzi 50 wanaoongoza katika shindano hilo yamebandikwa katika mtandao wa DSE (www.dse.co.tz) kwenye kipengele cha Investment Challenge.


  Sherehe za kuwatambua washindi na kuwapatia vyeti na zawadi zitafanyika tarehe 13 August 2014 jijini Dar es Salaam. Mialiko ya kuhudhuria sherehe hizo inaendelea kutumwa kwa njia ya simu.
   (sehemu ya umati wa wanafunzi walioshiriki katika elimu ya uwekezaji kwenye hisa na masoko ya mitaji nchini iliyoendeshwa na DSE kwa wanazuoni).

  Shindano la elimu ya uwekezaji kwa wanazuoni (DSE Scholar Investment Challenge) lilianza tarehe 01/04/2014 na kumalizika tarehe 30/06/2014. Wanafunzi washiriki walipewa nafasi ya kutumia simu zao za mkononi ili kununua na kuuza hisa zinazouzwa katika soko la hisa (DSE) la Dar es Salaam. Kila mshiriki alipewa mtaji (virtual capital) wa shilingi milioni moja. Ushiriki kwa shindano hili ulikuwa ni bure na huru kwa yeyote aliyependa.


  Nia kubwa ya shindano hili ni kuwapatia vijana walio katika vyuo vya elimu ya juu nchini fursa ya kuwekeza katika soko la hisa kwa majaribio na kuangalia mitaji yao ikikua. Elimu hii pia ni muhimu katika kujenga utamaduni wa utunzaji fedha na uwekezaji miongoni mwa vijana walio vyuoni (ambao ni viongozi, wawekezaji, wahasibu, wachumi, na washauri watarajiwa).


  Washiriki walitegemewa kushindana kukuza mitaji waliyopewa kwa kipindi cha miezi mitatu. Mafanikio ya shindano na elimu hii ni makubwa sana. Mwanafunzi anayeongoza amekuza mtaji wake kutoka shilingi milioni moja aliyopewa na kufikisha shilingi milioni nne (kwa kipindi cha miezi mitatu tu).

  DSE inawapongeza zaidi ya wanafunzi 5,000 walioshiriki katika shindano na elimu hii muhimu kwao na taifa kwa ujumla.  Shindano na elimu hii imepangwa kufanyika tena mwakani na kuwahusisha wanafunzi wengi zaidi ya elfu tano walioshiriki mwaka huu. DSE imepanga kuwawezesha wanafunzi na vijana nchini kutumia simu pamoja na intaneti mwakani ili kuwapa uwanja mpana zaidi wa kushiriki. Mipango ya baadaye ni kuwashirikisha wanafunzi walioko kwenye shule za sekondari pia.


  0 0

  Jana tarehe 10 Agosti 2014, Watanzania wanaoishi katika Muungano wa Visiwa vya Comoro waliamzisha rasmi Jumuiya yao. Lengo la kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ni kuwaunganisha wanachama wake, kuwawezesha kushirikiana katika kutambua fursa za maendeleo na kutoa mchango kwa taifa lao la Tanzania. 
  Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikuta wa Ubalozi wa Tanzania, Moroni. Wakati akifungua mkutano huo, Mhe. Chabaka Kilumanga, Balozi wa Tanzania nchini Comoro aliwaeleza Watanzania hao kwamba Serikali ya Tanzania inathamini sana na kutambua mchango wa raia wanaioshi nje nchi. Kutokana na kutambua umuhimu wao Serikali imeanzisha Idara inayoshughulikia Watanzania wanaoishi Ughaibuni katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 
  Aidha, Kitengo kama hicho kimeanzishwa katika Ofisi ya Rais wa Zanzibar. Sambamba na hilo, Viongozi wote wamekuwa wakikutana na Watanzania wanaoishi Ughaibuni, kila wanapata fursa ya kufanya hivyo, wanapokuwa nje ya nchi. Mkuu wa Utawala wa Ubalozi, Nd. Ali Jabir Mwadini alitoa mada kuhusu misingi ya uanzishaji wa Jumuiya za Kiraia na kubainisha vipengele muhimu vinavyopasa kuzingatiwa husasan katika katiba ya Jumuiya. Mwisho, ulifanyika uchaguzi wa viongozi wa muda waliopewa jukuma la kuandaa katiba.
  Viongozi wapya wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Kilumanga. Mwenye kanzu kushotoni mwa Balozi, Bw. Salum Ali Abdallah (Mwenyekiti), wa kulia kutoka alipo Balozi ni Bw. Khalfan Salum Khalfan (Makamu Mwenyekiti) anayefuatia kulia ni Bibi Rukia Selemani (Katibu).
   Mhe. Balozi Kilumanga pamoja na watendaji wa Ubalozi wakifuatilia mkutano.
   Sehemu ya Watanzania wanaoishi Comoro wakifuatilia hotuba ya Mhe. Balozi Kilumanga.


