Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 492 | 493 | (Page 494) | 495 | 496 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Kutoka kulia waliosimama. 1. Abdallah Shomari (Tandamti no. 3 )2. Nassoro kalumbanya (simba str.) 3. Said Chamwenyewe (Aggrey/Congo str.) 4. Mtoro Ally (Muhonda str.) 5. John Rupia (Misheni kota) 6. Julius Nyerere( Pugu Sekondari ) 7. Said Chaurembo (Congo/ Mkunguni str.) 8. Jumbe Tambaza( Upanga ) 9. Sheikh Suleiman Takadir (Mafia /Swahili) 10. Dossa Aziz ( Mbaruku /Somali kipande ) 11. Mshume Kiyate (Tandamti) 12. Juma Sultan (Kitchwele karibu na kanisa dogo ) 13. Maalim Shubeti (Masasi/ Likoma) 14. Rajab Simba  ( kiungani str.) 15. Waziri Mtonga (Kilosa no. 18 , Ilala) 16. Mwinjuma Mwinyikambi ( Mwananyamala) 17. Maxi Mbwana ( Aggrey /Kongo ) 18. Usia Omari (Sungwi ,Kisarawe) 19. Sheh Issa Nasir ( Bagamoyo)

  0 0

   Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mheshimia Omar Mjenga akiwa na wanadiplomasia wenzake  kwenye salaam hizo za mtawala wa Umm Al Quwain. Wa tano kushoto mwa Mhe. Mjenga ni mtawala wa Falme ya UMM AL Quwain.


  0 0

   Malkia wa Swaziland Mheshimwa Nomsa Matsebula akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Ndugu Nurdin Babu mara baada ya helikopta iliyomchukua kutua kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Nyamisati huko wilayani Rufiji ambako alikwenda kutembelea Shule ya Wamanakayama inayomilikiwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA. Tarehe 2.7.2014. Kulia ni Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete.

   Mke wa Mfalme Mswati III wa Swaziland Malkia Nomsa Matsebula akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Wamanakayama Dkt. Ramadhan Dau mara baada ya mgeni huyo kuwasili huko Nyamisati
   Malkia wa Swaziland Nomsa Matsebula akiwa amefuatana na mwenyeji wa Mama Salma Kikwete akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Nyamisati waliofika kumlaki mara baada ya helikopta iliyomleta kutua kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Nyamisati
   alkia wa Swaziland Nomsa Matsebula akionyeshwa namna wanavyotumia I-pad katika baadhi ya masomo yao hapo shuleni Wamanakayama na mwanafuzi Rehema Shao aneyesoma kidato cha pili huko mwanafunzi Asia Idd (kushoto) akisubiri zamu yake.
   Mwanafunzi Assia Idd akimwonyesha Malkia Matsebula kutoka Swaziland namna ya kutumia i-pad kwenye masomo ya sayansi na hesabu wakati Malkia huyo alipotembele Shule ya Sekondari ya Wamanakayama inayomilikiwa na Taasisi ya WAMA inayoongozwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.


  0 0

   Hon. Bernard K. Membe, Minister for Foreign Affairs and International Cooperation giving country's position during the joint SADC/ICGLR Ministerial Meeting held in Luanda, Angola July 2, 2014.
  The second joint ministerial meeting of the Southern Africa Development Cooperation (SADC) and the International Conference on the Great Lakes Region (ICGLR) countries was concluded in Luanda July 2, 2014 with concrete steps to finding sustainable peace in the region.

  The well attended meeting by all country members represented by foreign and defence ministers deliberated heavily on a single agenda of voluntarily disarmament of the Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR).


  Hon. Bernard Membe, Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, led the Tanzania delegation whereby the Tanzania Defence Minister was represented by the Tanzanian Army Chief of Staff Lt. Gen. Samuel Ndomba.  

