Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 487 | 488 | (Page 489) | 490 | 491 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Madereva wa Mabasi yanayokwenda katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Kagera jioni hii wameingia kwenye mgomo wa kutosafirisha abiria wakiwa mkoani Singida, kwa madai kwamba wanatozwa faini kubwa sana na Askari wa Usalama barabarani mkoani hapo.Baadhi ya abiria wanaosafiri na mabasi hayo wameulalamikia uamuzi wa madereva hao, kwani ni kama wanapewa adabu kwa uamuzi huo.Globu ya jamii inaendelea kufatilia sakata hilo kwa ukaribu zaidi na tutaendelea kufahamishana zaidi.  0 0

  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Apple ilipofanya uzinduzi wa simu mpya ya iPhone 5s pamoja na ofa kabambe kwa wateja wa Airtel, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Ofa hiyo itawawezesha wateja wa Airtel kupata sms 5000, muda wa maongezi dakika 1500 pamoja na kifurushi cha internet cha 3GB. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa Airtel, Prisca Tembo (kulia) na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa kampuni ya Apple.
  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Apple ilipofanya uzinduzi wa simu mpya ya iPhone 5s pamoja na ofa kabambe kwa wateja wa Airtel, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Ofa hiyo itawawezesha wateja wa Airtel kupata sms 5000, muda wa maongezi dakika 1500 pamoja na kifurushi cha internet cha 3GB. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa Airtel, Prisca Tembo ( wa pili kulia) na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa kampuni ya Apple.

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
  ·Ni kampuni ya kwanza ya mawasiliano nchini kuingia mkataba wa ushirikiano na Apple.

  KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa huduma bora na nafuu leo imetangaza ushirika wake na kampuni kubwa inayotengeneza simu za mkononi ya Apple.Airtel imeweka historia kwa kuwa kampuni ya kwanza ya mawasiiliano nchini Tanzania kuingia mkataba na Apple kupitia simu ya iPhone S5.

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa simu huo jijini Dar es Saalam Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo alisema” leo tunazindua  simu ya iPhone 5s na kuwapatia wateja wetu ofa kabambe ya vifurushi vya muda wa maongezi , ujumbe mfupi na internet. Mteja atakaponunua simu ya iphone S5 atapata kifurushi cha internet cha 3GB, dakika 1450 za maongezi na SMS 5000 kwa mwezi. Natoa wito kwa watanzania na wateja wetu kutumbelea maduka yetu na mawakala wetu ili kuweza kujipatia simu hii.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano Bi, Beatrice Singano alisema “Uzinduzi huu leo utato fulsa kwa wateja wetu  kupata uzoefu tofauti wa huduma zetu na kuwawezesha  kuendelea kufurahia huduma yetu ya SWITCH on, huduma ambayo imezinduliwa ili kuwawezesha wateja wetu kupata internet yenye kasi zaidi bila kikomo kupitia mtandao wa Airtel”

  0 0

  MHE. RASHID MTUTA (PICHANI) AMETOA SOMO KWA WAKAAZI WA  MKURANGA NA VITONGOJI VYAKE, MHE. MTUTA ALITOA ELIMU YA UZALENDO,AMANI UTULIVU N UMUHIMU WA KATIBA MPYA.  WAKAZI HAO WAMEKIRI KUELEWA NA KUTAMKA KUWA WANATAKA KATIBA MPYA,NA HAYAKO TAYARI KUUNGA MKONO KUNDI LOLOTE LENYE NIA  YA KUKWAMISHA MCHAKATO HUU ULIANZISHWA KWA NIA NJEMA NA RAIS WETU.
  Akitoa mfano wa  Katiba iliyopo ambayo ina mambo mengi yasiyohitajika na jamii. Mhe. Mtuta aliwaeleza wakaazi hao kuwa hawako bungeni kubadili idadi ya serikali bali kubadili mustakabali mzima wa Taifa kwa kuwa na katiba inayohusu maisha yote na kueleza kuwa iwapo watawaunga mkono wale wanaotaka katiba hii ikwame ni Sawa na kuunga mkono upotevu wa Mali za umma ambazo hadi sasa tangu kuanza Kwa tume mabilioni  ya walalahoi tayari yametumika
  Pia alieleza kuwa yeye alikuwa mmoja ya wana UKAWA,lakini alipoona makubaliano ndani ya ukawa hawafikiwi aliona hakuna haja kuendelea kuwa nao,yeye alishauri wenyeviti wenzio kupambana ndani ya bunge Kwani hapo Ndio eneo sahihi kisheria kufunga katiba ya nchi.
  Mhe Mtuta alienda mbele zaidi Kwa kuwaomba wana Mkuranga kutumia akili zao zaidi na sio kuelezwa kila kitu na wanasiasa, kwa kuwa katiba si Mali ya wanasisa.

