Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 511 | 512 | (Page 513) | 514 | 515 | .... | 3270 | newer

  0 0

  afrimma_flyer_web2

  Baada ya BET Dimond anarejea tena nyumbani Afrika,akiwa nominated kwenye Tuzo za  #Afrimma( AFRICAN MUSIC MAGAZINE AWARDS) awards,zitakazofanyika jijini Richardson, Texas,tarehe 26 july.

  akiwa nominated kwenye category 5.

  Best male East Africa
  Song of the year(number1).
  Video of the year (number 1)
  Best collabo (number 1 rmx)ft Davido
  And Best Afrikan Artist of the year
  Ili ku-vote fuata link hii  http://afrimma.com/afrimma-nominees-2014/

  Kisha vote kwenye kila category niliyopo.
  Ahsanteni 
  Hapa chini angali video mpya ya Diamond "Mdogo Mdogo"

  0 0


  0 0

   Kwa mara ya 7 mfululizo AUTOFEST sasa imekuja na mashamsham kabambe kwa wadau wote wa magari. Maonyesho haya yatahusisha
  - wauzaji magari

  - Vipuri vya magari

  - watoa huduma shirikishi (Bima , Bank,n.k)

  - Kwa upande wa Michezo Zawadi zakumwaga bila kusahau 4 x 4 challenge , Norinda (Drifts).

  - V.I.P lounge na Nyama Choma Kama   kawaida


  UNAKARIBISHWA KUCHUKUA NAFASI 
  YAKO MAPEMA KAMA UNAHUSIKA NA:

  Commercial Vehicles 4 WD's

  Transportation Vehicles

  Motorcycles & Scooters

  Auto Spare Parts

  Tyres & Batteries, Oil & Lubricants

  Logistics

  Traffic Safety and Signage Products

  Garage Tools & Equipment

  Petrol Station Products

  Car Accessories, Car Care Products

  Car Loans/Finance

  Automotive Paints

  Automotive Security Products

  Trucks & Trailers' Spare Parts


  Mawasiliano:

  tel: 22 2664283 Cel: +255 754/784 280 491 / 0715 847 466 e:info@autofest.co.tz

  w: www.autofest.co.tz

   Mashindano ya magari  
   Maonesho ya magari aina mbalimbali
   Wenye bisahara zinazohusu magari
   Show kabambe ya magari ya kila aina
  Watoa huduma za magari toka taasisi na makampuni mbalimbali

  0 0


  CHATA YA TIMBER LAND JOGING AND SPORTS CLUB YOMBO KILAKALA JIJINI DAR ES SALAA<
   Kanali Mstaafu Iddi Kipingu wa tatu kushoto akikabidhi misaada ya vyakula kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha Daru-Alqm cha Yombo misaada iliyotolewa na Timber Land Jogging and Sports Club

  0 0

   KATIKA KUELEKEA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA EID EL FITR NA KUHAKIKISHA KWAMBA WATU WANATOKA NA PAMBA KALI NA ZA KISAWASA WAKATI WOTE,DUKA LAKO PENDWA LENYE VIWALO VYA NGUVU NA VYA KISASA JIJI LA DAR ES SALAAM LINALOFAHAMIKA KAMA J&M VIRGO,LIMESHUSHA MALI MPYA NA ZA UHAKIKA KABISA KWAKO WEWE MTANZANIA.

  HIVYO FIKA DUKANI KWAO PALE MIKOCHENI KWA WARIOBA,JENGO LA C&G PLAZA GHOROFA YA KWANZA ILI UWEZE KUJIPATIA VITUZZ NA VIWALO VYA KIJANJA,POCHI BABKUBWA,MOKA ZA KISASA NA MICHUCHUMIO YA HAJA KWA KINA DADA.

  KWA TAARIFA ZAIDI TEMBELEA LIBENEKE LAO

  KWA KUBOFYA HAPA
   MIKOBA YA KISASA
   KIVAZI CHA KINA DADA
   KOBAZI MATATA KABISA KWA KINA BABA
  MOKA YA NGOZI YA CHATU NA MKANDA WAKE.

  0 0

  Benki Kuu ya Tanzania inapenda kukanusha habari zinazosambazwa kwenye mitandao kuwa kesho Jumatatu Benki ya FBME itafungwa na shughuli zote za benki hiyo zitakuwa chini ya Benki Kuu.

