Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 518 | 519 | (Page 520) | 521 | 522 | .... | 3285 | newer

  0 0

   Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kanali James Ruzibiza Stashahada ya Usalama na Stratejia (Diploma in Security and Strategic Studies) katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014. Kushoto ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi. Kanali Ruzibiza, ambaye anatokea Rwanda, ni mmoja wa washiriki tisa wa kozi waliotoka nchi za nje. Washiriki wengine kutoka nje ya nchi walitoka Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Uganda, zambia na Zimbabwe. Jumla ya wahitimu 30, wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali. 

   Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Luteni Jenerali C.L. Makakala Shahada ya Uzamili ya Falsafa ya Usalama na Stratejia katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014. Luteni jenerali Makakala, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi wa kwanza, amekuwa mtunukiwa wa kwanza wa Shahada hiyo hapo chuoni.
   Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia baada ya kutunuku shahada katika  mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014.Jumla ya wahitimu 30 wamehudhuria kozi hiyo wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali. Washiriki wengine tisa wametoka  nchi za nje ambazo ni Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Rwanda Uganda, Zambia na Zimbabwe.
   Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaambia kuwa sasa ni zamu yao kupiga picha ya kumbukumbu bila yeye wahitimu wa Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014.
  Picha ya Pamoja.PICHA NA IKULU

  0 0

  KAMPUNI ya Nakumatt Holdings, imezindua rasmi tawi la kwanza kati ya matawi yake matatu makubwa nchini Tanzania ambayo awali yalimilikiwa na Kampuni ya Shoprite ya Afrika ya Kusini. 
  Ikiwa ni mpango wake mpya wa kuboresha zaidi huduma zake, Nakumatt holdings, imezindua tawi hilo kubwa ambalo litakuwa utambulisho muhimu wa huduma zake katika eneo la biashara la Mlimani City litakaloitwa Nakumatt Mlimani. 
  Tawi hilo la 48 la Nakumatt limepambwa kwa rangi na mwonekano wa alama za Nakumatt na kwa ubunifu wa hali ya juu. Pamoja na Nakumatt Mlimani, kampuni hiyo pia iko mbioni kuzindua tawi lengine kubwa litakalojulikana kama ‘Nakumatt Pugu Road’ jijini Dar es salaam ambako pia kutakuwa makao yake makuu. Pia itafungua Nakumatt Arusha siku zijazo. 
   Kwa kufungua matawi yake matatu moja baada ya jingine, Nakumatt pia itakuwa imefikisha matawi 50 katika mtandao wake wa huduma za uuzaji bidhaa na hivyo kutekeleza mkakati wake wa maendeleo ambao ulizinduliwa mwaka 2011.
   Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka lake la kwanza in Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Nakumatt Holdings, Atul Shah alisema kufunguliwa kwa matawi matatu mapya yaliogharimu takriban dola za Marekani milioni 3 ni sehemu ya mpango wa upanuzi wa huduma za uuzaji bidhaa katika kanda ya Afrika. Kutokana na uzinduzi wa Tawi la Nakumatt Mlimani, Shah alisema kuwa Nakumatt sasa ina maduka mawili makubwa yanayofanya kazi nchini Tanzania. 
  Nakumatt Mlimani inaungana na duka jingine la la Nakumatt Moshi lililofunguliwa mwaka 2011 katika mji huo ambako kuna Mlima Kilimajaro. 
  ”Uzinduzi wa Nakumatt Mlimani ni ndoto ya muda mrefu ambayo sasa imekuwa kweli ambapo tumekuwa tukifikira mahali pa kuweka duka letu jijini Dar es salaam na maeneo mengine nchini Tanzania,” alisema Shah na kuongeza: “Uzinduzi huu pia ni hatua nzuri itakayopelekea uzinduzi mwingine wa duka letu la 50 katikati ya Agosti ambapo tutakuwa tumefanikiwa kufikia malengo yetu tuliyojiwekea kuyafikia Februari mwakani.” Maduka matatu ya Shoprite yalifungwa mwezi uliopita ili kufanikisha kazi ya kuyaboresha zaidi sambamba kwa kuzingatia viwango na uzoefu wa Nakumatt. 
  Pia Nakumatt inatarajia kufungua matawi mengine matatu ya biashara nchini Kenya kabla ya mwisho wa mwaka huu.
   Pia kampuni hiyo itakuwa na duka kubwa katika eneo kubwa la kifahari la Green Square mjini Kericho nchini Kenya. Shah alisema Nakumatt ina mkakati wa kukuza biashara wa kampuni ambao unategemea zaidi uwepo wa vitega uchumi ambapo kampuni inaweza kuendesha shughuli zake za maduka ya supermaketi. Shah aliongeza kwa kusema:
   “ Kwa sasa tunaendesha shughuli zetu katika nchi 12 na tunashirikiana na wamiliki wa maeneo ya biashara nchini Kenya ambao wanaweza kutoa huduma za kujenga maeneo ya maduka makubwa katika maeneo ya Machakos, Nyeri, Kajiado, Garissa, Embu, Naivasha,Narok Busia and Homabay.” 
  Ili kutimiza masharti ya Nakumatt, Shah aliwahimiza waendelezaji wa maeneo ya biashara na Mameneja wa Miradi kushauriana na wataalam wa Nakumatt kuhusu namna ya kuboresha uchoraji wa ramani na ujenzi wenye mvuto kwa wateja katika maduka ya kampuni hiyo.
  Wafanyakazi wa Nakumatt Mlimani wakifurahia wakati wa sherehe za ufunguzi wa mall hiyo Mlimani City jijini Dar es salaam leo
  Furaha ya kuanza kazi Nakumatt Mlimani leo
  Mkurugenzi Mtendaji wa Nakumatt Holdings, Atul Shah akimuonesha baadhi ya bidhaa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Janet Mbene wakati wa ufunguzi huo leo
   Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Janet Mbene akiangalia bidhaa wakati wa ufunguzi huo leo