  Pia wananchi walieleza kushangazwa kwao na UKAWA HASA BAADA KA KUTOKA KWA LENGO la kukwamisha katiba na sasa wanatangaza kuweka rais mmoja, wao NRA  wanasema wanachanganyikiwa na hatua hiyo kwani walidhani lengo lilikuwa katiba na haya mengine yanawatia njia panda.
  Mhe Mkiti aliambatana na N/KATIBU mkuu taifa ,mhe Hassan kisabya na Katibu mwenezi taifa CCK MHE Richard Kiyabo.

  Mwenyekiti wa NRA Mhe Mtuta akiendelea kuongea na wakaazi wa Mkuranga


  0 0
 • 06/28/14--18:09: Hilali ya Ramadhani
 • Hilali ya Ramadhani - First view of the First Crescent with Jupiter to its left top right corner as seen in Dar es salaam. Picture by N. T. Jiwaji

  0 0

   Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akiingia eneo lililopata madhara kutokana na kuungua moto usiku wa kuamkia leo, katika soko la Keko, katika jimbo hilo jijini Dar es Salaam. Mtemvu amewapa pole walipoteza mali zao kutokana na moto huo ambao chanzo cha ke hakijajulikana.  Hadi inakisiwa imepatikana hasara ya zaidi ya sh. milioni 97.
   Naibu Katibu wa soko la Keko, Hassan Gitigi (kushoto) akimpa maelezo Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu kuhusu madhara yaliyosababishwa na moto huo
   Baadhi ya wafanyabiashara katrika soko hilo akieleza hasara walizopata. Wameeleza kwamba mbali na waliopata hasara ya kuunguliwa bidhaa na mabanda yaop ya biashara, pia wapo waliopata hasara kwa maduka na mabanda yaop ya biashara kuporwa na vibaka wakati wa tukio hilo la moto.
   Mtemvu akizungumza na waliopatwa na madhara kuhtokana na moto huo
  Mtemvu akizungumza na baadhi ya viongozi waliofika kutoa pole kwa walipatwa na madhara kwenye soko hilo. Picha zote na Bashir Nkoromo

  0 0
 • 06/28/14--18:15: Kumbukumbu
 • Tarehe kama ya leo ya maka 2013 mpendwa wetu Anna Ntamubano Gwitaba uliitwa na Bwana maana yeye alikupenda zaidi na tayari amekuandalia taji zuri kwa ajili ya Ufalme wake .
  Wewe ulikuwa moja ya maua mazuri yaliyopandwa katika bustani ya Bwana na wakati ulipochanua na kuvutia Bwana alikuchuma na kukuweka mahali pazuri mno. 
  Daima unakumbukwa na familia yako wakiwemo watoto wako (Adam, Irene, Edgar na Kelvin) na baba yao, mama yako mpendwa (Bibi Naomi), dada zako, kaka zako, watoto wote uliowalea, wajukuu, mawifi, mashemeji, wajomba, mashangazi, wakwe, marafiki, wafanyakazi wenzako na majirani wote. 
  Bwana ametoa na Bwana ametwaa, 
  Jina lake lihimidiwe
  AMINA

  0 0

  Hapa hukatizi ndugu yangu!Wachezaji wa Timu ya Rwamishenye wakicheza muziki baada ya kusawazishaMashabiki ndio usiseme...walijaa uwanjani KaitabaMashabiki kibao. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili nchini Rose Muhando ameibuka na wimbo mpya uitwao Facebook. 

  Akizungumzia  wimbo huo, Rose amesema  ana imani wimbo huo utakuwa kivutio kikubwa kwa jamii hasa vijana kwa sababu una ujumbe mzuri ambao utagusa wengi.

  “Sitaki kuwaambia nimeimba nini, lakini Facebook ni wimbo mzuri na mashabiki wangu naamini wanatambua kwamba mimi si mtu wa masihara ninapotunga kazi zangu,” alitamba mwimbaji huyo.