  Habari hizi si za kweli na kwamba benki hiyo haipo chini ya usimamizi wa Benki Kuu na itaendelea kutoa huduma kama kawaida.

  IMETOLEWA NA
   IDARA YA UHUSIANO NA ITIFAKI, BENKI KUU YA TANZANIA.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati alipokuwa mgeni rasmi kukabidhi Tuzo za washindi wa mashindano ya kuhifadhi qur-aan, yaliyofanyika leo Julai 20, 2014, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa pili wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, ambaye ni Mtanzania, Said Omary Said, wakati wa hafla ya hitimisho la mashindano hayo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, leo Julai 20, 2014. Wa pili kushoto ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, Hatham Sadar, kutoka nchini Kenya wakati wa hafla ya hitimisho la mashindano hayo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, leo Julai 20, 2014. Wa pili kushoto ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu wa mashindano hayo baada ya kukabidhiwa zawadi zao
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mashindano hayo baada ya kukabidhiwa zawadi zao
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu na majaji wa mashindano hayo baada ya zoezi la kukabidhi zawadi. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam, wakati akiondoka kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya kukabidhi zawadi za washindi wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, yaliyomalizika leo Julai 20, 2014, jijini Dar es Salaam. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam, wakati akiondoka kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya kukabidhi zawadi za washindi wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, yaliyomalizika leo Julai 20, 2014, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR


  0 0
 • 07/20/14--21:54: msiba
 • Mdau Michael Machella amefiwa na Mtoto wake wa kike, Everlyne Michael Machellah,  katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
  Marehemu, ambaye alikuwa ana umri wa mwaka mmoja,  alikuwa akisumbuliwa na Malaria pamoja na kuharisha.
  Mazishi yanatarajiwa kuyafanyika kesho.  Muda na wapi tutawajulisha.
  Bwana alitoa na Bwana ametwaa 
  Jina la Bwana lihimidiwe milele 
  Amina.

  0 0

   Sheikh Suleiman Amran Kilemile Alipokuwa akifungua Kituo Cha Jamaat Islamiyyah Madrassa and Nursery School Cha Kisarawe. Sheikh Kilemile aliwahusia wazazi kuwasomesha watoto wao Masomo yote kwani husaidia kupata Viongozi Waadilifu na wenye Huruma katika Maendeleo ya Jamii.
  Sehemu ya Majengo ya Kituo Kipya cha Masomo ya Awali Cha Jamaat Islamiyya Kisarawe Pwani.
    Sheikh Suleiman Kilemile akiwa na Mbunge wa Kisarawe Mh. Suleiman Jaffu pamoja na watoto wa Wilaya hiyo wakionyesha Matumaini Mapya Baada ya Taasisi ya Kalamu Education Foundation Kukabidhi kituo Cha Jamaat Islamiyyah Madrassa and Nursery School Kisarawe.


   Mh. Aisha Dodo Mtwangi (Wapili Kulia) akiwa Pamoja na Wajumbe wenzake wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation wakati wa Ufunguzi wa Kituo Cha Masomo ya awali. Wengine ni Maryam Abdulkadir, Neema Idd na Farida Mohamed.
   Mgeni Rasmi Sheikh Suleiman Amran Kilemile akisindikizwa na Mbunge wa Kisarawe Mh. Suleiman  Said Jaffu mara baada ya Uzinduzi wa Kituo Cha Masomo ya Awali na Elimu ya Dini wilayani Kisarawe Kilichojengwa na Kalamu education Foundation.
  Baadhi ya Wajumbe wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation wakiwa pamoja na Viongozi Mbali Mbali wa Kidini wa wilaya ya Kisarawe wakati wa Uzinduzi wa Kituo Cha Elimu ya Awali wilayani hapo.

  0 0

  Na Liberatus Mwangombe “Libe”

  Libe akifuatilia mkutano Ubalozini

           Ijumaa July 18, 2014 tulikuwa na mkutano kwenye ubalozi wa Tanzania Wshington D. C. ulio tuhusisha wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kwenye jumuia ya DMV, viongozi wa Tume ya Uchaguzi, ATC Metro Board members na kusimamiwa na balozi Liberata Mulamula. Kwenye mkutano huu wagombea tulitoa malalamiko ya jinsi uchaguzi umekuwa ukiendeshwa bila haki na sintofahamu lote linalo uzunguka uchaguzi huu. 

