Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 503 | 504 | (Page 505) | 506 | 507 | .... | 3278 | newer

  0 0

   Msanii wa filamu na unenguaji Mwajuma Thabiti 'Mwajuma Jimama' akiwa katika pozi na mume wake Melela Mussa baada ya kufunga ndoa hivi karibuni Ilala Bungoni na kufuatia na mnuso babu  kubwa. Bwana harusi ni mfanya bihashara na Bi Harusi ni msanii wa kujitegemea

  0 0
 • 07/12/14--20:00: Sheikh Bahero - SAUMU

 • 0 0  0 0


  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakinunua samaki katika kibanda huko Bweni Wilaya ya Pangani juzi wakati Rais alipokwenda kuzindua mradi wa maji na kuweka jiwe la msingi kwaajili ya ujenzi wa maabara shuke ya sekondari Kipumbwi. 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakinunua samaki katika kibanda huko Bweni Wilaya ya Pangani juzi wakati Rais alipokwenda kuzindua mradi wa maji na kuweka jiwe la msingi kwaajili ya ujenzi wa maabara shuke ya sekondari Kipumbwi.(picha na Freddy Maro)

  0 0

  SERIKALI kupitia Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), itaendelea kutoa mafunzo ya wafanyabiashara wadogo na wakati (SMEs) ilikuboresha zaidi mahusiano ya kibiashara na wafanyabishara wakubwa na makampuni.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji),Dkt. Mary Nagu, alisema jijini Dar es Salaam hivi karibu kuwa tayari wajasiriamali  214 wameshafaidika na mafunzo hayo hapa nchini. Miongoni mwa walionufaika 152 ni wanaume na 62 ni wanawake.
  “Kupitia mafunzo haya, wajasiriamali wadogo na wakati wataunganishwa na makampuni makubwa katika sekata za mawasiliano, ujenzi, kilimo, saruji, madini,viwanda vya samaki, bia, viwanywaji baridi na hoteli,” alisema waziri Nagu.
  Kwa mujibu wa Dkt. Nagu, Mafunzo hayo yanayojulikana kama ‘Business Linkage’ yana umuhimu mkubwa wa kuboresha mahusiano ya kibiashara katika wajasiriamali wadogo na wakati na wafanyabiashara wakubwa/makampuni.
   “Sisi kama serkali, tumedhamiria kwa dhati kuisaidia zaidi kada ya wajasiriamali wadogo na wakati kukua na kuiwezesha kuchangia ipasavya katika ukuaji wa uchumi wetu wa taifa,” aliongeza.
  Waziri Nagu alisema mafunzo hayo yameshafanyika Dar es Salaam, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya), Kanda ya Kaskazini (Kilimanjaro), na Kanda ya Ziwa(Mwanza).
  Akifafanua zaidi kuhusu mafunzo hayo ya kuboresha mahusiaono ya kibiashara,wafanyabiashara/wasambazaji 54 walihitimu mafunzo ya usambazaji bidhaa za ndani(Local Suppliers) sawa na asilimia  85.3.
  “Tayari tafiti zilizokwisha fanywa kwa wajasiriamali ambao wameshapata mafanzo zinaonyesha kuwa mpaka sasa wanafanya vizuri sana katika biashara zao,” alisisitiza waziri Nagu na kuelezea umuhimu wa mafunzo kama hayo kwa wajasiriamali.
   Kwa upande mwingine, Waziri Nagu alisema kuwa TIC ilishatembelea jumla ya miradi 99 ya wawekezaji na kutoa huduma bora (Aftercare Services) na kujenga mahusiano mazuri na wawekezaji hapa nchini.
   “Ziara hizi ambazo zimeshafanywa sehemu mbalimabali hapa nchini zilikuwa za manufaa makubwa kwani zilitoa fursa kwa kituo kusikiliza kero wanazozipata wawekezaji na kuzifikisha sehemu husika kwa ufumbuzi,” aliongeza.
  Waziri huyo mwemye dhamana ya uwekezaji na uwezeshaji, alisema kuwa serikali ya Awamu ya Nne nchini ya Dkt. Jakaya Kikwete imefanya mageuzi makubwa katika nyanja za uwekezaji hapa nchini na bado inafanya jitihada zaidi katika kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuwekeza.
   Kwa mujibu wa taarifa ya hivi karibuni ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Biashara na Maendeleo (UNCTAD), mwaka 2013,Tanzania ilikuwa na mitaji toka nje yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 12.7 ikiipita Kenya iliyokuwa na dola bilioni 3.4 na Uganda dola bilioni 8.8.

