Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

RAIS KIKWETE AFUNGUA DARAJA LA RUHEKEI LINALOUNGANISHA WILAYA YA MBINGA NA WILAYA YA NYASA MKOANI RUVUMA

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katikati akifurahia kikundi cha Ngoma cha mkoa wa Ruvuma katika sherehe ya uzinduzi wa Daraja la Ruhekei lililopo katika barabara Mbinga –Mbamba bay mkoani Ruvuma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katikati akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli wa kwanza kulia wakifanya ishara ya kuweka jiwe la msingi na kufungua Daraja la Ruhekei linalounganisha kati ya Mbinga na Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria kufungua Daraja la Ruhekei lililopo katika Barabara ya Mbinga-Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, Mama Salma Kikwete pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali wakipita juu ya Daraja la Mto Ruhekei baada ya kulifungua mkoani Ruvuma. Daraja hilo ni kiungo muhimu kati ya Wilaya mpya ya Nyasa pamoja na Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) kushoto akizungumza na Mwenyekiti wa kamati ya Miundombinu Profesa Juma Athumani Kapuya (Mb) kabla ya uzinduzi wa Daraja la Ruhekei lililopo katika Barabara ya Mbinga-Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) katikati akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe wakati wakisubiri kuwasili kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mheshimiwa Dkt.Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya ufunguzi wa Daraja la Mto Ruhekei mkoani Ruvuma.

TAMASHA LA MATUMAINI 2014 LIVE: YEMI ALADE, SHILOLE KUONYESHANA KAZI AGOSTI 8, 2014

how germany won the world cup

$
0
0
By Alex Kajumulo
GERMANY WON THE 2014 WORLD CUP. People think Germany winning the world cup was a coincidence. If you know what is going in around soccer you have to stop watching soccer as fans and you need to start analyzing. Germany had a plan to win the World Cup this year they used Barcelona to win the World Cup.  Just how Spain used Barcelona to win the World Cup.
When Spain won the World Cup in 2010 they had ...nine players from Barcelona on on Spain's national team they had very good chemistry as you know Bayern Munich hired Pep Guardiola to coach Bayern Munich because they had nine players that play for Germany's national team. 
They hired him to work on the team chemistry to prepare those nine players for the World Cup. Now Spain and Germany had the same results. Nine players from Spain played for Barcelona and nine players from Germany played for Bayern Munich and the won the World Cup. 
This guy pep Guardiola is the one who helped those two countries to win the World Cup. So guys be smart when you watch soccer and when coaches are being transferred around. 
And when Germany playe brazil in the semi finals they used exactly Barcelonas attacking system. The Brazilian coach prepared them to think Germany was going to play long balls. Before he adjusted it was too late Anyway he didn't recognize the system they braught him in to help them out. Most of the kids are in the academy but registration but most of the time they send them back to play in street soccer. 
Right now soccer is played by low income people because they recognize that street level soccer players are the ones that have the ability to bring Germany to victory. Klinsmann started bringing good players who are from low income that's play in street soccer some in Germany and some in u.s. This time brazil got punished because they used too many players from academy's who have no creativity. 
Meanwhile Germany stopped doing that and started getting players from the streets. America's economy is in trouble because they send a bunch of their products to be made in china. 
Brazil is in trouble now because the send their players to be manufactured somewhere else. Barcelona does the same thing. They register their players in the academy but send them back to play in the streets.