  FDLR a politico-military organization whose combatants are exclusively freedom fighters originally from Rwanda settled in DRC, wrote an appeal letter to SADC secretariat expressing their readiness to surrender and hand over their weaponry to African relevant authorities. The letter also requested assistance from the organ to oversee the process of Disarm, Demobilize, Repatriate, Resettle and Re-integrate (DDRRR) in accordance to the directives of other neighbouring countries including Tanzania.

  Apart from accepting the said letter, SADC member states welcomed the FDLR willingly surrender and adherence to the DDRRR process. They however strongly suggested other stakeholders such as AU, UN and ICGLR to oversee the process while Rwanda and DRC were urged to take part in the process.  

  In a joint session, delegates discussed the provisional six-month time frame given to the FDLR to complete the DDRRR process as proposed by the technical experts meeting prior to ministerial meeting. Democratic Republic of Congo (DRC) supported by majority countries including Tanzania insisted that the allocated timeframe was right while Rwanda claimed the past experiences proved 3 months to be enough.


  However the chair and the host of the said meeting, Angola, ruled out for the six months proposal but should be revised by the third month to gauge progress.
  It is the expectation of all countries in attendance that the DDRRR process is implemented within the given time frame with full engagement of both DRC and Rwanda.


  The ICGLR/SADC member countries also urged international community and neighbouring countries to join hands with DRC and Rwanda in this historical peace - making process.  

  The third meeting of this nature is expected to take place within the next three months.


  Issued by:


  Government Communication Unit;


  Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation


  0 0


  These are the world’s most elite military teams. They’re highly trained, best equipped and well-prepared fighting units specializing in surgical military operations, from ending a hostage situation swiftly to stealthily eliminating top terrorists.For more and source CLICK HERE
  MONUSCO FIB commander Brig Gen. James Mwakibolwa receives  members of  an advance team of the intervention brigade with a special mandate to neutralize and disarm armed groups in e#Eastern Democratic Republic of the Congo, DRC, as it arrives in Goma.
   members of  an advance team of the intervention brigade with a special mandate to neutralize and disarm armed groups in e#Eastern Democratic Republic of the Congo, DRC, as it arrives in Goma.
  members of  an advance team of the intervention brigade with a special mandate to neutralize and disarm armed groups in e#Eastern Democratic Republic of the Congo, DRC, as it arrives in Goma. Photo: MONUSCO

  0 0

  Mwanahabari wa Reuters nchini Bw. Fumbuka Ng’wanakilala (aliyebeba msalaba), pamoja na wadogo zake, Lugendo  (kushoto) na Manyanda (kulia), wakiwaongoza waombolezaji waliobeba jeneza lenye mwili wa Baba yao, Marehemu Mwl. Nkwabi Ng’wanakilala baada ya kuwasili nyumbani kwao Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam Julai 01 mwaka huu, kwa ajili mazishi. 
  Mwl. Ng’wanakilala, ambaye alikuwa Mhadhiri katika Idara ya Habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), jijini Mwanza alifariki Juni 27, katika Hospitali ya Bugando baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo na tumbo. PICHA ZOTE/JOHN BADI
  Mzee Nkwabi Ng'wanakilala enzi za uhai wake.
  Ndugu, jamaa na waombolezaji wakilitelemsha jeneza lenye mwili wa Mwl. Ng’wanakilala kutoka kwenye gari baada ya kuwasili nyumbani Kibamba.
  Sehemu ya waombolezaji wakiwa msibani Kibamba.
  Mkurugenzi Msaidizi  wa Idara ya Habari MAELEZO  BW. Raphael Hokororo  (kati) akiwa na wadau wa habari waliokuwepo mazishini