  Alieleza kuwa wimbo huo utakuwa katika albamu yake mpya iitwayo Kamata Pindo la Yesu anayotarajia kuizindua jijini Dar es Salaam katika siku itakayotangazwa wakati wowote kuanzia leo.Baadhi ya nyimbo zilizompa umaarufu msanii huyo ni pamoja na Mteule Uwe Macho, Nipe Uvumilivu, Yesu Nakupenda, Akina Mama, Nakuuliza Shetani, Yerusalemu, Mwambieni Mungu na Nakaza Mwendo.

  Pia nyimbo nyingine zilizompa umaarufu ni Kitimutimu, Imani, Onjeni, Sikilizeni Enyi Makahaba, Mungu Wangu, Moyo Wangu, Najitoa Sasa, Hey Mbona Watenda Dhambi na Wapendwa.

  Nyingine ni Utamu wa Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia. Nyimbo hizo zipo katika albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi), Jipange Sawasawa na Utamu wa Yesu.

  Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya katika albamu ya Vua Kiatu.


  0 0

   Meza Kuu katika sherehe za kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza Mkoani Mwanza (katikati) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja ambaye pia ndiye aliyekuwa Mgeni rasmi katika sherehe hizo zilizofana katika Ukumbi wa Gereza Kuu Butimba, Mwanza.
   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba fupi kwa Maofisa wa Jeshi la Magereza na Wageni Waalikwa (hawapo pichani) katika Sherehe za kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza Mkoani Mwanza.
   Maafisa na Askari wa Magereza Mkoani Mwanza wakimsikiliza Mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati akitoa hotuba yake fupi katika sherehe za kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza Mkoani Mwanza katika Ukumbi wa Bwalo la Gereza Kuu Butimba, Jijini Mwanza.
   Aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoani Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Mstaafu, Raphael Mollel akitoa nasaha zake kwa niaba ya Wastaafu wote wa Jeshi la Magereza Mkoani Mwanza katika sherehe za kuwaaga Wastaafu wa Magereza Mkoani Mwanza.
   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja ( tai nyekundu) katika picha ya pamoja na Maafisa na Askari wa Magereza Mkoani Mwanza ambao Wanastaafu kwa mujibu wa Sheria ifikapo Julai 1, 2014. Sherehe ya kuwaaga imefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Gereza Kuu Butimba, Mwanza.
   Wageni Waalikwa katika sherehe za kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza Mkoani Mwanza wakitosi vinywaji na Meza Kuu kama inavyoonekana katika picha.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja (tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Magereza ya Mkoa wa Mwanza katika sherehe za kuwaaga Wastaafu wa Jeshi la Magereza ambao wanastaafu Utumishi wao kwa mujibu wa Sheria ifikapo Julai 1, 2014. Sherehe hizo zimefanyika Juni 28, 2014 katika Ukumbi wa Bwalo la Gereza Kuu Butimba, Jijini Mwanza
  Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.

  0 0

   Waziri Mkuu Mhe.Mizengo Pinda akihutubia Bunge kabla ya kuahirishwa hadi Novemba 4, 2014 
   Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya akijibu Hoja za Wabunge kuhusu Mswada wa Fedha wa Mwaka 2014 ambao umepitishwa na Bunge Leo.
   Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya mashariki Mhe.Samweli Sita akibadilishana mawazo na waziri Mwenzake Mhe,Mary Nagu.

   Mwanasheria Mkuu Mhe.Jaji Frederick Werema akimpa mkono wa kumpongeza  Waziri Mkuu Mhe.Mizengo Pinda mara baada ya kulihuitubia Bunge.
  SpikaMhe.Anna Makinda akiahirisha Bunge 

  Wabunge wakisimama baada ya Bunge kuahirishwa rasmi hadi Novemba 4, mwaka huu. Picha na Deusdedit Moshi wa Michuzi Blog Kanda ya Kati

  0 0

  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Ilala Mhandisi Raymond Mushi akimlaki Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea Malabo Equtorial Guinea ambapo alikwenda kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika(AU) uliomalizika jana.Kushoto ni Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange Picha na Freddy Maro