JUMUIYA YA WATANZANIA WALIOSOMA KOREA (KOICA/KAAT) YAPATA UONGOZI MPYA

$
0
0
Na Saidi Mkabakuli 
Jumuiya ya Watanzania waliosoma Korea imefanikiwa kupata uongozi mpya, utaongoza umoja wa Watanzania hao kwa muda wa miaka miwili. Waliochaguliwa kuongoza KAAT ni pamoja na Bw. Stephen Katemba ambaye amechaguliwa kuwa Rais wa Jumuiya. Bw. Katemba atasaidiwa na Bw. Bukheti Juma (Makamu wa Rais, Zanzibar) na Bw. Emmanuel Burton (Makamu wa Rais, Tanzania Bara). 
Katika nafasi ya Uweka Muweka Hazina, aliyechaguliwa ni Bw. Stephen Matee, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) ulio chini wa Mama Anna Mkapa. 
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa rasmi jukumu la kuiongoza Jumuiya hiyo, Bw. Katemba ambaye ni Mtaalamu wa Masuala ya Uchumi na Biashara za Kimataifa, amesema kuwa Tanzania ina fursa kubwa katika eneo la biashara za kimataifa kuwa kuzingatia rasilimali zilizopo nchini na kuchagiza kuwa fursa hizo zinaweza kutumiwa ipasavyo kwa kujitangaza tu. 
Bw. Katemba aliongeza kuwa kama Watanzania tukiwa na uzalendo wa dhati na kuwa mabalozi wazuri, Tanzania itakuwa na uhakika wa kukamata masoko makubwa ikiwemo Korea na Bara la Asia kwa ujumla. “Kwa mfano kwa mujibu wa hali ya uchumi wa Taifa, kwa mwaka 2013, mwenendo wa biashara ya bidhaa na huduma nje haukuwa wa kuridhisha ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2012. Thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma nje ilipungua kwa asilimia 1.7 kutoka Dola za Kimarekani milioni 8,675.6 mwaka 2012 hadi Dola milioni 8,532.0,” alisema. 
Kwa mujibu wa Bw. Katemba kuwa ili kufikia malengo ya kimkakati ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ulio chini ya Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambao umelenga kufungulia fursa za ukuaji wa uchumi, Tanzania haina budi kufikia malengo ya kikao cha tisa cha Shirikisho la Biashara Ulimwenguni (WTO) ambalo linalenga kuziwezesha kibiashara nchi wanachama kuboresha biashara zao.
 “Katika kikao cha tisa cha WTO, Mawaziri wa nchi wanachama 159 wa Shirikisho walikubaliana kuwa na “Mpango wa Bali” ambao unalenga kuziruhusu nchi zinazoendelea kuwa na fursa zaidi ya kuzalisha chakula cha akiba, kuinua kiwango cha biashara kwa nchi changa na kusaidia maendeleo ya nchi changa kibiashara. Hivyo, tunaweza kufikia malengo haya kwa kutangaza bidhaa zetu hasa za vyakula kwa mataifa yenye uhitaji wa bidhaa hizo,” alifafanua.
 Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mwakilishi Mkazi wa KOICA, Bw. Seung-Beom Kim alisema kuwa Tanzania ina bidhaa nyingi ya kuziuza kwenye soko la Korea na kutolea mfano mchele wa Kyela kuwa ni bidhaa nzuri kwenye soko hilo.
 Rais Mpya wa Jumuiya ya Watanzania waliosoma Korea (KAAT), Bw. Stephen Katemba (Kulia) akizungumza mara baada ya kuchaguliwa. Anayemsikiliza ni Mwakilishi Mkazi wa KOICA, Bw. Seung-Beom Kim (Kushoto).
 Viongozi wapya KAAT na viongozi wa zamani wakipongezana mara baada ya uchaguzi huo.
 Makamu wa Rais wa KAAT aliyemaliza muda wake, Bibi Margaret Alfanies (Katikati) akizungumza machache mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo. Kushoto ni aliyekuwa Muweka Hazina wa KAAT, Bibi Emilia Maingu na kulia ni Bw. Stephen Matee ambaye ni Mweka Hazina mpya.
 Makamu wa Rais wa KAAT aliyemaliza muda wake, Bibi Margaret Alfanies (Wapili Kulia) akikabidhi nyaraka za KAAT kwa uongozi mpya. Kutoka kushoto pichani ni Bw. Emmanuel Burton (Makamu wa Rais, Tanzania Bara), Bw. Bukheti Juma (Wapili kushoto) ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar). Wengine ni Rais Mpya Bw. Stephen Katemba (Katikati) na Bw. Stephen Matee (Kulia)ambaye ni Muweka Hazina mpya.
 Uongozi mpya wa KAAT wakizungumza na Mwakilishi Mkazi wa KOICA, Bw. Seung-Beom Kim 
Wakiwa katika picha ya pamoja ni uongozi mpya wa KAAT na baadhi ya viongozi wa zamani wa Jumuiya hiyo.

