Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 496 | 497 | (Page 498) | 499 | 500 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Promota wa mbambano wa ngumi usiokuwa na ubingwa, Rashid Kipanga akiwatambulisha, Manenono Osward(Mtambo wa Gongo) kulia na Abdalah Pazi (Mudi Mbabe) wanaotarajia kuchuana Augosti 10,2014.Utambulisho wa pambano hilo ulifanyika katika Ukumbi wa Mwinjuma Dar es Salaam jana.
  Mchezaji wa Ngumi, Abdalah Pazi (Mudi Mbabe) akisaini mkataba wa kupigana na Bondia Maneno Osward (Mtambo wa Gongo) hapo Augosti 10,2014 katika Ukumi wa CCM Mwinjuma jijini Dar es Salaam.Kulia ni Rais wa Chama cha Ngumi Tanzania(TPBC), Chaurembo Palasa akishuhudia.
  Mchezaji wa Ngumi, Maneno Osward (Mtambo wa Gongo) akisaini mkataba wa kupigana na Abadalah Pazi (Mudi Mbabe) Augosti 10,2014 katika Ukumi wa CCM Mwinjuma jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Rais wa Chama cha Ngumi Tanzania(TPBC), Chaurembo Palasa akishuhudia.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya J.V anayejenga barabara ya Makutano-Nyamuswa - Ikoma Gate, sehemu ya (Makutano-Natta km50) kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha mradi huo kwa wakati. Waziri Magufuli alitoa tamko hilo jana wakati akihutubia mamia ya wakazi wa mji Butiama mkoani Mara.

  “Najua bado mnaidai serikali zaidi ya shilingi bilioni tatu lakini hii isiwe sababu ya kushindwa kuendelea na kazi japo mlishaonyesha mfano mzuri wa kuanza kujenga daraja la Kyarano” alisema Waziri Magufuli Aidha, Waziri Magufuli aliahidi kuwa ndani ya wiki mbili atatafuta fedha kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi huyo ili aweze kuendelea na kazi kwa kasi kubwa.

  “Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara yupo hapa pamoja na wataalamu wangu, tutahakikisha ndani ya wiki mbili tutatafuta fedha kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi pamoja na fidia na kuondoa nguzo za umeme” Aligusia Waziri Magufuli Pia Waziri Magufuli aliwatoa hofu Wananchi wa Butiama kwa kusema kuwa wale wote waliofuatwa na barabara katika maeneo yao watafidiwa kama sheria inavyoeleza.

  “Nawahakikishia kuwa wale wote mliofuatwa na barabara hii mtafidiwa kwa mujibu wa sheria, ila kwa wale wote walioifata barabara wabomoe wenyewe nyumba zao” Aidha, Waziri Magufuli amepinga wazo la Halmashauri ya Wilaya ya Butiama kutaka kumtoza fedha Mkandarasi wa Kichina kwa ajili ya mawe anayotumia kujengea barabara mkoani Mara.

  “Hapa sikubaliani na wazo lenu yaani Mkandarasi anachukua mawe anapasua kokoto kwa ajili ya kujenga barabara halafu nyie mnataka kumtoza fedha” Waziri Magufuli aliongeza kuwa kuna watu wa mikoa mingine hawajawai hata kuona rangi ya lami na wangetamani kuwapa hao wachina mawe ili wawajengee barabara, hivyo Halmashauri itatakiwa ibadili uamuzi huo haraka.

  Pia Waziri Magufuli amemtaka Mkandarasi huyo wa Kichina kutumia mawe hayo katika ujenzi wa barabara na si vinginevyo. Katika hatua nyingine Waziri Magufuli amewaasa Wakazi wa Butiama kuilinda Amani iliyopo nchini.