  0 0

  IMG_8020Balozi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Washington Dc na Mexico Liberata Mula mula akiwa kwenye picha ya pamoja na wagombea uongozi DMV, wajumbe wa bodi na wajumbe wa tume ya uchaguzi kwenye ofisi za ubaloi Washington Dc Ijumaa Julai 18,2014. IMG_7900Mh.Balozi akifungua kikao hicho. 

  0 0

  Familia ya Chagula inasikitika kutangza kifo cha baba yao mpendwa Clement Chagula kilichotokea siku ya Ijumaa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, Dar es salaam.
  Misa ya kumuaga marehemu itafanyika katika kanisa la st Albans jijini Dar es salaam siku ya Jumatatu tarehe 21 Julai 2014 saa saba mchana. Baada ya hapo mazishi yatafanyika katika makaburi ya kinondoni.

  Bwana alitoa Bwana ametwaa
  Jina lake na lihimidiwe
  Amen

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi miche bora ya kahawa mkulima mdogo Bi Dorothea Komba wakati alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam katika kijiji cha Lipokela wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma leo.Kampuni ya Olam imepanga kutoa jumla ya miche milioni tatu kwa wakulima wadogo elfu mbili katika vijiji vinne vinavyozunguka shamba hilo katika kipindi cha miaka mitano ili kuwashirikisha kuzalisha kahawa bora. 
   Meneja wa Shamba la Kahawa la AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam Bwana Medappa Ganapati akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mche bora wa kahawa iliyozaa vyema wakati Rais alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa katika kijiji cha Lipokela, wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma leo
    Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akibemba mtoto aliyekuwepo kwenye sherehe za ufunguzi wa  Soko la Kimataifa la Mkenda lililopo katika kijji cha Mkenda Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania
   Soko la Kimataifa la Mkenda lililopo katika kijji cha Mkenda Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua Soko la Kimataifa la Mkenda lililopo katika kijji cha Mkenda Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania leo.kulia ni mbunge wa Peramiho Mh.Jenister Mhagama.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma. Picha na Freddy Maro


  0 0

  Good morning!
  Just to let you know that I am in MWANZA and safe. My email account has been hacked and an email is sent claiming that I am in London and that I have been robbed and badly need financial aide.
  THIS IS NOT TRUE!
  Please and ASAP help me send information out there as I can not access all my contacts: 
  JOSEPH IS IN MWANZA, SAFE AND HE HAS NOT BEEN ROBBED AND IN THAT EFFECT DOES NOT NEED ANY FINANCIAL SUPPORT, AT LEAST NOT AT THE MOMENT.

  Joseph Alex Mlinzi
  City Public Relations Officer
  Mwanza City Council
  P. O. Box 1333
  Mwanza
  Tanzania

  0 0


  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye amesema Chama Cha Mapinduzi hakimzuii mwanachama yeyote kutangaza nia ya kugombea Uongozi katika muhula unaofuata isipokuwa Chama kimezuia kampeni za mapema kwani ndio chanzo cha makundi ndani ya Chama akizungumza kwenye kipindi cha Baragumu kinachorushwa na Channel 10.
  Nape  alisema taratibu za kugombea Uongozi ndani ya chama zipo na kuna Kanuni mbili, moja ni ya Kanuni za Viongozi na Maadili na pili Kanuni zinazosimamia Uchaguzi ndani ya CCM, 
  Akinukuu kutoka kwenye kitabu cha Kanuni za Viongozi na Maadili ,Nape alisema "Wanachama wenye nia ya kugombea nafasi ya uongozi katika muhula unaofuata anaweza kutangaza nia ya kugombea lakini haruhusiwi kufanya kampeni kabla ya muda".
     Akizungumzia juu ya adhabu wanazopewa waliokiuka alisema adhabu hizi zina shabaha ya kuwasaidia wanachama na Viongozi kujirekebisha.
  Nape pia alizungumzia suala zima la upatikanaji wa Katiba Mpya,alisema CCM imeshikamana sana kiasi cha kuwachanganya Wapinzani, aliendelea kwa kusema Kanuni,Sheria zinazotumika ni makubaliano ya wote.(Wapinzani walishiriki katika kamati kutengeneza kanuni na sheria na zikapitishwa Bungeni wakiwemo na Rais akasaini).
  Chanzo: kamerayangublog.com

