Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 522 | 523 | (Page 524) | 525 | 526 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0  0 0
 • 07/30/14--20:32: ushauri wa bure


 • 0 0

   Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda  akiwa katika picha na Bw. Anic Kashasha, Mwenyekiti Mtendaji wa TACIN alipomtembelea  nyumbani kwake Oyserbay, Dar es Salaam, kumpa taarifa ya maendeleo ya maandalizi ya Mtwara Festival, itakayofanyika tarehe 16 - 17 Agosti, 2014 katika viwanja vya Chuo Cha Ualimu Mtwara(TTC). 
  Mh. Mizengo Pinda, anatarajiwa kuwa  Mgeni Rasmi wa Mtwara Festival, ambao ni mpango mkakati wa mawasiliano wa kuhamasisha wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi, kizitambua fursa shirikishi zinazosisimuliwa na uchumi wa gesi asilia. 
  Kauli mbiu ya Mtwara Festival ni "FURSA ZIMEFUNGUKA, TUZITAMBUE, TUJIANDAE, TUZICHANGAMKIE". Akizungumza mara baada ya kukutana na Waziri Mkuu, Bw. Kashasha alisema mpango huo wa elimu kwa umma, utachangia kwa kiasi kikubwa kutengeneza ajira na kipato kwa wananchi wa mikoa hiyo na hivyo kubadilisha hali za maisha ya wananchi hao.

  0 0

  IMG-20140727-WA0011
  Miss Tanzania USA 2014, Joy Kalemera katika pozi kabla ya mahojiano na Mtangazaji wa kipindi cha "Mimi na Tanzania" Hoyce Temu nchin Marekani.

  Mpigie Kura Miss Tanzania USA, Joy Kalemera anayeshiriki kinyang'ayiro cha kumtafuta Miss Africa USA. Mtangazaji wa Mimi Na Tanzania Hoyce Temu ambaye pia ni Miss Tanzania 1999 yupo nchini Marekani na amefanya mahojiano na mrembo huyo.
  Usikose kuangalia marudio ya mahojiano hayo kwenye kipindi cha "Mimi na Tanzania" Jumamosi ya tarehe 2 August ,2014 Saa saba mchana katika kituo cha Televisheni cha Channel Ten.
  IMG-20140727-WA0013
  Miss Tanzania 1999 ambaye pia ni Mtangazaji wa kipindi cha "Mimi na Tanzania" Hoyce Temu akipata ukodak na Miss Tanzania USA, Joy Kelemera baada ya mahojiano maalum nchini Marekani.
  Joy Kelemera
  Namna ya kushiriki kumpigia kura moja kwa moja kwenye profile yake Bonyeza hapa utakuwa umeingia kwenye profile ya Joy Kalemera na bonyeza kitufe chenye alama ya mkono (sehemu iliyozungushiwa duara na wino mweusi) na moja kwa moja utakuwa umempigia kura Mtanzania mwenzetu anayeiwakilisha vyema nchini yetu kwenye kinyan'ganyito hicho.
  NOTE: Unaweza kupiga kura mara nyingi uwezavyo kila baada ya dakika mbili kwa kubofya sehemu ile ile.
  Let us all wish her all the best! Ushindi wake ni wa Nchi! Piga Kura Sasa!
  IMG-20140727-WA0014
  Pichani ni Hoyce Temu, Joy Kalemera na camera crew/IskaJojo studios (katikati) aliyefanikisha kukerokodi maojiano hayo.
  IMG-20140727-WA0015
  Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu na Miss Tanzania USA 2014, Joy Kalemera katika pozi za madaha.

  0 0

   Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova akiongea na Waandishi wa Habari Huku akionyesha baada ya Silaha Kituo cha Polisi cha Kati Dar es salaam.
  --
  MAJAMBAZI 10 wanaounda mtandao hatari wa uhalifu nchini, wametiwa mbaroni wakati wa msako mkali uliofanikisha pia kukamatwa kwa silaha mbalimbali.

  Silaha hizo ni bunduki tisa zikiwemo SMG tatu, bastola mbili, short gun nne na risasi 15 zilikamatwa.

  Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, aliyasema hayo ofisini kwake kwenye mkutano na waandishi wa habari.

  Majambazi hao wamekamatwa katika msako mkali unaoendelea jijini Dar es Salaam katika harakati za kuhakikisha kwamba maisha na mali za wakazi wa Dar es Salaam vinalindwa kikamilifu.