  0 0
 • 08/10/14--23:12: in loving memory

 • Simon Raphael Towo 
  09/10/1938-11/08/1994 
  Today marks the 20th year since you departed us to be with The Lord.
  We have many reasons to thank the Almighty God for your life whilst on earth and everything you did for us. We are here today because of your determination ,hard work and sacrifice. 
  Your life was a blessing to many, your memory is a treasure and your presence continue to be felt today, you left behind a legacy spiritually and emotionally. You taught us to love and have liberal souls for others. 
  You are always in our hearts and deeply missed by your wife Cecilia sons Fred, Hillary and Erick, daughters Christine and Sarah, siblings, grandchildren and friends.
  Proverbs 13 vs 22. A good man leaves an inheritance to his children's children.

  0 0

  DSC_0308
  Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph akionyesha baadhi ya vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO. Kulia ni Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko.
  DSC_0313
  Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akikabidhi sehemu ya msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi kwa Mwanafunzi Evaline Gerald wa kidato cha pili shule ya sekondari ya wasichana MWEDO uliotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Afisa Miradi Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko (kulia) na kushoto ni Afisa Mradi wa Shirika la Wanawake wa Kimasai (MWEDO) liliojenga shule hiyo, Martha Sengeruan.
  DSC_0315
  Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, Walimu na Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO.
  DSC_0332  DSC_0356
  Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya MWEDO wakishusha maboksi yaliyosheheni vitabu vya masomo ya sanyansi vilivyotolewa na Shirika la Read International kupitia UNESCO.
  PICHA ZAIDII BOFYA HAPA

  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Abrahman Kinana wakati akiwasili katika ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Mitaala kwa Vyuo vya Kiislam lililozinduliwa juzi Agosti 09, 2014 katika chuo Kikuu cha Kiislam Morogoro. Katikati ni Ramadhan Dau Mkurugenzi wa NSSF
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake  wakati akiwasili wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Mitaala kwa Vyuo vya Kiislam lililozinduliwa juzi Agosti 09, 2014 katika chuo Kikuu cha Kiislam Morogoro. Katikati ni Ramadhan Dau Mkurugenzi wa NSSF.
    Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais, wakati akiwahutubia kwenye ufunguzi.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti matunda aina ya Shokishoki, kwa kumbukumbu baada ya kufungua rasmi  Kongamano la Kimataifa kuhusu Mitaala kwa Vyuo vya Kiislam lililozinduliwa juzi Agosti 09, 2014 katika chuo Kikuu cha Kiislam Morogoro. Katikati ni Ramadhan Dau Mkurugenzi wa NSSF
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Professa wa Chuo cha Sokoine, Ally Aboud, kuhusu ufugaji wa njia raihisi na gharama nafuu wa Samaki baada ya kufungua rasmi Kongamano la Kimataifa kuhusu Mitaala kwa Vyuo vya Kiislam lililozinduliwa juzi Agosti 09, 2014 katika chuo Kikuu cha Kiislam Morogoro. Katikati ni Ramadhan Dau Mkurugenzi wa NSSF. Picha na OMR.
  Picha ya pamoja.

