Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 521 | 522 | (Page 523) | 524 | 525 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Courtesy of Citizen TV

  0 0


  0 0


  0 0

  Obasanjo
  Former Presidents Thabo Mbeki from South Africa, Olusegun Obasanjo of Nigeria and Festus Mogae of Botswana are set to arrive in Dar today to attend the African Leadership Forum to be held on July 31st, 2014.
  The forum, which has been convened by H.E. Benjamin William Mkapa, former President of the United Republic of Tanzania and coordinated by UONGOZI Institute will be kick started with a plenary session with H.E. Thabo Mbeki as the keynote speaker. 
  Mbeki
  Mogae
  The plenary will also feature a panel discussion including Mr. Carlos Lopes, Executive Secretary of the United Nations Economic Commission for Africa, Ms. Wendy Luhabe, founder of The Women Private Equity Fund of South Africa, and Mr. Omari Issa, CEO of the Presidential Delivery Bureau in Tanzania. 
  According to a statement issued this week by UONGOZI Institute, the Forum, which will gather more than 150 participants from Tanzania and across Africa will discuss the challenges of meeting Africa’s transformation.
  Mkapa

  “The forum will provide a platform to reflect on the journey thus far, take stock of the challenges and opportunities and forecast prospects for Africa’s future,” said the statement.
  The African Leadership Forum will bring together selected number of key influential leaders and thinkers across the continent, including former heads of state or government, as well as leaders from the business sector, government, civil society and academia.


  0 0


  0 0

  Hapa ni barabara ya Morocco (sasa Kawawa Road) mitaa ya Kimnondoni. Hivi sasa barabara hii iko katika ujenzi mpya kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka. Na hiyo ngoma unayosikia ni ya Kundi la Sisi Tambala

  0 0

  MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili, Rose Muhando amelalamika kuwa albamu yake ya "Kamata Pindo la Yesu" albamu anayotarajia kuizindua Jumapili wiki hii imeingizwa mtaani na wezi wa kazi za wasanii, hivyo kuonya wananchi wawe makini kwani albamu yake halisi itatoka Jumapili.
  Taaifa kwa vyombo vya habari aliyoitoa Muhando jana, ilieleza kuwa albamu yake halisi bado haijaingia mtaani na kwamba hiyo wanayoiona wananchi sasa ni bandia na mtu atakayewauzia wamripoti polisi.
  “Albamu ya Kamata Pindo la Yesu itaanza kuingia mtaani baada ya uzinduzi wangu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jumapili wiki hii. Albamu yangu ina nembo ya TRA (Mamlaka ya Kodi ya Mapato nchini).
  “Hizi CD zinazouzwa hivi sasa si zangu, hao ni matapeli na nawaomba wananchi tushirikiane kudhibiti wizi. 
  Hao ni maharamia wa kazi za wasanii wanataka kunyonyajasho langu, naomba sana wananchi mnisaidie.
  “Nasisitiza albamu yangu sijaiachia sokoni bado mpaka uzinduzi ukamilike, Watanzania wenzangu na mashabiki wangu kote duniani mnielewe na naomba tusaidiane katika hili maana CD feki zimezagaa,” alisema Muhando na kuongez akuwa tayari ameripoti taarifa hiyo kwa vyombo vya dola.
  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions inayoratibu uzinduzi huo, Alex msama naye katika taarifa hiyo ya pamoja alionya wote watakaobanika kuwa CD za albamu ya Rose Muhando watakumbana na mkono wa sheria.
  “Inasikitisha sana kuona baadhi ya watu wanataka kutumia jasho la wengine kujinufaisha. Watanzania kuweni macho, msubiri albamu yenyewe ya Rose Muhando Jumapili pale ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam,” alisema Msama.
  Albamu hiyo ya Muhando itakayozinduliwa Jumapili ina nyimbo za Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook.
  Hivi sasa Rose anatamba na albamu yake ya Utamu wa Yesu, ambapo pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi), Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu Anacheka na Wololo.

  0 0

  MTAWA KAPALATA MWAIJUMBA, MSHIRIKI WA MASHINDANO YA VIPAJI VYA KUIGIZA Tanzania Movie Talents (TMT) KUTOKA NYANDA ZA JUU KUSINI, MBEYA, ANAOMBA KURA YAKO
  NAMBA YAKE YA USHIRIKI NI 04.