  0 0

  Na John Gagarini, Kibaha

  JESHI la Polisi mkoani Pwani limewataka madereva kuwa makini waendeshapo magari na kuacha matumizi ya vilevi ili kuepukana na ajali zisizo za lazima ambazo zinaweza zikajitokeza wakati wa kipindi cha sikukuu ya Eid el Fitr. 

  Pia limewataka wanafamilia kutotoka wote majumbani bila ya kuacha watu au kutoa taarifa kwa majirani ili kuepuka wizi na uhalifu unaoweza kujitokeza wakati wa sikukuu.

  Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani humo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) Ulrich Matei alisema kuwa baadhi ya madereva wamekuwa wakitumia vilevi wakati wa kiendesha magari jambo ambalo ni hatari kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri na watembea kwa miguu.

  “Jeshi la polisi liko makini katika kipindi hichi cha sikukuu ili kuhakikisha wananchi wanasherehekea sikukuu bila ya matatizo na linawaomba madereva kuachana na tabia ya kutumia vilevi ili kuepuka ajali wakati huu,” alisema Kamanda Matei.

  Aidha alisema kuwa kikosi cha usalama barabarani kitahakikisha madereva wanafuata sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali ambazo zianweza kutokea na kuleta madhara kwa watu.

  “Tunasisitiza madereva kuachana na ulevi wakati wa kuendesha kwani uzoefu unaonyesha ajali nyingi zimekuwa zikitokana na matumizi ya ulevi hivyo waache matumizi hayo na endapo watabainika watachukuliwa hatua kali za kisheria,” alisema Kamanda Matei.

  Kwa upande wa wananchi aliwataka kutumia ulinzi jirani kwa kuacha mtu au watu badala ya kuondoka wote na kuacha nyumba peke yake jambo ambalo linaweza likasababisha wizi majumbani.

