Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 52 | 53 | (Page 54) | 55 | 56 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Mbunge wa Kawe Mheshimiwa Halima Mdee amesema watoto wa viongozi kusoma shule za binafsi maarufu kama “Academia” inachangia matokeo mabovu ya kidato cha nne kwa shule za kawaida. Mdee aliyasema hayo wakati akijibu swali la chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu mwaka hadi mwaka wakati akiongea na Fina Mango katika Kipindi cha Makutano.

   “Kwa Mtazamo wangu mimi, zamani watoto wa viongozi tulikuwa tunasoma shule hizi za umma, kwa siku hizi tunawasomesha hizi shule za academia, kwa ubinafsi wetu hawa huku kwa kuwa watoto wetu hawapo hata ule moyo wa kutoa maelekezo unakuwa haupo” .

  Mdee aliongezea kusema hii yote inachangiwa na mipango ya serikali iliyowekwa kwa kiwango kikubwa sana cha fedha kushindwa kutekelezeka au kusimamiwa ipasavyo ili yaweze kutekelezeka na kutolea mfano wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari.

  (MMES II) ambao serikali ilitenga Shilingi bilioni 200 wakati huo kiwango cha ufaulu daraja la kwanza hadi la tatu ukiwa 37% ikiwa na malengo kiwango kipande hadi 70% lakini ilipofika 2009 kiwango cha ufaulu kikashuka hadi 17%, 2011 kikashuka tena hadi 9% na mwaka jana kikazidi kudidimia mpaka 5%.

  Mdee alisisitiza kuwa tatizo kubwa linalozikabili shule za kata ni miundombinu ya shule na maslahi ya walimu kwa kusema “Kinachojitekeza sasa ni mrundikano wa frustration za walimu, wamekata tamaa kabisa kwa sababu vipato vyao ni vidogo sana, lakini pamoja na kuwa vidogo vile wanavyotakiwa kuvipata kutokana na vipato kuwa vidogo hawavipati , na zaidi wakati walimu wanasema wanadai serikali inasema hawadai”.

  Mheshimiwa Halima Mdee alimalizia kwa kusema anadhani ni wakati sasa kama taifa lazima serikali iamue inataka kufikisha wapi elimu kwa kuwepo bajeti inayotosheleza mahitaji na kuzingatia hali halisi ya maisha na soko, na kusisitiza uwepo wa mitaala inayoeleweka tofauti na hivi sasa ambapo waalimu wanasema wanapokea maelezo tu na kujiandalia wenyewe mitaala. Pia alisisitiza uwepo wa mgawanyo wa walimu bila upendeleo kwa kila shule tofauti na sasa ambako kuna shule hazina walimu wa kutosha na pia uwepo mamlaka ya usimamizi wa elimu yenye nguvu.

  Mahojiano yote yanapatikana katika: http://www.hulkshare.com/81arza49bg5c

  Mheshimiwa Halima Mdee akinukuu ilani ya uchaguzi ya CCM wakati akijibu swali.
  Mtangazaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango na Mbunge wa Kawe Halima Mdee baada ya kipindi.
  Fina Mango akimuuliza Halima Mdee swali wakati wa mahojiano ya moja kwa moja katika kipindi cha Makutano.

  0 0
 • 02/24/13--02:49: Ajali Mbaya yatokea Iringa
 • Ajali hii iliyohusisha magari mawili,Toyota Rav 4 na Toyota Cresta imetokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la jirani na Maktaba ya mkoa,mjini Iringa,ambapo gari hiyo aina ya RAV 4  iliruka ukingo la barabara  uliojengwa kwa sementi na kutua juu ya Gari hiyo aina ya Toyota Cresta (Taxi) na kushindwa kuendelea na safari.inasemekana kuwa isingesimama gari hiyo aina ya Toyota Cresta,basi dereva wa gari hiyo aina ya Rav 4 labda angekuwa katika wakati mgumu zaidi au kuoteza maisha kabisa. hakuna aliepoteza maisha kwenye ajali hiyo. Picha na Meshack Maganga-Iringa

  0 0


  Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki Eng. Oscar Mwanjesa akSikata keki ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake mbele ya wafanyakazi wenzake wa Mamlaka hiyo wakati wa hafla ya family day iliyofanyika katika hoteli ya Southan Beach Kigamboni Dar es Salaam. Watatu kutoka kulia ni Kaim Meneja Mawasliano wa TCRA Semu Mwakyajala.
  Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  kanda ya Mashariki wakishindano kufukuza kuku wakati wa katika ufukwe wa haoteli ya Southan Beach Kigamboni ikiwa ni sehemu moja wapo ya kusherehekea siku ya Familia iliyoandaliwa na Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
  Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki wakishindana kukumbia na Magunia ikiwa ni sehemuya shamlashamla za kusherehekea siku ya Familia iliyofanyika katika hoteli ya Southan Beach Kigamboni jijini Dar es Salaam.