  Katika msako huo watuhumiwa walisachiwa katika miili, makazi, na maficho yao na wakakamatwa na jumla ya silaha 9 kama ifuatavyo:-
  1. SMG NO. 13975 ikiwa na risasi 11 na magazine 2
  2. SMG 1 haikuwa na magazine na namba hazisomeki.
  3. BASTOLA 1 aina ya LUGER yenye namba 5533K
  4. BASTOLA 1 aina ya BROWNING yenye namba TZACR83494 S/No.7670 Na risasi 6 ndani ya magazine.
  5. S/GUN PUMP ACTION na risasi 55
  6. MARCK IV iliyokatwa mtutu na kitako yenye magazine 1 na risasi 4
  7. BASTOLA 1 yenye namba A963858 browning ambayo ina risasi 1
  8. SMG 1 ambayo iko kwa mtaalam wa uchunguzi wa silaha (Balistic)
  9. SHOT GUN TZ CAR 86192 ilitelekezwa baada ya msako

  Majina ya watuhumiwa ni ifuatavyo:-
  1. MAULIDI S/O SEIF MBWATE miaka 23, mfanyabishara, mkazi wa Mbagala Charambe.
  2. FOIBE D/O YOHANES VICENT miaka 30, hana kazi, mkazi wa Mbagara Kibondemaji.
  3. VICENT S/O OGOLA KADOGOO miaka 30, mkazi wa Mbagara Kibondemaji
  4. SAID S/O FADHIL MLISI – miaka 29, dereva wa Bodaboda, Mkazi wa Gongolamboto
  5. HEMEDI S/O AWADHI ZAGA miaka 22, dereva wa Bodaboda, mkazi wa Gongolamboto
  6. MOHAMED S/O IBRAHIM SAID miaka 31, Fundi welder mkazi wa Kigogo.
  7. LUCY MWAFONGO. Miaka 41, mama lishe mkazi wa Vingunguti Ukonga
  8. RAJABU S/O BAHATI RAMADHANI, miaka 22, Mkazi wa Kariakoo
  9. DEUS JOSIA CHILALA miaka 30, Mgonga Kokoto Kunduchi , mkazi wa Yombo Kilakala.
  10. MARIETHA D/O MUSA miaka 18, mkazi wa Yombo Kilakala
  Mwanamke pekee katika kundi hilo anayejulikana kwa jina la FOIBE D/O YOHANES VICENT ameshiriki katika matukio ya uporaji wa kutumia silaha, mauaji, n.k. na yeye mwenyewe alikuwa akitumia bunduki aina ya SMG.
  Katika baadhi ya matukio wananchi walioshuhudia matukio haya wamekuwa wakitoa taarifa kwamba alikuwepo mwanamke aliyekuwa akifyatua risasi na hatimaye polisi walifanikiwa kumkamata akiwa na wenzake katika kundi hilo.
  Licha ya kukamatwa kwa mtandao huu hatari Jeshi la Polisi linaendelea na misako ya mitandao mingine ya ujambazi kwa madhumuni yaliyotajwa hapo juu.
  Hivyo tunawashukuru wananchi kwa namna walivyoendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutokomeza uhalifu.
  Majambazi hao watafikishwa mahakamani baada ya Mwanasheria wa Serikali kutafuta majalada yao ya kesi mbali mbali.
  S.H. KOVA
  KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM

  DAR ES SALAAM

  0 0


  Meneja rasilimali watu wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL Bw. Aidan Kaune (mwenye suti ya kijivu) akijumuika pamoja na baadhi ya watoto 500 mayatima kusherehekea sikukuu ya Eid wakati wa karamu ya chakula iliyoandaliwa na taasisi ya Al-Madina na kufadhiliwa na IPTL. Kulia ni meneja maswala ya kampuni ya IPTL (Company Affairs Manager) Bw. Kulwinder Singh Jheeta na wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa taasisi ya Al-Madinah Sheikh Ally Mubarak.
   Meneja rasilimali watu wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL Bw. Aidan Kaune (kulia) na Meneja maswakla ya kampuni wa IPTL (Company Affairs Manager) Bw. Kulwinder Singh Jheeta (katikati) wakikabidhi sehemu ya bidhaa zilizonunuliwa wakati wa karamu ya chakula kwa watoto yatima wapatao 500 kutoka vituo mbali mbali Dar es Salaam na Wilaya ya Kondoa, kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr. Kushoto ni Mkurugenzi wa taasisi ya Al-Madinah Sheikh Ally Mubarak, ambao waliandaa karamu hiyo baada ya kufadhiliwa na IPTL.
   Meneja rasilimali watu wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL Bw. Aidan Kaune (mwenye suti ya kijivu) akijumuika pamoja na baadhi ya watoto 500 mayatima kusherehekea sikukuu ya Eid wakati wa karamu ya chakula iliyoandaliwa na taasisi ya Al-Madina na kufadhiliwa na IPTL. Kulia ni meneja maswala ya kampuni ya IPTL (Company Affairs Manager) Bw. Kulwinder Singh Jheeta.
  Meneja maswala ya kampuni ya kufua umeme ya IPTL (Company Affairs Manager) Bw. Kulwinder Singh Jheeta akijumuika pamoja na baadhi ya watoto 500 mayatima kutoka vituo mbalimbali Dar es Salaam na Wilaya ya Kondoa kusherehekea sikukuu ya Eid wakati wa karamu ya chakula iliyoandaliwa na taasisi ya Al-Madina na kufadhiliwa na IPTL.


