Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

RAIS KIKWETE ALIPOKABIDHIWA KITAMBULISHO NAMBA 1 CHA USHIRIKI KATIKA MAONESHO YA 38 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA SABASABA (DITF) KUTOKA MAXMALIPO .

$
0
0
Rais  Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akabidhiwa kitambulisho Maalumu cha kielektoniki kwaajili ya Kuingia katika Maonesho ya 38 ya biashara ya Kimataifa ya Sabasaba kutika Kwa bwana Ahmed Lussasi Mkurugenzi uendeshaji wa kampuni ya Maxmalipo

Rais. Jakaya Mrisho alipata Nafasi ya kuzungumza na Maafisa wa Maxmalipo Juu ya Mfumo wa Kieletroniki wa Ticket (e-Ticketing System) uliofungwa na Maxmalipo Katika viwanja Vya Sabasaba. Pia Mheshimiwa Rais alijionea Jinsi Mfumo huu unavyodhibiti na kuboresha Ukusanyaji wa Mapato katika msimu huu wa Maonesho ya sabsaba. Mfumo huu wa kisasa pia Unauwezo wa kusimamia mapato katika nyanja mbalimbali kwa kutumia Barcode technology pia na Facial detection.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Maxmalipo Bw. Ahmed Lusasi akifafanua Jambo kwa Mh. Dr. Jakaya Mrisho wakati alipo Tembelea Banda la Maxmalipo ndani ya Viwanja vya sabasaba.
 Mh.Dr. Jakaya Mrisho Kikwete (Rais) Akitizama kwa Umakini na kupata maelekezo Juu ya mfumo wa kielektoniki wa Ticket unavyotumika sabasaba na unavyowezakutumika sehemu Mbalimbali.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UKWEPAJI KODI SH 662,500 - MHE AMOS MAKALLA (MB)

$
0
0
Nimesoma habari gazeti la UHURU la leo tarehe 9 Julai,2014 lenye kichwa cha habari TRA YAZUIA GARI LA NAIBU WAZIRI.Adaiwa kukwepa kulipa kodi kwa miaka miwili kodi ya leseni ya barabara.
Nachukua fursa hii kukanusha habari hizo kuwa ni za uongo zenye hila na mwelekeo wa kisiasa kwa aliyeandika kwa makusudi kwa lengo la kunichafua na kunishushia heshima yangu.Habari iliyoandikwa imejaa uzushi,hila na upungufu mkubwa wa kimaadili ya kiuandishi wa habari.
NAOMBA uuma wa watanzania kujua yafuatayo:

1.MIMI AMOS GABRIEL MAKALLA si mmiliki wa gari tajwa noT534BFP
2.Kodi inayodaiwa sh 662,500(laki sita sitini na mbili elfu mia tano tu) kwa mujibu wa taarifa za mwenye gari mpaka habari hii inaandikwa zilikwisha kulipwa.
HIVYO BASI,kutokana na ukweli huo habari hii ililenga kunichafua kwa makusudi na ina chembechembe za kisiasa na hila dhidi yangu na  kwa uzito huo
1.Nimemwagiza mwanasheria wangu AMICUS Advocates kuwaandikia gazeti la UHURU,MHARIRI na MWANDISHI WA HABARI HII kuniomba radhi  NDANI YA siku SABA kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti  kwa matoleo MATATU MFULULIZO 
2.Kinyume na hilo nawashitaki gazeti,mchapishaji,mhariri na mwandishi na kunipa fidia Tshs 1,000,000,000(Tshs Bilioni moja tu)
NARUDIA kusisitiza kuwa uandishi wa aina hii si tu unatia mashaka taaluma ya mwandishi aliyeandika bali pia ametumia kalamu yake kufanya siasa za maji taka na ili ukweli ujulikane nawakaribisha mahakamani ...
asanteni
AMOS G MAKALLA
Mbunge mvomero na naibu waziri maji

