Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 495 | 496 | (Page 497) | 498 | 499 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akitoa heshima za mwisho kwenye Kanisa la Anlikana la Mt. Joseph, kumuaga Mzee Rugambwa ambaye ni baba wa mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Idara ya Ulaya na Marekani Bi. Felista Rugambwa Jumamosi Julai 5, 2014.  
  Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara John Haule na Mkurugenzi wa Idaho ya Ulaya na Marekani Balozi Joseph Sokoine, wakifuatilia misa iliyofanyika kwenye kanisa la Mt. Josefu, Dar es salaam Jumamosi tarehe 5 Julai 2014. 

  Felista Rugambwa (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na ndugu zake wakifuatilia misa.
  Familia ya Marehemu Mzee Rugambwa wakitoa shukrani.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule akitoa shukrani kwa niaba ya Wizara (pichani chini)

  0 0

  ZAIDI ya watu  60 wenye  uhitaji  wamewezeshwa na asasi  isiyo ya kiserikali ya Ladies Circle International katika mahitaji mbalimbali ikiwemo elimu, matibabu ,malazi pamoja na mitaji  .

  Hayo yalisemwa  na Rais wa asasi hiyo  hapa Tanzania ,Julieth Anthony wakati akizungumza katika uzinduzi rasmi wa asasi hiyo uliofanyika mjini hapa hivi karibuni.

  Alisema kuwa , asasi hiyo ilianza kufanya kazi hapa nchini mwaka 2012 ambapo ina jumla ya matawi matatu kwa nchi nzima ,huku asasi hiyo ikiwa kwenye nchi 37 hapa duniani.

  Alisema kuwa, lengo hasa la kuanzishwa kwa asasi hiyo ni kuhamasisha wanawake kuwa na moyo wa kujitolea kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii, kusaidia kuhimiza elimu na masomo ya sayansi kwa watoto wa kike wakiwemo yatima .

  Aidha lengo lingine ni kuboresha huduma ya mama na mtoto ili kuzuia kifo cha mama na mtoto ,na kuendeleza ujasirimali kwa vijana wanawake pamoja na kufadhili elimu kwa watoto yatima na kuwapatia mahitaji yao.

  Julieth alisema kuwa, kuwepo kwa asasi hiyo hapa nchini ambayo inaundwa na wanawake wenyewe kutasaidia sana kutatua changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii hususani zinazowakabili wanawake na watoto wa kike kwa ujumla.

  Naye Katibu Mkuu wa shirika la Love for all people Tanzania na Mratibu wa uanzishwaji wa asasi hiyo, Anthony Musani alisema kuwa,kuanzishwa kwa asasi hiyo hapa nchini ni baada ya kutembelea nchi za nje na kukuta wakiwa na asasi hiyo ambayo wamekuwa wakisaidia jamii zenye uhitaji ndipo alipoguswa na kuomba kuanzishwa hapa nchini .

  Musani alisema kuwa,watu wengi wana uwezo mkubwa sana wa kusaidia jamii zenye uhitaji ila changamoto kubwa inakuja katika kupata wawezeshwaji wa miradi ama vikundi vyao watakavyoanzisha.

   
  Aidha Musani aliwataka wadau mbalimbali wa maendeleo nchini kuhakikisha wanaitumia asasi hiyo ipasavyo kwa kusaidia jamii mbalimbali zenye uhitaji wakiwemo wajane, yatima na hata wenye mahitaji maalumu.

  Naye Mgeni rasmi katika uzinduzi huyo,Mbunge wa bunge maalumu la katiba, Yasmin Aloo aliunga mkono uanzishwaji wa asasi hiyo sambamba na kuanzisha mfuko wa kuwezesha asasi hiyo ili kuendeleza mipango yake ya kusaidia jamii.