  0 0

     Mkurugenzi Mtendaji wa Shirila la Usafiri (UDA) Bw. Simon Bulenganija (kushoto) akisisitiza jambo kwa Paroko Msaidizi wa Kigango cha Kanisa la Mavurunza, Padri Xavery Kassase kabla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 15 kwa Kigango cha Kanisa la Mtakatifu Rita kusaidia mradi wa ujenzi wa nyumba ya mapadri wakati wa harambee iliyofanyika kanisani hapo hivi karibuni.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Shirila la Usafiri (UDA) Bw. Simon Bulenganija (kushoto) akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa Paroko Msaidizi wa Kigango cha kanisa la Mavurunza, Padri Xavery Kassase (kulia) kusaidia mradi wa ujenzi wa nyumba ya mapadri wakati wa harambee iliyofanyika katika Kigango cha Kanisa la Mtakatifu Rita hivi karibuni.
  Paroko Msaidizi wa Kigango cha Kanisa la Mavurunza, Padri Xavery Kassase(kulia) akionyesha hundi ya shilingi milioni 15 zilizotolewa na  Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) kwa kigango cha Kanisa la Mtakatifu Rita jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Mchango huo wa kampuni ulitolewa kusaidia ujenzi wa nyumba ya mapadri kanisani hapo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirila la Usafiri (UDA) Bw. Simon Bulenganija.

  MAENDELEO ya kijamii na kiuchumi yataweza kupatikana endapo tu kila mtu ataweza kutoa mchango wake kuwasaidia wale wanaohitaji msaada ili kubadilisha maisha yao na kuwa wachangiaji wakubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa. Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), Bw. Simon Bulenganija wakati wa harambee ya kusaidia ujenzi wa nyumba ya mapadri katika Kigango cha kanisa la Mtakatifu Rita lililopo Kimara jijini Dar es Salaam, ambapo UDA ilichangia shilingi milioni 15.

  “Watanzania wasisubiri mpaka makampuni makubwa yajitokeze na kutusaidia kubadilisha hali zetu za kiuchumi na mfumo wetu wa maisha. Mabadiliko yataweza kufikiwa tu endapo kila mmoja wetu ataweza kuchangia kwa nafasi yake kikamilifu. Makampuni yote makubwa na madogo na watu binafsi wenye uwezo wa kusaidia, wawashike mkono wale wanaohitaji msaada ili tuweze kuendelea pamoja,” alisema. Bw. Simon Bulenganija alisema kuwa kampuni yake imekuwa ikijihusisha na shughuli mbali mbali za kijamii ikiwa ni jitihada madhubuti zinazolenga katika upatikanaji wa maendeleo miongoni mwa watanzania wote.

  Alisema kuwa shilingi milioni 15 zilizotolewa na UDA zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupiga jeki maendeleo ya kanisa hilo hususani katika ujenzi wa nyumba ya mapadri na baadae kuendelea na mradi wa ujenzi wa kanisa jipya.“Japokuwa bado kampuni yetu ni kampuni changa ya kitanzania, tumeunda programu yetu ya shughuli za kijamii katika namna ya kwamba shughuli tunazojihusisha nazo, zitasaidia katika kutekeleza ajenda yetu yenye kaulimbiu “ukuaji wa kampuni yetu uwe sambamba na ukuaji wa kiuchumi wa jamii yetu”. Hii pia ni njia pekee ya kurudisha sehemu ya pato letu kwa jamii,” alisema Bw. Bulenganija.

  Naye, Bw. Frederick Msumali, Mwenyekiti wa Kigango cha Mtakatifu Rita, aliipongeza kampuni hiyo kwa mchango wake na ushiriki wa Mkurugenzi wa UDA wakati wa shughuli hiyo ya harambee ambayo iliwezesha kanisa hilo kukusanya zaidi ya shilingi milioni 60 zitakazotumika katika mradi huo.


