Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

SALAMU ZA EID KUTOKA KWA PAPAAA HASSANI KANIKI MUTU YA KILO YA TRANSHPOO

$
0
0
Nikiikala hapa ku Daresalama ninawaombea wato nyote sikukulu nyema yenye furaha na upendo. Hivi sasa nalikuaga kutayarishaga singo yangu mupya kwa ajiri ya Iddi hii, lakini produza akasemaga ana makazi bwerere ya kina Dayamond na Omi Dimpoz hivyo singo yangu itaitokaga kunako mwezi wa kenda. Haina neno lakini Iddi jema ku wato nyote.

BREAKING NYUUUZZZZZ: VIONGOZI WA CHUO NA HOSPITALI YA IMTU WATINGA MAHAKAMANI, DPP AWAONDOLEA MASHTAKA

$
0
0
Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), aliwapandisha kizimbani vigogo wanne wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba (IMTU) na baadaye kuwaondolea mashitaka kupitia hati ya Nole ya kuwaondolea mashtaka ya kushindwa kufukia viungo vya binadamu na kupeleka hati ya kufukia viungo vilivyotumika kufundishia kwa Kampuni Coroner. 
 Vigogo hao ni, Venkat Subbaian (57), Appm Shankar (64), Prabhakar Rao (59) na Dinesh Kumar (27) ambao walisomewa mashtaka yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo  saa 8:07  mchana.  Washtakiwa hao walisimama kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kwey Lusemwa. 
Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Magoma Magina alidai kuwa Julai 20, mwaka huu washtakiwa wakiwa na nyadhifa  tofauti, Profesa, Mtawala na wahadhiri, kwa makusudi walishindwa kufukia mifuko 83 iliyokuwa na viungo vya binadamu kinyume cha sheria ya 128 kifungu cha 8 na cha 9 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA). 
 Magina alidai kuwa katika shitaka la pili, washtakiwa wote kwa pamoja walishindwa kupeleka hati ya kumtarifu kwamba wamefukia viungo hivyo baada ya kutumika kufundishia kama sheria inavyowataka. Hakimu Lusemwa alisema washtakiwa watakuwa nje kwa dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili raia wa Tanzania kila mmoja. 
Hata hivyo, kabla mahakama haijasikiliza kipengele cha dhamana, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Salum Ahmed aliwasilisha hati ya Nole kutoka kwa DPP akidai kuwa anawaondolea vigogo hao mashtaka na kwamba hana nia ya kuendelea kuwashitaki. 
 Ahmed alidai kuwa DPP anawaondolea washtakiwa mashitaka hayo chini ya kifungu cha 91 kidogo cha (1) cha CPA kwa kuwa hana nia ya kuendelea kuwashitaka. 
 Wakili wa washtakiwa Gaudiosus Ishengoma alisema kwamba inaonekana kuna mbinu kubwa dhidi ya washtakiwa. Alisema anavyofahamu kwamba hati ya mashitaka ingekuwa na kasoro wateja wake wangepata dhamana na baadaye ingewezekana kubadilishwa. 
Alisema kutokana na sababu hiyo, ana wasiwasi kwamba inawezekana DPP ana nia ya kuwafungulia wateja wangu kesi yenye mashitaka yasiyokuwa na dhamana ili wakasote mahabusu. 
 Viwanja vya mahakama hiyo vilikuwa tulivu huku wanaodaiwa kuwa wafanyakazi wa IMTU wakiwa wamesimama katika makundi makundi wakijadiliana hili na lile. 
Kupitia magari ya Jeshi la Polisi, T 366 AVG aina ya Rav4 alipanda mshtakiwa wa tatu kwa madai kuwa ni mgonjwa na washtakiwa wengine waliondoka mahakamani hapo katika gari yenye namba za usajili KX06EFY aina ya Toyota Landcruiser na kurudishwa mahabusu ya jeshi hilo.
 Washtakiwa wakiwa katika gari la polisi 
 Wakipanda gari baada ya kusomewa mashitaka
 Wakitoka mahakamani baada ya kusomewa mashitaka
 