Rais Kikwete ziarani Nyasa

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa Daraja la Ruhekei zilizofanyika katika kijiji cha Mkaole wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma leo.Kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli.
Daraja la Ruhekei lililozinduiwa rasmi leo na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika kijiji cha Mkaole wilyani Nyasa mkoani Ruvuma leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mamia ya wakazi wa mji Songea wakati alipoingia katika uwanja wa michezo wa Majimaji mjini humo ambapo aliwahutubia katika mkutano wa Hadhara.Rais Kiwete yupo katika ziara ya kikazi ya wiki moja mkoani Ruvuma kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo(picha na Freddy Maro).

SOMO LA MAPISHI TOKA KWA CHEF ISSA LEO..........

Prof. Mchome awataka Watumishi wa Wizara ya Elimu kuwa Wabunifu

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kuwa wabunifu zaidi na kuhakikisha kuwa wanachokibuni kiwe kinatekelezwa na kuchukua hatua kwa wasiotekeleza maelekezo ya kisera pamoja na kuwazawadia wanaotekeleza kwa ufanisi maelekezo yanayotolewa.

“Watumishi wa Wizara hii tunatakiwa tujiulize tunafanya ubunifu gani ili kuhakisha wahitimu katika ngazi mbalimbali wanapata maarifa yanayotakiwa na wanaoweza kusaidia nchi katika kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali,” alisema Profesa Mchome.

Profesa Mchome alikuwa akizungumza na Watumishi wa Makao Makuu na Taasisi zilizoko chini ya Wizara hiyo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Julius Nyerere International Convention Centre), Ijumaa 18 Julai, 2014 ikiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana na watumishi hao na kujadiliana namna bora zaidi ya kuboresha utendaji kazi katika wizara.

Aidha, Profesa Mchome alizungumzia umuhimu wa kuboresha Muundo wa Wizara hiyo ili kuwezesha namna bora ya kutekeleza majukumu yake baada ya ugatuaji wa uendeshaji na usimamizi wa shule za Sekondari kwenda kwenye Halmashauri chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI na kwa kufuata Hati Idhini iliyounda Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliyotolewa na Mheshimiwa Rais, Desemba 2010.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome akiongea na Watumishi wa wizara yake katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Julius Nyerere International Convention Centre), Ijumaa 18 Julai, 2014 ikiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana na watumishi hao na kujadiliana namna bora zaidi ya kuboresha utendaji kazi katika wizara.
Mmoja wa Watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Grace Naburi akizungumza katika kikao cha Wafanyakazi wa wizara hiyo na Katibu Mkuu wao Profesa Sifuni Mchome.
Watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakiimba wimbo wa Mshikamano katika kikao cha Wafanyakazi wa wizara hiyo na Katibu Mkuu wao Prof. Sifuni Mchome.
Mmoja wa Watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza katika kikao cha Wafanyakazi wa wizara hiyo na Katibu Mkuu wao Profesa Sifuni Mchome.

MEYA KINONDONI MH. YUSSUF MWENDA AFUTURISHA WANANCHI WA MANISPAA YAKE

$
0
0
Meya wa Manipaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda amewataka wananchi wa Manispaa yake na nchini kote kuwasaidia watoto yatima na wasiojiweza ili kupunguza tatizo la watoto wa mitaani na mayatima ambao wamekuwa wakiongezeka kila siku jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa futari aliyoiandaa kwa wananchi wa Manispaa yake, viongozi wa Kiserikali na kidini, Dar es Salaam juzi Meya huyo alisema kuwa Manispaa yake ni kubwa na hivyo endapo watu watachukua maamuzi ya kusaidia watoto hao basi tatizo hilo litakuwa limepungua kwa kiasi kikubwa katika Manispaa hiyo na jijini kwa ujumla.

“Wito wangu kwenu tuwasaidie watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu katika Manispaa yetu ili kuondoa tatizo hili la watoto wanaozagaa mitaani kwani nao wana haki kama walivyo watoto wengine wenye wazazi na wanaoishi kwenye mazingira mazuri. Nazungumza hili kwa kuwa hili ni tatizo sugu katika Manispaa yetu.” Alisema.