DKT.MAGUFULI AENDELEA NA ZIARA MWANZA NA SINGIDA AZINDUA KIVUKO CHA MV.TEMESA NA KUKAGUA DARAJA LA MBUTU

$
0
0
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea na ziara ya kikazi Jijini Mwanza ambapo leo amezindua kivuko cha MV.TEMESA kitakachofanya safari zake kutokea Luchele kupitia mwambao wa ziwa Victoria. 
Kivuko hiki kimetengenezwa/kimejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 640 na ni kivuko pekee chenye mwedo kasi kuliko vyote Tanzania, kina uwezo wa kubeba tani 65. 
Wengine walioshiriki katika uzinduzi huo ni Mhandisi Mussa Iyombe (Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi), Mhandisi Evarist Ndikilo (Mkuu wa Mkoa wa Mwanza), Mkuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Bodi zilizo chinin ya Wizara ya Ujenzi, Wakurugenzi wa Wizara ya Ujenzi, Wafanyakazi wa TEMESA, wafanyakazi wa SUMATRA pamoja na wananchi. Aidha, Dkt.Magufuli amesafiri mpaka Singida na kuelekea kwenye ujenzi daraja la Mbutu linalojengwa na Wakandarasi Wazalendo - Mbutu JV kwa gharama ya shilingi bilioni 12. 
Kwa ujumla kazi za ujenzi wa daraja zimefikia asilimia 95 ambapo deki la daraja limekamilika. Ukubwa wa daraja hilo umechukua takribani urefu wa kilomita tatu. Katika ukaguzi huo, Waziri wa Ujenzi aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Wilaya, Katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Wenyeviti wa Bodi na Wananachi.
Dkt.Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kivuko,wengine ni Mhandisi Everist Ndikilo (Mkuu wa Mkoa wa Mwanz, Mkuu wa Wilaya, Mhandisi Mussa Iyombe (Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi), Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Wakurugenzi wa Wizara ya Ujenzi, Wenyeviti wa Bodi mbalimbali na wananchi.
Dkt.Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mkuu wa Wilaya wakitoka ndani ya kivuko.
Dk.Magufuli, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Wilaya wakipozi ndani ya kivuko cha Mv.TEMESA kwa pamoja na wafanyakazi wa SUMATRA na TEMESA.
Dkt.Magufuli akifanya ukaguzi daraja la Mbutu

MGOMBEA URAIS WA MSUMBIJI ATUA TANZANIA KUSAKA KURA, AKUTANA NA MAMA MARIA NYERERE KUOMBA BARAKA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimlaki mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Chama cha Ukombozi cha FRELIMO, Mhe Filipe Nyusi alipowasili leo jioni Julai 9, 2014, kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya ziara ya siku tatu, kusaka kura kwa wananchi wa Msumbiji wanaoishi Tanzania, kufuatia kampeni za Urais zinazoendelea nchini kwake.
Mgombea huyo wa Urais Filipe Nyusi akimsalimia Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia alifika Uwanja wa Ndege pamoja na Kinana. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.
 Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Frelimo Filipe Nyusi akisalimiana na wana-CCM waliofika kumlaki Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere. Kulia ni Mwenyeji wake, Abdulrahman Kinana.

INTRODUCING VICKY KAMATA'S NEW VIDEO "MOYO WA MTU KICHAKA"

introducing "Mrembo wa Kiafrika", Bongo Flava Trak Mpya toka Kwa 3G

$
0
0

Vijana wa Kitanzania watatu wajulikanao kama 3G, wako mbioni kuachia singo yao ya kwanza, "Mrembo wa Kiafrika". Vijana hawa, ambao wali-rekodi singo hiyo mwaka jana ni G Fullah, Frankie G na Oz Bitala. 

Hivi sasa wimbo huo, ambao pamoja na harmony na kuchana, una mandahari ya zilipendwa kama za Miriam Makeba na Abeti Masikini. Wimbo una ladha tofauti kidogo, na ni mziki ulioyotulia ukiambatana na acoustic guitar pekee.


