Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

Bi Rusi Manfred ndiye Bibi Bomba 2014

$
0
0
Mashindano ya kumtafuta Bibi bomba mwaka 2014 yalifanyika Mikocheni katika ukumbi wa Saadani Parking national hotel jijini Dar es salaam , mgeni rasmi alikuwa Bi.Anna Kilango. Aliyefanikiwa kuibuka mshindi usiku huo ni Bi Rusi Manfred ambaye alijipatia zawadi ya shilingi milioni kumi za kitanzania na kiwanja chenye thamani ya shilingi Milioni tano.
Bi Rusi akikabidhiwa zawadi yake


Mashabiki wakimshangilia Mshindi


Bi Rusi akiwa ameshikiria Hati ya kiwanja kama
moja ya zawadi yake


Mkurugenzi wa Tanzania Women's Bank (TWB) Bi Margareth Chacha  akitoa pongezi zake. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOFANYA MAKAMUZI CALIFORNIA JUMAMOSI

$
0
0

 Diamond Platnumz mwanamuziki wa bongo fleva asieshikika sasa hivi ambaye ni maarufu zaidi kwenye wimbo wake wa my number one aliyemshirikisha mwanamuziki mwingine wa Nigeria anayefanya vizuri sasa hivi Davido akifanya show kali jijini Los Angeles, California siku ya Jumamosi June 28, 2014 ikiwa pia akijiandaa kwenye BET award'14 inayofanyika leo jijini humo wimbo wake wa my number one aliyeshirikiana na Davido umekuwa nominated kwenye katagoli ya international collaboration. Mgeni wa heshima alikua Mhe. Ahmed Issa ambaye ni Balozi wa Heshima wa Tanzania California.
Mashabiki wa Diamond wakipagawa kwenye showa ya Diamond Platnumz iliyofanyika Los Angeles, California nchini Marekani.
 Diamond Platnumz akiwachengua mashabiki waliohudhuria showa yake ya California wakati 
 akishambulia jukwaa na kuwapagawisha mashabiki wake wa California nchini Marekani.
 Diamond Platnumz akishambulia jukwaa.
mashabiki wakipagawa kwa show ya kukata na shoka toka kwa rais wa wasafi Diamond Platnumz
Picha na Abdul Majid mwakilishi wa Vijimambo Los Angeles California.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

KAGASHEKI CUP 2014 MJINI BUKOBA LEO - KASHAI 3 vs BAKOBA 0,

$
0
0
Na Faustine Ruta, Bukoba
Michuano ya Kagasheki Cup 2014 imeendelea tena leo kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini kwa siku ya pili na kushuhudia mahasimu wawili Mmoja akimliza mwenzake bao 3-0.
Mtanange wa leo hii Jumapili ulizikutanisha timu mbili matata kwenye hii ligi za Kashai na Bakoba FC na kushuhudia Timu ya Bakoba ikifungwa bao 3-0 bao zilizofungwa kipindi cha kwanza mbili na kipindi cha pili moja.
Timu ya Kashai FC walianza kuifunga timu ya Bakoba bao la kwanza katika dakika ya 8 bao likifungwa na Joha Johansen. 
Bao la pili lilifungwa na Msengi Gerard katika dakika ya 38 kipindi cha kwanza na kufanya bao kuwa 2-0 dhidi ya mahasimu wao Bakoba ambao mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika walikuwa hawajapata kitu.
Kipindi cha pili licha ya timu zote mbili kukamiana kwa sana timu ya Bakoba ilipata nafasi kama tatu lakini haikuweza kuifunga timu ya Kashai na hatimaye Kashai kupata bao lao la tatu katika dakika ya 60 kipindi cha pili bao lililotiwa nyavuni na Mchezaji wa Kashai FC Shamte Odilo na Kipute kumalizika kwa dakika 90 Kashai ikiibuka kwa bao 3-0. 
Michuano hii itaendelea tena kesho Jumatatu na kutakuwa na Mitanange miwili wakwanza utachezwa saa nane kati ya Nshambya FC ikiumana na timu ya Kibeta Fc saa 8:00 mchana na mtanange wa saa 10:00 ni baina ya Kagondo Fc na Buhembe Fc.