  0 0


  Matokeo ya Mtihani wa Majaribio (Mock) kwa mtihani wa Kidato cha Nne mwaka huu na Kidato cha Sita mwakani, yatachangia alama 10 za Alama Edelevu (CA). 
  Kwa utaratibu huu, matokeo ya mwisho ya mtahiniwa, yatatokana na asilimia 30 ya Alama Endelevu na asilimia 70 ni mchango wa Alama za Mtihani wa Taifa. 
  Asilimia 30 za Alama Endelevu, zitapatikana kutokana na mitihani mbalimbali. Kwa Kidato cha Nne mwaka huu, alama hizo zitatokana na matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha pili ambao utakuwa na alama 10, matokeo ya kidato cha tatu muhula wa kwanza na wa pili alama tano, matokeo ya mtihani wa majaribio (mock) wa Kidato cha Nne ni alama 10 na majaribio ya kazi alama tano. 
  Utaratibu huu umetokana na viwango vipya vya ufaulu, vilivyoainishwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kwenye kitabu cha Mwongozo wa Matumizi ya Viwango vya Ufaulu na utaratibu wa kutunuku matokeo ya kidato cha nne na sita. 
  Kwa Kidato cha Sita, zitatokana na matokeo ya mtihani wa Kidato cha Tano muhula wa kwanza na pili alama 15, matokeo ya 'mock' alama 10 na kazi mradi itakuwa ni alama tano.
  “Katika somo ambalo mtahiniwa hakufanyia Kazi za majaribio, alama za matokeo ya Mitihani ya 'Mock' ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita, itachangia alama 15 badala ya 10 zilizoainishwa,” imefafanua sehemu ya mwongozo huo. 
  Hata hivyo, katika Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka jana na Kidato cha Sita mwaka huu, mchanganuo wa alama 30 za Alama Endelevu ni alama 15 zinazotokana na matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha Pili, asilimia 10 ilitokana na maendeleo ya mitihani ya kidato cha Tatu muhula wa Kwanza na Pili na matokeo ya muhula wa Kwanza Kidato cha Nne na kazi za majaribio asilimia tano. 
  Kwa Kidato cha Sita, alama endelevu ni matokeo ya Kidato cha Tano kwa mihula yote miwili ni alama 15, muhula wa kwanza wa Kidato cha Sita ni asilimia 10 na kazi za majaribio ni asilimia tano. 
  Aidha, Baraza limebadili utaratibu wa kupanga madaraja ya kufaulu, kutoka mfumo wa Pointi na kuwa wa Wastani wa Alama za Mtahiniwa (GPA). 
  Mfumo unaotumiwa sasa wa pointi, huonesha wastani wa pointi alizopata mtahiniwa kwa masomo aliyofaulu zaidi, na kupanga madaraja kuanzia la kwanza hadi la nne. 
  Madaraja ya mfumo wa GPA, hupangwa katika utaratibu wa Distinction, Merit, Pass na Fail. Daraja la Distinction ni la ufaulu wa juu zaidi na daraja Pass ni ufaulu wa chini. 
  Mtahiniwa hutunukiwa madaraja A, B+, B, C, D, E au F kutegemeana na ufaulu wake katika somo ambapo uzito wa alama katika madaraja A = 5, B+= 4, B = 3, C=2, D = 1, E = 0.5 na F = 0. 
  Mtahiniwa atahesabiwa kuwa amefaulu somo, endapo atapata Daraja D ambayo ni sawa na uzito wa alama moja. Ukokotoaji wa jumla ya GPA ya mtahiniwa hufanyika kwa kuzingatia masomo, ambayo mtahiniwa amefaulu angalau kwa daraja D na kuendelea (D, C, B, B+ na A). 

  GPA anayopata mtahiniwa hutokana na wastani wa pointi alizopata katika masomo saba aliyofanya vizuri zaidi kwa Mtihani wa Kidato cha Nne au masomo matatu ya mchepuo kwa Mtihani wa Kidato cha Sita. 

  Aidha, GPA ya mtahiniwa huandikwa katika nafasi moja ya desimali ambapo nafasi ya pili ya desimali hukadiriwa katika makumi yaliyokaribu. 

  Mfano, mtahiniwa mwenye GPA ya 3.15 itakuwa sawa na 3.2 na mtahiniwa mwenye GPA ya 3.14 itakuwa sawa na 3.1. 
  Muundo wa madaraja ya GPA kwa kidato cha nne, Distinction ni 3.6-5.0, Merit 2.6 -3.5, Credit 1.6-2.5, Pass 0.3-1.5, Fail 0.0-0.2 wakati Kidato cha sita ni Distinction 3.7-5.0, Merit 3.0-3.6, Credit 1.7-2.9, Pass 0.7-1.6, Fail 0.0-0.6.