  0 0

  Makamu mwenyekiti wa klabu ya Gofu ya Moshi ,Chris Martin akimuonesha uwanja utakaotumika kwa mashindano hayo Meneja Mauzo wa kampuni ya Megatrade Investment Ltd kanda ya kaskazini ,Edmund Rutaraka. Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akiongoza Kikao cha Mazungumzo ya Awali na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio(hayupo pichani) kuhusu Uwekezaji katika maeneo ya Jeshi la Magereza Mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio akifanya mazungumzo ya Awali na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja(hayupo pichani) kuhusu Uwekezaji katika maeneo ya Jeshi la Magereza Mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara leo Agosti 11, 2014 Jijini Dar es Salaam.
   Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia mazungumzo ya Awali na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw William Erio(hayupo pichani) kuhusu Uwekezaji katika maeneo ya Jeshi la Magereza Mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(katikati) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga(Kushoto) ni Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Magereza, Solomon Urio akifuatilia kwa makini mazungumzo hayo.
   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja(kushoto) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio eneo linalofaa Uwekezaji wa Hoteli kubwa ya Kimataifa lililopo Ukonga, Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa PPF amefanya mazungumzo ya Awali na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza kuhusu Uwekezaji katika maeneo ya Jeshi la Magereza leo Agosti 11, 2014 Jijini Dar es Salaam.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini John Casmir Minja akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio(kulia) mara tu baada ya kufanya mazungumzo ya Awali kuhusu Uwekezaji katika maeneo ya Jeshi la Magereza katika Mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara. Mkurugenzi Mkuu wa PPF amefanya mazungumzo hayo leo Agosti 11, 2014 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

  Nyota wa  muziki wa bongo fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platinum' akilitawala jukwaa pamoja na baadhi ya wacheza shoo wake katika onyesho la kwanza la tamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza lililofanyika mwishoni mwa wiki,tamasha hilo litaendelea kwenye miji mingine ya Bukoba na Kahama mwishoni mwa wiki.
   Baada ya kazi ya kuwaburudisha mashabiki wake,Mara Wema Sepetu a.k.a shemeji nae akajiunga kumpa sapoti mpenzi wake jukwaani.
  Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
   Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. 
    Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. PICHA NA MICHUZI JR-MWANZA


  0 0
 • 08/11/14--02:02: SIMBA YAMTIMUA KOCHA WAKE
 • Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana jioni wakati akitoa taarifa ya kumfuta kazi kocha aliyekuwa akiinoa timu hiyo,Zdravko Logarusic 'Loga' (hayupo pichani). Wengine pichani ni Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa Simba, Collin Frisch na Saidi Tully.
  Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Klabu ya Simba, Collin Frisch (kulia), akimsindikiza kwenda kupanda gari kocha wa timu hiyo Zdravko Logarusic 'Loga', wakati wakitoka katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana jioni, baada ya kutimuliwa kuifundisha timu hiyo. Kocha huyo alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja wa kuifundisha timu hiyo. 
  Kocha akiondoka huku akiwa aamini kilichomtokea.
  Gari namba T 853 BGS alilotumia kocha huyo wakati akiondoka katika hoteli hiyo baada ya kutimuliwa.

  0 0

  Wakati uchumi wa Tanzania ukiendelea kukua siku hadi siku, ongezeko la wananchi wenye kipato cha kati nalo limezidi kukua, na hivyo kuleta changamoto mpya katika masoko ya bidhaa mbalimbali hapa Waagizaji wa kinywaji Kutoka Uholanzi cha Bavaria eneo la Afrika ya Mashariki, Jovet (Tanzania) Limited wamedhamiria kuleta changamoto hiyo baada ya kuzindua kampeni rasmi ya mbio za kuelekea kileleni, na hivyo kuongeza wigo wake katika soko hili la Afrika ya Mashariki, ambalo limekua likikua kwa kasi kiuchumi.

  Akiongea katika chakula cha jioni na mawakala wakubwa wa kinywaji hicho katika eneo la Afrika ya Mashariki kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam, bwana John Kessy, Mkurugenzi mkuu wa Jovet (Tanzania) Limited, alisema, Kampeni hii ya Bavaria ya kuelekea kileleni imelenga kuleta changamoto kubwa katika eneo hili la Afrika ya mashariki, kwa kuwa litasaidia kutengeneza ajira zaidi, na kuongeza kipato binafsi na kwa serikali kwa ujumla.

