Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 517 | 518 | (Page 519) | 520 | 521 | .... | 3348 | newer

  0 0

  KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imetoa msaa wa vyakula kwa vituo vitatu vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu vya jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuvisaidia viweze kusherehekea vizuri siku kuu ya Eid El Fitr. 

  Msaada huo wenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 3 umekabidhiwa na Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, ambaye alisema utaratibu huo ni wakawaida kwa kampuni yao kusaidia makundi na taasisi na idara anuai kwa masuala ya kijamii. 

  Bi. Mwakalebela alivitaja vituo ambavyo vimekabidhiwa msaada huo ni pamoja na Kituo cha Watoto Yatima cha Mama Theresa kilichopo Mburahati, Kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni na Kituo cha Chakuwama cha Sinza vyote vya jijini Dar es Salaam. 

  “…Msaada huu ni maalum kwa ajili ya kusherehekea siku kuu ya Eid El Fitr, jambo hili la leo ni utaratibu wa kampuni ya TTCL kusaidia makundi, taasisi na idara mbalimbali kuhusu mambo yanayohusu maendeleo na ustawi wa jamii,” alisema Bi. Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura. Msaada uliotolewa kwa vituo hivyo ni pamoja na mchele, mafuta ya kupikia, sukari, unga, unga wa sembe, maharage pamoja na katoni za juisi za maboksi.

   Kwa upande wao wawakilishi wa vituo hivyo waliishukuru Kampuni ya TTCL kwa uamuzi wake wa kuwakumbuka watoto yatima ili nao waweze kusherehekea vizuri siku kuu ya Eid El Fitr kama ilivyo kwa familia nyingine majumbani.
  Wawakilishi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mama Theresa kilichopo Mburahati, wakipokea msaada wao toka kwa Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL. Wawakilishi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mama Theresa kilichopo Mburahati, wakipokea msaada wao toka kwa Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.Vikundi vya Watoto Yatima vya Mama Theresa kilichopo Mburahati, Kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni na Kituo cha Chakuwama cha Sinza katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea zawadi zao jijini Dar es Salaam. Vikundi vya Watoto Yatima vya Mama Theresa kilichopo Mburahati, Kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni na Kituo cha Chakuwama cha Sinza katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea zawadi zao jijini Dar es Salaam.Wawakilishi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mwandaliwa cha Mbweni wakipokea msaada wao toka kwa Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL. Wawakilishi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mwandaliwa cha Mbweni wakipokea msaada wao toka kwa Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL. 

  0 0

  Waziri katika Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Mheshimiwa Prof. Mark Mwandosya alifanya ziara ya kutembelea Mamlaka za Udhibiti wa huduma za umma na shughuli zingine za kiuchumi kwa nia ya kufahamu utendaji, mafanikio na changamoto zinazowakabili katika kutekeleza majukumu waliyokabidhiwa na Serikali kuyafanya. Ziara hiyo ambayo ilianza tarehe 21 hadi 23 Julai, 2014 ilihusisha Mamlaka za udhibiti za SUMATRA, EWURA, TCAA, TCRA, TIRA na SSRA.

  Katika ziara yake hiyo Waziri Prof. Mwandosya alieleza kuwa madhumuni ya ziara yake ilikuwa ni kujifunza na kubalishana uzoefu katika shughuli za udhibiti hapa Tanzania. Waziri Prof. Mwandosya alieleza kuwa shughuli za udhibiti Tanzania zilianza rasmi kwa kuanzisha Mamlaka za Udhibiti kwa kujibu wa sheria zilizopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania takriban miaka 10 iliyopita.

  Waziri Prof. Mwandosya alieleza kuwa pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika kutekeleza majukumu yao, Mamlaka za Udhibiti hapa nchini bado zina changamoto nyingi ambazo inabidi kukabiliana nazo kwa kujifunza na kubadilisha uzoefu. Kipindi cha miaka 10 kinatosha kuweza kutathimini tulikotoka, tulipo na tunakoelekea. Hii ni pamoja na kuweka malengo ya kukabiliana na changamoto za kuwa na uchumi mzuri kwa miaka kumi ijayo.