  0 0

   Millard Ayo akipokea Tuzo ya Mtangazaji wa Radio wa kiume anayependwa mara baada ya kuibuka mshindi katika kipengele hiko
   Akiwashukuru Wadau waliompigia kura na kumpa sapoti
   Salim Kikeke kutoka Idhaa ya Kiswahili ya BBC akiwashukuru wadau wake waliomuwezesha kushinda Tuzo 
  King Majuto akifurahi mara baada ya kuppokea Tuzo yake mara baada ya kutangazwa mshindi wa Kipengele cha Msanii Bora anayependwa wa Kiume.Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog.

  0 0
 • 06/28/14--20:00: ngoma azipendazo ankal

 • 0 0


  0 0

   NI FURAHA TELE. Mwalimu wa kozi fupi wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma (VETA) – Dar es Salaam, Bi. Bertha Ogwal, kushoto, akimkabidhi Bi. Jamila Mwenda, ripoti ya mahudhurio ya kozi ya awali ya usekretari/kompyuta, hivi karibuni. Jamila ni miongoni mwa vijana 11 toka mikoa mbalimbali nchini waliofadhiliwa masomo na shirika lisilo la kiserikali la Help for Underserved Communities Inc. (HUC), lenye makao yake Marekani, ambalo linayosaidia upatikanaji wa maji safi na salama ya visima, maktaba za kijamii na ufadhili wa masomo ya ufundi. (Picha zote na Nathan Mpangala wa HUC).
   Mkuu wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma (VETA) – Dar es Salaam, Bw. Samuel Ng’andu wa pili toka kushoto, akimkabidhi cheti ya mafunzo ya awali ya ufundi magari, Yasini Musa hivi karibuni. Yasin ni mmoja wa vijana waliopata ufadhili toka shirika lisilo la kiserikali la Help for Underserved Communities Inc. (HUC). Wengine katika picha ni Msajili wa kozi Bi. Violet Fumbo na Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Kozi fupi Bw. Rocky Mongi.
   Kijana Joseph Mboya (kulia) akilamba ganda lake la ufundi magari toka kwa Mkuu wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma (VETA) – Dar es Salaam, Bw. Samuel Ng’andu, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
   Mwalimu wa Umeme wa magari wa Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na Huduma (VETA) – Dar es Salaam, Bw. Saidi Mbwana, akimkabidhi cheti ya mafunzo ya awali ya umeme wa magari, Bi. Neema Bungara jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Neema ni mmoja wa vijana  11 waliopata  ufadhili wa masomo ya ufundi toka shirika lisilo la kiserikali la Help for Underserved Communities Inc. (HUC).
  HAKIKA WAKIWEZESHWA WANAWEZA. Bi. Neema Bungara akionesha ganda lake lililosheheni ‘A’ tupu. Neema ni mmoja wa vijana 11 waliopata ufadhili wa masomo ya ufundi toka shirika lisilo la kiserikali la Help for Underserved Communities Inc. (HUC).

  0 0

  Mtanange ulikuwa  mgumu. Brazil hawakuvutia kabisa. Lakini ilitosha kuwapeleka robo fainali za Kombe la Dunia,  ingawa kwa mbinde,  baada ya kuitoa Chile kwa njia ya penati katika mchezo wako wa raundi ya 16  kwenye uwanja wa Mineirao mjini Horizonte.


  Neymer ndiye aliyeweka kimiani bao la ushindi wakati Brazil ikiwa chini kwa mabao 3-2, lakini shujaa wa siku hakuwa yeye bali kipa wao Julio Cesar aliyeokoa mikwaju miwili,


  0 0

  Colombia imepeleka mashabiki wake wanaovutia kwa ushangiliaji wao hadi kwenye robo fainali za kombe la Dunia baada ya nyota wake James Rodriguez akifunga mabao yote. Colombia waliifunga Uruguay ya mng’ata meno Suarez bao 2-0 katika mchezo wao wa raundi ya 16 kweny uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro jana.

  Angalia goli la mwaka la Rodriguez ambalo ni tamu sana kiasi hata huchoki kuangalia. Huku goli la adui likiwa nyuma yake, kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 kwanza aliweka gambani  pasi aliyoletewa, halafu kabla mpira haujatua ardhini aligeuka na kupiga bao dakika ya 28, akiwa nje ya 18.


  Hebu cheki mwenyewe. Mambo kama haya ni marehemu Edward Chumilla tu aliyeweza kuyafanya hapa nyumbani.