  0 0

   alozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga, aungana na Mabalozi Wadogo wenzie wanaoziwakilisha nchi zao Dubai kwenda kukutana na kutoa salaam za Eid kwa Wafalme wa Dubai, Sharjah, Ajman, Fujairah, Umm Ul Quwain na Ras Al Kheimah.
   Wafalme wa Dubai, Sharjah, Ajman, Fujairah, Umm Ul Quwain na Ras Al Kheimah (walioketi)
   Wafalme wa Dubai, Sharjah, Ajman, Fujairah, Umm Ul Quwain na Ras Al Kheimah wakifungua kinywa na mabalozi wadogo
   Sehemu ya mabalozi wadogo wakiwa kwenye hafla hiyo
  Mhe. Omar Mjenga akiwa na Mhe. Jose De Francio Balozi Mdogo wa Msumbiji, Dubai.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis, makabidhiano hayo yamefanyika uwanja wa ndege mkongwe Kiembesamaki leo.
  Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Getrudi Mpaka akitoa salam za Mkoa huo wakati wa kuukabizi Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Mjini Magharibi leo july 30.
  Vijana wa Chipkizi wakiimba nyimbo ya Mwenge.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala Bora Dkt. Mwinyihaji Makame akishika mwenge wa Uhuru ulipowasili Zanzibar.
  Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Hamza Ibrahim kutoka Mjini Magharibi na maaskari wakiukimbiza Mwenge.
  Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hasan Mussa Takrima kwa ajili ya kuukimbiza katika Wilaya yake.
  Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Hasan Mussa Takrima akikimbiza Mwenge wa Uhuru mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini tayari kuanza ziara yake.(Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar).

  0 0

  Jana tarehe 29 Julai, 2014 nimefanya mahojiano katika kipindi cha PowerBreakFast kinachorushwa na Clouds FM. Baadhi ya vyombo vya habari vimeandika mahojiano yale. Napenda nitoe ufafanuzi kidogo kuhusu msimamo wangu kuhusu mchakato wa Katiba.

  Kwanza, Mimi sijawahi kuwa UKAWA wala kundi lolote lile katika Bunge Maalumu la Katiba isipokuwa kundi linalotaka maridhiano. Msimamo wangu kuhusu Muungano ni Serikali Tatu Zilizoboreshwa (S3z) ili kuwa na Muungano imara usio tegemezi wala egemezi kwa Washirika wake.

  Pili, Mimi niliunga mkono ‘protest’ ya baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupinga lugha za matusi na lugha za kibaguzi zilizokuwa zinaendelea ndani ya mkutano ule. Vilevile niliunga mkono kwamba Rasimu inayopaswa kujadiliwa ni Rasimu iliyotokana na Tume ya Marekebisho ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba. Nasisitiza umuhimu wa kupata Katiba BORA itakayoimarisha DOLA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Tatu, kwa hali ya sasa kuna mkwamo katika kupatikana kwa Katiba Bora. Mkwamo unaotokana na kutokuwepo kwa nia ya dhati ya kupata maridhiano ya pande zinazopingana. UKAWA hawataki mazungumzo na Viongozi wa Bunge la Katiba badala ya kujenga maridhiano kila siku wanawabeza UKAWA jambo ambalo kamwe haliwezi kujenga mwafaka. Ushauri wangu ni kuahirisha mchakato mzima wa kuandika Katiba mpaka mwaka 2016 baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Katiba ya sasa ifanyiwe marekebisho machache kama ifuatavyo;

  i) Tume ya Uchaguzi ili iwe huru na ionekane kuwa huru, ikiwemo kuwaondoa watumishi wa Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji katika kusimamia uchaguzi

  ii) Kuruhusu mgombea binafsi

  iii) Kuondoa Mafuta na Gesi kama Jambo la Muungano ili Zanzibar ianze mara moja kusimamia kwa uhuru utafutaji wa Mafuta katika vitalu vilivyopo upande huo wa Muungano

  Mkutano wa Bunge Maalumu utakaofanyika bila kuwepo kwa maridhiano utakuwa hauna maana yeyote na itakuwa ni sawa na kupoteza muda na fedha za walipa kodi ambazo zingeweza kununua madawa vijijini. Mimi binafsi sitahudhuria mkutano wa Bunge Maalumu kama makundi hasimu hayatakuwa yamefikia maridhiano.