Aidha aliwahakikishia wananchi hao kuwa Manispaa itaendelea kufanya kila inachoweza kuhakikisha inaboresha hali ya maisha ya wananchi wake bila kujali itikadi za kisiasa wala kidini ili kuondoa umasikini kwa wananchi hao. Pia alisema Manispaa itaendelea kusimamia kampeni yake ya kuweka mazingira safi ya Manispaa kwa kuhakikisha inatimiza malengo yake iliyojiwekea.

“Niseme kuwa sisi (Manispaa) ndio tunaoondoa taka kwa asilimia 75 hapa jijini, nawapongeza Madiwani wangu kwa kusimamia vema kampeni mbalimbali tunazozianzisha katika Halmashauri yetu.” Alisema

Kwa upande wake Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Saluma aliwahimiza waumini wa dini ya Kiislam kuzidisha ibada katika kumi hili la mwisho la mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kusema kuwa endapo muumini atakutwa na usiku wa lailatul qadir basi ni sawa na kufunga miezi 1000 ambayo ni sawa na miaka 83.
Shehe wa Wilaya ya Kinondoni, Alhaj Mohamed Mwenda (mbele) akiowaongoza waumini katika swala ya Magharibi, kabla ya kupata futari iliyoandaliwa na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda kwa wananchi wa Manispaa yake, viongzoi wa kiserikali na kidini, Dar es Salaam jana. Kutoka kulia (mstari wa mbele) ni Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaabn Bin Simba, Imam wa Msikiti wa Alfarouq, Mwita Kambi, Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda, viongozi mbalimbali wa dini na wa kiserikali.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kulia) akiwaongoza wageni mbalimbali kupakua futari aliyoindaa kwa wananchi wa Manispaa yake, viongozi wa kiserikali na wa kidini, Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Shehe wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (wa pili kushoto0 akipata futari pamoja na Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban Bin Simba (kushoto kwake), Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) na Shehe wa Wilaya ya Kinondoni, Alhaj Mohamed Mwenda wakati wa futari aliyoiandaa kwa wananchi, viongozi wa kiserikali na kidini wa Manispaa yake, jijini jana.
Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan (kulia) akibadilishana mawazo na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (wa tatu kushoto) wakati wakipata futari iliyoandaliwa na Meya huyo kwa wananchi, viongozi wa kiserikali na kidini wa Manispaa yake, Dar es Salaam jana. Wengine ni Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban Bin Simba (wa tatu kulia), Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum (wa pili kulia) na viongozi wengine wa kidini na kiserikali.


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 19.07.2014

NAJUA WAJUA YA CAPTAIN GARDINER G. HABASH NDANI YA MICHUZI TV LEO

Kampeni ya "Najiamini Naweza" Ya Mitandao Ya Jamii

$
0
0
Napenda kukutambulisha juhudi yetu mpya inayoitwa “Najiamini Naweza” - ambayo ni matokeo ya ushirikiano kati ya Maanisha! Limited (http://www.maanisha.co.tz/) na Hivos Twaweza (http://www.twaweza.org/).  
Kampeni hii imelenga kuonyesha harakati za kila siku za maisha ya Watanzania.  Kampeni inahamasisha wananchi kutambua uwezo na wajibu walio nao katika kutafuta suluhu za kero/changamoto wanazokumbana nazo. Tunafahamu kwamba mabadiliko huanza na mtu mmoja na pia jinsi huyo mmoja anavyoweza kuwapa hamasa wengine waige.
Mahojiano ya “Najiamini Naweza” yalifanyika kwa kipindi cha miezi 4 - yakijumuisha wananchi wa Dar es salaam na Morogoro. Mafanikio ya kampeni hii yatatusaidia kufikia wananchi wengi na kufanya sauti zao zisikike maeneo mengine hapa Tanzania. Video zote zinapatikana katika ukurasa wetu wa Youtube: https://www.youtube.com/user/MaanishaTV . Tanzania bora inajengwa na sisi.