  Bwana Kessy aliongeza na kusema kuwa, Tumeweza kupenya katika soko hili na kutengeneza mahusiano mazuri na wafanyabiashara. Tutaendelea kukua siku hadi siku tukiwapatia wateja wetu kilicho Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia hamsini ya wanywaji wa vinywaji vya shayiri wako eneo la Mashariki ya kati na Afrika na asilimia hii hutumia hektolita milioni 18 kwa mwaka, na hii imetokana na kwamba watu wengi wamekua wakijali zaidi afya zao, na hivyo Bavaria inataka kutumia fursa hii kujikita zaidi katika eneo hili, na kuwapa fursa walaji kupata uchaguzi zaidi.

  Mawakala hawa pia waliweza kupata fursa ya kujifunza mengi kuhusu kinywaji cha Bavaria, na pia mbinu za kufanya biashara katika siko hili ambalo limekua likikua kwa kasi na lenye ushindani mkubwa. Pamoja na kujifunza mengi kuhusu Bavaria na mbinu za kibiashara, mawakala hao pia waliweza kujishindia zawadi mbalimbali, zikiwemo seti za Televisheni, Simu za Mkononi na vinywaji mbalimbali vya familia ya Takwimu za hivi karibuni za mwaka 2010-2015 zinaonyesha kuwa soko la vinywaji linatarajiwa kukua na kuzalisha zaidi ya dola za kimarekani bilioni 1.9, na tafiti hii
  Mkurugenzi Mkuu wa Kovet (t) limited,Ndugu John Kessy akitafakari jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni yam bio za kuelekea juu na Bavaria zilizofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Jovet (t) Limited Ndugu John Kessy akimpongeza Bi. Christina wa K-Pub, kama mmoja wa mawakala bora wa kinywaji hicho.
  Mkurugenzi wa Jovet,Ndugu John Kessy akifurahi jambo na wakala kutoka Rwanda Ndugu Innocent Gasangwa.
  Baadhi mawakala wa Bavaria wakibadilishana mawazo wakati wa chakula cha jioni katika hoteli ya serana, Jijini Dar es salaam.

  0 0

  Dotto Mwaibale

  VIJANA nchini wametakiwa kuwa makini kwa kutumiwa na wanasiasa ili kuvuruga amani na usalama wa nchi uliodumu kwa muda mrefu.


  Mwito huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM), Khamis Juma Sadifa wakati wa hafla ya kuwasimika makamanda tisa wa umoja huo wa matawi katika Kata ya Kimanga jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


  "Ninyi vijana ndio walengwa wakubwa kutumiwa na wanasiasa kuvuruga amani na usalama wa nchi hivyo kuweni makini katika jambo hilo kwani tunachokihitaji ni amani na usalama wa nchi kwa watu wote na itikadi za vyama vyetu" alisema Sadifa


  Sadifa alisema hata nchi hii ikitokea kuongozwa na chama kingine lakini bila ya kuwa na amani ni kazi bure hivyo ni vema kila mmoja wetu akatambua kuwa hana budi kuilinda amani iliyopo na usalama wa nchi.


  Katika hatua nyingine Sadifa alitoa baraka zake kwa Kamanda wa Vijana wa CCM wa Kata ya Kimanga iliyopo Wilaya ya Ilala, Scollastica Kevela kuendelea na utendaji kazi wake wa kuinua uhai wa chama katika kata yake kwa kuwatembea vijana na wanachama ili kujua changamoto zinazo wakabili.


  "Nakuomba kamanda wangu Kevela endelea kufanya kazi yako ni kuimarisha chama katika matawi kwa kukukutana na vijana na si kukiuka sheria ya kuanza kufanya kampeni kama inavyodaiwa" Sadifa alitoa onyo.


  Sadifa aliongeza kuwa kazi kubwa ya ukamanda wa vijana ni kuwakutanisha vijana na kusikia changamoto walizonazo na kuziwakilisha ngaji ya juu kwa ajili ya kuzipatia ufumbuzi.


