Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

banda la Wizara ya Fedha.lavutia wengi maonesho ya sabasaba

$
0
0
Mwananchi (kulia) akiwauliza maswali wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania(kushoto)  juu ya huduma mbalimbali za Benki hiyo leo jijini Dar es salam wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Tasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA )Mzee Boma(wa pili kulia) akisaini Kitabu cha wageni leo jijini Dar es salaam wakati yeye na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) DKT. Joseph Kihanda (kulia) walipotembelea  Banda la Wizara ya Fedha kwenye maonesho ya  38 ya Kimataifa ya Biashara. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano wa TIA Lilian Mpanju(kushoto) na Mhasibu wa TIA George Kadutu.
 Mhasibu kutoka Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) George Kadutu akiwaelimisha wanafunzi wa Shule za Sekondari mbalimbali leo jijini Dar es salaam juu ya shughuli za Taasisi wakati wa maonesho ya  38 ya Kimataifa ya Biashara.
  Watumishi wa kutoka Mfuko wa Pesheni kwa Watumishi wa Umma (kushoto) wakitoa elimu kwa wananchi mbalimbali waliotembelea banda la Wizara ya Fedha leo jijini Dar es salaam juu ya shughuli za Mfuko huo wakati wa maonesho ya  38 ya Kimataifa ya Biashara.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) DKT. Joseph Kihanda (kulia) akibadilishana mawazo na Wafanyakazi wa TIA kwenye Banda la Wizara ya Fedha leo wakati alipotembelea maonesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara. Wengine ni mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa TIA Mzee Boma(wa pili kulia) , Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano Lilian Mpanju(kushoto) na Mhasibu wa TIA George Kadutu.
PICHA NA GCU- WIZARA YA FEDHA


RAIS KAGAME WA RWANDA AZUNGUMZIA UHUSIANO WA NCHI YAKE NA TANZANIA, ASEMA NI MATAIFA NDUGU NA YATAENDELEA KUWA HIVYO

$
0
0
Kwa hisani ya Idhaa ya Kiswahili DW

majambazi yashambulia kwa risasi karandinga la magereza jijijni dar es salaam leo, shuhuda asimulia kilichotokea

$
0
0
Kwa mujibu wa mdau aliyeshuhudia tukio lote hilo live anatupasha:
Ishu ilikuwa hivi, kuna gari ndogo ilikuwa inatokea njia ya Kawe kwenda Shopperz au ilikuwa inaelekea mjini kwa kutumia hii njia ya Mwai Kibaki road. Hiyo gari ndogo ilipofika Maeneo ya Million Hairs Salon jirani kabisa na Regency park hotel ikakwama kwenye foleni ndefu sana. Nyuma ya hiyo gari ndogo kulikuwa na magari mengine yameunga hiyo foleni.
Gari ya magereza ikiwa na wafungwa ilikuwa ni kama ya sita au ya nne nyuma ya hiyo gari ndogo mara ghafla tukasikia puuu! puuu! pooo! poooo! poooo!  kama risasi 6 au 8 hivi - kumbe ile gari ndogo inavyosemekana ilikuwa imebeba kiasi kikubwa cha pesa na hakukuwa na escort yoyote. 
Majambazi wakiwa kwenye pikipiki waliifuata ile gari pale kwenye foleni wakamuamrisha yule jamaa atoe fedha na jamaa akaachia mkwanja. 
 Sasa lile gari la magereza kwa vile liko juu sana kama gorofa askari wake wakaiona hiyo inshu live. Sasa ile wanajiandaa tu na mabunduki yao majambazi nayo wakashitukia mchezo na wakaanza wao kuwashambulia kwa risasi wale askari magereza. Askari magereza ile wanajiandaa kujibu mapigo tu majambazi haooooo wakawasha pikipiki na kuondoka kwa speed ya 220. Kiukweli ilitisha na watu waoga kama mimi nilikimbilia kujificha sehemu. Yaani ilikuwa kama Movie (ya ulaya, sio Bongo Movie).
  Sehemu ya kioo cha pembeni cha karandinga la Jeshi la Magereza baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi  leo katika barabara ya Mwai Kibaki jirani na Mayfair Plaza jijini Dar es salaam. 
 Wapita njia  wakiwa wamelizungika karandinga la Magereza baada ya kushambuliwa. 
Foleni ilikuwa kali mahali hapo kwa masaa kadhaa kabla karandinga halijaondolewa.