Dakika 90 zimemalizika waamuzi wanatoka uwanjani ...
Kashai 3 vs Bakoba 0.


mbunge wa kalenga mhe godfrey mgimwa atembelea wapiga kura jimboni kwa baiskeli

$
0
0
Mbunge  wa  jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akiwa katika usafiri wa Baiskeli akienda kutembelea wapiga kura wake kata ya Ifunda eneo la Kivalali 
Wananchi wa Kivalali kata ya Ifunda  wakijiandaa kupeana mikono na mbunge Mgimwa 
Mbunge Mgimwa akisalimiana na wanakikundi cha burudani Kivalali kata ya Ifunda

Nike yaongoza mtanange wa makampuni ya vifaa vya michezo katika kombe la dunia Brazil

$
0
0
 Na Sultani Kipingo 
wa Globu ya Jamii

Uwezo wa kifedha wa Nike unaipaisha kampuni hiyo katika vita vya Kombe la Dunia 2014 kwa kuiongoza kampuni ya Adidas kwa mabao 4 katika awamu ya makundi ya michuano hiyo huko Brazil. 
Kampuni ya Nike ambayo ndio kubwa zaidi duniani kwa vifaa vya michezo imeonesha umwamba wake baada ya nyota inayowadhamini kufunga mabao 61 katika awamu hiyo ya makundi, huku Adidas ikifuatia kwa magoli 57.

 Lakini Adidas wanaweza kupata ahueni kwa kuwa na njumu bora, kwa mujibu wa wataalamu wa mambo hayo. Kiatu cha Adizero kinachovaliwa na nyota wakali kama  Lionel Messi, Robin van Persie, Arjen Robben, Karim Benzema na  Thomas Muller kimechangua magoli 38 katika awamu hiyo, huku kiatu cha Nike cha Superfly IV kinachovaliwa na
Alexis Sanchez  wa Chile na Xherdan Shaqiri wa Uswisi kimepiga mabao 21 hadi sasa (kabla mechi za mtoano kuanza). 
Adidas pia wanaongoza katika chati ya magoli ya kusaidia, kwa kuchangia mabao 65 katika awamu ya makundi, dhidi ya 54 ya Adidas, wakati kampuni ya Umbro ikijikongoja kupata goli, na hadi sasa ina goli moja la usaidizi kwa mchezaji Mauricio Pinilla aliyetoa pasi katika mchezo wa Chile dhidi ya Australia, ila kiatu chao hakijafunga bao hadi sasa. 
Wachezaji wanaovaa kiatu cha Puma wamefunga mabao manane, wakati kampuni ya Mizuno na Warrior kila mmoja akichangia mabao matatu. Kampuni ya Under Armour pia imemaliza awamu ya makundi bila kupata bao. 
 Nike wanaomdhamini Neymar wa Brazil wana mabao 61
  Cristiano Ronaldo wa Ureno anadhaminiwa na  Nike
  Robin van Persie wa Uholanzi anavaa kiatu cha  Adidas aina ya Adizero 
Adidas wanaomdhamini Lionel Mesii wa Argentina wana mabao 57

VIONGOZI NA WATAALAM WA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO WAKAGUA MAENDELEO MRADI WA MAKAA YA MAWE MCHUCHUMA

$
0
0
 Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa pili kulia), akipata maelezo juu ya Mradi wa Makaa ya Mawe Mchuchuma kutoka kwa Meneja Utawala Msaidizi wa kampuni ya Tanzania – China International Mineral Resources Limited (TCIMRL) Bw. Israel Mkojera. Pamoja nae ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NDC Bw. Mlingi E. Mkucha (wa kwanza kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Viwanda Mama wa NDC Bw. Ramson Mwilangali (wa kwanza kushoto), Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango Bi. Florence Mwanri (wa pili kushoto), Erasmus Masumbuko, Tume ya Mipango (wa tatu Kushoto).
 Viongozi pamoja na Maofisa kutoka Tume ya Mipango wakiangalia sehemu ambayo makaa ya mawe yanaonekana juu ya ardhi. Kulia ni mhandisi wa madini kutoka kampuni ya TCIMRL. Kampuni hii ni ya ubia kati ya Serikali ya Tanzania, na kampuni ya Sichuang Hongda Group Limited ya China. 
 Sehemu ambayo makaa ya mawe yanaoneka kwa juu katika uhalisia wake.
Shimo hili lilichimbwa mwaka 1956 kwa ajili ya utafiti kuangalia tabaka za makaa ya mawe katika eneo hilo la Mchuchuma.

goli la penati dhidi ya mexico yaipeleka uholanzi robo fainali kombe la dunia brazil leo

$
0
0
Kocha wa Uholanzi Louis van Gallakimpongeza Arjen Robben kwa kufanyiwa rafu iliyozaa penati na hatimaye bao la ushindi dhidi ya Mexico leo