  Kwa upande wake Kevela alisema kazi ya kuwainua vijana kiuchumi ndio kipaumbele chake cha kwanza na atahakikisha anafanya hivyo kupitia vikoba ambako yeye ni Makamu wa Rais wa chama hicho nchini.


  Alisema amekuwa akifanya ziara katika matawi mbalimbali kwenye kata yake ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake ya kuimarisha chama hangamoto zinazowakabili vijana hao.  Katika hafla hiyo Sadifa alitoa vifaa vya michezo jezi na mipira kwa vilabu mbalimbali vya matawi katika kata hiyo ikiwa ni pamoja na fedha za ujenzi wa ofisi ya CCM katika eneo hilo ambapo zaidi ya sh. 500,000 zilipatikana.
  Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Khamis Juma Sadifa, akielekea meza kuu tayari kwa shughuli ya kusimika makamanda hao.
  Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kata ya Kimanga, Scollastica Kevela (katikati), akizungumza na wanachama wa CCM wakati wa hafla ya kusimikwa kwa makamanda tisa wa vijana wa matawi katika Kata ya Kimanga Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Khamis Juma Sadifa na Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Ilala, Alfred Tukiko.
  Makamanda tisa wa Matawi Kata ya Kimanga wakila kiapo baada ya kusimikwa.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  On Sunday 10Th August, will mark the 15 th Anniversary celebration of Tanzania renowned Pan African designer Mustafa Hassanali. An exclusive by invitation only niche event will be held, whereby Mustafa Hassanali will launch his Couture collection aptly named “Meremeta Na Hassanali”   “I can’t believe how time flies by so fast, what started as just a hobby has actually not only build my  brand but has also been a catalyst to the growth of the Fashion industry in Tanzania” stated the fashion guru, Mustafa Hassanali

  Mustafa has showcased in 27 cities in 18 counties globally, a major feat achieved by none in the fashion industry in Tanzania. His new collection will be showcased in Dar es salaam after a  hiatus of 5 years. This collection has been inspired by the true brand essence to what is a Mustafa Hassanali Signature style IQ. As they aptly put in Kiswahili “gauni usipomeremeta na Hauna Mkia, Haujavaa Hassanali” (translation- if your gowns doesn’t bling and doesn't have a trail then it isn't a Hassanali)
   
  “I would like to take this opportunity to thank all the media, clients, various sponsors, and international organizers for their tremendous support they have given me over the past 15 year and I shall hope to get your continued support over the forthcoming year. Last but not least, I want to thank Team at Mustafa Hassanali and friends and the almighty Allah for his continued Guidance, ameen “Concluded Hassanali

  “Meremeta na Hassanali “ collection will feature various top models and celebrities walking down the ramp choreographed and produced by one of South Africa's leading Show producers.


  0 0

  Waziri Tibaijuka akifunga majadiliano juu ya mradi huo.
  Waziri Tibaijuka akiwa ameshikana mikono na mbunge was Kigamboni Faustine Ndungulie na baadhi ya madiwani na viongozi wengine kuonyesha maridhiano namna mradi utakavyotekelezwa.
  Kaimu Mkurugenzi Msaidizi, Usanifu Miji na Uendelezaji Hellenic Mpetuta akitoa mada namna mji mpya utakavyopangiliwa katika mkutano huo uliofanyika Chuo Kikuu cha Kivukoni Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya wadau wakifuatilia mawasilisho ya mada mbalimbali juu ya mradi huo.
  Baadhi ya wadau wakifuatilia mawasilisho ya mada mbalimbali juu ya mradi huo.
  Wadau wakipata picha ya pamoja na waziri Tibaijuka (katikati) mara baada ya majadiliano juu ya mradi huo.Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com.

  0 0


  0 0

  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, BARAKAEL .N. MASAKI – ACP anawatangazia Wananchi wote ya kuwa orodha ya majina ya vijana waliomaliza Kidato cha Nne mwaka 2013 na cha Sita mwaka 2014 na kuchaguliwa kufanya usalii wa kujiunga na Jeshi la Polisi inapatikana kwenye tovuti ya Polisi: www.policeforce.go.tz au wafike ofisi ya kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya iliyopo Forest jirani na Mahakama kuangalia majina yao.