  0 0


  Mechi namba 120 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Februari 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Yanga kuibuka ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam imeingiza sh. 239,686,000.

  Watazamaji 39,315 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 58,794,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 36,562,271.19.

  Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 33,315 na kuingiza sh. 165,655,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 485 na kuingiza sh. 9,700,000.

  Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 29,895,725.82, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 17,937,435.49, Kamati ya Ligi sh. 17,937,435.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 8,968,717.75 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 6,975,669.36.

  Boniface Wambura
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 24, 2013.
  Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa Dkt Nkosazana Clarice Dlamini-Zuma akisaini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maalumu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 24, 2013.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe Ban Ki-moon akiweka saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa hafla hiyo maal: umu iliyofanyika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia, leo Februari 24, 2013.

  0 0

   Washiriki wa Miss Utalii Tanzania wakiwa wamewasili Baraza la Michezo Tanzania( BASATA) kwa ajili ya uzinduzi wa safari yao kuelekea Bagamoyo kutembelea vivutio vya watalii katika safari ya Utalii wa Ndani iliyodhaminiwa na kampuni mashuhuri ya utalii ya Lakeland Africa
   .Washiriki wa Miss Utalii Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja katika Fukwe ya Bahari ya Hindi, Bagamoyo.
   Ngome kongwe, Bagamoyo 
   Washiriki wa Miss Utalii tanzania  wakiwa katika moja ya Makaburi ya zamani Kaole Bagamoyo.
  Washiriki wa Miss Utalii Tanzania wakiwa katika moja ya Kaburi maarufu la Wapendanao.
   .
  Washiriki wa Miss utalii Tanzania wakiwa katika jengo la Ngome kongwe Bagamoyo.

  0 0


   Kikosi cha Simba kilichoanza katika mchezo wa leo.
   Kikosi cha Mtibwa Sugar.
   Mshambuliaji wa Simba, Amri Kiemba akichuana na kiungo wa Mtibwa Sugar, Shaban Nditi.
  Wachezaji wa akiba wa Simba wakiwa awaamini macho yao wakati jahazoi la timu hiyo likiwa linazama
  Golikipa wa Mtibwa Sugar, Hussein Shariff akidaka mpira mbele ya mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngasa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Mtibwa imeshinda bao 1-0. 

   Waamuzi wa mchezo wa leo wakitoka uwanjani
  Kocha wa Simba, Mzee Patrick Liewig akitoka uwanjani baada ya mchezo.
  Kwa hisani ya Habari Mseto Blog

  0 0


  Na Freddy Macha

  Waziri wa Nishati, Profesa Sospeter Muhongo (pichani) amewasili Uingereza leo jumapili tarehe 24.2.13 kwa ziara ya siku nne.

  Waziri alipokewa na Balozi wetu mheshimiwa Peter Kallaghe na anatazamiwa kukutana na viongozi mbalimbali wa serikali ya Uingereza na wataalamu wanaohusiana na shughuli za madini, maendeleo ya kimataifa.

  Miongoni mwa maofisa anaotazamiwa kukutana nao kesho Jumatatu  ni pamoja na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Kiafrika, Jumuiya ya Madola na nchi za Kigeni, Bwana Mark Simmonds;  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa Uingereza, Bi Lynne Featherstone na Mbunge wa Stratford chama cha Conservative, Jeremy Leffroy  ambaye pia ni mwenyekiti wa kundi la Wabunge wa Uingereza wanaoshughulikia Tanzania (APPG).

  Jumanne saa kumi na moja jioni Waziri ambaye pia ni Mbunge wa kuteuliwa amepanga kuongea na Watanzania wanaoishi Uingereza ukumbi wa Ubalozi wetu London. Ukumbi uko 3 Stratford Place, London W1C 1AS. Stratford Place iliyojishika na barabara kuu  ya Bond- ni sekunde chache tu mbele ya kituo cha magari moshi na mabasi cha Bond Street.