BREKING NYUUZZZZZ: WATANGAZAJI DJ FETTY NA ADAM MCHOMVU WA CLOUDS FM WASIKIKA WAKIZICHAPA LIVE REDIONI

$
0
0
Redio ya Clouds FM 88.5 ya Mikocheni jijini Dar es salaam leo imetoa ya mwaka wakati DJ Fetty na Dj Adam Mchomvu waliposikika wakizichapa live wakati kipindi kipo hewani. Juhudi za kuupata uongozi wa Clouds FM zinaendelea kutaka kujua mustakabali wa watangazaji hao maarufu nchini. Hebu sikiliza mambo yalivyokuwa. Bofya mshale mwekundu hapo..

CHEF ISSA ATOA SOMO LA KUBANIKA MKATE KWA KUTUMIA KUNI KWA VIJANA WA SCOUT UGHAIBUNI

$
0
0
Mkate uliotayari kwa kuliwa ooohhh asikwambie mtu saafi sana!
 Chef Issa anashukuru Allah kupata  bahati ya kualikwa na chama cha scout kwenda kuwafundisha vijana mbinu za mapishi wakiwa porini. Dah! waliipenda na kufagilia sana walitengeneza mkate wa kubanika kwa kutumia mti na moto wa kuni.
Kundi la vijana wa scout na uongozi wao hapa ni baada ya kuwasha moto tukisubiri upungue na kuni zote zishike moto tuanze kubanika mkate.
Chef Issa (kulia) akiwa na vijana wa scout
Huu ndio mkate wenyewe ukiwa unaelekea kuiva
Baada ya moto kupungua na magogo kuwaka kama mkaa hapo sasa safi unaweza endelea kubanika mkate wako hakikisha fimbo ni ndefu ili usiungue mikono. Mtembelee Chef Issa BOFYA HAPA


JK aomboleza kifo cha Nkwabi Ng’wanakilala

$
0
0
Nkwabi-Ng’wanakilala
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha mwandishi wa habari mkongwe na mhadhiri mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Mt. Augustine, Bwana Nkwabi Ng’wanakilala.
Bwana Ng’wanakilala ambaye alifariki dunia mwishoni mwa wiki kwenye Hospitali ya Rufani ya Bugando mjini Mwanza kwa matatizo ya figo na tumbo, alizikwa  Jumatatu, Julai Mosi, 2014, nyumbani kwake Kibamba, Dar es Salaam.
Katika salamu ambazo amemtumia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mt. Augustine, Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, Rais Kikwete amesema: “Kifo hiki kimelinyang’anya taifa letu mmoja wa wanataaluma wa habari mahiri sana na mtumishi hodari wa umma ambaye alithibitisha sifa hizo katika nafasi zote alizozishikilia. Tasnia ya habari imepoteza kiongozi hodari.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Alithibitisha sifa hizo kwenye nafasi ya Ukurugenzi wa Idara ya Habari, kwenye Ukurugenzi wa Redio Tanzania Dar Es Salaam (RTD) na kwenye Ukurugenzi wa Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA). 

Aidha, marehemu alithibitisha vipaji vyake siyo kwenye uandishi wa habari tu bali hata kwenye uandishi wa vitabu, utafiti na uhadhiri, shughuli ambayo ameifanya hadi mauti yalipomfika.”
“Naungana na wanafamilia, wanajumuia ya Chuo Kikuu cha Mt. Augustine na wanataaluma wa tasnia yote ya habari nchini kuomboleza kifo cha Bwana Ng’wanakilala. Aidha, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke pema roho ya Marehemu Nkwabi Ng’wanakilala. Amina.”