  Muhimu:

  • Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye kulingana na tarehe zinavyoonesha kwenye jedwali hapo juu ili mradi tu awe amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili. Jeshi la Polisi halitahusika na lawama yoyote ile kwa mtu atakayekwenda kwenye kituo cha usaili hali ambapo jina lake si miongoni mwa walioitwa kufanya usaili.

  • Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyake vyote vya masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s) ], nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.

  • Mwombaji awe na namba ya simu itakayotumika kumjulisha endapo atachaguliwa..

  • Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.

  Ni muhimu sana kwa kila mwombaji kuzingatia muda wa kuanza usaili.

  TAREHE YA USAILI KWA MKOA WA MBEYA NI 28.09.2014 HADI
  01.10.2014. SAA 08:00 ASUBUHI HADI 10:00 JIONI.

  0 0

  Mzee Yusuph (Kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa filamu yake ya Kwanza iitwayo NITADUMU NAE ambapo filamu hiyo imeingia sokoni leo Jumatatu na inasambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited, Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampun ya Proin Promotions Limited, Evans Stephen.
  Mzee Yusuph akibadilishana Mkataba na Mwanasheria wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Halima Mara baada ya Kumaliza kutiliana saini katika Mikataba.Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited
  Hatimaye Mzee Yusuph atambulisha rasmi ujio wake katika Tasnia ya Filamu leo mara baada ya kuitambulisha filamu yake mpya na ya Kwanza iitwayo NITADUMU NAE ambapo filamu hiyo ni moja ya filamu ambazo zimetoka katika nyimbo zake.

  Akiongea na Waandishi wa Habari Mzee Yusuph alisema "Filamu hii nimeitengeneza muda mrefu sana na imetoka katika nyimbo zangu lakini nilishindwa kuisambaza kutokana na kukosa Msambazaji ambaye anaweza kukubaliana na vigezo vyangu lakini Kwa bahati nzuri Proin Promotions imeweza kuwa na vigezo ambavyo mimi nimekubaliana navyo na nimeridhika navyo ndio maana nimeona wanaweza kusambaza filamu yangu" 

  Na Pia ameelezea sababu kubwa ya yeye kuamua kufanya kazi na Proin Promotions ni kwamba "Kampuni ya Proin Promotions hainunui hakimiliki za wasanii ndio maana nimeona nifanye nao kazi"
  Vilevile Filamu ya Mzee Yusuph ishaingia sokoni leo na inasambazwa na Kampuni mahiri ya Proin Promotions Limited ambapo filamu hiyo inapatikana Nchi nzima kuanzia leo.

  Mbali na hiyo pia Mzee Yusuph amesema kuwa sasa anabadili nyimbo zake kwenda kwenye filamu kwasababu nyimbo zake zote zina uwezo mkubwa wakuwa filamu ndio maana kwa kuanza ameanza na Nyimbo yake ya Nitadumu Nae.

  0 0


   Kina mama wakionyesha mfano wa kuwanyonyesha watoto wachanga katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo akizundua kitabu maalum cha Mwongozo wa Mafunzo ya Ulishaji wa watoto wachanga na wadogo katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa Juzi (kushoto) ni kaimu mkurugenzi wa mtendaji wa taasisi ya chakula na lishe tanzania Dk. Joyceline Kaganda na katibu tawala mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo akionyesha kitabu maalum cha Mwongozo wa Mafunzo ya Ulishaji wa watoto wachanga na wadogo mara baada ya kukizundua rasmi katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa Juzi (kushoto)ni katabu tawala mkoa wa Iringa na kulia nimwakilishi wa Unisef tanzania Paul Edwards.
   Baadhi ya wanafunzi wa uuguzi wakiwa katika maandamano wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa.
   mwakilishi wa shirika la kuhudumia watoto la umoja wa mataifa (UNICEF) nchini Tanzania  Paul Edwards akizungumza. (picha zote na Denis Mlowe).

