Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 502 | 503 | (Page 504) | 505 | 506 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. James Kajugusi akisisitiza jambo wakati akiwahamasisha vijana wa Mchinga kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali ili kuunda SACCOS ya vijana. Kulia ni Afisa Tarafa ya Mchinga, Bi.Hadija Mringwa. (Picha zote na Concilia Niyibitanga,Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo)
  Afisa Kata wa Kata ya Mchinga, Bi. Sharifa Mkwango, akisisitiza jambo kuhusu vijana kujiunga katika vikundi vya uzalizashaji mali.

   Vijana  wa  Kata ya Mchinga, Lindi Vijijini  wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bw. James Kajugusi  (hayupo pichani) wakati akiwaelekeza namna ya kuunda vikundi na kupata mikopo kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana mwishoni mwa wiki.
  ============  ========  =========

  Serikali imewataka vijana Mchinga kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kujiinua kiuchimi na kuleta maendeleo ya taifa kwa ujumla. Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Bw. James Kajugusi alipokuwa anaongea na Vijana wa Halmashauri ya Lindi Vijijini Kata ya Mchinga jana  kuhusu masuala ya maendeleo ya Vijana.Bw. Kajugusi amewaeleza vijana umuhimu wa kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali  ili kuunganisha nguvu za kimtaji na kufikiri kwa pamoja namna ya kuboresha maisha yao ya kila siku.

  Vijana wanapokuwa katika vikundi ni rahisi sana kutambulika nani yuko wapi anafanya nini na anahitaji nini hivyo kuirahisishia Serikali kuwasadia. Amesema Bw. Kajugusi.

  Amesema kuwa kijana wa sasa anatakiwa kujitambua na kujua kuwa yeye ndiyo tegemeo la taifa hivyo kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo yeye mwenyewe na taifa kwa ujumla.


  Changamoto kubwa ya vijana ni kutojitambua hivyo kufikiri kwamba wanahitaji mitaji kwanza wakati bado hawana hata wazo la kuwekeza na mtaji huo. Amesema Bw. Kajugusi. Amesema kuwa ni muhimu vijana hao wakajiunga katika vikundi vya uzalishaji mali ili waweze kuunda SACCOS yao kwa ajili ya kupata fedha ya mkopo kutoka katika Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili kukuza mtaji na kuzalisha mali kwa ajili ya maendeleo endelevu.

  Bw. Kajugusi amewaeleza kuwa kupitia SACCOS ya vijana wataweza kupatiwa mikopo yenye riba nafuu ya asilimia 10 ya mkopo ambapo asilimia 5 ya riba hiyo inabaki kwenye SACCOS husika, asilimia 2 inabaki Halmashauri na asilimia 3 inarudi mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili kuutunisha na kuwawezesha vijana wengine kukopa.   Aidha, amewataka vijana kujali afya zao hususan kuepuka matumizi ya dawa za kulevya kwani yanaharibu akili na viungo vya mwili hivyo kuathiri kiwango cha kufikiri na kuathiri utendaji kazi na uzalishaji wa kijana.

  Halikadhalika, amewataka kujikinga na magonjwa ya zinaa na mimba za utotoni ili kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya jamii. Naye Afisa Tarafa ya Mchinga, Bi. Hadija Mringwa aliwataka vijana wa Kata hiyo kuhakikisha kuwa wanakamilisha zoezi la kujiunga katika vikundi na kuanzisha SACCOS mapema iwezekanavyo ili waweze kufaidi fursa ya mkopo kutoka katika Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.

  0 0

  NI MIAKA ISHIRINI IMEPITA TANGU MTUTOKE GHAFLA, WATOTO WENU PAMOJA NA FAMILIA KWA UJUMLA TUNAWAKUMBUKA SANA KILA KUNAPOKUCHA KWA UPENDO MWINGI NA MALEZI MAZURI MLIOTUACHIA.
  SISI WATOTO WENU, WILBARD, EDWIN, GODWIN, ELVIRA, ELMA NA AVELINA TUNAMUOMBA MUNGU AWAPUMZISHE KWA AMANI. MISA YA KUMBUKUMBU ITAFANYIKA DAR ES SALAAM, PAROKIA YA KIMARA JUMAMOSI TAREHE 12/07/2014.