IJUE HISTORIA YA GLOBU YA JAMII

CRDB WAFUNGUA HUDUMA ZA BENKI BABATI

$
0
0
Na Woinde Shizza,Manyara

Wananchi wa Mkoa wa Manyara, wametakiwa kutumia fursa ya kuwepo kwa huduma ya benki ya CRDB Tawi la Babati, kwa kujiwekea akiba na kuchukua mikopo kwa lengo la kujinufaisha kiuchumi na kuongeza pato la Taifa.

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo aliyasema hayo wakati wa zoezi la benki ya CRDB tawi la Babati, lilipoanza kutoa huduma ya fedha kwa wateja wake na yeye kuwa mtu wa kwanza kuweka fedha kwenye tawi hilo.

Mbwilo aliwataka wananchi wa mkoa huo kufungua akaunti za fedha kwenye benki tofauti ikiwemo CRDB, NMB, NBC, Posta na Exim, ambazo zipo mjini Babati, kuliko kuweka kwenye benki moja na kuitegemea yenyewe pekee.

"Waswahili wanasema usiweke mayai yote kwenye kapu moja, hivyo tutumie fursa hii kwa kuweka akiba katika benki tofauti tofauti, hapa unaweka sh200, kule sh300, pengine sh100 ndiyo nidhamu ya fedha ilivyo," alisema Mbwilo.

Hata hivyo, alisema Waziri Mkuu Mizengo Pinda au Rais Jakaya Kikwete mmoja wao ndiye atakayekuja kulizindua rasmi Tawi hilo na alitoa wito kwa benki hiyo ya CRDB kuanzisha matawi mengine kwenye wilaya za mkoa wa Manyara.

"Siku za nyuma tulikuwa tunaona gari la benki linakuwa hapa kwa wiki mara moja ila sasa mmeweza kuweka Tawi hapa Babati, sambaeni na sehemu nyingine huko wilayani msogeze huduma hizi karibu na jamii," alisema Mbwilo.

Naye, Meneja wa CRDB Tawi la Babati Ronald Paul aliwataka wafanyabiashara, watumishi, wakulima na wafugaji wa mkoa huo kutumia fursa ya kuwepo kwa benki hiyo kwa ajili ya kupata huduma za kifedha ikiwemo kuweka akiba.

"Jamii itumie nafasi hii kwa kuweka na kutoa fedha na pia hapa Babati ni kwenye barabara kuu hata viongozi wengi wanapita kuelekea Dodoma, hivyo watatumia fursa hii ya kuwepo kwa tawi letu kupata huduma ya fedha," alisema Paul.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa mkoa huo, wakiwa kwenye Tawi la Babati la Benki ya CRDB ambalo jana lilianza kutoa huduma kwa wateja wake, wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Babati Khalid Mandia, akifuatiwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Manyara, Ndeng'aso Ndekubali na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Omary Chambo na Meneja wa Benk ya CRDB Kanda ya kaskazini Chiku Issa.
Meneja wa Benki CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara, Ronald Paul akizungumza na waandishi wa habari ambapo kwa mara ya kwanza Tawi hilo.
Afisa wa Benki ya CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara akitoa maelezo ya kibeki kwa baadhi ya Askari wa Jeshi la Wanzanchi waliofika kwenye Benki hiyo.