  Kwa mujibu wa takwimu hizo, kwa mwaka 2013 Tanzania peke yake ilivutia mitaji ya uwekezaji toka nje yenye thamani ya dola bilioni 1.9 na kuipita mbali Kenya iliyovutia dola milioni 514 katika kipindi hicho.

  0 0

  Mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kati ya Tanzania (Serengeti Boys) na Afrika Kusini (Amajimbos) itachezwa kwa kiingilio cha sh. 2,000.

  Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam ndiyo utakaokuwa mwenyeji wa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 9 kamili alasiri.

  Waamuzi wa mechi hiyo wanatoka Shelisheli. Mwamuzi wa kati ni Allister Barra wakati wasaidizi wake ni Gerard Pool na Jean Joseph Felix Ernest wakati mezani atakuwa Nelson Emile Fred.

  Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Andriamiasasoa Doda Nirimboavonjy kutoka Madagascar.

  Kikosi cha Serengeti Boys chini ya kocha Hababuu Ali Omari kipo kambini kwa zaidi ya wiki mbili sasa kikijiandaa kwa mechi hiyo. Mechi ya marudiano itachezwa kati ya Agosti 1 na 3 nchini Afrika Kusini.

  Wakati huo huo, Alfred Kishongole Rwiza wa Tanzania ameteuliwa kuwa Kamishna wa mechi ya marudiano ya michuano hiyo ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kati ya Rwanda na Uganda.

  Mechi hiyo itachezwa nchini Rwanda kati ya Agosti 1 na 3 mwaka huu. Waamuzi wa mechi hiyo watatoka Burundi wakiongozwa na Pacifique Ndabihawenimana.

  BONIFACE WAMBURA
  OFISA HABARI NA MAWASILIANO

  SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0

  Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine (kushoto), akikabidhi Shs. milioni 5 kwa Mwenyekiti wa Vikoba Kata ya Engutoto, Bilhuda Kisasa,  ikiwa ni sehemu ya mchango wake wa shs. milioni 10 alizoahidi kuwasaidia akinamama wa kata hiyo. (Na Mpiga Picha Wetu)
  Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine (kulia), akizindua katiba ya vikundi vya vikoba katika kata ya Engutoto Wilayani Monduli jana. Hafla hiyo ilikwenda sambamba na harambee ya kutunisha mfuko wa vikoba, ambapo katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 12 zilipatikana. Kushoto ni Mwenyekiti wa vikoba kata ya Engutoto, Bilhuda Kisasa .

  Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine (kulia), akizindua katiba ya vikundi vya vikoba katika kata ya Engutoto Wilayani Monduli jana. Hafla hiyo ilikwenda sambamba na harambee ya kutunisha mfuko wa vikoba, ambapo katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 12 zilipatikana. Kushoto ni Mwenyekiti wa vikoba kata ya Engutoto, Bilhuda Kisasa . 
  ==========  =======  =======
  WANACHAMA wa vikundi vya kuweka na kukopa (VIKOBA) mkoani Arusha wametakiwa kutumia na kupanga vizuri matumizi ya fedha wanazokusanya ili ziwasaidie kutoka daraja mhadi jingine katika maisha yao.

  Kauli hiyo ilitolewa jana wilayani hapa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha Namelok Sokoine alipokuwa akiendesha utunishaji wa fedha kwa Umoja wa Wanavikoba wa Kata ya Engutoto yenye vikundi 20 na wanachama 600.

  Katika utunishaji huo, Namelok alichangia Sh. Milioni 10 huku kiasi cha Sh. Milioni 12 kikipatikana katika shughuli hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Umoja wa Wanawake UTW wilayani Monduli.