  “Tungependa kwa kiasi kikubwa kutoa shukrani zetu kwa mchango uliotolewa na UDA.  Msaada huu kwa kiasi kikubwa utasaidia kupiga jeki mradi wetu wa ujenzi wa nyumba ya mapadri na baadae kuendelea na ujenzi wa kanisa jipya utakaofanyika karibu na kanisa hili la sasa. “Lakini pia, tunaishukuru UDA kama kampuni na Bw. Bulenganija mwenyewe kwa kuwa mgeni wetu rasmi. Mfano huu unahitaji kuigwa na makampuni mengine nchini,” alisema Bw. Msumali.

  0 0

  Maadhimisho ya siku ya Mwanamke wa Afrika yaliyo ratibiwa na Women in Law and Development in Africa-WiLDAF yafana jijini Dar es salaam. Ni siku ya Mwanamke wa Afrika na husheherekewa kila mwaka tarehe 31 July toka ilipotamkwa rasmi mwaka 1963 July 31 na wanawake wa Pan African waliokutana Dar es Salaam kwa wakati huo.Mada mbalimbali zilitolewa ikiwemo mchakato mzima wa katiba mpya na changamoto zake. Kulikuwa na watoa mada mbalimbali wakiwemo Dr Khoti Kamanga na Mh. Getrude Mongela.  0 0

  Mbunge wa Ilala Mh. Mussa Zungu ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) akikata utepe kuashiria uzindunzi wa maadhimisho ya chuo hicho kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wakiangalia moja ya picha ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopigwa wakati akifungua Chuo hicho Januari, 1965. Kutoka kushoto ni Mkuu wa chuo hicho Prof. Emanuel Mjema, Mh. Musa Zungu (Mb) jimbo la Ilala,Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda,Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho Prof. Mathew Luhanga na Prof.Eliuta Mwageni Makamu Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha.
  Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Mbunge wa Ilala Mh. Mussa Zungu na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (katikati). Nyuma ni bango lenye picha ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyopigwa wakati akifungua Chuo hicho mwaka 1965.
  Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda kwa niaba ya wanafunzi waliosoma katika chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam akizungumza na wadau na wanajumuiya wa Chuo hicho wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho jijini Dar es salaam.


  0 0

  Mkurugenzi wa 100.5 Times Fm, Rehure Nyaulawa akizungumza na watoto wanaolelewa kwenye Shule ya msingi Wamato (hawapi pichani) wakati walipowatembelea.
  100.5 Times Fm kwa kushirikiana na makampuni ya MeTL, Shamo, Simba Trailer, Hugo Domingo, M2 Advertising, Ifatar, kampuni ya vipodozi ya Darling walijitolea na kupata chakula cha jioni kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu wanaosomeshwa katika shule ya msingi Wamato kwa udhamini wa taasisi ya Help2Kids.

  Tukio hilo lililofanyika wiki iliyopita liliambatana na michezo mbalimbali na hotuba zilizolenga katika mipango ya kuisaidia zaidi shule hiyo ya msingi ya Wamato iliyoko eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam ili kuhakikisha watoto hao wanapata elimu bora zaidi kwa maisha ya baadae.

  Akiongea na 100.5 Times Fm, mwanzilishi wa kituo hicho Bi. Basila Chuwa ameishukuru taasisi ya Help2Kids kwa kuendelea kuisaidia shule hiyo kwa kila hali pamoja na makampuni yote yaliyojitokeza kuhakikisha yanakuwa karibu na kituo hicho kwa lengo la kusaidia huku akitoa wito kwa makampuni mengi zaidi kuiga mfano huo kwa kuwa serikali imelemewa.

  Mwanzilishi wa Kituo cha MAWATO,Bi. Basila Chuwa
  “Nilikuwa na shirika la wa Canada lilikuwa linaitwa Canadian Christian Child Fund, ile ilinisaidia kwa miaka zaidi ya kumi. Walikuwa wanafanya vitu vingi sana. Walijenga hata majengo haya, walikuwa wanasaidia nguo, walikuwa wanawaangalia hata nyumbani wazazi. Hata sabuni ya kufulia walikuwa wanawapatia na chakula. Lakini sasa hivi...serikali haiwezi kutusaidia kila kitu (serikali yenyewe imelemewa).”

  Ameeleza kuwa nia yake ni kuanzia ‘daycare’ sehemu ambayo watoto watakuwa wanaachwa kwa siku nzima wakisoma na kuangaliwa huku wazazi wao wakiwa katika mihangaiko kisha wanawapitia jioni wakielekea majumnbani. Lakini upungufu wa majengo ni moja kati ya kikwazo kikubwa.