  Waziri Prof. Mwandosya aliendelea kueleza kuwa Mamlaka za Udhibiti zinapaswa kujiuliza kuwa zimefanya nini katika kutekeleza majukumu waliyokabidhiwa na Serikali, nini kimesababisha wao kushindwa kutekeleza baadhi maeneo yao ya udhibiti na kwa kiwango gani mahusiano yao na Serikali yamesaidia au kuathiri utendaji wa mamlaka hizo. Na mwisho ili kupata suluhu mamlaka zinashauri nini kifanyike ili mahusiano yao na Serikali yaweze kuboresha utendaji wao.

  Aidha Waziri Prof. Mwandosya alitoa ujumbe kwa watendaji wa Mamlaka za Udhibiti kuwa pamoja na kwamba vyombo vya udhibiti vilianzishwa kwa ajili ya kusimamia huduma za umma (utilities) lakini kimsingi vyombo hivyo vilianzishwa kwa lengo kuu la kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi katika nchi. 

  Waziri Prof. Mwandosya alitoa angalizo kuwa kuna haja ya kuongeza wigo kutoka kwenye udhibiti huduma za umma na kushirikisha pia udhibiti wa shughuli za kiuchumi zikiwemo za bima na hifadhi ya jamii. Pamoja na mamlaka hizi kusimamia sekta tofauti lakini zinakabiliwa na changamoto zinazofanana. Kutokana na hali hiyo Waziri Prof. Mwandosya alishauri kuna haja kuwa na chombo kimoja ambacho kitajumuisha vyombo vyote vya udhibiti kwa ajili ya kujadiliana na kubadilishana uzoefu katika kutekeleza majukumu yao.

  Waziri Prof. Mwandosya pia aliwaasa Mamlaka hizi za udhibiti kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo badala ya kufuata maelekezo au kufanya maamuzi ya kuwafurahisha wanasiasa. Muelekeo ni kwamba kunakuwepo na huduma kwa umma ili wananchi waweze kuchangia ipasavyo katika uchumi wa nchi.
  Mheshimiwa Prof. Mark Mwandosya akizungumza na Uongozi wa Mamlaka ya Udhibiti Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) alipotembelea ofisi za Mamlaka hiyo katika ziara yake tarehe 21 Julai, 2014. Kushoto kwa Waziri Prof. Mwandosya ni Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA Bwana Gilliard Ngewe. 
  Baada ya majadiliano na Uongozi wa SUMATRA Mheshimiwa Prof. Mark Mwandosya alimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA Bwana Gilliard Ngewe kitabu cha Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi Tanzania alichokiandika Prof. Mwandosya.
  Mheshimiwa Prof. Mark Mwandosya katika picha ya pamoja na Uongozi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) alipotembelea ofisi za Mamlaka hiyo katika ziara yake tarehe 21 Julai, 2014. Kulia kwa Waziri Prof. Mwandosya ni Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Bwana Felix Ngamlagosi.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Dr Joel Bendera Leo amewaongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Morogoro kumzika Mke wa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini, Mh lnocenti Kalogeris. Watu mbali mbali wakiwemo wabunge,wakuu wa mikoa wastaafu na watu mashuhuri wamefurika nyumbani kwa mbunge huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro 
   Mkuu wa mkoa akimpeleka Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh  Innocent Kalogeris  kupokea mwili wa mpendwa mke wake,kulia ni dada wa mbunge huyo.

   Marehemu Elizabeth Kapoloma enzi za Uhai wake , Bi,Elizabeth Kapoloma alifariki Alhamisi Kwa Ugonjwa Moyo.
   Mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani kwake kwajili ya Heshima za Mwisho na Ibada kabla ya Mazishi leo    


    Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh Dk Joel Bendera akimbembeleza Mume wa marehemu Mhe lnocent Kalogeris
  MATUKIO NA VIJANA

  0 0


  0 0


  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Mwigulu Nchemba akiwapungia wananchi alipokuwa akiingia kuhutubia katika mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Furahisha, jijini Mwanza leo. ambapo alizungumzia utata kuhusu Umoja wa Katiba ya Wananchi na kufutwa kwa baadhi ya misamaha ya kodi
  Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Mwigulu Nchemba akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Furahisha, jijini Mwanza leo. ambapo alizungumzia utata kuhusu Umoja wa Katiba ya Wananchi na kufutwa kwa baadhi ya misamaha ya kodi. 
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   We are taking this opportunity to thank our entire fans around the globe for your support to this band. It is your support that makes the Ngoma Africa band prosper, without you there will be no success!
  Please, we ask you again to keep on supporting and let the band be on the top most position in every event, festival, media etc.
  Let others around you join the band at www.ngoma-africa.com
  here they will have the opportunity to enjoy music at:
  Yours Sincerely
  The Ngoma Africa Band
   In action  
   Dedicated to making our fans happy
   Always full house
  Thank you...Thank you....Thank you... Thank you...

