Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live

TEAM IDDI "TEAM TANZANIA" INAOMBA KURA ZENU: KUWAKUTANISHA WATANZANIA KAMA WANA DMV BILA KUJALI MENGINEYO

$
0
0
MHE IDDY SANDALY

Katika Historia ya DMV kwa Miaka miwili mfululizo ya Uongozi wangu  tumeweza kuwajumuisha watanzania kwenye mambo mbali mbali. Tumeweza kufanya SUMMER PICNIC kwa watanzania wote wa DMV . Tuliweza kujipanga na Kuhakikisha watoto, vijana na Wazee wanajumuishwa pamoja na kufurahia, Watanzania bila Kujali Vyama na mengineyo tuliweza kujumuika kwa pamoja na kufurahi.  Lengo DMV MOJA.

Kwa Kuendeleza kuonyesha ni jinsi Gani umoja Ndio Lengo la Jumuiya na Sio Kupata Mamilioni ya Fedha wala Kuleta Siasa au Mengineyo.Kwa Miaka yote miwili ya uongozi na Timu yangu tuliweza kuandaa Party Ya Mwaka Mpya Kwa Watanzania Wote Hapa DMV na Kwa Gharama Nafuu. Lengo ni Kushereheka kwa Pamoja na Kuwa Pamoja kama watanzania DMV. Tuliserebuka na Kulisaka Bomboka kwa Raha Zetu. Mpango Pale Pale Mwaka huu December 31, 2014.
DUAL CITIZENSHIP /HAKI YA KUZALIWA


Nimekuwa mstari wa mbele katika kulipigania swala la Dual Citizenship . Nilianzisha PETITION kwa watanzania wote ulimwenguni ili kuweza kupeleka mawazo na nguvu zetu Diaspora tulio nje Bungeni Tanzania. Petition hii nilianzisha na kuhakikisha inawafikia wabunge na Mawaziri nyumbani Tanzania ilikuweza kulisukuma swala hili la Haki ya Kuzaliwa/Dual Citizenship. Mpaka Hii leo petion hii ishatiwa sign na Watanzania 1,754, ulimwenguni. http://www.change.org/petitions/honourable-bernard-membe-we-tanzanians-in-the-diaspora-believe-that-dual-citizenship-is-a-great-thing-for-the-country-please-support

Nimeshirikiana na Viongozi wenzangu wa Jumuiya za watanzania hapa Marekani, ITALIA, IRELAND, UK, ZADIA na DIACOTA kwenye kuhakikisha swala Hili la Dual Citizenship linafanikiwa. Tumekuwa tukifanya mikutano ya Kila Jumapili kujadili na kupanga mikakati katika swala hili.  

Kwa Hivi Sasa Viongozi Wenzangu wa Jumuiya za Marekani Kwa Kazi nzuri ninayoifanya na kwa imani na uaminifu walionao juu yangu, wamenichaguwa Kuwa Mwenyekiti Wa Umoja  wa Viongozi wa Watanzania Marekani.
PESA zimekuwa zikikusanywa kutokana na MAOMBI ya muwakilishi wa wanadiaspora kwenye bunge la katiba Mr. Kadari Singo. Pesa hizi zina lengo moja tu la kuhakikisha swala hili linafanikiwa. Lengo kuu ni kuwapa semina wabunge kuhusu swala hili kama tulivyoshauriwa na Waziri wa mambo ya Nchi za Nje Bwana Bernad Membe, Mabalozi wetu na Baadhi ya Viongozi. Pia Baadhi ya Pesa zitatumika kwenye Publicity kwenye Radio, TV na nk.

Jumla ya $9,405 zimekusanywa mpaka sasa na lengo ni kukusanya $25,000 . Mimi Nilikuwa Mchangaji namba mbili (2) . Kama kuna swali wasiliana na muwakilishi wa wanadiaspora kwenye bunge la katiba Mr. Kadari Singo au kiongozi yeyote wa Jumuiya za Watanzania Marekani kwenye link hii  http://www.gofundme.com/7jtyuw.  Mr. Kadari Singo singojr@gmail.com

