Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 497 | 498 | (Page 499) | 500 | 501 | .... | 3278 | newer

  0 0

   Wafanyakazi wa Benki ya Twiga Bancorp wakiwa katika picha ya pamoja nje ya banda lao mapema leo ,kwenye  maonesho ya 38 ya biashara ya kimataifa jijini  Dar es Salaam.

   Mama Mjasiliamali wa kampuni ya Tree of Life,Bi.Jessica Msamba akifafanua jambo kwa  Afisa Masoko wa Twiga Bancorp,Bwa.Adalbert Alchard mapema leo mchana kwenye  maonesho ya 38 ya biashara ya kimataifa jijini  Dar es Salaam.Bi Jesca ni mmoja wa wateja wakubwa wa benki hiyo na amekuwa akiendesha biashara zake za ujasiliamali kupitia mikopo mblimbali ya benki ya  Twiga Bancorp.
   Mkuu wa Shughuli za Kibenki wa Twiga Bancorp,Bwa.Richard Kombole akielezea jambo kwa baadhi ya Wanahabari hawapo pichani,mapema leo kwenye  maonesho ya 38 ya biashara ya kimataifa jijini  Dar es Salaam,waliotaka kufahamu huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo kwa wateja wao,kulia ni Meneja wa Tawi wa benki hiyo Makao Makuu jijini Dar,Bwa.Sigisbert  Komba na nyuma ni Msimamizi wa Usalama wa Majengo benki ya Twiga Bancorp.
   Afisa Masoko wa Twiga Bancorp,Bwa.Adalbert Alchard akihojiwa na moja ya chombo cha habari,mapema leo mchana kwenye  maonesho ya 38 ya biashara ya kimataifa jijini  Dar es Salaam,kuhusiana na huduma wazitoaza kwa wateja wao,Bwa.Adalbert amesema kuwa benki yao,Twiga Bancorp inatoa huduma mbalimbali kama vile Akaunti ya Akiba,Akaunti ya Biashara,Akaunti ya Amana,Huduma za Kibenki za Kimataifa,mikopo,utumiaji wa fedha na nje ya nchi,''Dira yetu kubwa ni kuwa taasisi ya kifedha inayoongoza kutoa huduma bora za kibenki nchini'',alisema Bwa.Adalbert.
   Baadhi ya Wateja walipatiwa vipeperushi vilivyosheheni huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo ya Twiga Bancorp.

  0 0

  Banda la Bunge katika Viwanja vya Sabasaba
  Wananchi wakiangalia picha za Maspika ambao walishawahi kuongoza Bunge tangu enzi za ukoloni hadi sasa.
  Majengo ambayo wamewahi kutumiwa na Bunge nayo yawa kivutio. Hapa Wananchi wakiangalia picha hizo katika Banda la Bunge.
  Afisa wa Bunge Ndg. Dickson Bisile akigawa vipeperushi vya Historia ya Bunge kwa wananchi wanaoingia katika Banda la Bunge kupata Elimu kuhusu Bunge.
  Afisa wa Bunge Bi. Asia Minja akitoa maelezo kuhusu hatua mahususi ambazo Muswada hupitia kabla ya kupitishwa kuwa Sheria na Bunge.
  Ndg. Patson Sobha akitoa elimu kuhusu Maana ya Siwa na matumizi yake Bungeni kwa wananchi waliofika katika Banda la Bunge.

  0 0

  Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Mama Mwanamwema Shein (kulia) akisalimiana na Mke wa Kwanza wa Mfalme Muswati wa Swasiland Mama Nomsa Matsebula,alipofika Ikulu ya Migombani na ujume wake leo,akiwa katika ziara ya siku mbili nchini.
  Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Mama Mwanamwema Shein (kulia) akizungumza na Mke wa Kwanza wa Mfalme Muswati wa Swasiland Mama Nomsa Matsebula,alipofika Ikulu ya Migombani na ujume wake leo,akiwa katika ziara ya siku mbili nchini.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