Washtakiwa wakisubiri kuingia mahakamani.
Picha na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii

President Obama participates in a town hall at the Summit of the Washington Fellowship for Young African Leaders

$
0
0
The President participates in a town hall at the Summit of the Washington Fellowship for Young African Leaders. The three-day Summit will cap off the Washington Fellowship, the flagship program of the President’s Young African Leaders Initiative (YALI), and give 500 of sub-Saharan Africa’s most prominent young leaders the opportunity to engage with U.S. government officials, entrepreneurs and civil society representatives as well as leaders in international development. Courtesy of The White House
 Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari akiwa na wenzake kwenye mkutano uliohutubiwa na Rais Obama leo
 Rais Obama akiongea na viongoi vijana wa Afrika leo
Rais Obama akijibu maswali 

mambo ya gado

$
0
0

Fraudulent Tycoon Somaia Jailed in UK


mambo ya gado

Introducing Alex Kajumulo's newest single "Take Me Home"

Balozi adadi amtembelea balozi mdogo wa Tanzania Dubai Mhe Omar Mjenga

$
0
0
 Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Mhe Adadi Rajabu akiwa na  Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai Mhe Omar Mjenga, Jumeirah, Dubai, leo Mhe Adadi yuko Dubai kwa ziara ya kikazi

Tangazo La Form 5 2014 BAHARI BEACH HIGH SCHOOL DAR ES SALAAM


SHEREHE ZA EID EL FITR DMV

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiongea na mmoja wa Watanzania wa DMV(kulia) wakati sherehe ya Eid iliyofanyika Wheaton, Maryland nchini Marekani siku ya Jumatatu July 28, 2014 na kuhudhuliwa na Watanzania wa DMV na marafiki zao, katikati ni afisa wa maswala ya uhamiaji Bwn. Abbas Missana.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania wa DMV na marafiki zao waliohudhuria sherehe ya Eid iliyofanyika siku ya Jumamosi July 28, 2014 Wheaton, Maryland nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiwa kwenye sherehe ya Eid iliyofanyika Wheaton, Maryland siku ya Jumatatu July 28, 2014 na kuhudhuliwa na Watanzania wa DMV na marafiki zao.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa TAMCO na Watanzania waliohudhuria sherehe ya Eid iliyofanyika Jumatatu July 28, 2014 Wheaton, Maryaland nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani akiwa katika picha na Watanzania wa DMV na marafiki zao katika sherehe ya sikukuu ya Eid iliyofanyika siku ya Jumatatu July 28, 2014 Wheaton, Maryland nchini Marekani. Picha zote kwa hisani ya Missy Temeke
kwa picha zaidi bofya HAPA

WAZIRI WA UCHUKUZI DK.HARRISON MWAKYEMBE AFANYA ZIARA YA KIKAZI KATIKA MAKAO MAKUU YA OFISI ZA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA (TCAA)

$
0
0
 Waziri wa Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe (kulia)akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Ndege wa Mamlaka Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Nuis Kasambala alivyokuwa akimuelezea na kumuonyesha jinsi wanavyofanya mitihani kwa wanafunzi wa ndege  wakati alipofanya  ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi ya Mamaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wanafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA. Waliosimama nyuma ni Kamati ya bodi ya Mamlaka hiyo wakifuatilia kwa makini. 
  Waziri wa Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe (kulia)akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Ndege wa Mamlaka Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Nuis Kasambala alivyokuwa akimuelezea na kumuonyesha jinsi wanavyofanya mitihani kwa wanafunzi wa ndege  wakati alipofanya  ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi ya Mamaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam
 

 Waziri wa  Uchukuzi  Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akikabidhiwa  na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha moja ya tuzo waliyotunukiwa Tanzania na Baraza la Usafiri wa Anga Duniani kwa kutambua mchango wa TCAA. Anayeshuhudia katikati ni Makamu Mweneyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka hiyo Dkt.Weggoro Nyamajeje,  wakati alipofanya ziara ya kikazi  Makao Makuu ya Ofisi  ya Mamaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wanafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi  ya TCAA. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