  0 0

  Wagombea wa nafasi ya Urais katika Klabu ya Simba, Evans Aveva (katikati) na Andrew Tupa na wakipiga kura wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa klabu hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
   Hassan Dalali akipiga kura.
   Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu na Rais wa Simba anayemaliza muda wake, Ismail Aden Rage wakipiga kura.
   Rais wa Simba aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage akiagana na mgombea wa Urais wa Simba, Evans Aveva (katikati).
   Wagombea wakitafakari.
  PICHA ZAIDI YA TUKIO HILI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Othman Khamis Ame, OMPR
  Timu ya Soka ya African Boys ya Kijiji cha Kitope imetawazwa ubingwa wa mashindao ya Kombe la Zaweda baada ya kuitandika timu ya New Star ya Kiwengwa kwa Magoli 4 -3 katika pambano la fainal ya mashindano hayo yaliyoshirikisha Timu 12 za Soka za Jimbo la Kitope. 
  African Boys ya Kitope ilibeba kombe hilo la Zaweda baada ya kutoka suluhu ya bila kwa bila na wapinzani wake New Star ya kiwengwa kwenye dakika 90 za mchezo huo na kulazimika kupigiana Penalti zilizoibua mshindi wa pambano hilo lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Santiago Benabao uliopo Kitope. 
  Mgeni rasmi wa Fainali hiyo Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza African Boys ya Kitope ambayo ilipata fedha taslim shilingi Laki 500,000/-, Seti ya Jezi, Kikombe, Mipira pamoja na Seti ya Tv na Dikoda yake iliyotolewa na Mke wa Mbunge wa Jimbo hilo Mama Asha Suleiman Iddi.
   Mshindi wa Pili New Star ya Kiwengwa ikazawadiwa shilingi Laki 300,000/- taslim, Jezi, Kikombe pamoja na Mipira wakati mshindi wa tatu Timu iliyoalikwa ya soka ya Mahonda Kids akajinyakulia shilingi Laki 200,000/- Taslim, jezi pamoja na mpira. Mapema Balozi Seif alikabidhi zawadi ya fedha taslim kwa washindi wa mashindano ya mchezo wa pete { netball } ambapo mshindi wa kwanza ni timu ya wanawake ya Biasha Kitope, mshindi wa Pili alikuwa timu mualikwa Mahonda na wa Tatu alikuwa Timu ya Mabanati wa Kitope “ B “. 
  Akizungumza na wana michezo hao wa mashindano ya Zaweda Cup Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif alielezea furaha yake kutokana na zoezi zima la mashindano hayo lililoonyesha nidhamu ya hali ya juu na kuwataka wanamichezo hao kuhakikisha kwamba nidhamu hiyo wanaichukulia kuwa kigezo cha kuiendeleza katika michezo mengine itakayowakabili hapo baadaye.
   Mbunge wa Kitope Balozi Seif ali Iddi akizungumza na wanamichezo mara baada ya kumalizika kwa fainali ya mashindano ya Zaweda Cup hapo uwanja wa michezo wa Kitope Wilaya ya Kaskazini “ B”. Kushoto yake ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kaskazini “ B “ Ndugu Hilika Khamis Fadhil.
   Balozi Seif akikabidhi zawadi za mipira na jezi kwa timu shiriki za mashindano ya Zaweda Cup yaliyofanyika ndani ya Jimbo lake la  Kitope.
   Balozi Seif akikabidhi zawadi za mipira na jezi kwa timu shiriki za mashindano ya Zaweda Cup yaliyofanyika ndani ya Jimbo lake la  Kitope.
   Balozi Seif akikabidhi zawadi za mipira na jezi kwa timu shiriki za mashindano ya Zaweda Cup yaliyofanyika ndani ya Jimbo lake la  Kitope.
   Mabingwa wapya wa kombe la Zaweda African Boys ya Kitope wakishangilia ushindi wao dhidi ya New Star ya Kiwengwa kwa mikwaju ya Penalti 4-3 baada ya kumaliza muda wa dakika 90 bila kwa bila.
  Wanandinga wa African Boys ya Kitope wakiitia mikononi seti ya TV aina ya Phillips na King’amuzi chake ikiwa ni miongoni mwa mzawadi walizojikusanyia baada ya kushinda fainali ya kombe la Zaweda dhidi ya New Star ya Kiwengwa. Picha na Hassan Issa wa  OMPR

older | 1 | .... | 487 | 488 | (Page 489) | 490 | 491 | .... | 3272 | newer