  “Wezi wamekuwa wakitumia mwanya wa kuiba kwenye nyumba ambazo hazina watu hivyo hata kama nyumba nzima imetoka ni vyema wakatoa taarifa kwa majirani ili wawalindie nyumba zao,” alisema Kamanda Matei.

  Aliwataka wamiliki wa kumbi za starehe kutojaza watu kupita kiasi ili kuepuka athari ambazo zinaweza kujitokeza endepo watakuwa wamejaza watu wengi kwenye kumbi zao.

  “Kuna hatari nyingi zinazotokana na kumbi kujaa kupita kiasi mfano watu kukosa hewa na kusababisha vifo au bahati mbaya shoti ya umeme endapo itatokea hivyo lazima wazingatie masharti ya leseni zao zinavyowataka ili kuepusha athari kama hizo,” alisema Kamanda Matei.

  Alibainisha kuwa jeshi lake limejipanga kuhakikisha kuwa sherehe hizo zinafanyika kwa amani na utulivu kwa kuweka ulinzi kwenye maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya doria mitaani.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ulinzi ya Ultimate security,Jacqui Bothma na Meneja wa huduma kwa wateja wa kampuni hiyo Pambwe Maulid wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa magari mapya 12 na pikipiki 14 zitakazotumika kwaajili ya kutoa huduma mbalimbali katika jamii.
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ulinzi ya Ultimate security,Jacqui Bothma(kushoto)akimsikiliza Meneja wa huduma kwa wateja wa kampuni hiyo Pambwe Maulid,(hawapo pichani)akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa magari mapya 12 ya kampuni hiyo na pikipiki 14 zitakazotumika kwaajili ya kutoa huduma mbalimbali katika jamii.
  Baadhi ya walinzi wa kampuni ya Ultimate Security ya jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye pikipiki mpya zilizonunuliwa na kampuni hiyo kwaajili ya matumatumizi ya huduma za ulinzi katika jamii,wakati wa uzinduzi wa magari mapya 12 ya kampuni hiyo na pikipiki 14.
  Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Ultimate Security ya jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi rasmi wa magari mapya na pikipiki zilizonunuliwa na kampuni hiyo kwaajili ya matumitumizi ya huduma za ulinzi katika jamii.
  Msafara wa magari mapya 12 ya kampuni ya Ultimate Security ya jijini Dar es Salaam,yakiongozwa na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo katika barabara ya Alhassan Mwinyi,tayari kwaajili ya matumatumizi ya huduma za ulinzi katika jamii.


  0 0

  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. John Gurisha akipimwa kabla ya kuchangia damu katika zoezi lilioendeshwa na Shrika la Red Cross katika kuchangia damu Mkoani Rukwa. Kumekuwepo na uhaba mkubwa wa damu katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa na vituo vingine uhaba ambao unafikia nusu kwa nusu ukilinganisha kiasi kinachopatikana na mahitaji yaliyopo. Uhaba huo umesababishwa na muamko hafifu wa wananchi kuchangia damu kutokana na hofu inayosababishwa na dhana potofu kuwa uchangiaji damu una madhara kwa mchangiaji. Madaktari hao wa Hosptali Kuu ya Mkoa pamoja na watumishi wengine wa Serikali waliamua kujitolea ili kuonyesha mfano kwa wananchi waweze kuondokana na hofu hiyo waweze kujitokeza kuchangia damu kuokoa maisha ya watanzania wanaohitaji huduma hiyo muhimu.
  Baadhi ya madaktari wa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa wkichangia damu.
  Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Esther Kasegezya akichangia damu katika zoezi hilo.
  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa Dkt. Samwel Marwa akipatiwa vipimo muda mfupi kabla ya kuchangia damu.
  Dkt. Marwa akichangia damu.
  Mchangiaji baada kutoa damu hupata viburudisho ikiwemo vinywaji baridi na biskuti maalum.
  Sehemu ya damu iliyokuwa imechangiwa katika zoezi hilo.
  Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