  “Baadhi ya nchi nyingine zinajuta kutokana na machafuko yaliyopo mfano Burundi, Misri, Iraq na Libya” Alisema Waziri Magufuli.
  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKISHUKA KUANZA UKAGUZI WA DARAJA LA KYARANO LENYE UREFU WA MITA 53.5 NA UPANA WA MITA 10 KWENYE BARABARA YA MAKUTANO-NYAMUSWA-IKOMA SEHEMU YA MAKUTANO NATTA KM 50.
  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI WAPILI KUTOKA KUSHOTO AKIPITA KWENYE MOJA YA NGUZO ZA DARALA LA KYARANO KATIKA WILAYA YA BUTIAMA MKOANI MARA.
  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKIENDELEA NA UKAGUZI WA BARABARA YA MAKUTANO-NYAMUSWA-IKOMA SEHEMU YA MAKUTANO NATTA KM 50.
  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKIKAGUA UJENZI WA MAKARAVATI YA DUARA (PIPE CULVERTS) KATIKA ENEO LA MKANDARASI.
  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKISALIMIANA NA MBUNGE WA BUTIAMA NIMROD MKONO BAADA YA KUKAGUA KAZI ZA UFYATUAJI WA MAKARAVATI YA DUARA (PIPE CULVERTS) KATIKA ENEO LA MKANDARASI.
  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKITETA JAMBO NA MBUNGE WA BUTIAMA NIMROD MKONO KABLA YA KUHUTUBIA MAMIA YA WAKAZI WA BUTIAMA KATIKA ENEO LA MAKUTANO KUHUSU UJENZI WA BARABARA YA MAKUTANO NATTA YENYE UREFU WA KILOMITA 50.
  WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKIHUTUBIA MAMIA YA WAKAZI WA MAKUTANO KATIKA WILAYA YA BUTIAMA MKOANI MARA.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho kikwete akipozi na viongozi na wafanyakazi katika banda la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) alipofanya ziara ingine tena leo Julai 6, 2014 baada ya ziara yake ya jana kutokamilika kutokana na muda
   Rais Jakaya Mrisho kikwete akipozi na vijana wa Skauti wanaofanya kazi ya  ulinzi wa viongozi alipofanya ziara ingine tena leo Julai 6, 2014 baada ya ziara yake ya jana kutokamilika kutokana na muda

   Rais Jakaya Mrisho kikwete akipozi na viongozi na wafanyakazi katika banda laPPF  alipofanya ziara ingine tena leo Julai 6, 2014 baada ya ziara yake ya jana kutokamilika kutokana na muda

   Rais Jakaya Mrisho kikwete akipozi na viongozi na wafanyakazi katika banda la TTCL  alipofanya ziara ingine tena leo Julai 6, 2014 baada ya ziara yake ya jana kutokamilika kutokana na muda

   Rais Jakaya Mrisho kikwete akipozi na viongozi na wafanyakazi katika banda la TRA alipofanya ziara ingine tena leo Julai 6, 2014 baada ya ziara yake ya jana kutokamilika kutokana na muda
  Rais Jakaya Mrisho kikwete akipozi na viongozi na wafanyakazi katika banda Ardhi University  alipofanya ziara ingine tena leo Julai 6, 2014 baada ya ziara yake ya jana kutokamilika kutokana na muda


  0 0


  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Karimjee leo wakati alipokua akitangaza Uzinduzi mkubwa wa Albam ya Shikilia Pindo maarufu kwa jina la FACEBOOK ya mwimbaji nguli wa muziki wa injili Rose Muhando, 

  Msama alisema kuwa albamu hiyo itazinduliwa Agosti 3 mwaka huu katika ukumbi wa Diamond-Jubilee jijini Dar es Salaam na baada ya hapo itatambulishwa katika mikoa kadhaa nchini.

   Msama amesema kuwa baada ya albamu hiyo kuzinduliwa jijini Dar,Rose Muhando ataitambulisha tena albamu hiyoa kwa mashabiki wake Agosti 10 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
   
  Amesema kuwa kwa upande wa mkoa wa Mwanza,Rose Muhando ametoa kipau mbele kwa jiji hilo kuwa chaguo lake la kwanza baada ya uzinduzi wa jijini Dar es Salaam.Msama amewataka mashabiki wa mwimbaji huyo nyota wa nyimbo za injili hapa nchini kujitokeza kwa wingi na kumuunga mkono.
   