  0 0


  0 0

  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKIKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA DARAJA LENYE UREFU WA MITA 67.95 KATIKA BARABARA YA USAGARA –KISESA YENYE UREFU WA KM 16.8
  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKIPANDA KWENYE TUTA MARA BAADA YA UKAGUZI WA BARABARA YA USAGARA –KISESA YENYE UREFU WA JUMLA YA KM 16.8.
  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKIWAHUTUBIA MAMIA YA WAKAZI WA KATA YA FELA KUHUSU MAENDELEO NA CHANGAMOTO ZA UJENZI WA BARABARA YA USAGARA –KISESA YENYE UREFU WA JUMLA YA KM 16.8.
  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKIAGANA NA WAKAZI WA KATA YA FELA MARA BAADA YA KUWAHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA HADHARA JANA.
  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKITOA MAELEKEZO KWA KAIMU MENEJA WA TANROADS MKOA WA MWANZA MHANDISI ERNEST NGAILE KUHUSU UJENZI WA BARABARA YA USAGARA –KISESA.

  0 0


  0 0

  Mke wa Mfalme Mswati wa Swaziland Nomsa Matsebula kulia akipata maelezo kutoka kwa Mwalimu wa Chuo cha Kilimo Kizimbani Fumu Ali Garo kuhusu Mmea wa Mchaichai na faida zake wakati alipotembelea katika Shanba la Viungo Kizimbani ikiwa ni Miongoni mwa Ziara yake Zanzibar.
  Mmea wa Mmanjano kama Unavyoonekana ambao ni miongoni mwa mimea yenye faida kubwa ambao hupatikana sehemu ya Kizimbani Zanzibar.
  Mke wa Mfalme Mswati wa Swaziland Nomsa Matsebula Katikati akipata maelezo kuhusu Mmea wa Mmanjano na faida za Manjano Kwa Mwalimu wa Chuo cha Kilimo Kizimbani Fumu Ali Garo wakati alipotembelea katika Shanba la Viungo Kizimbani ikiwa ni Miongoni mwa Ziara yake Zanzibar.
  Mke wa Mfalme Mswati wa Swaziland Nomsa Matsebula akishika Mmea wa Mvuje na kupata maelezo yake kwa Mwalimu wa Chuo cha Kilimo Kizimbani Fumu Ali Garo wakati alipotembelea katika Shanba la Viungo Kizimbani ikiwa ni Miongoni mwa Ziara yake Zanzibar.
  Mke wa Mfalme Mswati wa Swaziland Nomsa Matsebula akipata maelezo kutoka kwa Mtembezi wa Watalii Shaaban Ali Hassan kuhusiana na Kima Punju alipotembelea katika maeneo ya Jozani Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni Miongoni mwa Ziara yake Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

  Wakati Taifa Stars inaingia kambini Tukuyu mkoani Mbeya kesho (Julai 9 mwaka huu), kocha Mart Nooij amesema kambi ya wiki mbili nchini Botswana imekisaidia kikosi chake kujiandaa kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam leo (Julai 8 mwaka huu) kuhusu maandalizi ya timu hiyo, Nooij amesema timu yake inafanya mazoezi kwenye maeneo ya baridi kwa sababu za kitaalamu, hivyo kambi ya Tukuyu kama ilivyokuwa ya Botswana itawasaidia kwa mechi dhidi ya Msumbiji.

  Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka kwa ndege kwenda Mbeya ikiwa na kikosi cha wachezaji 25, na itarejea jijini Dar es Salaam siku tatu kabla ya mechi hiyo.

  Wachezaji walioko kwenye msafara huo ni Aggrey Morris, Aishi Manula, Amri Kiemba, Benedictor Tinoko, Deogratius Munishi, Edward Charles, Emmanuel Namwando, Erasto Nyoni, Haruni Chanongo, Himid Mao, John Bocco na Jonas Mkude.

  Wengine ni Joram Mgeveke, Kelvin Friday, Kelvin Yondani, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa, Mwagane Yeya, Nadir Haroub, Oscar Joshua, Pato Ngonyani, Ramadhan Singano, Said Juma, Said Moradi, Shomari Kapombe, Simon Msuva,

  Mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Afrika (AFCON) dhidi ya Msumbiji itafanyika Julai 20 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  BONIFACE WAMBURA
  OFISA HABARI NA MAWASILIANO
  SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0

  Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Property International Bwana. A. Haleem alipomtembelea banda la kampuni hiyo inayoshiriki Maonesho ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es salaam. Kampuni hiyo inatoa huduma za kupima ardhi na viwanja kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

  0 0

  Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi ya Finland imeanzisha Programu ya’Panda Miti Kibishara’ (Private Forestry Programme). Programu hiyo yenye makao makuu Njombe inayo madhumuni ya kuwahamasisha wananchi kupanda miti kwa kuzingatia kuwa miti ni zao la biashara.