Na Sultani Kipingo

wa Globu ya Jamii

Yaani huko Old Trafford katika  klabu ya Manchester United nchini Uingereza atakoenda kufundisha msimu ujao tayari waliishaanza kuandaa ofisi ya meneja wao mpya Louis van Gall anayeifundisha timu ya Uholanzi katika kombe la dunia, baada ya kuhisiwa kuwa ataaga mashindani hayo Jumapili hii walipocheza na Mexico. 
Unaambiwa hadi zikiwa zimesalia dakika tatu mchezo uishe, Uholanzi walikuwa bado wako nyuma kwa bao 1-0, huku kila mtu akiamini kuwa bao la kipimndi cha pili  la Mexico lillofungwa na Giovanni Dos Santos limewamaliza. 
Lakini baada ya kazi za ziada za kipa wa Mexico Guillermo Ochoa kuzuia Uholanzo wasilete madhara, Uholanzi ambao michuano iliyopita mwaka 2010 huko Afrika ya Kusini walifia fainali, wakapiga mabao mawili ya haraka haraka na kuwaacha Mexico hoi. 
Kwanza ilikuwa ni  Wesley Sneijder  aliyesawazisha mnamo dakika ya 87 kufuatia mpira wa kona uliomdondondokea akiwa katika mkao wa kula.
Ndipo katika dakika ya sita za muda wa nyongeza katika muda wa mapumziko mafupi ya kunywa maji, Arjen Robben aliangika chini baada ya kuchezewa rafu ndani ya 18. 
Wakati huo, tayari Robben alishakataliwa penati ya wazimkatika kipindi cha kwanza kilichotawaliwa na Mexico, na bila shaka safari hii alihisi anadaiwa kitu. Kwa vyovyote vile, Klaas Jan Huntelaar aliyeingia badala ya Robin van Persie ambaye ngoma leo ilimkataa, alifunga kwa mkwaju wa chini kuipa Uholanzi tiketi ya robo fainali.
 Dakika ya sita za muda wa nyongeza katika muda wa mapumziko mafupi ya kunywa maji Arjen Robben anafanyiwa madhambi
Wesley Sneijder  aliyesawazisha mnamo dakika ya 87 akifurahia

kutoka maktaba: matangazo ya viota vya maraha enzi hizo


Taste Of Tanzania:Morden Swahili Recipes For The West ON SALE NOW!!

$
0
0

"To my Muslim Community, a blessed month of Ramadhan to you and your families; May the Spirit of this special month illuminate your homes and your souls" 
For those in USA, Taste of Tanzania has reduced the price of Pilau Masala for this month of Ramadhan. Its time to stock for Eid-Ul-Fitr. http://www.amazon.com/gp/product/B00G2U1NW6/
In Addition coming just on time for Eid-Ul-Fitr, Taste of Tanzania: Modern Swahili Recipes For The West, cookbook is now Available at Amazon World-wide. Check Amazon in your country. Also in USA you can get at Walmart and Barnes and Noble Online or ask your nearest store. Now on sale at Amazon USA http://www.amazon.com/dp/0988735903/ 
Thank you Miriam Kinunda Author of Taste of Tanzania Cookbook

SHUKRANI: TEAM LIBE FOR DMV COMMUNITY PRESIDENT 2014

$
0
0
Liberatus "Libe"
 mgombea nafasi ya Urais

Team Libe for DMV Community President 2014 tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa kila mmoja aliye weza kufika kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara jana Meadowbroak Park. Pia tunapenda kuwashukuru wale walio kuwa na nia ya kuja lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao wakashindwa kutimiza hadhma hiyo.  Asanteni!

Pia, Team Libe for DMV Community President 2014 tunapenda kuwashukuru wagombea wengine kwa kujitokeza na kuonyesha ushirikiano chanya na kufurahia mazungumzo na wapiga kura; asante mama Salma Manyoka/mgombea makamu wa Rais, asante Heriet Shangarai/ mgombea makamu wa Rais, asante Solomon Cris/mgombea makamu wa katibu
 
Mama Salma/Mgombea makamu wa Rais
Zaidi, shukrani zetu za dhati zinaenda kwa Ndg. Hamza Mwamoyo/Mwenyekiti wa board, Mzee Safari/ Mkiti wa tume ya uchaguzi na mke wake mama Safari, kaka yetu Jabil  Jongo/ mjumbe tume ya uchaguzi na mchungaji Malekela kwa kuonyesha mapenzi yasio na ukomo kwa jumuia yetu ya DMV.
 