  0 0

  Ujumbe wa Tanzania uliopo nchini Canada kwa ziara ya mafunzo ukiongozwa na Naibu Waziri Nishati na Madini, Charles Kitwanga (aliyenyoosha mkono), ukiwa katika chumba cha kusimamia mitambo ya kuzalisha methano (haionekani pichani) katika kiwanda cha kuzalisha malighafi hiyo kilicho katika jimbo la Alberta nchini Canada.
  Ujumbe wa Tanzania uliopo nchini Canada ukiongozwa na Naibu Waziri Nishati na Madini, Charles Kitwanga (wa nne kutoka kushoto, waliosimama), ukiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa kampuni ya kimataifa ya kuzalisha na kusafirisha methano ya nchini Canada mara baada ya kufanya ziara ya mafunzo katika kiwanda hicho. Wengine katika picha ni Naibu Waziri, TAMISEMI, Kassim Majaliwa, (wa nne kutoka kulia, waliosimama). Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Ummy Mwalimu, (wa pili kutoka kulia waliosimama) pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

  Kampuni ya kimataifa inayotengeneza na kusafirisha malighafi methano ya nchini Canada  ‘Methanex’ imeeleza Kuwa Tanzania ni moja ya maeneo muhimu duniani yanayofaa kwa uwekezaji wa viwanda vya kutengeneza malighafi hiyo ambayo inatumika    kuzalisha kemikali mbalimbali kutokana na uwepo wa  hazina kubwa ya gesi asilia.

  Hayo yamesemwa na Bw.Kevin Handerson, Makamu wa Rais wa kampuni ya Methanex kwa upande wa Amerika Kaskazini wakati alipokuwa akizungumza na ujumbe wa  Tanzania ulioongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga uliofika katika kiwanda cha kuzalisha methano kilicho katika  jimbo la Alberta nchini Canada ikiwa ni sehemu ya ziara ya mafunzo  kuhusu  usimamizi na uendelezaji wa tasnia ya uziduaji.

   Bw.Handerson ameeleza kuwa uzalishaji wa methano  utakuwa na  manufaa makubwa kwa Tanzania   kutokana na malighafi hiyo kutumika  katika masuala mbalimbali ikiwemo kutengeneza vifaa  vya plastiki, gesi inayotumika majumbani, kutumika kwenye vyombo vya usafiri, viwanda vya kutengeneza rangi,  viwanda vya mbao, kuzalisha umeme, kusafishia maji n.k

  " Pamoja  na Tanzania Kuwa ni eneo muhimu kwa uwekezaji wa viwanda hivi vya kuzalisha methano ni muhimu Serikali ikatenga    eneo maalum  kwa ajili ya uwekezaji wa namna hii, na kuzingatia uwepo wa sera,  sheria, kanuni  madhubuti zinazoongoza sekta hii, pia kuwe na miundombinu imara ya usafirishaji, maji, umeme wa uhakika pamoja na uwepo wa  rasilimali watu". Alisema Bw. Handerson

  Akieleza kuhusu uwezo wa kampuni hiyo,  Makamu Rais wa Methanex amesema kuwa, kampuni hiyo  ina uwezo wa kuzalisha  tani milioni 8.5 za methano kwa mwaka  na   husafirisha  malighafi  hiyo  katika  sehemu mbalimbali duniani ikiwamo  Hongkong, Shanghai, Beijing, Seoul, Tokyo, na Brussels.


   Vilevile Bw. Handerson ameeleza kuwa kampuni hiyo ya Methanex ipo  tayari kuja  kuwekeza nchini Tanzania kwa kuwa wanauzoefu wa zaidi ya miaka 40 katika uwekekezaji wa viwanda hivyo, wana mfumo mzuri wa kutoa mafunzo kwa wazawa ili kushiriki katika miradi ya methano, vilevile wako tayari kushirikiana na serikali ya Tanzania ili kuendeleza  rasilimali hiyo kwa manufaa ya wananchi.