  Msama amesema kuwa Rose Muhando anaendelea kujipanga vyema kuhakikisha anawapa burudani ya nguvu,

  Kwa mujibu wa Alex Msama amesema kuwa nyimbo zilizopo katika albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu ni Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook.

  Hivi sasa Muhando anatamba na albamu yake ya Utamu wa Yesu yenye nyimbo saba, ambazo ni Utamu wa Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia.

  Mbali na Utamu wa Yesu, Rose Muhando pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu Anacheka, Wololo.Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya.

  Kitimutimu, Mungu Anacheka, Wololo.Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya.


  0 0

  KISIWA CHA SAANANE NI MOJA KATI YA VIVUTIO  VILIVYOKO CHINI YA HIFADHI ZA TAIFA ,TANZANIA (TANAPA) ,TIZAMA MANDHARI ZA KUVUTIA KUZUNGUKA HIFADHI HIYO ILIYOKO JIJINI MWANZA. Video imepigwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini


  0 0

  Mashabiki wa Diamond Platnumz wakipata nae picha ya pamoja na Rais huyo wa Wasafi alipokuwa akiwasili kwenye mji wa Olathe jimbo la Kansas ilipo Radio hiyo ya GENN kwa mahajiano kabla ya show yake inayotarajiwa kufanyika muda si mrefu katika anuani ya 8625 Troost Ave, Kansas City, Missouri.
  Mtangazaji wa GENN Radio AJ (mwenye kofia nyeusi wapili toka kulia) akimfanyia mahojiano Diamond Platnumz ndani ya Studio ya Radio hiyo ambayo inapatikana mtandaoni www.gennmedia.com wengine ni Dj Romy Jons Poromota DMK na Dj Bston (kulia) .
  Diamond Platnumz akiendelea kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na AJ huku Dj Romy Jons akifuatilia kwa makini maswali na majibu yaliyokua yakiulizwa AJ na kujibiwa na Diamond Platnumz.
  Diamond Platnumz akijibu moja ya maswali kutoka kwa AJ.
  Kwa taarifa kamili na picha kibao BOFYA HAPA

  0 0

  IMG_1291
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa.

  WATEJA wanaotembelea banda la MeTL Group lililopo kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea kwenye mabanda ya SabaSaba katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, leo Jumatatu wanatarajiwa kuchezeshewa droo maalum itakayotoa zawadi mbalimbai ikiwemo pikipiki.
  Katika droo hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na atakabidhi zawadi kwa wateja mbalimbali watakaojishindia zawadi hizo.
  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya MeTL GROUP, Fatema Dewji- Jaffer alieleza kuwa, droo hiyo ni maalum kwa ajili ya wateja wote waliopata kutembelea banda hilo tokea siku ya kwanza na kujiorodhesha majina yao
  Fatema alisema MeTL Group imeamua kutoa zawadi hizo kama shukrani na kujitangaza zaidi kwa wateja na wananchi waliopata kutembelea na kununua bidhaa za MeTL Group.
  “Kwa ubora wa bidhaa zetu za MeTL Group, kama inavyojulikana, ‘The People’s Brand’, kwa droo hii wateja wetu watafurahia kwa zawadi hizo nono” alisema Fatema.
  Katika droo hiyo, zawadi kuu ni pamoja na Pikipiki, zawadi za khanga, vitenge, mashuka, sabuni za kuogea na kufulia, mafuta ya kupikia, unga na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo.
  Aidha, MeTL Group imetambulisha rasmi vinywaji vyake vipya kwenye maonyesho hayo ya Saba Saba, ikiwemo kinywaji kinachopendwa na wengi kwenye maonyesho hayo, MO Cola, MO Portello na MO Malt. Vingine ni MO Lemon Mint, MO chungwa na MO Bomba (Energy drink).