  Waziri Muhongo anaongozana na Dk Athanas Macheyeki wa Ukaguzi wa Madini Tanzania, Seleman Hatibu Chombo wa idara ya Nishati katika Wizara ya Madini na Nishati na Bwana Sosthenes Masau Bigambo Massola, katibu wake muhtasi.

   Waziri Muhongo ni msomi aliyebobea ndani ya masuala ya kisayansi na taaluma ya mawe na madini. Mbali na kuwa profesa na mhariri wa jarida la  “Journal of African Journal Sciences” ni vile vile mwanachama wa  jumuiya mbalimbali za madini na sayansi za kimataifa. Jumuiya hizo ni “Geological Society of London,” “Geological Society of America,” “Chinese Academy of Geological Sciences” na “Tanzania Academy of Sciences.”

   Kiongozi huyu ni  Makamu Rais wa Tume ya Tume ya Ramani ya Madini duniani iliyoundwa 1881  Ufaransa. Lengo la tume hii ni kuendeleza masuala ya mazingira, madini na hali ya hewa ya ulimwengu  na Rais wake ni Philippe Rossi.

  Mshindi wa tuzo kadhaa za kielimu na kisayansi, Profesa Muhongo alizaliwa Musoma mwaka 1954 akamaliza masomo yake vyuo vya Dar es Salaam na Ujerumani. Mwaka juzi alizawadiwa “Ordre des Palmes Academiques” ya serikali ya Ufaransa – inayotolewa kwa wataalamu waliochangia masuala ya kielimu na kitamaduni toka lipoanzishwa na Mfalme maarufu Napoelon karne ya 19.

   Mwaka 2007 kiongozi huyu alipewa tuzo la heshima (“Honours Award”) na Jumuiya ya Madini ya Afrika Kusini na 2004 akatunukiwa tuzo la “Robert Shackleton” la  Jumuiya ya Madini Afrika. Robert Shackleton aliyefariki 2001 ni Mwingereza aliyeendeleza uchimbaji madini Afrika Mashariki.

  Nchini Tanzania Waziri Muhongo amepata zawadi ya Makamu wa chuo kikuu (1977), zawadi ya Gondwana (1979) na tuzo la kitaifa la utafiti wa kisayansi na teknolojia (NARST) linalotolewa na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania(2006).  0 0