  0 0

  Mwakilishi wa Jimbo la Uzini (CCM) Mohamedraza Hassanal (kulia) akizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Hoteli ya Grand Palace mjini Zanzibar. Katika mazungumzo yake alisema ni Vyema Bunge la Katiba likaahirishwa ili kutoa fursa zaidi Watu wajihusishe na harakati za Uchaguzi Mkuu wa 2015 na Kupatikane Wasaa mpana wa kujadiliana kwa dhamira ya dhati ya kupata Katiba Bora inayoridhiwa na upande wa Bara na Visiwani.


  0 0  0 0

    

  Na Sultani Kipingo

  Mnamo mwaka 1960 wapiga picha wa kujitegemea huko Italy walijipatia umaarufu mkubwa kutokana na filamu moja iliyokuwa mashuhuri duniani iliyoenda kwa jina la La Dolce Vita (“Maisha Matamu” kwa Kitaliani)  iliyotengenezwa na Producer Federico Fellini wa huko huko Italy.


  Hadhithi ya filamu hiyo ya La Dolce Vita inamhusu mwanahabari mchunguzi aliyeitwa Marcello (muigizaji akiwa Marcello Mastroianni) na mpiga picha wake aliyeitwa Paparazzo (muigizaji Walter Santesso). Ingawa bado kuna ubishi wa maana ya jina “Paparazzo”, lakini mfanano wake na jina la mbu mkubwa aitwaye Papataceo kwa lugha ya Kitaliani, ilileta maana kwa kulinganisha maneno ya producer Fellini mwenyewe kwenye taarifa aliyotoa wakati huo.


  “Jina Paparazzo kwangu mimi ni kama mbu  anayeruka huku na kule akitafuna watu walio kwenye starehe zao”, alisema Fellini, na kuachia mchoro wa aina ya mtu asiye na mifupa (angalia picha hapo juu kulia) akiwa ameshika kamera ambayo flashi yake inawaka, akimaanisha kwamba paparazzi, kama walivyo mbu, ni wadudu wasumbufu.


  Baada ya filamu ya La Dolce Vita kuzinduliwa huko Italy, neno “Papaparazzi likawa linafananishwa na wapiga picha za udaku waliokuwa wakiwinda nyota mbalimbali wa filamu na watu maarufu na kuwaanika magazetini.  Hata hivyo, Fellini alisema yeye hakuwa anawaiga hao wapiga picha za udaku, bali alidai yeye anachofanya ni kuyaingiza magazeti katika filamu, wakati stori zake zilizohusu maisha ya kuponda raha wanayoishi nyota wa filamu ziliuza sana magazeti ya udaku.


  Hapana shaka kwamba kuingia kwa neno Paparazzi katika lugha ya Kiingereza kunatokana na hiyo filamu ya La Dolce Vita, pale ilipozinduliwa nchini Marekani huo  mwaka 1961. Na lilikuwa ni jarida maarufu la Time Magazine lililowezesha jina hilo la Paparazzi kupata umaarufu na kuwaganda wapiga picha wa kujitegemea waliokuwa wakisaka habari za udaku za nyota wa filamu.


   Makala ya jarida hilo iliyokuwa na kichwa cha habari cha “Paparazzi on the Prowl” (yaani paparazzi mawindoni), pamoja na picha ya wapiga picha kibao waliokuwa wamezuia gari la Binti Mfalme mmoja aliyekuwa ziarani Rome, ndiyo vilivyokoleza moto.