UFUNGUZI WA WARSHA YA MAFUNZO YA MAFUNDI MAJOKOFU NA VIYOYOZI JIJINI ARUSHA LEO

$
0
0
Pichani kulia ni Mkurugenzi msaidizi Idara ya Mazingira kutoka ofisi ya makamu wa Rais Bi Magdalena Mtenga, akifafanua jambo katika ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya mafundi majokofu na viyoyozi kuhusu teknolojia mbadala za upozaji na rafiki kwa tabaka la ozoni mjini Arusha leo.
 Sehemu ya washiriki katika warsha ya Mafunzo ya mafundi majokofu na viyoyozi mjini Arusha kuhusu Teknolojia Mbadala za upozaaji  na rafiki kwa tabaka la ozoni.
 Aliyesimama, Mkurugenzi wa idara ya Mazingira Ofisi ya makamu wa Rais dkt. Julius Ningu akizungumza  machache kwa wanawarsha na wataalam katika warsha ya mafunzo kuhusu teknolojia mbadala za upoozaji na rafiki kwatabaka la ozoni mjini Arusha leo.. Aliyekaa ni Mkuu wa Chuo cha VETA Moshi. Bw.Daniel Komba(Picha zote na Evelyn Mkokoi)

KALAMU FOUNDATION YAPONGEZWA KUTEMBELEA VIJIJINI MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

$
0
0
Mjumbe wa Taasisi ya Misaada ya Kibinaadam Ya Kalamu Education Foundation Mh. Asha Mtwangi (Kushoto) ambae ni Mjumbe wa Bunge la Katiba Akimsikiliza Kwa Makini Bint Simba wa Kituo Cha Jaribu Orphans Center akielezea Maisha ya Kila Siku ya watoto wa Kituo Hicho wa Jamii ya Kijiji Cha Jaribu Rufiji - Pwani. Alisema "laiti taasisi mbali mbali zingetembelea huku vijijini kama mlivyofanya nyinyi ambako hali zetu ni ngumu zaidi, wananchi wengi tungefarijika sana hasa kipindi hiki cha mwezi Mtukufu".
Baadhi ya wanakamati wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation wakiteta jambo na Bint Simba ambaye ni Bibi Mleze wa Kituo Cha watoto yatima Kijiji cha Jaribu. Bint Simba Alishukuru sana kwa Taasisi ya Kalamu Foundation kwa kuwajali wananchi wa vijijini kipindi hiki Cha Mwanzo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Baadhi ya Watoto Mayatima wanaoishi katika Kijiji Cha Jaribu - Rufiji walipopiga picha ya Pamoja na Wajumbe wa Taasisi ya Kalamu Foundation baada ya Kukabidhiwa vyakula Mbali Mbali na Magodoro 25 kwa ajiri ya Kituo cha watoto yatima Kijijini Hapo.
Wajumbe wa Taasisi ya kijamii ya Kalamu Education Foundation walipokuwa wakimkabidhi Binti Simba Vifaa Mbali Mbali pamoja na Nguo, Sabuni, Mashuka na Viatu kwa ajiri ya Kituo Cha Jaribu Orphans Center wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani kwa ajiri ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