  Amesema mpango huo wa ‘daycare’ ni bora zaidi ya kuwa na kituo cha kuwatunza moja kwa moja watoto kwa kuwa kufanya hivyo kutaendelea kuwaweka karibu na malezi ya familia na malezi ya kituo pia.
  Mkurugenzi wa 100.5 Times Fm, Rehure Nyaulawa akizungumza jambo na baadhi ya watoto hao.

  Naye Mkurugenzi wa 100.5 Times Fm, Rehure Nyaulawa amesema Times Fm inaendelea kutoa misaada katika jamii na inakuwa sio tu sehemu ya jamii bali sehemu ya msaada pia kadri inavyowezekana na kwamba kwa kipindi hiki wameamua kusaidia pia katika upande wa elimu kwa watoto ili kutengeneza viongozi bora wa baadae.

  “Times Fm ni radio ambayo inapenda kujishughulisha na shughuli za kijamii katika kusaidia jamii na kama tunavyosema kwamba tusisubiri wafadhili, serikali ama taasisi ije kutusaidia. Kwa sisi wenyewe tunaona kile kidogo tulichonacho tunajaribu kukaa na wadau tunatengeneza mipango tunakuja tunafanya vitu kama hivi vya kusaidia watoto au communities mbalimbali.” Amesema Rehule Nyaulawa.

  Amesema shirika la M2 Advertising liliguswa na shughuli za awali za kijamii zilizokuwa zikifanywa na Times Fm awali kama kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), kupaka rangi na kutoa vifaa kwa kituo cha polisi cha Kawe, hivyo shirika hilo kaamua kuungana na mazoezi hayo ya kimaendelea na kuyavuta makampuni mengine pia.

  Bwana Rehure ameyashukuru makampunii yote yaliyoshirikiana na 100.5 Times Fm na kuendelea kutoa wito kwa makampuni mengi zaidi kuungana na kituo hicho cha radio.

  “Hili tulilifanya kama lilivyo na nafikiri ni njia nzuri ya kuanzia au kuwafuata na kuwaambia ‘jamani tulifanya moja basi twendeni kwenye lingine na lingine’, na pia mashirika mengine ambayo yanahisi kwamba yanaweza kufanya basi nayakaribisha.”

  Kupitia mtandao wa Twitter, shirika la Help2Kids lilitoa shukurani zake kwa makampuni yote yaliyosaidia katika kukamilisha tukio hilo.

  “help2kids would like 2 say thank u 2 @M2Advertising & @TimesFMTZ 4 such a wonderful event yesterday. U truly warmed a lot of child's hearts” Walitweet Help2Kids.

  0 0

  Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye (katikati) na mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka, wakiagana na viongozi wa dini wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati na Usharika wa Purana Mirerani, baada ya kuzindua DVD ya kwaya ya Sauti ya mtu aliaye nyikani ambapo sh18 milioni zilipatikana.
  Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye (katikati) akinong'onezwa jambo na Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka, kwenye Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Usharika wa Purana Mirerani, katika uzinduzi wa DVD ya Kwaya ya Sauti ya mtu aliaye nyikani.
  Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye (kushoto) na mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka, wakiagana na viongozi wa dini wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati na Usharika wa Purana Mirerani, baada ya kuzindua DVD ya kwaya ya Sauti ya mtu aliaye nyikani ambapo sh18 milioni zilipatikana.

  0 0

  Mchekeshaji Mahiri kutoka nchini Uganda,Anne Kansiime (wa pili kulia) akifafanua jambo mbele ya Wanahabari kuhusiana na burudani kubwa ya uchekeshaji atakayoionyesha kwa mashabiki wake hapo kesho Agosti 2,2014  katika ukumbi wa Golden Tulip,jijini Dar,Kulia kwake ni mchekeshaji mwingine kutoka nchini Kenya,Fred Omondi.
   Mmoja wa wachekeshaji mahiri kutoka nchini Tanzania,atambulikae kwa jina la kisanii Mc Pili Pili akielezea jambo kwenye mkutano wa Wanahabari uliofanyika mapema leo jijini Dar,wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis,ambao ndio waandaaji wa Onesho hilo la vichekesho.
   Baadhi ya Wanahabari walioshiriki mkutano huo wa wasanii wa vichekesho uliofanyika mapema leo jijini Dar

  ========  ======  ====== 

  Mchekeshaji Anne Kansiime anatarajiwa kutoa burudani kubwa siku ya Jumamosi kwa mashabiki wake katika ukumbi wa Golden Tulip.


  Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sports Lounge, mkali huyo wa kuchekesha na sanaa za majukwaani amesema mashabiki wake watarajie mambo makubwa hapo Jumamosi.