Heried Shangarai/Mgombea makamu wa Rais
Mwisho, tunawashukuru wana DMV wote kwa kuwa na ushirikiano thabiti na kusaidiana kwenye raha na shida. Kama imani ya kimsingi ya “, Team Libe for DMV Community President 2014”inavyo sema “binadamu tupo hapa ili tushirikiane na sio kushindana wala kutengana.”
Solomon Cris/Mgombea makamu wa katibu

Team Libe for DMV Community President 2014 
wishes all Muslims Ramadan Kareem.

Tanzania celebrates International Day in abuja, Nigeria

$
0
0
 On Friday 27 June 2014 it was an International Day at Springhall British School Abuja and Tanzania was among the African countries celebrated. With the support from Tanzania High Commission Abuja, pupils showcased Tanzania's History,Tourism attractions as well as culture- specifically food and attire.
 Tanzania pupils showcasing their country's traditional attires
Tanzania stall

pele akishangilia timu yao 2014, na mambo aliyofanyaga enzi zake

BET AWARDS 2014 RED CARPET & BACKSTAGE LIVE STREAM

ngoma azipendazo ankal

RATIBA YA RAMADHAN LEICESTER UK

$
0
0
Assalaamu Alaykum,
Jumuia ya Kiislamu ya An Noor ya Leicester Uingereza inapenda kuwatakia
Waislamu wote mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Allah akujaalieni nyote afya na nguvu za kutekeleza ibada nyingi zaidi ndani Ya Mwezi huu Adhimu. Pia awape Shufaa ndugu zetu wenye matatizo ya Kiafya na mengineyo. Amin

Jumuia ya An Noor inapenda pia kuwatangazia Waislamu wenzao waishio Leicester Na vitongoji vya karibu kuwa Programu ya Ramadhan InshaaAllah
Itaendelea kama kawaida mwaka huu kwa utaratibu wa Kawaida.
Kila Jumamosi na Jumapili kutakuwa na Darasa za Mwezi wa Ramadhan
Kuanzia Saa Moja na Nusu jioni katika jengo letu 170a Belgrave Gate LE1 3XL Leicester
Baada ya hapo tutakuwa na Futari ya pamoja.
Kama kawaida kila Familia itashiriki katika kuleta futari
Kadhalika kila Familia inakumbushwa kuchangia £5 kila wiki kwa ajili ya Maandalizi.
Programu InshaaAllah itaanza Jumamosi 5/7/2014.
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na hawa wafuatao:

Malik 07983614261 au ust Farid 07792174408
au tutumie email: madrasatulnoor.01@gmail.com
Kullu Am Wa Antum Bikhayr


Mohammed Omar, 
Mwenyekiti wa Jumuia 


Article 2

MRADI MPYA WA SHUGA UNAOELEKEZA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA VVU KWA VIJANA WAANZISHWA KATIKA REDIO JAMII

$
0
0
DSC_0125
Meneja wa kituo cha Sengerema FM Redio, Ndg. Felician Ncheye, akitoa nasaha za ukaribisho kwa washiriki wa mradi wa SHUGA na mgeni rasmi. Katikati ni Mgeni rasmi Mratibu wa UKIMWI halmashauri ya Sengerema mkoa wa Mwanza kupitia mradi wa TACAIDS, Ndg. Geofrey Mabu na Kulia ni Afisa Mipango VVU/UKIMWI UNESCO, Ndg. Herman Mathias.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

Na Mwandishi wetu, SENGEREMA - MWANZA
Redio za jamii nchini zimeaswa kutumika vizuri katika kuelimisha kamii juu ya kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kupitia vipindi vya redio. Hamasa hiyo imetolewa na Ndg Geofrey Mabu ambaye ni mratibu wa UKIMWI halmashauri ya Sengerema mkoa wa Mwanza kupitia mradi wa TACAIDS wakati akifungua warsha ya siku tatu ya mradi mpya ujulikanao kama SHUGA, unaotekelezwa na shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana Shirika la Mfuko wa Watoto (UNICEF) inayofanyika katika kituo cha Redio Jamii Sengerema mkoani Mwanza.