  Naye Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Charles Kitwanga  aliikaribisha kampuni hiyo kuja kuwekeza nchini Tanzania kwa kuwa kuna kiasi kikubwa cha gesi asilia cha zaidi ya futi za ujazo trilioni  50 ambacho pamoja na kutumika kuzalisha umeme pia inaweza kutumika  kwa shughuli nyingine za kiuchumi ikiwamo kutengeneza methano na mbolea.

  Alisema kuwa kuwa serikali  ya Tanzania  inakaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika sekta za Nishati na Madini ili kuleta maendeleo endelevu ya sekta hizo na kwamba zipo   sera, sheria na kanuni nzuri ambazo pamoja na mambo mengine zinalenga kuvutia  uwekezaji katika tasnia hiyo.

  Katika Ziara hiyo ya Mafunzo, Naibu Waziri Kitwanga ameambatana na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu  ya Bunge ya Nishati na Madini, Naibu Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira,  Ummy Mwalimu na Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ( TAMISEMI), Kassim Majaliwa.

  0 0

  On 9th July over 500 past and present Chevening Scholars representing 118 countries gathered at Chevening House to mark 30 years of the UK’s most prestigious scholarship programme and to invite the brightest graduates around the world to apply.

  Deputy Permanent Secretary of the Ministry of Information, Youth, Culture and Sports, Prof. Elisante Ole Gabriel was chosen among the Chevening alumni to represent Tanzania in an historical event celebration.

  “I have been lucky to be selected among the six (6) Chevening candidates in 1998 out of 9,000 applicants. The recruitment process of Chevening Scholarships is clean and professional. I benefited a lot from my experience, exposure and knowledge gained for the time I spent in the UK under Chevening scholarship. Therefore, I can boldly say, I am what I am today because of Chevening scholarship” said Prof. Elisante Ole Gabriel.

  The event was hosted by Minister of State in the Foreign and Commonwealth Office, Hugo Swire. The Chevening Scholarships Programme finances graduates from around the world with potential to be influential leaders and decision makers to study postgraduate courses at British universities.

  The Alumni attending the 30th anniversary event included some of the most prominent people from the programme’s history including Mr Sigmundur Davíð Gunnlaugsson, Prime Minster of Iceland and Dr Hania el Sholkamy, Professor - Social Research Center, the American University, Cairo, highlighting the strength of the global network the UK Government has built up through the Scholarships.

  Minister of State Hugo Swire said: “This event shows how successful the Chevening Scholarships programme has been in building relationships for the UK with decision makers in businesses and Governments all around the world.

  “Following the tripling of scholarships set out by the Chancellor in his Budget, I hope this event will encourage the brightest graduates around the world to apply to study in the UK so we can continue to build mutually beneficial and long-lasting relationships.”

  Chevening Alumni Nart Dohjka from Jordan said: “Being a Chevening Scholar marks a graduate out as someone with drive and ability, and also as someone who wants to contribute to the development of their country. It offers students like me a unique opportunity to gain academic experience and at the same time to broaden our global and social outlooks.

  Above all, it empowers us with a sense of pride and responsibility. I believe that the role of Chevening scholars is very important in building bridges between their home countries and UK universities. In short, a Chevening Scholar learns how to be an ambassador for knowledge and for leadership.”

  The event included an exhibition of the GREAT campaign to promote Britain as one of the best countries in the world to visit, study and do business with to influential decision makers from around the world.