  Aidha aliitaka asasi hiyo kutumia chombo hicho kwa malengo yaliyowekwa ikiwemo kuanzisha kituo cha afya kijiji cha ndani mkoani Dodoma na kuanzisha kituo cha ushauri nasaha na mafunzo ya ufundi kwa watoto wa mitaani waliotelekezwa baada ya kupata mimba katika umri mdogo mkoani Arusha.
  IMG-20140705-WA0001Rais wa asasi ya Ladies circle  kwa hapa Tanzania ,Julieth Anthony akizungumza katika uzinduzi rasmi wa asasi hiyo uliofanyika jijini Arusha katika hotel ya Naura springs.
   IMG-20140705-WA0002Janeth Julius ambaye ni mwenyekiti wa Ladies circle Tanzania.
  IMG-20140705-WA0005Mgeni rasmi katika uzinduzi huyo,Mbunge wa bunge maalumu la katiba, Yasmin Aloo.

  IMG-20140705-WA0004Picha ya pamoja

  0 0

   Na Mwandishi Maalum, New York
  Wakati mchakato wa maandalizi ya ajenda na malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya 2015 ukiendelea kushika kasi kwa mijadala mbalimbali inayoendelea hapa Umoja wa Mataifa. Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa upande wake imesisitiza kuwa pamoja na kukubaliana kwamba suala la utawala bora ni muhimu katika utekelezaji wa maendeleo na kupiga vita umaskini, hata hivyo eneo hilo halipashwi kuwa la upande mmoja. 
   “Hoja ya utawala bora ni muhimu sana, ni muhimu sana katika uboreshaji na utoaji wa huduma za afya, elimu na hata upatikanaji wa nishati endelevu kwa watu wetu.Lakini utawala bora hauwezi kuelekezwa au kuwa ni hoja ya nchi moja moja au kanda, bali ni hoja inayokwenda mbali zaidi, utawala bora unatuhusu sote hadi katika ngazi ya kimataifa sote tunapashwa kuwajibika katika eneo hili” akasema Balozi Tuvako Manongi.
  Moja ya eneo ambalo alilitolea mfano kama linalohitaji uwajibikaji wa pamoja inapokuja hoja ya utawala bora ni eneo la fedha haramu au kwa maneno mengine utoroshwaji wa fedha kutoka nchi zinazoendelea na kwenda kufichwa nje.
   Akisema ufumbuzi wa tatizo hilo ambalo kwa namna moja ama nyingine lina changia katika ukwamishaji wa maendeleo linahitaji ushirikiano wa pamoja. Muwakilishi huyo wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, ameyasema hayo mwisho wa mkutano wa siku nne wa Kilele wa Kisiasa ulioadaliwa na Baraza Kuu la Uchumi na Maendeleo la Umoja wa Mataifa ( ECOSOC) na kuwashirikisha nchi wanachama, wanazuoni , wawakilishi wa makundi maalum pamoja na Asasi zisizokuwa za kiserikali. 
  Mkutano huo wa siku nne, ulijadili mada mbalimbali lakini zote zikijikita katika mihimili mikuu mitatu inayosimamia maendeleo endelevu kama yalivyoainishwa katika Mkutano wa Kimataifa wa RIO+20 uliofanyika nchini Brazili. Maeneo hayo na ambayo yanatakiwa kutekelezwa sambamba ni maendeleo ya Kijamii, maendeleo ya Kiuchumi na Mazingira.
  Pamoja na kuzungumzia hoja ya utawala bora, Balozi Tuvako Manongi pia amesema majadiliano ya DOHA kuhusu fursa za biashara kwa nchi zinazoendelea yapashwa kukamilishwa.
   Kwa kile alichosema majadiliano ya DOHA ni kiungo muhimu katika utekelezaji wa Maendeleo endelevu baada ya 2015.
   “ Biashara ni muhimu sana katika maendeleo, na kwa sababu ya umuhimu wake, ujumbe wangu ungependa kusisitiza kwamba majadiliano ya DOHA yanapashwa kukamilishwa kama ilivyoahidiwa huko Bali, Indonesia. Kuhusu nafasi ya sekta binafsi katika kuchagiza maendeleo, Balozi Manongi alisema, akiongezea kuwa sekta binafsi inatakiwa kuwezeshwa kwa kuundiwa sera na mazingira ambayo itaiwezesha kukua , kuimarika na hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kuchangia utekelezaji wa maendeleo na kupanua wigo wa ajira. 
  Kuhusu mchakato mzima wa maandalizi ya agenda mpya za maendeleo na malengo yake, Muwakilishi huyo wa Tanzania, alitahadharisha kuwa, agenda hizo na malengo yake, ni lazima yazingatie hali halisi ya kila nchi, uwezo wake na utayari wa kuyatekeleza, kipi kinahitaji na kipi haikihitaji. Kwa kile alichosema nchi hazifanani ,ni tofauti na hata katika kiwango cha umaskini zinatofuatiana.
    Ujumbe  kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,  Bw. Ahmed Makame Haji wa Tume ya Mipango  na Bihindi Nassor Khatib Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha wakifuatilia majadiliano kuhusu maendeleo endelevu.
  Sehemu ya  washiriki wa  Mkutano wa Kilele wa Kisiasa wa siku nne  uliofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ukiwashirikisha wajumbe kutoka mataifa mbalimbali,  wanazuoni,wataalamu wa kada mbalimbali,  makundi maalum na Asasi zisizo za kiserikali.
  Muwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi akichangia wakati wa Mkutano wa siku nne wa Kilele wa Kisiasa uliokuwa ukijadili mada mbalimbali zinazohusiana na  masuala ya maendeleo endelevu. Mkutano huo  uliandaliwa na Baraza Kuu la  Uchumi na  Maendeleo la Umoja wa Mataifa 9 ECOSOC). katika ujumbe wake Balozi aliyeongoza ujumbe wa Tanzania katika  mkutano huo, aliikumbusha  jumuiya ya kimataifa kuwa   suala la utawala bora  ni jumuishi ambapo jumuiya  ya kimataifa pia inahusika nalo. Nyuma ya  Balozi ni Bi Amina Shaaban Mkurugenzi  Mtendaji,  Tume ya Mipango Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