VODACOM NA CRDB BENKI WAZINDUA HUDUMA MPYA YA M-PESA

$
0
0
Mkurugenzi wa Huduma Mbadala za Benki wa CRDB Joseph Witts akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya kutoa pesa kwenye M-pesa kupitia ATM za benki bila kuhitaji kuwa na kadi wala akaunti ya beki hiyo. Wengine pichani ni Ofisa Mkuu wa Biashara Mtandao wa Vodacom Jacques Voogt na Meneje Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Ofisa Mkuu wa wa Biashara Mtandao wa Vodacom Jacque Voogt akittumia ATM ya Benki ya CRDB kutoa pesa kwenye akaunti ya M-pesa katika simu yake ya mkononi muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa huduma hiyo mpya. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma Mbadala za Benki wa CRDB Joseph Witts. Huduma hiyo humuwezesah mteja yoyote wa M- pesa kutumia ATM za benki hiyo kuchukua pesa bila kujali kama ni mteja wa CRDB.
Mkurugenzi wa Huduma Mbadala za Benki wa CRDB Joseph Witts akitumia ATM ya Benki ya CRDB kutoa pesa kwenye akaunti ya M-pesa katika simu yake ya mkononi muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa huduma hiyo mpya. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Biashara Mtandao wa Vodacom Jacques Voogt. Huduma hiyo humuwezesha mteja yoyote wa M-pesa kutumia ATM za CRDB popote nchini kutoa pesa hata kama si mteja wa benki hiyo.
Ofisa Mkuu wa wa Biashara Mtandao wa Vodacom Jacques Voogt na Mkurugenzi wa Huduma Mbadala za Benki wa CRDB Joseph Witts (katikati wenye suti nyeusi) wakipongezana baada ya kuzindua huduma m-pya ya kutoa pesa kwenye M-pesa kupitia ATM za CRDB nchi nzima. Wengine pichani ni wafanyakazi wa Vodacom na wa Benki ya CRDB. Huduma hiyo huweza kutumiwa na mteja yeyote wa M-pesa hata kama si mteja wa benki hiyo.

WANAHABARI WAPATIWA ELIMU YA MFUMO UTAKAOTUMIKA KUBORESHA DAFTARI LA KUDUMU LA KUPIGA KURA.

$
0
0
 Mjumbe wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu John Mkwawa  wakati akisoma taarifa wakati   akifungua mkutano wa siku moja na waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa unaohusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza na matumizi ya Teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa. 
 Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wa NEC kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza na matumizi ya Teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mkoa wa Iringa. 
Mkurugenzi wa Idara ya habari na Elimu kwa Wapiga Kura Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Ruth Mashama akizungumza kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza na matumizi ya Teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za mkuu wa mkoa wa Iringa.

OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YAKAGUA MRADI WA MAKAA YA MAWE NGAKA

$
0
0
Viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na wale wa NDC wakipata maelezo kuhusu mradi wa makaa ya mawe Ngaka kutoka kwa Mtaalam wa Kudhibiti Ubora (Quality Control Superintendent) Bw. Boscow R. Mabena.
Timu kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na NDC wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kikundi cha Wanawake cha Mbalawala, Bi. Joyce Haule juu ya matumizi ya makaa ya mawe majumbani. Makaa hayo hutumika majumbani kwa kutumia majiko maalum baada ya kubadilishwa kitaalam na kuwa rafiki kwa matumizi ya majumbani. Mbalawala kinajihusisha na shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni jitihada za kumkwamua mwanamke kiuchumi.
Majiko maalum yanayotumia mkaa uliotokana na makaa ya mawe kwa ajili ya kupikia majumbani.
Mtaalam wa Kudhibiti Ubora, Bw. Boscow R. Mabena akitoa maelezo namna ambavyo Coal Briquett Machine (Pichani) hutumika kubadili makaa ya mawe kutoka hali yake ya mwanzo baada ya kuchimbwa na kutengenezwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Picha na: Thomas Nyindo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (ORTM), Dkt. Philip I. Mpango, (wa tano kutoka kushoto) akikagua Mradi wa Makaa ya Mawe Ngaka. Wengine ni viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na Shirika la Maendeleo la Taifa – NDC pamoja na wataalam wa kampuni ya TANCOAL inayojishughulisha na uchimbaji wa makaa ya mawe. 
Viongozi na Maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na NDC wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Kampuni ya TANCOAL ndani ya mgodi wa makaa ya mawe. Kampuni ya TANCOAL ndiyo inayohusika nauchimbaji wa makaa ya mawe katika Mradi wa Mkaa ya Mawe Ngaka.