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi kituo cha afya katika Gereza la Kitai wilayani Mbinga jana.Kushoto ni Mkuu wa Gereza hilo Alexander Richard Nyefwe.Kituo hicho kitatoa huduma kwa askari magereza,wafungwa na vijiji jirani
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi miche bora ya kahawa mkulima mdogo Bi Dorothea Komba wakati alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam katika kijiji cha Lipokela wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma leo.Kampuni ya Olam imepanga kutoa jumla ya miche milioni tatu kwa wakulima wadogo elfu mbili katika vijiji vinne vinavyozunguka shamba hilo katika kipindi cha miaka mitano ili kuwashirikisha kuzalisha kahawa bora.
   Meneja wa Shamba la Kahawa la AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam Bwana Medappa Ganapati akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mche bora wa kahawa iliyozaa vyema wakati Rais alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa katika kijiji cha Lipokela, wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma leo.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua Soko la Kimataifa la Mkenda lililopo katika kijji cha Mkenda Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania leo.kulia ni mbunge wa Peramiho Mh.Jenister Mhagama.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma

   Sehemu ya  Soko la Kimataifa la Mkenda lililopo katika kijji cha Mkenda Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania leo.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma..(picha na Freddy Maro).


  Saidieni watu kutoka kwenye umasikini, 
  Rais awaagiza viongozi


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amezitaka taasisi za Serikali kuongeza kasi ya kupunguza umasikini miongoni mwa wananchi, akisisitiza kuwa wananchi wamekaa katika umasikini kwa muda mrefu mno kupita kiasi.        

  Rais Kikwete amesema kuwa wanachotarajia wananchi kutoka kwa taasisi za Serikali ni kusaidiwa kutoka kwenye umasikini kwa kasi kubwa zaidi kwa sababu wamekaa katika hali ya umasikini kwa muda wa kupita kiasi. 
  Rais Kikwete ametoa maelekezo hayo leo, Jumapili, Julai 20, 2014, wakati alipokagua shamba la kisasa la zao la buni kwenye kijiji cha Lipokela, Wilaya ya Songea, ikiwa ni moja ya shughuli zake katika siku ya nne ya ziara yake ya siku sita katika Mkoa wa Ruvuma.
  Rais Kikwete amesimama kwenye shamba hilo akiwa njiani kutoka Wilaya ya Mbinga kuelekea Wilaya ya Songea ambako leo amefungua soko la kimataifa katika kijiji cha Mkenda, kilicho mpakani kabisa mwa Tanzania na Mozambique. Baadaye, Rais amekagua daraja kwenye Mto wa Ruvuma ambalo linaunganisha Tanzania na Mozambique.
  Rais Kikwete ametoa maelekezo hayo baada ya kuambiwa kuwa pamoja na kwamba shamba hilo, pengine ni kubwa kuliko jingine lolote la buni nchini, limefanikiwa kupata miche 3,000,000 ya buni za kisasa ambayo lilihitaji lakini wakulima wa kawaida wa zao hilo la kahawa wanashindwa kupatiwa kiasi hicho hicho cha miche ya buni.
  “Kwanini tunashindwa kupata miche milioni tatu kwa ajili ya wananchi ambayo wenyewe mmesema kuwa gharama yake yak uizalisha ni shilingi milioni 900? Kwanini tunashindwa kupata miche ya kutosha ili wakulima wetu wapande na kuongeza kipatoc hao?”Rais Kikwete amemwuuliza Profesa James Teri, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Kahawa Tanzania (TACRI).