Matumizi yanayofanyika kwenye Pesa hizi ni LAZIMA yapitishwe na Viongozi wote wa Jumuiya hizi za watanzania. Unaweza kuwasiliana na kiongozi yeyote hapa http://www.gofundme.com/7jtyuw kwa maelezo , maoni au maswali. Pesa hizi ambazo bado ziko under gofund,com zitakuwa Transfered kwenye Jumuiya ya Hapa DMV, halafu maelekezo ya Matumizi yatafanywa na Viongozi wote. Matumizi ya $700 yalipitishwa na Viongozi wa Jumuiya za Watanzania Marekani yalifanyika, AMBAPO MIMI NIMETUMIA PESA ZANGU BINAFSI ($700) na kutumwa kwa Kaka Kadari Singo kwa Maandalizi ya awali ya swala hili la Dual Citizenship. Pesa zangu nitarudishiwa Mara tu hela zitakapokuwa Transfered kwenye account ya Jumuiya.
Kwa contacts za Viongozi wa Jumuiya za Watanzania Marekani nenda  http://www.gofundme.com/7jtyuw
Kwa mapicha kibao BOFYA HAPA


DKT.MAGUFULI AZOA WANACHAMA WAPYA 350 HUKO MARA, AFUNGUA KOMBE LA LUGOLA

$
0
0
Katika ziara yake Mkoani Mara Dkt.Magufuli alifanya ziara Kijiji cha Mwibara (M/Kiti - TLP), Kata ya Mwibara (Diwani-TLP) Jimbo la Mwibara (Mbunge - CCM). 
Akiwa katika kijiji cha Mwibara alifungua kombe la Kangi Lugola kisha kuhutubia wananchi. Kwa upendo M/Kiti na Diwani wa kata ya Mwibara wote kutoka TLP- walimzawadia Mbuzi wawili. Aidha, Magufuli aliweza kuzoa wanachama wapya zaidi ya 200 kata ya Mwibara na akafanya mkutano kata jirani ya Iramba na kuzoa wanachama wengine zaidi ya 150. 
 Dkt.Magufuli aliweza kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja kwenye mfuko wa maendeleo wa jimbo hilo. Jimboni kwa Nimrodi Mkono alizindua kivuko kipya cha MV Mara kitakachofanya safari zake kati ya Jimbo la Mwibara (Iramba) kwenda Jimbo la Musoma Vijijini (Majita). 
Kivuko hiki kimeigharimu serikali shilingi milioni 545.2. Awali wananchi walisafiri kilomita 240 lakini kwa kutumia kivuko hiki watatumia dakiki 30 tu, zaidi ya hapo nauli walikuwa wakilipa shilingi 2000/- kwa mtu mmoja lakini kwa kivuko hiki kipya nauli ni shilingi 500/- na wanafunzi bureee! 
 Dkt.Magufuli pia aliweza kukagua ujenzi wa barabar ya Bunda - Kisorya sehemu ya Kisorya - Bulamba inayojengwa kwa shilingi bilioni 51.1/-. 
 Waliohudhulia: Kangi Lugola (MB), Nimrodi Mkono(MB),Mhandisi Iyombe (Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi), Mhandisi Evarist Ndikilo (RC-Mwanza & Ag.Mara), Ester Bulaya (MB-Viti Maalum), Wenyeviti wote wa Bodi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Kamati ya Ulinzi ya Mkoa n.k
 Dkt.Magufuli akifungua michuano ya  kombe la Lugola kwa kupiga penati golikipa akiwa Kangi Lugola, wanaoshuhudia ni Mhandisi Iyombe (Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi),Mhandisi Evarist Ndikilo (RC-Mwanza & Ag.Mara). Matoke, Magufuli alifunga goli.
Golikipa Kangi Lugola baada ya kupangua penati ya Magufuli...Hadi refa alishangilia!
Dkt.Magufuli akizawadiwa Mbuzi wawili 
Wananchi wakinyoosha mikono kuapa kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Mwibara 
Dkt.Magufuli, Mhe Kangi Lugola na Mhe Nimrodi Mkono wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa MV.Mara

MFUMUKO WA BEI NCHINI UMEPUNGUA - OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU.

