Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 509 | 510 | (Page 511) | 512 | 513 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Jasmine Kairuki akiongea na waandishi wa habari katika mkutano wa majumuisho ya ziara yake ya siku tano katika taasisi zinazotoa msaada wa kisheria jijini Dar es Salaam. Ziara hiyo imemalizika leo (Ijumaa, Julai 18, 2014). Wengine ni Wajumbe wa Bodi ya Sekretarieti ya Msaada wa Kisheria (LAS) Dkt. Hellen Kijo-Bisimba (kulia) na Bi. Theodosia Muhulo.

  0 0

  Rt. Hon. Dato' Sri Mohammad NajibTun Abdul Razak, 
  Prime Minister of Malaysia


  H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a condolence message to Rt. Hon. Dato' Sri Mohammad NajibTun Abdul Razak, Prime Minister of Malaysia following the loss of lives due to the crash of a Malaysian airliner on Thursday 17th July 2014. The message reads as follows:

  “Rt. Hon Dato' Sri Mohammad Najib Tun Abdul Razak,
  The Prime Minister of Malaysia,
  Kuala Lumpur.
  Malaysia

  I have learnt with great shock and sorrow the sad news of the loss of so many lives due to the crash of a Malaysian airliner on its way from Amsterdam to Kuala Lumpur that occurred on Ukrainian territory on Thursday 17th July 2014.

  The crash is an immense tragedy not only for the loved ones of those who perished but also for all the people of Malaysia and their friends. As a country, our thoughts and prayers are with the people of Malaysia in this time of grief.

  On behalf of the Government and the people of the United Republic of Tanzania, and indeed on my own behalf, I offer you our sincere condolences, support and solidarity.

  Please accept, Your Excellency the assurances of my highest consideration”.

  Issued by: The Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam

  18th July, 2014

  0 0

  Na John Gagarini, Kibaha

  SAKATA la Umoja wa wafanyabiashara wa nyama na mazao yake  wilayani Kibaha mkoani Pwani (UWABINK) leo umechukua sura mpya  baada ya kufanya mgomo wa kutochinja ngombe na kusababisha nyama kukosekana kwenye mji wa Kibaha na vitongoji vyake.

  Kutokana na mgomo huo wa kutochinja ngombe kumesababisha nyama kukosekana katika maeneo ya kuanzia Maili Moja hadi Visiga na Kibamba CCM wilaya ya Kinondoni Jijijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa umoja huo Athumani Mkanga alisema kuwa wameanza mgomo huo kwa muda usiojulikana kutokana na Halmashauri hiyo kuwahamisha kutoka katika machinjio ya Maili Moja na kuwahamishia machinjio mpya ya Mtakuja kata ya Pangani jirani hifadhi ya msitu wa Ruvu.

  Mkanga alisema kuwa hawakatai kuhamia katika machinjio hayo mpya lakini wanashindwa kufanya hivyo kutokana na mapungufu yaliyopo hususani miundombinu kutokuwa rafiki kiusalama , kutokuwa na umeme unaolingana na kazi yao na maji.

  “Katika machinjio ya awali walikuwa wakigharamia maji kwa sh 30,000 kwa siku ambapo kwasasa watatakiwa kugharamia maji kutoka Maili Moja kwa sh 150,000 ambayo kwa mwezi ni zaidi ya sh mil 4,” alisema MKanga.

  Kwa upande wa mfanyabiashara wa nyama Maliseli Boniface alisema machinjio hayo mapya haijakidhi mahitaji wakihofia kupoteza mali zao kutokana na machinjio hiyo kuwa umbali wa km zaidi ya 5 kutoka Maili Moja na wafanyabiashara hao wakitakiwa kufuata nyama nyakati za alfajiri kukiwa giza huku eneo hilo likiwa limezungukwa na msitu.

  “Machinjio hiyo mpya ni ndogo ukilinganisha na ile ya awali kwani ilikuwa ikichinja ng’ombe 35 -40 kwa siku na kwasasa wanaotakiwa kuhamia watakuwa wakichinja ng’ombe 15-20 jambo ambalo itazorotesha biashara hiyo,” alisema Boniface.

  Aidha msimamo wa wafanyabishara hao ni kuhamia Machinjio ya Mlanizi kama halmashauri hiyo ikiendelea na msimamo wa kuwahamishia katika machinjio ambayo haijakamilika kimiundombinu .