  Ameongeza Rais Kikwete: “Hatuwezi kuwabakiza wananchi wetu katika umasikini kwa miaka mingine 30 kwa sababu tu hatuna uwezo wa kuzalisha miche ya kutosha. Hatuwezi kufanya hivyo, wameishi kiasi cha kutosha katika umasikini.”         
  Amesisitiza Rais Kikwete: “Kazi yetu ni kuwatoa watu wengi zaidi katika umasikini kwa haraka kubwa zaidi kwa sababu wamechelewa mno. TACRI inaweza kufanya hivyo kwa kuwapa wananchi mbegu bora zaidi ya buni, ili waondokane na mibuni ya zamani ambayo uzalishaji wake ukochini. Hivyo, nataka kujua tunaweza kufanya nini kufanikisha hili siyo kuniambia habari ya changamoto ambazo TACRI inakumbana nazo katika kutimiza majukumu yake.”
  Ameongeza Rais Kikwete: “Siridhiki na kasi ya kujaribu kuwatoa watu wetu katika umasikini. Nahitaji kupata miche milioni tatu kwa ajili ya wananchi wetu. Kama iliwezekana kulipatia shamba hilo miche milioni tatu kwa nini isiwezekane kwa wananchi?”
              Shamba hilo kubwa la mibuni (inayozalisha kahawa) ni mali ya Kampuni ya AVIV, ambayo ni kampuni tanzu ya Kampuni ya Olam International, ambayo inaendesha shughuli za biashara katika nchi 65 duniani.

  Olam iliingia Tanzania miaka 20 iliyopita na shughuli zake kubwa ni katika mazao ya korosho na kiwanda cha kuchambua pamba kilicho Bunda, Mara.

  Duniani, Olam ina mashamba ya mibuni katika nchi tano ambazo ni Tanzania, Zambia, Ethiopia, Laos na Brazil.
  AVIV ambayo inapanda mibuni ya kuzalisha kahawa yaa ina ya Arabica ilipanda miche ya kwanza miaka mitatu iliyopita na inakaribia kuvuna kwa mara ya kwanza. Katika kijiji hicho cha Lipokela, AVIV ina ardhi yenye ukubwa wa hekta 2,000.Rais Kikwete anaendelea na ziara yake katikaMkoa wa Ruvuma leo kwa kutembelea na kukagua shughuli za maendeleo katika Wilaya ya Namtumbo.

  Imetolewa na;

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu – Dar es Salaam.

  20 Julai,2014  0 0

  1970462_1454799778083088_1638018053_n
  Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku mwanamuziki wa bendiya Vijana Jazz
  1486871_1427285270834539_2027172492_n
  Marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku aliyekuwa mwamuziki wa bendi ya Vjana Jazz enzi hizo.
  ......................................................................................................
  Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku ni Mtoto wa mwanamuziki wa zamani marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku aliyekuwa akiimba katika bendi ya umoja wa vijana Vijana Jazz enzi hizo ambapo anasema amekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu japokuwa kama ilikuwa kama kujifurahisha

  Komweta Hemed Maneti alianza muziki kama kazi mwezi Agosti mwaka 2013 akiimba katika bendi ya Vijana Jazz ambayo marehemu baba yake Mzee Hemedi Maneti Ulaya aliitumikia kwa mafanikio enzi za uhai wake.
  Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku amekuwa akijizolea umaarufu mkubwa katika bendi hiyo kwani mashabiki wengi wamekuwa wakimkumbuka marehemu baba yake mara anapoimba jukwaani kwani kwa kiasi kikubwa sauti zinaendana na marehemu baba yake.

   Bendi ya Vijana Jazz imekuwa ikipata umaarufu siku hadi siku katika maonyesho yake yanayofanyika kwenye klabu ya Kilwa Road Pub Ijumaa, Jumamosi wanapiga Jet Lumo na Jumapili kwenye ukumbi wa Vijana Hall Kinondoni.
  Komweta mpaka sasa ana Nyimbo mbili na zipo mbioni kutoka akiwa ameimba kwa kushirikiana na bendi ya Vijana Jazz mtunzi akiwa ni yeye mwenyewe nyimbo yake Inaitwa "Walimwengu" na nyingine inaitwa "Nitajuaje" ukiwa ni utunzi wa Shomary Ally lakini yeye akiwa mwimbaji kiongozi katika wimbo huo pamoja naye Julius Mwesiwa.

  Wanamuziki wakongwe waliobaki kwenye bendi ya vijana Jazz ambao waliwahi kuimba na marehemu Hemed Maneti ni Shomary Ally,Abdallah Mgonahazeru na Roshy Mselela.

  Ndoto za Komweta Hemed ni kuwa mwanamuziki wa kimataifa na kuipepeprusha vema bendera ya Tanzania ndani na nje ya mipaka ya TANZANIA ameolewa na ana mtoto mmoja wa miaka 5 anayeitwa Fahad. Anaongeza kuwa Changamoto za kazi ya muziki na malezi ni nyingi lakini muhimu ni kujua jinsi gani utapanga ratiba zako vizuri na kuhakikisha unafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mtoto na hili halinishindi natimiza majukumu yangu vizuri kama mama.