  Makala hiyo ilikuwa inazungumzia jinsi kundi la wapiga picha wa kujitegemea walivyokuwa kama mbwa mwitu mawindoni, wakipita huku na kule kuwinda watu wenye majina makubwa katika jamii, kuwapiga picha wakipinda raha  na kuwaanika kwenye magazeti ya udaku. 
  Paparazzi wa Italy wakiwa kazini...  0 0


  Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga, akifanya kikao nyumbani kwake na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), BW. Nehemiah Mchechu na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ujenzi ya DAMAC ya Dubai, Bw. Sonil Vohor.
  Kampuni ya DAMAC imekubali kuingia ubia na NHC kwenye ujenzi wa nyumba za makazi na biashara, na hotel za nyota tano na kiwanja cha golf.
  Mwezi huu Julai tarehe 17, DAMAC walifanya ziara Tanzania kupata taarifa muhimu (fact finding mission). Mwenyekiti wa DAMAC Bw. Hussain Sajwan, atafanya ziara Tanzania mwezi Septemba 2014.

  Bw. Sonil Vohor (kulia), Mhe. Omar Mjenga(katikato) na Bw. Nehemiah Mchechu (kulia) katika picha ya pamoja.

  0 0


  Mwili wa Marehemu Sydney Damson ambaye aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo cha Uhasibu Dar es Salaam(sasa kikijulikana Taasisi ya Uhasibu Tanzania) ukiwasili nyumbani kwake Tandika Magorofani, Wilayani Temeke tayari kwa taratibu za kuaga kabla ya kwenda mazikoni.
  Mchungaji wa Kanisa la Moravian, Mchungaji Mwakalinga(kushoto) akiendesha Ibada Maalum ya kumuombea Marehemu Sydney Damson kabla ya zoezi la kuuaga mwili wa Marehemu kuanza nyumbani kwake Tandika Magorofani leo Julai 27, 2014 Temeke Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kulia aliyeketi) ni Mtoto wa kwanza wa Marehemu ambaye ni Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Masokola Damson.
  Baadhi ya Watu waliojitokeza kuuaga mwili wa aliyekuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Dar es Salaam(TIA) wakimsikiliza Mchungaji wakati wa Ibada Maalum ya kumuombea Marehemu iliyofanyika nyumbani kwake Tandika Magorofani, Temeke Jijini Dar es Salaam.
  Mke wa Marehemu Sydney Damson akisindikizwa na ndugu na jamaa kuuaga mwili wa Marehemu.
  Mtoto wa Marehemu, John Damson akiweka Shada la Maua katika kaburi Baba yake baada ya kukamilisha taratibu za mazishi katika Makaburi ya Wireless, Temeke Jijini Dar es Salaam.
  Umati wa ndugu na jamaa waliojitokeza katika mazishi ya aliyekuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Dar es Salaam(TIA) Marehemu Sydney Damson ambaye amezikwa leo Julai 27, 2014 katika Makaburi ya Wireless, Temeke Jijini Dar es Salaam(Picha na Lucas Mboje).

  0 0

  Wadau Bw.Suleiman Saleh na Bw.Iddi Seif Bakari wa Washington DC, Markani,  wanapenda kuwatakia Watanzania wote Iddi yenye  kheri nyingi na utulivu.Tunamshukuru Mungu kwa kutujaalia Ramadhani njema.

  0 0

  Courtesy of KTN

  0 0

  Katika kuendeleza wajibu wake wa kutoa mafunzo ya muda mfupi, Chuo cha Diplomasia kimeendesha mafunzo ya juma moja ya Itifaki na Uhusiano ‘PROTOCOL AND PUBLIC RELATIONS’ 
  Mafunzo haya yalilenga kuwaongezea uwezo maafisa mbali mbali kutoka serekalini na sekta binafsi. Mafunzo haya ni muendelezo wa mafunzo ya muda mfupi yatolewayo na Chuo cha Diplomasia, mathalan usuluhishi na utatuzi wa migogoro (Conflict Resolution and Mediation skills) na Itifaki na Uhusiano ( Protocol and Public Relations)
  Mafunzo hayo yalihusisha maofisa wa kada mbalimbali kutoka idara za Serikali na sekta binafsi kama Benki Kuu ya Tanzania, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Chuo cha Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Meya Kinondoni, NSSF, Idara ya Uhamiaji, Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Umoja wa Mataifa (UN) na Clouds Media.