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akizindua mradi wa maji kwenye kijiji cha Mbala kata ya Vigwaza.kushoto ni askofu mkuu wa Jimbo la Mashariki ya kanisa la Waadventista wasabato,Askofu Mark Malekana.

  Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akifungua maji kwenye bomba mara baada ya kuzindua mradi wa maji kwenye kijiji cha Mbala kata ya Vigwaza.
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizindua mradi wa maji kwenye Kijiji cha Mbala hapa anaonekana akifungua maji kwa ajili ya kunyweshea mifugo.
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akinamama wa jamii ya kimasai baada ya kuzindua mradi wa maji kwenye kijiji cha Mbala kata ya Vigwaza wilayani bagamoyo.

  Na John Gagarini, Bagamoyo

  IMEELEZWA kuwa maendeleo ya Tanzania yataletwa na Watanzania wenyewe na si kutegemea misaada mbalimbali toka kwa wafadhili wa kutoka nje ya nchi kama baadhi ya watu wanavyofikiri.

  Hayo yalisemwa jana kwenye Kijiji cha Mbala wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na askofu mkuu wa kanisa la waadventista wa Sabato Kanda ya Mashariki, Mark Malekana wakati wa uzinduzi wa mradi wa kisima cha maji kilichojengwa na wamuni wa kanisa hilo wa Manzese Jijini Dare s Salaam.

  Askofu Malekana alisema kuwa Watanzania wanapaswa kuhakikisha wanaanzisha miradi ya maendeleo kwa ustawi wananchi na si kutegemea kila kitu kutoka kwa wafadhili.

  “Ustawi wa nchi untegemea wananchi wenyewe kwani siyo kila jambo kuwategemea wafadhili hasa wale wan je lakini tukifanya wenyewe inaonyesha uzalendo na watu kuipenda nchi yao lazima tubadili mtazamo na kuanza kufadhili miradi sisi wenyewe,” alisema Askofu Malekana.

  Aidha alisema kuwa kanisa hilo mbali ya kutoa huduma za kiroho pia imekuwa ikitoa huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na miradi ya maji, elimu na afya ambapo kanisa hapa nchini linamiliki vituo vya afya 34, shule za msingi 11, sekondari 15 na Chuo Kikuu kimoja.

  Kwa upande wake mgeni rasmi katika uzinduzi wa kisima hicho cha maji pamoja na sehemu ya kunyweshea mifugo, Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete changamoto ya maji ni kubwa na ailikuwa ikisababisha migogoro.

  Ridhiwani alisema kuwa migogoro hiyo inatokana na pande mbili baina ya wafugaji na wakulima ambapo maji wanayokunywa watu yamekuwa yakinyweshewa mifugo hali ambayo inasababisha migogoro baina ya pande mbili hizo.

  “Tunawapongeza waumini hawa wa Manzese kwa kuona umuhimu wa kuchimba kisima hicho ambacho kitasaidia kukabiliana na changamoto hiyo ya upatikanaji wa maji kwenye Kijiji hicho na vijiji jirani,” alisema Ridhiwani.

  Alisema kuwa mbali ya changamoto hiyo pia wafugaji wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa majosho pamoja na madawa ya mifugo hali ambayo inasababisha vifo vya mifugo hiyo ambayo ni tegemeo kwa wafugaji katika kuendeshea maisha yao.

  Akisoma risala kuhusiana na mradi huo mkaguzi wa mali za kanisa hilo William Gomera alisema kuwa mradi huo mara utakapokamilika utasaidia kupunguza tatizo la maji kwenye eneo hilo la kijiji hicho na umegharimu kiasi cha shilingi milioni 76 na ulianza mwaka 2009. Mradi huo mbali ya kujengwa na waumini hao pia mradi wa maendeleo wa umoja wa mataifa (UNDP) hapa nchini, Taasisi ya Third Millenium Peace Initiative Foundation (TMPIF), Renewable Energy Development Company of Tanzania Ltd (REDCOT)

  0 0

  KUMEKUCHA! Miss Kinondoni anayemaliza muda wake, Lucy Tomeka, ametamba ni lazima mrembo wa Redd’s Miss Tanzania mwaka huu atoke Kinondoni.