  0 0

  IMG-20140704-WA0013Waziri wa Maliasili na utalii Mh. Lazaro Nyarandu akifungua rasmi mkutano wa 30 wa asasi ya wamiliki wa makampuni ya kusafirisha watalii TATO jijini Arusha hivi karibuni. 
  IMG-20140704-WA0009Wadau mbalimbali wa utalii wakisikiliza mada kwa umakini
  IMG-20140704-WA0004
  MAKAMPUNI ya kitalii hapa nchii yametakiwa kuutangaza kwa kiasi kikubwa utalii wa vivutio vyetu hapa nchini  ndani ya nchi pamoja na nje ya nchi ili kuwapa wanachi moyo wa kizalendo katika kujali vivutio walivyo navyo.
   
  Hayo yalisemwa juzi jijini Arusha na waziri wa Maliasili na utalii Mh. Lazaro Nyarandu wakati akifungua mkutano wa 30 wa asasi ya wamiliki wa makampuni ya kusafirisha watalii TATO ambapo  alisema kuwa hii ndio nafasi kubwa waliyokuwa nayo makampuni hayo makubwa ya uendeshaji shughuli za kitalii.
   
  Pamoja na hayo pia ameyataka makampuni hayo ya kitalii kuhakikisha yanaongeza kiasi kikubwa cha watalii wanaoingia hapa nchini ili kuingizia serekali fedha nyingi za kigeni na kuachana na kasumba iliyozoeleka ya kupandisha ada ya kiiingilio cha katika hifadhi zetu pamoj a na vivutio.
   