Jaji Mfawidhi kanda ya Dar es Salaam ahitimisha ziara ya ukaguzi wa mahakama mkoa wa pwani

$
0
0
Jaji Mfawidhi kanda ya Dar es Salaam Mhe. SS Kihiyo akihitimisha ziara yake ya ukaguzi wa mahakama Mkoa wa Pwani. Pichani anakutana na Mhe. Ridhiwani  Mbunge wa Chalinze (wa kwanza kulia) Mhe. Shah Mbunge ea Mafia (hayupo pichani) na viongozi wengine  wakijadili changamoto mbalimbali na maboresho ya mahakama mkoa wa Pwani.Wengine ni Me. William Mutaki,msajili wa Kanda ya Dar es salaam,  na mahakimu katika kiwanja cha ndege cha Mafia muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kurejea Dar es salaam

State University of Zanzibar wins Carnegie African Diaspora Fellowship Programme (ADF)

Mtandao wa Wanawake na Katiba Wazungumzia Katiba Mpya

$
0
0
Mwakilishi kutoka Asasi ya Wanawake ya Ulingo, Dk. Avemaria Semakafu (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mkutano na wahariri wa vyombo vya habari. 
Mwakilishi kutoka Asasi ya Wanawake ya Ulingo, Dk. Avemaria Semakafu (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mkutano na wahariri wa vyombo vya habariMkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka taasisi moja wapo inayounda Mtandao wa Wanawake na Katiba akiwasilisha mada katika mkutano huo. Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka taasisi moja wapo inayounda Mtandao wa Wanawake na Katiba akiwasilisha mada katika mkutano huo.Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba
Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari wakiuliza swali kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. 
Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari wakiuliza swali kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba.
Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari wakiuliza swali kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. 
Mmoja wa wahariri wa vyombo vya habari akiuliza swali kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba.Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba. Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano na baadhi ya wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba.[/caption] MTANDAO wa Wanawake na Katiba umevitaka vyombo vya habari kuacha kuyumbushwa na upepo wa kisiasa katika suala zima la kupigania mambo ya msingi kwa jamii ambayo yanaitaji kuingizwa kwenye Katiba mpya kwenye mchakato unaoendelea hivi sasa wa kuandika katiba mpya. 

 Kauli hiyo imetolewa na baadhi ya wajumbe wanaounda mtandao huo jijini Dar es Salaam walipokuwa wakizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuelezea msimamo wa wajumbe hao kwenye mchakato wa uandikaji katiba mpya. 
 Mwakilishi kutoka Asasi ya Wanawake ya Ulingo, Dk. Avemaria Semakafu aliviomba vyombo vya habari kuwaunga mkono wanamtandao hao ambao pamoja na mambo mengine wamejipanga kupigania kero za wananchi kuhakikisha zinapata majibu katika mchakato wa uundaji katiba mpya hivyo kuwataka wanahabari kuwaunga mkono. 
 Alisema vyombo vya habari visikubali kupelekeshwa na wanasiasa kwa kupaza sauti kwenye maslahi ya wanasiasa zaidi na kushindwa kujadili masuala ya msingi ya jamii, ambayo endapo yatapata majibu katika mchakato wa uundaji katiba mpya wananufaika ni wananchi wote tofauti na masuala ya utawala (madaraka). 
 "Waandishi wa habari msikubali kuchezeshwa ngoma za wanasiasa, ambao mara zote wanapigania maslahi yao kiutawala...tupiganie maslahi ya jamii, jamii inaitaji kuona huduma bora za afya, elimu na mgawanyo sawa wa rasilimali," alisema Dk. Semakafu. 
 Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka taasisi moja wapo inayounda Mtandao wa Wanawake na Katiba akiwasilisha mada kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari alisema vyombo vya habari vina nguvu za kipekee katika kuleta mabadiliko kwenye jamii na mamlaka hivyo kuwaomba watumie fursa hiyo ipasavyo katika kupigania maslahi ya umma. 
 "...Hivyo vyombo vya habari, kama msingi wa kupatikana kwa taarifa yoyote, na kuongoza katika ushawishi vina sehemu muhimu sana katika kuongoza kuleta mabadiliko yawe ya sera, tabia au utamaduni," alisema Bi. Msoka ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge la Katiba. 
 Hata hivyo alivitaka vyombo vya habari kuwaunga mkono wanawake kwani licha ya kuwa na mchango mkubwa katika jamii wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za kusahaulika kwenye fursa anuai zilizopo. 
"...Wanawake ni asilimia 80 ya nguvu kazi vijijini na ni asilimia 60 ya wazalishaji wakuu wa chakula...lakini tunachangamoto nyingi," alisema Bi. Msoka. Mtandao wa Wanawake na Katiba ni muunganiko wa asasi za kijamii na kitaaluma zipatazo hamsini zilizoungana kudai katiba inayozingatia masuala ya kijinsia na inayotokana na mchakato ulioshirikisha sauti za makundi yote. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