KAGASHEKI CUP 2014: PENATI ZAPIGWA TENA LEO KAITABA, KITENDAGURO FC YAIBUKA BINGWA NA KUSONGA NUSU FAINALI KWA PENATI 6-5 DHIDI YA TIMU YA RWAMISHENYE FC

$
0
0
Mikwaju ndio iliwatoa Rwamishenye na hapa ni kipa wake akipelekeshwa katika mkwaju wa Mwisho!! mpira umepigwa huku yeye akajitupa kule!!Wachezaji wa Kitendanguro wakishangilia kwenda Nusu Fainali baada ya kuwatoa kamasi Wanabodaboda timu ya Rwamishenye Fc penati 6-5kushoto ni kipa wa Makhirikhiri Kitendaguro Fc akifurahia ushindi na mwenzakeUshindi Mtamu!!! tunaenda Nusu Fainali!!!Dada Shabiki wa Timu ya Kitendaguro alishindwa kujizuia akajikuta katikati ya Uwanja! Kwa picha zaidi za Faustine Ruta BOFYA HAPA

shimozzz upanga mbele ya shule ya Sekondari Tambaza

$
0
0
Kadri siku zinavyozidi kwenda na simo hili linazidi kushika kasi ya kuendelea kuchimbika,jambo ambalo linaweza sababisha madhara makubwa hapo baadae.Shimo hili lipo usoni kabisa mwa Shule ya Sekondari Tambaza,Upanga jijini Dar.

KIKOSI CHA TAIFA STARS KUELEKEA NCHINI AFRIKA KUSINI KESHO

$
0
0
Msafara wa watu 27 wa kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kinaondoka kesho (Julai 30 mwaka huu) saa 10 jioni kwa ndege ya Air Tanzania kwenda Afrika Kusini ambapo kitapiga kambi ya siku mbili kabla ya kuingia Maputo kuikabili Msumbiji (Mambas).

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itawasili saa 9 asubuhi kesho (Julai 30 mwaka huu) kwa ndege ya Fastjet kutoka Tukuyu mkoani Mbeya, na baadaye jioni kuunganisha safari ya Afrika Kusini.

Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji itachezwa Agosti 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa uliopo Zimpeto nje kidogo ya Jiji la Maputo.

Msafara huo wa Taifa Stars kwenda Afrika Kusini unajumuisha wachezaji 19 na waliobaki ni maofisa wa Benchi la Ufundi lililo chini ya Kocha Mkuu Mart Nooij kutoka Uholanzi.

Wakati kiungo Mwinyi Kazimoto ametua leo (Julai 29 mwaka huu) nchini kuungana na wenzake, washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wao wataungana na wenzao kesho (Julai 30 mwaka huu) jijini Johannesburg wakitokea Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Wakati huo huo, Serengeti Boys imewasili salama jana (Julai 28 mwaka huu) jijini Johannesburg kwa ajili ya mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 dhidi ya wenyeji Afrika Kusini (Amajimbos).

Serengeti Boys imefikia hoteli ya Garden Court, na mechi hiyo itachezwa Jumamosi (Agosti 2 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Dobsonville uliopo Soweto. Timu hizo zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyochezwa karibu wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam.

EAC Students’ Debate 2014 set for September in Nairobi

$
0
0
The EAC Deputy Secretary General, Mr. Charles Njoroge makes his remarks at the start of the Preparatory Meeting ahead of the 3rd EAC University Students Debate. He is flanked by the Principal Political Affairs Officer, Ms. Isabelle Waffubwa (left) and the GIZ-EAC Programme Junior Advisor, Ms. Venelina Gancheva.
The participants at the Planning Meeting pose for a group photo. The meeting is reviewing the activities of the EAC Youth Ambassadors Platform and make preparations for the forthcoming 3rd EAC University Students Debate 2014.

The 3rd East African Community University Students’ Debate 2014 is scheduled to be held on September 4-5, 2014, in Nairobi, Kenya.

