Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 50 | 51 | (Page 52) | 53 | 54 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Imeandikwa na Urban Pulse na Freddy Macha -Picha zote za Urban Pulse 14. Wanamitindo wa Kitanzania kwenye London Fashion Week 2013. Anna Lukindo, Christine Mhando, Jacquiline Kibacha-pic by Urban PulseWanamitindo wa Kitanzania- Anna Lukindo, Christine Mhando na Jacqueline Kibacha Jumapili mchana wilaya ya Westminster jijini London ilikuwa na mashindano ya ubunifu na urembo katika maonyesho ya kimataifa ya London Fashion Week. Mashindano haya yalifanyika jumba la Somerset lililosimama imara kwenye upembe wa kaskazi ya mto Thames. Nje ya Jumba la Somerset- Samson Soboye, Jacqueline Kibacha, Mama Kallaghe, Anna Luks na Rose Kiondo-pic by Urban PulseNje ya Jumba la Somerset- Samson Soboye (Mpangaji wa maonyesho), Jacqueline Kibacha ("Heart 365"), Mama Balozi Joyce Kallaghe, Anna Lukindo ("Anna Luks") na Rose Kiondo (Mratibu wa maonyesho) Maonyesho ya London Fashion Week, bado yanaendelea jumba hili la Somerset toka tarehe 14 hadi tarehe 28. Wiki hizi mbili nzima zitakutanisha kila mtu anaye husika na biashara ya mavazi na urembo. Magwiji na mapapa wa mitindo, wabunifu, walimbwende, watafuta vipaji, wafanya biashara, wazalishaji mali ghafi na wamiliki viwanda. Wote hukutana katika maonyesho haya. Hapa si vipaji tu vinavyojionyesha, bali pia watu wa biashara. LondonFashion2013 booklet
  Siku hii Tanzania ilikuwa moja ya nchi mbili tu za Kiafrika zilizochaguliwa na British Council na "London Fashion Week" kushiriki mashindano ya kutafuta vipaji chipukizi kwenye tasnia ya ubunifu wa mavazi na urembo. Watanzania Anna Lukindo, Jacqueline Kibacha na Christine Mhando ndio wasanii waliobeba bendera ya taifa letu na kutuwakilisha katika mashindano haya ya kimataifa yanayofanyika kila mwaka kwa zaidi ya miaka 27 sasa. Barabara ya The Strand copyBarabara maarufu ya The Strand... Ili kuunga mkono maendeleo ya Tanzania na Watanzania, Ubalozi wetu Uingereza na Bodi ya Utalii Tanzania, nao pia walichukua nafasi hii kuwasaidia wananchi hawa kufanikisha mahitaji yao ya ushindani. Ubalozi umetoa Ukumbi wa Nyumba Ya Tanzania ulioko Bond Street ili wasanii hao waweze kuonyesha nguo na sanaa zao kwa juma zima kama sheria za London Fashion Week zinavyoamuru. Vile vile Bodi ya Utalii ya Tanzania imesaidia katika mchango wa mali ghafi zilizotumika katika shughuli hizi ili kuiuza Tanzania kimataifa. Anna Luks -pic by Urban PulseAnna Luks Mshindi wa tukio alikua Estonia. Ingawa Tanzania haikuwa mshindi wa mwanzo- ilichaguliwa kati ya Kumi Bora jambo ambalo limetikisa nyoyo na vichwa vya waandaaji, wabunifu,wafanya biashara na watafuta vipaji vya kimataifa. Hii ni mara ya kwanza kwa taifa letu kushiriki katika shughuli na wote wameguswa na kupumbazwa na usanii wa hali ya juu ulioonyeshwa na wasanii watatu wa Kitanzania. Maneno Lukindo, Mhando na Kibacha wamechukua nafasi waliyopewa kwa mikono miwili na wote wameisogeza Tanzania hatua moja zaidi ndani ya ulingo wa kimataifa na katika biashara hii ya mavazi na urembo ambayo inasemekana ina thamani ya Pauni bilioni 10 ama Shilingi trilioni 25 za Tanzania.