  0 0

  Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi. 

   Imeelezwa kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kukabiliana na tatizo la uzagaaji wa silaha ndogo ndogo na nyepesi kutokana na nchi nyingine za Afrika kuja kujifunza jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo hapa nchini. 

   Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bw.Meshack Ndaskoi wakati akifungua semina ya jinsia na uthibiti wa silaha ndogondogo na nyepesi iliyofanyika katika chuo cha Taaluma za Polisi (DPA) jijini Dar Es Salaam jana na kuwashirikisha wadau wa usalama na jinsia hapa nchini. 
   Bw. Ndaskoi alisema Tanzania imekuwa ikifanya vyema kutokana na kuchukua hatua mathubuti ikiwemo ya kuziweka alama silaha zote zilizopo nchini ili kuweza kutambulika kwa urahisi pindi zinapotumika katika matukio ya uhalifu. 
   “Tumeweza kutekeleza sera ya kudhibiti silaha na kuunda kamati ya kitaifa ya kudhibiti uzagaaji wa silaha ndogondogo na nyepesi hapa nchini na yamekuwa yakitolewa mafunzo mbalimbali kwa wadau ili kuungana katika kulikabili tatizo hili” Alisema Ndaskoi. 
   Kwa upande wake Mratibu wa kitaifa wa Kudhibiti silaha ndogondogo na nyepesi Nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi Essaka Mugasa amesema lengo la Semina hiyo ni kutathmini kwa kina mahusiano yaliyopo baina ya uzagaaji wa silaha na jinsia hapa nchini na barani Afrika kwa ujumla kwa kuwa tatizo hilo hivi sasa limekuwa likikua siku hadi siku. 
   Aidha alisema pamoja na zoezi la kuweka alama silaha ambalo linaendelea hivi sasa lakini pia wanafanya operesheni za mara kwa mara na kutumia dhana ya Polisi Jamii na ulinzi shirikishi katika kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
  Alisema kwakupitia Polisi Jamii na ulinzi shirikishi wamekuwa wakipata taarifa ambazo zimewezesha kusalimishwa kwa silaha mbalimbali hapa nchini ambazo zilikuwa zikimilikiwa isivyo halalai. 
  Nao washiriki wa Semina hiyo walisema itawasaidia katika utendaji kazi wao wa kila siku na kutoa elimu kwa wengine ili kutokomeza uzagaaji wa silaha ndogondogo na nyepesi hapa nchini.