  Mafunzo hayo ya juma moja yaliyofanyika Kurasini Dar es salaam, washiriki walijifunza jinsi ya kuratibu itifaki za dhifa, sherehe za kitaifa na mikutano mingine mbali mbali. Pia walijifunza Diplomasia, uhuisiano wa umma na namna bora ya kuandaa taarifa kwa ajili ya mawasiliano na umma.
  Akifunga mafunzo hayo, Mkuu wa Idara ya Utafiti, Uchapishaji, Ushauri na Kozi fupi, Bw. Juma M. Kanuwa alisisitiza kwamba mafunzo hayo yatawasaidia maofisa hao kuboresha utendaji wa kazi zao. 
  “Kazi zinazohusiana na itifaki na uhusiano wa umma (Protocol and Public Relations) zinahitaji utaalam ambao utamfanya mtu aweze kutimiza majukumu yake kwa ufasaha na kufikia malengo na matokeo mazuri. Hivyo mafunzo haya ya Itifaki na mengine yote yanayotolewa na Chuo cha Diplomasia yana lengo la kuwajengea uwezo na utaalam washiriki wote ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kupata matokeo bora,” alisema.


  Akaongeza kuwa, kutokana na uhitaji mafunzo haya  yatarudiwa tena Tarehe 18 -22 Agasti 2014 hapa chuo cha Diplomasia, na kuwataka wale wote wanaohitaji wafike chuoni ama kupiga namba 0713667303 kwa maelezo zaidi na kupewa utaratibu.


  Kwa kawaida wawezeshaji wa mafunzo hayo ya muda mfupi katika Chuo cha Diplomasia, huwa ni mabalozi na wakufunzi waliobobea katika mambo ya Diplomasia na hivyo kuwapa washiriki uzoefu na mafunzo ya kiutendaji zaidi ili kuwajengea uwezo na ufanisi katika kuboresha majukumu yao. 

  Mshiriki Baby Kabaye wa Clouds Media akionesha cheti chake kwa furaha
  Mshiriki Godfrey Makupa wa GRM Productions akifurahia cheti chake
  Washiriki wakiwa darasani
  Mshiriki Baby Kabaye wa Clouds Media akifafanua jambo.
  Imetolewa na Shoo Innocent, Afisa Uhusiano


  0 0

  Ndugu Wanajumuiya,

  Mkutano wa Wanajumuiya wote utafanyika Jumamosi, tarehe 2 Agosti 2014 kwenye Jengo la Ubalozi address hii: 30 Overhill Rd, Mount Vernon, NY 10552 (Pale pale tulipofanyia uchaguzi mwaka jana, 2013), kuanzia saa nane mchana hadi saa moja jioni. 

  Mkutano utajadili maendeleo ya Jumuiya, tulipotoka na tunakoelekea. Katika Mkutano huu wamajumuiya watapata fursa ya:

  ·      Kusikia kutoka kwa kila kiongozi wa Jumuiya ni nini kila kiongozi alichokifanya tokea achaguliwe Oktoba 2013 mpaka sasa;

  ·      Kusikia jinsi ya Bodi na Kamati Kuu zinavyofanya kazi pamoja na ni nini “future” ya Jumuiya kwa ujumla;

  ·      Kupata taarifa ya mahesabu kutoka kwa Mweka Hazina;

  ·      Kupata Taarifa ya Katibu kuhusu Jumuiya tangu Mwaka Jana Oktoba mpaka sasa;

  ·      Kuuliza maswali na kutoa mapendekezo ya nini wanachotaka kifanyike katika kipindi kingine cha miezi sita ijayo.