HOFU YATANDA KWA WASHIRIKI WA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS, HUKU WENGINE WAKITAMANI WIKI IJAYO ISIFIKE

$
0
0
Baadhi ya washiriki wa Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakiwa mbele ya Majaji tayari kwa kupewa maoni yao na hatimaye kutaja watakaotoka chomwa na jua la utosi kwa Wiki hii. Kutoka Kulia ni Tishi Abdallah, Katikati ni Mtawa Kapalata na Kushoto ni Joshua Wambura.
Anneth Peter (katikati) akiwa mwenye huzuni kubwa kutokana na Mshiriki mwenza kutoka kanda ya Kaskazini Kareb John (hayupo pichani) kutoka kwenye shindano mara baada ya kuchomwa na jua la utosi.
 Washiriki wawili waliondolewa katika Shindano kwa wiki hii wakiwa mbele ya Jukwaa mara baada ya kutangaziwa kushindwa kuendelea kutokana na kuwa na idadi chache ya kura kutoka kwa watazamaji.Wa kwanza kushoto ni Kareb John na Malima Deogratius ambao wameaga mashindano
  Kareb John na Malima Deogratius mara baada ya kutangaziwa kuyaaga mashindano..
 Mara baada ya Kareb John Kuaga mashindano Mshiriki kutoka kanda ya Kaskazini Annet Peter alionekana mwenye huzuni kubwa
 Washiriki wakiwa na huzuni kutokana na wenzao kuaga mashindano.Picha zote na Josephat Lukaza wa Proin Promotions, Dar Es Salaam

 Na Josephat Lukaza - Proin Promotions 
Limited - Dar Es Salaam.

Ni wiki ya Pili sasa ya mchujo katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo washiriki wengine wawili wamechomwa na Jua la Utosi na hatimaye kuaga shindano. Mchujo huo ni muendelezo wa Mchujo ambao kila wiki washiriki wawili watachomwa na jua la utosi na hatimaye kupelekea kuaga shindano la TMT.
Mpaka sasa Washiriki wanne tayari wameshayaaga mashindano na kupelekea washiriki 16 kubakia katika mchujo unaofuata.
Mpaka sasa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limekua ni shindano lililoteka hisia za watanzania wengi waliopo ndani na nje ya Nchi kutokana na ubora, Uhalisia na Ubunifu wa hali juu kutoka kwa Waandaaji na waendeshaji pamoja na washiriki kuonyesha Vipaji vyao.
Ili kuweza kumnusuru mshiriki wako asichomwe na Jua la Utosi unachotakiwa ni kumpigia kura kadri uwezavyo ili kumfanya abaki ndani ya Nyumba ya TMT.
Mara baada ya washiriki wa wiki hii kuondolewa katika shindano hali imezidi kuwa ni simanzi kwa washiriki kutokana na kutokujua ni zamu ya nani kutoka wiki ijayo.
Washiriki waliotoka wiki hii ni Kareb John ambae alikua mmoja kati ya Washindi watatu kutoka kanda ya Kaskazini Mkoani Arusha huku Mshiriki Malima Deogratius akiwa ni Mshindi kutoka KAnda ya Pwani Mkoani Dar Es Salaam.
Ili kuweza kumnusuru mshiriki umpendae unachotakiwa kufanya ni Kuandika neno "TMT" ikifuatiwa na namba ya Mshiriki halafu unatuma kwenda namba 15678. Mfano TMT00 tuma kwenda 15678. Piga kura kadri uwezavyo ili kumnusuru mshiriki wako kutochomwa na Jua na Utosi wiki ijayo.
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ni shindano lililobuniwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited ambayo inahusika na utengenezaji, Usambazaji na Uuzaji wa filamu za Kitanzania huku ikiwa na malengo pia ya Kuibua vipaji vya Kuigiza na Mpira wa Miguu kwa Wanawake. Shindano hili Pia linaendeshwa na Kusimamiwa pia na Kampuni bora ya Usambazaji wa Filamu nchini ya Proin Promotions Limited.
Huzuni na Simanzi zaendelea kutawala ndani ya Nyumba ya TMT kwa washiriki hao wawili kuondoka lakini Pia Hofu Yaendelea Kutanda ndani ya Nyumba ya TMT kwa washiriki kwa kutokujua ni zamu ya nani sasa kuchomwa na jua la utosi litakalompelekea kuaga shindano kwa wiki ijayo.