Mabu amesema kuwa mradi huo umekuja wakati muafaka ambapo malengo yake yakizingatiwa na kutekelezwa kama ilivyopangwa utasaidia kufikia malengo ya serikali ya kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI hadi Zero.
DSC_0129
Mgeni rasmi Mratibu wa UKIMWI halmashauri ya Sengerema mkoa wa Mwanza kupitia mradi wa TACAIDS, Ndg. Geofrey Mabu akifungua warsha ya siku tatu ya mradi mpya kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi mapya ya VVU ujulikanao kama SHUGA.

Amesema kuwa redio za jamii ni kiungo muhimu katika kuelimisha jamii na kuwa kama zitatumika vizuri kusambaza elimu ya UKIMWI kupitia vipindi vyake zitasaidia kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali kupitia TACAIDS.
Vile vile ameziomba redio zitakazoshiriki katika mradi huu, kutumia vizuri fursa hii waliyoipata kuhakikisha wanafanikisha malengo ya mradi kwa kiwango cha juu kwa kufanya hivyo pia watakuwa wamelinusuru taifa na janga hili la UKIMWI.
DSC_0069
Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu akitoa maelezo kuhusu madhumuni ya warsha inayohusisha mradi wa SHUGA.

Awali Mkufunzi wa Radio za jamii kutoka shirika la UNESCO Bi Rose Mwalimu akitoa ufafanuzi wa malengo ya semina hiyo, amesema kuwa mradi huu wa SHUGA unalenga kupambana na maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI kwa vijana hapa nchini kupitia vipindi vya mchezo wa redio kubadili tabia.

Amezitaja redio 10 zinazoshiriki katika mradi huu nchini Tanzania kuwa ni FADECO Redio ya Karagwe mkoani Kagera, ORS ya Manyara, Sengerema FM mkoani Mwanza, Pangani FM ya mkoani Tanga na Kahama FM kutoka Shinyanga. Nyingine ni Kitulo FM ya Makete Njombe, Kyela FM ya Mbeya, Nuru FM kutoka Iringa, Pambazuko FM Ifakara na Kwanza Jamii Redio FM kutoka Njombe.
DSC_0269
Afisa Mipango VVU/UKIMWI UNESCO, Ndg. Herman Mathias akitoa mada kuhusu VIjana, Balehe na Mahusiano ya Ngono wakati warsha ya siku tatu ya mradi mpya kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi mapya ya VVU ujulikanao kama SHUGA.

HAPPY BIRTHDAY MWANDISHI MKUU WA MBEYA YETU BLOG JOSEPH MWAISANGO

$
0
0
Mwandishi mkuu wa Mbeya yetu Blog, Joseph Mwaisango
******

TONE MULTIMEDIA GROUP Ambao ni wamiliki wa Mtandao huu wa Mbeya yetu Blog , Tunapenda Kuungana na wadau wetu wote Kumpongeza Bwana Joseph Mwaisango ambaye ndiye Mwandishi Mkuu wa Blog hii ya Mbeya yetu  na Mmoja wa wakurugenzi wa Tone Multimedia Company Limited (TMCL)  ambao pia ni wamiliki wa Blogs za Mikoa TanzaniaTone Radio-Tz , This Day MagazineStay In Tanzania(Tanzania Tours) , Tone Tube Tz  , Matukio na Wanavyuo na Watanzania waishio nje ya Nchi kwa kutimiza miaka yake kadhaa siku ya Leo.

Tunapenda kumpa Hongera sana kwa kazi nzito ambazo anazifanya ili kuwaletea wadau habari zilizo sahihi na za uhakika zaidi kutoka pande zote za Mkoa wa Mbeya, Pia tunamuombea kwa Mungu ampe siku nyingi zaidi , Afya Njema na aendelee kuchapa kazi zaidi na zaidi bila kusahau kuongeza Ubunifu zaidi.

Pia katika Hili tunapenda kuwashukuru wadau Mbali mbali wa Habari wakiwemo Bloggers wote wa Tanzania, Magazeti, Radio na TV kwa kuendelea kuonesha ushirikiano mkubwa ili kazi ziendelee kwa ufanisi mkubwa

Mwisho tunapenda kumshukuru kila mmoja wetu ambaye ni mdau mkubwa wa Blog ya Mbeya yetu,  wote tupo pamoja katika kusherekea siku hii ya leo.

TAARIFA MBALIMBALI ZA MICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

$
0
0
STARS YAJIPIMA KWA BOTSWANA
Timu ya Taifa (Taifa Stars) inacheza mechi ya kirafiki na Botswana leo (Julai Mosi mwaka huu) kuanzia saa 9 alasiri kwa saa za huko.