  0 0

  Mgeni Rasmi katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt. Seif Rashid akitoa ufafanuzi wa Wizara juu ya maswala ya afya hapa nchini wakati wa Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
   Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa yote hapa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh. Abbas Kandoro akizungumza wakati akifunga Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa yote hapa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh. Abbas Kandoro kwa ajili ya kufunga Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
  Msajili wa Baraza la Pharmacy Tanzania,Dkt. Mildred Kinyawa akiwasilisha mada yake ya kuuhusiana na Usajili wa Maduka ya Dawa Baridi Vijijini wakati wa Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
  Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania,Nevile Meena akiwasilisha ya kuhusu Mchango wa Vyombo vya Habari katika Sekta ya Afya,katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
  Meneja Ufuatiliaji na Tathmini ya Mipango Kazi na Mpango Mkakati kutoka Bohari Kuu ya Dawa Tanzania (MSD),Cosmas Nalimi akiwasilisha Mada ya Kuhusu Upatikanaji wa Dawa Vijijini,katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
  Baadhi ya Wanahabari kutoka Vyombo mbali mbali vya Habari wakifatilia kwa makini Mada zinazotolewa kwenye Kongamano hilo la nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
  Wakali wa Uchoraji wa Vibonzo hapa nchini,toka kulia ni Masoud Ally Kipanya,King Kinya pamoja na Nathan Mpangala a.k.a Kijast Bikozzz wakifatilia kwa makini Mada zinazotolewa kwenye Kongamano hilo la nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
  Wadau Stephen Wang'anyi (Muwakilishi wa ITV na Radio One,Shinyanga),Augustine Nigendi wa Channel Ten,Mara) pamoja na George Maratu wa ITV Mara wakipitia Libeneke la Glogu ya Jamii.
  Mdau wa Globu ya Jamii kutoka Mkoani Lindi,Abdulaziz Video akiendeleza libeneke wakati wa Kongamano hilo la nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.


  0 0


  0 0

  Pichani ni baadhi ya Wasanii watakao tumbuiza kwenye tafrija ya Montage Charity Ball itakayofanyika jioni ya leo ndani ya Serena Hotel,jijini Dar.Kutoka kushoto ni Peter Msechu,Kidumu kutoka Kenya,Barnaba pamoja na Deo Mwanambilimbi ambaye ni kiongozi wa Kulunde Band.
  Pichani shoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda (katikati) akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea kufanyika kwa tafrija maalum ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball,itakayofanyika jioni ya leo, Februari 22 kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam

  Aidha Teddy ameeleza kuwa malengo hasa ni kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Wanawake wenye matatizo mbali mbali.Mgeni rasmi katika Tafrija hiyo anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA),Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.Kulia kwake ni baadhi ya Wasanii watakaotumbuiza kwenye tafrija hiyo ambao ni Kidumu kutoka Kenya,Barnaba pamoja na Deo Mwanambilimbi ambaye ni kiongozi wa Kulunde Band naPeter Msechu ambaye hayupo pichani.

  0 0

  MKOA wa Mbeya nao umechaguliwa kubeba jahazi la kufanyika Tamasha la Pasaka Aprili mosi mwaka huu.

  Mapema wiki hii waandaaji wa tamasha hilo walisema kuwa siku yenyewe ya sikukuu ya Pasaka, Machi 31 litafanyika jijini Dar es Salaam na kwamba walikuwa wakihangaika kutafuta mahali litakapofanyika siku inayofuata. 

  “Tumekubaliana kuwa Jumatatu ya Pasaka, ambayo itakuwa Aprili mosi, tamasha letu lifanyike mkoani Mbeya. Hivyo tayari tumepata mikoa miwili ambayo tamasha litafanyika bado mingine mitano.

  “Mkoa wa Mbeya umechukua jukumu la kufanyika Jumatatu ya Pasaka kutokana na idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa wameomba awali siku yenyewe ya tamasha ifanyike mkoani  humo, lakini kwa kuwa Dar es Salaam iliongoza tukaamua Mbeya iliyoshika nafasi ya pili basi ipewe jukumu la kuandaa Jumatatu ya Pasaka,” alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo,Bwa. Alex Msama.

  Alisema kamati yake ilikuwa ikiendesha kura za maoni kwa mashabiki wao wa eneo lipi tamasha hilo lifanyike na kwamba Dar es Salaam na Mbeya ndizo zimeshika nafasi za juu.

  Alisema dhamira yao mwaka huu ni kufanya matamasha katika mikoa saba tofauti, hivyo bado wanajipanga kuona maeneo mengine ambapo tamasha hilo linaweza kutumbuiza.


