Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

HAFLA FUPI YA KUMUAGA MSAIDIZI WA KATIBU MKUU KIONGOZI

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi balozi Ombeni Sefue(Kushoto) akimpa zawadi Bwana Francis Mwaipaja na mkewe wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika katika mgahawa wa Great Wall jijini Dar es Salaam jana.
Akiongea katika hafla hiyo Balozi Sefue alisema kwa Bwana Mwaipaja ni mtu wa kuaminika katika utendaji wake wa kazi na ni mtulivu na makini.Bwana Mwaipaja amehamishiwa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Bwana Mwaipaja aliyekuwa msaidizi wa Katibu mkuu kiongozi alimshukuru Balozi Sefue na kusema amejifunza mengi ikiwemo kuzingatia muda katika utendaji kazi,kutekeleza majukumu kwa ufasaha na ufuatiliaji mambo kwa karibu.(picha Freddy Maro)


RAIS KIKWETE AKIFUNGUA WARSHA MAALUMU KATIKA HOTEL YA WHITE SANDS

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua warsha maalumu itakayojadili mikakati ya kutekeleza  ili kufikia Dira  ya Maendeleo Tanzania 2025 katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo inaongozwa na Waziri Idris Jala Kutoka Malaysia aliyebobea katika masuala ya Uchumi na Maendeleo.
Baadhi ya Washiriki wanaohudhuria Warsha Maalum itakayojadili mikakati ya kutekeleza  ili kufikia Dira  ya Maendeleo Tanzania 2025 katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo inaongozwa na Waziri Idris Jala Kutoka Malaysia aliyebobea katika masuala ya Uchumi na Maendeleo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal(Watatu Kushoto),Waziri Mkuu Mizengo Pinda(wane kushoto) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(Wapili kulia) na,Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu.Wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya ufunguzi wa Warsha Maalumu itakayojadili mikakati ya kutekeleza ili kufanikiwa kufikia Dire ya Maendeleo Tanzania 2025 inayofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.Warsha hiyo inaongozwa na Waziri Idris Jala Kutoka Malaysia(wapili kushoto)(picha na Freddy Maro)

Mh. Joshua Nassari aendesha mafunzo kwa madereva wa bodaboda jimboni kwake

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mh. Joshua Nassari akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo maalum ya uendeshaji wa pikipiki kwa mmoja wa Waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda, muda mfupi baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo yaliyoongozwa na Mh. Nassari kwa kushirikiana na Makamanda wa Polisi Mkoani Arusha.Mafunzo hayo yanadhaminiwa na Mbunge huyo wa Arumeru Mashariki na hili ni kundi la kwanza linalounganisha vijana zaidi ya 105.
Mbunge wa Jimboni la Arumeru Mashariki,Mh. Joshua Nassari akizungumza na Vijana hao wa Bodaboda wakati alipokuwa akitoa mafunzo ya namna wanavyotakiwa kuwa katika uendeshaji wa vyombo hivyo.

Umoja wa Mataifa wasema Hali Ni Tete Na Ya Hatari Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo

$
0
0
Mwakilishi Maalum wa Katibu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,Bw. Rogers Meece akitoaa taarifa mbele ya Baraza Kuu la Usalama ambapo alionya kwamba hali ni tete na ya hatari nchini DRC kiasi cha kuwapo uwezekano mkubwa wa kuibuka machafuko wakati wowote. Akalitaka Baraza hilo kuridhia upelekeji wa Brigedi mpya ili pamoja na masuala mengine ikasaidie kuimarisha hali ya ulinzi na usalama. Aidha amelisihi pia Baraza Kuu kuridhia matumizi ya nguvu katika harakati hizo za kutatufa amani ya kudumu nchini DRC.

tbc na vita foam wakabidhi msaada wa magodoro wenye thamani ya sh.mil. 3 shule ya msingi uhuru mchanganyiko jijini dar

$
0
0

Shirika la Utangazaji nchini (TBC) pamoja na Kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) Limited,wamekabidhi msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya shilingi Milioni 3 kwa Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam. Msaada huo ni sehemu ya marejesho ya faida inayoipata kwa jamii (CSR). 