NSSF YABEBA TUZO YA HUDUMA BORA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

$
0
0
Makamu wa Pili wa Raisi, Balozi Seif Idd, akimkabidhi tuzo ya ushindi wa  kwanza katika sekta ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (DITF), katika Vinwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mh. Balozi Ally Seif akipata ufafanuzi kutoka kwa  Meneja Miradi Mhandisi John Msemo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kuhusu Mradi wa DEGE ECO VILLAGE. Kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda alipotembelea Banda la NSSF katika maonyesho ya kimataifa ya 38 (Sabasaba) katika viwanja vya Mwalimu Jilius Nyerere. Wa pili kulia ni Kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii-NSSF.
 Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Janeth Mbene akipata maelezo kuhusu mpango wa uchangiaji wa wakulima kwa wanachama walio katika sekta isiyo rasmi kutoka kwa Meneja Kiongozi Uhusiano na Huduma Kwa Wateja Mrs Eunice Chiume wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) alipotembelea Banda la NSSF katika maonyesho ya 38 ya kimataifa ya Sabasaba. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Crescentius Magori.
Mh. Waziri mkuu Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusu mradi wa DEGE ECO VILLAGE  kutoka kwa Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi P. J. Msemo alopotembelea Banda la NSSF katika maonyesho ya Sabasaba. Kulia ni Waziri wa viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda. 
Wafanyakazi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakifurahia tuzo za ushindi wa jumla katika sekta ya Hifadhi ya Jamii na Bima katika maonyesho ya kimataifa ya 38 (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YANG’ARA KWENYE MAONESHO YA SABA SABA

$
0
0
Mjiolojia Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Mwara Shoo akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini kwenye maonesho ya kimataifa ya Saba Saba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa Utaalam Elekezi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Advera Mwijage akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda hilo.
Wataalam kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mstaafu wa Shirika hilo Bw. Gray Mwakalukwa mara alipotembelea banda hilo.


Mh. Pinda atembelea Banda la PSPF kwenye Maonyesho ya Sabasaba

$
0
0
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, (Kushoto), akipatiwa maelezo na Mkurugenzi wa ukaguzi wa ndani, wa PSPF, Goddfrey Ngonyani, wakati alipotembelea banda la mfuko huo kwenye maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Mawasiliano, Mahusiano na Masoko, Costantina Martin.
Mkazi huyu wa jijini Dar es Salaam, akipatiwa huduma na mtafiti mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Maagi Thomas, kwenye banda la Mfuko huo lililoko kwenye jengo la wizara ya fedha kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere kunakofanyika maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, Jumatano Julai 2, 2014.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (Kushoto), akizungumza na Waandishi wa habari kutoka Uingereza, Oliver Moss(Katikati), na Carla de Campos, walipotembelea banda la PSPF kwenye maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, Jumatato Julai 2, 2014.
Msanii wa majigambo, Mrisho Mpoto, a.k.a Mjomba, (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa ndani, Goddfrey Ngonyani,watatu kushoto), Meneja Mawasiliano, Masoko na Uenezi, Costantina Martin, (Watatu kulia), kwenye banda la Mfuko huo kwenye maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, Jumatano, Julai 2, 2014.

HARVARD CLUB OF WASHINGTON WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Harvard Club Of Washington, Bi. Caren A. Pauley akiutambulisha umoja wa wanafunzi waliowahi soma Chuo Kikuu cha Harvard waishio Washinton Metro Area kwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula siku ya Jumatano July 2, 2014 umoja huo ulipotembelea Ubalozi wa Tanzania kwa ajili ya kukutana na jumuiya mbalimbali za Kitanzania na Taasisi zinazoshughulika na maswala ya Tanzania na kuweza kuongea pamoja kufahamiana na kubadilishana mawazo.
Afisa Immaculata Diyamett anayeshughulikia maswala ya Utalii kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, akiwakaribisha wageni wote Tanzania House na kuwaambia wajisikie wapo nyumbani.
Rais wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo Kikuu cha Harvard (Harvard Club Of Washington, Bi Yi-Fun Hsueh ambaye pia ni mmoja ya waratibu akiongea machache na kumshukuru Balozi Liberata Mulamula kwa kukubali kuwakaribisha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kuja kukutana na Jumuiya za Kitanzania na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kujuana na kubadilishana mawazo.
Balozi wa Tanzania nchini Marekanai Mhe. Liberata Mulamula akiwakaribisha Umoja wa wanafunzi waliosoma Chuo Kikuu Cha Harvard waishio Washinton Metro Area kikundi kinachobeba jina la  Harvard Club of Washington kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na kuwaelezea kuhusu Tanzania na vivutio vyake chini ni maelezo aliyokuwa akitoa Mhe. Balozi MSIKILIZE