  0 0

  Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe katikati ya wiki hii aliongoza ujumbe wa Tanzania nchini Zambia katika kikao cha 58 cha Baraza la Mawaziri wanaosimamia uendeshaji wa Reli ya Tazara. Kikao hiki cha siku mbili kiliwajumuisha Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Uchukuzi), Mhe. Saada Salum (Fedha) na Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda (Viwanda na Biashara) na Mawaziri wa sekta husika kutoka Zambia. Aidha, kikao hiki kilitanguliwa na kikao cha Bodi ya TAZARA. Ujumbe wa Tanzania ukiwa nchini humo uliweza kumtembelea Rais wa kwanza wa Zambia Mhe. Kenneth Kaunda katika ofisi zake ambapo katika kikao cha pamoja na Rais huyo, Mhe. Kaunda alisisitiza mshikamano na upendo miongoni mwa waafrika na kuwahimiza ‘vijana’ viongozi waliopewa jukumu la kusimamia TAZARA kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi wa RELI hii ili iendelea kuwasaidia wananchi wa nchi zote mbili.
  Waziri wa Uchukuzi Mhe. Dkt. H. Mwakyemba, (Aliyesimama) akiongea mbele ya Rais wa kwanza wa Zambia Mhe. Kenneth Kaunda wakati wajumbe kutoka Tanzania walipomtembelea Rais huyo katika ofisi zake. Wengine katika picha ni wajumbe wa Bodi ya Tazara kutoka Tanzania.
  Rais wa Kwanza wa Zambia Keneth Kaunda wa nne kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tanzania na Zambia. Kulia kwa Mhe. Kaunda ni Balozi wa Tanzania nchini Zambia mama Grace Mujuma na anayefuata ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Eng. Omar Chambo. Kushoto kwa Mhe. Kaunda ni Waziri wa Uchukuzi Mhe. Dkt. Mwakyembe, akifuatiwa na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum na anayefuta ni Waziri wa Uchukuzi wa Zambia Mhe. Christopher Yaluma, Wengine katika picha ni Wajumbe wa Bodi ya TAZARA kutoka Tanzania.

  0 0
 • 02/22/13--04:33: IN LOVING MEMORY
 • THE LATE ESTHER NYIMBO BADI

  It is exactly one year today since the fateful Wednesday, 22nd February 2012 at 6.30 p.m when you left us without a word of "kwaheri". We continue to celebrate your life our beloved mother Esther Nyimbo Badi. The pain of loosing you, Mum, still remains fresh in our hearts. Mum, no words are sufficient to describe the significant role you played in our lives; your discipline and leadership qualities greatly influenced the lives of all children who passed through your hands. You were a great pillar in our family.

  Days may break and night may fall; seasons may start and seasons may end; years may come and years may go; but your memory lives in our hearts, perpetuated by the destiny of time.

  You are profondly remembered and cherished by your children Blandina, Bertha, Stella, Joseph, Lilian, John and Upendo; your in-laws Cashmir, Modest, James, Ken and Afro; your grand children Kim, Abraham, Faith, Jeff, Deborah, Larry, Caleb, Karen, Sarah, Brandon, Dillan, Esther and Suzana.

  Mum in God’s hands rest in peace, in our hearts you live forever.
  May the Lord shower you with favor until we meet again.

  Psalm 103: 1 ‘Bless the Lord o my soul, and that all that is within me, bless His holy name’.

  0 0


   Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akifafanua jambo wakati mkutano na wafanyakazi wa Kampuni ya Mwananchi Communications kuhusu mikopo ya Saccos kwa wanachama wa NSSF. Kushoto ni Meneja Kiongozi, Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume na Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika hilo, Mseli Abdalah. 
  Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd, Bakari Machumu akizungumza wakati wa mkutano na viongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuhusu mikopo ya Saccos.
   Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mseli Abdalah akifafanua jambo kuhusu mikopo ya Saccos kwa wanachama wa NSSF wakati wa mkutano na wafanyakazi wa Mwananchi Communications Ltd jijini Dar es Salaam. Kushoto ni  Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd, Bakari Machumu, Meneja Kiongozi, Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori.
  Mwenyekiti wa  Saccos ya Mwananchi Communications Ltd, Haura Shamte akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
  Mpoki Bukuku akizungumza wakati wa semina iliyoandaliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa wafanyakazi wa Mwananchi Communications Ltd kuhusu mikopo ya Saccos kwa wanachama wa NSSF.  
   Wafanyakazi wa Mwananchi Communications wakiwa katika mkutano huo.
  Meneja Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mseli Abdalah akitoa mada kuhusu mikopo ya Saccos kwa wanachama wa NSSF wakati wa mkutano na wafanyakazi wa Mwananchi Communications Ltd jijini Dar es Salaam, leo.Picha na Francis Dande.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage (iliyoandaa hafla hiyo),Teddy Mapunda akimpa zawadi ya heshima Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete mara baada ya kuifanikisha vyema tafrija maalum ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball,iliyofanyika jioni ya leo kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana.

  Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimkabidhi Bwa.Charles Stith ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania cheti chake cha heshima ,mara baada ya kuchangia  $ 10,000 kwenye hafla ya kukusanya kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Wanawake wenye matatizo mbali mbali,Anaeshuhudia pichani kulia ni Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana usiku huu,ndani ya hoteli ya Serena,jijini Dar.
  Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimkabidhi Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BOT),Bwa.Benno Ndulu cheti chake cha heshima ,mara baada ya kuchangia  Milioni Kumi kwenye hafla ya kukusanya kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Wanawake wenye matatizo mbali mbali,Anaeshuhudia pichani kulia ni Mke wa Makamu wa Rais,Mama Asha Bilal,aidha katika tafrija hiyo iliyofana sana kiasi cha shilingi milioni 142 na laki tano zimepatikana usiku huu,ndani ya hoteli ya Serena,jijini Dar.
  Mgeni Rasmi,Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akimkabidhi cheti cha heshim mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Powerbreakfast kutoka Clouds FM,Said Bonge a.k.a Bonge Barabarani ambaye pia alichangia kiasi cha shilingi laki tisa. 

  PICHA ZAIDI INGIA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

  0 0
 • 02/22/13--19:00: ngoma azipendazo ankal

 • 0 0
 • 02/22/13--19:00: CHEKA UNENEPE
 • Cheka Unenepe na Mr Bean

  0 0


  High Commissioner Tajammul Atlaf (left) of the High Commission for the Islamic Republic of Pakistan earlier today paid a courtesy visit to Ambassador Mbelwa Kairuki (right), Director of the Department of Asia and Australasia in the Ministry. Among other things, the two Ambassadors discussed areas of continued cooperation in the fields such as
  industry, agriculture, health and education.

  High Commissioner Tajammul Atlaf making a point during his discussion with Ambassador Kairuki.

  Listening on is Ambassador Kairuki (right) reviewing documents while listening to Ambassador and Mr. Charles Faini, Foreign Service Officer in the Ministry. 
  All photos by Tagie Daisy Mwakawago of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation

  0 0

   Naibu mkuu wa pili wa Idhaa za Kiswahili wa DW, Josephat Charo. akimpa mkono wa heri kwa furaha Mtangazaji Stumai George baada ya kumaliza muda wake wa mwaka mmoja kuhudumu kama mtangazaji DW.
    Stumai George akipewa mazagazaga  na kulambishwa nondo ya bye bye  mama lakini uwe unakumbuka DW na Naibu mkuu wa pili wa Idhaa za Kiswahili wa DW, Josephat Charo mjini Bonn.
   Wafanyakazi wa DW katika hafla fupi ya kwa heri ya kuonana  Stumai George ambae anarudi Star TV Dar es Salaam.
  Wafanyakayi wa DW na Kicheko kinachoashiria dhahiri kwamba Stumai George pamoja na kuondoka lakini mwenzao wa dhati.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli (Mb) amezindua bodi ya Usajili wa Makandarasi Contractor Registration Board (CRB) pamoja na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) jijini Dar es Salaam

  <![endif]-->Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa  Dk. John  Pombe Magufuli (Mb) akungumza na wajumbe wa wapya na wazamani wa Bodi za (ERB) na (CRB)  hawapo pichani kabla ya kuzindua bodi hizo jijini Dar es Salaam

  Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli akimkabidhi zawadi ya shukrani mjumbe wa zamani wa Bodi ya (CRB)  Dk.Dalali Kafumu.

  Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa  Dk. John  Pombe Magufuli (Mb) akimkabidhi  Samsung Galax kama kitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi ERB  Mhandisi Profesa Ninatubu Lema mara baada ya kuzindua bodi hizo mbili.     

  Msajili wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Steven Mlote akizungumza kabla ya kuzinduliwa kwa bodi hizo mbili

  Mwenyekiti wa Bodi ya usajili wa Makandarasi (CRB) Mhandisi Consolatha Ngimbwa (CRB) akizungumza kabla ya kuzinduliwa kwa bodi ya CRB

  0 0

  David  feared his wife Eshe wasn't hearing as well as she used to and he thought she might need a hearing aid. Not quite sure how to approach her, he called the family Doctor to discuss the problem.