  Akizungumza na wanavikundi hao Mbunge Namelok aliwataka wanawake kujitokeza na kujiunga katika vikundi huku akiwataka kuacha kuogopa kufanya shughuli za ujasiriamali.

  “Wanawake nawaomba sana muendelee kujitokeza na kujiunga katika Vikoba kwani huku ndipo eneo ambalo litatuwezesha tuwe na sauti ya kujitegemea kimapato.

  “Lakini pia naomba niwakumbushe jambo muhimu hizi fedha tunazokusanya nawaomba sana muonyeshe mfano wa kuzitumia vizuri ili kesho zitusaidie kutoka daraja moja kwenda daraja jingine katika maisha yetu,” alisema Namelok.

  Kwa upande wake Katibu wa UWT Kata ya Engutoto Glory Emmanuel alisema wana vikundi wengi waliopo kwenye vikoba wanakabiliwa na changamoto ya elimu ya ujasiriamali.

  “Tunaomba suala la ofisi za vikoba uliangalie kwani vikundi havina ofisini.Pia wanachama hawana elimu hatua inayosababisha kukopa na kutumia sivyo kutokana na kutokuwa na elimu ndogo ya biashara,” alisema Glory.

  Naye mwana kikundi Zaituni Mwishehe alibainisha jinsi alivyonufaika na kuwa katika vikundi hivyo vya kuweka na kukopa ambapo hadi sasa ameweza kujitegemea katika matumizi ya kawaida ndani ya nyumba.

  “Sasa hivi naweza kulipia michango midogomidogo ya mwanangu shuleni. Lakini pia hata kutatua matatizo mengine ya kifamilia kupitia mikopo ninayochukua kwenye kikundi bila hata kumsubiria mume wangu,” alisema Zaituni.

  0 0

  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Jasmine Kairuki (MB) anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku tano kuanzia Jumatatu, Julai 14  hadi Ijumaa 18, 2014 katika jiji la Dar Es Salaam akitembelea asasi mbalimbali zinazotoa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi kwa lengo la kujionea huduma zinazotolewa na asasi hizi ikiwa ni pamoja na kukutana na wananchi wanaopata huduma hii. 

  Pamoja na kujionea huduma hizi Mh. Naibu Waziri anatarajiwa kujionea ufanisi wa kazi zinazofanywa na asasi hizi, changamoto zinazowakabili pamoja na kupokea maoni, ushauri na kubadilishana mawazo ili kujua jinsi ambavyo serikali inaweza kuboresha utoaji wa huduma hii.

  Katika ziara hiyo, Mhe. Kairuki anatarajia kutembelea jumla ya asasi 13 ikiwa ni pamoja na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Taasisi ya Haki za Binadamu na Mazingira (Envirocare), Kamati ya Msaada wa Kisheria ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Nyingine ni pamoja na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC) na Kituo Kinachoshughulikia Maslahi ya Wanawake na Watoto (TWCWC).

  Taasisi nyingine atazozitembelea ni Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wajane na Watoto  (CWCA), Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Kituo cha Msaada wa Kisheria cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Nyumba ya Amani na Ofisi ya Mfuko wa Huduma za Kisheria (Legal Services Facility).

  Mheshimiwa Kairuki anatarajia kumaliza ziara yake siku ya Ijumaa, Julai 18, 2014 kwa kutembelea Sekretariati ya Msaada wa Kisheria Tanzania ijnayoratibu shughuli za utaoji wa Msaada wa Kisheria Tanzania na kisha kufanya mkutano wa majumuisho na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria kuanzia saa 5:00 asubuhi.