  Mshindi wa pili wa DStv Rewards, Juliet Naivasha, akifurahia zawadi yake ya kitita cha Tshs Milioni 5 kama inavyoonekana katika mfano wa hundi aliyoishikilia.
  Kwa wiki ya pili mfululizo, wateja wa DStv wanaolipia akaunti zao kila mwezi kabla hazijakatwa na hivyo kuingia katika droo maalumu inayochezeshwa kila wiki na kutoa nafasi kwa wateja kujishindia mamilioni ya fedha imeendelea tena kwa kumpata mshindi wake wa pili. Kupitia kampeni hiyo ambayo imepewa jina la DStv Rewards, Juliet Naivasha, mfanyakazi wa National Bank Of Commerce (NBC), amekuwa mshindi wa pili na kujishindia kitita cha Tshs 5,000,000 (Milioni 5).
  Mshindi wa pili wa DStv Rewards, Juliet Naivasha ( wa pili kutoka kushoto), akiwa na wafanyakazi wa MultiChoice Tanzania (Ronald Shelukindo na Furaha Samalu) pamoja na Mama yake mzazi, Hilder Lawrence Nyambo (anayemfuatia katika picha) pamoja na mdogo wake Lisa (kulia)
  DStv Rewards ni sehemu ya kampeni maalum ya kampuni ya MultiChoice Tanzania kuwashukuru wateja wao kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka kwao. Akiongelea DStv Rewards, Meneja Masoko wa kampuni ya MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu, amesema DStv Rewards ipo wazi kwa kila mteja na hivyo amewashauri waendeleee tu kulipia akaunti zao kabla hazijakatwa ili wapate nafasi ya kuibuka washindi. Wakati huo huo: Mteja wa DStv, Bwana John Komakoma,ameibuka mshindi katika droo nyingine ambayo imepewa jina la Spot The Rewards Box ambapo pindi mteja akiwa anatizama televisheni na kufanikiwa kuona kibox fulani chenye nembo ya DStv, anatakiwa kutuma SMS yenye majina yake yote mawili na namba yake ya simu kwenda katika namba +27 711 745 622 ndani ya dakika tano tangu alipokiona "kibox". Kwa ushindi huo Bwana John Komakoma ameshinda Subscription ya mwaka mzima (miezi 12) ya DStv.Kwa maana hiyo, Bw.John ataendelea kufaidi DStv bila malipo yoyote kwa kipindi cha mwaka mzima!
  Mshindi wa droo ya Spot The Rewards Box, Bw. John Komakoma (katikati) akipongwezwa na Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania, Baraka R.Shelukindo huku Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu akishuhudia. Bw. John Komakoma amesema yeye ni shabiki wa Liverpool wa kutupwa!
  Kampuni ya MultiChoice Tanzania kupitia DStv inawapongeza washindi wote.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  maafisa mbalimbali wa ubalozi wa Tanzania Nchini Ethiopia katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa leo jioni ya Februari 24, 2013 baada ya kuhudhuria hafla ya Utiaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Rais Kikwete, kabla ya kurejea Dar es salaam leo, alikwenda Uganda kuhudhuria mazishi ya baba mzazi wa Rais Yoweri Kaguta Museveni, Mzee Amos Kaguta, aliyefariki siku ya Ijumaa na kuzikwa kijijini kwake
  Rwakitura.
   Kwaheri Mheshimiwa...
   Karibu tena Mheshimiwa...
   Safari njema mkuu 
  Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Profesa Joram M. Biswaro akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Balozi Naimi Aziz (kati) na Afisa ubalozi Samwel Shelukindo wakipungia kumuaga Rais Kikwete wakati ndege yake ikiondoka uwanjani hapo leo jioni ya  Februari 24, 2013

  0 0

  The Mahege Secondary School Head Teacher Faulu Maeda (centre) receives a 10m/- cheque from the Azania Bank Principal Business Development Officer Othman Jibrea as part of the bank’s donation to the school’s dining construction project in the back ground.
   The Mahege Secondary School Head Teacher Faulu Maeda (right) displays a 10m/- cheque handed over by the Azania Bank Principal Business Development Officer Othman Jibrea (left) being part of the bank’s contribution to the school’s dining construction project
   The Azania Bank Principal Business Development Officer Othman Jibrea (left) hands over a dummy cheque to the Mahege Secondary School Head Teacher Faulu Maeda (right) being part of the bank’s contribution to the school’s dining construction project.
   The Azania Bank Principal Business Development Officer Othman Jibrea (centre) poses for a gropu photo with a cross section of Mahege Secondary School students shortly after handing over the bank’s contribution to the school’s dining construction project
   A cross section of Mahege Secondary School students having their lunch outside the school’s premises. 
   The Mahege Secondary School Head Teacher Faulu Maeda (right) shows the Azania Bank Principal Business Development Officer Othman Jibrea (left) the school’s dining construction project


  0 0
 • 02/24/13--19:00: cheka unenepe
 • Charlie Chaplin na mwenzie wakila kiatu

  0 0
 • 02/24/13--19:00: ngoma azipendazo ankal
 • Ngoma ya Super Mazembe ya 'Kasongo' ilitikisa enzi hizo

  0 0

  Picha na habari na Freddy Maro
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana aliungana na mamia ya wananchi wa Uganda katika kushiriki Mazishi ya Mzee Amos Kaguta(97) Baba ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda,yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura,magharibi ya Uganda.
   Rais Kikwete aliwasili katika mazishi hayo akitokea Addis Ababa mji Mkuu wa Ethiopia alipokuwa huko kuhudhuria Mkutano wa viongozi wa cnhi za Maziwa Makuu uliokuwa na lengo la kutafuta amani ya kudumu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 

  Akitoa salamu zake za RambiRambi katika msiba huo Rais Kikwete alisema kuwa Watanzania wapo pamoja na ndugu zao wa Uganda wakati huu wa majonzi na kusema kuwa yeye binafsi anampa pole Rais Museveni na familia yake na kumtaka awe na moyo wa subira katika kipindi hichi na kumuombea marehemu. 