  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea maduka mbali mbali ya nguo na viatu katika maeneo ya Mlandege, Mchangani na Darajani Zanzibar jana usiku, kuangalia hali ya upatikanaji wa bidhaa hizo katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Eid- El-Fitri. Picha zote na Salmin Said, OMKR
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea maduka mbali mbali ya nguo na viatu katika maeneo ya Mlandege, Mchangani na Darajani Zanzibar
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na wafanyabiashara alipotembelea maduka mbali mbali ya nguo na viatu katika maeneo ya Mlandege, Mchangani na Darajani Zanzibar

  "Asalaam aleikhum...."
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimia wananchi alipotembelea  maduka mbali mbali ya nguo na viatu katika maeneo ya Mlandege, Mchangani na Darajani Zanzibar
  "...Hii bei gani?...

  0 0

  Jeshi la Polisi Tanzania linapenda kutoa shukrani za dhati kwa wananchi wote, vyama vya siasa, taasisi mbalimbali za serikali, madhehebu ya dini, asasi za kiraia na vyombo vya habari kwa ushirikiano wa dhati katika kusimamia masuala ya amani na usalama hapa nchini. 

  Tunapoelekea kipindi hiki cha kusherehekea sikukuu ya Eid-El-Fitr, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote kuwa makini na kusheherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani. 
  Ikumbukwe kuwa, wananchi wenye imani ya kiislam na hata madhehebu mengine hutumia muda huo kwenda kuabudu pamoja na muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya starehe. Uzoefu umeonyesha kuwa baadhi ya watu hutumia kipindi hicho cha sikukuu kama mwanya wa kufanya matukio ya uhalifu kutokana na mikusanyiko hiyo ya watu. 
  Jeshi la Polisi linapenda kuwaondoa hofu wananchi wote kuwa, limejipanga kikamilifu kuhakikisha wananchi kote nchini wanasherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu. Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote, aidha,  tunapenda kuwatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara, kuwa makini kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kwenda mwendo kasi na kutumia vilevi wawapo kazini. 
  Katika kuhakikisha usalama kwenye kumbi za starehe, wamiliki wa kumbi hizo wazingatie uhalali na matumizi ya kumbi zao katika uingizaji wa watu kulingana na uwezo wa kumbi hizo, badala ya kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita kiasi.
  Jeshi la Polisi linapenda kuwashukuru wale wote ambao tayari wamefunga kamera za CCTV katika maeneo yao ya starehe, hususani yale yanayokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu, yakiwemo maduka, hoteli na maeneo ya benki. Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea kuwasisitiza wale ambao bado hawajaweka kamera hizo, kuweka ili ziweze kusaidia kubaini wahalifu na hata kurahisisha ukamataji endapo uhalifu unatokea. 
  Vilevile, wazazi wawe makini na watoto wao na hasa disko toto, ili kuepuka ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara juu yao. 
  Aidha wananchi wachukue tahadhari watokapo kwenye makazi yao wasiache nyumba wazi ama bila mtu na watoe taarifa kwa majirani zao, na pale wanapowatilia mashaka watu wasiowafahamu wasikae kimya bali watoe taarifa haraka kwenye vituo vya Polisi vilivyo karibu nao au kwa namba ya simu ifuatayo 0754 785557, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa haraka.
   Imetolewa na:
  Advera John Bulimba - SSP
  Msemaji wa Jeshi la Polisi.