$
0
0
Na Aron Msigwa – MAELEZO.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeeleza kuwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Juni 2014 umepungua ikilinganishwa na mwezi uliopita kutokana na kupungua kwa bei ya bidhaa na huduma za jamii katika maeneo mbalimbali. 
 Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na sensa ya Watu na Makazi Bw. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Juni, 2014 umepungua na kufikia asilimia 6.4 kutoka asilimia 6.5. 
 Amesema kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma mbalimbali kwa mwezi Juni 2014 imepungua ikilinganishwa na ile iliyokuwepo mwezi Mei kutokana na hali ya kupungua kwa bei kwenye bidhaa na huduma 
 Ameeleza kuwa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na migahawa kwa mwezi Juni umeongezeka hadi asilimia 8.5 kutoka asilimia 7.9 za mwezi Machi mwaka huu na kuongeza kuwa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi imeongezeka hadi asilimia 7.8 kutoka asilimia 7.2 za mwezi uliopita huku badiliko la fahirisi za bidhaa zisizo za vyakula likipungua hadi asilimia 4.9 kwa mwezi Aprili 2014 kutoka asilimia 7.2 iliyokuwepo mwezi uliopita. 
 Kwa upande wa mfumuko wa bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi Bw. Kwesigabo amesema kuwa umepungua kwa asilimia 0.6 ikilinganishwa na kupungua kwa asilimia 0.4 kama ilivyokuwa kwa mwezi Mei mwaka huu, huku fahirisi za bei za taifa zikiongezeka hadi kufikia 148.98 kwa mwezi Juni 2014 kutoka 140.00 za mwezi Juni 2013. 
 Amezitaja bidhaa zilizochangia ongezeko la fahirisi za bei nchini kuwa ni pamoja na mchele, mahindi,unga wa Muhogo, Viazi vitamu, dagaa, matunda jamii ya machungwa,mbogamboga na vitunguu maji. Kuhusu mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula zinazotumika nyumbani na migahawani amefafanua kuwa kwa mwezi Juni umepungua hadi kufikia asilimia 8.7 kutoka asilimia 9.3 
 Aidha, amesema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za jamii kutoka mwezi Septemba 2010 hadi Juni 2014 umeongezeka hadi shilingi 67 na senti 12 kutoka shilingi 66 na senti 72 za mwezi Mei mwaka huu.
 “Kupungua kwa bei ya bidhaa kwa mwezi Juni kunamaanisha kwamba, uwezo wa fedha yetu umeongezeka,hii inamaanisha mfumuko wa bei unaposhuka, thamani ya shilingi nayo inapanda” Amesema. 
 Kuhusu ulinganifu mfumuko wa bei wa Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki amesema kuwa una mwelekeo unaofanana na kueleza kuwa mfumuko wa bei nchini Kenya umeongezeka na kufikia asilimia 7.39 kwa mwezi Juni 2014 ikilinganishwa na asilimia 7.30 za mwezi Mei , huku Uganda ikiwa na mfumuko wa asilimia 4.9 kwa mwezi huu ikilinganishwa na 5.4 za mwezi uliopita.
Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na sensa ya Watu na Makazi Bw. Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu kupungua kwa  mfumuko wa bei nchini.

suitably qualified consultant sought!

$
0
0
Restless Development is the leading youth-led development agency, operating in Tanzania since 1993. Our mission is to demonstrate that young people can and are placed at forefront of change and development.  Our vision is to see young people taking up leadership roles which contribute to urgent development needs in support of the Government of Tanzania efforts as set out in the National Strategy for Growth and Reduction of Poverty (NSGRP/MKUKUTA II.
We provide training, mentoring, peer education and opportunities to in and out of school youth, youth networks, and youth-led organizations to lead development from community to national level using innovative youth-to-youth strategies. We are recognized as an expert, and also support governments, bi-lateral organizations, and the private sector to engage with young people to ensure their strategies are inclusive.
Restless Development has been implementing Sexual and Reproductive Health and Rights, and Life Skills education to young people in and out of school since 2007.  
Within this period, the agency has built up a wide range of SRHR and Life Skills materials which would now benefit from being upgraded and integrated into consolidated toolkits for facilitators who are our staff and young volunteer peer educators in schools and communities.
We are seeking a suitably qualified consultant to review, refine, and consolidate our SRHR materials while integrating Life Skills to be in line with the new East and Southern Africa (ESA) Commitment to comprehensive sexuality education as signed by the Government of Tanzania in 2014. 

If you have what it takes please visit  http://restlessdevelopment.org/work-with-us for application package!

The deadline for this post is on 15th July, 2014!