  Rais Museveni alimshukuru Rais Kikwete kwa kufika katika msiba huo ambapo alisema kuwa Marehemu Mzee Amos atakumbukwa kwa kuthamini elimu ambapo aliwapeleka watoto wake shule na kwa kufanya mabadiliko ambapo alikubali kufuata njia bora za ufugaji wenye tija jambo ambalo ni gumu kwa wazee wengi wenye umri wake.

  Rais Museveni alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwatunza vyema wazazi wao ili waishi muda mrefu na kulaani tabia ya baadhi ya vijana kuishi kwa kutegemea mali za wazazi wao badala ya kuzalisha mali yao wenyewe akiongeza kuwa wazee wana hazina kubwa ya maarifa kutokana na kukumbana na changamoto nyingi katika maisha yao. 

   Marehemu Mzee Amos Kaguta alizaliwa mwaka 1916 katika kijiji cha Kabahambi,Kikoni Mtungamo nchini Uganda. Rais Kikwete na ujumbe wake akiwemo Waziri wa Ulinzi Mh.Shamsi Vuai Nahodha waliondoka kurejea jijini Dar es Salaam baada ya mazishi hayo.

  Rais Dkt. Jakaya Kikwete juu akiweka shada la maua kwenye jeneza na kutoa heshima zake za mwisho. Chini kabisa akiwa na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakiweka udongo kwenye kaburi la Mzee Amos Kaguta  wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura. Kulia ni Mama Janet Museveni

  0 0


  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar akihutubia kwenye Maulid Mjini Kiuyu
  Makamu wa Kwanza akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Wete, Omar Khamis Othman Mjini Kiuyu

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa watu wenye nia mbaya wameamua kuyatumia matukio ya kuuawa na kujeruhiwa kwa viongozi wa kidini ili kuvunja umoja wa Wazanzibari.

  Alisema hivi sasa Wazanzibari ni wamoja na watu hao wenye nia mbaya wanayachukulia matukio hayo kwa kutaka kuwagawa na kuwaletea mtafaruku kwa kuonyesha kuwa kuna tofauti za kidini Zanzibar wakati sio kweli.

  Maalim Seif alisema hayo juzi usiku alipokuwa akihutubia katika hafla ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), Mjini Kiuyu, Wilaya ya Wete, Kaskazini Pemba.

  Alisema inasikitisha kuona wapo baadhi ya viongozi wenye nia chafu dhidi ya Zanzibar wenye tabia ya kutoa kauli za kujenga chuki na fitna miongoni mwa Wazanzibari chini ya kivuli cha matukio hayo.

  “Ni jambo la kusikitisha kuna watu wenye nia chafu dhidi ya Zanzibar, ambao wameamua kuyatumia matukio haya kujenga chuki miongoni mwa Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe,” alionya Maalim Seif.

  Makamu wa Kwanza wa Rais alisema kinachoonekana kuna ajenda imetayarishwa ya kutaka kulazimisha chuki za kidini Zanzibar, licha ya kuwa Zanzibar ina historia ya miaka mingi ya watu kuvumiliana na kuishi kwa pamoja, pamoja na kuwepo watu wa imani tafauti.

  Aliwataka wananchi wote wa Zanzibar hivi sasa wawe macho na ajenda zinazolengwa kuwavuruga na waendelee kuishi kwa mshikamano na umoja kama ambavyo wamekuwa wakiishi.

  Maalim Seif alisema vitendo vya kuuawa na kujeruhiwa viongozi wa kidini Zanzibar ni mambo mageni na kwa miaka mingi Zanzibar imekuwa ni mfano bora wa uvumilivu wa kiitikadi za kidini, licha ya kuwa asilimia 98 ya wananchi wake ni Waislamu.

  Alieleza kwamba wingi wa Waislamu Zanzibar haukuifanya ifunge milango kwa watu wa imani zingine na kwa wakati wote wamekuwa wakiabudu kwa mujibu wa imani zao bila ya bugudha yoyote.