  Kabwe Zitto, 
  MB/MBMK

  0 0

  Wana DMV BALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIANCHI MAREKANI, MHE. LIBERATA MULAMULA, ANAWAALIKA WATANZANIA KUTOKA KWENYE MAENEO YA DMV PAMOJA NA MAJIMBO MENGINE HAPA MAREKANI, KUHUDHURIA MKUTANO MAALUM WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DR. JAKAYA KIKWETE, UTAKAOFANYIKA TAREHE 2 AGOSTI, 2014 KATIKA HOTELI YA MARRIOT, 1221 22ND ST NW,WASHINGTON DC 20037, KUANZIA SAA 12.00 KAMILI JIONI.

  KWA WANA DMV WATAKAOITIKIA MWALIKO HUU NA KUTAKA KUHUDHURI, WANAOMBWA NA KUHIMIZWA KUJIANDIKISHA MAJINA Kupitia.
   Kama Kuna Maswali Tunaomba Uwasiliane na :
   Iddi Sandaly - President 

  301-613-5165

                                                          Raymond Abraham - Vice President

  301-793-4467  Amos Peter Cherehani - Secretary 
  240-645-2131

  Genes Malasy - Teasury
  301-367-8151 

  0 0  0 0


  0 0

  image
  The current conflict between Israelis and Palestinians has once again brought to the forefront the suffering of the Palestinian people. It has reignited the debate on collective punishment they are made to endure as well as the unequal application of firepower by Israel.  
  After close to 20 days of Israeli air raids followed by a ground invasion of Gaza, the casualties from the conflict have been lopsided, with 80% to 90% of the casualties on the Palestinian side being civilians. 
  The death toll has climbed to over 1,000 Palestinians killed and 5,500 wounded.  On the Israeli side, 42 soldiers and 3 civilians have lost their lives in the conflict. It begs the question: what is the value of a Palestinian life?

  0 0  0 0

  Wachezaji wa timu zote mbili Miembeni Fc na Bilele Fc  wakisalimiana kabla ya Mtanange kuanza jioni hii katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Kikosi cha Timu ya Miembeni Fc
  Kikosi cha Timu ya Bilele Fc

  Mabingwa watetezi wa kombe la KAGASHEKI, Bilele Fc, wamefungwa leo na Timu ya Miembeni Fc bao 2-1 kwenye mtanange uliopigwa dakika 120, dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa  kutoshana nguvu kwa bao 1-1 katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Timu ya Bilele Fc ndio walianza kupata bao la mkwaju wa penati katika dakika ya 62 kupitia kwa Fikiri David na Miembeni Fc wakasawazisha bao hilo ndani ya dakika moja na Rashid Mandawa kupita katika dakika 63 baada ya mpira kuanza kati na kufanya shambulizi.
  Dakika 90 zilimalizika na kwenda katika dakika za ziada na katika dakika ya 105 Miembeni walifanikiwa kupata bao la ushindi na mtanange kumalizika. Mtanange huu pia haukuweza kumalizika vyema kwani wachezaji wawili wa Miembeni Fc wameoneshwa kadi nyekundu 2 na kucheza pungufu katika dakika za mwishoni kwa kufanya makosa tofauti tofauti.
  Ushindi huu unawapeleka  Miembeni Fc  hatua ya Fainali wakisubiri mshindi wa kesho kati ya Kitendaguro Fc na Kagondo Fc.
  Bilele Fc wao wanasubiri atakayefungwa kesho kati ya Kitendaguro na Kagondo ili waje wakutane kutafuta mshindi wa tatu.Fikiri David wa timu ya Bilele Fc akimfunga kipawa wa Miembeni Samwel Geofrey kwa Mkwaju wa penati katika kipindi cha pili dakika ya 62.

  0 0


  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 
  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete 

older | 1 | .... | 521 | 522 | (Page 523) | 524 | 525 | .... | 3270 | newer