  ‘Hii ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania, hivyo mashabiki wangu watarajie burudani ambayo itaacha mbavu zao hoi, lakini pia watapata nafasi ya kujifunza vitu vingi kupitia vichekesho vyangu’ alisema Anne.


  Kwa upande wake, mchekeshaji mwingine kutoka Kenya atayetoa burudani, Fred Omondi, amesema watanzania watarajie burudani kali kama lilivyo jina la burudani yenyewe, Cheka Kwa Nguvu.


  ‘Usiku wa Jumamosi utawakutanisha moja ya wachekeshaji mahiri barani Afrika, hivyo watanzania waje kwa wingi kushuhudia burudani hii’ alisema Fred.


  Naye mchekeshaji Pilipili kutoka Tanzania amesema usiku wa leo utakuwa usiku wa kukumbukwa hasa kwa vichekesho alivyowaandalia mashabiki wake.Usiku wa Cheka Kwa Nguvu unaandaliwa na kituo cha Radio 5 na pia utaambatana na burudani ya muziki kutoka ODAMA Band.

  Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis amewataka wapenzi wa burudani ya vichekesho kuhudhuria kwa wingi ili wafurahie burudani waliyowaandalia.  ‘Usiku huo utakuwa ni maalumu kwa watanzania kufurahia Utanzania wao, kwani kucheka ni sehemu muhimu kwa maisha ya mwanadamu’ alisema Robert.

  Kansiime amejipatia umaarufu kupitia mitandao ya kijamiii ambako alianza kwa kuweka vipande vya video akiigiza kama mwanamke wa kiafrika anayekutana na changamoto mbalimbali za maisha.


  Mchekeshaji huyo wa kike, ambaye pia huendesha kipindi cha “Don’t Mess With Kansiime” kwenye kituo cha Citizen TV, anatajwa kuwa mwanamke mwenye kipaji cha pekee nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla. 

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Mafuta na Petroli Tanzania (TPDC), James Andilile (kulia), akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu uchimbaji wa gesi na mafuta. Kutoka kushoto ni Rais wa Umoja wa Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam, Jane Mihanje na Mkurugenzi mstaafu wa TPDC, Yona Killagane.
  Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa TPDC, Dk.Wellington Hudson, akitoa mada katika semina hiyo.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Mafuta na Petroli Tanzania (TPDC), James Andilile (wa tatu kulia), akiwa na viongozi wengine katika semina hiyo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi mstaafu wa TPDC, Mr Killagane, Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa TPDC, Dk.Wellington Hudson, Rais wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam, Jane Mihanje, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Mafuta na Petroli Tanzania (TPDC), James Andilile, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Vitega Uchumi wa TPDC, Mhandisi Joyce Kisamo na Kaimu Meneja wa Utafutaji wa TPDC Kelvin Komba.
  Rais wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam, Jane Mihanje akizungumza katika semina hiyo.
  Sehemu ya Wadau walioshiriki Semina hiyo.


  0 0

  Mpigie Kura Mdau Richard Magumba kupitia Filamu yake ya SHEGENA iliyoingia kwenye kinyang'anyiro cha Tuzo za Filamu Fupi zinazoandaliwa na Focus on Ability.

  BOFYA LINK HAPO CHINI KWENDA KUMPIGIA KURA.

  0 0

  Viongozi na Watumishi wa umma wameaswa kuzingatia Kanuni za Maadili ya utendaji kazi ili kujenga Utawala Bora na kuimarisha mapambano dhidi ya Rushwa nchini.

  Rai hiyo imetolewa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Salome Kaganda wakati akizindua filamu ya “The Minister” iliyoandaliwa na Kampuni ya Equity Links Enterprises (ELE) katika ukumbi wa CENTURY CINEMAX THEATRE Jijini Dar es Salaam.

  Mhe. Kaganda alifafanua kuwa katika utumishi wa umma kuna Kanuni za Maadili ya utendaji zinazowahusu watumishi wenye kushika nyadhifa fulani za uongozi na Kanuni zinazowahusu watumishi wote wa umma. Aidha, Mhe. Kaganda aliendelea kusema kuwa Kanuni hizo zimeainishwa katika Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya 1995, Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma za 2005 na Kanuni zinazohusu Taasisi za Kitaaluma.

  “Mwitikio wa watumishi wa umma kwa Kanuni hizo ni muhimu katika kujenga Utawala Bora yakiwemo mapambano dhidi ya rushwa. Maadili katika utumishi wa umma wa nchi yeyote ni lazima yalenge katika kuainisha misingi ya mwenendo mwema wa mtumishi wa umma kwani misingi hivyo inatarajiwa kukuza dhana nzima ya uwajibikaji na uwazi kwa watumishi wa umma” alifafanua Mhe. Kaganda.