  Imetolewa na Wizara ya Katiba na Sheria,
  Dar es Salaam,
  Jumapili, Julai 13, 2014

  0 0

   Mbunge wa jimbo la Kilolo Prof. Peter Msola akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwatasi katika kata ya Bomalang'ombe katika jimbo la Kilolo wilayani Kilolo Mkoani Iringa.
   baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mwatasi waliohudhuria mkutano wa hadhara katika kiwanja cha shule ya msingi Mwatasi wakisikiliza hotuba ya mbunge wao Prof Peter Msola
   Mmoja wa wakazi wa jimbo la Kilolo, Ayubu Sanga akitoa taarifa ya kijiji cha Mwatasi mbele ya Mbunge wa jimbo hilo Prof. Peter Msola


   -============ 
  Na Denis Mlowe, Kilolo
   
  MBUNGE wa jimbo Kilolo, Profesa Peter Msola amewataka wananchi wa jimbo hilo kuwekeza katika elimu kwa kuwapeleka watoto wanaotakiwa kuanza shule na kuondokana na janga la kukosa elimu katika wilaya hiyo.
   
  Profesa Msola aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kilolo katika kijiji cha Mwatasi kata ya Bomalang’ombe wakati wa ziara ya siku moja kwa wananchi wa jimbo hilo juzi na kusisitiza umuhimu wa wazazi kuwaelimisha na kuwapatia elimu watoto wao.
   
  Msola alisema kuna wazazi ambao wanashindwa kuwekeza katika elimu na kuwafanya watoto wao kukimbilia mijini ambapo maisha ya huko ni magumu bila kuwa na elimu na kuwataka kukazania elimu kwa watoto wao kwanza.
   
  Alisema kuwa  maendeleo miongoni mwa jamii yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na kiwango cha uwekezaji katika elimu, ni vema jamii iwekeze kwa kiwango kikubwa katika sekta ya elimu ili kujikwamua na umaskini uliopo na kupambana katika soko la ajira. 

  “Tukumbuke kwamba kuwekeza katika elimu ni mkakati wa muda mrefu unaohitaji dhamira, subira na kwamba matokeo yake huonekana baada ya muda mrefu wa uwekezaji na faida kwa wazazi mara baada ya mtoto kusoma na kuweza kumsaidia pindi azeekapo” alisema Prof. Msola
   
  Aidha Prof Msola alisema wilaya ya Kilolo ina rasilimali nyingi zinazohitaji viongozi wabunifu watakaohakikisha zinatumiwa vizuri kwa faida ya watu wote hivyo bila kuwekeza katika elimu rasimali hizo zitatumiwa vibaya na watu wasiojua faida ya elimu.
   
  Aliongeza kuwa  katika mipango yake ya kuifikisha wilaya hiyo kwenye kilele cha mafanikio, atahakikisha barabara zinazotakiwa kuiunganisha wilaya hiyo na wilaya nyingine zaidi zinajengwa.
   

  Alisema hatua hiyo itaongeza shughuli za uwekezaji, utalii, kilimo na biashara na hivyo kuwaongezea kipato wananchi wake.

  0 0

   Maafisa wa Ubalozi, Bwana Amos Msanjila na Dada Caroline Chipeta, Wakimkaribisha Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Mizengo Pinda na Mkewe (Mama Tunu Pinda) walipowasili katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, London
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Mizengo Peter Pinda akipokewa, kukaribishwa na kusalimiana na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi pamoja na Wawakilishi wa Jumuiya za Watanzania waishio nchini Uingereza.

   Baadhi ya Watanzania waliohudhuria Mkutano wao na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Mizengo Pinda, alikutana na kuzungumza na Watanzania wanaoishi nchini Uingereza siku ya Jumamosi tarehe 12 Julai 2014, mara baada ya ziara yake fupi ya kikazi nchini humo.

  Mkutano huo na Watanzania ambao uliofanyika Ubalozini, Mheshimiwa Waziri Mkuu alitoa taarifa mbalimbali za maendeleo nchini, hususan mchakato wa Katiba mpya, sera ya Diaspora na maandalizi ya chaguzi mbalimbali zinazokuja. 
  Mkutano huo ulimalizika kwa maswali na majibu na baadae wananchi kupiga picha na Waziri Mkuu kama inavyoonekana kwenye picha hizi hapo chini.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wananchi kwenye  kilele cha Sherehe za Miaka 78 ya kanisa la Tanzania Assemblies of God  katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo Julai 13, 2014. 
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua kitabu cha  Tanzania Assemblies of God (TAG) akiwa na  Askofu Mkuu wa TAG Dkt Barnabas Weston Mtokambali wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 78 ya kanisa hilo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo Julai 13, 2014
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa tuzo na Askofu Mkuu wa Tanzania Assemblies of God (TAG) Dkt Barnabas Weston Mtokambali wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 78 ya kanisa hilo katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya leo Julai 13, 2014.PICHA NA IKULU
     