  0 0


  0 0

  Katibu wa Kikundi cha Sayari, Bibi. Mwanaisha Ali akikabidhi Risala ya Kikundi hicho kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bibi. Sihaba Nkinga mwishoni mwa wiki alipotembelea kikundi hicho kwa ajili ya kukagua maendeleo ya shughuli za vikundi vya Vijana Wilayani Kilwa, Mkoani Lindi.
  Mwenyekiti wa Kikundi cha Sayari, Bw. Ramadhan Sungura akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bibi. Sihaba Nkinga (hayupo pichani) wakati alipokutana na kikundi hicho kwa ajili ya kukagua maendelo ya shughuli za kikundi hicho mwishoni mwa wiki.
  Mmoja wa wanakikundi wa Kikundi cha Vijana cha Maamuzi, Bw. Juma Ismail Hassan (aliyevaa tshirt ya blue) akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kikundi hicho na Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bibi. Sihaba Nkinga (hayupo pichani) alipotembelea kikundi hicho mwishoni mwa wiki Kilwa Kivinje, Mkoni Lindi.Katibu Mkuu aliktembelea kikundi hicho ambacho kiko kwenye hatua za kupunguza matumizi ya dawa za kulevya ili kukihamasisha kuacha kabisa matumizi ya dawa hizo na badala yake wajikite katika shughuli za uzalishaji.
  Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bibi. Sihaba Nkinga (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Kikundi cha Maamuzi pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Kilwa. Wa tatu kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Bw. James Kajugusi, anayefuata ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Bw. Charles Mwaitege na wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilwa, Bw. Simon Manjurungu na wa kwanza kulia ni Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Lindi, Bibi Makalaghe Shekalaghe Nkinda.

  Na Concilia Niyibitanga
  Halmashauri zote nchini zinawajibika kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya vijana pamoja na kuwatengea vijana asilimia 5 ya mapato ya halmashauri husika kwa ajili ya kuwezesha shughuli hizo. Hayo yamesemwa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bibi Sihaba Nkinga wakati akikagua maendeleo ya vijana Wilayani Kilwa, mkoani Lindi.

  Amesema kuwa vijana ndiyo nguvu kazi ya taifa na kwa maana hiyo wanatakiwa waongozwe na wawezeshwe ili kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo kwa lengo la kujikwamua katika umaskini.

  Vijana wanatakiwa kuhamasishwa kuunda na kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali na kuunda SACCOS za vijana ili waweze kupatiwa mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa ajili ya kuongeza mitaji na kupanua uzalishaji. Amesema Bibi Nkinga. 

  Akiongea na Kikundi cha Vijana cha Maamuzi kilichopo Kilwa Kivinje ambacho kina wanachama 21 ambao hapo awali wamekuwa wakijihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya na sasa kuamua kupunguza matumizi ya madawa hayo, aliwataka kuendelea kupunguza na hatimaye kuacha kabisa kwani madawa hayo yanaathiri afya zao na kupunguza uwezo wa uzalishaji.

  Aidha, alikitaka kikundi hicho kuendelea kuwahamasisha vijana wenzao walioathirika na madawa hayo kujiunga katika kikundi hicho ikizingatiwa kuwa Wilaya ya Kilwa ina Vijana zaidi ya 100 walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevya.

  Aliwataka kuendelea kushiriki katika shughuli za kujitolea wanaozifanya sasa za usafi wa mazingira na wasikate tamaa wasonge mbele kwa kuwa familia zao na jamii nzima inawategemea wao kama nguvu kazi ya taifa.
  Wakati huo huo, akiongea na kikundi cha vijana cha Sayari chenye wanachama 22 kinachojihusisha na biashara ya uuzaji chakula cha mifugo aliwataka kuendelea kuwa wabunifu na kuanzisha miradi mingi zaidi ya kuwaingizia kipato na kutunisha mfuko wao.

  Pia aliwataka kuhakikisha kuwa wanasajili kikundi chao ili kiweze kutambulika kisheria na pia wajiunge katika SACCOS ya vijana ili iwe rahisi kupatiwa mikopo ya kuendeleza shughuli zao za uzalishaji mali.