  The Doctor told him there is a simple informal test the husband could perform to give the Doctor a better idea about her hearing loss. 'Here's what you do,' said the Doctor, 'stand about 40 feet away from her, and in a normal conversational speaking tone see if she hears you. If not, go to 30 feet, then 20 feet, and so on until you get a
  response..'

  That evening, the wife is in the kitchen cooking dinner, and he was In the den.
  He says to himself, 'I'm about 40 feet away, let's see what happens.'Then in a normal tone he asks, 'Honey, what's for dinner?'

  No response.
  So the husband moves closer to the kitchen, about 30 feet from his wife and repeats, 'Eshe, what's for dinner?'

  Still no response.
  Next he moves into the dining room where he is about 20 feet from his Wife and asks, 'Honey, what's for dinner?'

  Again he gets no response.
  So, he walks up to the kitchen door, about 10 feet away. 'Honey, what's for dinner?'

  Again there is no response.
  So he walks right up behind her. 'Eshe, what's for dinner?'
  (I just love this)
  'For God's sake, Davie, for the FIFTH time, CHICKEN!'

  0 0


  Mzungu Kichaa has been selected to perform at the Danish showcase festival SPOT (www.spotfestival.dk) in May 2013. The tour also includes performances in Tanzania, Germany and the UK. Concert details will be announced on www.facebook.com/mzungukichaa
  Mzungu Kichaa has been selected to perform at SPOT festival, which is one of the most prestigious showcase festivals in the country. At SPOT Mzungu Kichaa will launch a new performance setup, which will be ”unplugged” and more ”raw” than ever.
  ”I realised that when I try to enter a new territory with my music, the main problem I face is mobility. My band is from Tanzania and I feel a band from Europe cannot replace them. Therefore I decided to reinvent my music and create an ”unplugged” setup. However, in August and November I will be touring Denmark again with my full Tanzanian band. But I am very excited about standing on my own two feet and getting close and personal with my audience through my ”unplugged” concerts this spring”.– Mzungu Kichaa
  Danish born Mzungu Kichaa grew up in Africa. His eclectic life journey is reflected in his vibrant sound, shaped by the diverse musical traditions he has encountered. The award-winning artist is considered one of the most popular touring acts in East Africa and is steadily gaining popularity on the international scene with his unique interpretation of the Tanzanian genre, Bongo Flava.
  When Mzungu Kichaa released his debut album ”TukoPamoja” in 2009, all his songs were in Swahili. In December 2012, he released an EP titled "Hustle", which includes his first songs in English and resulted in a nomination for a Danish Music Award in the category "Best World Track".
  “For my new release I decided to share my story with my non-Swahili speaking fans by writing in English. Hustle is a project of self-discovery in search of my sound and identity. It represents the universal fight for an existence and a plea to never give up your dreams.” – Mzungu Kichaa
  GENRE: Bongo Flava
  INSPIRED BY: Franco LuamboMakiadi, Toots and the Maytals, Jimi Hendrix
  CAREER START: 2009 
  DISCOGRAPHY
  Hustle – EP – Caravan Records 2012
  TukoPamoja – Album – Caravan Records 2009

  LINKS

  0 0
 • 02/23/13--01:38: MSIBA KIBAHA
 • Familia ya Dr. Denis William Issa mkuu wa kituo cha utafiti wa miwa Kibaha Mkoa wa Pwani inasikitika kutangaza kifo cha Dr Denis Wiliam Issa (pichani) kilichotokea 21 February 2013 katika Hospitali  ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

  Mazishi yanategemewa kufanyika nyumbani kwa marehemu  Picha ya Ndege mjini Kibaha leo Juma mosi, tarehe 23 February, 2013 kuanzia saa5 asubuhi.  Habari ziwafikie wanandugu wote wana Mtwara na wafanyakazi wa wizara ya Kilimo pamoja na Watafiti Wote
  Mawasiliano 0715297361
  Bwana Ayubu Makoja