  Aidha kwa upande wa kutunza utalii wa Utamaduni Waziri wa maliasili mh. lazaro Nyarandu amezitaka kampuni hizo zinazohusika na kuwa shafirisha watalii katika mbuga kuhakisha wanawapitisha watalii katika sehemu za kiutamaduni kwa maana kama wanyama watalii wameshawaona na upande wa utamaduni nako kuna ulazima mkubwa sana.
   
  Pia Waziri wa maliasi na utalii alisema kuwa kwa sasa wizara yake imejipanga katika kutangaza utalii hapa nchini na sasa hivi wanaanza kutangaza katika shirika katika mashirika makubwa ya habari kiwemo Shirika la hababri la BBc pamoja na CCN.
   
  Naye Mwenyekiti wa TATO Bw. Willey Chambulo ametoa malalamiko yake kwa serekali na kuwakilisha kwa waziri wa Maliasili Mh. Lazaro Nyarandu kuhusiana na tatizo la hivi karibuni la kuwepo kwa mageti yasiyo rasmi katika baadhi ya hifadhi hapa nchini.
   
  Alisema kuwa, hii imetoke hivi karibuni katika mbuga ianayomilikiwa na TANAPA mnamo tarehe 01 mwezi huu na kudaiwa ongozeko la kodi amabalo wao hawakuwa  taarifa na hivyo kuwapa usumbufu kupelekewa kukamatwa kwa watalii waliokuwepo kuzuiliwa na kuwekwa chini ya Ulinzi hivyo kupelekea kurudisha nyuma hali ya utalii hapa nchini.
   
  Hata hivyo Waziri wa Maliasili Mh. lazaro Nyalandu  alijibu malalamiko hayo kwa kusema kuwa akiwa kama waziri mwenye dhamana ameshatoa maagizo kwa mamlaka zote za uhifadhi pamoja na mbuga kusitisha mara moja kusumbua watalii na kuwataka kutumia lugha nzuri katika kudai mapato.
   

  Mkutano huu wa TATO wa 30 unatarajiwa kupitia Mahesabu yaliyopita pamoja na kufanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wapya wa Asasi hiyo.(Pamela Mollel wa jamiiblog).


  0 0

  Mwenyekiti Mtendaji we shirika lisilo la kiserikali la TACIN, Bw. Anic Kashasha,(katikati) akiwa pamoja na uongozi wa juu wa Shirika la Maemdeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) akiwemo Mkurugenzi Mtendaji Bw. Yona Kilaghane (wa pili kulia) na Bibi Joyce Kisamo, Mkurugenzi wa Masoko na Uwekezaji, alipotembelea banda la shirika hilo kwenye viwanja vya Saba Saba jijini Dar ea Salaam, mapema leo. 
  TACIN ni washirika wa TPDC kwenye maandalizi ya Mtwara Festival ambayo ni mkakati wa mawasiliano wa kuhamasisha jamii ya Wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi, kizitambua fursa shirikishi zinazotokana na uongezekaji mkubwa wa uwekezaji katika mikoa hiyo kutokana na uchumi mkubwa wa gesi asilia ili wajiandae na kuzichangamkia.  Mtwara Festival 2014 itafanyika katika viwanja vya Nangwanda Sijaona, tarehe 16 na 17 Agosti, 2014 mjini Mtwara. 
  Mtwara Festival itakuwa ni mchanganyiko wa mawasiliano, michezo mbalimbali, maonyesho ya utalii, huduma na bidhaa. Washiriki wanakaribishwa kutoka sekta zote. Hayo yote yatasindikizwa na burudani kutoka kwa wasanii na vikundi mbalimbali.

  0 0

  Maelezo ya picha;Makamu mwenyekiti Uenezi CHADEMA kanda ya Magharibi Deogratius Liyunga akiwa amelazwa katika Hospital ya Mkoa wa Kigoma(Maweni)baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana(Picha na Editha Karlo).

  Na Editha Karlo, Kigoma.

  WATU wasiojulikana wamemvamia na kumpiga pamoja na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia vitu vyenye ncha kali Makamu Mwenyekiti wa uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kanda ya Magaharibi,Deogratius Liyunga na kupelekea kulazwa katika Hospita ya Mkoa wa Kigoma (Maweni).