  0 0

  1
  Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete na Diwania wa Kata ya Bwilingu Bw. Ahmed Nasser wakiwa wamelala kwenye moja ya vitanda Vitanda 267 vilivyotolewa na mbunge huyo katika shule mbalimbali za sekondari kwa jimbo zima la Chalinze wakati wa makabidhiano yaliyofanyika kwenye shule ya sekondari ya Lugoba jana, Shule ambazo zimepewa vitanda hivyo ni shule ya sekondari Chalinze 50, Moleto Lugoba 50, Mandera 25, Talawanda 24, Kiwangwa 50, Lugoba 38 na Kikaro 30.katika hatua hiyo Mh. Ridhiwania pia amepiga hatua kwa kutekeleza mambo mbalimbali aliyoahidi wakati wa kampeni zake. Katika utekelezaji huo ametoa Baiskeli 10 kwa walemavu, Miwani na mafuta kwa Maalbino, Jezi pea 100 kwa ajili ya mbunge Cup mashindano ambayo yataanza baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhan, Visima 3 kata ya Kibindu, na 16 kwa shule zote za sekondari jimbo zima kila shule kisima kimoja kitachimbwa.
  Ametoa Transforma kubwa ya umeme kata ya Lugoba na kumaliza kabisa tatizo la umeme katika kata hiyo, Kwa upande wa barabara amesema mvua zimekwisha hivyo barabara zote za jimbo hilo ambazo ziliharibwa na kutopitika sasa zitafunguliwa baada ya kupatikana kwa mdau ambaye atatoa mashine (Mitambo)za kukarabati barabara na mafuta yapo ya kutosha kuhakikisha kazi hiyo inakamilika kabla ya kuanza tena kwa mvua za masika ili kuzinfungua upya.
  Mh. Ridhiwani pia ametoa mipira kwa shule za Msingi jimboni humo,, ametoa Microscope kwa Zahanati ya kanisa Lugoba. na atajenga darasa 1 shule ya msingi Kiwangwa.
  Wengine katika picha kulia ni Abukbakary Mlawa Meneja Uhusiano wa kampuni ya Mamba Cement ambayo ndiyo iliyotoa vitanda hivyo na kushoto ni Diwani wa Kata ya Lugoba Bi Rehema Mwene.
  3
  Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Mamba ment ambayo ndiyo iliyotoa vitanda hivyo wakivikabidhi kwa Diwani wa kata ya Bwilingu Bw. Ahmde Nasser na Mwalimu Mkuu wa Shule ya sekondari Chalinze Bw. Emmanuel Kahabi katika makabidhiano yaliyofanyika kwenye shule ya sekondari ya Lugoba.
  4
  Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi vitanda Mkuu wa shule ya seondari ya Sekondari ya Mandera Bi. Rose Jumila, kushoto ni Diwania wa Viti maalum kata ya Msoga Bi. Maria raban Moreto.
  5
  Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lugoba wakipiga pichya pamoja mbele ya vitanda hivyo kwa niaba ya wenzao.


  0 0

  Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudentia Kabaka akisaini katika kitabu cha wageni wakati alipotembelea katika banda la Mfuko wa Mafao ya Kustaafu wa GEPF,kwenye Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es salaam leo.Mwenye Fulana nyeusi ni Meneja Masoko na huduma kwa wateja katika Mfuko wa Mafao ya Kustaafu wa GEPF Bw Aloyce Best Ntukamazina. 
  Meneja Masoko na huduma kwa wateja katika Mfuko wa Mafao ya Kustaafu wa GEPF,Bw. Aloyce Best Ntukamazina akitoa maelezo ya kina kwa Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudentia Kabaka kuhusu mafanikio ya ushiriki katika maonesho ya sabasaba pamoja na huduma na mafao mapya kwa wanachama wa GEPF.  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akimpa maelezo, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, wakati alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam Jumatatu Julai 7, 2014.
   Msanii maarufu nchini, Mrisho Mpoto, (Katikati), akionyesha kadi mpya ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mkuuwa Mfuko huo, Sdam Mayingu, (R), kwenye maqonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam jana. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (Kulia), akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko huo, Mwanachama Mpya, Msanii maarufu nchini, Mrisho Mpoto (Katikati), kwenye maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam jana Jumatatu Julai 7, 2014. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi

  0 0

  Mgeni rasmi kwenye hafla ya kufuturisha watoto waishio katika mazingira magumu mjini Zanzibar,Kadhi Mkuu wa Zanzibar,akiwasili kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa na Vodacom Foundation na kupokewa na Meneja wa Vodacom tawi la Zanzibar, Mohamed Mansoor.
  Baadhi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu mjini Zanzibar wakimsikiliza Kadhi Mkuu Zanzibar Khamis Haj alipokuwa anazungumza nao wakati wa hafla ya kufuturisha watoto hao iliyoandaliwa na Vodacom Foundation jana.
  Kadhi Mkuu wa Zanzibar akikabidhi vyakula,mbuzi, mafuta, mchele na madaftari kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi mjini Zanzibar kwa niaba ya Vodacom Foundation,Wakati wa hafla ya kufuturu hapo jana,Anaeshuhudia kushoto ni Meneja wa Vodacom Tanzania tawi la Zanzibar Mohamed Mansoor.
  Viongozi wa dini mjini Zanzibar pamoja na wa Vodacom Tanzania wakiongozwa na mgeni rasmi Kadhi wa Zanzibar Khamis Haj wakipata futari katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kwaajili ya watoto waishio katika mazingira hatarishi mjini Zanzibar.
  Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Khamis Haj akihutubia kwenye hafla ya kufuturisha watoto wanaoishi katika mazingira magumu mjini Zanzibar,Hafla hiyo iliandaliwa na Vodacom Foundation.
  Juma Haji mkazi wa Zanzibar akisaidia kuwagawia Maji na vyakula baadhi ya watoto waishio katika mazingira magumu waliohudhuria hafla ya kufuturu iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kwaajili yao hapo jana.