  Akizungumzia mgomo huo Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kibaha Jennifer Omolo  alisema kuwa  hana taarifa kuhusiana na mgomo huo .

  Omolo alibainisha kuwa bado anasimamia agizo lake la kuwataka wafanyabiashara hao kusitisha mgomo huo na kuwa machinjio ya Maili Moja isitumike kuanzia julai 18 na badala yake itumike machinjio mpya ya Mtakuja ambayo imekamilika  .

  Kutokana na mgomo huo umeathiri kwa kiasi kikubwa walaji kwa kutokuwa na nyama mabucha yote ya maeneo ya kibaha na bucha chache zikiwa zinauza nyamailiyolala(ndaza )kwa sh . 6,000 ambayo ni bei ya nyama ya kawaida.

  Hata hivyo halmashauri ya kibaha mji imekuwa ikipokea ushuru wa machinjio ya awali kwa kiasi cha sh. sh. mil 1.6 kwa mwezi ikiwa ni sh.5,000 kwa kichwa kimoja cha ng’ombe hivyo kuhofiwa Halmashauri hiyo kupata hasara ya mapato ya ndani.

  0 0

  Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania -TRL  unaWAtaARIFU WAKAZI WA JIJI NA WANACHI KWA JUMLA kusitishwa kwa huduma ya treni ya jiji hapo kesho Jumamosi Julai 19, 2014, ili kupisha ukarabati wa miundo mbinu ya reli KATI ya Dar Stesheni hadi Ubungo Maziwa itakayofanyika kwa siku za Jumamosi na Jumapili.

  Hata hivyo huduma hiyo itarejea tena kama kawaida kuanzia Jumatatu Julai 21, 2014 . Atakayesikia AU KUSOMA TAARIFA HII amuarifu na mwenziye.

  Uongozi wa TRL unasikitika kwa usumbufu utakaojitokeza.

  Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL

  Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu,

  Dar es Salaam,


  Julai 18, 2014 


  0 0

   HOLY QURAN MEMORIZATION CHARITABLE TRUST-TANZANIA
  P.o.box :      66 Mkuranga- Pwani
  Website:      www.quran.or.tz
  Phone:         +255652805897
                          + 255713981811


  0 0
  0 0

  Zile habari zilizosambaa kwenye mitandao  ya kijamii  kuonesha  kwamba hotel ya Naura Spring ya jijini Arusha inawaka moto zilikuwa si za kweli ni watu wametengeza picha hizo ambazo zilikuwa zimeenea kila pembe.
  Kamanda wa Polisi Arusha Liberatus Sabas ameongea jioni hii na vyombo vya habari na kukanusha habari za hotel hiyo ya kitalii jijini Arusha kwamba iliwaka moto hizo ni picha za kutengeneza hotel ipo salama kabisa kama unavyoona kwenye picha ya juu. Picha ya chini yake ndiyo iliyosambazwa na watu wasiojulikana.  
  Wananchi wengi wamepiga simu dawati la usiku la Globu ya Jamii na kueleza masikitiko yao kwa mchezo huu unaoenea kwa kasi nchini hivi sasa. Wamevitaka vyombo husika sio tu kudhibiti uhalifu huu bali pia kuwachukulia hatua watakaobainika kuhusika nao. 
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas  ambaye amekanusha kwamba  Naura Springs Hotel imewaka moto.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), akipokea Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Chiola, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi baada ya Mwenge huo kumaliza kukimbizwa katika Wilaya Ruangwa. Mwenge huo wa Uhuru ambao mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” utakimbizwa katika Wilaya ya Nachingwea ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo itafunguliwa pamoja na kuzinduliwa.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), akisalimiana na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda baada ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru uliotoka Wilaya ya Ruangwa na kuingia Wilaya ya Nachingwea. Wapili Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo ambaye ndio aliyekabidhiwa rasmi Mwenge huo kutoka Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda (kulia) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chiola (hawapo pichani) baada ya kufungua Mradi wa Nyumba ya Mganga katika Kijiji hicho kilichopo Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe. Mwenge huo wa Uhuru ambao mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” utakimbizwa katika Wilaya ya Nachingwea ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo itafunguliwa pamoja na kuzinduliwa.
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda (aliyebeba ndoo ya maji) akishangiliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (wapili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo pamoja na wananchi baada ya kubeba ndoo ya maji baada ya kufungua mradi wa maji katika Kijiji cha Mituguru, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akiwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Regina Chonjo. Mwenge wa Uhuru ambao mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” umengia katika wilaya hiyo ambapo unatarajiwa kufungua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ikungu, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi baada ya kukabidhi Bajaj kwa walemavu na Pikipiki kwa watendaji wa Wilaya na Kata mbalimbali katika wilaaya hiyo zikiwa ni kwa shughuli za maendeleo katika Halmashauri hiyo. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe. Mwenge huo wa Uhuru ambao mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” utakimbizwa katika Wilaya ya Nachingwea ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo itafunguliwa pamoja na kuzinduliwa.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), akiwasalimia wapiga kura wake wa Kijiji cha Ikungu wakati wa ukimbizaji wa Mwenge wa Uhuru katika Jimbo lake la Nachingwea. Waziri Chikawe alimshukuru Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda pamoja na timu yake kwa kuzindua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake. Picha na zote na Felix Mwagara.