  Ingawaje Programu hiyo imeshiriki kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya Sabasaba ilikuwa kati ya sehemu zilizowavutia watu wengi ndani banda la Maliasili na Utalii. Wananchi walotembelea waliuliza maswali kuhususiana na aina za miti ya mbao inayofaa kupandwa katika sehemu zao na upatikanaji wake.

  Programu ya Panda Miti Kibiashara inatekelezwa katika wilaya sita za Ludewa, Makete, Njombe, Kilolo, Mufindi na Kilombero. Programu hii ni ya miaka 16 lakini itatekelezwa kwa awamu za miaka minne kila moja.

  Lengo la Programu hiyo  ni  kuongeza kipato cha wananchi  waishio  vijijini kwa kupanda miti. Lengo hilo litafanikiwa kama wananchi watalima mashamba ya miti kitaalam kwa kuzingatia matumizi  ya  mbegu bora na kulihudumia shamba kitaalam ili mazao yatakayopatikana  yaweze kuvutia soko la ndani na nje.

  Lengo jingine ni kuanzisha shughuli  ya kujiongezea kipato nje ya shamba la miti wakati wahusika wakisubiri miti ifikie umri wa kuvunwa. Shughuli hizo ni kama vile kilimo cha matunda na ufugaji nyuki. Aidha wananchi  wamehimizwa kuunda vikundi vya Wakulima wa Miti ili iwe rahisi kwa Programu kutoa msaada kwao. 

  Kwa sasa miche ambayo itapandwa na wananchi walioko katika wilaya zinazohudumiwa na Programu inakuzwa kwenye vitalu ili iwe tayari kupandwa mwezi Desemba mwaka huu na Januari mwakani.

  Programu imeazimia kuwa katika kipindi cha awamu ya kwanza ya Programu (mwaka 2014 hadi 2017) jumla ya hekta 15,000 zitapandwa na wananchi waliojiunga na Vikundi vya Wakulima wa Miti.


  0 0

   Mwana wa mfalme wa Japan Prince Fumihito Akishino na mkewe Kiko, wakifurahia ngoma za makabila la Wadatoga (Barbaig) na ile ya Wamasai, katika eneo la mlango wa Loduare kwenye hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro, pamoja nao wapo pia maafisa wa mamlaka hiyo, Bruno Kawasange na Adam Akyoo pamoja na Mkuu wa wilaya ya Karatu, Felix Daudi Ntibenda.
   wakiwa wanafurahia ngoma za wamasai pamoja na wabarabaigi.
   Katika picha nyingine Mwana huyo wa mfalme wa Japan akipewa maelezo kuhusu shughuli za uhifadhi ndani ya mamlaka hiyo katika kutuo cha habari cha Loduare Gate.


  0 0

  Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Excel Management and Outsourcing,Deogratius Kilawe (wa tatu kulia) akikabidhi sehemu ya Misaada kwa Sista Silvanus ambaye ni Msimamizi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Msimbazi jijini Dar.Kampuni ya Excel Management and Outsourcing imetoa msaada huo baada ya kuguswa na kuona uhitaji wa Watoto hao.
  Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Excel Management and Outsourcing,Deogratius Kilawe pamoja na timu yake wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi msaada wao kwa Kituo cha Watoto Yatima cha Msimbazi,jijini Dar.
  Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Excel Management and Outsourcing,Deogratius Kilawe akisaini kitabu cha Wageni kwenye Kituo hicho.

  0 0

  Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawaarifu wananchi kwa jumla kuwa imefanikiwa kuwasafirisha kuja Dar abiria takriban 678 waliokwama katika Stesheni ya Manyoni. Zoezi hilo linaloendeshwa kwa awamu mbili tofauti lilianza usiku wa manane hadi saa 10 usiku wa kuamkia leo .