  0 0

   .Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Abraham Nyanda akisoma hotuba yake wakati wa kufunga  Mafunzo Unganishi(Bridging Course)yatakayowawezesha kujiunga na mafunzo ya  Stashahada ya Uandisi,kushoto ni Mtaalam wa Umwagiliaji kutoka Japan,Nobuyoshi Fujiwara na Mkuu wa Chuo,Dk Richard Masika. 
   Baadhi ya wanafunzi waliomaliza Mafunzo Unganishi(Bridging Course) na Kozi Awali(Pre-Entry Course)wakiwa makini kusikiliza hotuba ya Mgeni rasmi,mafunzo  yatawawezesha  kujiunga na mafunzo ya  Stashahada(Diploma) ya Uandisi  katika Chuo cha Ufundi Arusha.
   Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Dk Richard Masika akimpongeza mmoja wa wanafunzi waliohitimu mafunzo hayo,Aneth Chotto wakati akijiandaa kupokea Cheti kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho,Abraham Nyanda.
    Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Abraham Nyanda akimkabidhi Cheti mmoja wa wanafunzi waliohitimu mafunzo hayo.
  Uongozi wa Chuo katika picha ya pamoja na wahitimu wa kike wanaotarajiwa kujiunga katika ngazi ya Stashahada ya Uandisi.

  0 0

  Balozi wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva,  Mhe.  Modest Mero (kanzu jeupe) akila futari pamoja na wageni wake mbalimbali wakiwepo watanzania waishio Geneva katika futari maalum aliyowaandalia nyumbani kwake jana. 
  wageni mbalimbali wakijipakulia futari hiyo katika makazi ya Balozi.

  0 0  0 0


  Anaitwa IBRAHIM SAID

  NI MKOMORO NA HAJUI KUONGEA KISWAHILI
  NI MWANAFUNZI ANASOMA ZOOM POLYTECHNIC COLLEGE, DAR.
  NI MWENYE UMRI WA MIAKA ISHIRINI. 

  NI KIJANA MWENYE  MATATIFO YA AFYA YA AKILI.

  KATOROKA NYUMBANI JUZI ALHAMIS MAJIRA YA ALFAJIRI

   Mara ya mwisho Alionekana Maeneo ya Magomeni  Mapipa,  Dar es salaam, akiwa Amevalia T.shirt Ya Bluu na jeans.

   Yeye ni Mwembamba, Mrefu kidogo na ni maji ya kunde.
   Atakaye Mwona Atoe Taarifa Kituo Cha Polisi Kilicho Karibu.

  0 0

  Ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa wasanii wa Tanzania kuwa atachangia kuinua kiwango cha ujuzi na weledi wao kwa kuwaandalia mafunzo yatayoendeshwa na magwiji wa sanaa kutoka Marekani sasa imetimia.

  Terrence
  Akizindua Kampeni ya Uzalendo kwa Vijana inayoendeshwa na Muungano wa Wasanii Tanzania kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma mwezi uliopita, Juni 14, 2014, Rais Kikwete aliahidi kuchangia kuinua kiwango cha usanii na weledi wa wasanii wa Tanzania kwa kusaidia kuandaa mafunzo yatakayoendeshwa na wasanii maarufu kutoka Marekani.

  Chaka Zulu
  Katika kutimiza ahadi hiyo ya Rais Kikwete, kundi la wasanii kutoka Marekani limewasili nchini usiku wa Alhamisi, Julai 10, 2014, kwa ajili ya kuendesha mafunzo hayo yanayofanyika keshokutwa, Jumatatu, Julai 14, 2014, kwenye Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) mjini Dar es Salaam. Kiasi cha wasanii 250 wamealikwa kushiriki semina hiyo inayoitwa Mafunzo ya Uendelezaji Usanii.

  Banner
  Wasanii ambao wako nchini kwa ajili ya kuendesha mafunzo hayo ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.

  Wengine ni Terrence J. (Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shughuli za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group.

  Mbali na kuendesha shughuli za mafunzo ya wasanii ambazo wamekuwa wakizifanya kwa makundi madogo madogo tokea walipowasili nchini, pia wanamuziki hao wa Marekani na kundi la wapiga picha watatembelea sehemu mbali mbali  nchini ambako watapiga picha na kuandaa vipindi vya kuitangaza Tanzania katika vyombo vya habari vya Marekani.


  Imetolewa na;

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.