  0 0

  Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai Mhe Omari Mjenga akiwa na wanadiplomasia wenzake kwenye  sherehe za kimataifa za usomaji Quran jijini Dubai leo
   Mgeni rasmi   Mtukufu Sheikh Maktoum bin Mohamed bin Rashid al Maktoum akiwa picha ya pamoja na washindi. Kulia kwake ni kijana kutoka Nigeria akiyeibuka mshindi.
   Mheshimiwa Mjenga akiwa na bw. Ali Mwalimu, mshiriki kutoka Tanzania. 
  Mheshimiwa Balozi Mdogo Mjenga akiwa na familia yake kwenye sherehe hizo.

  0 0

  Na Andrew Chale
  TAASISI ya  Mwangaza wa buradani Zanzibar  (Zanzibar Light Entertainment ) ya mjini Unguja,  Zanzibar, Imemtangaza rasmi  Hotel ya Kendwa Rocks  kuwa eneo litakapofanyika  michuano m aalum ya soka la ufukweni  lijulikanayo kama  (Zanzibar Beach Soccer Championship Bonanza) linalotarajiwa kufanyika Agosti  Mbili mwaka huu.

  Kwa mujibu wa taarifa yao hiyo  kwa vyombo vya habari, iliyotolewa na Mwandaaji wa michezo hiyo, Muslim Nassor ‘Jazzphaa’  ilieleza kuwa,  kamati ya mashindano hayo, ambayo kwa sasa hipo katika harakati mbalimbali zikiwemo za kusaka ufadhili kwa wadau, tayari baadhi ya wadau wameanza kuitikia wito huo huku Kendwa Rocks Hotel Beach, wakijitosa kudhamini ‘venue’.

  “Kadri siku zinavyozidi kwenda ndipo maandalizi yanakuwa magumu zaidi. Tunafuraha kutoa taarifah kuwa ndipo tutakapofanyia mashindano haya ya Zanzibar Beach Soccer Bonanza 2014.” Alisema Muslim Nassor  Jazziphaa.

  Aidha, Muslim Nassor Jazziphaa aliweka bayaana kuwa,  Director wa Kendwa rocks, Bwana Ally Kilupi  tayari ametoa   baraka  zote za kufaanyika mchezo huo huku akifurahia mchezo kufanyika eneo hilo,  huku akitoa rai kuwapo kwa amani na utulivu siku hiyo na siyo kuanza ugomvi na vitu ambavyo havina maana.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa nne kulia) akijumuika na waislamu na Viongozi katika swala ya Magharibi katika viwanja vya Ofisi ya Uhamiaji Tunguu kabla ya futari aliyowaandalia wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akijumuika na Viongozi katika futari aliyowaandalia wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja jana katika viwanja vya Ofisi ya Uhamiaji Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
  Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja kwa pamoja wakijumuika katika fuitari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein jana katika viwanja vya Ofisi ya Uhamiaji Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
  Akinamama wa Mkoa wa Kusini Unguja wakijumuika katika futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika Ukumbi wa Ofisi ya Uhamiaji Tunguu Mkoa wa Kusini jana.
  Naibu Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na MIchezo Bi. Hindi Hamadi Khamis (wa pili kulia) akijumuika na Viongozi wengine katika futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein kwa wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja katika Ukumbi wa Ofisi ya Uhamiaji Tunguu Mkoa wa Kusini jana.
  Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Unguja Dk.Idriss Muslim Hija,akitoa shukurani kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wake jana baada ya futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya Ofisi ya Uhamiaji Tunguu.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja jana baada ya futari iliyowaandalia katika viwanja vya Ofisi ya Uhamiaji Tunguu.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dk.Idriss Muslim Hija baada ya Futari aliyowaandalia wananchi wa Mkoa huo jana katika viwanja vya Ofisi ya Uhamiaji Tunguu Wilaya ya Kati Unguja. [PICHA ZOTE NA RAMADHAN OTHMAN,IKULU]