  Kwa mujibu wa taarifa ya uongozi zoezi la pili litaanza tena kuanzia saa asubuhi ya leo kwa abiria wapatao 699 waliosalia kutegemeana na kupatikana mabasi mengine zaidi ya 11 yanayohitajika.

  Kukwama kwa treni hiyo iliyokuwa ikitokea Tabora kuja Dar kumesababishwa na ajali ya treni ya mzigo iliyokuwa ikienda Bara ambapo ilitokea kati ya Stesheni za Kintinku na Makotopora km 539/6-0 jana saa 6:50 mchana. Katika ajali hiyo mabehewa 7 yalianguka na moja liliacha reli.

  Tathmini ya Wahandisi wetu ni kuwa kazi ya kukarabati njia itachukua saa 12 na hivyo njia inatarajiwa kufunguliwa saa 6 usiku wa manane leo.

  Safari ya abiria kwenda bara ya leo Julai 08, 2014 itaendelea kama ilivyopangwa hata hivyo muda wa kuondoka umesogezwa mbele ambapo itaondoka stesheni ya Dar es Salaam saa 2:30 usiku.

  Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi 
   Kipallo Aman Kisamfu.
  TRL Makao Makuu, 
   Dar es Salaam. 
   Julai 08, 2014

  0 0

   Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan S. Kaganda leo tarehe 08.07.2014 akiongea na waandishi wa habari na kutoa ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali ikiwemo kukamatwa kwa wahamiaji haramu 17 kutoka nchini Burundi
   Sehemu ya wahamiaji haramu 17 kutoka nchini Burundi wakiwasili kituo cha kati Tabora
  Mmoja wa wahamiaji haramu 17 kutoka nchini Burundi akiongea na wanahabari

  0 0

  Mkurugenzi wa Amref Health Africa Tanzania Dr. Festus Ilako (wa kwanza Kushoto) Akimkaribisha Waziri wa Afya Dr. Seleman Seif Rashid kuzindua Nembo Mpya.
  Waziri wa Afya, Mwenyekiti wa bodi ya kimataifa ya Amref Health Africa Mr. Omari Issa, Dr. Festus Ilako na wafanyakazi wa Amref Health Africa Tanzania katika picha ya pamoja baada ya Uzinduzi.
  wadau na wageni waalikwa katika uzinduzi huo
  Picha ya pamoja ya meza kuu na wadau 
  wa Amref Health Africa baada ya Uzinduzi.

  SHIRIKA la kimataifa lisilokuwa la kiserikali la Afrika Medical and Research Foundation (Amref) limezindua rasmi jina na nembo yake mpya ambapo sasa litajulikana kama Amref Health Africa Tanzania.
  Uzinduzi huo ulifanywa jijini Dar es Salaam Ijumaa ya tarehe 4/7/2014 na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid ambapo Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Festus Ilako, alisema imebidi kubadili jina na nembo yao ili kuendana na majukumu yao ya sasa ambayo yamekuwa ni zaidi ya utafiti na utoaji wa huduma za tiba.
  “Kwa sasa tunajikita pia katika uimarishaji wa mifumo ya utoaji wa huduma za afya, mafunzo, mikakati ya utoaji wa huduma/miradi ya afya ya mama na mtoto, ukimwi, kifua kikuu, malaria, huduma za madaktari bingwa na maabara.
  “Mabadiliko ya jina na nembo yetu hayataathiri aina ya walengwa wetu wakuu; tutaendelea kufanya kazi kwa karibu kabisa,” alisema Dk. Ilako.
  Alitoa mfano kuwa kila siku wanawake 22 wanapoteza maisha nchini wakati wa kujifungua na kwamba mpango wa Amref ni kupunguza vifo hivyo. Waziri Seif katika hotuba yake ya uzinduzi, alisema serikali inatambua mchango mkubwa wa taasisi hiyo na kwamba wamesaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, mimba za utotoni na upatikanaji wa majisafi na salama.