BOOK TRAILER - Mists of Sense Require Fierce Poesy

$
0
0
New poetry book that dares you to emerge with a kind heart: despite the thickness of the mist, the pride you will have displayed, the tears you will have shed, the rants you will have made, the fierce poems you will have written and winning attitudes you will have dared.

KÖNIGSWINTER, Germany – In “Mists of Sense Require Fierce Poetry” (published by AuthorHouse), author Gloria D. Gonsalves takes readers into miracles of embracing oneself as divine being; adulthood and its dilemmas, troubles and heartaches; and national identity, broken homelands with violence and destruction of land and human spirit.

However, the human spirit is resilient. "I hope at the end readers will celebrate with me the winning attitudes with triumphs over trials,"says Gonsalves.

She invites readers to visit her at www.auntieglo.com 
“Mists of Sense Require Fierce Poesy”
By Gloria D. Gonsalves
Dust Jacket Hardcover| 6 x 9in | 112 pages | ISBN 978-1-49698-458-6
Available at Amazon and Barnes & Noble

About the Author
Gloria D. Gonsalves is from Tanzania, has lived in Ireland and currently resides in Germany. She enjoys writing poetry and tales for both children and adults. Her literary works aim at supporting humanitarian related projects and creativity in others, especially children, by having them participate through drawings or stories. Gloria also writes photographic snippets for her non-boring nature blog titled “Petals in a Lawyer”. 

Msondo, Sikinde uso kwa uso Iddi Mosi TCC Club

$
0
0
Mlimani Park Orchestra “Sikinde”
Msondo Ngoma Band
Magwiji wa muziki wa dansi nchini, Msondo Ngoma Band na Mlimani Park Orchestra “Sikinde” siku ya Iddi Mosi watachuana vikali katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe, Temeke. 
Mpambano huo wa Nani Mtani Jembe ni kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Id El Fitr na pia litaamua ni bendi ipi kali kati yao. 
Mratibu wa mchuano huo, Joseph Kapinga amesema pambano hilo litaanza saa nane alasiri hadi majogoo. Kapinga alisema bendi zote mbili ziko msituni kujiandaa na mpambano huo. Mratibu huyo alisema kila bendi itapiga kwenye jukwaa lake ili kulinda upinzani wao. 
Kiongozi wa Msondo Ngoma Saidi Mabera amesema watapiga nyimbo zao zote kali ili kuhakikisha wanaisambaratisha Sikinde. 
Baadhi ya wanamuziki wanaounda Msondo Ngoma ni Shaaban Dede, Mabera, Eddo Sanga, Juma Katundu, Roman Mng’ande `Romario’ na Hassan Moshi. 
Naye kiongozi wa Sikinde Hamisi Mirambo alijigamba kuwa wataibuka na ushindi mnono. “Tuna waimbaji wazuri na hakuna itakachotuzuia kushinda,” alisema Mirambo. 
 Baadhi ya wanamuziki wanaounda Sikinde ni Hassan Rehani Bitchuka "Stereo", Hassan Kunyata, Abdala Hemba, Musemba Waminyugu. Ramadhani Mapesa, Adofth Mbinga, Kelvin Mausi Mjusi Shemboza, Tonny Karama, Bonny Bass, Habibu Abass Jeff , Juma, Juma Choka, Mbaraka Othman, Hamisi Mirambo, Ali Yahaya, Yusuph Benard na Ali Jamwaka. Pambano imedhaminiwa na Konyagi na Saluti5.