  Makamu wa Kwanza wa Rais alisema Katiba ya Zanzibar imeweka wazi haki ya mtu kuabudu kwa mujibu wa imani yake na uhuru wa mtu kuabudu umelindwa.
  “Ni Sultani wa Zanzibar ambaye alikuwa Muislamu ndiye aliyetoa ardhi kwa Wakiristo kujenga Kanisa. Juzi nilipokwenda kutoa salamu za rambi rambi kwa Baba Askofu Shayo, baada ya kifo cha Padri Mushi, aliweka bayana kuwa lililotokea lisihusihwe na tafauti za kidini,” alisema Maalim Seif  

  Hata hivyo, Maalim Seif alisema inasikitisha kuona wakati Rais Jakaya Kikwete katoa maelekezo uchunguzi wa kina ufanyike na Kamishna wa Polisi Zanzibar ameshaweka wazi kuwa uchunguzi unaendelea, baadhi ya viongozi na magazeti ya Tanzania Bara yanachochea chuki za kidini na kusema kuwa Zanzibar kuna ugaidi.

  Alisema hali hiyo inaonesha kuwa kuna ajenda imetayarishwa kutaka kulazimisha chuki za kidini Zanzibar, kwa sababu huko Tanzania Bara kumetokea matukio mabaya zaidi, lakini hayajahusishwa na ugaidi.

  Alitoa mfano matukio ya kuuawa kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza na kuchinjwa kwa Padri huko Geita, kuwa ni mabaya kabisa, lakini hakuna hata chombo cha habari kimoja kilichohusisha matukio hayo na ugaidi.

  “Nasema Zanzibar hakuna ugaidi, hakuna ugomvi wa kidini. Yanayotokea yametusikitisha sana, ni matokeo ya uhalifu wa kupindukia, linaloweza kufanywa lifanywe kuwanasa wahalifu hawa na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sharia,” alisema Makamu wa Kwanza wa Rais.
  Aliwataka wananchi wote  wa Zanzibar kwa wakati huu kuwa watulivu na wasitawaliwe na jazba na wala wasichokozane, pia wasikubali kuchokozeka.
  Akizungumzia matokeo ya mtihani wa kidato cha nne yaliyotolewa hivi karibuni, Makamu wa wa Kwanza wa Rais alisema ni matokeo mabaya na ya kuliza, kwa sababu hayaoneshi mustakabali mwema kwa watoto wetu na nchi yetu hapo baadaye.

  Alisema ni wakati muafaka Serikali, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, walimu na jamii nzima kujiuliza nini sababu ya matokeo hayo mabaya, na kujiuliza pia nchi inaelekea wapi?

  Maalim Seif alisema sasa si wakati tena wa kutupiana lawama, lazima pande zote zikae zijadili wapi pamekosewa, ili ufumbuzi uweze kupatikana na hali kama hiyo isitokee tena siku zijazo.

  Katika salamu za wananchi wa Kiuyu kwenye Maulid hayo yaliyojumuisha waumini kutoka maeneo mbali mbali ya Pemba, Unguja na Dar es Salaam walisema miongoni mwa malengo yao ni kuona umoja wa wananchi wote unaimarika. 

  0 0


  Hon. Bernard K. Membe (MP), Minster for Foreign Affairs and International Co-operation earlier today held a tête-à-têtemeeting with H.E. Yousuf bin Alawi bin Abdullah, Minister Responsive for Foreign Affairs of the Sultanate of Oman, prior to Official Opening of the Tanzania-Oman Joint Permanent Commission of Cooperation (JPC). The meeting officially commenced today and is expected to end on February 25, 2013 at the Hyatt Regency (Kilimanjaro) Hotel in Dar es Salaam.

  Hon. Membe and H.E. Abdullah share a laughter during their tête-à-tête meeting.

  Mr. John M. Haule, Permanent Secretary of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation, gives his welcoming remarks to Hon. Membe.

  Hon. Membe gives his opening remarks during the Tanzania-Oman Joint Permanent Commission.

  H.E. Abdulla gives his opening remarks during the meeting.
  Hon. Membe opens one of the clusters.
  Hon. Membe opens one of the clusters during the Tanzania/Oman roundable
  Oman delegation that was led by Hon. Membe.
  Hon. Membe walks H.E. Abdullah after opening one of the clusters. All photos by Tagie Daisy Mwakawago of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation.