  Tukio hilo limetokea jana majira ya  saa tano usiku katika eneo la Mlole Manispaa ya Kigoma Ujiji,wakati kiongozi huyo akiwa njiani kurudi nyumbani kwake akitokea eneo la Mwanga kuangalia mechi za  kombe la Dunia.

  Akiongea na mtandao huu wodini na alipolazwa juu ya tukio hilo,kiongozi huyo alisema kuwa alibakiza hatua 25 iliaweze kuingia nyumbani kwake ghafla walitokea watu wanne,mmoja alimvamia na kumkaba shingo huku wale wengine wakimshambulia kwa kisu,nyembe na ubao.

  Alisema mbali ya watu hao kumpiga na kumjeruhi lakini walimpora fedha kiasi cha shilingi 63,000 ingawa hawakufanikiwa kumpora simu yake ya mkononi iliyokuwa mfukoni.

  Baada ya watu hao waliomvamia kuondoka alifanya mawasiliano kwa watu wake wa karibu wakiwemo wanachama wa CHADEMA ambao walifika eneo la tukio na kumkimbiza Hospital kwaajili ya matibabu.

   Makamu Mwenyekiti alisema kuwa tukio hilo lililomkuta linahusiano mkubwa na masuala ya kisiasa kwani kabla ya tukio hilo amekuwa akipokea ujumbe mfupi wa maneno ya vitisho  kwenye simu yake ya mkononi kutoka kwa watu wanaodaiwa kuwa ni wananchama wa chama kipya cha ACT.

  Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma,Frasser Kashai alipopigiwa simu na mtandao huu kuthibitisha juu ya tukio hilo alisema hana taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo.

  ''Mimi hiyo taarifa sijaipata ofisini kwangu bado ndo nina isikia kutoka kwako ngoja nifuatilie nitakujulisha''alisema Kashai.

  0 0
  0 0

  Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akipokewa na Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC Tanzania, William Kallaghe na Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Dk. Mussa Assad (kulia) alipoalikwa kama mgeni rasmi katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NBC Tanzania, Dk. Mussa Assad (wa pili kushoto) wakichukua mlo wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu (wa pili kushoto) Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula Mfugale (kushoto), wafanyakazi na wateja wa benki hiyo wakijumuika pamoja katika hafla ya futari iliyoandaliwa na NBC kwa wateja wake jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakijumuika katika futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu ( kushoto) akiwaongoza baadhi ya wateja wa benki hiyo kushiriki futari waliyowaandalia jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wageni waalikwa wakifuturu katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya NBC ikiwa ni sehemu ya jitihada za benki hiyo katika kuwajali na kuwa karibu wateja wao.

  0 0

  Na John Gagarini, Kibaha

  WAKAZI wa Mitaa ya Vikawe, Vikawe Shuleni, Vikawe Bondeni na Vikawe wilayani Kibaha mkoani Pwani wamepatiwa ofa ya kutumia maji bure kwa miezi mitatu baada ya huduma hiyo kuanza kupatikana ambapo mitaa hiyo haikuwa na maji ya bomba tangu kuanzishwa kwake.

  Maji hayo tayari yameshaanza kutoka yanatokana na chanzo cha maji cha Ruvu Juu baada ya mitaa hiyo kutokuwa na maji kabisa ambapo awali walikuwa wakitumia maji ya visima na mto .

  Akizungumza na mabalozi, makatibu na viongozi wa Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Mkuza wilayani Kibaha wakati wa semina ya viongozi hao iliyofanyika jana mjini Kibaha, Mbunge wa Jimbo la Kibaha Silvestry Koka alisema kuwa maji yameanza kutoka kwenye mitaa hiyo hivi karibuni.