  0 0
 • 07/13/14--20:00: MAULID YA HOMU, ZANZIBAR

 • 0 0

  Mgeni rasmi kwenye kikao kilichoambatana na mafunzo ya mfuko wa taifa wa bima ya afya mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Lindi Vijijini bi Oliver Vavunge,ambapo aliwataka wawakilishi wafanyakazi kuwakumbusha kutimiza wajibu ili maslai yaweze kuboreka sanjari na kusisitiza kuwa watambue NHIF ina msaada mkubwa kwao na kwetu kama waajiriwa hivyo watumishi wa sekta ya afya wana jukumu kubwa la kusimamia huduma ili ziboreke zaidi kupitia fedha zinazolipwa kupitia bima ya afya,kushoto ni mwenyekiti Talgwu mkoa wa Lindi.
  Washiriki wakimsikiliza kwa makini hayupo pichani meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya mkoa wa Lindi Bi Fortunata Raymond,ambapo aliweka bayana makusudio ya ofisi ya Mkoa wa Lindi ilivyoweka mkakati wa kutoa elimu inayohusu umuhimu na faida za kujiunga na mifuko ya afya ya jamii(CHF), sanjari na maboresho ya kitita cha mafao cha NHIF kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi mkoani Lindi.
  katibu wa Kamati ya uratibu Talgwu Mkoa wa Lindi ndg kambogoro Rashidi akitoa  taarifa ya  madhumuni ya mkutano wa mwaka wa viongozi na kamati ya uratibu na utoaji wa elimu kutoka NHIF kwa mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Lindi Vijijini Oliva Vavunge.
  Meneja wa mfuko mkoa wa Lindi Fortunata Raymond akifafanua jambo kwa mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Lindi Vijijini Bi Oliva Vavunge wa pili kulia..
   Meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya mkoa wa Lindi Fortunata Raymond,akitoa elimu kwa viongozi na wawakilishi wa Talgwu ngazi ya kata na mkoa,kuhusu faida za kuwa mwanachama wa NHIF na mfuko wa afya ya jamii CHF kwenye ukumbi wa kanisa katoliki la Mt. Francisi Axvery mkoani Lindi Jana

  0 0

  Kati ya Juni 25 na Julai 6, jiji la Washington DC lilikuwa mwenyeji wa maonyesho ya kila mwaka ya yanayohusu maisha a watu na jamii mbalimbali.
  Mwaka huu, nchi ya Kenya ilishirikishwa, wakionyesha utamaduni wao na changamoto za kuzidumisha katika zama hizi za sayansi na teknolojia.
  Kwanza Production ilipata fursa ya kutembelea maonyesho hayo na kuzungumza na baadhi ya washiriki wa maonyesho hayo ambapo walieleza mengi ya kufurahisha.
  KARIBU UUNGANE NASI

  Zaidi ya washiriki 100 kutoka nchini Kenya waLIkuja hapa jijini kuonyesha mambo mbalimbali kama kutengeneza vyungu kwa ufinyanzi, uchongaji vinyago, mapambo ya shanga, useremala, nakshi za majengo, ujenzi wa majahazi, mapishi , muziki na mengine yanayotunza utamaduni wa nchi hiyo
  Maelezo ya ujenzi na sehemu za JAHAZI (DHOW) toka kwa Ali Skanda aliyetoka Lamu Kenya
  Na mtangazaji mkongwe abdushakur Aboud mbele ya Jahazi lililoletwa kwenye makumbusho ya hapa Washington DC kutoka Lamu nchini Kenya
  Mtaalamu wa mapambo yatokanayo na shanga na usimamizi wa filamu nchini Kenya Emmah Irungu
  Mwandishi wa habari kutoka Kenya BMJ Mureithi