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Clement Mshana amesema Jamii inayo wajibu wa kusaidia makundi ya watoto wenye ulemavu nchini ili kuwapa faraja na wajione nao ni sehemu ya jamii.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana akikabidhi moja ya mashine inayotumiwa na watoto walemavu wa macho kuandikia kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mang'enya wakati TBC kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana akikabidhi sehemu ya magodoro 100 yenye thamani ya shilingi milioni 3 kwa Mratibu wa Elimu Kata ya Gerezani, Seraphina Mdamu kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi walemavu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko wakati shirika hilo kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) Limited walipokwenda kutoa msaada huo shuleni hapo, Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Shule .
 Mkutubi msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, joyce Nyamuhokwa (katikat) akimwelezea Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana kuhusu maktaba hiyo wakati shirika hilo kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Shule hiyo, Anna Mang'enya (wa pili kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Vitafoam, Justine Mwakalinga (wa tatu kushoto) na wafanyakazi wengine wa Vita Foam, TBC na walimu wa shule hiyo.
 Mkutubi msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Joyce Nyamuhokwa (kulia) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana (kushoto) moja ya kompyuta zinazotumiwa na wanafunzi walemavu kusomea wakati TBC kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam. 
Mkutubi msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Joyce Nyamuhokwa (kulia) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana sehemu ya vitabu vya Maktaba ya watoto hao walemavu wakati TBC kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Vitafoam, Justine Mwakalinga.hiyo, Anna Mang'enya na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Vitafoam, Justine Mwakalinga (wa pili kulia).

Article 7

WEZI WA NAZI ZANZIBAR WAMUUA MWENYE SHAMBA

$
0
0
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

Mzee mmoja mkazi wa eneo la Kitopeni mkoa wa Kaskazini Unguja Zanzibar Bw. Ali Khamis Ali (65), ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni na watu wasiojulikana.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Unguja, ACP Ahmada Khamis, alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa 8.00 mchana huko kwenye eneo la Kitope mashambani.

Alisema Marehemu Mzee Ali, alikuwa amekwenda shambani kwake kukagua mazao yake ikiwemo minazi.

Amesema alipofika shambani hapo aliwaona vijana waliokuwa wakiangua nazi na wengine wakiwa chini ya mnazi wakiziandaa ili kuondokanazo kwa maana ya kuziiba.

Kamanda Ahmada amesema baada ya Marehemu kuwabaini wezi hao, inaonekana kuwa alianza kupandana nao lakini walimzidi nguvu na kumchona na kitu hicho chenye ncha kali ambacho kinaaminika kuwa ni kisu.

Amesema eneo la tukio walikuta rungu na ala la kisu kinachoaminika kumuulia marehemu. Amesema eneo la tukio hilo pia kulikuwa na damu nyingi na lilikuwa limevurugwa kutokana na mapambano.

Kamanda alisema baadhi ya wananchi wameitambua rungu hiyo kuwa ilikuwa ya marehemu aliyokuwa akiitumia kwa kulindia mazao yake ambayo mara kwa mara yamekuwa yakiibwa na wezi.

Kamanda Ahmada amesema kuwa pamoja na marehemu huyo kuuawa lakini inaonekana pia mmoja wa wezi hao wa mazao naye amejeruhiwa katika mapambano hayo kwani kulionekana michirizi na matone ya damu ya mtu aliyeondoka eneo la tukio na kutokomea kusikojulikana. Amesema uchunguzi wa tukio hilo umeanza na amewataka wananchi kutoa taarifa Polisi endapo watawaona watu ama mtu mwenye majeraha ili akamatwe kwa kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo.

Hata hivyo Kamanda Ahmada alisema kuwa mauaji hayo ni ya kuwania mali na ametaka kutohusishwa na hisia za imani yoyote ama za kisiasa, kishirikina, wivu wa kimapenzi, kulipiza kisasi ama imani za kidini.

“Haya ni mauaji ya kawaida na hayana hisia zozote. Ni mauaji kama mauaji mengine yanayotokea katika maeneo mengine ya nchi yetu.” Alisema Kamanda Ahmada na kuwaonya wananchi kutoweka hisia tofauti na tukio lenyewe.

Amewaomba pia Waandishi wa Habari kutoweka maoni yao binafsi wanaporipoti taarifa za tukio hilo ili kuepuka kuwatia hofu wananchi.