  0 0

  bom 1Mbunge viti maalum Mhe.Catherine Magige kupitia chama cha mapinduzi CCM akimjulia hali Deepak Gupta (25 aliyepoteza mguu wake ) mmoja wa majeruhi wa bomu lililolipuka jana usiku majira ya saa 4 usiku  katika mgahawa wa VAMA Traditional Indian Culture jijini A rusha na majeruhi hao  kukimbizwa katika hospital ya Selian
  bom 2Mhe. Mbunge Catherine Magige akimjulia hali mmoja wa majerui katika hospital ya Selian,kushoto ni Mkurugenzi wa tiba ambaye pia ni kaimu mgamga mkuu wa hospitali hiyo kulia ni Dk.Afizay Mkufya.
  bom 4Mhe.Mbunge Catherine Magige akiangalia  kwa uchungu namna Deepak Gupta (25 )mmoja wa majeruhi katika bomu ambapo alipoteza mguu wake wa kushoto .
  bom7
  Mhe.Mbunge Catherine Magige akimjulia hali mtoto Ridtwaik Lwal (13)aliyejeruhiwa mkononi kwa bomu

  Mbunge wa viti Maalum kupitia chama cha mapinduzi CCM Mh.Catherine Magige amelaani vikali  tukio la Bomu lililotokea katika mgahawa wa VAMA Tradition Indian Culture  jijini Arusha huku akiitaka serikali kuwachukulia hatua kali kwa wale wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo

  Mh.Magige aliyasema hayo leo katika hospitali ya Selian wakati alipowatembelea majeruhi nane Raia wa Asia waliolazwa katika hospitali hiyo ambapo wengi wa majeruhi waliumia katika maeneo ya miguu,mikono na tumboni hali iliyopelekea mmoja wa majeruhi kupoteza mguu wake wa kushoto

  Magige alisema kuwa kutokana na matukio ya aina hiyo kutokea kwa mfululizo, hali hiyo imesababisha jiji la Arusha kupoteza amani ili hali Tanzania ni Nchi ya Amani'

  "Inasikitisha sana kwa kweli matukio kama haya kujirudia rudia inatia hofu sana kwa wakazi wa Arusha pamoa na wageni wanaokuja katika jiji letu"alisema

  Aidha alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa vyombo vya dola kufanikisha kukamatwa kwa wale wote wanaohusika na matukio ya uvunjifu wa amani.(Pamela Mollel wa Jamii blog)

  0 0


  0 0

   Mgeni rasmi Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) akiwaonesha wajumbe wa Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mfumo wa Kushughulikia Malalamiko ulioandaliwa na Ofisi hiyo mara baada ya kuuzindua leo katika kikao cha kwanza cha Baraza hilo mkoani Tanga. Katikati ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar Mohamed Hafidh Rajab na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.
   Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) akiwaonesha wajumbe wa Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Mkataba wa Huduma kwa Mteja ulioandaliwa na Ofisi hiyo mara baada ya kuuzindua leo katika kikao cha kwanza cha Baraza hilo mkoani Tanga. Katikati ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar Mohamed Hafidh Rajab na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.

   Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akimkabidhi mgeni rasmi Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) Mkataba wa Huduma kwa Mteja katika kikao cha Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kilichofanyika  leo mkoani Tanga. Katikati ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar Mohamed Hafidh Rajab.
  Mgeni rasmi Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya Salum (Mb) akimkabidhi cheti kama zawadi ya Mfanyakazi bora Bi. Sylivia Meku ambaye ni Mtakwimu Mkuu na Mwenyekiti mpya wa TUGHE –Tawi la Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kikao cha Baraza la Nne la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo  kilichofanyika  leo mkoani Tanga. (PICHA ZOTE NA NBS, TANGA)

  0 0

   Mdau Kheri A. Mahimbali akiwa na mzee wake Abdul Ahmed Dau (kushoto) na mtoto wa simba Ahmed Dau baada ya kula nondoz ya MSc in Oil and Gas Enterprise Management.
   Mdau Kheri A. Mahimbali akiwa na professor wake Professor David MacDonald mtaalam wa mas-ala ya Geology.
   Wadau kutoka kushoto bwana Haruna Mbeyu "Meya wa London" akiwa na Al-watan wa Leicester bwana Abdul Dau akifuatiwa na graduate bwana Kheri Mahimbali na wa mwisho bwana Ahmed Dau "mtoto wa simba" wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Aberdeen wakijiandaa na safari.