  “Wananchi hao wamepata ofa hiyo ya kutumia maji bure lakini baada ya miezi mitatu wataanza kuyalipia maji hayo baada ya kukosa maji ya bomba kwani kulikuwa hakuna maji kabisa na walikuwa wakichota maji kwenye visima na mto ambapo baadhi walipoteza maisha kwa kukamatwa na mamba walipokuwa wakichota maji mtoni,” alisema Koka.

  Katika hatua nyingine Koka alisema kuwa mji wa Kibaha utaondokana na tatizo kubwa la ukosefu wa maji baada ya mradi wa bomba kubwa kutoka chanzo cha mto Ruvu kuanza.

  Koka alisema kuwa kwa muda mrefu wa mji huo umekuwa ukikabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa maji huku wakati mwingine maji yakiwa yanatoka kwa mgao kutokana na chanzo kilichopo kutokuwa na uwezo wa kutoa maji ya kutosha.

  “Mradi huu kwa sasa uko kwenye hatua nzuri ambapo uchimbaji wa mtaro utaanza muda wowote kuanzia sasa kwani taratibu zingine zimekamilika na bomba litakalopitishwa litakuwa ni kubwa ambalo litapitisha maji mengi,” alisema Koka.

  Kwa upande wake katibu wa (CCM) Kibaha Mjini Abdala Mdimu alisema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo ni utekelezaji wa ilani ya chama ambayo ni ahadi kwa wananchi ili kuboresha utoaji huduma.

  Mdimu alisema kuwa chama kupitia kwa viongozi wake kitahakikisha ahadi zote zinatekelezwa kwa wakati uliopangwa ili wananchi waondokane na kero za huduma muhimu.

  0 0

  Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli(wa pili kulia), akigonanija chupa za bia ya Ndovu Special Malt na wadau wa bia hiyo wakati wa hafla ya kupongezana baada ya bia hiyo kutwaa tuzo ya ubora wa kimataifa(Ndovu High Quality Trophy) kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa hivi karibuni.Hafla ilifanyika jijini Mbeya hivi karibuni.
  Meneja wa Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli akizungumza na wadau wa bia hiyo wakati wa hafla ya kupongezana baada ya bia hiyo kutwaa tuzo ya ubora wa kimataifa(Ndovu High Quality Trophy) kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa hivi karibuni.Hafla ilifanyika jijini Mbeya mwishoni mwa wiki.
  Wadau wakipata Bia ya Ndovu Special Malt wakati wa hafla ya kupongezana baada ya bia hiyo kutwaa tuzo ya ubora wa kimataifa(Ndovu High Quality Trophy) kutoka kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Monde Selection nchini Ufaransa hivi karibuni.Hafla ilifanyika jijini Mbeya mwishoni mwa wiki.

  0 0  0 0  Ofisa Masoko wa Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania UTT, Waziri Ramadhani akijaza fomu ya mtoto aliyejiunga na Mfuko wa Watoto wakati wa Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (DITF), kwsenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Ofisa Masoko Mwandamizi wa UTT, Martha Mashiku.
  Mtoto aliyejiunga na Mfuko wa watoto akipewa zawadi.
  Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT, Daudi Mbaga akizungumza na wateja waliotaka kujua faida watakazopata baada ya kujiunga na Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji. 
   Ofisa Masoko wa UTT, Waziri Ramadhani akijaza fomu za kujiunga na Mfuko huo wa Dhamana ya Uwekezaji kwa mwanachama mpya.