Rais Kikwete awasili Jijini Addis Ababa leo

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 23, 2013 kuhudhuria utiwaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). PICHA NA IKULUU


Bodi ya TRL yazinduliwa leo jijini dar

$
0
0
Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe(katikati) akizundua rasmi Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) . Dkt. Mwakyembe amezindua Bodi hiyo leo jijini Dar es salaam ambapo ameitaka kuhakikisha inasaidia kuimarisha reli ili mizigo mingi inayokwenda ndani na nje ya nchi isafirishwe kwa njia ya reli ili kuokoa barabara. Picha na MAELEZO-Dar

Taarifa Kutoka TFF leo

Hon. Membe welcomes Oman's Foreign Minister to Tanzania

$
0
0

a
Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation, in talks with his counterpart H.E. Yousuf bin Alawi bin Abdullah, Minister Responsible for Foreign Affairs of the Sultanate of Oman. H.E. Abdullah had just arrived at the Julius Nyerere International Airport in Dar es Salaam, ready to attend the two-days Joint Permanent Commission of Cooperation between Tanzania and Oman.

The meeting is scheduled to start on February 24 to 25, 2013 at Hyatt Regency (Kilimanjaro) Hotel in Dar es Salaam.

Hon. Membe (right), H.E. Abdulla (center) and H.E. Yahya bin Moussa al Bakri, Ambassador of the Sultanate of Oman in the United Republic of Tanzania.

Hon. Bernard K. Membe (MP), exchanges views with Ambassador Simba Yahya (2nd right -standing), Director of the Department of Middle East in the Ministry of Foreign Affairs and H.E. Ali Ahmed Saleh (kneeling down), Ambassador of the United Republic of Tanzania in Oman.

H.E. Yahya bin Moussa al Bakri, Ambassador of Sultanate of Oman in the United Republic of Tanzania in discussion with H.E. Yousuf bin Alawi bin Abdullah, Minister Responsible for Foreign Affairs of the Sultanate of Oman.

Delegation from Oman, upon their arrival today at the Julius Nyerere International Airport in Dar es Salaam.
Hon. Membe welcomes again H.E. Abdullah to the United Republic of Tanzania, during their arrival at the Hyatt Regency (Kilimanjaro) Hotel in Dar es Salaam.
Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation in a discussion with Ambassador Simba Yahya (2nd left), Director of the Department of Middle East in the Ministry of Foreign Affairs. Others are H.E. Ali Ahmed Saleh (right), Ambassador of the United Republic of Tanzania in Oman and Mr. Togolani Mavura (2nd right), Private Assistant to Honorable Minister Membe. 
All photos by Tagie Daisy Mwakawago of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation. 

Washiriki wa warsha ya Sera ya Uhamiaji na Maendeleo

$
0
0
Picha ya pamoja ya wadau walioshiriki katika warsha  ya  Sera ya Uhamiaji na Maendeleo (Migration and Devepoment Policy)  iliyoandaliwa na African Diaspora Policy Centre ya The Netherlands kuanzia tarehe 18-21 Feb 2013 katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es salaam. Lengo la warsha hiyo ni kushirikisha wadau kutoka Wizara mbalimbali ili kutoa michango yao kuhusu uanzishwaji wa Sera hiyo mpya.

WADAU WA PSPF WAONESHWA NYUMBA ZA MKOPO ZILIZOPO BUYUNI CHANIKA

$
0
0


Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) umekamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 641 katika mikoa mitano ambazo zilianza kuuzwa tangu Novemba mwaka 2012. Mradi huo unalenga kutatua tatizo la makazi kwa wanachama wake na jamii kwa ujumla.

Mikoa iliyojengwa nyumba hizo na idadi ya nyumba katika mabano ni Dar es salaam – Buyuni (491), Morogoro – Lukobe (25), Shinyanga – Ibadakuli (50), Tabora – Usule (25) na Mkoa wa Mtwara – Mang’amba (50).

Aidha kwa Muji wa maelezo ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bwana Adam Mayingu amewaambia wanaadishi wa habari na viongozi mbalimbali waliotembelea eneo la mradi huo Mkoawa Dar es Salaam kuwa Shirika lake limejenga nyumba za aina nne ambazo ni za nyumba viwili, Vyumba vitatu, Nyumba za vyumba vitatu kimoja ikiwa ni Master na Nyumba ya vymba vine kimoja kikiwa ni Master.