Thank you

Oscar Kimaro | Restless Development Tanzania
Marketing &Communications Assistant Programme Coordinator

TBL YATOA MSAADA WA SH. MIL. 25 ZA KUCHIMBA KISIMA CHA MAJI ZAHANATI YA MAKUBURI, DAR

$
0
0
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni,Joseph Nicholous 9kushoto) akimkabidhi Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni,  ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Dk. Gunini Kamba mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 25 ikiwa ni msaada uliotolewa na TBL kwa ajili ya ujenzi wa kisima cha maji katika Zahanati ya Makuburi, Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika zahanati hiyo. Kulia ni Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Stella Kivugo na katikati ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwongozo katika kata hiyo ya Makuburi.James Ngoitanile.
 Jengo la zahanati ya Makuburi
 Viongozi wa Manispaa ya Kinondoni,viongozi na wahudumu wa zahanati hiyo pamoja na Wajumbe wa kamati ya maji ya mtaa huo Mwongozo wakifurahia kupata msaada huo kutoka TBL.

Wabongo wamtaka Rose Muhando amlete Rebecca Malope

$
0
0
MWIMBAJI mahiri nchini, Rose Muhando amesema mashabiki wengi nchini wameomba malkia wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Rebecca Malope, awepo kwenye uzinduzi wa albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu Agosti 3, mwaka huu.

Uzinduzi huo utafanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam na tayari wasanii mbalimbali nchini wameshaalikwa kushiriki.

“Nimekuwa nikipokea simu nyingi za mashabiki wangu wakitaka nimualike Rebecca, najua kuna gharama zake kubwa, hivyo kwa kushirikiana na wasaidizi wangu tunalifanyia kazi.“Napenda mashabiki wangu wafurahi, lakini pia itategemea ratiba yake naye inasemaje, hivyo kazi kubwa itafanyika,” alisema Rose.

Rebecca amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006).

Nyimbo zilizopo katika albamu hiyo mpya ya Muhando ni Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook. Hivi sasa Muhando anatamba na albamu yake ya Utamu wa Yesu yenye nyimbo saba, ambazo ni Utamu wa Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia.


Mbali na Utamu wa Yesu, Rose Muhando pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu Anacheka, Wololo.Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya.

RAIS WA ZANZIBAR DKT ALI MOHAMED SHEIN ATEMBELEA PEMBA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dk.Juma Malik Akili,wakati alipotembelea maendeleo ya Ujenzi wa barabara tatu za Mkoa wa Kaskazini Pemba,ikiwemo Konde,-Wete,Wete Gando na Gando –Ukunjwi,katika ziara ya Mkoa huo
 Mkurugenzi  Mtendaji  wa Kampuni ya Mecco Tanzania Abdulkadir Sheikh Bujet akitoa maelezo kwa Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipotembelea maendeleo ya Ujenzi wa Bara bara tatu za Mkoa wa Kaskazini Pemba,ikiwemo Konde,-Wete,Wete Gando na Gando –Ukunjwi,katika ziara ya Mkoa huo
 Mkandarasi msimamizi wa Kampuni ya J.Burrow ya Dar es salaam Mohamed Hussein akitoa maelezo kuhusu utengenezaji wa barabara wakati Rais  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati alipotembelea maendeleo ya Ujenzi wa Bara bara tatu za Mkoa wa Kaskazini Pemba,ikiwemo Konde,-Wete,Wete Gando na Gando –Ukunjwi,katika ziara ya Mkoa huo
 Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa maagizo kwa watendaji kampuni ya Ujenzi wa barabara tatu za Mkoa wa Kaskazini Pemba,ikiwemo Konde-Wete-Wete Gando na Gando –Ukunjwi,alipotembelea kuona maendeleo ya kazi zinazofanyika katika ziara ya Mkoa huo
 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Raha Shehia ya Ukunjwi,Jimbo la Gando Mkoa wa Kaskazini Pemba wakijiorodhesha wakati walipotakiwa Wananchi walioathirika na Nyumba zao kutokana na Ujenzi wa Barabara tatu za Mkoa wa Kaskazini Pemba,ikiwemo Konde-Wete-Wete Gando na Gando –Ukunjwi,wakati Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipofanya ziara leo katika Mkoa huo
 Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi wa kijiji cha Raha Shehia ya Ukunjwi,Jimbo la Gando Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati alipofanya ziara leo katika Mkoa huo ya kutembelea  maendeleo ya Ujenzi wa Bara bara tatu za Mkoa wa Kaskazini Pemba,ikiwemo Konde,-Wete,Wete Gando na Gando –Ukunjwi
Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa  maelekezo kwa Afisa Mdhamini wa Wizara Mindombinu na Mawasiliano Pemba   Hamadi Ahmed Baucha kuhusu malipo ya fidia ya Nyumba ya Mzee Mohamed Waziri Mbwa Mkaazi wa Kijiji cha Raka (katikati) wakati alipotembela ujenzi wa barabara tatu za Konde,-Wete,Wete Gando na Gando –Ukunjwi, Mkoa waKaskazini Pemba. 
Picha na Ramadhan Othman wa Ikulu.