  Mhe. Kaganda aliendelea kubainisha kuwa ni wajibu wa mtumishi wa umma kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zinazomwongoza. Aidha, Mhe. Kaganda aliendelea kusisitiza kuwa Mtumishi wa Umma anatakiwa kutekeleza na kusimamia sera na malengo ya serikali kwa juhudi, uaminifu na uadilifu.

  Akizungumza kuhusu filamu ya “The Minister” Mhe. Kaganda aliwapongeza waandaaji wa Sinema hiyo na kuelezea hisia zake kuwa filamu hii itasaidia kufundisha na kuwakumbusha Viongozi pamoja na Watumishi wa Umma kuhusu matatizo ya rushwa, matumizi mabaya ya madaraka, uzembe, ubadhirifu na ufuska.
  Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Salome Kaganda akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa filamu ya “The Minister”, uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa Century Cinemax uliopo katika jengo la Dar Es Salaam Free Market, jijini Dar es Salaam.
  Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji (Mst.) Salome Kaganda akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuzindua filamu ya “The Minister”.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi Juliana Yassoda (Katikati) akiongea na Wanahabari (Hawapo pichani) kuhusu makocha wa Timu ya Barcelona kutoka nchini Hispania ambao wako nchini kwa ajili ya mafunzo ya makocha wa Tanzania yatakayofanyika kwa muda wa siku mbili.Wengine picha toka kulia ni Balozi wa Spain nchini Mh. Luis Manuel Ceuesta Civis, Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,Kushila Thomas,Kocha Isaac Oriol Guerrero Hernandes,Kocha Daniel Bigas Alsina.mafunzo hayo yanatolewa kwa ushirikiano na Kampuni ya  Bia Tanzania (TBL).
  Balozi wa Hispania nchini Tanzania Mh. Luis Manuel Ceuesta Civis (Kulia) akiongea na Makocha kutoka Timu ya Barcelona ya nchini Hispania katika mkutano wa Wanahabari uliofanyika jijini Dar es Salaam jana (leo), makocha hao wapo nchini kwa ajili ya kutoa mafunzo ya siku mbili kwa makocha wazalendo, wa kwanza kushoto ni Kocha Daniel Bigas Alsina na katikati ni Kocha Isaac Oriol Guerrero Hernandes
  Kocha Isaac Oriol Guerrero Hernandes kutoka timu ya Barcelona ya nchini Hispania (katikati) akitoa maelezo kwa wanahabari (hawapo pichani) kuhusu mafunzo ya siku mbili watakayotoa kwa makocha 30 wakizalendo.kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Bi. Juliana Yassoda na wa kwanza kushoto ni kocha Kocha Daniel Bigas Alsina.
  Makocha wa Kizalendo 30 ambao wanatarajiwa kupewa mafunzo ya siku mbili kutoka kwa makocha wa Barcelona wakiwa katika picha ya pamoja Picha zote na Benjamin Sawe kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WHVUM

  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ametoa saa 30 na kutaka kupatiwa majibu ni kwa nini maelekezo aliyotoa kuhusu kiwanda cha kusindika nyama cha Mbeya hayajafanyiwa kazi.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Agosti Mosi, 2014) wakati akizindua Kongamano la siku tatu la Uwekezaji la Mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya la mwaka 2014 ambalo limeanza leo kwenye ukumbi wa Benjamini Mkapa jijini Mbeya.

  “Mbeya inaweza kuwa na fursa kubwa ya viwanda vya usindikaji nyama, unga wa mahindi ili kuongeza thamani ya mazao mnayozalisha katika mkoa wenu. Nilipokuwa hapa ziara yangu ya mwisho 2012, niliagiza kiwanda hiki kitafutiwe mwekezaji ili kianze uzalishaji. Jana nimeuliza kiwanda cha nyama kimefikia wapi, naambiwa watu bado wanaongea. Wanaongea nini?,” alihoji.

  “Mtu akija kusikia habari ya kiwanda hiki atatuona ni wajinga tena ni wajinga wa kujitakia, kisa watu bado wanazungumza… hiki kiwanda cha nyama ni cha Mbeya na manuafaa yake ni kwa ajili ya wana Mbeya. Hivi wahusika ni kwani hamuioni hiyo fursa?” alisema.

  “Dk. Mary Nagu watafute watu wa CHC waje hapa kujieleza ni kwa nini suala hili limechukua muda mrefu. Kabla sijaondoka hapa Mbeya kesho nataka nipate majibu kuhusu jambo hili,” aliagiza.