  0 0


   Head ofRelationshipand Customer ServicesFund (NSSF), EuniceChiumespeaking toreportersabout thebenefitsof Tanzanians livingabroadWESTADIforpaymentof the $300justintransportingthe bodyof the deceasedburiedTanzania(RepatriationBenefit) and the benefitsoffree medical careforrelatives4memberliving inTanzania(HealthInsuranceBenefit). Contributions ofthese benefitsnowmade​​to the network(onlinepayment) through a system of4PAYthereby simplifyingandreducing the cost ofsharingthe transfer ofmoneytothe member.

   By Staff Reporter

  National Social Security Fund (NSSF) has called upon Tanzanians living abroad to register in the 2011 established Welfare Scheme for Tanzanians in Diaspora (WESTADI)


  The Scheme inaugurated by H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, the President of the United Republic of Tanzania during the 50 years anniversary of  Independence in Maryland, USA.


  The response from Diaspora has been less than ideal causing the scheme which intends to benefit the Tanzanian community abroad by providing Repatriation Benefit for the deceased member and Health Insurance Benefit to four (4) dependents of the underlying member living in Tanzania to stall.

  NSSF Chief, Public Relations and Customers Service, Ms Eunice Chiume talking to the media on the Diaspora scheme WESTADI at DITF grounds.


  The NSSF Chief, Public Relations and Customer Service, Ms Eunice Chiume stated" The main objective of the Scheme is to alleviate the high cost of transporting a Tanzanian deceased body for burial at homeland and to reduce the burden of cost medical cover for dependents of a Tanzanian living abroad".

  It has been witnessed through social media and other communication platforms that when a Tanzanian dies abroad it is a costly exercise to transport the body home; likewise Diaspora members are frequently faced with the challenge of sending money home for medical costs.

   With these two challenges NSSF designed WESTADI for the Tanzanians living overseas. Ms. Chiume also stated that since its inauguration the Scheme has improved its services by providing an online payment platform dubbed as NSSF 4 PAY which cuts significantly on time and cost of money transfers for members.  Members of WESTADI are obliged to pay a contribution of USD 300 per year per member for the cover. She urged all Tanzanians to respond to this key scheme for their peace of mind.


  Francis Dande 12:37 (2 hours ago) to me, Othman  Head ofRelationshipand Customer ServicesFund (NSSF), EuniceChiumespeaking toreportersabout thebenefitsof Tanzanians livingabroadWESTADIforpaymentof the $300justintransportingthe bodyof the deceasedburiedTanzania(RepatriationBenefit) and the benefitsoffree medical careforrelatives4memberliving inTanzania(HealthInsuranceBenefit). Contributions ofthese benefitsnowmade​​to the network(onlinepayment) through a system of4PAYthereby simplifyingandreducing the cost ofsharingthe transfer ofmoneytothe member.

  The NSSF Chief, Public Relations and Customer Service, Ms Eunice Chiume stated" The main objective of the Scheme is to alleviate the high cost of transporting a Tanzanian deceased body for burial at homeland and to reduce the burden of cost medical cover for dependents of a Tanzanian living abroad".  It has been witnessed through social media and other communication platforms that when a Tanzanian dies abroad it is a costly exercise to transport the body home; likewise Diaspora members are frequently faced with the challenge of sending money home for medical costs.