  0 0


  0 0

  Rais wa TALISS Swimming Club Bi. Najat Saleh Ahmed (mwenye miwani nyeusi) akizungumza na washiriki pamoja na wageni waalikwa wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kuogelea yaliyoshirikisha Club mbalimbali na kwa rika tofauti yaliyodhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors wauzaji wa magari ya kisasa hapa nchini yaliyofanyika katika bwawa la kuogelea la shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST).
  Amesema Mashindano hayo hufanyika kila mwaka na kushirikisha vilabu na watu binafsi wenye ujuzi wa kuogelea unaofikia kiwango cha kushiriki mashindano.
  Aidha Bi. Najat Ahmed ameomba wadau zaidi kujitokeza kudhamini mashindano hayo na kuiomba Serikali ijitokeze na kujenga mabwawa yanayohitajika kwa ajili ya watu kujifunza kuogelea ili kuweza kujiokoa katika ajali za majini.
  Pichani juu na chini washiriki wa club mbalimbali za kuogelea wakipita mbele wazazi na makocha kwa ajili ya utambulisho.
  Official wakijipanga tayari kuanza mashindano hayo yaliyohusisha Clubs mbalimbali kutoka sehemu tofauti.
  Pichani juu na chini ni washiriki wajitosa kwenye bwawa hilo kuchuana katika mashindano ya kuogelea yaliyoratibiwa na TALISS Swim Club na kudhaminiwa na kampuni ya CFAO Motors ya jijini Dar.
  Picha juu na chini Sehemu ya watazamaji wakishuhudia mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST).
  Picha juu na chini Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akiwavalisha medali washindi wa mashindano hayo katika kategori mbalimbali. CFAO Motors imeamua kudhamini mashindano hayo baada ya kuona umuhimu wa vijana kujua kuogelea ili kuweza kujiokoa katika majanga yanayohusiha ajali za majini zinazopelekea vifo vya watoto ikiwa ndio lengo la TALISS.
  Rais wa TALISS Swimming Club Bi. Najat Saleh Ahmed akikabidhi medali kwa mmoja wa washindi wa mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors.
  Picha juu na chini ni Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya CFAO Motors Wayne Mcintosh ambaye pia alikuwa MC katika mashindano hayo akikabidhi vikombe kwa washindi wa jumla walioshiriki TALISS Swimming Championships 2013.
  Umati wa watu wakiwemo wazazi, ndugu na jamaa pamoja makocha waliohudhuria kushuhudia mashindano ya kuogelea ya TALISS yaliyohusisha vilabu kutoka sehemu mbalimbali.
  Baadhi ya wageni waliohudhuria kutazama mashindano ya kuogelea katika shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) wakikagua gari mpya aina ya Nissan Y62 inayosambazwa na Kampuni ya CFAO Motors.

  0 0

  Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Mhe. Mohamed Chande Othman akisaini kitabu cha wageni  alipotembelea ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mwanza asubuhi hii. Kushoto  ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Tume, Mhe. Fakih Jundu. Mhe. Jaji Mkuu pamoja na ujumbe alioambatana nao wapo mkoani humo kwa ajili ya kuongea na wajumbe wa Kamati ya Maadili ya Mkoa huo lengo likiwa ni Kujenga mahusiano mazuri ya kiutendaji na Kamati Hilo. 
    Katibu wa Tume ya Utumishi  wa Mahakama, Bw. Hussein Kattanga akiongea na wajumbe wa Kamati ya Maadili ya Mkoa wa Mwanza katika mkutano unaofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu mkoani Mwanza hivi sasa. Mbali na kuwa Katibu wa Tume, Bw. Kattanga pia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.

  Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Maadili ya mkoa wa Mwanza wakiwa Katika mkutano na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Picha na mdau Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania

  0 0
 • 02/24/13--22:59: APPRECIATION

 • The family of late Moses Tito Kachima would like to express their sincere thanks to TOM MBOYA LABOUR COLLEGE, (KENYA), PPF, TUCTA, FIBUCA, COTWU, CHODAWU, TUGHE, CWT, RAAWU, MINISTRY OF TRANSPORT, NEIGHBOURS WITHOUT BORDERS, NMB, DONALDSON & WOOD ADVOCATES, OYSTERBAY ALLIANCE and JUMUIYA YA MTAKATIFU PETRO PAROKIA YA IMMACULATE – UPANGA; together with family relatives and friends for their kindness and support shown during the funeral of the late Moses Tito Kachima.


  He appears gone, but his spirit still lives on amongst many of us today, tomorrow and beyond.


older | 1 | .... | 52 | 53 | (Page 54) | 55 | 56 | .... | 3348 | newer