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakati alipowasili katika hafla ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu leo. Katikati ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na kumpongeza Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, mara baada ya balozi huyo kumaliza kusoma hotuba yake iliyochanganywa na Kiswahili, wakati wa hafla ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu leo. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli.
   Balozi wa Japan Nchini Tanzania, Masaki Okada, akishiriki kucheza sebene la bendi ya Msondo Ngoma na Vijana wa kikundi cha uhamasishaji cha Temeke, wakati wa hafla hiyo.
   Baadhi ya wanamuziki wa bendi ya Msondo Ngoma, wakishambulia jukwaa kutoa burudani wakati wa halfa hiyo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakifunua kitambaa kwa pamoja ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu leo. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (kushoto) wakishiriki kwa pamoja kukata utepe ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu leo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Wazee wastaafu wa CCM, mara baada ya kumaliza kupiga nao picha ya pamoja ya kumbukumbu wakati wa hafla ya ufunguzi wa mradi wa Upanuzi wa Barabara ya Kilwa, eneo la Mbagala Rangi tatu leo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi kutembea na kukagua sehemu ya Barabara ya Kilwa eneo la Mbagala Rangi tatu, baada ya kufungua rasmi barabara hiyo iliyokamilika kwa Upanuzi na ukarabati. Hafla hiyo ya ufunguzi imefanyika leo. Picha na OMR

  0 0

  WAZIRI MKUU  Mhe. Mizengo Pinda ameunda Tume maalum itakayofanya uchunguzi wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ambayo yalitangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa Februari 18, mwaka huu.
  Katika matokeo hayo yaliyotangazwa Jumatatu wiki hii, asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne Oktoba, 2012 walifeli.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Peniel Lyimo amesema Tume hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kazi wakati wowote wiki ijayo inajumuisha wadau kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tanzania Association of Managers and Owners of Non-Government Schools/Colleges (TAMONGSCO), Taasisi za Dini zinazotoa huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) zinazoshughulikia masuala ya elimu.
  Wadau wengine watatoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA).
  Amesema Serikali inawaomba wadau wa elimu, wazazi, walezi na wananchi wote kwa ujumla watoe ushirikiano kwa Tume ili iweze kufanya kazi yake kwa ufanisi.
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 3021,
  DAR ES SALAAM.
  JUMAMOSI, FEBRUARI 23, 2013.

  0 0

  Frederick-Mwakalebela.jpg
  ZAIDI ya watoto 30 wanaoishi katika mazingira magumu na yatima wamepelekwa shule za sekondari mbalimbali mjini hapa na Asasi isiyo ya Kiserikali ya TCDA  ya mjini Iringa kupitia udhamini wa Fredrick Mwakalebela aliyekuwa mgombea ubunge mwaka 2010

  Akizungumza na Ripota wetu Msemaji na Mwanasheria wa Asasi hiyo Daniel Kibiki alisema kwamba Mwakalebela amejitolea kuwasomesha wanafunzi hao walikuwa katika mazingira magumu na yatima walioko katika halmashauri ya manispaa na nje ya mkoa.

  Kibiki alisema kwamba malipo ya awali ya shilingi milioni 13.6 zimeshatumika katika malipo ya awali kwa wanafunzi hao katika shule wanazosoma kama malipo ya ada, sare za shule, na matumizi ya kawaida kwa wanafunzi hiyo.

  Aidha Kibiki alitoa wito kwa wanafunzi hao mbalimbali kuweza kujitokeza katika asasi hiyo kuweza kupata msaada zaidi wa kimasomo kuliko kuendelea kuzurura mitaani bila kazi na kuongeza kwamba wanafunzi waliopata msaada huo watasomeshwa hadi kidato cha sita kama wakifanya vizuri katkika mitihani yao ya kidato cha nne.

  Naye mfadhili wa wanafunzi hao Fredrick Mwakalebela aliwataka wadau mbalimbali kuweza kujitokeza kuwasaidia watoto yatima na wanaoshi katika mazingira magumu kuliko kuendekeza starehe.
  “naomba sana mashirika mbalimbali na watu wenye uwezo kujitokeza kuwasaidia watoto hawa kwani kwa sasa wamezidi sana mkoani kwetu”

  Mwakalebela alisema kuwa kila mwaka ataongeza idadi ya wanafunzi hasa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kupitia asasi ya TCDA." nitajitahidi kuongeza kila mwaka wanafunzi wenye uhitaji wa elimu ya sekondari na nitawasomesha hadi kidato cha sita hasa kama wakifanya vizuri katika kidato cha nne"
  Na  Denis Mlowe Iringa.

older | 1 | .... | 50 | 51 | (Page 52) | 53 | 54 | .... | 3270 | newer