  Katika hotuba yake ya ufunguzi, Waziri Mkuu alisisitiza suala la watendaji wa mikoa na wilaya kuchukulia kwa umakini suala la uwekezaji kwani wasipofanya hivyo wao ndiyo watageuka kikwazo na kukwamisha maendeleo ya wananchi wanaowaongoza.

  “Ndugu zangu wa Serikali za mitaa msiwe vikwazo, kuwezi wawezeshaji. Ninyi si watawala bali ni waleta maendeleo kwa jamii. Natoa wito mshirikiane na wafanyabiashara kuharakisha maendeleo ya wananchi mliokabidhiwa kuwaongoza. Acheni kudai hongo, kwani badala ya kuwasadia jamii, mtajikuta ninyi ndo mnakuwa vikwazo vya maendeleo,” alionya.

  Alisema Serikali za Mitaa zinapaswa kuwa wawezeshaji na siyo wakwamishaji wa masuala ya maendeleo na ili kufanikisha hilo aliwataka wakuu wa mikoa waanzishe one-stop centre katika ngazi ya mkoa na Halmashauri ili wawekezaji wanapofika katika mikoa yao wasizungushwe na kukatishwa tamaa kwa sababu ya mlolongo wa taasisi zilizopo.

  “Uzoefu unaonyesha kuwa baada ya kufanya makongamano kama haya, wawekezaji wengi wanajitokeza lakini katika ngazi ya Mkoa na Halmashauri wanakosa mahali ambapo wanaweza kushughulikiwa na kupata huduma bora kwa pamoja “One Stop Centre”. Hali hiyo huwafanya wakate tamaa.”

  “Ninashauri kila Mkoa na kila Halmashauri iweke mfumo mzuri wa kuwapokea wawekezaji hususan kuwa na Mratibu (Focal Point) wa masuala ya uwekezaji ambaye ndiye atakuwa “One Stop Centre” wa kushughulikia wawekezaji wanaojitokeza na kuwahudumia kwa ufanisi bila urasimu. Ni imani yangu kuwa tukifanya hivyo, tutawezesha Kanda hii kuwa kitovu kikubwa cha uwekezaji katika nchi yetu,” aliongeza.

  Alisema kila mmoja hana budi kuendelea amani na utulivu wa nchi ili uwekezaji uweze kufanikiwa na kushamiri. “Hakuna uwekezaji endelevu na wenye tija katikati ya fujo na migogoro, na uwekezaji utashamiri pale tu penye amani na utulivu,” alisisitiza.

  Mapema, Waziri wa Nchi (OWM-Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk. Mary Nagu alisema ili uwekezaji uweze kuwanufaisha wananchi, ni lazima rasilmali za nchi zigeuzwe kuwa bidhaa. “Ukiangalia chuma cha Liganga kipo pale miaka mingi, bila kukigeuza kuwa bidhaa, bado hakiwezi kuwanufaisha wananchi wetu,” alisema. Alisema bila uwekezaji hakuna uchumi, na bila uchumi hakuna maendeleo na bila maendeleo hakuna maisha bora kwa kila Mtanzania.

  Katika hatua nyingine, Wakuu wa mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe walipewa nafasi ya kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo ikiwa ni pamoja na kuelezea fursa mahsusi zilizomo kwenye mikoa yao.

  Mada zitakazowasilisha katika kongamano hilo ambalo kaulimbiu yake ni “Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii katika Nyanda za Juu Kusini” zinahusu fursa za uwekezaji katika sekta za uchumi na miundombinu katika kanda hiyo, fursa za uwekezaji katika sekta za huduma za jamii katika kanda hiyo, fursa za uwekezaji katika kilimo cha mazao ya bustani (matunda, mboga, maua na viungo) na mchango wa taasisi za fedha katika uwekezaji.

  Nyingine ni mchango wa sekta binafsi katika uwekezaji, na nafasi ya MKURABITA katika kukuza mitaji ya uwekezaji.

  0 0

    Mbunge wa jimbo la Ukonga Eugen Mwaiposa akimkabidhi kombe la ubingwa nahodha wa timu ya Ilala Academy Maisala Adam baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka wa Ilala juzi.
   Mbunge wa jimbo la Ukonga Eugen Mwaiposa akimkabidhi kombe la ubingwa nahodha wa timu ya Temeke All Stars Maulid Jamal baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka wa Temeke juzi.


   Mbunge wa jimbo la Ukonga Eugen Mwaiposa akimkabidhi kombe la ubingwa nahodha wa timu ya Kinondoni Academy Jafali Said baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka wa Kinondoni juzi.

  0 0
 • 08/01/14--07:43: PONGEZI KWA RAIS KIKWETE


older | 1 | .... | 522 | 523 | (Page 524) | 525 | 526 | .... | 3272 | newer