Tafadhali sikiliza track hii, alafu tungependa kujua maoni yenu: je, mnaionaje kwa soko letu hili la kibongo? Ahsanteni! Download free MP3 hapa! 
Joett Music - 3G Management 

JK KATIKA ZIARA YA KIKAZI MKOANI TANGA

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Pikipiki mmoja wa maafisa watendaji kata Wilaya ya Kilindi Bi.Elizabeth Mwita muda mfupi kabla ya Rais Kuhutubia Mkutano wa hadhara mjini Songe Kilindi. Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi mkoani Tanga.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi kombe katibu wa TFF Wilaya ya Kilindi Bwana Omari Javu wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Songe Kilindi jana.Kombe hilo lijulikanalo kama Kikwete cup litashindaniwa katika ligi ya wilaya ambapo mshindi atakabidhiwa kombe hilo na zawadi nyinginezo kibao
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mkutano wa hadhara mjini Songe Kilindi Mkoani Tanga 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara mjini Songe Kilindi mkoani Tanga. Picha na Freddy Maro wa Ikulu

Mheshimiwa Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai, aongea katika mkutano wa sekta ya nyumba

$
0
0
mahojiano ya Mheshimiwa Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai, akihojiwa na Cloudstv wakati wa mkutano wa uwekezaji sekta ya nyumba uliofanyika tarehe 11 Juni, 2014 katika Hotel ya Jumeirah Madnat Dubai. Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt Mohamed Bilal alikuwa mgeni rasmi.

introducing Sajo More ft 4b1 "LifeStyle"

Qaswida~ Subira

viwalo vipya vya Michuzi Media Group kutoka kitaa wear, wajasiriamali vijana bongo

$
0
0
 Baada ya kuvutiwa na ubunifu wa wajasiriamali vijana wa Kitanzania wanaokwenda kwa jina la KITAA WEAR Michuzi Media  Group chini ya Ankal imeona ni vyema kuwaunga mkono kwa kuweka oda kubwa ya T-shirts kwa ajili ya timu yake pamoja na wadau wa Globu ya Jamii na Michuzi TV. Wadau wengi wanavaa Kitaa Wear wakiwemo Diamond, Fid Q na mastaa wengine kibao. Kama umependezwa angalia maelezo hapo chini. Jamaa wako sharp na very professional. Siku nne tu mzigo tayari... KAZI KWAKO!
KITAA WEAR In Store Today
We got a variety of T-Shirts. Its your choice

You choose we deliver ....

Make your choice now and contact us:
WhatsApp / Viber: +255 754 310 202

BBM CHAT: 22696DDA

Skype: mwakatundu.m 
Twitter ; Mike_Tee1

Available colors for T-Shirts are (Brown,Black,Red,Blue and White)

Sizes Available ( Small, Medium,Large, Free Size, and Xtra Large)

mwandani wa mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere (New Terminal III Project)

$
0
0
Hii ni mojawapo ya kazi za MICHUZI MEDIA GROUP. Wasiliana nasi ukihitaji huduma kama hii kwa kampuni ama taasisi yako...Bofya hapo "Contact us" kwa mawasiliano na huduma zenye ubora wa kimataifa.

mashindano ya kuhifadhi Qur'an tukufu KWA MWAKA HUU WA 2014

Kinana azungumza na Filipe nyusi

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mgombea wa Urais wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi kwenye hotel ya Golden Tulip ambapo alikuwa na mazungumzo naye .
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria akisalimiana na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Frelimo Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi, kabla ya kuanza mazungumzo kwenye hoteli ya Golden Tulip.
 Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Frelimo Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari ambao walitaka kufahamu mahusiano yao na CCM pamoja na namna Demokrasia inavyoendeshwa nchini Msumbiji,Mheshimiwa Nyusi alisema mahusiano yao na CCM ni mazuri na ya kihistoria Tangia wakati wa mapambano ya Ukombozi,alipoulizwa kuhusu uwezo wake wa kuongea Kiswahili vizuri alisema wakati wa mapambano ya Ukombozi aliwahi ishi Tunduru na Nachingwea nchini Tanzania.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dr.Asha-Rose Migiro(Kulia),Katibu wa NEC Oganizesheni Dr.Mohamed Seif Khatibu na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Maofisa wengine wa Chama Cha Mapinduzi kwenye meza ya mazungumzo na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya chama cha Frelimo Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi na Ujumbe wake kwenye ukumbi wa  Nyerere,Golden Tulip Hotel.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dr.Asha-Rose Migiro(Kulia),Katibu wa NEC Oganizesheni Dr.Mohamed Seif Khatibu na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye meza ya mazungumzo na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya chama cha Frelimo Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi na Ujumbe wake kwenye ukumbi wa  Nyerere,Golden Tulip Hotel.