Mechi itakayofanyika Uwanja wa Taifa jijini Gaborone ni sehemu ya maandalizi ya Taifa Stars kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji (Mambas) itakayochezwa Julai 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kurejea nchini Julai 6 mwaka huu kuendelea na programu nyingine kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji.

Wakati huo huo, kutakuwa na utaratibu maalumu kwa waandishi wa habari za michezo kwa ajili ya kuripoti mechi ya Stars dhidi ya Msumbiji. Hivyo, vyombo vya habari vinatakiwa kutuma majina mawili ya waandishi watakaoripoti mechi hiyo. Mwisho wa kupokea majina hayo ni Julai 8 mwaka huu.
 WACHEZAJI WATANO WAOMBEWA ITC
Wachezaji watano wameombewa Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) ili waweze kucheza mpira wa miguu nchini na nje ya Tanzania.

Abdulhalim Humoud kutoka Simba, Crispine Odulla (Coastal Union) na Haji Ugando (Mbagala Market FC) wameombewa ITC na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) ili wakacheze nchini humo katika klabu za Sofapaka, Bandari FC na Nakuru All Stars.

Vilevile TFF imemuombea ITC mchezaji Ismaila Diarra kutoka nchini Mali ili aweze kujiunga na timu ya Azam FC. TFF inafanyia kazi maombi hayo, na mara taratibu zote zitakapokamilika itatoa ITC hizo kwa wachezaji wanaokwenda nje ya Tanzania.

SERENGETI BOYS YAJINOA KUIKABILI AFRIKA KUSINI
Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) inaendelea vizuri na mazoezi kujiandaa kwa mechi ya mashindano dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos).

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itachezwa Ijumaa ya Julai 18 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Hababuu Ali Omari ameshafanya mchujo wa awali wa wachezaji wa timu hiyo kutoka 39 na kubaki na 31. Timu hiyo imepiga kambi kwenye hosteli ya TFF iliyopo Uwanja wa Karume.

MBEYA CITY, PRISONS KUJARIBU TIKETI ZA ELEKTRONIKI
Timu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) za Mbeya City na Tanzania Prisons zinacheza mechi ya kirafiki Jumamosi (Julai 5 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Mechi hiyo ambayo itakuwa ya kwanza kuchezwa jijini Mbeya katika mfumo wa matumizi ya tiketi za elektroniki kwa washabiki wanaoingia uwanjani itaanza saa 10 kamili jioni.

Kiingilio ni sh. 3,000 kwa majukwaa yote ambapo tiketi zimeanza kuuzwa leo (Julai Mosi mwaka huu). Wakati huo huo, keshokutwa (Julai 3 mwaka huu) kutakuwa na mafunzo ya matumizi ya tiketi za elektroniki yatakayofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya kuanzia saa 3 asubuhi.

Washiriki wa mafunzo hayo ni wasimamizi wa mechi katika uwanja huo, viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), meneja wa Uwanja wa Sokoine na msaidizi wake, makatibu wa Tanzania Prisons na Mbeya City, maofisa habari wa Mbeya City na Tanzania Prisons, Ofisa Usalama wa MREFA na wasimamizi wa milangoni (stewards).

BONIFACE WAMBURA MGOYO
OFISA HABARI NA MAWASILIANO

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

PPF WAENDELEA KUTOA HUDUMA KWA WAKATI KATIKA MAONYESHO YA 38 YA SABASABA

$
0
0
 Afisa Huduma Kwa Wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Jackline Jackson akitoa ufafanuzi juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa wateja waliotembelea Banda la PPF kwenye maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea Kufanyika katika viwanja hivyo.
 Afisa Rasilimali Watu, Utawala na Ushauri wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Happiness Mmbando (Kulia) akimuhudumia mmoja wa wateja waliotembelea banda la PPF katika maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Katika Viwanja vya Sabasaba, Jijini Dar Es Salaam. 
 Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakiwahudumia wateja waliotembelea banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, Jijini Dar Es Salaam
 Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakiwa katika picha ya Pamoja na Mmiliki wa Mtandao wa Michuzi, Ndg Muhidin Issa Michuzi(mwenye suti nyeusi) mara baada ya kukabidhiwa zawadi na PPF wakati alipotembelea Banda la PPF kwenye maonyesho ya Sabasaba.
Mwandishi wa Habari mkongwe, Ndg Abdallah Majura (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko na Pensheni wa PPF pamoja na Mdau wa habari wakati walipotembelea banda la PPF katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba, Barabara ya Kilwa, Jijini Dar Es Salaam.Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images