  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino alieambatana na Mkewe Princess Akishino  walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo July 3, 2014.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Mkurugenzi wa Idara ya Asia Bw. Mbelwa Kairuki kwa Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe Princess Akishino waliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo July 3, 2014.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazunzumzo na Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe Princess Akishino Ikulu jijini Dar es salaam leo July 3, 2014. walioketi kulia ni Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akifuatiwa na Balozi wa Tanzaia nchini Japan Mhe Salome Sijaona
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapa historia ya Ikulu  Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe Princess Akishino  mbele ya lango kuu ya Ikulu hiyo ya Dar es salaam.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwatembeza Ikulu Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe Princess Akishino jijini Dar es salaam leo July 3, 2014.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe  Princess Akishino walipomtembelea jijini Dar es salaam leo July 3, 2014. Wengine ni WaZiri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe (wa pili kulia) , Naibu WaZiri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt Mahadhi Juma Maalim, balozi wa Tanzania nchini japan Mhe Salome Sijaona (kushoto) na balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe Masaki Okada (wa pili kushoto).
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwaonesha Simba waliotengenezwa Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino na Mkewe Princess Akishino walipomtembelea jijini Dar es salaam leo July 3, 2014.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya leo, Alhamisi, Julai 3, 2014, amemkaribisha Ikulu, Dar Es Salaam, Mwana wa Mfalme wa Japan, Prince Akishino pamoja na mkewe Princess Akishino.

  Mwana Mfamle huyo ambaye anatembelea Tanzania, amewasili Ikulu kiasi cha saa nne asubuhi na kufanya mazungumzo ya zaidi ya nusu saa na Mheshimiwa Rais Kikwete.

  Katika mazungumzo yao, Rais Kikwete amesema kuwa Japan ni mshirika mkubwa na muhimu sana wa maendeleo ya Tanzania. “Tunathamini sana mchango wenu katika maendeleo ya Tanzania na tunaendelea kuwashukuru sana. Ukizunguka nchini mwetu utaona kwa macho yako miradi mingi na mikubwa ambayo imejengwa ama inajengwa kwa msaada wa Japan.”

  Rais kikwete ameongeza:“Pamoja na ushirikiano huu. Bado tunaamini kuwa Japan inaweza kusaidia zaidi Tanzania hasa kwa kushawishi makampuni yake kuwekeza katika sekta binafsi. Ukipita mitaa ya Dar es Salaam, magari tisa kati ya 10 ni ya Kijapan. Ukiingia katika maduka ya vyombo vya elektroniki  - televisheni, kompyuta, camera, karibu kila kitu kinatoka Japan. Hali hii inathibitisha kuwa bidhaa vya Japan zina soko kubwa na zinaweza kuzalishwa hata hapa nchini na makampuni binafsi.”

  Rais Kikwete pia ameitaka Japan kuangalia jinsi gani inavyoweza kusaidia ongezeko la watalii kutoka Japan kuja kutembelea Tanzania kwa kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka huko hadi Tanzania na nchi nyingine za Afrika.

  “Wataalii wengi kutoka Japan wanashindwa kuja Afrika kwa sababu hakuna shirika hata moja la ndege la Japan ambalo lina safari za kuja Afrika, hata Afrika Kusini hakuna. Hii ndiyo maana hatuoni watalii wengine kutoka nchi za kusini mashariki mwa Bara la Asia kutembelea vivutio vyetu vya utalii,”amesema Rais Kikwete na kuongeza:

  “Kama kuna jambo halionekani sasa katika uhusiano wa Tanzania na Japan ni uwekezaji katika sekta binafsi. Hili ndilo jambo tunaloliomba.”


  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  IKULU

  DAR ES SALAAM

  3 Julai, 2014  0 0

  Kwa wale wanaohitaji kujiunga na elimu ya juu nchini Ujerumani.
   Kuanzia B.A,Bsc,M.A mpaka Phd Watanzania tumieni nafasi hizi,
  chuo kinapokea wanafunzi hata kwa vijana wa Kitanzania walio maliza kidato cha sita wana nafasi ya kujiunga na chuo hiki,maelezo zaidi,
  Tafadhali wasiliana na anuani hii hapa chini:

   International Student Office
   Carl von Ossietzky Universität Oldenburg
   Ammerländer Heerstr. 114-118,
   26129 Oldenburg
   Germany
  fax    : +49(0)441 7982461
   Pia fomu za maombi zinapatikana online katika link hii chini:

  0 0

  Yule Mdau wa Sweden aliyeandika katika blog hii hapo tarehe 8 septemba 2010 aliyeahidi kujenga studio ya kisasa kwa Watanzania, sasa iko tayari huko Sweden. Bado ni kwa Watanzania. 
  Mabadiliko ya sehemu ya kuijenga studio hii ni kutokana na hali halisi kuwa Sweden kuna Wataalamu wa aina zote tutakaowahitaji katika kazi zetu kadri wateja wetu watakavyotaka na vifaa muhimu katika kazi zinapatika haraka na kwa uhakika.
   Katika Project hii kuna mambo mengi sana yanayotakiwa kufanyika ili kukidhi kile kilichokusudiwa kwa walengwa (Wasanii wa muziki na filamu) ili kila mmoja akidhi kiu yake. Kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu, kampuni hii inaweza kuja kuwa ni kitengo cha utafiti katika maswala ya sanaa za nchi zinazoendelea na zilizoendelea. 
  Nimetafutwa na kuitwa kwa mahojiano. Swali lilikuwa, nadhani ni kwanini kuna utofauti mkubwa kati ya nchi zinazoendelea na zilizoendelea katika kusambaa na kununuliwa kwa muziki na filamu? Nimeshatoa maoni na ushauri wangu nionavyo kwa Tanzania. Nitajibiwa baada ya miezi kadhaa maana waamuzi sio walionihoji, bali ni watu wengine katika kamati zao za utafiti (EU). 
  Tutangulize maombi yetu kwa Mwenyezi Mungu. Tunaweza kupata utatuzi wa kitaalamu katika swala hili. Tembeleeni www.msolab.se tovuti ya Kampuni yetu MSOL na jitahidini na ninyi wenzangu kui-like MSOL ili kuonyesha kuwa inaungwa mkono na wengi ili tufikiriwe kuwa katika utafiti wao. Lakini mimi maelezo yangu yote nimetilia mkazo zaidi kwa nchi ninayoifahamu vizuri Tanzania. Jamani tutangulize uzalendo. Tanzania kwanza. Kwa mambo yooooooote BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Recorded by Vijimambo on  July 29,  2011 in Washington DC 

  0 0

  waandishi+wa+habari
   Na Boniface Wambura, Dar es salaam
  Taasisi moja kutoka Uingereza inayohusika na kampeni dhidi ya upangaji matokeo kwenye mpira wa miguu (match fixing) itafanya uwasilishaji (presentation) juu ya suala hilo kwa waandishi wa habari za michezo nchini.
   Uwasilishaji huo utafanyika kesho (Julai 5 mwaka huu) saa 11 jioni kwenye hoteli ya Accomondia iliyopo Barabara ya Nkrumah jijini Dar es Salaam.
   Wataalamu hao wa kupiga vita upangaji matokeo ambao pia wataelezea jinsi matokeo yanavyopangwa, jana (Julai 3 mwaka huu) walifanya uwasilishaji wao kwa wachezaji na benchi la ufundi la timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys).
   Taasisi hiyo yenye kibali kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) katika utoaji elimu ya kubaini upangaji matokeo, vilevile inatoa elimu juu ya athari zinazopatikana kutokana na upangaji matokeo.
  Wakati huo huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeendesha mafunzo ya matumizi ya tiketi za elektroniki kwa wadau wa mpira wa miguu mkoani Mbeya.
   Mafunzo hayo yamefanyika jana na leo (Julai 4 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Sokoine, na kushirikisha wasimamizi wa mechi, viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA) na makatibu na maofisa habari wa klabu za Tanzania Prisons na Mbeya City. 
  Wengine walioshiriki mafunzo hayo ni Meneja wa Uwanja wa Sokoine na msaidizi wake, wasimamizi wa milangoni (stewards) na waandishi wa habari wa mkoani Mbeya. 
  Mafunzo hayo yanahitimishwa kesho (Julai 5 mwaka huu) kwa mechi kati ya Tanzania Prisons na Mbeya City itakayochezwa Uwanja wa Sokoine kuanzia saa 10 kamili jioni. Kiingilio ni sh. 3,000, na tiketi zilianza kuuzwa Julai Mosi mwaka huu kupitia M-Pesa, CRDB Simbanking na maduka ya Fahari Huduma.