  0 0

  SEHEMU YA JENGO LA HOTEL HIYO LIONEKAVYO KWA NJE.
  MENEJA WA HOTEL HIYO BI.BEATRICE DALLARIS AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI,JUU YA  TAARIFA ZA UZUSHI ZILIZOSAMBAZWA KWENYE MITANDAO YA KIJAMI KUWA HOTEL HIYO IMEUNGUA MOTO MAPEMA LEO JIJINI ARUSHA.

  UTAWALA NA WAFANYAKAZI WA HOTELI YA NAURA SPRINGS IMESIKITISHWA KWA TAARIFA ZILIZOSAMBAA KWENYE MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII KUHUSU KUWA HOTELI YETU INAWAKA MOTO NA KUSABABISHA USUMBUFU MKUBWA KWA WATU WA MKOA WETU, NDUGU NA JAMAA WA WAFANYAKAZI WA HOTEL ,VIONGIOZI MBALIMBALI, VYOMBO VYA USALAMA, IDARA YA ZIMA MOTO, WAANDISHI WA HABARI WA VYOMBO MBALI MBALII VYA HABARI NA PIA KUSABABISHA WASIWASI NA KUTOWESHA UTULIVU NA AMANI WA MJI WETU.
  TUMESIKITISHWA SANA NA TUMEOMBA UONGOZI WA MKOA WETU WALISHUGHULIKIE SWALA HILI KIKAMILIFU KWANI HILI SIO LA KUCHUKULIA MZAHA NA TUNGEOMBA HATUA KALI ZICHUKULIWE KWA HARAKA SANA KWA ALIE TOA TAARIFA HIYO YA UONGO.

  TUNAWASHUKURU WATU WOTE WALIOFUATILIA SWALA HILI NAPIA TUNATOA TAMKO KUWA HABARI HIZI ZA KUWA HOTELI YETU INAUNGUA NI ZA UONGO.

  BEATRICE DIMITRIS DALLARIS

  HOTEL MANAGER

  0 0

  Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akifuturu pamoja na mabondia na wadau wa mchezo huo wa pili kushoto ni Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' Birali Ngonyani, Shomari Mirundi, Raymond Mbwago wakati wa futari iliyoandaliwa na kucha huyo nyumbani kwake Rozana Dar es salaam 
  Baadhi ya waumini wa dini ya kislam wakiomba duwa baada ya kufuturu katika futari iliyoandaliwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' mwenye kibagarashia na kanzu
  Mabondia na wadau mbalimbali wakifurahia futari iliyoandaliwa na kocha Super D. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Spika wa Bunge, Mhe Anne Makinda akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe Magese Mulongo (kulia) baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Arusha, jana tayari kwa  kuhudhuria Mkutano wa  45 wa Mabunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Bara la Afrika utakaoanza tarehe 20 hadi 27 Julai Mjini Arusha ambapo Tanzania ndio mwenyeji wa kongamano hilo. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa Jossey Mwakasyuka
  Spika wa Bunge, Mhe Anne Makinda akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa Jossey Mwakasyuka alipokwenda kukaguwa Ukumbi wa Ngurudoto, Arusha , jana, patakapofanyika Mkutano wa  45 wa Mabunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Bara la Afrika ambapo Tanzania ni mwenyeji wa kongamano hilo. 
  Spika wa Bunge, Mhe Anne Makinda akitowa maelekezo kwa kamati ya maandalizi ya Mkutano wa  45 wa Mabunge wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kwa Kanda ya Bara la Afrika alipotembelea Ukumbi wa Ngurudoto, mkoani Arusha  patakapofanyika kongamano hilo ambapo Tanzania ndio mwenyeji

  0 0


  0 0
 • 07/18/14--20:03: KUMBUKUMBU
 • MWALIMU JANE GRACE SUFIANI

  Ni miaka 12 sasa tangu ulipoiaga dunia tarehe 19.07.2002. Upendo, ukarimu na wema wako havitasahaulika kamwe. Unakumbukwa na watoto wako Elizabeth, Sofia, Lucy, Robert na Michael; wajukuu zako Rodgers, David, Joel, Bernice na Ellyson. Unakumbukwa pia na ndugu, jamaa na marafiki wote.
  BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIBARIKIWE!