   “please, save this date for our community meeting”. 
  Ukipata taarifa hizi tunaomba umwambie mwenzako. Na tunawaomba wote mje kwa wingi tarehe 2 Agosti 2014 kwenye mkutano wa Jumuiya yetu.

  Kutakuwepo na vinywaji na refreshments.

  Asanteni, na kwa niaba ya viongozi wote,

  Katibu,
  Deogratius Mhella.
  New York Tanzanian Community.

  0 0

  TAHADHARI!!
  Kama unaendesha Gari mida ya Usiku, na ghafla ukaona Mayai (Eggs) yamerushwa na kupiga kwenye KiOO cha Gari yako cha mbele, tafadhari sana USISIMAME, Usiwashe WIPER na wala usimwage MAJI kwenye KIOO chako cha mbele, sababu Mayai na Maji hubadilika kuwa maziwa na kufanya kitendo hicho utazuia kabisa uwezo wako kuona MBELE kiasi cha kukulazimu kusimama na kusababisha KUVAMIWA na MAJAMBAZI. Na Majambazi wakishakuvamia sihitaji kukueleza nini kinatokeaga…. Mstue mwanzako ni moja ya Mbinu zitumikazo na WEZI.

  “Ujumbe huu umeletea kwenu na watu wa BONGO”
  Karibu Sana


  WARNING!!
  IF YOU ARE DRIVING AT NIGHT AND EGGS ARE THROWN AT YOUR WINDSCREEN, DO NOT STOP TO CHECK THE CAR , DO NOT OPERATE THE WIPER AND DO NOT SPRAY ANY WATER, BECAUSE EGGS MIXED WITH WATER BECOME MILKY AND BLOCK YOUR VISION UP TO 92.5%, AND YOU ARE THEN FORCED TO STOP BESIDE THE ROAD AND BECOME A VICTIM OF THESE CRIMINALS. THIS IS A NEW TECHNIQUE USED BY GANGS.
  SO PLEASE INFORM YOUR FRIENDS AND RELATIVES.

  Thank You.

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na maelfu ya Waumini wa Karismatiki Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam katika maombi maalumu kwa ajili ya kuliombea Taifa yaliyofanyika Kituo cha Karismatiki, Ubungo jijini Dar es Salaam. 
  Waziri Chikawe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo aliyataka Makanisa nchini kudumisha amani na utulivu na kuendelea kuliombea Taifa na kuepuka kuingia katika migogoro mbalimbali ambayo itasababisha taifa kuingia katika uvunjifu amani makanisani. 
  Aidha, Chikawe aliongeza kuwa migogoro katika Makanisa na Madhehebu mbalimbali nchini imekuwa mingi katika kipindi hiki ambapo migogoro hiyo inasababishwa na ubinafsi wa viongozi, kutofuata Katiba na Ubadhirifu wa mali za Kanisa. 
  Kutokana na migogoro hiyo Chikawe alisema “Serikali haitavumilia vitendo vya uvunjifu wa amani makanisani na ikibidi itafuta usajili wa madhehebu na makanisa yenye migogoro ili kuepusha shari”.
   
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto) akiungana na maelfu ya Waumini wa Karismatiki Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam katika maombi maalumu kwa ajili ya kuliombea Taifa. Maombi hayo yalifanyika katika Kituo cha Karismatiki, Ubungo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka "FFU Ughaibuni" yenye makao yake nchini Ujerumani, inawapa mkono wa IDD el Fitr wadau wote wa ndani na nje ya Tanzania.
  Sherehekeeni sikuu ya EID MUBARAKA kwa amani na furaha

  EID MUBARAKA ! EID MUBARAKA ! EID MUBARAKA
  msikose kusikiliza at www.ngoma-africa.com 

  0 0

  Picha kwa hisani ya Diamond Platinumz blog

  0 0
 • 07/27/14--15:54: Article 5

 • 0 0


older | 1 | .... | 518 | 519 | (Page 520) | 521 | 522 | .... | 3285 | newer