  12 Julai,2014


  0 0

  WAKAZI WAISHIO PEMBEZONI MWA BARABARA KUU YA IGUNGA - NZEGA WAKIMSILIZA WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI KUHUSU OMBI LA KUWEKEWA MATUTA. HATA HIVYO WAZIRI WA UJENZI ALIWAJIBU KUWA SHERIA HAIRUHUSU KUWEKA MATUTA KWENYE BARABARA KUU ILA TANROADS ITAWEKA ALAMA ZA BARABARANI KATIKA ENEO HILO ILI WANANCHI HAO WASIPATE SHIDA YA KUVUKA BARABARA.
  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKIPANDA JUU YA DARAJA LA MBUTU ILI KUKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WAKE AMBAO UMEFIKIA ZAIDI YA ASILIMIA 98 ILI KUKAMILIKA.
  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI KATIKATI AKITEMBEA JUU YA DARAJA LA MBUTU AMBALO LINAKARIBIA KUKAMILIKA UJENZI WAKE. WA KWANZA KULIA NI KATIBU MKUU WA WIZARA YA UJENZI MHANDISI MUSSA IYOMBE .
  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKIPOKEA MAELEZO YA UJENZI WA DARAJA LA MBUTU.
  KAZI ZA UJENZI WA TUTA LA DARAJA LA MBUTU UKIENDELE KWA KASI.
  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI WAKWANZA KUSHOTO AKIELEKEA KUWAHUTUBIA WANANCHI WA MBUTU MARA BAADA YA UKAGUZI WA DARAJA HILO LA MBUTU.
  WAKAZI WA MBUTU NA IGUNGA WAKISHUKA KWENYE DARAJA LA MBUTU KWENDA KUMSIKILIZA WAZIRI WA UJENZI DKT.JOHN MAGUFULI KATIKA MKUTANO WA HADHARA.
  SEHEMU YA TUTA LA DARAJA LA MBUTU LINAVYOONEKANA KATIKA PICHA.

  0 0

  Na Hassan Hamad, OMKR  

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, leo ameendelea na ziara yake ya kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa na wafiwa katika Mkoa wa Kusini Unguja. 
  Ziara hii ni mfululizo wa ziara zake za kuwatembelea wagonjwa katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan, ambapo Alkhamis iliyopita alitembelea Mkoa wa Kaskazini Unguja. 
  Akiwafariji wagonjwa hao, Mhe. Maalim Seif amewaombea wapone haraka ili waweze kuendelea na majukumu yao ya kimaisha. Nao wagonjwa hao wamemshukuru Makamu wa Kwanza wa Rais kwa kuamua kuwatembelea na kuwafariji, na kwamba ziara yake inaweza kuwa chachu ya kupata nafuu. 
  Katika ziara hiyo Maalim Seif ametembelea wagonjwa katika vijiji mbali mbali vya Mkoa wa Kusini Unguja vikiwemo Kitogani, Kajengwa Makunduchi, Kibele na Umbuji. 
  Wakati huo huo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Al-hajj Maalim Seif Sharif Hamad, jana alijumuika na Masheikh mbali mbali wa Zanzibar katika futari iliyofanyika nyumbani kwake Mbweni.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika ziara ya kutembelea na kuwafariji wagonjwa katika vijiji vya Mkoa wa Kusini Unguja.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika futari ya pamoja na Masheikh mbali mbali wa Zanzibar nyumbani kwake Mbweni.

  0 0

   Rais Obama wa MArekani akipata pizza na wananchi wa Denver, akiwa katika ziara yake ya kutembelea wananchi wa kawaida mitaani na kuzungumza nao mamo ya maisha na changamoto wazipatazo. Wananchi hawa walimwandikia barua Rais Obama na kumtaka awatembelee 
   Rais Obama akiongea na mwanamama Kinsey Button katika Mgahawa wa Magnolia mjini Austin, Texas 
  Rais Obama akiongea na wananchi mitaani Denver.
  Picha kwa hisani ya Pete Souza wa White House