  Lucy alisema ana uhakika huo mkubwa kutokana na kuwaona washiriki wa Redd’s Miss Kinondoni na kuona wana vigezo vyote vya kulitwaa taji hilo. Mrembo huyo ambaye atakabidhi taji la Redd’s Miss Kinondoni mwishoni mwa wiki alisema, ana uhakika huo kutokana na uzoefu alioupata wakati akishiriki Redd’s Miss Kinondoni.

  “Taji lazima lirudi nyumbani, warembo wa Kinondoni kusema kweli wana sifa zote, wana kila aina ya sifa. Tena mwaka huu naona upinzani ni mkali zaidi kuliko miaka yote, kutokana na sifa ya warembo hao,” alisema Lucy.

  Naye Mratibu wa Redd’s Miss Kinondoni, Husna Maulid, alisema warembo 20 wanatarajiwa kuchuana Ijumaa wiki hii ili kumpata mshindi kati yao. “Ijumaa fitina yote inaisha, kinachosubiriwa ni siku tu na warembo 20 wapo katika mazoezi makali kwa ajili ya shindano hilo.”

  Shindano la Redd’s Miss Kinondoni linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Escape 1 uliopo Mikocheni, Dar es Salaam huku kukiwa na burudani kali toka Malaika Band inayoongozwa na Christian Bella.  Taji la Redd’s Miss Kinondoni kwa sasa linashikiliwa na Lucy Tomeka, ambaye naye alivikwa na aliyekuwa Redd’s Miss Tanzania, Brigitte Alfred.

  Warembo wanaoshiriki shindano hilo wanatoka vitongoji vya Sinza, Msasani na Dar Indian Ocean, huku kiingilio kikitarajiwa kuwa Sh 10,000 kwa viti vya kawaida na Sh 30,000 viti maalumu.
  Wadhamini wa shindano hilo ni Redd’s Original, Kitwe General Traders, CXC Africa, Jambo Leo, Clouds FM, Michuzi Media Group, Father Kidevu, Greaters Salon, EFM na Mseto.

  0 0

  MABINGWA watetezi klabu ya mchezo wa Pool ya Top Land ya Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni jijini Dar es Salaam imemefanikiwa kutetea Ubingwa wake katika fainali za mashindano ya mchezo huo yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014” kwa kuwafunga timu ya klabu ya Meeda 13-5, yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mkoani humo na kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 800,000/ = pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni kwenye fainali za kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.

  Nafasi ya pili ilichukuliwa na Meeda Pool Klabu na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 400,000/= na nafasi ya tatu ni Jaba Pool Klabu ambao walijinyakulia fedha taslimu Shilingi 250,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na klabu ya JBS ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 100,000/=.

  Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume Salum Yusuf alifanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 400,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Kinondoni kwenye fainali za Taifa upande wa wanaume na nafasi ya pili ilichukuliwa na Mohamed Idd ambaye alizawadiwa Shilingi 250,000/=

  Mchezaji mmoja mmoja Wanawake, Grace Thomas alifanikiwa kutwaa ubingwa huo na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 300,000/ = pamoja na kuwakilisha mkoa katika fainali za kitaifa upande wa wanawake.Nafasi ya pili ilichukuliwa naCecilia Kileo ambaye alizawadiwa fedha taslimu Shilingi 200,000/=.

  Fainali za kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion” zinatarajiwa kufanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushilikisha Mikoa 17 ambayo ni Tabora,Shinyanga,Dodoma Mbeya,Iringa,Morogoro,Mwanza,Kagera,Manyara,Arusha,Tanga,Pwan i,Ilala,Lindi,Temeke,Kinondoni na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.

  Wachezaji wa timu ya Top Land wakishangilia kwa kucheza na kitita cha Shilingi 800,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa wa mashindano ya Safari Pool 2014 kwa Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga akimkabidhi Nahodha wa timu ya Top Land kitita cha fedha taslimu Shilingi 800,000/ = mara baada ya kuibuka mabingwa wa mashindano ya Safari Pool 2014 kwa Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

older | 1 | .... | 532 | 533 | (Page 534) | 535 | 536 | .... | 3278 | newer