Maalim Seif Sharif Hamad atembelea na kuwafariji wagonjwa na wafiwa Pemba

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amewakumbusha wagonjwa na wafiwa kuwa na subra na uvumilivu, wakielewa kuwa hiyo ni mitihani ya Mwenyezi Mungu. 
Akiwa katika ziara ya kutembelea wagonjwa na wafiwa katika Wilaya ya Mkoani, Maalim Seif amesema maradhi ni jumla ya mitihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba wanaopatwa na mitihani hiyo hawana budi kushuru na kuomba dua. 
Maalim Seif ambaye yuko kisiwani Pemba kwa ziara ya siku sita ya kuangalia wagonjwa, kutembelea masoko na kufutarisha, amewataka wananchi kuendeleza umoja na mshikamano uliopo kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla. 
Hapo jana Maalim Seif alifutari pamoja na wananchi wa kijiji cha Piki katika Wilaya ya Wete, na kuwashukuru wananchi wa kijiji hicho kwa kujitokeza kwa wingi kuungana nae katika futari hiyo. 
Wananchi hao wameelezea shukrani zao kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa kuamua kufutari pamoja nao, kitendo ambacho wamesema kimeongeza upendo kati yao na viongozi wakuu wa Serikali. 
Mapema wagonjwa waliotembelewa wameelezea kufarajika kwao kutokana na kitendo hicho, na kwamba kinaleta picha halisi kwa viongozi kuwajali wananchi wao katika mazingira yote. 
Katika ziara hiyo ya Wilaya ya Mkoani, Maalim Seif amewatembelea na kuwafariji wagonjwa wanane pamoja na wafiwa katika vijiji mbali mbali vikiwemo Chambani, Mwambe, Mtambile, Uweleni na Chokocho.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea na kuwafariji wagonjwa na wafiwa katika Wilaya ya Mkoani Pemba. 
Picha na Salmin Said, OMKR
 Maalim Seif akiwafariji  wagonjwa na wafiwa katika Wilaya ya Mkoani Pemba. 
 Maalim Seif akiwafariji  wagonjwa na wafiwa katika Wilaya ya Mkoani Pemba. 

Maalim Seif akiwafariji  wagonjwa na wafiwa katika Wilaya ya Mkoani Pemba. 

Sheikh Nurdin Kishki - Historia ya Uislam Afrika

JK azindua rasmi stendi ya Mabasi mjini Mbinga Mkoani Ruvuma, Barabara ya Peramiho -Mbinga

$
0
0
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa jiwe la Msingi kuzindua rasmi stendi ya Mabasi mjini Mbinga Mkoani Ruvuma leo.Rais Kikwete yupo mkoani Ruvuma Katika ziara ya Kikazi kukagua miradi ya maendeleo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua jiwe la msingi kufungua rasmi Barabara ya kilometa 78 ya Peramiho –Mbinga mjini  Julai 19,2014.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,Wairi wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli, katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bwana Servasius Likwelile, mwenyekiti  wa mfuko  MCC Tanzania Bwana Bernard Mchomvu. Picha na Freddy Maro
 Sehemu ya Barabara ya Peramiho -Mbinga yenye urefu wa Kilometa 78 iliyofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakivuta utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Peramiho-Mbinga yenye urefu wa Kilometa 78.

 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Peramiho-Mbinga 78Km huku akiwa  na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine wa Serikali na balozi wa China nchini.

 Mamia ya wakazi wa Mbinga wakifurahia wakati Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa anamshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa Utendaji wake mzuri wa kuwajali wakazi hao kwa kuwajengea miundombinu bora.

 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wa kwanza kulia akizungumza na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli kabla ya uzinduzi wa barabara ya Peramiho-Mbinga 78km .Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu.

 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katikati akimshukuru balozi wa China nchini aliye kushoto kwake kwa kazi nzuri iliyofanywa na Mkandarasi kutoka China Kampuni ya Synohdro. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia pamoja na Mawaziri wengine waliohudhuria ufunguzi wa barabara hiyo.

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katikati akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na baadhi ya Makatibu Wakuu na Mawaziri waliohudhuria katika ufunguzi wa barabara ya Perahimo-Mbinga. Picha na Jackson Msangula
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images