The debate which brings together students from various Universities and institutions of higher learning from the EAC region is an important avenue for sharing information, exchange of ideas and promoting discourse and sensitization.

Towards this end, the EAC in collaboration with the GiZ-EAC Programme, is holding a three-day preparatory meeting (July 28-30, 2014) in Nairobi to map out the strategies for the forthcoming debate.   The meeting was opened yesterday by the Deputy Secretary General of the EAC, Mr. Charles Njoroge. 

In his remarks, the Deputy Secretary General urged the youth to continue to be advocates championing the tenets of integration. Mr. Njoroge commended the EAC Youth Ambassadors Platform for the noble work of spearheading and popularizing EAC integration within the university community.

‘I also want to assure you that EAC is committed to strengthening the networks the Platform has created with University administrations over time as well as the EAC Youth Clubs in fulfillment of the principal of participation and involvement of all segments of the society in the integration agenda’, he said.

The Deputy Secretary General maintained that the Regional Economic Community was geared towards mobilizing sustainable resources for the Nyerere Centre for Peace and Research.

The meeting is evaluating the impact of sensitization programmes that have been undertaken from the period February – June 2014. It is also hopes to validate the lessons and challenges learnt by the Platform.
According to the Principal Political Affairs Officer at the EAC, Isabelle Waffubwa, the opportunity affords the EAC an opportunity to rethink, refocus where necessary, and evaluate the performance as well as the impact on targeted groups.

The Chair of the EAC Youth Ambassadors, Ms. Effie Owour lauded the Members of the Platform for their commitment and said that their contribution towards the integration progress was already bearing fruit.The GiZ-EAC Junior Advisor on Peace and Security in the EAC, Ms. Venelina Gancheva, affirmed the Organization’s commitment to assisting the region realize full integration. 

“To date, the Youth Ambassadors have been engaged in close to 30 sensitisation activities and over 6000 stakeholders have been targeted”, Ms. Gancheva remarked.

The University Debate was mooted by the EAC under the Nyerere Centre for Peace Research.  The debate among other things envisages the full participation of the young people in dialogue as well as in the exchange of ideas on concrete issues that have impact.

The EAC University Students’ Debate on Regional Integration 

The Forum was established to interest University students in regional integration. To this end, students have demonstrated commitment towards exchange of ideas and sharing of knowledge among themselves. Arising from the 2nd EAC University Students’ Debate, the EAC Secretariat launched the EAC Youth Ambassadors’ Platform (EAC-YAP) last year to enable structured engagement with the youth at Universities and other Higher Institutions of Learning.

The Platform spearheads information sharing and sensitization of young people through writing articles, debates on topical issues in the social media, hosting talk shows on the EAC Integration as well as holding sensitization forums across universities. The outcome of such activities has enhanced sensitization of peers and dissemination of information of the EAC integration, opportunities and challenges.

KALAMU EDUCATION FOUNDATION YALA EID MUBARAK NA WATOTO WAGONJWA HOSPITALI YA MWANANYAMALA.