NA MPIRA UMEISHAAAAAA.....Brazil mbendembende....UJERUMANI YAWAPIGA 7-1 kama wamesimama vile!

$
0
0

Ujerumani goli 7 na Brazil  bao 1.... wanalia. Mara ya mwisho Brazil kupigwa mabao kibao namna hiyo ilikuwa mwaka 1920 walipopigwa 6-0 Uruguay...
Taswira mbali mbali za ufungaji wa magoli saba ya Ujerumani dhidi ya Brazil.
 Mkongwe Miroslav Klose akishangilia bao lake.


TAARIFA MUHIMU/IMPORTANT WEATHER NOTICE

$
0
0
Tafadhali pokea tahadhari ya Upepo mkali pamoja na mawimbi makubwa katika maeneo yote ya ukanda wa pwani kuanzia tarehe 09 mpaka 12 July 2014. 
-------------------------------
Please receive the warning of strong winds and large waves along the entire coast from 09 to 12 July 2014. 
-------------------------------------------------
Imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania 
Issued by Tanzania Meteorological Agency.

NAJUA WAJUA YA CAPTAIN GARDINER G. HABASH NDANI YA MICHUZI TV LEO

WAZIRI MEMBE AFUNGUA RASMI MAFUNZO YA TAASISI YA UONGOZI YA AFRIKA MASHARIKI KWA MWAKA 2014

$
0
0
Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Taasisi ya Uongozi ya Afrika Mashariki, Prof. Rwekaza Mukandala akimkaribisha Waziri Membe kufungua rasmi mafunzo hayo. Wengine katika picha ni Dkt. Benson Bana (wa kwanza kulia), Mhadhiri na Mratibu wa Mafunzo hayo kwa mwaka 2014 na Prof. Betram Mapunda (wa kwanza kushoto).
 Waziri Membe akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
 Sehemu  ya Wanafunzi wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipowahutubia. 
Sehemu nyingine ya Wanafunzi wakimsikiliza Mhe. Membe alipowahutubia.
Taarifa zaidi BOFYA HAPA 

Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuanza septemba 20, 2014

$
0
0
Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa 2014/2015 itaanza kutimua vumbi Septemba 20 mwaka huu.

Awali michuano hiyo ilikuwa ianze Agosti 24 mwaka huu, lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limelazimika kuisogeza mbele kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kupitisha michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).

Michuano ya Kombe la Kagame inayoshirikisha mabingwa wa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) itafanyika Agosti mwaka huu nchini Rwanda.

Timu 14 zitashiriki Ligi Kuu msimu huu. Timu hizo ni mabingwa watetezi Azam, Coastal Union, JKT Ruvu Stars, Kagera Sugar, Mbeya City, Mgambo Shooting, Mtibwa Sugar, Ndanda FC, Polisi Morogoro, Ruvu Shooting, Simba, Stand United, Tanzania Prisons na Yanga.

Ratiba ya ligi hiyo itatolewa mwezi mmoja kabla ya michuano hiyo kuanza kutimua vumbi.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


WAZIRI MKUU APIGA STOP MATUMIZI YA KUNI KIWANDA CHA 21st CENTURY

$
0
0

PG4A8989
……………………………………………………………………………..
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ametoa mwezi mmoja kwa Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) iwe imetoa mapendekezo kwa Serikali kuhusu matumizi ya maji machafu yanayotokea kwenye viwanda vinne vya ngozi, magunia, nguo na maturubali (canvas).
 
Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumamosi, Desemba 7, 2013) mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kwenye kiwanda cha nguo cha 21st Century kilichopo eneo la Kihonda Viwandani nje kidogo ya mji wa Morogoro.
 
Akizungumza na uongozi wa mkoa, wilaya, kiwanda hicho pamoja na NEMC  ya mara baada ya kutembelea eneo ambalo limeathirika na maji yanayotiririka kutoka kwenye viwanda hivyo, Waziri Mkuu alisema tatizo lililopo linachangiwa na kutokuwepo kwa mtu au taasisi maalum ya kusimamia mabwawa ya mfumo wa majitaka (waste management ponds).
 
“Viwanda hivi vilibinafsishwa lakini mfumo wa usafishaji majitaka haukubinafsishwa… NEMC iishauri Serikali nini kinapaswa kifanyike. Ifanye utafiti kuhusu matumizi ya majitaka yanayotoka kwenye viwanda hivi na ilete uchambuzi huo Serikalini,” alisema.
 
Waziri Mkuu ambaye alitembelea eneo la Kihonda Mbuyuni katika kata ya Mafisi ambako maji hayo yanaingia korongoni na kuelekea mto Ngerengere, alishuhudia mifereja ya maji machafu yenye harufu kali na rangi mchanganyiko ya kijani na bluu ikitiririka katikati ya nyumba za watu.
“Hatuwezi kuendelea na hali hii ya kutiririsha maji kwenye makazi ya watu, ni bomu litakalolipuka hivi karibuni. Kuna watoto wanacheza katika maeneo yale wanaweza kunywa au kunawa yale maji, kuna mifugo inapita, inaweza kunywa yale maji, ni hatari kwa kila mmoja wetu,” alisisitiza.
 
Aliitaka NEMC iangalie uwezekano wa kumpatia mtu binafsi aendeshe mfumo huo hata kama itabidi asimamiwe na Halmashauri lakini kinachotakiwa ni kupatikana kwa mtu mwenye uwezo wa kuendesha mfumo huo kwa utaalamu. 
 
Aliipa NEMC miezi miwili ili iwe imekamilisha utafiti wake pamoja na kuangalia uwezekano wa kumpata mtaalamu wa kuifanya kazi hiyo.
Alitoa pia mwezi mmoja kwa Manispaa ya Morogoro kuwa imetafuta eneo jipya na kubwa zaidi kwa ajili ya kumwaga takataka kwani dampo lililopo katika kata hiyo linachangia uchafuzi wa mazingira na kuleta kero kwa wananchi.
 
“Wakati ule dampo linaletwa huku ilikuwa ni sahihi kwa sababu huku kulikuwa ni nje ya mji lakini kwa sasa siyo sahihi. Nimemwambia Meya akae na watu wake wafikirie kujenga dampo jingine la kisasa… watafute eneo kubwa na kuwe na mifumo ya kisasa,” alisema.
 
Kuhusu matumizi ya kuni katika kiwanda hicho, Waziri Mkuu alisema hakubaliani kabisa na matumizi ya kuni kwa sababu yanachangia uharibifu mkubwa wa mazingira. Aliutaka uongozi wa kiwanda hicho, uendelee na mpango wake mpya wa kutumia makaa ya mawe au hata kuangalia mpango wa kutumia umeme utakaotokana na gesi.
 
“Najua kuna gharama katika kubadilisha mfumo wa boilers zenu lakini matumizi ya tani 50 za magogo kwa siku hapana! Tani 50 nazilinganisha na magunia 500 ya mahindi, sasa kwa miezi sita au kwa mwaka mmoja, mtatumia kuni kiasi gani? Si Morogoro nzima itateketea? Alihoji Waziri Mkuu.
Akijitetea kuhusu suala hilo, mmiliki wa kiwanda hicho, Bw. Gulam Dewji alisema moto unaotokana na makaa ya mawe hauna nguvu ya kutosha kuzalisha mvuke wa kuzalisha umeme wa kuendeshea mitambo ya kiwanda hicho. “Tumeomba kwa mwaka mmoja tu tupewe ruhusa ya kuchanganya makaa ya mawe na vipande vya miti hadi tutakapopata boilers mpya,” alisema.
 