  0 0

   Ujumbe kutoka Tanzania ukiwa Chuo Kikuu cha Calgary katika jimbo la Alberta nchini Canada.Katika picha kutoka kushoto ni, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (wa saba), Naibu Waziri TAMISEMI, Kassim Majaliwa (wa tano), Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Ummy Mwalimu (wa sita). Wabunge, Richard Ndasa (wa nne), Deogratias Ntukamazina (wa tatu), Murtaza Mangungu  (wa pili) na Shafin Sumar (wa kwanza kushoto. Wengine (kulia) ni wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na watendaji kutoka Chuo Kikuu cha Calgary, Canada. 
  Ujumbe kutoka Tanzania ukiwa katika makao makuu ya Taasisi ya Udhibiti Nishati katika jimbo la Alberta nchini Canada.Katika picha ni, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (wa sita kutoka kulia), Naibu Waziri TAMISEMI, Kassim Majaliwa (wa tano kutoka kulia), Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Ummy Mwalimu (wa tatu kushoto). Wabunge, Richard Ndasa (wa nne kutoka kulia), Raya Khamisi (wa pili kutoka kulia). Wengine ni wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na watendaji kutoka Mamlaka ya Udhibiti Nishati ya Alberta wakiongozwa na Zeeshan Syed, Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kitaifa, Kimataifa na Serikali, (wa tatu kutoka kushoto).

  ============  =========  =========
  Serikali yashauriwa kuwabana wawekezaji.

  Serikali ya Tanzania imeshauriwa kuweka sheria madhubuti zitakazohakikisha wawekezaji wa kigeni wanaleta faida katika nchi badala ya kunufaisha makampuni yao tu.


  Hayo yamesemwa na Bw. Zeeshan Syed, Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kitaifa, Kimataifa na Serikali katika Taasisi ya Udhibiti Maendeleo ya Nishati ya Jimbo la Alberta nchini Canada wakati alipokuwa akizungumza na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga uliofika katika makao makuu ya Taasisi hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara ya mafunzo kuhusu sekta ya uziduaji.


  “kwa kawaida wananchi huwa wana matarajio makubwa ya manufaa ya rasilimali zinazowazunguka hivyo ni muhimu kwa serikali kuwa na sheria zitakazowabana wawekezaji ili wanapomaliza shughuli zao, pia faida ibaki kwa wananchi” Alisema Bw.Syed.


  Mkurugenzi huyo alieleza kuwa licha ya taasisi hiyo kuwa mdhibiti wa nishati lakini pia ina jukumu la kudhibiti uhifadhi wa mazingira ili kuhakikisha kuwa shughuli za uendelezaji wa nishati zinafuata sheria za nchi za utunzaji mazingira.


  Naye Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga alimweleza Bw.Syed kuwa licha ya Tanzania kuwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) lakini bado nchi inahitaji kujifunza kutoka kwa nchi nyingine zenye uzoefu ili kuboresha shughuli za udhibiti nchini Tanzania.


  “Shughuli za udhibiti nishati katika Taasisi hii zina zaidi ya miaka 75 na hivyo Tanzania inahitaji kupata uzoefu kutoka kwenu ili kufahamu hatua mlizopitia kufika hapa mlipo leo”. Alisema Waziri Kitwanga.

  Wakati huohuo Naibu Waziri na ujumbe wake unaojumuisha baadhi ya wabunge kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini walitembelea Chuo Kikuu cha Calgary ambacho kimebobea katika kutoa elimu juu ya masuala ya sera za Uchumi, Nishati, Mazingira na kutoa ushauri katika utengenezaji sera katika sekta ya uziduaji.


  Katika Chuo hicho ujumbe huo ulikutana na Mkurugenzi anayeshughulikia Sera za Umma, Bw.Jack Mintz ambaye   aliueleza ujumbe huo kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi sita duniani (huku ikiwa ni pekee kutoka Afrika) ambazo zinapewa kipaumbele na chuo hicho katika masuala ya ushirikiano wa kujenga uwezo kwenye masuala ya sera.