Gharama ya ununuzu wa nyumba hizo ambazo zinauzwa kwa wanachama wa Mfuko huo ni kati ya Shilingi Milioni 64 hadi milioni 94 gharama zikijumlishwa na Kodi ya ongezeko la Thamani.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam Mayingu (katikati) akiwaonesha maofisa wa Jeshi la Polisi moja ya nyumba 491 zilizopo katika mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ambazo zitkopeshwa kwa wanachgama wa mfuko huo. Nyumba hizo zipo katika eneo la Kigezi Kata ya Majohe wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Adam Mayingu (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa ziara hiyo ya kuakagua makazi hayo. Kulia ni  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Hery Mohamed Kessy Nyumba hizo zipo katika eneo la Kigezi Kata ya Majohe wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
 Wadau mbalimbali wakitembelea nyumba hizo hii leo.
 Ziara ikiendelea katika nyumba hizo zipatazo 491

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza atembelea mkoa wa Pwani

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza akitoa maelekezo ya kazi kwa (kutoka kushoto) Mkuu wa Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa, Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazji Hassan Saleh, Mkuu wa Idara ya Uhandisi - Ubora wa Huduma Nguvu Kamando na Meneja wa Vodacom Pwani Asajile Mwakisunga alipotembelea Kongowe Pwani
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza (wa pili kulia) akiwaelekeza jambo Ofisa MKuu wa Masoko wa Vodacom Charity Safford(wa kwanza kulia) na Mkuu wa Idara ya Chapa Vodacom na Mawasiliano Kelvin Twissa mjini Kongowe, Mkoani Pwani. Meza jana alifanya ziara ya kukagua mwenendo wa kibiashara wa Vodacom katika meneo kadhaa Mkoani Pwani baada ya Vodacom kufanya maboresho makubwa katika miundombinu ya utoaji wa huduma zake za simu za mkononi mkoani humo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza (wa pili kulia) akimsikiliza Mkuu wa Idara ya Uhandisi wa kampuni hiyo Nguvu Kamando  wakati Meza alipotembelea eneo la Kibaha kujionea hali ya soko kibiashara kwa Vodacom. Kushoto mwenye fulana nyekundu ni Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji Hassan Saleh
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza(mwenye fulana nyeusi) akiongea na vijana wa Mjini Kongowe namna wanavyopata huduma za Vodacom. Meza jana alitembelea maeneno mbalimbali ya mkoa wa Pwani kujionea upatakinajai wa huduma za Vodacom baada ya kampuni hiyo kufanya maboresho makubwa katika utoaji wa huduma zake mkoani humo
Vijana wa Kongowe mkoani Pwani wakifurahia kasi na ubora wa huduma za Vodacom baada ya kampuni hiyo kufanya maboresho makubwa ya kuongezea nguvu minara yake ili kuboresha huduma zake za simu z amkononi ikiwemo kiupiga simu,intaneti na M-pesa

MAADHIMISHO YA VITA VYA MAJIMAJI KUFANYIKA RUVUMA TAREHE 25-27 FEBRUARI 2013

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamis Suedi Kagasheki atakuwa mgeni rasmi katika siku ya kilele cha maadhimisho ya Kumbukizi ya vita vya Maji Maji na Utalii wa Utamaduni yatakayofanyika Songea mkoani Ruvuma Februari 27 mwaka huu.

Maadhimisho hayo ya siku tatu ambayo kitaifa yameandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Mkoa wa Ruvuma yatafunguliwatarehe 25 Februari katika Makumbusho ya Vita vya Majimaji mjini Songea.

Madhumni ya maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila mwaka ni kuwakumbuka mashujaa 67 walionyongwa tarehe 27 Februari 1906 walipokuwa katika harakati za kupinga ukoloni wa Mjerumani.  Baadhi ya mashujaa hao ambao wote walizikwa katika kaburi moja ni Ndugu Mputa Gama, Songea Mbano, Mpambalyoto Soko na MajiyaKuhanga Komba.

Katika siku tatu za maadhimisho wananchi na wadau mbalimbali wa utalii watapata fursa ya kutembelea na kujionea utajiri wa vivutio vya utalii ulioko Kusini mwa Tanzania hususan  Mkoa wa Ruvuma  ili waweze kuongeza uelewa na kushiriki kuvitangaza vivutio hivyo.

Aidha, Wizara itaendesha mdahalo Februari 25 katika Club ya Songea ili kutoa nafasi kwa wadau wa malikale na utalii kujadili namna bora ya kutumia fursa za uwekezaji katika sekta ya utalii Kusini mwa Tanzania.

Wananchi wote wa mkoa wa Ruvuma, na nchini kote kwa ujumla, wanakaribishwa kuhudhuria maadhimisho hayo ya Kumbukizi ya vita vya Maji Maji na Utalii wa Utamaduni.

G. Matiko
MSEMAJI

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII


ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Globu ya Jamii haijasahau watoto. Hapa ni ngoma ya Twinkle Twinkle Star....