  0 0

  Mkufuzi wa mafunzo ya waamuzi wa mchezo wa masumbwi Ally Bakari 'Champion' kushoto akiwaelekeza baadhi ya marefarii waliojitokeza katika mafunzo hayo yaliyo andaliwa na chama cha ngumi za kulipwa TPBC yaliyoanza Ilala CCM Dar es salaam juzi na kumalizika jumamosi  hii 
  Mkufuzi wa mafunzo ya waamuzi wa mchezo wa masumbwi Ally Bakari 'Champion' kulia akisisitiza jambo kwa wakati wa mafunzo hayo uku marefarii waliojitokeza wakimsikiliza kwa makini kutoka kushoto ni Kondo Nassoro, Sako Mtlya na Buchato Michael 
  Mkufuzi wa mafunzo ya waamuzi wa mchezo wa masumbwi Ally Bakari 'Champion' akitoa maelekezo kwa mabondia na marefarii kabla ya kupigana wakati wa mafunzo kwa vitendo ya urefarii wa mchezo huo
  BAADHI YA MAREFARII WALIOSHILIKI KATIKA KOZI HIYO KUTOKA KUSHOTO NI BUCHATO MICHAEL,PEMBE NDAVA,HAMISI KIMANGA,RAJABU MHAMILA 'SUPER D' ALLY BAKARI,Ayubu Tezikoma NA SAKO MTLYA

  0 0

  Kwa hisani ya ITV

  0 0
 • 07/26/14--14:21: cheka unenepe


 • 0 0

  Marehemu Henry Lymo maarufu kama Kipese.
  Na Dixson Busagaga
  TASNIA ya Habari na michezo mkoani Kilimanjaro imepata pigo kufuatia kifo cha ghafla cha Mtangazaji wa kituo cha radio cha Moshi FM Henry Lyimo, maarufu kama Kipese. Marehemu Kipese amefariki dunia usiku wa jana akiwa njiani akitokea Rombo katika eneo la njia Panda, Himo,  baada ya pikipiki aliyokuwa akitumia kugongana na pikipiki nyingine. 

  Taarifa za awali zinasema Marehemu Kipese alikuwa akitokea wilayani Rombo ambako amekuwa akifanya shughuli zake na kwamba wakati anarejea ndipo mauti yakamfika baada ya kuumia vibaya katika ajali hiyo.

  Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Kilema wilayani Rombo kungojea taratibu nyingine toka kwa ndugu zake.
  Tayari makundi mbalimbali ambayo marehemu amekuwa karibu nayo kwa shughuli za kikazi yametoa taarifa za masikitiko kufuatia kifo cha Kipese huku yakipanga kukutana asubuhi hii kwa ajili ya kupanga mambo mbalimbali kwa ajili ya kufanikisha mazishi hayo.

  Kundi la kwanza ni kundi la waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro kupitia klabu yake ya Media Club of Kilimanjaro wamepanga kukutana asubuhi hii katika eneo la Posta. Kundi la pili ni la wafanyakazi wote wa Moshi FM radio ambako marehemu alikuwa akifanya kazi hadi Mauti yanamkuta wamepanga kukutana asubuhi hii kuanzia majira ya saa 2.

  Kundi la tatu ni la wadau wa michezo mkoani Kilimanjaro ambako licha ya kwamba Marehemu Kipese alikuwa mtangazaji wa kipindi cha Michezo katika radaio aliyokuwa akifanyia kazi pia alikuwa mwamuzi wa mchezo wa soka. Wadau hao wamepanga kukutana katika ofisi za chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro (KRFA) kujadili namna ya kushiriki msiba huo mzito kwa tasnia ya habari na michezo.
  Globu ya Jamii inaungana na famili, ndugu jamaa na marafiki wa marehemu katika kuomboleza msiba huu mzito. 

  Matokeo ya Utafutaji

  1.  Inna Lillahi Wa Inna Ilahi Raaji'oon 


  0 0

   Msimamizi wa Uchaguzi Bw. Alfred Kayombo (kulia) akimtangaza mshindi wa nafasi ya mwenyekiti Bw. Ibrahim Ngogo.
  Kwa mara ya kwanza katika historia, chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Makete mkoani Njombe kimefanya uchaguzi wa uongozi mbalimbali ambapo Bw. Ibrahim Ngogo amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa ngazi ya wilaya.