  0 0

  Familia ya Bibi Mary Singano wa Sahare Tanga, inapenda kumshukuru Mungu kwa baraka na rehema zake katika kipindi cha msiba wa Marehemu Lt. Col (Rtd) Maurice Noel Singano kilichotokea tarehe 31/05/2014 Chennai, India . 
   Tunawashukuru Wizara ya Afya kwa msaada Wakati wa ugonjwa ,tunatoa shukrani za kipekee kwa Mganga Mkuu wa Serikali Dr Donan Mmbando,Dr Goloka Muambata wa Tanzania nchini india na wote waliojitoa kuokoa maisha ya mpendwa wetu . 
   Tunamshukuru Dr. Jayashree ,Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Apollo Chennai kwa matibabu katika kipindi cha ugonjwa Tunawashukuru father Maurusi, Jerome na father Francis kwa huduma za kiroho, Watanzania waliokwepo Apollo katika kipindi Chote Cha ugonjwa. Tunawashukuru Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Mathias Mlumba ,Jumuiya ya Mt Mathias Mtume wa Mikocheni DSM, Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Martha DSM na Mathias Mulumba Tanga. 
  Baba Askofu jimbo la Tanga .Jumuiya ya Mt Yuda Thadei Sahare, Wawata na Walei Tanga. Tunamshukuru Mkurugenzi wa St. Christina Bwana Gabriel Kessy, Mwenyekiti wa bodi ,Walimu,wafanyakazi na wanafunzi.Menejimenti na watumishi wa MSD,TFDA na Airtel kwa ushirikiano na kutufariji katika kipindi hiki kigumu. Jeshi la wananchi wa Tanzania kwa huduma ya mazishi. Tunawashukuru Ndugu jamaa,majirani na marafiki walioshirikiana nasi katika kipindi chote cha ugonjwa na msiba.
  Tumefarijika sana kwa upendo mlio tuonyesha na Mungu awabariki sana. Kutakua na mkesha tarehe 25/07/2014 utakaohitimishwa na misa siku ya tarehe 26/07/2014 nyumbani kwa Bibi Mary Singano- Sahare Tanga. 
  Wote mnakaribishwa “Raha ya Milele umpee ee Bwana na Mwanga wa milele umwangazie,apumzike kwa AMANI” “Nimepigana Vita vilivyo vizuri,nimeimaliza safari, imani nimeilinda” Timotheo 4:7

  The Family of Mrs Mary Singano of Sahare Tanga, would like to thank God for his blessings and mercies during the illness of her beloved husband Lt.  Col(Rtd) Maurice Noel Singano and ultimate demise  on 31/05/2014 in Chennai, India. 
  We would like to thank Dr Jayashree ,all Doctors and nurses of Apollo Speciality in Chennai who gave their time and efforts to save his life.
   We thank the Ministry of Health for their support during our beloved sickness and his passing away, we extend special thanks to the Government Chief Medical Officer Dr Donan Mmbando, Dr. Goloka attaché in India and all those who went out of their way to support us .
   We thank father Maurusi, father Jerome and father Francis for their spiritual support and guidance, all the Tanzanians who were at Apollo during his sickness.  We also thank St. Martha Parish Priest in Dar es salaam and St. Mathias Mulumba of Sahare Tanga Parish Priest. The Bishop of Diocese of  Tanga , Communities of St Mathias Apostle of Mikocheni Dar es salaam and St. Juda Thadei of Sahare, Wawata and Walei  Diocese of Tanga.
  We thanks the Managing Director of St Christina Mr.  Gabriel Kessy, Board Chairman and its members ,teachers, workers and students.
  We also thank the management and Staff of MSD,TFDA and Airtel for their condolences and  support during this difficult time
  We thank the Tanzania Peoples Defense Forces for their support and burial services.
  To friends, relatives and neighbors your presence eased our pain and for that we are thankful. May God bless you all 
  There will be a Thanks giving program on Friday evening 25/07/2014 followed by a Thanks Giving Mass at 8.00am and Lunch on Saturday the 26/07/2014 at Mrs  Mary Singanos’ residence at Sahare Tanga. You are all welcome.