CHEKA UNENEPE

$
0
0
Cheka unenepe na kipande cha Peter Sellers katika filamu ya "The party"

Naibu spika atembelea Bunge la Majlis Shura nchini Oman

$
0
0
 Naibu Spika na ujumbe wake wakiwa na wenyeji wao katika ukumbi wa Bunge la Majlis Shura nchini Oman.
 Katibu wa Bunge la Majlis Shura Sheikh Al Al Mahrooqi (katikati) akitoa maelezo kwa Naibu Spika kuhusu historia ya nchi hiyo.Naibu Spika yuko nchini Oman kwa ziara ya kibunge.
 Naibu Spika Mhe.Job Ndugai akiwasilisha ujumbe maalum wa Bunge la Tanzania kwa Spika wa Bunge la Oman lijulikanalo kama Majlis Shura.Naibu Spika na wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge wako Muacat Oman kuanzisha mahusiano maalum ya kibunge baina ya nchi hizo mbili. Pichani kulia ni viongozi kadhaa wa Majlis Shura na kushoto ni ujumbe wa Tanzania uliomshirikisha pia  Kaimu Balozi Nd.Abdallah Kilima(kwanza Kushoto).
Naibu Spika Job Ndugai akimkabidhi mwenyeji wake ambae ni Spika wa Bunge la Majlis Shura, Sheikh Khaled bin Nasser Al Mawwali zawadi maalum ya jengo la Bunge la Tanzania

Maonesho ya SHANGAA-Art of Tanzania yatia fora New York

$
0
0

 Mhe. Tuvako Manongi, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa akiongea katika hafla hiyo
 Mhe. Tuvako Manongi, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa akitoa shahada ya heshima kwa waandaaji

Queense Community Collage ambacho ni sehemu ya mtandao wa Vyuo vikuu vya Jiji la New   York  ( City University of New York )  mwishoni wa wiki kiliandaa maonesho   sanaa za kitanzania.

Maonesho    hayo  yaliyofanyika katika Chuo hicho  yanaelezwa na   waandaji  ni ya kwanza kufanyika nje ya Tanzania na Ujerumani,  yalipewa  jina  la  SHANGAA-Art of Tanzania likihusisha mkusanyiko  sanaa zaidi ya  112 lakini  kila moja ikibeba maudhui yake. Kwa kweli kama lilivyo  jina la maonesho hayo, ziliwashagaza wageni mbalimbali waliohudhuria maonesho hayo.

 Tuvako Manongi, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ndiye aliyepamba maonesho hayo  kama mgeni wa heshima, akiambatana  na Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania Nchi Marekani, Bi. Lily Munanka.

Sanaa zilizopamba maonyesho hayo  zilikuwa ni za kuchonga nyingi kati yake zikitoka katika Mikoa ya  Usukumani na Umakondeni. Laini pia kulikuwa na video zilizokuwa zikionyesha aina mbalimbali za ngoma zikionyesha mila na utamaduni wa mtanzania katika uhalisia wake.

Jumla ya  sanaa 121 zilikusanywa kutoka wa wadau mbalimbali lakini ni 112 tu zilizoweza kuoneshwa kutokana na uhaba wa nafasi.

Kwa kutambua umuhimu wa maonyesho hayo  Halmashauri ya Jiji la New York ilitoa Hati kwa waandaaji wa maonesho hayo.



NAIBU WAZIRI WA FEDHA AKAGUA VITEGAUCHUMI VYA VYA PSPF JIJINI DAR

$
0
0

SIKU MOJA baada ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kuwatembezea wadau na wanachama wake katika nyumba za mradi wa nyumba za makazi ambazo zimejengwa na Shirika hilo eneo la Buyuni kata ya Majohe Chanika Wilayani Ilala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam,  Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene nae ametembelea na kujionea nyumba hizo na kuumwagia sifa Mfuko huo kwa ubunifu na kuwajali wananchama wake. 

Mbene pia alitembelea Ujenzi wa jingo la Kitegauchumi la Ghorofa 35 linalojengwa na Mfuko huo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu akimpa maelezo Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene juu ya muundo kamili wa Jengo hilo la ghorofa 35 ambalo linajengwa na PSPF jijini Dar es Salaam na litakuwa na maduka, makazi na Ofisi.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Jengo hilo la PSPF Tower, Ghazi Al Shamali (kushoto) akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu juu ya hatua zilizofikiwa hadi sasa katika ujenzi huo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images