  0 0

  Timu ya Riadha ya Mkoa wa Tabora ikiwa kwenye mazoezi makali katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ikijiandaa kushiriki mashindano ya riadha taifa yanayotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki hii jijini Dar.

  Na Allan Ntana,Tabora

  TIMU ya Riadha ya mkoa wa Tabora ipo katika mazoezi makali kujiandaa na mashindano ya Riadha Taifa yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa wiki hii jijini Dar e s salaam.

  Katibu wa chama hicho Mkoa wa Tabora Salum Tarraddady, alisema jumla ya wanariadha 15 wa kike 9 na wa kiume 6 wapo kambini wakijifua kwenye uwanja wa Ali Hassan kujiandaa na mashindano hayo.

  Alisema vijana wake wapo katika hali nzuri na wana ari kubwa ya kufanya vizuri kwenye mashindano hayo huku akiahidi kuuletea sifa mkoa wa Tabora kwa kunyakua medali nyingi.

  “Vijana wetu wapo vizuri sana wakijiandaa na mashindano hayo ya kitaifa na wameahidi hawatawaangusha wananchi na wapenzi wa mchezo huo wa Tabora”Alisema.

  Alibainisha kwamba wanafanya mazoezi asubuhi, mchana na jioni kila siku katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Mratibu wa Riadha Mkoa wa Tabora, Allan Ntana, alisema wanamichezo wa Tabora katika mashindano hayo watashiriki mbio za mita 100, 200, 400, 800, 1,500, 3,000, 5,000 na 10,000 ikiwemo mbio za kupokezana vijiti (relay) huku michezo mingine ikiwa ni kuruka chini na juu, miruko mitatu, kurusha mkuki, kisahani na tufe.

  Ntana ambaye pia ni Afisa Habari wa Chama cha Riadha Mkoa wa Tabora, alisema vijana hao wamedhamiria kufanya vizuri zaidi tofauti na walivyofanya mwaka jana katika mashindano hayo kwani walirudi na medali zipatazo 10 zikiwemo dhahabu, fedha 3 na Shaba.

  Alitoa wito kwa uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Tabora na wadau wengine wa michezo kuisaidia timu hiyo kifedha ili kufanikisha gharama za kuipeleka jijini Dar es salaam kushiriki mashindano hayo.

  "Kila kitu kikienda kama tulivyopanga, tuna uhakika vijana wetu kutuwakilisha vema kama walivyotuwakilisha mwaka jana"Alisema. Mambo yakienda vizuri timu hiyo inatarajia kuondoka Mkoani Tabora Alhamisi wiki hii ikiwa na Viongozi wawili pamoja na wanamichezo 15.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akimpa maelezo, Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudentia Kabaka, wakati alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam Jumatatu Julai 7, 2014.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (Kulia), akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko huo, Mwanachama Mpya, Msanii maarufu nchini, Mrisho Mpoto (Katikati), kwenye maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam jana Jumatatu Julai 7, 2014. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi.
  Msanii maarufu nchini, Mrisho Mpoto, (Katikati), akionyesha kadi mpya ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mkuuwa Mfuko huo, Sdam Mayingu, (R), kwenye maqonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam jana. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi.