MWANAMFALME AKISHINO WA JAPAN AWASILI NCHINI KWA ZIARA RASMI

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akizungumza na Mwanamfalme Akishino wa Japan mara baada ya Mwanamfalme huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza ziara yake ya siku tano hapa nchini.
Mhe. Mahadhi na Mwanamfalme Akishino wa Japan wakiendelea na mazungumzo huku Mke wa Mwanamfalme huyo (kulia) pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mhe. Salome Sijaona (kushoto) na Balozi wa Japan hapa nchini, Mhe.  Masaki Okada wakisikiliza.
Mazungumzo yakiendelea.

mwaliko wa futari kwa jumuiya ya watanzania waishio UAE

Musley Al Rawahi apania kufanya mambo makubwa Simba

$
0
0
Musley Al Rawahi akisisitiza jambo.
Mjumbe mpya wa kamati ya utendaji wa klabu ya Simba, Musley Al Rawahi, amesema kuwa silaha kubwa ya kufikia maendeleo katika klabu hiyo ni umoja na kufanya kazi kwa kujituma na uadilifu mkubwa.
Musley ambaye mwaka jana alimzawadia gari kiungo wa Simba SC, Ramadhani “Messi” Singano kwa kucheza vizuri katika ligi kuu ya Tanzania Bara,  alisema hayo mara baada ya kutangazwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu hiyo na pia kuwa miongozi mwa wajumbe wanaounda kamati ngumu na nyeti ya usajili wa klabu hiyo.
Alisema kuwa anashukuru kuteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji na usajili wa klabu hiyo na anaamini uteuzi wake umetokana na jinsi alivyokuwa mstari wa mbele kutafuta maendeleo ya klabu hiyo.
Kwa mujibu wa Musley, Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva hajafanya makosa katika uteuzi wa wajumbe wa kamati ya utendaji, usajili, mashindano na soka la vijana kwani hizo ndizo nguzo za ustawi wa klabu na kufanikisha mambo mengi ya maendeleo.
“Tukisajili wachezaji wazuri, ndiyo watatuletea ushindi ndani ya klabu na hivyo kamati ya mashindano kufanyakazi zake kwa ufanisi mkubwa, hivyo natoa wito kwa wajumbe wateule, tufanye kazi kwa bidii na kuleta maendeleo makubwa klabuni na kuendelea kumpa sifa waliotuteua kushika nadhifa hizo,” alisema Musley.
Alisema kuwa yeye ana historia kubwa sana katika klabu hiyo na amekuwa mwanachama tangu akiwa mdogo na hiyo ilitokana na mapenzi makubwa ya baba yake kwa Simba.
“Mzee wangu amekuwa mwanachama wa klabu hii kwa miaka mingi, mimi nimefuata nyayo zake na mpaka sasa nimekuwa na klabu hii kwa miaka mingi, nina uchungu nayo sana, ninaahidi kufanya kazi kwa bidii ili kufikia lengo,” alisema Musley.
Alisema kuwa changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni matarajio ya wanachama na mashabiki wa Simba kwani wanachotaka wao ni ushindi na kutwaa ubingwa.
“Wana-Simba wanataka ubingwa, hakuna kingine ambacho wanakitaka, tunahitaji kusajili wachezaji wazuri, wenye kuleta ufanisi na kutufikisha kule tunakotaka,” alisema.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images