  0 0

  Leo Jumapili Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (MB) amefanya ziara ya kushtukiza kukagua miradi ya maendeleo ujenzi wa barabara za Usagara - Kisesa yenye urefu wa kilomita 16 iliyopo mkoa wa Mwanza na barabara ya Makutano - Natta illiyopo mkoa wa Mara.
  Ukaguzi barabara ya Makutano - Natta (Mkoani Mara)
   Ukaguzi daraja la Kyarano (Wilayani Butiama)
  Ujenzi Daraja la Kyarano akiwa na Mh.Mkono
  Ukaguzi daraja la Nyashishi barabara ya Usagara - Kisesa, mkoani Mwanza

  0 0

  NDUGU MDAU MICHUZI TV SASA IPO HEWANI. 
  JIUNGE HARAKA UPATE MAMBO MOTOMTO!!
  TUNAANZIA  NA WATEJA WA VODACOM KWA SASA, AMBAO WANAKARIBISHWA KUFUATA HATUA HIZI TANO RAHISI:

  (i)  PIGA  *149*01#  
  (ii) KISHA CHAGUA NAMBA 6 SIMU.tv (MPYA) 
  (iii) HALAFU NENDA  NAMBA 2. Habari (BURE), 
  BAADA YA HAPO 
  (iv) CHAGUA NAMBA 5 Michuzi TV (BURE) 
  (v) KISHA CHAGUA NAMBA 1 KUJIUNGA...

  UNAKUWA UMESHAJISAJILI KWA HUDUMA HII MPYA. 
  LIBENEKE OYE!

  0 0

  1w
  Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na David Shambwe Kulia Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba (NHC) na Felix Maagi Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika hilo, Wakati alipowasili katika banda la (NHC) na kukagua, Kupata maelezo mbalimbali ya shughuli za miradi inayotekelezwa na shirika hilo. Wakati alipotembelea maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (TANTRADE) maarufu kama Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam. Yanayofikia tamati kesho jijini Dar es salaam , Katikati ni Dr. Abdallah Kigoda Waziri wa Viwanda na Biashara.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
  2w
  Rais Dr. Jakaya Kikwete akimsikiliza Bw. David Shambwe Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara Shirika la Nyumba (NHC) wa pili kutoka kulia ni Elias Msese Meneja Miliki Uendeshaji Makao Mkuu na Edith Ngunwe Afisa Mawasiliano NHC.
  4w
  Rais Dr. Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Shirika la Nyumba NHC kwenye maonyesho ya Sabasaba Viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere Barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam wanaoshuhudia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Dr. Abdalla Kigoda na Nalindwa Norbert mmoja wa maofisa wa Shirika la Nyumba NHC.
  5w
  Baadhi ya maofisa wa Shirika la Nyumba NHC wakiwahudumia watu mbalimbali waliotembelea banda lao ili kupata maelezo mbalimbali ya shughuli zinazofanywa na shirika hilo.
  6w
  Baadhi ya wakuu wa vitengo wa shirika hilo na maofisa kutoka kulia ni Yahya Charahani Meneja Uhusiano wa NHC , Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara (NHC) Bw. David Shambwe , Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha Bw. Felix Maagi , Benedict Kilimba Mkurugenzi wa Uendeshaji Miliki na Bw. Muungano Saguya Meneja wa Huduma za Jamii (NHC).
  7w
  Baadhi ya wakuu wa vitengo wa shirika hilo na maofisa kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara NHC Bw. David Shambwe , Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha Bw. Felix Maagi, Bw. Muungano Saguya Meneja wa Huduma za Jamii (NHC) na Yahya Charahani Meneja Uhusiano wa (NHC) wakisubiri kuwasili kwa Mh. Rais Dr. Jakaya Kikwete katika banda lao.
  3w
  Rais Dr. Jakaya Kikwete akiendelea kupata maelezo kutoka kwa Bw. David Shambwe Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara Shirika la Nyumba (NHC) wakati alipotembelea banda hilo.

  0 0  0 0

   Mtoto Zalex Joseph Kusaga akimlisha keki Baba yake Bwa.Joseph Kusaga ,mapema jioni ya leo mara baada ya wageni waalikwa mbalimbali kupata futari ya pamoja ndani Escape Two,Mbezi jijini Dar,na baadae ikafuatia hafla ndogo ya mtoto Zalex ambaye alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.
   Zalex akimlisha keki Mama yake Mdogo,Bi.Mariam Shamo
   Zalex akikata keki huku akiwa amezungukwa na watoto wenzake waliofika kushiriki nae kwenye hafla hiyo ya siku ya kuzaliwa.
   Mtoto Zalex Joseph Kusaga akimlisha keki Mama yake,Bi Juhayna Kusaga .
   Dada yake Zalex,Natalia akisaidia kukata keki
   Watoto wakiimba kwa pamoja.
   Mama yake Zalex,Bi Juhayna Kusaga akiwasha mishumaa.