  Mkurugenzi huyo alieleza kuwa, Chuo cha Calgary pia kitashirikiana na Tanzania katika kuwajengea uwezo watumishi kwa kutumia pia vyuo vingine ambavyo wana ushirikiano navyo na kwamba mafunzo hayo yanaweza kufanyika ndani na nje ya Tanzania .


  Pamoja na suala la kujenga uwezo kwa watanzania ili kuweza kuandaa sera zitakazokuwa na manufaa kwa nchi Bw.Mintz aliueleza ujumbe huo kuwa ni muhimu kwa serikali ikawa ndiyo msimamizi mkuu wa rasilimali  za nchi ili faida zinazotokana na rasilimali hizo ziwafikie wananch wote.


  Naye Naibu Waziri Katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Majaliwa pamoja na kushukuru kwa Tanzania kupewa kipaumbele na Chuo hicho katika kujenga uelewa, alimweleza Mkurugenzi huyo wa Chuo kuwa Tanzania kwa sasa inakaribisha wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza Tanzania hivyo suala la kupata elimu na uzoefu zaidi ili kuendana na kasi ya uwekezaji linapewa kipaumbele. 

  0 0

  Hiyo ndiyo mfano wa hundi ya shilingi milioni 42 iliyotolewa na kampuni ya TanzaniteOne kwa shule hiyo ya New Vision ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ambapo ina wanafunzi 400 kati yao 67 ni watoto yatima (kushoto) ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya TanzaniteOne Halfani Hayeshi.
   Katibu Tawala wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Elias Ntiruhungwa akionyesha picha iliyochorwa na mwanafunzi wa shule ya msingi New Vision, Gift Junior baada ya shule hiyo kukabidhiwa msaada wa sh42 milioni na kampuni ya TanzaniteOne kulia ni Mkurugenzi wa shule hiyo Recho Robinson Mneney.
   Mchungaji wa KKKT, Usharika wa Imanueli, Dayosisi ya Meru, Ernest Mola, ambaye pia ni Mwenyekiti wa bodi ya shule ya msingi New Vision akisoma risala ya shule hiyo kwenye hafla ya shule hiyo kukabidhiwa sh42 milioni na kampuni ya kuchimba madini ya TanzaniteOne.

   Ofisa wa Polisi Jamii Tarafa ya Moipo Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, As/Insp Amiry Mlemba akiwa kwenye tafrija ya shule ya msingi New Vision ya Mji mdogo wa Mirerani kukabidhiwa sh42 milioni na kampuni ya kuchimba madini ya TanzaniteOne.

   Wanafunzi wa shule ya msingi New Vision wakishuhudia tukio la shule hiyo kukabidhiwa sh42 milioni na kampuni ya TanzaniteOne.

  0 0

   Maofisi wa Magereza la Isangaa - Dodoma Afande Kapitukaa Pamoja na Afande Hassan wakikagua msaada wa chakula kutoka Taasisi ya Kalamu Education Foundation kama Mchango wao kwa wafungwa katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Pamoja na Maofisa hao Kulia ni Dada Safia na Dada Amina kutoka taasisi hiyo. 
  Wajumbe wa Kalamu Education Foundation Dada Safia na Dada Safina Mara Baada ya Kutoa Shukran kwa Ushirikiano walioupata kutoka kwa Jeshi la Magereza kuhakikisha kwamba wafungwa wanakumbukwa na Jamii vipindi maalum hasa vya kiroho kwani wengi hupata faraja na kuona bado ni sehemu ya Jamii husika na huchangia kuhamasika kiroho na kuwa raia wema.

  0 0

   Germany ndio mabingwa wa kombe la Dunia  2014 FIFA World Cup, wakinyakua kombe kwa mara ya nne katika historia yao baada ya kuwashinda  Argentina 1-0 kwa bao la muda wa nyoingeza la  Mario Gotze (pichani juu kushoto) katika uwanja wa Maracana huko Rio de Janeiro.