  Na Edwin Moshi, Makete
  Akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi huo Bw. Alfred Kayombo amesema Bw. Ibrahim Ngogo amepata kura 25 akifuatiwa na Isaac Sanga aliyepata kura 6 na Shaaban Mkakanze aliyepata kura 1.
  Bw. Kayombo amesema kutokana na umuhimu wa demokrasia ndani ya chama hicho, wameamua kufanya uchaguzi huo kwa mara ya kwanza toka chadema iingie wilayani hapa, hivyo kuonesha kuwajali wanachama wake
  Mbali na viongozi hao wa juu wa chama pia Bw. Lazaro Chaula amechaguliwa kuwa katibu mwenezi wa Chadema wilaya ya Makete kwa kupata kura 30, Bi. Rose Mbilinyi amechaguliwa kuwa Mtunza hazina wa wilaya kwa kupata kura 26.
  Aidha Bw. Atukuzwe Mahenge amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la vijana (BAVICHA) wilaya na Bw. Shadraack Mwachota akichaguliwa kuwa katibu wake na wote wamepita bila kupingwa.
  Bi. Beatrice Kyando amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la wanawake wa chadema wilaya (BAWACHA), Bi Christina Timoth akichaguliwa kuwa katibu wa BAWACHA, na Bi. Mariam Asheli akichaguliwa kuwa Katibu wa uhamasishaji wa BAWACHA na wote wamepita bila kupingwa.
  katika uchaguzi huo pia Bw. Abiud Elia amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la wazee kwa kura 3, Abeli Juma Sanga akipata kura 1 na kuchaguliwa kuwa Makamu mwenyekiti, pamoja na Simon Nyasanga kuwa katibu wa baraza la wazee wilaya.
  Katika hatua nyingine wamechaguliwa wajumbe 4 waliochaguliwa kuingia kwenye kamati tendaji ambao ni John Sanga, Patison Pela,Orignal Sanga na Alafat Msigwa, huku Bw.Illomo Werner Naftal akichaguliwa kuwa mwakilishi wa wilaya kwenye mkutano mkuu taifa.
  Akiahirisha mkutano huo mwenyekiti wa Chadema wilaya Bw. Ibrahim Ngogo amewasihi wajumbe kuondoa makundi na kutokubali kutumia kwa ajili ya kukibomoa chama na badala yake washikamane wawe kitu kimoja kukijenga chama.
  "Makamanda uchaguuzi umeisha haitakiwi tuwe na makundi, tushikamane kukijenga chama chetu, hilo ndilo la msingi kwa sasa, sisi viongozi mtupe ushirikiano" amesema Ngogo  0 0

  Shule ya chekechea na msingi ya Blue Tanzanite iliyopo Kata ya Endiamtu, Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, iliyoanzishwa mwaka 2008 na yenye wanafunzi 360, yazindua eneo lake na majengo yake.
  Mkurugenzi wa shule ya chekechea na msingi Blue Tanzanite iliyopo Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara, Raphael Alex Ombade  akizungumza kwenye sherehe za shule hiyo.
  Padri Pastory Kijuu wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozali Takatifu, iliyopo Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, akizungumza na wanafunzi wa shule ya Chekechea na msingi Blue Tanzanite, baada ya kuzindua kwa maombi, majengo na eneo  la shule. 
  Wanafunzi wa shule ya chekechea na msingi Blue Tanzanite ya Mtaa wa Sekondari, Kata ya Endiamtu, Mji mdogo wa Mirerani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakimuomba Mungu wakati wa uzinduzi wa majengo na eneo la shule yao jana, lililofanywa kwa njia ya sala na maombi yaliyoongozwa na Padri Pastory Kijuu wa Kanisa Katoliki Mirerani.
  Baadhi ya wanafunzi wa shule ya chekechea na msingi Blue Tanzanite iliyopo Mtaa wa Sekondari, Kata ya Endiamtu, Mji mdogo wa Mirerani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakishuhudia tukio la uzinduzi wa majengo na eneo la shule yao jana, lililofanywa na Padri Pastory Kijuu wa Kanisa Katoliki Mirerani. Picha na Joseph Lyimo