  0 0

  Balozi wa Norway nchini Mheshmiwa Balozi Ingunn Klepsvik akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Baraza la Habari,Wahariri na wadau wengine wa Habari kwenye Hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach.
  (Picha kwa Hisani ya kamerayangublog.com) .
   Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania Ndugu Kajubi Mukajanga akizungumza wakati wa tafrija ya kumuaga Balozi wa Norway nchini Mheshmiwa Balozi Ingunn Klepsvik kwenye Hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach. Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari alimsifia Balozi wa Norway kwakuwa rafiki wa kweli kwa Baraza la Habari la Tanzania.
    Meneja wa Rasilimali Watu Baraza la Habari Tanzania Ziada Kilobo akimsaidia Balozi kufunga kilemba ikiwa sehemu ya zawadi ya vazi la asili la Kiafrika alilozawadiwa Balozi,kulia ni Meneja Uthibiti na Viwango  Pili Mtambalike wakati wa tafrija ya kumuaga Balozi wa Norway nchini Mheshmiwa Balozi Ingunn Klepsvik kwenye Hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach.
   Rais wa Bodi ya Baraza la Habari Tanzania Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na  Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania Ndugu Kajubi Mukajanga wakiangalia picha ya Balozi ambayo alipewa kama zawadi wakati wa tafrija hiyo ya kumuaga  Balozi wa Norway nchini Mheshmiwa Balozi Ingunn Klepsvik kwenye Hotel ya Ledger Plaza Bahari Beach.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) Bi. Margaret Chacha akizungumza na kikundi cha kinamama wenye watoto wenye ugonjwa wa mtindio wa ubongo na mgongo wazi kituo cha kigamboni(Chawawaki), wakati ya mafunzo ya ujasiriamali na kuwaelimisha juu ya fursa zinazotolewa na benki ya TWB, Mafunzo hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Tanzania Women Of Achievement(TWA)
    Mwenyekiti wa Tanzania Women Of Achievement(TWA) Bi.Sadaka Gandi akizungumza na kinamama wenye watoto wenye ugonjwa wa mtindio wa ubongo na mgongo wazi kituo cha Kigamboni(Chawawaki) pembeni yake ni Bi. Margaret Chacha Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Wanawake Tanzania na Bi. Hellen Kiwia Katibu Mkuu wa Taasisi ya TWA.
    Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) Bi. Margaret Chacha akifurahia jambo na Katibu mkuu wa Tanzania Women Of Achievement(TWA) Bi. Hellen Kiwia wakati mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa kwenye kituo cha Chawawaki Kigamboni.
  Bi Blandina Sembo akiongea na kinamama wa Chawawaki
    Mshauri nasaha na mtoa mafunzo wa CCBRT Bi. Mgaya Mhamanda na Bi Suzane Mrema wakiongea na kinamama hao.
  Kinamama wa Kituo cha watoto wenye ugonjwa wa mtindio wa ubongo na mgongo wazi wa Kigamboni(Chawawaki) wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa benki ya Wanawake (TWB)Bi. Margaret Chacha(hayupo pichani)wakati wa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Taasisi ya Tanzania Women Of Achievement(TWA).

  0 0

   Leo tarehe 19 mwezi wa saba ni siku ya kuzaliwa mdau Krantz Mwantepele mwanzilishi na  mkurungezi wa  ufundi  mwanaharakati mzalendo media ambao ni wamiliki wa blog tatu mwanaharakati mzalendo blog, harakati180 na 255 trending news   pia ni Mkurungezi wa masoko wa KAJO ITECH  kampuni ya kizalendo inayohusika na it ,printing na event management
  Napenda kuwashuku sana wadau wangu wote tunaoshirikiana nao kila siku katika  ujenzi wa ktaifa katika kuhabarishana na pia kutoa elimu kupitia mitandao ya kijami   
  Napenda kuwakaribisha kuendelea mitandao yetu 
  Mwanahakati mzalendo blog link www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com
  Harakati180   link www.harakati180.blogspot.com
  255 trending news .link www.mzalendo89.blogspot.com
   Na website www.chochote.co.tz
  ASANTENI SANA


older | 1 | .... | 509 | 510 | (Page 511) | 512 | 513 | .... | 3282 | newer