  “May His Soul Rest in Eternal Peace, Amen”

  “You have fought a good fight, finished the race, kept the faith” Timothy 4:7

  0 0

   Mwandishi wa habari wa Shirika la Utangangazi la Tanzania (TBC) Fatma Matulanga akiwa mwenye furaha baada ya kuhitimu shahada ya uzamili katika uandishi wa Habari za Biashara Kimataifa (Global Business Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Tsinghua, kilichopo Beijing nchini China leo Ijumaa. Bi Matulanga ni miongoni mwa wahitimu 20 kutoka nchi 16 duniani, akiwa wa pekee kutoka bara la Africa katika darasa lake
   Fatma Matulanga akiwa mwenye furaha baada ya kuhitimu shahada ya uzamili katika uandishi wa Habari za Biashara Kimataifa (Global Business Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Tsinghua, kilichopo Beijing nchini China
   Fatma Matulanga akipokea cheti cha kuhitimu shahada ya uzamili katika uandishi wa Habari za Biashara Kimataifa (Global Business Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Tsinghua, kilichopo Beijing nchini China
  Fatma Matulanga na wenzie wakirusha kofia juu baada ya kuhitimu shahada ya uzamili katika uandishi wa Habari za Biashara Kimataifa (Global Business Journalism) kutoka Chuo Kikuu cha Tsinghua, kilichopo Beijing nchini China

  0 0
 • 07/04/14--10:11: Anatafutwa na Ndugu zake
 • Jina: Dickson Samwel Mbiling'i
  Umri miaka 27
  Kabila: Mkinga
  Dini: Mkristo
  Maeneo anayopenda kutembelea:
  Iringa, Mbeya, Dar es Salaam na Bagamoyo.

  Mtajwa hapo juu anatafutwa na ndugu zake. Kwa mara ya mwisho alionekana nyumbani kwake Mwananyamala Mchangani jijini Dar es Salaam siku ya Jumatano ya  Julai 2, 2014.

  Wajihi wake ni maji ya kunde mrefu kiasi mwembamba wa wastani. Msamaria mwema yeyote mwenye taarifa zake au atakayemuona popote anaombwa kuwasiliana na ndugu zake kwa namba:-

  0754 477226-Moses Mbiling'i
  0754 301095-Adrew Mwilingu
  0757 000014-Bartholomew Mbiling'i
  0784 890389-Ahadi Kakore.

  0 0

   Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi,Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Dkt. Pindi Chana akifungua rasmi mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara mjini Dodoma leo.
   Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Sera - Utumishi ambaye pia ni Katibu wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara Bw.Mathias Kabunduguru akimkaribisha Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi,Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mh.Pindi Chana (hayupo pichani) kufungua mkutano wa Baraza hilo lilozinduliwa rasmi mjini Dodoma leo.
   Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi,Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe.Pindi Chana (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza hilo mjini Dodoma leo.
   Mkurugenzi Msaidizi - Utumishi Bi. Hilda Kabisa akiwasilisha mada baada ya ufunguzi wa mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara mjini Dodoma leo
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi katika Utumishi wa Umma Tanzania Bara wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi,Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe.Pindi Chana (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza hilo mjini Dodoma leo.