$
0
0
 Baadhi ya wajumbe wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation wakichukua baadhi ya Madawa ya kufanyia usafi ambayo taasisi hiyo imechangia katika wodi ya watoto katika hospitali ya Mwananyamala Dar es salaam kuboresha usafi katika Hospitali Hiyo Kubwa Jijini Dar es Salaam.
 Dr. Mohamed wa Wizara ya Afya, Mh. Asha Mtwangi Mjumbe Bunge Maalum la Katiba na Ndugu Hassan Swedi, Meneja wa Fedha BORDA – Tanzania wakisikiliza kwa makini taarifa ya Muuguzi wa zamu juu ya Changamoto za kuwaangalia watoto wenye matatizo mbali mbali na jinsi wanavyopambana nayo katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala – Dar es salaam.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation Bw. Mohamed Kamilagwa akimfaraji Mmoja wa Wazazi wa Mtoto anayesumbuliwa na Malaria katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala.
 Mh. Asha Dodo Mtwangi akipata Maelezo kutoka kwa wazazi wa watoto waliolazwa katika hospitali ya Mwananyamala. Mh. Asha Mtwangi alifanya ziara hiyo asubuhi ya siku ya EID El Fitr pamoja na wajumbe wenzake wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation ili kuwafariji watoto na wazazi wa watoto katika Hospitali ya Mwananyamala – Dar es Salaam.
 Mh. Asha Mtwangi akifurahi  na mtoto mchanga aliyezaliwa usiku wa mkesha wa siku ya EID. Anayeangalia pembeni ni Bwana Hassan Swedi akiwa na Muuguzi wa Mwandamizi wa zamu wa Hospitali ya Mwananyamala wakati wa Ziara Maalum ya Kusheherekea Sikukuu ya Eid el Fitr.
Baadhi ya Wajumbe wa Kalamu Education Foundation wakitafakali mafanikio na changamoto za uendeshaji wa hospitali za Umma hasa kwa watanzania wa kipato cha chini wakati wa ziara ya wajumbe wa Taasisi hiyo katika Hospitali ya Mwananyamala Siku ya Eid el Fitr.

BWAWA LA MAINI OYE!

$
0
0
Reds complete Origi deal
Timu ya Liverpool imethibitisha kukamilisha usajili wa mchezazji Divock Origi kutoka timu ya  Lille. Mchezaji huyo mwenye miaka 19, alisikika akisema amefurahi sana kujiunga na Liverpool timu kubwa Uingereza yenye historia ndefu na yupo tayari kucheza kadri ya uwezo wake akisaidiana na wachezaji wenzake kuipeleka Liverpool mbele.

TIMU YA TAIFA YA MCHEZO WA CHESS YAKABIDHIWA BENDERA YA TAIFA KWENDA KUSHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA NCHINI NORWAY

$
0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi (kulia), akimakabidhi Bendera ya Taifa, mmoja wa wachezaji wa timu ya Taifa wa mchezo wa Chess, Hemed Mlawa (wa pili kushoto), Dar es Salaam leo asubuhi kwa ajili ya kuondoka kesho kwenda kushiriki mashindano ya kimataifa nchini Norway. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini, kushoto ni mchezaji Emmanuel Mwaisumbe. Safari hiyo imedhaminiwa na Tanzania Chess Foundation na Kasparov Foundation.
Hapa ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi (katikati), Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini (kulia), mchezaji Hemed Mlawa (kushoto) na Emmanuel Mwaisumbe (wa pili kushoto), wakifurahi baada ya kucheza mchezo huo wakati wakiwaonesha waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi (katikati), akizungumza na wanahabri kabla ya kukabidhi bendera. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini na kulia mchezaji Hemed Mlawa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini, akizungumza na wanahabari. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini, akizungumza na wanahabari.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MABONDIA WAPIMA UZITO KUPIGANA IDDI PILI MANYARA PARK MANZESE

$
0
0
Bondia Peter Mbowe akioneshana umwamba wa kutunishiana misuli na Ibrahimu Tamba baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao yutakaofanyika katika ukumbi wa Manyara Park Tandale CCM siku ya Iddi pili 
Bondia Karim Ramadhani akipima uzito
Bondia Karim Ramadhani kushoto akitunishiana misuli na bondia Stevin Kobelo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya iddi pili katika ukumbi wa Manyara Park manzese CCM wa pili kushoto ni bondia Nassibu Ramadhani na Kocha Jafari Ndame
Mjumbe wa kamati ya utendaji wa chama cha ngumi za kulipwa nchini Ally Bakari ' Champion' akiwakumbusha mabondia na wasaidizi wao sheria mbalimbali za mchezo wa ngumi kabla ya mpambano wao
Rais wa TPBO CHAUREMBO PALASA AKISISITIZA JAMBO.
Picha zote na Super D

mambo ya gado

Bongo Tambarare: mkeka wa tegeta

$
0
0
Hapa ni njia panga ya Kawe na Bagamoyo Road jijini Dar es salaam. 
Foleni kwishnei
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images