  0 0

  British Foreign Office Minister for Africa, Mark Simmonds (pictured), arrived in Dar es Salaam today on a two day visit to the country.  This is Mr Simmonds’ third visit to Tanzania in just over a year, showing the importance the UK attaches to relations with Tanzania.  

  One the key objectives of Mr Simmonds’ visit is to review progress on the UK-Tanzania High Level Prosperity Partnership agreed between Mr Simmonds and President Kikwete last June.  Mr Simmonds kicked off his visit by co-chairing together with Hon Samuel Sitta, Minister for East African Cooperation, a high level review of progress in the Partnership’s four priority areas: oil and gas, agriculture, renewable energy and strengthening the business environment.  

  Another key focus of the visit will be on poaching and the illegal wildlife trade, following up on the London Conference on the Illegal Wildlife Trade that President Kikwete and Minister Nyalandu attended in February.  Accompanied by Hon Lazaro Nyalandu, the Minister for Natural Resources and Tourism, Mr Simmonds will see for himself the challenges facing Tanzania and confirm UK support for action against organised crime.

  Mr Simmonds will also launch the new British Chamber of Commerce during his visit.

  Speaking at the outset of his visit Mr Simmonds said:

  “I am absolutely delighted to be back in Tanzania again, almost a year to the day of my last visit. The UK sees Tanzania as one of its key partners in Africa. I am here to review the progress made on our High Level Prosperity Partnership. Our ambition is clear: to work in partnership with Tanzania to increase our bilateral trade and investment, support development, and generate prosperity for both our countries. I will also be visiting the Selous with minister Nyalandu to see stepped up efforts to tackle poaching and the illegal wildlife trade.  The UK will continue to look for every opportunity to build on the strong partnership we have with Tanzania across an increasing range of shared priorities”.

  Notes for Editors

  The UK is the Number 1 investor in Tanzania with 35% share of foreign direct investment.  According to the Tanzania Investment Centre, UK companies invested around $ 5.1bn (TSh 8,415,000,000,000) in Tanzania in the period 1990-2013 (June), creating 271,000 jobs – almost four times as many as any other investor. Bilateral trade was worth $ 340 million (Tsh 561,000,000,000).  British firms play an important role in all the major sectors including energy, communications, construction, banking, agriculture, and the nascent oil and gas sector, where the British company BG Group alone has invested in excess of $ 1 billion (Tsh 1,650,000,000,000), with substantially more in prospect.

  The UK has pledged to help Tanzania achieve middle income status through accelerated and inclusive, private sector led growth. This will be an increasing focus of UK development cooperation in Tanzania, and will include sharing UK experience of public private partnerships and promotion of partnerships between UK and Tanzanian companies to maximise local job creation and develop local skills.  

  Tanzania is one of only five African countries with which the UK has signed a High Level Prosperity Partnership, focussing on 4 priority areas: agriculture, extractives, renewable energy and improving the business environment.  We are also working in partnership with the Government of Tanzania to implement a G8/Tanzania Land Transparency Initiative. 

  Tanzania is one of DFID’s largest African country programmes.  Our development budget for Tanzania for this year alone (2014/15) is £165 million (Tsh 452 billion). Of this figure, £71.5 million (Tsh 196 billion) is direct budget support to the Government of Tanzania. An independent review of donor support to the Government’s budget last year concluded that UK funding had enabled Tanzania to expand services, especially in education and roads, throughout the country, making an important contribution to improving lives and opportunities for poor people.


  The UK also does a lot of work on English Language Teaching, Education and the Arts, creating opportunities for young Tanzanians to engage with other cultures and develop international perspectives. This is helping young Tanzanians access the best educational opportunities at home and abroad to improve their skills in preparation for study and work. For example, the British Council has some 300 school links between Tanzania and the UK through which 3,000 school leaders and 30,000 teachers have been trained in 25 hubs around Tanzania.  We are also creating opportunities for young Tanzanians to study abroad on scholarship programmes like the Chevening and Commonwealth Scholarship Schemes.


older | 1 | .... | 497 | 498 | (Page 499) | 500 | 501 | .... | 3278 | newer