  Mchezaji huyo aliyeingia kama mchezaji wa akiba aliweza kuua uwezekano wa kupigiana penati kwa bao lake la uamuzi baada ya timu hizo kutoka suluhu hadi mapumziko katika mchezo uliojaa kila aina ya msisimko. Bao lake hilo liliwamaliza kabisa Argentina ambao walishindwa kujibu mapigo, na Germany wakaongeza nyota ingine katika historia yao kufuatia ubingwa wao wa mwaka 1954, 1974 na 1990.

  Wananchi wa Bagamoyo wakifuatilia mchezo wa fainali za kombe la Dunia usiku wa kuamkia leo ambapo Germany ilifanikiwa kunyakua kombe hilo dhidi ya Argentina ya kina Messi

  0 0


   Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakishiriki katika futari iliyoandaliwa na Idara ya rasilimali ya kampuni hiyo  kwa ajiri ya wafanyakazi wake  ikiwa ni sehemu ya  muendelezo wa mfungo wa mwezi  mtukufu wa ramadhani. Hafla hiyo ilifanyika makao Makuu Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  .Meneja wa Vodacom Foundation,Grace Lyon akishiriki katika futari iliyoandaliwa na Idara ya rasilimali ya kampuni hiyo  kwa ajiri ya wafanyakazi wake  ikiwa ni sehemu ya  muendelezo wa mfungo wa mwezi  mtukufu wa ramadhani. Hafla hiyo ilifanyika makao Makuu Mlimani City jijini Dar es Salaam.
   :Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakishiriki katika futari iliyoandaliwa na Idara ya rasilimali ya kampuni hiyo  kwa ajiri ya wafanyakazi wake
   :Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakishiriki katika futari iliyoandaliwa na Idara ya rasilimali ya kampuni hiyo  kwa ajiri ya wafanyakazi wake
   Mkuu wa Idara ya Mauzo na biashara wa Vodacom Tanzania Ally Z.Ally akishiriki katika futari iliyoandaliwa na Idara ya rasilimali ya kampuni hiyo  kwa ajiri ya wafanyakazi wake  ikiwa ni sehemu ya  muendelezo wa mfungo wa mwezi  mtukufu wa ramadhani. Hafla hiyo ilifanyika makao Makuu Mlimani City jijini Dar es Salaam.
   Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania, Salehe Mohamed akishiriki katika futari iliyoandaliwa na Idara ya rasilimali ya kampuni hiyo  kwa ajiri ya wafanyakazi wake  ikiwa ni sehemu ya  muendelezo wa mfungo wa mwezi  mtukufu wa ramadhani. Hafla hiyo ilifanyika makao Makuu Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakishiriki katika Futari iliyoandaliwa na Idara ya rasilimali watu ya kampuni hiyo  kwa ajili ya wafanyakaziwake  ikiwa ni sehemu ya mwenzi mtukufu wa ramadhani hafla hiyo ilifanyika makao Makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Mlimani City jijini Dar es Salaam

  0 0


  Meneja  Biashara Kanda ya Ziwa Raphael Daudi (wa tatu kutoka kulia) akiwa na Meneja wa Masoko Kanda Emanuel Raphael (wa kwanza kulia) pamoja na  Meneja wa Airtel mkoa wa Mwanza David Wankulu wakikabidhi msaada wa chakula cha kufuturisha katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  kwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kuendeleza Quran na Suna Tanzania (JUQUSUTA)  Twaha bin Bakari Utari (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha na wadau wengine wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza.
  Vijana wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza wakishusha vyakula toka katika gari la wadau wa Airtel ambao wamedhuru katika kituo hicho kwaajili ya kusababisha tabasamu kwa watoto hao kwa kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani..
  Upakuaji ukiendelea.
  Ni sukari, chumvi, majani ya chai, mchele, sabuni, mafuta, unga wa sembe, unga wa ngano, juice za matunda na vinginevyo kama sehemu ya msaada wa chakula toka Airtel Tanzania kwa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza. 
  Picha zaidi BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 503 | 504 | (Page 505) | 506 | 507 | .... | 3278 | newer