  0 0  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana Jumapili Julai 6, 2014 alitembelea kwa mara ya pili maonesho ya kimataifa ya bishara katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, baada ya ratiba yake kutokamilika katika ziara yake aliyoifanya siku ya Jumamosi kutokana na muda. Na kama ilivyo ada wananchi walifurahi kuwa naye karibu kama ambavyo yeye pia alifurahi kujumuika nao kwenye maonesho hayo ya kila mwaka. Watoto ndio waliokuwa wakimvutia zaidi Rais Kikwete ambapo kila mara alisimama na kuwasalimia. 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waliotembelea maonyesho ya Sabasaba.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiteta na watoto aliokutana nao Sabasaba.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaaga wananchi mara baada ya kujumuika nao pamoja kwenye Maonyesho ya Sabasaba jijini Dar. PICHA NA IKULU

  0 0


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiongozana na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Klaus Chilima kukagua gwaride maalum la makaribisho kwa Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Tanzania baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Lilongwe kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Malawi zilizofanyika Jumapili tarehe Julai 06, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Malawi, Saulos Klaus Chilima, wakifurahia ngoma za asili za Malawi, wakati wa mapokezi kwenye Uwanja wa Lilongwe, alipowasili kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Malawi zilizofanyika Jumapili tarehe Julai 06, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiagana na Rais wa Malawi, Profesa Arthur Peter Mutharika, baada ya shughuli za maadhimisho ya Sherehe ya miaka 50 ya uhuru wa Malawi kukamilika katika uwanja wa Civo, jana Julai 06, 2014. Nyuma yake ni Mama Asha Bilal.
  Wa pili (kushoto) ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Rais wa Malawi Profesa Arthur Mutharika akifuatiwa na mkewe, Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Asha Bilal na viongozi wengine wakifuatilia sala maalum ya kuombea nchi ya Malawi wakati wa sherehe za miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo zilizofanyika jana Jumapili Julai 06, 2014 katika uwanja wa Civo jijini Lilongwe, Malawi. Picha na OMR.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Jumapili Julai 06, 2014 ameiwakilisha Tanzania katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Malawi, sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Civo jijini Lilongwe.

  Katika sherehe hizo pamoja na Makamu wa Rais wa Tanzania, pia alihudhuria Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, Waziri Mkuu wa Msumbiji na viongozi mbalimbali waliowakilisha nchi kutoka Afrika.

  Sherehe hizo zilianza kwa ibada ya misa asubuhi na kisha kuhamia katika uwanja wa Civo mchana ambapo Rais wa Malawi Prof. Athur Peter Mutharika alikagua gwaride na kisha kuwasha Mwenye wa Jubilee ya miaka 50 na baadaye kulihutubia taifa.

  Akizungumza katika sherehe hizo, Rais Mutharika alisisitiza kuhusu umuhimu wananchi wa Malawi kuwa wamoja na akaeleza nia yake ya kujenga umoja kwa nchi zinazoizunguka Malawi pamoja na zile za Kusini mwa Afrika. Baada ya hotuba hiyo, sherehe hizo ziliendelea na mchezo wa soka baina ya timu ya taifa ya Malawi na Msumbiji.

  Malawi ilipata uhuru wake mwaka 1984 ikiongozwa na Rais wake wa kwanza Dkt. Kamuzu Banda hadi mwaka 1994. Baada ya mwaka huo alifuata Rais Dkt. Bakili Muluzi aliyetawala kuanzia mwaka 1994 hadi 2004.

  Baaada ya mwaka huo alifuata Rais Profesa Bingu wa Mutharika aliyetawala hadi mauti yalipomkuta mwaka 2012. Dkt. Joyce Banda aliyekuwa Makamu wa Rais wa Mutharika alichukua madaraka na kukaa hadi mwaka huu 2014 ambapo Malawi iliingia katika uchaguzi mkuu na kisha Rais Profesa Arthur Peter Mutharika aliposhinda uchaguzi huo na hivyo kuwa Rais wa nne wa Malawi.

  Katika sherehe hizo Mheshimiwa Makamu wa Rais pia alifuatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Mahadhi Juma Maalim na Mheshimiwa Makamu wa Rais amerejea nyumbani Tanzania Julai 07, 2014 tayari kuendelea na majukumu mengine ya kitaifa.

  Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais Julai 06, 2014 
  Lilongwe:
  Malawi

  0 0


older | 1 | .... | 496 | 497 | (Page 498) | 499 | 500 | .... | 3270 | newer