  0 0

   Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe Juma Nkamia  katika picha ya pamoja na kikosi cha JKT  Dodoma mara baada ya kukagua vikosi hivyo.Timu hizi ndizo zilizo funguwa mashindano haya ya Klabu Bingwa ya Netiboli katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe Juma Nkamia  katika picha ya pamoja na Kikosi cha Police Dodoma  baada ya kukagua vikosi hivyo.Timu hizi ndizo zilizo funguwa mashindano haya ya Klabu Bingwa ya Netiboli katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe Juma Nkamia akikagua Kikosi cha JKT 
   Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe Juma Nkamia akikagua  Kikosi cha Police Dodoma
   Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe Juma Nkamia akilenga kapu(kufunga goli) akiashiria ufunguzi rasmi wa kufunguwa mashindano ya Klabu Bingwa ya Netiboli katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe Juma Nkamia akiangalia mpira alioulenga wakati akifungua mashindano ya Klabu Bingwa ya Netiboli katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma

  Na Deusdedit Moshi wa Mtendaji Mkuu wa Photo Solutions wawakilishi mwa Michuzi Blog Kanda ya Kati.

  0 0

  Katika maisha ya kiujasiriamali ya sasa, hauwezi kuepuka matumizi ya Tekinolojia.Tekinolojia siyo tu inakuwezesha kufikia watu wengi zaidi, bali pia kuongeza ubora na ufanisi wa huduma zako kitu kitakachokufanya uwe wa kipekee.
  Wajasiriamali wengi wamekuwa na shauku na hamu kubwa ya kutumia tekinolojia ili kuongeza ufanisi wa huduma zao. Kwakuwa wengi wa wajasiriamali hawa hawana uelewa mkubwa wa mambo ya tekinolojia (na si kazi yao), hivyo hujitoa kafara kwa watu wa tekinolojia wakiamini wao ndiyo msaada wao mkubwa. Lakini si mara zote mambo yanaenda sawa.
  Tangu kuanzishwa kwa Dudumizi Technologies, tumekuwa tukipokea wateja wengi ambao wamekuwa wakilizwa au kukatishwa tamaa na hawa watu wa tekinolojia. Hivyo ili kuwasaidia wengine, katika makala hii, tutaangalia mambo muhimu ya kuzingatia pindi unapochagua mtoa huduma wa tekinolojia (IT). Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akijumuika na Viongozi mbali mbali na wananchi,katika futari iliyoandaliwa na Benki ya watu za Zanzibar PBZ katika Ukumbi wa Salama Bwawani
  Baadhi ya wananchi wa manispaa ya  Mji wa Zanzibar na wateja wa Benki ya watu wa Zanzibar PBZ,wakiwa katika futari iliyoandaliwa na Benki hiyo katika Ukumbi wa Salama Bwawani
  Picha na Ramadhan Othman Ikulu.

  0 0

  [20:21:38] Ngoma Africa: :jamaa wana roho mbaya sana hawa, asalamaleko wallahi....
  [20:22:57] Ngoma Africa: tena gitaa lenyewe bei mbaya harafu made in Gerezani (sido)  kariakoo,Uswahilini ndani huko....
  [20:24:55] Ngoma Africa: na mlinzi Sajenti kopro (Dog) Domobaya alikuwa kalala fofofoooo (worry) Wallahi  nitamfuta kazi akiendelea na tabia hizi. Juzi juzi tu walitaka kulamba bundi, yeye kalala fofofoooo....ebo! Jibwa gani hili?
  [20:26:24] Ngoma Africa: Gitaa lenyewe  limetengenezwa kwa chuma cha pua na nyuzi zake ni za nondozzzz. Uzito nusu tani. jamaa walitia timu na winchi, we acha tu! Kama nisingekuwa jirani ingekuwa kwishnei...

  0 0
 • 07/12/14--14:59: dubai


 • 0 0

   Msanii mkongwe kwenye game la Bongo Fleva anajulikana kwa jina la Prof Jay leo mchana alikuwa akishoot video yake mpya aliyomshirikisha Diamond inaitwa KIPI SIJASIKIA. Video hiyo iliyokuwa ikishutiwa pale Sinza Makaburini ilipo Mahakama. Video imesimamiwa wa Dir Adam Juma kutoka Next Level
   Diamond kama wakili wa Profesa J

older | 1 | .... | 502 | 503 | (Page 504) | 505 | 506 | .... | 3272 | newer