Waziri Mkuu alimweleza Bw. Dewji asubiri majibu ya maombi yake kutoka NEMC ambako maombi hayo yalipelekwa lakini pia akawaonya viongozi wa NEMC kuwa makini wakati wanapitia maombi hayo ili waweze kuwa na mbinu za kubainisha kama kweli vitatumika vipande vya miti au watarudia utaratibu wao wa zamani wa kutumia magogo lakini wanayakata katika vipande vidogo vidogo.
 
Hata hivyo, katika kikao hicho Meya wa Manispaa ya Morogoro, Bw. Amiri Nondo na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bw. Said Amanzi walielezea kutoridhishwa kwao na uhusiano uliopo baina ya uongozi wa kiwanda hicho na mamlaka zilizopo wakidai kufungiwa mageti na kutotekelezwa kwa maelekezo yanayotolewa na mamlaka husika.
 
Waziri Mkuu alimtaka mmiliki wa kiwanda hicho, Bw. Gulam Dewji ajenge mahusiano mazuri na uongozi wa mkoa kwa sababu viwanda vyake viko katika mkoa huo na hivyo hana budi kuzingatia maslahi ya wakazi wa Morogoro kwanza. “Wao ni viongozi wa mkoa lakini pia ni wawakilishi wa wananchi, kwa hiyo wanawajibika kwa wananchi, linapotokea jambo wao ndiyo wataulizwa na wananchi,” alisisitiza.

CULTURAL WARS SASA IMEKAMILIKA NA SASA UNAWEZA KUPATA COPY YAKO, PITIA HII TRAILER.

$
0
0
Filamu Mpya ya Cultural Wars Sasa Yapatikana! Wahi Kujipatia DVD! 


Ile filamu mliyokuwa mnaisubiri kwa hamu iitwayo “Cultural Wars” iliyoandikwa na kutengenezwa na Deogratius Mhella (Mtanzania anayeishi New York) akishirikiriana na Watanzania na Wamarekani waishio New York, New Jersey Boston na Connecticut sasa imetoka kwa mara ya kwanza na inapatikana kwenye DVD na unaweza kupata “electronic Copy” 
Filamu hii inazungumzia baadhi ya changamoto za kimapenzi wazipatazo vijana wa Kitanzania hapa Marekani. Na ni ya kwanza iliyochezwa na Watanzania na Wamarekani hapa New York kwa kutumia lugha ya Kiingereza. Baadhi ya “Actors” wa Kitanzania ni Khalifa Siwa aka “Bob”,  Ny Ebra aka “Vijimambo New York”, Akida aka “Mshenga”, Chemi Whitlow aka “Chemponda” na Isaac Kibodya aka “Father”. Wote mliosaidia katika kufanikisha filamu hii ambao hamjatajwa hapo juu, mnapewa shukrani za dhati kabisa. 




Usikose kujipatia nakala yako kwa kuinunua hapa chini: 

KAMPUNI YA MEGATRADE YATOA MSAADA YA VYAKULA MASHULENI

$
0
0

CMeneja Masoko wa kampuni ya Megatrade Ivestment Goodluck Kway kulia, akimkabidhi msaada wa vyakula  diwani wa kata ya sokoni one Michael Kivuyo kwaajili ya shule za msingi katika kata hiyo ambazo ni shule ambazo  zinaukosefu mkubwa wa chakula cha wanafunzi hali inayopeleka masomo kudorora na wanafunzi kuzimia ovyo kwa ajilii ya njaa mashuleni hali hiyo ilipelekea kampuni hiyo kujitolea msaada uliogharimu kiasi cha shilingi Milioni moja,msaada huo ni Magunia ya mahindi,maharagwe na mafuta ya kula, jana jijini Arusha
DMeneja Masoko wa kampuni ya Megatrade Ivestment Goodluck Kway kulia akimkabidhi gunia la maharagwe diwani wa kata ya sokoni one Michael Kivuyo jana jijini Arusha kwaajili ya shule za msingi katika kata hiyo,shule zilizonufaika na msaada huo ni shule ya Sokoni 1,Sinoni,Ukombozi,Engosengiu na Sinoni
BDiwani wa kata ya sokoni one Michael Kivuyo akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ukombozi Bi.Fatuma Mashombo gunia la mahindi kwaajili ya wanafunzi wa shule yake. (Pamela Mollel jamiiblog).