  0 0

   Wadau wakiendelea kumiminika kwa wingi kwenye Banda la Benki Kuu lililopo kwenye Viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba).
   Mmoja wa Maafisa wa Benki Kuu akitoa maelezo kwa Wadau waliotembelea kwenye Banda hilo ili kufahamu maswala mbali mbali ya Kibenki,wakati wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
   Maafisa wa Benki Kuu wakiendelea kutoa somo wa watu mbali mbali waliofika kwenye banda hilo,huku moja wa somo ni lile la kuweza kutambua na kutofautisha noti bandia na noti halali.
   Benki kuu yatoa sarafu ya jero (mia tano) kama ionekanavyo pichani,ila bado haijaingia mtaani mpaka hapo itakapotangazwa kuanza kwa matumizi yake.
   Ndani ya Banda hilo kuna sehemu ya kubadili noti chakavu na ukapata mpya. 
   Picha za Magavana wa Benki Kuu toka wa kwanza mpaka wa sasa.
   Wadau wakiendelea kupatia taarifa za kibenki. 
   Sehemu ya Mapokezi.
   Taswira ya ndani katika muonekano wa jicho la samaki.
  Timu nzima ya wafanyakazi wa Benki Kuu waliopo kwenye Maonyesho ya Sabasaba wakiwa kwenye picha ya pamoja.

  0 0  0 0

  CHAMA CHA MAPINDUZI TAWI LA UINGEREZA KINAPENDA KUWATANGAZIA WANACHAMA NA WAPENZI WOTE WA CCM KUTOKA PANDE ZOTE ZA UINGEREZA KWAMBA KUTAKUWA NA MKUTANO MKUU WA TAWI TAREHE 30.08.2014.

  KATIKA MKUTANO HUO PIA KUTAFANYIKA UCHAGUZI WA MWENYEKITI MPYA WA TAWI LA CCM UINGEREZA ILI KUJAZA NAFASI ILIYOACHWA WAZI NA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA TAWI HILI TOKA KUANZISHWA KWAKE NDUGU MAINA OWINO ANAYENG’ATUKA KATIKA NAFASI HIYO.

  WANACHAMA WOTE WENYE SIFA MNAKARIBISHWA KUCHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA NAFASI HIYO YA MWENYEKITI WA TAWI KAMA AMBAVYO TAYARI MMETANGAZIWA KATIKA MASHINA YENU NA KWAMBA FOMU HIZO ZINAPATIKANA KWA MAOMBI YA UJUMBE WA BARUA PEPE KUTUMWA KWA KATIBU WA ITIKADI, SIASA NA UENEZI/KAIMU KATIBU WA TAWI NDUGU LEYBAB MDEGELA KWA ANUANI leybabmdegela@ccmuk.org. NA KURUDISHWA KWA KATIBU WA SHINA LAKO. MWISHO WA KURUDISHA FOMU NI TAREHE 12/07/2014

  WANACHAMA NA WAPENZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI UINGEREZA MNAHIMIZWA NA KUKUMBUSHWA KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA MKUTANO HUO MAALUMU AMBAO UTALENGA KULETA MABADIRIKO YA KWELI NA YENYE DIRA KATIKA TAWI LETU.

  “KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!”

  Imetolewa na Idara ya Itikadi Siasa na Uenezi
  Chama Cha Mapinduzi Tawi La Uingereza.

older | 1 | .... | 495 | 496 | (Page 497) | 498 | 499 | .... | 3283 | newer