  0 0

   Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Idara ya Uwindaji wa Kitalii,Cites na Utalii wa Picha Kanda ya Kaskazini ,wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo ,Lazaro Nyalandu leo kwenye ziara yake mkoani Arusha.
   Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akisalimiana na Askari Wanyama Pori  jijini Arusha leo.
   Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu(wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa  Idara ya Uwindaji wa Kitalii,Cites na Utalii wa Picha Kanda ya Kaskazini.
   Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akifurahia Keki zilizoandaliwa katika Chuo cha Taifa cha Utalii Arusha.
  Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu(wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa  Chuo cha Taifa cha Utalii kilichopo Sakina jijini Arusha na  Idara ya Uwindaji wa Kitalii,Cites na Utalii wa Picha Kanda ya Kaskazini.

  0 0

   

  Kutoka Arusha taarifa zinasema msako mkali unaendelea kufuatia shambulio la bomu la mkono alilotupiwa  Sheikh wa msikiti wa Qiblatan Sood Ally Sood (37) uliopo eneo la Kilombero jijini Arusha  wakati akila daku.
  Kwa mujibu wa taarifa hiyo imedaiwa kuwa Sheikh huyo amejeruhiwa sehemu mbalimbali ikiwemo miguu yake yote miwili sehemu za mapajani pamoja na Kifuani na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote miwili.

  Mbali na Sheikh huyo pia kuna mtu mwingine aliyekuwa nyumbani kwake hapo aliyetajwa kwa jina la Muhaji Kifea (38) ambaye ni mkazi wa Dar es salaam naye amejeruhiwa na wote wamelazwa katika hospital ya mkoa Mount Meru kwa ajili ya matibabu.


  Akizungumza hospitalini hapo sheikh Sood amesema tukio hilo lilitokea nyumbani kwake eneo la majengo ya chini ,usiku wa kuamkia leo majira ya saa 5 wakati yeye pamoja na mgeni wake walikuwa wakila chakula sebuleni Amesema alishangaa kusikia mlio mkubwa ulioambatana na vyuma mbalimbali vilivyokuwa vikiruka hewani ,ambapo bomu hilo linaelezwa kuwa ni guruneti lililorushwa kupitia dirishani baada ya watu wasiofahamika kufanikiwa kuvunja kioo cha dirisha la chumbani katika nyumba hiyo. 

  Ameongeza kuwa wahusika wanafahamika maana walishawahi kumtishia kupitia waraka wa maandishi pamoja na kumfyatulia risasi.

   Amesema kuwa siku tatu kabla ta tukio hilo alikoswakoswa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika wakati akitoka msikitini na kutoa taarifa katika kituo kikuu cha polisi jijiji hapa juu ya tukio hilo. 

  Sheikh Sood, ambaye ni kiongozi Alswasun kanda ya kaskazini, inasemekana amekuwa akitofautiana na waamini wenzake kutokana na msimamo wake mkali wa kutokukubaliana na makundi ya kigaidi yanayojiita jihadi yanayotokana na vijana wenye msimamo mkali.

   Inahofiwa waliofanya udhalimu wanahusika na vikundi vya ugaidi na kwamba  wanasakwa hivi sasa na vyombo vya ulinzi na usalama. Tutaendelea kuwapasha taarifa zaidi kwa kadri zitavyopatikana.


  0 0

  Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya banda lao,kwenye Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba).
  Afisa Masoko wa Shirika la Posta Tanzania,Happy Iteba (kushoto) akitoa maelezo kwa wateja waliotembelea banda la Posta kwenye maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
  Maafisa Masoko wa Shirika la Posta Tanzania Happy Iteba na James Musyaji wakiwahudumia wateja waliotembelea banda hilo.

  0 0
 • 07/04/14--11:00: INTRODUCING Madee's "Sheeda"

older | 1 | .... | 492 | 493 | (Page 494) | 495 | 496 | .... | 3270 | newer