  0 0

   Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akitoa tamko kuhusu Bunge la Katiba litakaloanza Agosti 5, 2014 ambapo walishauri Bunge hilo likae wiki mbili badala ya miezi miwili kama ilivyopangwa ili kupunguza matumizi makubwa ya fedha za Umma. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Kamati na Uongozi Jukata Omar Ali Omar,  Meneja Habari na Mawasiliano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Kenny Ngomuo, Makamu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda na  Mratibu wa Jukata, Diana Kidara.
   Makamu Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda, akisoma tamko hilo.
   Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

  0 0

  Na Othman Khamis Ame, OMPR
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwa na wajibu na jukumu kubwa la kuwatunza na kuwathamini wazee wasiojiweza hivi sasa kutokana na mchango wao mkubwa walioutoa kwa nchi hii wakati wa kulitumikia Taifa lao. 
  Alisema mchango wa wazee hao umekuwa ukiendelea kutumiwa na wananchi walio wengi hapa nchini ikiwemo kigezo cha amani na utulivu kinachotokana na juhudi za wazee hao wakati wa kupigania utu wa mwafrika.
  Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati wa ziara yake fupi ya kuwasalimia Wazee wanaotunzwa katika Nyumba za Serikali za Welezo na Sebleni na kuwapatia zawadi ya nguo kwa ajili ya kusherehekea vyema siku Kuu ya Iddi El Fitri inayotarajiwa kufanyika mapema wiki ijayo. 
  Alisema wazee wa Taifa hili wametumia muda wao mkubwa wa kujenga mazingira bora ili kizazi chao kiendelee kuishi kwa amani na furaha tofauti na enzi zao zilizokumbwa na mitihani ya kutawaliwa jambo ambalo liliwakosesha uhuru wa kidemokrasia wa kufanya wanalolihitaji katika maisha yao. 
  Akitoa skurani kwa niaba ya wazee hao wa Welezo na Sebleni Mzee Omar Said alimpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa juhudi zake za kuendelea kufuatilia changamoto zinazowakabili wazee hao juhudi ambazo zimekuwa zikiwapa faraja wazee hao na kuendelea kujenga imani kwa Serikali ambayo inaelewa mchango wao katika ukombozi wa Visiwa hivi. 
  Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii, Vijana Wanawake na Watoto Bibi Asha Abdulla alisema Nyumba za Wazee ziliopo Welezo zimekuwa zikihudumia wazee wapatao 42 wakati zile la Sebleni zinahudumia wazee 46 wakiwa chini ya usimamizi wa Idara ya Ustawi wa Jamii iliyopewa jukumu la kuwahudumia wazee hao.
   Baadhi ya Wazee wa nyumba za Serikali za Welezo wakifutilia maelezo ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi alipowatembelea kwenye makazi yao.
   Balozi Seif akigawa zawadi kwa mmoja wa wazee wa Welezo alipowatembelea na kuwafariji wakiwa ndani ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani
   Balozi Seif akimkabidhi zawadi mmoja wa watumishi wa wazee wanaoishi katika nyumba za Serikali zilizopo Welezo nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
   Baadhi ya Wazee wa nyumba za Sebleni wakifuatilia hotuba ya Balozi Seif hayupo pichani wakati akijiandaa kuwapatia zawadi kwa ajili ya siku kuu ya Iddi el Fitri.

   Balozi Seif akibadilishana mawazo na baadhi ya wazee wa kike wanaotunzwa katika nyumba za Serikali zilizopo Sebleni Mjini Zanzibar.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akitoa zawadi kwa Wazee wa kiume wa Sebleni
  Mzee Omar Said wa Nyumba za Sebleni kwa niaba ya wazee wenzake wa Sebleni na Welezo akimshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar hayupo pichani kwa juhudi zake za kufuatilia changamoto zinazowakabili wazee hao.
  Picha na Hassan Issa wa  OMPR 


  0 0
 • 07/26/14--19:30: Article 5


 • 0 0  0 0


  Dj MusMus a.k.a Mussa Maingu, DJ DOC B, and DJ W6 on One and Two....

  KUSIKILIZA LIVE HIVI SASA BOFYA HAPA!
  Na kila Jumamosi 3-6pm ET
  For more CLICK HERE


older | 1 | .... | 517 | 518 | (Page 519) | 520 | 521 | .... | 3348 | newer