Wakazi wa Mtwara na Lindi kushuhudia fursa za Utalii na Uchumi kupitia Tamasha la Utamaduni la Mtwara,Waziri mkuu pinda kuwa mgeni rasmi.

$
0
0
 

Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Tamasha la Mkoa wa Mtwara, ‘Mtwara Festival’, linatarajia kufungua milango ya fursa kwa wakazi wa mikoa ya Mtwara na Lindi katika kuziona fursa kadhaa kwenye sekta ya Utalii na Uchumi.Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia mwezi Agosti 16 na 17 mwaka huu kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona  ulipo Mtwara mjini. Mgeni rasmi katika Tamasha hilo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda huku likiwa na kauli mbiu isemayo ‘Fursa Zimefunguka, Tuzitambue, Tujiandae, Tuzichangamkie.


Tamasha hilo limeandaliwa kwa ushirikiano wa Tanzania Creative Industries Network (TACIN) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) huku likisaidiwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Akizungumzia Tamasha hilo Mwenyekiti Mtendaji wa TACIN, Anic Kashasha alisema kuwa mikoa hiyo inautajiri mkubwa katika utalii, uchumi na vivutio vingi mbalimbali.


"Mikoa hiyo ina utajiri mkubwa tena sana katika rasilimai zake mbalimbali kama vile fukwe nzuri na za kuvutia, utajiri mkubwa wa historia yake utamaduni na hata ubunifu wa aina mbalimbali hivyo matamasha kama haya yanasaidia kwa kiasi kikubwa kutangaza utajiri huo," alisema Kashasha. Aliongeza kuwa, "Kwa sasa mikoa hiyo imeghunduliwa kuwa ina utajiri mkubwa wa gesi na hivyo kuna watu mbalimbali wameshaajiliwa ikiwa pamoja na kupatikana kwa fedha nyingi tayari kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake na taifa zima kwa ujumla."


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu  ya TTB, Devota Mdachi alisema kuwa utalii umekuwa kwa kiasi kikubwa ukisaidia maendeleo ya uchumi wa nchi. Anasema kuwa katika tamasha hilo ambapo kutakuwa na shughuli mbalimbali za kiutamaduni, sanaa na nyinginezo ni nafasi kubwa ya kukuza utalii pia hasa utalii wa ndani au utalii wa kiutamadunia. "Ni nafasi kwao katika kutangaza mengi kuhusiana na masuala ya Utalii, hapa nchini au hata utai wa shughuli za kiutamaduni pia ni muhimu na hii ndio nafasi ya kipekee kwao na kwa wadhamini mbalimbali kujitokeza kuunga mkono Tamasha hili la aina yake," alisema Mdachi.



Tamasha hilo limedhaminiwa na Ofisa ya Mkuu wa Mkoa Mtwara, Mkuu wa Wilaya wa Mtwara na Mikindani Baraza la Wilaya la Mtwara Vijijini, Baraza la Biashara, KIlimo na Viwanda (TCCIA). Wengine ni Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Pride FM, Radio of Mtwara pamoja na Kampuni ya Mawasiliano ya Strictly Communications. 


aua kikongwe baada kufanya unyama manetomango, wengine adakwa na bangi kilo 12 na lita 21 za gongo bagamoyo