  Ni kweli kwamba mara nyingi nakuwa nafanya kazi siku za wikiendi hivyo nakosa muda wa kutosha wa kukaa na mtoto ukizingatia ndiyo siku na yeye anakuwa anapumzika haendi shule, lakini kama mama unatakiwa kujua majukumu ya familia yako ninafurahia maisha na familia yangu na mtoto wangu ni mweye furaha sana ninamshukuru mungu kwa hilo,
  hata hivyo siku za jumatatu zinakuwa zina changamoto kubwa sana hasa katika kumwandalia mahitaji yake kwa ajili ya kwenda shule kwakuwa nakuwa nimechoka na kazi.
  Mwanamuziki huyo anasema mashabiki wa bendi ya vijana wamempokea vizuri sana kusema kweli anaongeza kuwa "Nashukuru Mungu sana kwa hilo
  na hili linajidhihirisha ninapokuwa nafanya shoo zangu...watu hawakai chini mara nyingi wanakuwa wakicheza..."
  Anamaliza kwa kusema "Umaarufu wa marehemu baba Maneti upo na siwezi kuuepuka...lakini kubwa watu wananipima kutokana na utendaji na ufanisi wangu wa kazi yangu niwapo jukwaani".

  0 0

  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye amesema Chama Cha Mapinduzi hakimzuii mwanachama yeyote kutangaza nia ya kugombea Uongozi katika muhula unaofuata isipokuwa Chama kimezuia kampeni za mapema kwani ndio chanzo cha makundi ndani ya Chama akizungumza kwenye kipindi cha Baragumu kinachorushwa na Channel 10.

  Nape  alisema taratibu za kugombea Uongozi ndani ya chama zipo na kuna Kanuni mbili, moja ni ya Kanuni za Viongozi na Maadili na pili Kanuni zinazosimamia Uchaguzi ndani ya CCM, akinukuu kutoka kwenye kitabu cha Kanuni za Viongozi na Maadili ,Nape alisema "Wanachama wenye nia ya kugombea nafasi ya uongozi katika muhula unaofuata anaweza kutangaza nia ya kugombea lakini haruhusiwi kufanya kampeni kabla ya muda".

     Akizungumzia juu ya adhabu wanazopewa waliokiuka alisema adhabu hizi zina shabaha ya kuwasaidia wanachama na Viongozi kujirekebisha.Nape pia alizungumzia suala zima la upatikanaji wa Katiba Mpya,alisema CCM imeshikamana sana kiasi cha kuwachanganya Wapinzani, aliendelea kwa kusema Kanuni,Sheria zinazotumika ni makubaliano ya wote.(Wapinzani walishiriki katika kamati kutengeneza kanuni na sheria na zikapitishwa Bungeni wakiwemo na Rais akasaini).
  Chanzo: kamerayangublog.com 

  0 0

   Mkali wa kuchekesha na sanaa za majukwaani Afrika Mashariki, Anne Kansiime anatarajiwa kutoa burudani kali hapo August 2, katika ukumbi wa Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
                        
  Tukio hilo linaloandaliwa na kituo cha Radio 5 litaambatana na burudani ya muziki kutoka ODAMA Band, pamoja na mchekeshaji Fredi Omondi kutoka Kenya na Pilipili wa Tanzania.

  Akizungumzia tukio hilo Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis alisema kuwa wameamua kumualika Kansiime kwa sababu ana kipaji cha hali ya juu katika uchekeshaji na ana mashabiki wengi Tanzania.  

  “Kansiime ni mchekeshaji ambaye amejizolea umaarufu mkubwa Afrika Mashariki kwa uwezo wake wa kuweka utani kwenye maisha ya kawaida’ alisema Francis.

  Kansiime amejipatia umaarufu kupitia mitandao ya kijamiii ambako alianza kwa kuweka vipande vya video akiigiza kama mwanamke wa kiafrika anayekutana na changamoto mbalimbali za maisha.

  Mchekeshaji huyo wa kike, ambaye pia huendesha kipindi cha “Don’t Mess With Kansiime” kwenye kituo cha Citizen TV, anatajwa kuwa mwanamke mwenye kipaji cha pekee nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla. 