Daraja la waendao kwa miguu kimara lavutia

$
0
0
Magari yakipita chini ya daraja la watembea kwa miguu eneo la Kimara, Dar es Salaam, lililojengwa na Kampuni ya Ujenzi ya Strabag eneo la Kimara katika mradi wa ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo Kasi Dar es Salaam. (PICHA NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA)

Mfalme wa reggae Ras Jhikoman kutoka Bagamoyo,Tanzania atua mjini Tubingen,Ujerumani

$
0
0
 Mwanamuziki nyota wa reggae barani Afrika Jhiko Manyika aka Jhikoman kutoka Bagamoyo,Tanzania amewasili mjini Tubingen,Ujerumani kwa ajili ya kushiriki katika maonyesho makubwa ya 5th International African Festival Tübingen 2014, yatakayoanza 17 julai 2014 mpaka 20 Julai 2014 katika viwanja ya Festplatz, mjini Tübingen. 
Watayarishaji wa maonyesho hayo Afrikaktiv.org wamemtaja mwanamuziki Jhikoman kuwa ni nyota inayong'aa kutoka Afrika na wamemwalika kwa ajii ya kuja kuzidisha mwangaza katika soko la ulaya. 
Mkurugenzi wa maonyesho hayo Madam Susan Tatah alisema kuwa ujio wa mwanamuziki Jhikoman nchini Ujerumani unazidisha uhusiano mzuri katika sekta ya sanaa na utamaduni kati ya Ujerumani na Tanzania pia Afrika kwa ujumla.
Madam Susan Tatah alisema ujio wa Jhikoman una maana kubwa kwa wajerumani kwa mwanamuziki huyo anatoka katika mji wa Bagamoyo ambako ndipo palikuwa makao makuu ya serikali ya ukoloni ya kijerumani na ndipo Wajerumani walipojenga shule ya mwanzo Afrika Mashariki, Madam Susan Tatah alisema Jhikoman pia atatia sahini
mkataba wa ushirikiano wa kudumu wa "Cultural Exchange program" pamoja Afrikaktive pia na mji wa Tübingen.

MBUNGE MAGIGE AHIDI KUWAINUA AKINAMAMA KIUCHUMI KUPITIA CATHERINE FOUNDATION

$
0
0
 
MA7Mbunge wa viti maalum(uvccm)na mwenyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ya mjini Arusha aliyevalia ushungi mweupe katikati Catherine Magige,akiwa na kikundi cha  akinamamalishe baada ya kuwawezesha vifaa vya upishi kwaajili ya kuendeleza biashara yao ya chakula katika eneo la kilombero jijini Arusha leo ambapo aliwawezesha wanawake wajasiliamili 150 wa jijini Arusha wanaojishughulisha na uuzaji wa mbogamboga,mama ntilie,machinga.
1.Wakina mama wakiwa wanamsikiliza Mbunge wa viti maalum(uvccm)na mwenyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ya mjini Arusha Mhe.Catherine Magige

2Mbunge wa viti maalum(uvccm)na mwenyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ya mjini Arusha Mhe.Catherine Magige akiwakabidhi kikundi cha akinamama kiasi cha shilingi laki mbili kwa kila kikundi ambapo alichangia jumla ya shilingi Milioni Moja na nusu kwa vikundi hivyo vya akina mama kwaajili ya kuwaezesha kuendeleza vikundi vyao vya vikoba.

Introducing new single "Kila Siku" by Vellice

DKT SHEIN ATEMBELEA MASHAMBA NA KUZINDUA MSIMU MPYA WA KARAFUU PEMBA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizindua ununuzi wa karafuu kwa msimu wa mwaka 2014-2015 katika kituo cha ZSTC Mkoani Pemba,(kushoto) Waziri wa Biashara,Viwanda  na Masoko Nassor Ahmed Mazrui ,zoezi hilo lilifanyika leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiangalia zao la karafuu alipotembelea katika shamba la Bw.Said Sinani  (hayupo pichani) Shumbageni Kusini Pemba akiwa katika ziara maalum.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Bw.Said Sinani (kulia) baada ya kulitembelea shamaba lake la mikarafuu leo akiwa katika ziara Mkoa wa Kusini Pemba. Picha na Ramadhan Othman.
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live




Latest Images