$
0
0

Na John Gagarini, Kibaha
JESHI la Polisi mkoani Pwani linamshikilia Fikiri Mwinyimvua (35) mkazi wa Mfuru Kivukoni kata ya Marumbo Tarafa ya Maneromango wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani kwa tuhuma za kumlawiti bibi kizee mwenye umri wa miaka (60) kisha kumwua kwa kumnyonga shingo.
Kabla ya kumwua mtuhumiwa alikuwa akinywa pombe za kienyeji  na marehemu lakini aliwahi kuondoka eneo la kinywaji kisha kumvizi marehemu na kumfanyia vitendo hivyo ambavyo vilisababisha kifo chake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani Pwani, kamanda mwandamizi msaidizi wa jeshi la polisi (SACP) Ulrich Matei alisema kuwa tukio hilo limetokea Kijiji cha Mfuru Kivukoni wilayani humo.
Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo Julai 10 mwaka huu majira ya saa 1:30 usiku Kijijini hapo ambapo mtuhumiwa alimvizia marehemu kwenye eneo la kichaka kisha kufanya unyama huo.
Katika tukio lingine Nuran Hamis (31) anashukiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma ya kusafirisha bangi kilo 12 akiwa kwenye basi dogo la abiria aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili namba T 618 CMU.
Kamanda Matei alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa jana majira ya saa 2:00 usiku kwenye kizuizi cha Maliasili cha Kibiti kata na Tarafa ya Kibiti wilayani Rufiji.
Aidha watu watano wakazi wa Kidongo Chekundu kata ya Magomeni Tarafa ya Mwambao wilaya ya Bagamoyo wanashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kukutwa na pombe ya Moshi maarufu kama Gongo lita 21 kwenye matukio tofauti.
Aliwataja wathumiwa hao kuwa ni Hadija Shaban (37), Rajabu Michael (37), Msafiri Ramadhan (38), Seif Omary (35), Asha Ramadhan (40) pia wakazi watatu wa Ikwiriri wilayani Rufiji nao walikamatw awakiwa na lita 4 za pombe hiyo ambao ni Tabia Salehe (31), Hamis Rwambo (27) na Abdul Rwambo (40).

DKT SHEIN AFUTARISHA WANANCHI KASKAZINI PEMBA

$
0
0
 Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) akiwakaribisha Mashekhe katika futari  aliyoiandaa kwa Wananchi  waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba huko Viwanja vya Ikulu ya Wete
 Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakijumuika kwa pamoja katika futari iliyoandaliwa na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,kwa wananchi hao katika viwanja vya Ikulu ya Wete pemba
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (katikati) akijumuika na akinamama   na Viongozi katika Mkoa wa Kaskazini Pemba katika futari aliyowandalia katika ukumbi wa Ikulu ya Wete Pemba
 Baadhi ya  akinamama mbali mbali wa  Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiwa katika futari aliyowandalia na Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein,katika ukumbi wa Ikulu ya Wete Pemba 
 Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (aliyesimama) alipokuwa akitoa shukurani pamoja na kuomba dua baada ya kumaliza kufutari wananchi waumini wa Dini ya kiislamu,futari iliyoandaliwa na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,kwa wananchi hao katika viwanja vya Ikulu ya Wete pemba
 Wananchi waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiitikia Dua iliyoombwa na  Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (hayupo pichani) baada ya kumalizika futari iliyoandaliwa na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, jana katika viwanja vya Ikulu ya Wete 
Picha na Ramadhan Othman,Pemba.

EU Tanzania Newsletter for July 2014

JARIDA LA WIZARA YA NISHATI NA MADINI

SERIKALI YA JAPAN YATOA MSAADA WA CHAKULA KWA WAKIMBIZI NCHINI

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kupokea msaada wa chakula kwa ajili ya Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu, mkoani Kigoma chenye thamani ya Dola ya Marekani 1.4 sawa na zaidi ya Shilingi 2.3 Bilioni, ambazo zimetolewa na Serikali ya Japan. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada na Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Richard Regan. Waziri Chikawe alipokea msaada huo na kumkabidhi Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa WFP, Regan, Bandari ya Dar es Salaam leo.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akipokea galoni ya mafuta ya kula kutoka kwa Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada (kushoto) ikiwa ni ishara ya makabidhiano ya chakula cha msaada kwa ajili ya Wakimbizi kilichotolewa na Serikali ya Japan. Kulia ni Mkurugenzi Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Richard Regan akipokea msaada huo kutoka kwa Waziri Chikawe ambao una thamani ya Dola za Marekani 1.4 sawa na zaidi ya Shilingi 2.3 bilioni katika tukio la makabidhiano lililofanyika jijini Dar es Salaam leo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akimshukuru Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada (kushoto) kwa msaada wa chakula wenye thamani ya Dola za Marekani 1.4 milioni ambao ni sawa na Shilingi 2.3 Bilioni ambao Serikali yake imetoa kwa ajili ya Wakimbizi wa Kambi ya Nyarugusu, mkoani Kigoma. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Richard Regan ambaye alikabidhiwa msaada huo baada ya Waziri Chikawe kuupokea katika sherehe fupi ya makabidhiano iliyofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI


WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images