  Burudani hii ya Kansiime, ambayo itakwenda kwa jina la Cheka Kwa Nguvu, itaanza saa moja usiku na tiketi zitauzwa shilingi elfu 90,000 kwa mtu mmoja, na shilingi 700,000 kwa meza ya watu nane. 

  ‘Kama ambavyo mwandishi wa vitabu, Maya Angelou alivyowahi kusema, “Simwamini mtu yeyote asiye cheka” tukio hili linalenga kuonesha umuhimu wa kucheka katika maisha yetu ya kila siku” alihitimisha Francis.   0 0

  Meneja Masoko wa Airtel Tanzania Rebeca Mauma akizungumza wakati wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars iliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Baadhi ya washiriki wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars wakifutilia kwa makini moja ya mada zilizowasilishwa kwenye semina hiyo iliyofanyika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa akisisitiza jambo wakati wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars iliyofanyika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiteta na Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa wakati wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars iliyofanyika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi na Mwenyekiti wa DRFA Almasi Kasongo. 

  ==========   -==========  -========
  Katibu Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Selestine Mwesigwa amesisitiza umuhimu wa programu za vijana kwa maendeleo ya soka nchini na kuitaka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kuangalia uwezekano wa kuwa wadhamini wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20. 

  Akifungua semina elekezi kwa makatibu wakuu wa mikoa inayoshiriki mashindano ya vijana ya Airtel Rising Stars (ARS) iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi Julai 19, 2014 Mwesigwa alisema hali halisi inaonyesha kwamba miaka michache ijayo wachezaji wengi watakaounda timu ya taifa ya U-20 watatokana na ARS hivyo ni vema kampuni ya Airtel ikawa mdhamini mkuu wa timu hiyo. 

  Alisema kuwa suala la programu za vijana ni agenda namba moja ya TFF na kuzitaka timu za ligi kuu kuzingatia maagizo ya shirikisho hilo la kuwa na timu za vijana. “Klabu ya Simba imefanikiwa sana katika suala hili na ni vema timu nyingine za ligi kuu zikaiga mfano huo”, alisema Mwesigwa na kuipongeza Airtel kwa kuwekeza katika soka la vijana. 

  “Wachezaji wanapolelewa na klabu tangu wakiwa wadogo inakuwa ni rahisi kwao kuendana na maadili ya klabu hiyvo kuwa na wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu tofauti na wachezaji waosajiliwa kutoka sehemu mbali mbali wakiwa na umri mkubwa”, alisema. 

  Aliwataka makatibu hao wa mikoa kuzingatia kanuni ikiwa ni pamoja na umri ili kuwafanya vijana watakaoshiriki mashindano ya Airtel Rising Stars kuwa na ushindani ulio sawa. Mashindano ya ARS yanashirikisha vijana chini ya umri wa miaka 17. 

  Mwesigwa aliungwa mkono na Mwenyekiti wa kamati ya vijana ya TFF Ayoub Nyenzi aliyesema kuwa programu za vijana e.g. ARS ndiyo mkombozi wa kweli wa soka popete pale duniani. 
  Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi katika ngazi ya mkoa Julai 27 na kushirikisha mikoa ya Mbeya, Morogoro, Mwanza, Ilala, Kinondoni na Temeke kwa upande wa wavulana huku timu za wasichana zikitoka mikoa ya Mwanza, Mbeya, Zanzibar, Ilala, Kinondoni na Temeke. 

  Akiongea katika semina hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando aliwapongeza viongozi wa mikoa kwa kazi nzuri iliyoiwezesha Tanzania kutwaa ubingwa wa mashindano ya kimataifa ya ARS (wasichana) yaliyofanyika Nigeria na kuzawadiwa USD 10,000, medali na vikombe. 
  “Vile vile timu ya wavulana ilifanya vizuri sana na ni imani yangu kwamba mwaka huu Tanzania itashinda vikombe kwa wasichana na wavulana”, alisema na kusisitiza nia thabiti ya Airtel kuendelea kuboresha mashindano hayo. 

  Naye Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi aliwataka makatibu hao kufanyakazi kwa karibu na kamati ya vijana ya TFF inayosimamia mashindano hayo.

older | 1 | .... | 511 | 512 | (Page 513) | 514 | 515 | .... | 3270 | newer